Saturday, 15 January 2022
Friday, 14 January 2022
TBS YASHIRIKI TAMASHA LA NANE LA BIASHARA VISIWANI ZANZIBAR, YATOA ELIMU YA VIWANGO
Afisa Masoko TBS Bi. Rhoda Mayugu akitoa elimu ya viwango kwa mjasiriamali aliyeshiriki katika wa Tamasha la 8 la Biashara liliofanyika visiwani Zanzibar
Afisa Masoko TBS Bi. Rhoda Mayugu akitoa elimu ya viwango kwa wanafunzi waliotembelea Banda la TBS na ZBS wakati wa Tamasha la 8 la Biashara liliofanyika visiwani Zanzibar.
********************
Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limeendelea kutoa elimu ya Viwango kwa wazalishaji, wasamabazaji waagizaji wa bidhaa nje ya nchi na Wafanyabishara visiwani Zanzibar .
Elimu hii imetolewa wakati wa Tamasha la 8 la Biashara Zazinbar lililofanyika kuanzia tarehe 2/1/2022 hadi 15/1/2022.
Akizungumza wakati wa Tamasha hilo Afisa Masoko (TBS) Bi Rhoda Mayugu amesema shirika limetumia Tamasha hili kutoa elimu kuhusu majukumu yake ikiwa ni uthibitishaji wa bidhaa na mifumo, usajili na majengo na bidhaa za chakula na vipodozi, upimaji, uandaaji wa viwango na udhibiti wa bidhaa kwa bidhaa zinanotoka nje ya nchi.
“TBS ni shirika lililopewa dhamana ya kusimamia ubora wa bidhaa zinazozalishwa nchini na zile zinatoka nje ya nchi hiyo basi wazalizaji, wasambazaji, waagizaji wa bidhaa nje ya nchi na wafanyabiashara wanatakiwa kuhakikisha bidhaa wazaozalisha na zile zinazotoka nje ya nchi zimethibishwa na kukidhi matakwa ya viwango kabla ya kuingizwa sokoni” alisema Mayugu
Aliongeza kuwa wananchi kama watumiaji wa bidhaa wao wananafasi kubwa ya kufanya katika kuhakikisha bidhaa zilipo sokoni zimekidhi matakwa ya Viwango kwani wao ndio wanofanya maamuzi ya kununua au kutokununua bidhaa
“Wananchi kama watumiaji wa mwisho wa bidhaa ndio waathirika wakubwa wa bidhaa hafifu na endapo watajenga utamaduni wa kununua bidhaa zile tu ambazo zimethibitishwa ubora wake taratibu lakini kwa hakika soko la Tanzania litajazwa na bidhaa zilizokidhi matakwa ya viwango tu na kwa pamoja kama Taifa tutakuwa tumeishinda vita ya bidhaa hafifu.
Jukumu la kuhakikisha Tanzania inakuwa na bidhaa zilizokidhi matakwa ya Viwango si la TBS pekee yake bali ni jukumu la kila Mtanzania kuanzia mzalishaji wa bidhaa, muagizaji wa bidhaa nje ya nchi,msambazaji wa bidhaa, muuzaji wa bidhaa na mtumiaji wa bidhaa. Hiyo basi tukiamua kwa pamoja tutajenga Taifa salama na kukuza uchumi wa nchi kwani bidhaa zetu zitakubalika katika masoko ya kitaifa na kimataifa. Alisisitiza Bi Mayugu
MTANGAZAJI MASHUHURI ZUHURA YUNUS ATANGAZA KUONDOKA BBC SWAHILI
GGML KUANZA KUTUMIA RASMI UMEME WA TANESCO MWISHONI MWA 2022
NA MWANDISHI WETU
MKUU wa Mkoa wa Geita, Rosemary Senyamule amesema mpango wa kuunganisha umeme wa gridi ya taifa kuelekea katika mgodi wa Geita Gold Mine Limited (GGML) unaendelea ambapo ujenzi wa laini maalumu za kwenda mgodini zimekamilika kwa asilimia 90.
Hatua hiyo imekuja baada ya kukamilika kwa mradi wa ujenzi wa kituo kubwa cha kupoozea umeme cha Mpomvu kilichopo Mjini Geita ambapo kinauwezo wa Megawatt 90.
Mkuu huyo wa mkoa ametoa kauli hiyo jana mjini Geita kutokana na taarifa zilizosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kwamba Shirika la Umeme nchini (TANESCO) limeshindwa kupeleka umeme unaohitajika na mwekezaji Geita Gold Mine.
Akifafanua zaidi Senyamule alisema kwa upande wa Mgodi (GGML) wanaendelea na hatua za ujenzi wa kituo cha kupooza umeme cha msongo wa Kilovolt 33 kuwa Kilovolt 11 ndani ya mgodi wa GGML chenye uwezo wa Megawatt 40.
“GGML wanatumia voltage level tofauti na inayosambazwa na TANESCO hivyo tunategemea shughuli zote mpaka December 2022 zitakamilika,” alisema.
Mgodi wa GGML unatumia zaidi ya MW 40 zinazozalishwa kwa kutumia jenereta zinazotumia mafuta ya dizeli tangu mwaka 2018.
Hata hivyo, katika mipango ya TANESCO imekuwa ikitekeleza mradi huo wa Mpovu kuhakikisha inapeleke umeme wa zaidi ya MW 20 katika mgodi huo.
Kituo hicho cha Mpomvu chenye eneo lenye ukubwa wa takribani heka tano kitapokea umeme wa Msongo wa Kilovolt 220 na kutoa Kilovolt 33 kisha kuvinufaisha vijiji 11 vitakavyopitiwa na mradi na wakazi 1,424 walio jirani.
Mikoa jirani kama Mwanza na Kagera itaweza kunufaika na umeme huu kwani ni wa kutosha.
Mradi huo mkubwa wa umegharimu zaidi ya Sh bilioni 50 ili kuwezesha wananchi wa Mkoa wa Geita na maeneo ya jirani kupata umeme wa uhakika na gharama nafuu.
Aidha, mkuu huyo wa mkoa aliongeza kuwa, kukamilika kwa kituo cha kupooza umeme cha Geita kitawezesha Mkoa wa Geita kuwa na umeme wa uhakika utakaowezesha uwekezaji katika sekta mbali mbali hususan uchimbaji wa Madini na Viwanda.
Kwa upande wake, Kampuni ya GGML imethibitisha kuwa utaratibu wa mananuzi ya mitambo ya kupoozea umeme yaani transformers uko katika hatua ya manunuzi na ujenzi wa kituo hicho unatarajiwa kukamilika kufika November 2022.
Makamu Rais wa Kampuni hiyo, Simon Shayo amesema GGML imekamilisha majadiliano na kuandaa rasimu ya mkataba wa kuuziana umeme (power selling agreement) na TANESCO ili kuhakikisha kampuni hiyo inapata umeme wa uhakika na kwa ubora unaotarajiwa ili kuepuka kuathiri shughuli za uzalishaji kwa Kampuni.
“WEWE NI WANGU MILELE” ...NILISIKIA AKINONG’ONEZA
Video Mpya : AGGY BABY Ft STOMPION - KAMNYWESO
WAZIRI BASHUNGWA AZINDUA KALENDA ZA UTEKELEZAJI WA MITAALA YA ELIMU YA AWALI, MSINGI, SEKONDARI NA MAFUNZO JIJINI DODOMA
WAANDISHI WA HABARI MWANZA WAKUTANA KWA MAJADILIANO BAADA YA AJALI ILIYOGHARIMU MAISHA YA WAANDISHI WA HABARI
Video : BHUDAGALA MWANAMALONJA - WALE WALE
CHAMA ATAMBULISHWA RASMI SIMBA SC
MHADHIRI ANAYEFAULISHA WANAFUNZI WA KIKE KWA NGONO ATUPWA JELA
Thursday, 13 January 2022
Ashikiliwa Na Jeshi La Polisi Kwa Tuhuma Za Kumuua Baba Yake Mzazi Kwa Kisu
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia MUSSA EDWARD NDONDE @ SANGA MAPESA [31] Askari wa JWTZ MT.109772 Kikosi cha Ruvu JKT mkoani Pwani na Mkazi wa Mlandizi kwa tuhuma za kumuua baba yake mzazi aitwaye EDWARD NDONDE [75] Mwalimu Mstafuu, Mkazi wa Lumbila Jijini Mbeya kwa kumkatakata visu sehemu mbalimbali za mwili wake.
Tukio hilo limetokea mnamo tarehe 12.01.2022 majira ya saa 09:00 asubuhi huko Mtaa wa Lumbila uliopo Kata ya Iwambi, Tarafa ya Iyunga, Jijini Mbeya ambapo mtuhumiwa aliuawa EDWARD NDONDE [75] ambaye ni baba yake mzazi kwa kumchoma kisu sehemu mbalimbali za mwili wake na kisha kumkata kiganja cha mkono.
Chanzo cha tukio ni tuhuma za ushirikina kwani inaelezwa kuwa mtuhumiwa anadai kuwa marehemu ambaye ni baba yake mzazi ni mchawi anamloga ili hasifanikiwe kwenye mambo yake. Awali mtuhumiwa alifika nyumbani kwa marehemu majira ya 09:00 asubuhi pasipo kutoa taarifa yoyote ya kuja Mbeya na kuingia moja kwa moja sebuleni na kuanza kumshambulia kwa kisu na stuli na kupelekea kifo chake.
Mwili wa marehemu umehifadhiwa Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya kwa uchunguzi wa kitabibu. Mtuhumiwa anaendelea kupatiwa matibabu chini ya ulinzi Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya baada kushambuliwa na wananchi waliojichukulia sheria mkononi kutokana na tukio alilofanya.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linalaani tukio hili baya kutokea na litahakikisha mtuhumiwa anafikishwa kwenye mamlaka husika ya sheria kwa hatua zaidi. Aidha Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linatoa rai kwa wananchi kuachana na Imani potofu za kishirikina hasa kuamini waganga wapiga ramli chonganishi kwani ni hatari kwa ustawi wa jamii na maendeleo ya Taifa.
Imetolewa na:
[CHRISTINA A. MUSYANI – ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Rais Samia amuapisha Balozi wa Tanzania Nchini Kuweit na Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimuapisha Ndugu. Aisha S. Amour kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi) katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu Chamwino, Mkoani Dodoma leo tarehe 13 Januari 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimuapisha Ndugu. Said Shaibu Mussa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Kuwait katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu Chamwino, Mkoani Dodoma leo tarehe 13 Januari 2022.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa katika picha ya pamoja na Ndugu. Aisha S. Amour Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi) kushoto na Ndugu. Said Shaibu Mussa Balozi wa Tanzania nchini Kuwait kulia, mara baada ya kuwaapisha katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu Chamwino, Mkoani Dodoma leo tarehe 13 Januari 2022.