Friday, 28 January 2022

HELVETAS TANZANIA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI UPANDAJI MITI


AFISA Mazingira Mkoa wa Simiyu Juma Kazula (mwenye tisheti ya kijani) akitoa elimu ya namna ya kuondoa kiriba kabla ya kupanda mti mbele ya wanafunzi wa sekondari Lubiga iliyopo wilayani Meatu mkoani humo, katikati ni Afisa Mazingira wilaya ya Meatu Thomas Shishwa.

***

Na COSTANTINE MATHIAS, Simiyu.

Shirika lisilokuwa na Kiserikali la Helvetas Tanzania lenye makao makuu jijini Dodoma linatarajia kupanda miti zaidi ya elfu 16 mkoani Simiyu ili kuendelea kulinda Uoto wa Asili pamoja na kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi.

Shirika hilo ambalo pia linatekeleza miradi ya elimu, kilimo, vijana na utunzaji wa mazingira na kwamba miradi hiyi inatekelezwa katika mikoa ya Dodoma, Rukwa, Katavi, Mbeya, Singida na Simiyu.

Aidha, Katika mikoa ya Simiyu na Singida ili kuwezesha akina mama kuweka akiba na kukopeshana ili kumudu hali ya uchumi na kujikwamua kimaisha pamoja shughuli za kilimo hai na utuzajia ili kurejesha uoto wa asili ikiwemo kupanda miti.

Afisa Mtathimini na Ufuatiliaji kutoka shirika hilo Loveness Msemwa anaeleza kuwa wanatekeleza miradi ya kuwezesha akina kuweka na kukopeshana, kilimo hai pamoja na utunzaji wa mazingira katika mikoa miwili nchini.

Anasema kupitia mradi wa kilimo hai unaotekelezwa mkoani Simiyu wanashirikiana na kampuni ya Alliance Ginnery na GIZ kutekeleza mradi wa kilimo hai ndani yake wakipanda miti ili kurejesha uoto wa asili kwa ajili ya kutekeleza shughuli za kilimo hai kisichotumia mbolea wala kemikali za viwandani.

‘’Kilimo hai kinahitaji uoto wa asili, mazao yanayozalishwa hayahitaji mbolea za viwandani wala kemikali, hivyo sisi tunatunza mazingira kwa kupanda miti, wenzetu Alliance ginnery wanafundisha wakulima kilimo hai’’ anaeleza Loveness.

Anafafanua kuwa katika mkoa wa Simiyu, mradi huo unatekelezwa wilaya ya Meatu kwenye kata za Kisesa na Lubiga na wanatarajia kupanda miti 16,715 kwenye taasisi za umma na kila mwananchi atagawiwa miti mitano mitano bure.

‘’Lengo ni kuboresha mazingira katika taasisi za umma, kurejesha uoto wa asili na kufanya utunzaji wa mazingira endelevu…tumejikita kwenye taasisi za umma kwa sababu zina rasilimali watu wa kutunza miti hiyo’’ anasema Loveness.

Anafafanua kuwa kupitia kugawa miti mitano kila kaya, jumla ya kaya 2343 zatapanda miti na wataendelea kufuatilia ukuaji wa miti hiyo kwa sababu mradi huo unatekelezwa kwa muda wa miaka mitatu.

Anasema kuwa wameshakutana na wananchi kupitia mikutano ya vijiji ili kuunda kamati za mazingira za vijiji na kwamba wajumbe wa kamati hizo wamekuwa mabalozi wazuri wa upandaji miti.

Anafafanua kuwa kamati hizo zimewasaidia kuzifikia taasisi za umma ikiwemo shule, zahanati, misikiti na makanisa na kwamba hadi sasa kila mwananchi anashiriki kupanda miti nyumbani kwake na kwenye taasisi.

Ofisa Mazingira wilaya ya Meatu Thomas Shishwa anawashukuru wadau wa maendeleo wanaojitokeza kupanda miti wilayani humo huku akiwataka wananchi kuunga mkono juhudi hizo kwa kupanda miti katika maeneo yao.

Anasema lengo la Halmashuri ni kupanda miche milioni 1.5, kupitia kwenye taasisi za umma ikiwemo shule za msingi na sekondari, zahanati, vituo vya afya pamoja na nyumba za ibaada lakini pia kila mwananchi atahakikisha anapanda miti mitano.

Hivi karibuni, Afisa Mazingira Mkoa wa Simiyu Juma Kazula alishiriki uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti iliyofanyika katika kata za Lubiga na Kisesa wilayani Meatu mkoani humo, na kuwataka wadau wa mazingira kujitokeza kuunga mkono juhudi za serikali kwenye upandaji miti.

Kupitia Mradi wa utunzaji mazingira unaotekelezwa na Helvetas Tanzania, Kazula anawataka wadau na wananchi kupandaji miti ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi ambayo yanasababisha madhara makubwa kwa binadamu, wanyama na mimea.

Anayataja madhara hayo kuwa ni ukosefu wa mvua ambao husababisha ukosefu wa malisho, ukame, kukauka kwa vyanzo vya maji, kuongeza kwa joto, mmonyoko wa udongo na kuongezeka kwa hewa ukaa.

Kazula anataka jamii kutunza miti iliyopo pamoja na kuongeza kasi ya upandaji ili kuongeza uoto wa asili ambao unachangia kuleta mvua, kulinda vyanzo vya maji pamoja na kupunguza hewa ya kabondayoksaidi. 

Kazula anawashukuru wadau hao wa maendeleo kwa juhudi za kushirikiana na serikali kupanda miti ili kurudisha hifadhi ya mazingira ambayo ilikuwa imeanza kupotea kutokana na ongezeko la ukataji miti ovyo.

‘’Tunawashukuru Helvetas Tanzania kwa kushiriki kupanda miti wilaya ya Meatu ambao watatusaidia kufikia malengo ya upandaji miti…mpango wetu kila Halmashauri ni kupanda miti milioni 1.5 na kufanya mkoa mzima kuwa na jumla ya miti milioni 9 kwa mwaka mzima’’ Anasema Kazula.

Anasema wanaendelea kushirikiana na Wakala wa Misitu (TFS) pamoja na wazalishaji wengine wa miti ikiwemo kampuni ya Alliance ginnery ili kuifanya Simiyu kuwa ya kijani, huku akimtaka kila mwananchi kupanda miti mitano mitano katika eneo analoishi.

Anaongeza kuwa kupitia Helvetas Tanzania wamejikita zaidi kupanda miti kwenye taasisi za umma ikiwemo shule za msingi na sekondari, makanisani, misikitini pamoja na zahanati ili miti hiyo iweze kusimamiwa ipasavyo.

Oscar Kanuda mkazi wa Lubiga anawataka wananchi wenzake kushiriki kikamilifu upandaji miti katika maeneo yao ili waweze kurejesha uoto na asili hali ambayo tapungua majanga ya asili ikiwemo ukosefu wa mvua na ukame.

‘’Tunaishukuru serikali na wadau kwa kutuletea miti mpaka majumbani kwetu, niwaombe wananchi wenzangu tupande miti ili iweze kutusaidia baadae…miti inaleta mvua, inazuia upepo na pia inatunza vyanzo vya maji’’ anasema Kanuda.

Dotto Saimon Mwanafunzi wa darasa la saba shule ya msingi Lubiga aliwashukuru wadau wa mazingira kwa kuwaletea miti shuleni kwao ambapo alisema ikikua itazuia upepo, itatunza mazingira na vyanzo vya maji pia wataweza kupata kuni.

Naye Kabula Salehe mwanafunzi wa darasa la saba Lubiga shule ya msingi aliwataka wafunzi wenzake kuendelea kuitunza miti hiyo itakayowasaidia wanafunzi kupata hewa safi na kivuli wawapo shuleni.

Leticia Erasto mwanafunzi wa shule ya sekondari Lubiga anasema ameshiriki zoezi la upandaji miti shuleni hapo, huku akiwataka walimu kuwagawia wanafunzi kila mmoja miche ya miti ili aweze kuisimamia kuliko kuipanda kiholela.

‘’Tunawashukuru wadau walioleta miti shuleni, lakini niwashauri walimu wetu kila mwanafunzi agawiwe miti angalau miwili apande na kuisimamia hadi ikue ili tuweze kufika lengo la serikali pamoja na wadau la kupanda miti’’ anasema Mwanafunzi huyo.

Leticia anaiomba serikali kuendelea kutoa elimu kwa wananchi juu ya faida za upandaji miti ambapo baadhi ya maeneo yameathiriwa na ukosefu wa mvua, ukame na kuongezeka kwa joto ili jamii iweze kubadilika na kupanda miti ya kutosha.

