Baadhi ya Wafanyabiashara katika Soko la Bidhaa za Mitumba la Karume Mchikichini, Ilala Dar es salaam wakijaribu kutafuta vitu watakavyoweza kuokoa bila mafanikio kufuatia soko hilo kuteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo Jumapili Januari 16,2022.
Chanzo cha moto huo hadi sasa bado hakijafahamika.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Ng'wilabuzu Ludigija alifika kwenye eneo la tukio na kuzungumza na wafanyabiashara hao pamoja na viongozi wao, ambapo ameunda tume ya kuchunguza tukio hilo na kutoa siku 14 kwa tume hiyo kukamilisha uchunguzi huo.
Pia amelitaka Jeshi la Polisi kuhakikisha eneo hilo linakuwa kwenye uangalizi maalum na wafanyabiashara hao wameshauriwa kusubiri taarifa ya tume hiyo