Thursday, 27 January 2022
Wednesday, 26 January 2022
MTATURU ASISITIZA VIPAUMBELE MFUKO WA JIMBO
BODI YA FILAMU YAWATAKA WADAU KWENDA NA TEKNOLOJIA
MIGODI YA BARRICK NCHINI TANZANIA MBIONI KUFIKIA DARAJA LA KWANZA LA UZALISHAJI
WAZIRI BITEKO : UBIA BAINA YA SERIKALI NA BARRICK UMELETA TIJA KUBWA
Tuesday, 25 January 2022
MRADI WA AKILI BANDIA WAZINDULIWA UDOM
WADAU WA MASUALA YA ELIMU WAGUSWA NA MPANGO MKAKATI WA MAMLAKA YA ELIMU TANZANIA (TEA)
Wadau kutoka sekta na Idara mbalimbali za Serikali wamekuta leo jijini Dar es Salaam kujadili rasimu ya mpango mkakati wa nne wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) ambao utatumika kwa miaka mitano hadi 2026. Katika kikao kazi hicho cha siku moja, wadau wamefurahishwa na jinsi ambavyo TEA imeweka vipaumbele katika mambo ya kimkakati ikiwemo TEHAMA.
Katika majadiliano hayo, Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) imepongezwa kutokana na jitihada zake za kusimamia na kuboresha miundombinu ya Elimu hasa katika mazingira ambayo ni magumu kufikika kwa lengo la kuongeza upatikanaji wa elimu bora na kwa usawa.
Mkurugenzi Msaidizi kutoka TAMISEMI Bw. Musa Otieno ambaye alikuwa mmoja wa wadau katika kikao hicho amesema, TEA imefanya kazi nzuri sana ya kuboresha miundombinu ya shule ambapo imejenga madarasa, nyumba za waalimu, matundu ya vyoo, mabwalo ya vyakula pamoja na kununua madawati kwenye maeneo ya pembezoni mwa miji ambako ni ngumu kufikika.
Jitahada zote hizi zinalenga kusogeza huduma za sekta ya elimu karibu na wananchi ili kuhakikisha kila mtoto anapata nafasi ya kusoma karibu na mazingira anayoishi na hili linadhihirika wazi kwani mpango mkakati wa miaka mitano ijayo umebainisha kazi zinazooenda kufanyika katika kusimamia upatikanaji wa elimu bora, alisema Otieno
Nae mdau mwingine kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bw.Gerald Sando, ameishukuru Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) kwa kazi zake na kusema kazi hizo ni endelevu na zinaonekana kwa macho.
Sando amesema, kazi za TEA zinagusa maisha ya wananchi moja kwa moja na kuongeza thamani kwenye maisha ya wale wa kipato cha chini kupitia mradi wa kuongeza ujuzi (SDF) ambao unafadhiliwa na TEA.
Kikao kazi cha kupitia rasimu ya mpango mkakati wa Mamalaka ya Elimu Tanzania (TEA) wa miaka mitano hadi 2026 kimefanyika jijini Dar es Salaam na mgeni rasmi alikuwa Mkurugenzi Mkuu Bi. Bahati Geuzye.
Akitoa salaam za ukaribisho Mkurugenzi wa huduma za Taasisi Dr. Erasmus Kipesha ambaye alikuwa mwenyekiti wa kikao hicho alisema, tangia Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) imeanzishwa mwaka 2001, hii ni rasimu ya nne ya mpango mkakati.
Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) ni Taasisi ya umma iliyoanzishwa kwa Sheria ya Mfuko wa Elimu Na. 8 ya mwaka 2001 ikiwa na jukumu la kusimamia uendeshaji wa Mfuko wa Elimu wa Taifa kwa lengo la kuongeza nguvu za Serikali katika kuinua upatikanaji wa elimu bora kwa usawa katika ngazi zote za elimu Tanzania Bara na elimu ya juu kwa Tanzania Zanzibar.
Mkurugenzi wa huduma za Taasisi kutoka Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Dkt. Erasmus Kipesha akitoa salaam za ukaribisho kwa wajumbe (hawapo pichani) waliohudhuria kikao kazi cha siku moja kujadili rasimu ya mpango mkakati wa miaka mitano wa TEA.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Bi. Bahati Geuzye akitoa hotuba ya ufunguzi katika kikao kazi cha siku moja cha kujadili rasimu ya mpango mkakati wa miaka mitano wa TEA kwa wadau wa masuala ya elimu (hawapo pichani)
Baadhi ya wadau waliohudhuria kikao kazi cha siku moja wakifuatilia uwasilishwaji wa rasimu ya mpango mkakati wa miaka mitano wa TEA.
Baadhi ya wadau waliohudhuria kikao kazi cha siku moja wakifuatilia uwasilishwaji wa rasimu ya mpango mkakati wa miaka mitano wa TEA.
Mkurugenzi Msaidizi kutoka Ofisi ya Rais -TAMISEMI Bw. Musa Otieno akichangia maoni yake kuhusu rasimu ya mpango mkakati wa miaka mitano wa TEA
Bw.Gerald Sando kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa – Dar es Salaam akitoa maoni yake kuhusu rasimu ya mpango mkakati wa miaka mitano wa TEA.
Mkurugenzi wa huduma za Taasisi kutoka Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Dkt Erasmus Kipesha akiwasilisha rasimu ya mpango mkakati wa miaka mitano wa TEA kwa wadau wa masuala ya elimu.
WASINDIKAJI NA WAZALISHAJI WA MAZIWA WAMETAKIWA KUHAKIKISHA BIDHAA HIZO KUWA BORA
Monday, 24 January 2022
JESHI LAPINDUA SERIKALI...RAIS WA BURKINA FASO HAJULIKANI ALIPO
USAHA NA VIJIDUDU VILINITOKA, NILIVYORAMBA ASALI YA RAFIKI YANGU
Niliishi katika kaunti ya Marsabit karibu na jirani yangu Kim ambaye alikuwa pia ni rafiki wangu wa dhati kwani alinisaidia mambo mengi maishani.
Urafiki ule ulikuwa wenye kutamaniwa na wengi kwani hata watu wengi walisema kuwa tulikuwa marafiki lakini hiyo ilikuwa ni propaganda isiyo na msingi wowote.
Siku ziliposonga, Kim alifanikiwa kupata jiko na hapo ikawa urafiki wangu na wake ukaanza kudidimia kwa kuwa wakati mwingi alitumia kukaa na mke wake. Hatungepata tena wakati wa kwenda kutazama mechi, kulewa vilabuni na kadhalika.
Kwa wakati ule wote sikuwa nimefanikiwa kuoa kwani nilidhani kwamba wakati wangu murua haukuwa umefika. Kwa mara nyingi nilitembelea nyumba yao tukapiga gumzo na hata kushiriki vyakula kwa pamoja.
Kwa vile Kim alikuwa akifanya kazi ya bawabu wa usiku ilikuwa ni fursa muhimu kwangu kupata upenyo hadi nyumbani mwake kupiga gumzo na mke wake kwa wakati wowote.
Nilifanya mazoea ya kuingia kwenye nyumba ya Kim kila wakati alipokuwa katika shuguli za kazi usiku. Mke wake alikuwa mrembo ajabu mtoto wa kidigo aliyeumbwa akaumbika na hapo damu ilinichemka.
Mara nyingi tulizungumza hadi usiku wa manane lakini hakuna kitu kama uhusiano kilinukia kwa ajili ya uoga flani. Baada ya wiki hivi mazungumzo yetu yalianza kubadilika kwani tulianza kuzungumzia mambo ya mapenzi.
Dada yule alinielezea bayana kwamba hakufurahia kazi ya mume wake ya bawabu wa usiku kwani hali ile ilimwacha akisononeka na mwenye upweke. Alisema kuwa alitamani mume wake aiache kazi ile lakini hakuwa na budi kwa kuwa pato lao lilitoka kwenye kazi ile.
Nilifahamu fika kwamba alikuwa akizungumzia suala zima la lungula na hapo nilijiambia akilini kuwa ni mimi pekee nilikuwa shujaa wa kumwondolea upweke wake wakati wa usiku. Mapenzi yetu na mke wa Kim yalinoga kwani hata tulianza kushiriki uroda.
Nilirauka asubuhi na mapema kabla mume wake hajaingia ili kuepuka magombano au vita kwani nilikuwa nakula tunda la wenyewe. Nilifanya kitendo hiki kwa muda wa wiki tatu hivi.
Kim hakugundua lolote wala hakuuliza mke wake chochote na hii ilinipa fursa ya kujiita kinara katika shughuli nzima hii ya kutafuna mke wake.
Nilifahamu kwamba Kim asingegundua chochote. Baada ya siku majuma kadhaa mambo yalianza kuenda mrama. Usaha ulinitoka kwenye sehemu yangu ya siri huku ukiandamana na vijidudu vidogo mithili ya funza. Niligutushwa na mambo haya kwani hata sehemu zile zilikuwa kubwa ajabu hata kuvaa suruali ndefu ilikuwa ni mapigano kwa ajili ya uchungu.
Nilijiambia moyoni kwamba Kim alikuwa ametembelea mahali ili kukinga mke wake kutokana na anasa. Hili lilikuwa ni kweli baada ya Joseph rafikiye Kim kuniambia kwamba Kim alikuwa amemfunga mke wake kushiriki mapenzi na mume mwingine na kwamba daktari aliyefanikisha suala hili lote alijiita Kiwanga.
Niliposikia yale maneno machozi yalinitiririka kwa mpigo. Nilimwelezea Joseph anielekeze kwa daktari Kiwanga ili nirejeshe mambo kuwa kawaida. Nilipofika kwa ofisi za daktari Kiwanga alisema kuwa mtu aliyekuwa na uwezo wa kutatua shida yangu ni mume wa mke niliyeshiriki mapenzi naye na iwapo tu ningemuomba msamaha basi mambo yangu yangekuwa shwari.
Nilifunga safari na kurejea kwangu na hapo siku iliyofuatia nilipiga moyo konde na kumtafuta Kim ili nimwombe msamaha.
Alikubali kuzika mambo hayo kwenye kaburi la sahau na hali ikarejea shwari. Tangu siku ile mimi huona wake wa watu kama sumu.
Daktari Kiwanga ana uwezo wa kutatua migogoro ya mashamba, kumaliza swala zima la wizi na mengineyo. Anatibu magonjwa kama vile kifua kikuu, kifaduro, msukumo wa damu na mengineyo kwa siku tatu tu.
Kwa mengi zaidi wasiliana na Dkt. Kiwanga kutumia wavuti www.kiwangadoctors.com au kupitia barua pepe kiwangadoctors@gmail.com ama pia unaweza kupiga simu/WhatsApp kwa nambari +254769404965 kupata usaidizi.