Costantine Phabian, Afisa Kilimo kutoka Kampuni ya Alliance Ginnery anasema kampuni yao inajikita na kilimo hai ambacho hakitumii kemikali za viwandani na kinasaidia utunzaji wa mazingira na vyanzo vya maji.

Anasema wanashirikiana na Helvetas kwenye mradi wa kilimo hai na ndani yake wanapanda miti katika kata za Kisesa na Lubiga ambapo Alliance wanahudumia wakulima kwenye vikundi vya kilimo hai wakiwa na lengo moja na kutunza mazingira.

‘’sisi sote ni wadau wa mazingira, lengo la kilimo hai ni kuhifadhi mazingira na kutunza uoto wa asili, kurutubisha ardhi na kulinda vyanzo vya maji pamoja na viumbe wengine…tunafundisha wakulima kuhifadhi ardhi na kutokata mito ovyo’’ anasema Phabian.

Uchunguzi uliofanywa na Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Masuala ya Jamii (ESRF) mwaka 2003 umebainisha kuwa mambo makuu yanayosababisha umaskini ni uchumi duni, uharibifu wa mazingira na kukosekana kwa utawala bora.

Sera ya Mazingira ya mwaka 1997 imeainisha matatizo makuu sita ya mazingira yanayoikabili nchi yetu, ambayo ni Uharibifu wa ardhi, Kutopatikana kwa maji safi kwa wakazi wa mjini na vijijini, Uchafuzi wa mazingira, Upotevu wa makazi ya viumbe pori na bioanuai, Uharibifu wa makazi ya viumbe wa majini na Uharibifu wa misitu.

Kutokana na Sera ya Taifa ya Misitu ya mwaka 1998, Sera ya Taifa ya Hifadhi za Mazingira ya mwaka 2004 na Programu mbalimbali za kuhamasisha upandaji miti kila mwaka, ni dhahiri kuwa Serikali inahimiza wananchi na taasisi zishiriki kikamilifu katika suala la kupanda miti. 

Upandaji miti unaweza kufanywa na taasisi za serikali, makampuni ya wawekezaji, vikundi vya jamii, shule na hata watu binafsi na Watanzania wengi sasa hivi wanaelewa kuwa uchumi wa nchi na maisha yanategemea sana mazingira bora. 

Miti inaweza ikapandwa peke yake ikawa msitu, mti mmoja mmoja katika shamba, kuzunguka shamba, katika maeneo ya makazi, kando kando ya barabara na penginepo kwa kuzingatia ushauri wa wataalamu.

Mzee Oscar Kanuda (kushoto) akiwa na wanakiji wenzake wakishiriki zoezi la upandaji miti lililofanyika hivi karibuni shule ya msingi Lubiga, zoezi hilo liliratibiwa na shirika lisilokuwa la kiserikali la Helvetas Tanzania.
Wanafunzi wa shule ya Sekondari Lubiga iliyopo wilaya ya Meatu mkoa Simiyu wakishiriki zoezi la upandaji miti lililokuwa likiendeshwa na shirika la Helvetas Tanzania hivi karibuni.
Wanafunzi wa shule ya msingi Lubiga iliyopo wilaya ya Meatu mkoa Simiyu wakishiriki zoezi la upandaji miti lililokuwa likiendeshwa na shirika la Helvetas Tanzania hivi karibuni.
AFISA Mazingira wilaya ya Meatu Thomas Shishwa (aliyechumaa) akikata kiriba kwa ajili ya kupanda miti shule ya msingi Lubiga iliyoko wilaya ya Meatu mkoani Simiyu.
Share:

KITUO CHA ELIMU, USHAURI-TAASISI YA USTAWI WA JAMII CHAPIGA KAMBI SOKO LA KARUME


Banda la kituo cha elimu ushauri na msaada wa kisaikolojia cha Taasisi ya Ustawi wa Jamii lililopo katika uwanja wa ukumbi wa Jiji ilala ambapo huduma ya ushauri na elimu inatolewa bure kwa wafanyabiashara wahanga wa moto uliotokea soko la mchikichini karume Ilala Jijini Dar es Salaam.

Kutoka Kushoto mwenyekiti wa wafanyabiashara walemavu soko la mchikichini Mzee Juma Hamis akisikilizwa kwa umakani mkubwa na maafisa ustawi wa jamii Rukia Mwinyi kutoka kituo cha elimu, ushauri, na msaada wa kisaikolojia (Taasisi ya Ustawi wa Jamii) pamoja na Bi. Lilian Chilo afisa Ustawi wa jamii kutoka Ofisi ya Jiji la Dar es Salaam.

Baadhi ya wafanya biashara waliofika kwenye uwanja wa ukumbi wa jiji Ilala soko la mchikichini kupata huduma ya ushauri na elimu kutoka kwa maafisa Ustawi wa jamii wa kituo cha elimu na ushari cha Taasisi ya Ustawi wa Jamii na Jiji la Dar es salaam.

Msaikolojia kutoka kituo cha elimu na ushauri Taasisi ya Ustawi wa Jamii Dkt. Zainab Rashid akitoa huduma kwa mfanya baishara mlemavu Bw. Jamal Nassoro Lemu wa soko la mchikichini Ilala ambapo huduma ya elimu na ushauri inatolewa kwa wafanyabiashara wahanga wa moto sokoni hapo hasa wale wenye mahitaji maalum.

Mratibu wa kituo cha elimu, ushauri na msaada wa kisaikolojia Bi Rufina Khumbe akimhudumia mfanyabiashara wa bajaj eneo la soko la mchikichini Bi Ashura Sadiki katika uwanja wa ukumbi wa jiji ilala Dar es Salaam.

Maria Mayanzini afisa ustawi wa Jamii wa kituo cha elimu na ushauri na msaada wa kisaikolojia – Taasisi ya Ustawi wa Jamii akimsikiliza kwa makini mmoja wa wafanya biashara waliofika kupata huduma katika banda la kituo cha elimu na ushauri cha Taasisi ya Ustawi wa Jamii.

****************

Timu ya wataalam wa ustawi wa jamii na saikolojia kutoka kituo cha elimu, ushauri na msaada wa kisaikolojia kilicho chini ya Taasisi ya Ustawi wa Jamii imepiga kambi viwanja vya ukumbi wa jiji, Dar es Salaam kutoa huduma ya elimu, ushauri na msaada wa kisaikolojia.

Huduma hiyo inatolewa bure kwa wafanyabiashara wa soko la mchikichini maarufu Karume, hususani; walio katika kundi maalum, ambao ni wahanga wa janga la moto lilitokea Januari 16, mwaka huu.

Mratibu wa kituo hicho cha elimu na ushauri Bi. Rufina Khumbe amesema Taasisi ya Ustawi wa Jamii iliona ni vyema kwenda kutoa huduma hiyo kwa waathirika wa janga hilo ambao wanauhitaji mkubwa kwa wakati huu.

“Taasisi imekuwa ikitoa huduma kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ili kuhakikisha tunastawisha jamii yetu, kwa kutatua changamoto mbalimbali pia kama Taasisi mama chini ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum tumeguswa, na ni jukumu la kituo chetu cha ushauri kuja kutoa huduma ya elimu hii na ushauri ili wafanyabiashara hawa hasa wenye uhitaji waweze kulipokea hilo na kulikubali kama changamoto” alisema Bi Khumbe.

Bi. Rufina ameongeza kuwa kutokana na janga hilo la moto wengi wao wamekata tamaa ya maisha, kwasababu mali zilizokuwa zinawaingizia kipato na mitaji vimeteketea na moto huku wengine walichukua mikopo ili kukuza na kuanzisha biashara.

"Mali zimeteketea na hawajui wanalipaje hiyo mikopo. Ndio maana Taasisi ikaona ni vyema kuongea na wafanyabiashara hawa ili kuwapa tumaini tena la maisha yao," amesema Bi. Rufina.

Kwa upande wake msaikolojia kutoka Kituo hicho Dkt.Zainabu Rashidi amesema “tunatoa elimu juu ya kujikinga na majanga mbalimbali ikiwa ni pamoja na moto, mafuriko na pia tunatoa elimu ya namna ya kuyakubali na kuishi na majanga na matatizo baada ya kutokea”.

Aidha Dkt. Zainabu amesema watu wengi wanajua wakifika katika banda la Taasisi ya Ustawi wa Jamii (kituo cha elimu shauri na msaada wa kisaikolojia) watapata msaada wa fedha kwa ajili ya mitaji yao ya biashara.

“Jamii yetu haina uelewa juu ya umuhimu wa huduma ya ushauri na msaada wa kisaikolojia kama tiba ya namna ya kupata suluhu ya matatizo yao kwa kuzungumza na wataalam. Jamii haiamini katika ushauri pekee hivyo tuko hapa ili kuondoa hiyo dhana” amesema Bi. Zainabu.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara wenye ulemavu soko la Mchikichini (karume), mzee Juma Hamisi amesema anashukuru Taasisi ya Ustawi wa Jamii kwa elimu,ushauri, na msaada wa kisaikolojia.

“Tumepokelewa vizuri tumepata msaada wa ushauri wa kisaikolojia na elimu na tumewasikia, elimu hii inatupa ujasiri na tumejua kuwa janga hili lililotupata sio letu tu bali ni letu sote” amesema mzee Juma na kuongeza:

“Naishukuru serikali ya awamu ya sita kupitia Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi maalumu kwa kusikia sauti yetu na kuja kutupa msaada wa kisaikolojia na ushauri”.

Zaharan Sulemani mfanyabiashara wa leso, soksi na madaftari katika soko hilo ametoa shukrani kwa Taasisi na kusema kuwa elimu hiyo imewapa ujasiri wa kuanza upya.

“Tunashukuru Taasisi ya Ustawi wa Jamii kwa kuja kutoa elimu, ushauri na msaada wa kisaikolojia kwa wahanga wa janga la moto pia namshukuru mama Samia Suluhu Hassan kwa kutuweka sisi wamachinga kwenye kundi maalumu chini ya Wizara hii ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum kwani tunaaini tutapata usaidizi na usimamizi wa karibu zaidi utakaotufaidisha katika biashara tunazofanya”.

Pia Jumanne Kongogo mwenyekiti wa jumuia ya wafanyaniashara sokoni hapo ametoa wito kwa wafanyabiashara wa soko la karume kwenda kupata huduma hiyo ya elimu na ushauri kwenye banda la Taasisi ya Ustawi wa Jamii.

Ameiomba serikali iangalie jinsi itakavyo jenga soko ambalo miundombinu yake itakidhi kwa wafanyabiashara wenye uhitaji maalumu .

Naye mratibu wa huduma za ustawi wa Jamii kutoka Mkoa, Afisa Ustawi wa Jamii kutoka Jiji la Dar es Salaam Bi. Lilian Chilo ametoa wito kwa wafanyabiashara wa soko la mchikichini kujitokeza kupata huduma inayoendelea kutolewa katika uwanja wa ukumbi wa jiji Ilala kwa siku kumi na nne (14) ambapo huduma hiyo ilianzia katika viwanja vya mnazi mmoja.

Taasisi ya Ustawi wa Jamii chini ya Wizara mpya ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum inaunga mkono jitihada za Mh. Rais kutambua wamachinga kama kundi maalum, pamoja na makundi mengine katika jamii yetu.

Zaidi kwa kutoa kipaumbele na umuhimu wa pekee kwa makundi haya kupata huduma za Ustawi wa Jamii ili kuinua na kuboresha hali zao maisha na hasa pindi kunapotokea majanga mbali mbali kama hili la moto katika soko la mchikichini karume.

Taasisi ya Ustawi wa Jamii itaendelea kutoa ushauri wa kitaaluma na ushauri nasaha na msaada wa kisaikolojia kwa jamii ya watanzania na makundi maalum kama sehemu ya jukumu lake la kutoa ‘’Ushauri Weledi” katika fani bobezi.
Share:

LORI LAUA WATEMBEA KWA MIGUU KIMARA SUKA , DEREVA AKIMBIA



Watu wawili wamepoteza maisha na wengine nane (8) kujeruhiwa, hii leo Januari 28, 2022, katika ajali iliyohususha lori na watembea kwa miguu maeneo ya Kimara Suka Jijini Dar es salaam, baada ya dereva wa lori hilo kupita kwenye kivuko cha watembea kwa miguu bila kuchukua tahadhari.

Taarifa ya ajali hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro, na kusema kuwa ajali hiyo imesababishwa na uzembe wa dereva wa lori ambaye amekimbia baada ya kusababisha ajali hiyo.

Aidha Kamanda Muliro, amesema kuwa majeruhi wote katika ajali hiyo walikimbizwa katika hospitali ya Bochi.

Mashuhuda wa ajali hiyo wameeleza kuwa chanzo cha ajali hiyo gari hilo lilionekana kupoteza mwelekeo baada ya kufeli breki na kuwapitia watembea kwa miguu waliokuwa eneo hilo hivyo kusababisha vifo vyao na majeruhi.

“Mimi nimesimama pembeni naona gari linanifuata na lilikuwa katika spidi kubwa sana niliruka mtaroni ndicho kilichonisaidia bila hivyo sijui,” amesema John Kelvin aliyekuwa amepaki boda boda yake pembeni.

“Rafiki yangu mshtuko alikimbia mbio limemkuta huko huko nikamuona anaingia chini ya lori ndio wamemtoa ameshakufa jamani,” amesema.

Mmoja wa ndugu wa majeruhi ambaye hakuta jina lake kuandikwa amesema amefuatwa nyumbani na boda boda akaambiwa mke wake Aisha amekatika sikio.

“Nilitoka nyumbani haraka sana, nilikuwa mke wangu amewekwa kwenye Kirikuu nikamtoa nimeleta mwenyewe hapa Bochi nikasaidia na wengine wawili.
“Ajali ni mbaya jamani maana imewafuata watu pembeni mimi mke wangu alikuwa anaenda kazini jamani hali yake sio nzuri,” amesema.






Share:

KIOJA BAADA YA POLO MWANA-BODABODA, ALIYEMTAFUNA MKE WANGU KUKWAMA

Tuliishi na mke wangu katika jiji la Nairobi ambapo nilikuwa mwanabiashara jijini. Mara nyongi niliacha mke wangu pale nyumbani kwakua sikupenda akienda kazini kwani alikua ni mrembo ajabu na niliogopa iwapo angeenda kazini ingesambaratisha uhusiano wetu. 

Kwa mara nyingi nilihofia hata atembee kwenda dukani kwani nilihofia angenyakuliwa wakati wowote wanaume wenye tamaa. Ndoa yetu haikukumbwa na misukosuko kwa wakati wowote kwani tuliaminiana pakubwa.

 Ilifikia wakati ambapo nilitafuta kalameni mwanabodaboda ili awe akisambaza bidhaa za nyumba ambazo mke wangu alihitaji kila mara kwani sikufurahia mke wanhu akizurura kila mara. Basi jukumu hilo la usambazaji wa bidhaa nilimpa polo yule. 

Baada ya siku kadhaa za usambazaji wa bidhaa pale nyumbani, mwanabodaboda yule aliichukua fursa ile kumchanganya mke wangu akamtongoza na akaichukua nambari yake ya simu walioitumia kuwasiliana kila mara. 

Siku moja nilipata ujumbe kwenye simu ya mke wangu kwamba mwanabodaboda yule alikua akimshukuru akimsifu kuwa yeye ni mrembo wa kupendeza ajabu na hastahili kupendwa na mwanaume tu yeyote bali mtu kama yeye. 

Ujumbe huu ulinipandisha mori na nilipomuliza mke wangu kilichokuwa kikiendelea alikana kutohusiana na ujumbe ule kwani hata alisema kuwa ilikua ni nambari asiyoifahamu kamwe. Sikua na lolote la kuongeza wala kupunguza kwani tayari nilikua nimevunjika mtima.

Nilifahamu kua mwanabodaboda yule alikua akichovya asali yangu. Sikusitisha kazi yake ya kusambaza bidhaa pale nyumbani kwani siku moja nilifahamu fika kwamba ningemnasa hadharani mbele ya adinasi. Ingawaje niliendelea kusononeka moyoni sikua na budi kupiga moyo konde na kuendelea na shughuli zangu za kibiashara licha ya maovu niliyokuwa nikijua mke wangu alikua akifanya na polo mwanabodaboda mwenye tamaa. 

Siku moja rafiki yangu Ken alinitembelea kwenye duka langu na akapigwa na mshangao jinsi nilivokua nimesononeka. Nilimwelezea yote yaliyokua yanafanyika kwenye ndoa yangu. Alinielezea huo hakuwa mwisho wa mambo bali tu ulikua mwanzo wa mkoko kualika maua. Sikuelewa vizuri aliponieleza hivi kwani nilikua kabisa nimefinyika na tabia ya mke wangu japo nilimpenda kwa dhati nisimgombeze.

 Ken alinifungulia mtandao www.kiwangadoctors.com ambapo palikuwa na simulizi kama niliyokuwa napitia ambapo daktari Kiwanga alisuluhisha mambo yote. 

Nilimpigia daktari Kiwanga simu na akanitengea nafasi niweze kumtembelea katika ofisi zake. Mke wangu hakujua lolote kuhusu hili. 

Siku iliyofuatia nilifika afisini mwa daktari Kiwanga mapema tayari kuhudumiwa. Nilimaliza muda wa dakika thelathini unusu hivi na daktari akasema kua mambo yangu yalikua shwari.

 Nilirejea mjini kwenye biashara yangu. Jamaa yule wa bodaboda alikuja dukani kama kawaida yake kupelekea mke wangu bidhaa nyumbani.

 Ingawaje nilijua alichoenda kufanya baadaye sikuwa na shaka kwani daktari Kiwanga alikuwa amenihakikishia hali iko shwari kabisa.

 Baada ya dakika chache hivi nilipokea simu iliyokua inaniamrisha nifike nyumbani kwa haraka. Nilifunga biashara zangu na kukimbia nyumbani. Nilipigwa na butwaa nilipoona umati wa jinsi ulivyokuwa umejaa kwenye sehemu ya nyumba yetu.

 Sikufahamu fika ni kipi kilikua kimetokea. Nilipofika ndani ya nyumba nilipata kalameni yule wa bodaboda wakiwa wamekwamana na mke wangu kwenye kochi wakishiriki mapenzi. Walikuwa wanalia maumivu. Nilijiambia moyoni kwamba daktari Kiwanga ndio mambo yote na kuwa hakunidanganya yeye ndiye daktari bora kwenye ukanda wa Afrika Mashariki.

 Hili lilidhihirika wazi na mambo niliyoyaona chumbani mwangu. Baadaye nilimpigia daktari Kiwanga na mwanabodaboda yule alitakiwa kulipa kiasi cha shilingi elfu hamsini kutatua mambo.

 Familia yake ililipa pesa zile na daktari Kiwanga akafanya mambo yake akawakwamua. Tangu siku ile tuliishi kwa amani na mke wangu kwani tuliaminiana hata zaidi. 

Tuliishi kwa upendo na furaha. Mtu yeyote anayekumbwa na misukosuko sampuli hii kwenye ndoa namshauri atembelee dakatri Kiwanga kwa kuwa ndiye mwalimu wa suluhisho. Anasuluhisha biashara isiyo dhabiti, mapenzi yenye misukosuko, kukomesha uchawi na mambo mengineyo kwa siku tatu pekee. Waweza kumpata Dkt. Kiwanga kupitia wavuti www.kiwangadoctors.com barua pepe kiwangadoctors@gmail.com au piga simu kwa nambari +254769404965.
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO IJUMAA JANUARI 28,2022



Share:

Thursday, 27 January 2022

MTALII AKANYANGWA NA TEMBO HADI KUFA


MTALII mmoja amekanyagwa hadi kuuawa na Tembo katika mbuga ya wanyama nchini Uganda, baada ya mtalii huyo kutoka kwenye gari alilokuwa akisafiria tukio hilo lilitokea Jumanne usiku.

Marehemu, ambaye ni raia wa Saudia, alikuwa akitalii kwenye mbuga ya taifa ya wanyama ya Murchison Falls National Park iliyopo katika mji la Arua.

Inadaiwa kuwa marehemu pamoja na wenzake waliposimama kujisaidia. na alikwenda mbali zaidi ya gari, hakuweza kurejea.

Maafisa wa mbuga ya Wanyama walithibitisha tukio hilo na walisema upelelezi unaendelea walisema kuwa hatua zinachukuliwa kuzuwia matukio ya aina hiyo kutokea tena.
Share:

Tanzania, Morocco Zakubaliana Kuimarisha Ushirikiano


Tanzania na Morocco zimekubaliana kuimarisha ushirikiano katika nyanja za biashara na uwekezaji, elimu, utalii, uwezeshaji wa kiuchumi kwa wanawake na vijana.

Makubaliano hayo yamefikiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Morocco Bw. Nasser Bourita walipofanya mkutano wa kwa njia ya mtandao. Balozi Mulamula ameshiriki katika mkutano huo akiwa katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

“Tumezungumzia masuala ya kuimarisha uhusiano wetu baina ya Tanzania na Morocco na tumepitia makubaliano yaliyofikiwa wakati wa ziara ya Mfalme wa Morocco alipotembelea Tanzania mwaka 2016 pamoja na kuangalia mikataba mbalimbali iliyotiwa saini wakati wa ziara ya Mfalme wa Morocco ……… laikini pia tumejadili umuhimu wa kuwa na tume ya pamoja ya ushirikiano,” Amesema Balozi Mulamula.

Katika mkutano huo, viongozi hao wamejadili na kukubaliana kuimarisha ushirikiano wa karibu katika sekta za biashara na uwekezaji, utalii, elimu hasa katika kuongeza idadi ya ufadhili wa masomo kwa watanzania kutoka wanafunzi 30 hadi 50.

“Morocco ni nchi inayopata watalii wengi, hivyo tumekubaliana kushirikian kwa karibu zaidi ili kuweza kupata uzoefu ni njia gani wanatumia katika kukuza sekta ya utalii,” ameongeza Balozi Mulamula.

Katika tukio jingine, Balozi Mulamula amekutana na kufanya mazungumzo na Kaimu Balozi wa Oman nchini Dkt. Salim Saif Al Harbi katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

Mazungumzo ya viongozi hao yamelenga kujadilia masuala mbalimbali ya kuendeleza na kuimarisha ushirikiano uliopo baina ya Serikali ya Tanzania na Oman.


Share:

Mauaji Dodoma:dk.mpango Atoa Siku Saba


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango ametoa siku saba kwa vyombo vya upelelezi nchini kuhakikisha wahalifu waliotekeleza mauaji ya watu wa tano wa familia moja katika Kijiji cha Zanka wilaya ya Bahi mkoani Dodoma wanapatikana.

Makamu wa Rais amesema hayo alipotemblea Kijiji cha Zanka kuwapa pole na kuwafariji wafiwa pamoja na kuzungumza na wananchi wa eneo hilo.

Makamu wa Rais ameoneshwa kusikitishwa na kitendo cha mauaji ya wanafamilia hao licha ya kuwepo kwa majirani wengi wanaozunguka eneo hilo. Amesema jamii inapaswa kubadilika na kuishi kama ndugu pamoja na kuchukua tahadhari kwa wageni wote wanaoingia na kutoka katika vijiji hivyo.

Katika hatua nyingine Makamu wa Rais ameliagiza jeshi la Polisi nchini kuchukua hatua kukomesha vitendo vya mauaji yanayojitokeza hapa nchini. Amesema hivi karibuni maeneo mbalimbali ya nchi vimeibuka vitendo vya mauaji hivyo ni lazima wahusika kuchukuliwa hatua kali za kisheria ili iwe fundisho kwa wengine.

Makamu wa Rais amemuagiza Mkuu wilaya ya Bahi pamoja kamati ya Ulinzi na usalama ya a wilaya kufanya mkutano na wananchi wa eneo hilo ili kuimarisha ulinzi wa maeneo hayo.

Aidha ameuagiza uongozi wa Kijiji cha Zanka kufanya vikao vya mara kwa mara juu ya ulinzi na usalama wa maeneo hayo.

Makamu wa Rais amewasilisha rambirambi kwa niaba ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa familia hiyo iliopoteza watu watano na kuwaeleza kwamba Rais ametoa pole na amesikitishwa na mauaji hayo.

Baadaye Makamu wa Rais amefanya mkutano na wananchi wa kata ya Zanka na maeneo jirani na kuwasihi wananchi wa Kijiji cha Zanka na watanzania kwa ujumla kutafuta namna ya kutatua migogoro ikiwemo kutumia vyombo vya sheria badala ya kufanya matukio ya mauaji.

Makamu wa Rais amewaomba viongozi wa dini kuendelea kutoa mafundisho ya kukemea vitendo vya uhalifu ikiwemo mauaji hapa nchini.

Miili ya watu hao watano wa familia moja baba, mama, watoto wawili na mjuku mmoja walikutwa wameuwawa ndani ya nyumba yao Januari 22 mwaka huu na miili yao kutelekezwa.



Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo January 27



Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger