Tuesday, 8 February 2022

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMANNE FEBRUARI 8,2022

Magazetini leo Jumanne February 8 2022

Biashara kati ya Tanzania na Rwanda yafikia Bilioni 635.



Share:

Monday, 7 February 2022

YAKUBU- BAKITA JIENDESHENI KIBIASHARA


**************

Na. John Mapepele

Naibu Katibu Mkuu wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Saidi Yakubu ameitaka Menejimenti ya Baraza la Kiswahili la Taifa ( BAKITA) kuwa wabunifu na kujiendesha kibiashara ili kuliingizia taifa mapato.

Yakubu amesema hayo leo Februari 6, 2022 alipofanya kikao na Menejimenti ya BAKITA na kukagua shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na taasisi hiyo.

Amesema kwa sasa BAKITA linatakiwa kutumia fursa ya lugha ya Kiswahili kuwa lugha ya kazi katika mikutano ya Umoja wa Afrika kupanua utendaji wa kazi zake nje ya Tanzania.

Aidha, Yakubu ameeleza kuwa BAKITA linaweza kuweka mikakati mbalimbali ya kubidhaisha lugha ya Kiswahili kwa kuingia ubia na wataalam na taasisi mbalimbali.

"Tuangalie fursa ya Kiswahili kwa kuuza zao hili kama pamba, au korosho ndani na nje ya nchi". Amesisitiza Yakubu.

Pia, amelitaka Baraza liendelee kujitangaza na kutangaza shughuli ambazo linazofanya ikiwa ni pamoja na ufundishaji na kuratibu ukalimani, ufanyaji wa tafsiri wa nyaraka mbalimbali na ufundishaji wa lugha.
Share:

MADARASA YAGEUZWA KITUO CHA KUVUTIA BANGI



​​​​​​​WANAFUNZI wanaosoma katika shule mbili za msingi za Kijichi wilayani Temeke mkoani Dar es Salaam, wako hatarini kuathirika kiafya na kimaadili kutokana na madarasa yao kutumika kama sehemu ya kuvuta bangi.

Vitendo hivyo vimefichuliwa juzi na viongozi wa Jumuiya ya Wazazi Kata ya Kijichi waliotembelea shule hizo kwa ajili ya kutoa misaada kwa wanafunzi wanaoishi katika mazingira magumu katika kuadhimiasha miaka 45 ya kuzaliwa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Akizungumzia suala hilo, Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule ya Msingi Kijichi B, Stephano Cherehani, alisema matumizi ya dawa hizo za kulevya tayari yameonekana kuwa na athari katika maendeleo ya elimu kutokana na baadhi ya wanafunzi kupata madhara.

Alisema watu wanaoingia shuleni huko kila siku kwa nia ya kuangalia michezo ya mpira wa miguu, hutumia madarasa kuvuta bangi na kuacha mabaki kila mahali.

Cherehani alisema wakati mwingine watu hao wanavuta nje ya madarasa hayo kipindi cha asubuhi, jambo ambalo linaleta usumbufu kwa wanafunzi wanapotaka kuingia darasani kuanza vipindi vya masomo.

“Jambo hili linatuathiri sisi walimu na wanafunzi pia, uvutaji wa bangi umekuwa kama jambo la kawaida, lakini chanzo kikubwa ni huu uwanja wa mpira ambao unatumika na jamii muda wote,” alisema.

Aliomba serikali kuingilia kati kwa kudhibiti vitendo hivyo ili kuwaweka wanafunzi katika hali ya utulivu na kukidhi matakwa ya mazingira bora ya ujifunzaji na ufundishaji.

“Wanafunzi hawawezi kusoma kwa umakini kama kuna mabaki ya bangi au mtu anavuta nje ya darasa, tunaomba watu hawa wadhibitiwe haraka,” alisema.

Katibu wa Wazazi wa CCM katika kata hiyo, Magdalena Komba, alimhakikishia mwalimu mkuu huyo kuwa watalifanyia kazi haraka kwa kwenda kuripoti katika vyombo husika ili eneo hilo liwe salama kwa utoaji wa elimu kwa watoto.


“Pamoja na kwamba leo (juzi) tumekuja kuwasaidia watoto wetu wanaoishi katika mazingira magumu, lakini suala hili la uvutaji bangi holela limenigusa na nitakwenda kuwasiliana na vyombo husika ili kulikomesha,” aliahidi.

Komba pia alisema jumuiya hiyo ni sawa na kiranja katika malezi ya watoto na ndio maana katika maadhimisho hayo, wameamua kutoa misaada ya sare za shule na madaftari kwa wanafunzi 27 wanaoishi kwenye mazingira magumu.

Mwanafunzi Hamisi Shamte aliyenufaika na msaada huo, aliishukuru jumuiya hiyo kwa kuwatambua na kisha kuwapa msaada huo ambao utawasaidia katika safari yao ya elimu.

Diwani wa Kijichi, Athuman Nyamlani, aliahidi kuliwasilisha suala hilo kwenye vyombo vya dola ili wanaojihusisha na vitendo hivyo wachukuliwe hatua za kisheria.
Share:

BIASHARA YANGU ZILIZOKUWA ZINANISUMBUA SASA ZIMENOGA SANA

Biashara iliyokuwa ikinisumbua kila mwaka sasa hivi imenoga kunoga. Kila jirani yangu ananimezea mate. Mimi Naitwa Frank mzaliwa wa Ilala Tanzania ambako pia nimesomea. Nilitoka kidogo kwenda jijini Dar es salaam baada ya kidato cha nne kisha nikarudi nyumbani manake sikuwa na bahati ya kupata kibarua chochote Mjini. 

Dar kwa hakika nilikaa kwa muda wa mika nne na maisha yangu yalikuwa magumu hata nusra nianze kuiba kwani marafiki wangu wengi walikuwa wezi wa usiku na mchana mitaani. Nilipoona maisha yangu yanaelekea pabaya, niliamua kurudi kwa hiari nyumbani ili nifanye ukulima. 

Nilitoa hela kidogo kutoka kwa ukulima wa sukuma kisha nikaanza kuuza malimali hapo Singida Market lakini hiyo biashara ilinisumbua kwa muda mrefu huku nikiwa sasa nimeoa. 

Maisha yakawa magumu kwa muda mrefu hata karibu nikate tamaa. Kwa bahati nzuri, kuna shangazi yangu anayeishi Uganda alirudi kunitembelea Singida alipopata nikiangaika kila mara. Hata chakula ilikuwa shida. Akaniuliza nini mbaya nikamuambia kazi sina na sina bahati pia ya mjini ndipo alinisimulia alichofanya hadi akawa tajiri kupindukia. 

“Mimi nilitembelea daktari anayeitwa Kiwanga na akanifanyia Spells za biashara yaani Business Spells. Hata haikuchukua siku mbili biashara yangu ya nguo ikanoga na sasa nina magari mawili na ploti Uganda nimelipia nataka kujenga.

 Tafadhali hata wewe jitoe kwenye lindi hili la umaskini,” alinisihi. Kwa kweli nilimuomba nambari za simu za Kiwanga Doctors na kwa bahati akanipatia nikatafuta appointment na Daktari siku iliyofuata aliponifanyia Wealth Spells.

 Leo hii mimi ni tajiri ninauza kila aina ya hardware material. Niko hardware karibu kila mji. Kama una shida kama mimi usisite kumtembelea Daktari Kiwanga. Kiwanga Doctors wanatatua shida nyingi kama Kupata mpenzi, kurudisha mpenzi, kuleta furaha na amani katika familia. Pia wanasaidia kuimarisha nyota yako pamoja na kupata dawa ya mvuto kwa mwanaume au mwanamke. Pia wanatibu magonjwa sugu kama Kisukari, Pressure kwa kutumia miti shamba na mengineyo.

 Wasiliana na Kiwanga Doctors kwa nambari +254 769404965 Kwa WhatsApp ipo pia au tembelea Website yao: www.kiwangadoctors.com. Unaweza kuandika barua pepe yaani Email kwa: kiwangadoctors @gmail.com. Si lazima usafiri hadi ofisi zao. Ongea nao kwa njia ya simu/WhatsApp na utasaidika kwa haraka kama vile watu wengine wanavyopata usaidizi.
Share:

ASKARI WANAOCHAFUA JESHI LA POLISI NCHINI KUCHUKULIWA HATUA


Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini,akizungumza na mamia ya wananchi wa Mara, baada ya kupewa nafasi ya kuongea na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwenye Mkutano wa Hadhara uliofanyika Hospitali ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Kata ya Kwangwa, Musoma Mjini, Mkoani Mara.


Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini,akisisitiza jambo kwa wananchi wa Mara, baada ya kupewa nafasi ya kuongea na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwenye Mkutano wa Hadhara uliofanyika Hospitali ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Kata ya Kwangwa, Musoma Mjini, Mkoani Mara.

...............................................................

Na Mwandishi wetu.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini amesema Wizara itashughulikia askari wanaochafua Jeshi la Polisi kwa kupitia Tume ya Utumishi wa Jeshi la Polisi, Magereza, Zimamoto na Uokoaji na Uhamiaji, ili kurejesha imani ya wananchi kwenye Vyombo vinavyosimamia Ulinzi na Usalama wa mali zao.

Amesema kuwa Tume hiyo ni chombo kinachosimamia nidhamu za watumishi wa Vyombo hivyo na kwamba Mwenyekiti wa Tume hiyo ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni na Makamu wake ni yeye, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi hivyo watashugulikia kikamilifu maelekezo aliyoyatoa Rais Samia.

“Kuna maelekezo Mheshimiwa umeyatoa, mimi na Waziri Masauni tutayasimamaia kikamilifu. Ipo Tume ya Utumishi wa Jeshi Polisi, Magereza, Uhamiaji na Zimamoto na Uokoaji, chombo hiki ndio kinasimamia nidhamu za watumishi wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama.”

Naibu Waziri Sagini amezungumza hayo leo mbele ya mamia ya wananchi wa Mara, baada ya kupewa nafasi ya kuongea na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwenye Mkutano wa Hadhara uliofanyika Hospitali ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Kata ya Kwangwa, Musoma Mjini, Mkoani Mara.

Aidha Naibu Waziri Sagini amewataka Watanzania kutii sheria na kujiepusha na vitendo vya uhalifu vitakavyowapelekea kuwa wateja wa Vyombo vya Dola. Amesema kwamba Vyombo hivyo vinasimamia Sheria na utekelezaji wa Sheria na endapo mwananchi atakiuka sheria za Nchi basi lazima sheria itachukuliwa.

“Niwaombe wananchi hivi ni vyombo vya dola, Sisi tusingependa vyombo hivi vipambane na raia. Usipokuwa, raia atakaye kikuka sheria, raia atakayetenda vitendo vya uahalifu, atakaye mnyima mwenzake amani atakuwa tuu mteja wa Polisi, na baadae Mahakama, mwishowe Magereza”
Share:

BUNDI ATUA KANISANI..AIMBA KWAYA KWA MARINGO KAMA BINADAMU, TAZAMA HAPA


Video maridadi inayomuonyesha Ndege aina ya bundi,akiwatumbuiza waumini kanisani katika taifa la Jamhuri ya Dominika imewachangamsha wengi.

Bundi huyo  aliwaacha waumini vinywa wazi pamoja na wanamtandao baada ya kuonekana kanisani wakati wa ibada.

Huku wanakwaya hao wakiwatumbuiza waumini na nyimbo tamu, bundi huyo anaonyeshwa akiwa katika paa la kanisa akisakata densi kama inavyoonyeshwa kwenye video iliyopakiwa na @nowthisnews kwenye Instagram.

"Bundi huyu anaonekana kuwa na wakati mzuri wa kucheza muziki wa injili katika kanisa moja la Jamhuri ya Dominika," video hiyo ilinukuu.

Waumini wa kanisa hilo katika Jamhuri ya Dominika, walisema bundi huyo alicheza nyimbo hizo zote kwa saa moja.


Kwa mshangao wa wengi, bundi huyo alionekana kufurahishwa na wimbo wa wanakwaya waliokuwa wakiwatumbuiza waumini

Huku baadhi ya wanamtandao wakihusisha ndege huyo na uchawi, wengine walisema kuwa wimbo wa kwaya ulikuwa wa kupendeza na kuwaondolea ndege 'bahati mbaya'

@kitschykatz: "Inapendeza sana, siwezi! Mungu ni mzuri sana! Na kiumbe huyu ananitoa machozi!"

@dai_dreaming_ : "Huyo ni mtu ambaye amefariki hivi karibuni na anawatembelea tu!"

@joanflakes "Walifikiri ni mchawi (imani iliyozoeleka katika nchi za Amerika Kusini)."

@myartisindie: "Ndio, ningekuwa nikifanya vivyo hivyo, mara tu baada ya kisanduku cha mpigo kuwashwa."

@callmemisterj: "Bila shaka bundi alikuwa. Mungu, Wadominika na Jamhuri ya Dominika wote ni wa ajabu."

@mrckly: "Nilifikiri walisema ni mchawi na walikuwa wakijaribu kuitisha, lol." abn_ghozt210: Ninaiona kuwa ya kupendeza, lakini katika Amerika ya Kusini na Mexico hii inaweza kuwa roho au ishara mbaya."
Share:

PASTA ALA SUPU NA KUWAPA WAUMINI KIDOLE CHAKE WAKILAMBE KAMA KOMUNYO

Video ya pasta mmoja akiwapa kondoo wake kidole chake walambe kama komunyo imezua ghadhabu kwenye mitandao ya kijamii.

Pasta huyo alikuwa akiwalambisha waumini kidole chake baada ya kula chakula aina ya eba na supu kwenye madhabahu.

 Eba ni chakula kikuu kinacholiwa sana katika ukanda wa Afrika Magharibi, hususan nchini Nigeria na Ghana.

Katika video hiyo, mtumishi huyo wa Mungu anaonyeshwa akichukuwa chakula hicho kutoka kwa mhudumu wa wageni kwenye upande wake kushoto.

 Kisha anaweka kidole kichafu ndani ya mdomo wa muumini mmoja kama komunyo na kukiosha katika beseni iliyokuwa imeshikiliwa na mwanamke mwingine katika upande wa kulia.

Mchungaji huyo mwenye utata alirudia utaratibu huo kwa washarika wote walipokuwa wakienda madhabahuni mmoja baada ya mwingine kupokea 'meza ya Bwana.' 

Si mara ya kwanza pasta huyo kugonga vichwa vya habari na matukio tatanishi anayowafanyia kondoo wake. 

Hivi majuzi alinaswa kwenye video akiwaogesha waumini wa kike kanisani.
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATATU FEBRUARI 7,2022



Rais Samia aagiza mikataba kufutwa kwa wakandarasi walioshindwa kukamilisha ujenzi wa barabara
Share:

RC HAPI CHUPUCHUPU KUFYATULIWA...RAIS SAMIA AGEUKA MBOGO VIONGOZI WOTE WA MARA MTEGONI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipata maelezo kutoka kwa Daktari wa Kitengo cha Magonjwa ya Figo katika Hospitali ya kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Mkoani Mara Dkt. Ridhiwani Said kuhusu maendeleo ya utoaji wa huduma, wakati alipotembelea kukagua maendeleo ya Ujenzi wa Hospitali hiyo iliopo katika Kijiji cha Kwangwa Halmashauri ya Manispa ya Musoma Mjini Mkoani Mara leo tarehe 06 Februari, 2022, Mhe. Rais Samia yupo katika ziara ya Kikazi ya siku nne Mkoani Mara kutembelea kukagua Miradi mbalimbali ya maendeleo ya Wananchi.
****


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amemtaka Mkuu wa Mkoa wa Mara Ally Hapi, Wakuu wa wilaya na Wakurugenzi wa halmashauri za mkoa wa Mara wajitathmini kama wanafaa kuendelea na nyadhifa zao huku akiagiza watu wote waliohusika na ujenzi wa mradi wa makao makuu ya halmashauri ya wilaya ya Bunda vijijini kukaa pembeni kupisha uchunguzi dhidi ya tuhuma zinazowakabili ikiwemo rushwa hali iliyosababisha kukwama kwa mradi huo.


Rais Samia ametoa maagizo hayo mjini Musoma leo Jumapili Februari 6, 2022 baada kupokea taarifa mbalimbali juu ya kukwama kwa miradi ya maendeleo mkoa wa Mara akisema inasikitisha kuona miradi mingi ya maendeleo inashindwa kukamilika kwa wakati huku kukiwa na uongozi kuanzia ngazi ya mkoa hadi wilaya.


"Mkuu wa mkoa ni kama uliota maana leo nilikuwa nimepanga nikufyatue hapa hapa bahati yako umeeleza matatizo haya ya kukwama kwa maendeleo ina maana unafanya kazi na matatizo haya unayajua na umenoyesha umechukua hatua gani una bahati", amesema Rais Samia.


Amesema matatizo ya kukwama kwa maendeleo ya mkoa wa Mara yanasababishwa na viongozi waliopo ambao amedai kuwa ni wabinafsi na wabadhirifu hivyo kuwataka viongozi hao kujitathmini na kwamba suala la utendaji kazi wa viongozi hao anakwenda kulifanyia kazi na maamuzi atayatoa baada ya watu wake kufanya uchunguzi.

Share:

Sunday, 6 February 2022

KAMPUNI YA BETWAY YAZINDUA PROGRAMU YA MABORESHO YA VIWANJA VYA MICHEZO TANZANIA

Kampuni ya michezo ya kubashiri ya kimataifa, Betway Tanzania imezindua rasmi programu yake ya maboresho ya viwanja vya michezo. Programu hiyo ambayo ni sehemu ya kampuni hiyo kurudisha kwa jamii inalenga kuchangia katika juhudi za maendeleo ya sekta ya michezo nchini. Katika kutekeleza azma yake ya kuendeleza sekta ya michezo nchini Tanzania, kampuni ya Betway imeahidi kufanya mambo kadhaa ikiwemo kuchangia moja kwa moja katika maboresho ya miundombinu ya michezo, kuchangia vifaa na zana muhimu za michezo na kudhamini shughuli mbalimbali za michezo.


Kupitia programu hii ya maboresho ya viwanja vya michezo, Betway imepanga kuanza na viwanja vitano vya jijini Dar es Salaam. Kiwanja cha mchezo wa mpira wa kikapu wa Sea View kilichopo Ocean Road, Ilala, Dar es Salaam ni kiwanja cha kwanza kufanyiwa maboresho. Kiwanja hicho ambacho ni moja ya viwanja vyenye historia kubwa katika mchezo wa mpira wa kikapu jijini Dar es Salaam na nchini Tanzania kwa ujumla kimefanyiwa maboresho makubwa yaliyohitajika kukirudisha katika hadhi ya viwanja vya mpira wa kikapu kitaifa.


Uzinduzi wa programu hiyo umeenda sambamba na bonanza la uzinduzi wa kiwanja cha michezo wa mpira wa kikapu cha Sea View ambacho ni kiwanja cha kwanza kufanyia maboresho. Katika uzinduzi huo wadau mbalimbali wa mchezo wa kikapu wamejumuika kwa kushindana na kuburudika huku wakifurahia mandhari mapya ya uwanja huo.


Akizungumza na wadau walioshiriki hafla ya uzinduzi na makabidhiano ya kiwanja cha Sea View iliyofanyika Februari 5, 2022 jijini Dar es Salaam, Afisa Uendeshaji wa Betway Tanzania, Jimmy Masaoe ametaja maboresho yaliyofanyika katika kiwanja hicho ambacho ni sehemu ya kituo cha michezo cha Gymkhana.


“Kama sehemu ya kuimarisha miundombinu ya michezo na kuwafanya watanzania kuipenda na kufurahia michezo tumefanya maboresho makubwa ya uwanja huu ikiwemo maboresho ya majukwaa, eneo la kuchezea, magoli, na taa kwa ajili ya matumizi ya usiku. Maboresho haya yataongeza hadhi ya uwanja huu wenye historia kubwa katika mchezo wa mpira wa kikapu lakini pia utavutia wachezaji wengi wa mpira wa kikapu kufanya mazoezi na kufanya mashindano.” Alisema Masaoe.


Akifafanua kuhusu muendelezo wa program hiyo, Masaoe aliweka wazi kuwa uzinduzi wa maboresho hayo ni mwanzo wa utekelezaji wa awamu ya kwanza ya maboresho ambayo inatarajiwa kuendelea katika mikoa mingine ya Tanzania.

“Uzinduzi wa leo ni mwanzo wa utekelezaji wa awamu ya kwanza ya maboresho ya viwanja vitano katika jiji la Dar es Salaam. Maboresho hayo yamelenga viwanja ambavyo vina matumizi makubwa katika mchezo husika ili kutoa nafasi kwa wanamichezo na mamlaka kuwa na miundombinu yenye hadhi ya kuendesha shughuli za michezo. Tunawasihi wanamichezo na mamlaka za usimamizi kusimamia vyema miundombinu hii ili iweze kuleta tija inayotarajiwa kwenye michezo kwa muda mrefu.” Alisisitiza Masaoe.

Kwa upande wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF), Katibu Mkuu wa shirikisho hilo, Mwenze Fiston ametoa shukurani kwa kampuni ya Betway kwa kuja na programu ya maboresho ya uwanja ambayo imeifaidisha tasnia ya mchezo wa mpira wa kikapu. Fiston aliongeza kwamba wataendelea kuhirikiana na Betway na wadau wengine kukuza mchezo wa mpira wa kikapu nchini Tanzania ili kuongeza ajira kwa watanzania wengi zaidi kupitia mchezo huo.

“Ni furaha kubwa kwetu kuona Betway ambayo ni kampuni kubwa ya michezo duniani imeona na kutambua umuhimu wa mchezo wa mpira wa kikapu hapa nchini na kuamua kuelekeza nguvu katika kuboresha miundombinu ya michezo hiyo. Tumepokea kwa furaha sana program hii na tunaamini haitashia hapa bali itaendelea na mikoa mingine. TBF tunawaahidi kushirikiana na mamlaka nyingine kama Shirikisho la Mpira wa Kikapu jijini Dar es Salaam na Serikali katika kutunza miundombinu ambayo imeboreshwa na Betway ili iweze kusaidia michezo kwa muda mrefu zaidi". Alisema Fiston.


Katika bonanza la uzinduzi michezo mitatu ilichezwa ikiwemo mchezo wa maveterani wa wa mpira wa kikapu wa jiji la Dar es Salaam, mchezo kati ya Dream Team na Dar City kwa upande wa wanawake huku Dar es Salaam All Stars wakichuana na Pwani All Stars kwa upande wa wanaume. Wachezaji na mashabiki wa mpira wa kikapu wameonesha furaha yao kufuatia maboresho ya uwanja huo.
Share:

STANSLAUS NYONGO AJITOSA KUWANIA KITI CHA NAIBU SPIKA


Mbunge wa Maswa Mashariki Stanslaus Nyongo akionesha kwa Waandishi wa habari (hawapo pichani) fomu ya kuomba ridhaa kuwania kiti cha Naibu Spika ambapo ameahidi kuwa iwapo atachaguliwa atakuwa kiongozi mwema.

 Na Dotto Kwilasa Malunde 1 blog - DODOMA.

Mbunge wa Maswa Mashariki, Stanslaus Nyongo amefika Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) jijini Dodoma, kwa ajili ya kuchukua fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea nafasi ya Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Akiongea leo Februari 6,2022 na Waandishi wa habari mara baada ya kuchukua fomu amesema amefikia uamuzi huo kwa kuwa ana sifa nyingi za ziada zinazomtambulisha kwenye masuala ya uongozi.

"Natambua kuwa naweza kuongoza nafasi hii,mbali na ubunge nina sifa nyingi za ziada zinazonifanya nishawishike kuchukua fomu kutetea nafas hii ,"amesema.

Mbunge huyo wa Maswa Mashariki ametumia nafasi hiyo kuwaomba viongozi wake wa Chama kumuamini na kwamba ana matarajio makubwa katika kuwatumikia wananchi na Serikali.

"Endapo nitaipata nafasi hii,nitaitumia vizuri kuishauri Serikali ili kuleta manufaa kwa wananchi,tunatambua kuwa wananchi wa pembezoni wanahitaji Bunge liishauri vizuri Serikali ili wapate kuboreshewa huduma zote za msingi na kuwa na unafuu wa maisha mazuri,"amefafanua Mbunge huyo.


Mbali na kuwa mbunge wa Jimbo la Maswa Mashariki, Nyongo amewahi kushika nyadhifa mbalimbali za uongozi ikiwa ni pamoja na Naibu Waziri wa madini kwa Serikali ya awamu ya tano na Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya huduma na maendeleo ya jamii anayoitumikia hadi sasa.
Mbunge wa Maswa mashariki Stanslaus Nyongo akisaini kitabu cha wageni alipowasili Ofisi ya Itikadi na Oganaizesheni ya CCM Jijini Dodoma.

Mbunge wa Maswa Mashariki Stanslaus Nyongo akiongea na Waandishi wa habari Jijini Dodoma mara baada ya kuchukua fomu ya kuomba ridhaa ya kuwania kiti cha Naibu Spika wa Bunge.
Share:

BENKI YA EXIM, MASTERCARD ZAINGIA MAKUBALIANO KUBORESHA MALIPO YA KIDIJITALI



Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Exim, Bw Jaffari Matundu (Kulia walioketi) na Rais wa Mastercard Kanda ya Africa, Kusini mwa Jangwa la Sahara Bw. Mark Elliot (Kushoto walioketi) wakitia saini makubaliano ya ushirikiano wa miaka 5 ili kuendeleza ubunifu kupitia njia ya malipo ya kidijitali nchini ikiwa pia ni jitihada za benki hiyo za kutoa ufumbuzi wa hali ya juu wa kibenki kwa wateja wake ili kwenda sambamba na mabadiliko ya haraka ambayo sekta ya huduma za kifedha inashuhudia.

 Hafla ya utiaji saini huo ilifanyika Makao Makuu ya Benki ya Exim jijini Dar es Salaam hivi karibuni ikishuhdiwa na wawakilishi kutoka pande zote mbili.
Share:

TMA YATOA ANGALIZO LA MVUA KUBWA NA UPEPO MKALI




Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa angalizo kwa wananchi juu ya hali ya hewa katika siku kadhaa zijazo.

ANGALIZO la mvua kubwa limetolewa kwa maeneo machache ya mikoa ya Morogoro, Iringa, Njombe, Songwe, Mbeya, Ruvuma Lindi na Mtwara.
UWEZEKANO WA KUTOKEA: WASTANI.


KIWANGO CHA ATHARI ZINAZOWEZA KUTOKEA: WASTANI.

JUMATATU 07-02-2022

ANGALIZO la mvua kubwa limetolewa kwa maeneo machache ya mikoa ya Dodoma, Morogoro, Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia), Songwe, Mbeya, Iringa, Njombe, Rukwa, Ruvuma Lindi na Mtwara.

ANGALIZO la upepo mkali unaofikia kilomita 40 kwa saa na mawimbi makubwa yanayofikia mita 2.0 limetolewa kwa baadhi ya maeneo ya ukanda wa pwani ya bahari ya Hindi mikoa ya Lindi, Mtwara, Tanga, Dar es Salaam na Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia) pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.

UWEZEKANO WA KUTOKEA: WASTANI.
KIWANGO CHA ATHARI ZINAZOWEZA KUTOKEA: WASTANI.

JUMANNE 08-02-2022

ANGALIZO la mvua kubwa limetolewa kwa maeneo machache ya mikoa ya Morogoro, Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia), Songwe, Mbeya, Iringa, Njombe, Rukwa, Ruvuma, Lindi na Mtwara.



ANGALIZO la upepo mkali unaofikia kilomita 40 kwa saa na mawimbi makubwa yanayofikia mita 2.0 limetolewa kwa baadhi ya maeneo ya ukanda wa pwani ya bahari ya Hindi mikoa ya Lindi, Mtwara, Tanga, Dar es Salaam na Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia) pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.
UWEZEKANO WA KUTOKEA: WASTANI.
KIWANGO CHA ATHARI ZINAZOWEZA KUTOKEA: WASTANI.



JUMATANO 09-02-2022
ANGALIZO la upepo mkali unaofikia kilomita 40 kwa saa na mawimbi makubwa yanayofikia mita 2.0 limetolewa kwa baadhi ya maeneo ya ukanda wa pwani ya bahari ya Hindi (mikoa ya Lindi, Mtwara, Tanga, Dar es Salaam na Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia) pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba).
UWEZEKANO WA KUTOKEA: WASTANI.

Utabiri huu umetolewa,
Na, MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA
Share:

MHE. RAIS SAMIA ATEMBELEA HOSPITALI YA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE MKOANI MARA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akitembelea Hospitali ya kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Mkoani Mara kukagua maendeleo ya Ujenzi wa Hospitali hiyo iliopo katika Kijiji cha Kwangwa Halmashauri ya Manispa ya Musoma Mjini leo tarehe 06 Februari, 2022, Mhe. Rais Samia yupo katika ziara ya Kikazi ya siku nne Mkoani Mara kutembelea kukagua Miradi mbalimbali ya maendeleo ya Wananchi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipata maelezo kutoka kwa Daktari wa Kitengo cha Magonjwa ya Figo katika Hospitali ya kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Mkoani Mara Dkt. Ridhiwani Said kuhusu maendeleo ya utoaji wa huduma, wakati alipotembelea kukagua maendeleo ya Ujenzi wa Hospitali hiyo iliopo katika Kijiji cha Kwangwa Halmashauri ya Manispa ya Musoma Mjini Mkoani Mara leo tarehe 06 Februari, 2022, Mhe. Rais Samia yupo katika ziara ya Kikazi ya siku nne Mkoani Mara kutembelea kukagua Miradi mbalimbali ya maendeleo ya Wananchi.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger