Sunday, 9 January 2022

CCM WATANGAZA MCHAKATO WA KUPATA SPIKA WA BUNGE MPYA.... FOMU KUDAKA KITI CHA NDUGAI ZINAANZA KUTOLEWA KESHO


CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimetangaza kuanza mchakato wa kumsaka mrithi wa nafasi ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai ambaye alijiuzulu tarehe 6 Januari mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo tarehe 9 Januari, 2022 Visiwani Zanzibar, Katibu wa NEC- Itikadi Uenezi CCM, Shaka Hamidu Shaka amesema mchakato huo utaanza kuanzia tarehe 10 hadi 30 Januari mwaka huu.


Amesema hatua hiyo imekuja baada ya Ndugai kuandika barua kwa hiari yake na kuwasilisha kwa Katibu Mkuu wa CCM jijini Dodoma.


Amesema kufuatia hilo CCM kinawatangazia wanachama wake wote kwamba utaratibu wa ratiba ya mchakato wa kumpata mgombea atakayechaguliwa na wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kujaza nafasi ys Spika wa Bunge.


Amesema utaratibu huo ni kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 inayotambua Spika kuwa ndio kiongozi mkuu wa Bunge na nafasi hiyo haiwezi kuwa wazi na Bunge likaendelea kufanya shughuli zake.


Akinukuu Katiba hiyo amesema; Ibara ya 84 (i) kutakuwa na Spika ambaye atachaguliwa na wabunge kutoka miongoni mwa watu ambao ni wabunge au wenye sifa za kuwa wabunge, atakuwa ndio kiongozi wa Bunge na atawakilisha Bunge katika vyombo na vikao vingine vyote nje ya Bunge.


“Ibara ya 84(viii) inasema hakuna shughuli yoyote itakayotekelezwa katika Bunge isipokuwa uchaguzi wa spika wakati wowote ambao kiti cha spika kipo wazi.

“Ibara ya 86(i) kimeeleza kutakuwa na uchaguzi wa spika katika kikao cha kwanza cha mkutano wa kwanza wa Bunge jipya, na katika kikao cha kwanza chochote mara baada ya kutokea kiti cha spika kuwa wazi.

“Kwa minajili hiyo, katika kutekeleza matakwa ya kikatiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania, nichukue fursa hii kwa niaba ya chama kutangaza kwamba mchakato wa kujaza kiti cha Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania utatekelezwa kwa ratiba ifuatayo sambamba na vikao vya mchujo na uchaguzi wa wabunge wa CCM kabla ya kupelekwa bungeni kuendelea na utaratibu mwingine,” amesema.


Amesema kuanzia tarehe 10 hadi 15 zoezi la kuchukua fomu litaanza rasmi na tarehe 15 ifikapo alasiri zoezi hilo litakuwa limekamilika.

Amesema wale wenye sifa alizotaja wanakaribishwa kuchukua fomu katika makao makuu ya chama ofisi kuu, makao ya chama Dodom, ofisi ndogo Dar au Kisiwandui wakifika watapata maelekezo namna ya kcuhukua fomu hizo.

Amesema tarehe 17 Januri, 2022 Sekretarieti ya Halmashauri kuu ya Taifa itakutana kwa ajili ya kujadili wagombea na kuishauri Kamati Kuu ya Halmashuri kuu ya Taifa juu ya wagombea ambao wamejitokeza kuomba kiti hicho cha uspika.

“Tarehe 18 hadi 19 Januari kutakuwa na kazi ya kuchuja na kufanya uteuzi wa mwisho ambapo Kamati kuu ya Halmashauri Kuu itafanya kazi hiyo kwa eneo ambalo litaelekezwa.

“Kuanzia tarehe 21 hadi 30 Januari katika siku hizo, cocus ya chama ya wabunge wa CCM itapiga kura kumpata mgombea ambaye atakwenda bungeni kuomba kuchaguliwa kuwa Spika wa Bunge la Tanzania,” amesema.

Amesema itategemea kama mgombea atakuwa wa CCM au vyama vingine lakini kwa upande wa CCM mchakato wake utakamilishwa na cocus ya CCM ambayo itampata mgombea mmoja atakayepelekwa bungeni.


“Nichukue fursa hii kuwataka watanzania wote ambao wanakidhi vigezo kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na CCM, kwamba wana nafasi na wana fursa kujaza nafasi hii,” amesema.
Share:

WASIOJULIKANA WAFUKUA KABURI LA MTOTO, WATUPA MWILI WAKE MTAANI TANGA


Waombolezaji wakiwa kwenye mazishi ya mara ya pili ya mtoto Sharifa Abasi ambaye mwili wake ulifukuliwa na watu wasiojulikana na kukutwa umetupwa mtaani. Mwili huo umezikwa tena leo katika kata ya Msasa wilayani Handeni mkoani Tanga. Picha na Rajabu Athumani.
 
***
Siku moja baada ya mwili wa mtoto Sharifa Abasi kuzikwa, kaburi lake limefukuliwa na watu wasiojulikana huku mwili wake ukikutwa umetupwa mtaani ukiwa bado ndani ya sanda.

Mwili huo wa mtoto ambaye aliyefariki akiwa na mwezi mmoja na wiki mbili ulizikwa jana Jumamosi Januari 8, 2022 umekutwa katika mtaa wa Msasa Shule wilayani Handeni mkoani Tanga.

Akisimulia mkasa huo baba mkubwa wa marehemu, Athumani Ligotwe wakati wa mazishi ya pili ya mtoto huyo yaliyofanyika leo Jumapili asubuhi amesema ameshangazwa na tukio hilo kwani yeye ndio aliweka mwili wa marehemu kaburini jana na leo wamekuta kaburi limefukuliwa na mwili haupo.

Amesema alifika kwenye kaburi na kubaini mwili haupo na kurudi sehemu ambayo umeonekana na kuthibitisha kuwa ulikuwa wa mtoto wa mdogo wake ambaye alizikwa jana.

Hili ni tukio la kinyama sana lililotokea kwenye familia yetu, wamefukua kaburi ya mtoto wetu na kwenda kutupa mwili mita 300 kutoka hapa kwenye nyumba ya mtu, tunaomba Jeshi la Polisi kuwatafuta hawa watu", amesema Athumani

Chanzo - Mwananchi
Share:

BABU WA MIAKA 84 ADUNGWA CHANJO 11 ZA CORONA

Babu mmoja kutoka nchini India mwenye umri wa miaka 84, amekamatwa baada ya kudai kuwa amedungwa chanjo 11 ya virusi vya Corona.

Kwa mujibu wa ripoti ya gazeti la The New Indian Express, Brahmadeo Mandal mwenye umri wa miaka 84, mkazi wa jimbo la Bihar Mashariki alifanikiwa kupokea dozi hizo kwa kutumia vitambulisho tofauti na nambari za simu za jamaa zake.

Arubaini za mzee huyo zilifika alipokuwa amekwenda kwenye kituo cha afya akiwa anataka kupata dozi ya 12.

 Akielezea nia yake Mandal alisema serikali imefanya jambo la maana na ndio sababu yake ya kupata chanjo kupita kiasi.

Kulingana na mzee hiyo, kufikia mwishoni mwa mwaka 2021, alikuwa tayari ameshapokea jumla ya chanjo 11 na kuongeza kuwa anahisi vizuri.
Share:

Saturday, 8 January 2022

VIGOGO WALIOTEMWA BARAZA LA MAWAZIRI



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan leo Jumamosi, Januari 8, 2022 amefanya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri ambapo ameingiza mawaziri wapya na manaibu waziri huku akiwaacha aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria, Prof. Palamagamba Kabudi, aliyekuwa Waziri wa Ardhi, William Lukuvi, aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara, Prof. Kitila Mkumbo na aliyekuwa Waziri wa Uwekezaji, Geofrey Mwambe.

Kwa upande wa Manaibu Waziri walioachwa ni Mwita Waitara ambaye alikuwa Naibu Waziri wa Ujenzi, aliyekuwa Naibu wa Mambo ya Ndani, Khamis Hamza Chilo.


Tisa wabadilishwa wizara

Wizara ya Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora itaongozwa na Waziri mpya Jenista Mhagama ambaye amehamishwa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu - Sera, Bunge, Kazi, Ajira Vijana na watu wenye Ulemavu.

Aliyekuwa Waziri wa Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mohamed Mchengerwa atakuwa Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo kuchukua nafasi ya Inocent Bashungwa.

Innocent Bashungwa, anakuwa Waziri mpya wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Ummy Mwalimu, aliyehamishiwa Wizara ya Afya.

Aliyekuwa Waziri wa Afya, Dorothy Gwajima sasa nataongoza wizara mpya ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na watu wenye mahitaji maalum.

Aliyewahi kuwa Balozi wa Tanzania nchui Kenya, Pindi Chana sasa ameteuliwa kuongoza Wizara ya Sera na Bunge katika Ofisi ya Waziri Mkuu.

Waziri Mwingine Katika Ofisi ya Waziri Mkuu ni Profesa Joyce Ndalichako atakayeshugulika na Kazi na Ajira ambaye amehamishwa kutoka Wizara ya Elimu, Syansi na Teknolojia.


Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi sasa itaongozwa na Masauni Yusuph Masauni aliyepandishwa wadhifa kutoka Naibu waziri na anachukua nafasi ya Simbachawene, aliyehamishiwa Wizara ya Katiba na Sheria.

Simbachawene anachukua nafasi ya Prof. Palamagamba Kabudi ambaye ameachwa nje ya baraza.

Pia Aliyekuwa Naibu waziri wa Kilimo, Husseon Bashe sasa anakuwa waziri kamili akichukua nafasi ya Profesa Adolf Mkenda aliyehamishiwa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.

Naibu waziri mwingine aliyepandishwa cheo ni Anjelina Mabula atakayeongoza Wizara ya Ardhi, Nyumba na maendeleo ya Makazi kuchukua nafasi ya William Lukuvi, mwanasiasa mkongwe aliyedumu katika nafasi za juu serikali kwa muda mrefu na pia ni mbunge wa Ismani mkoani Iringa kwa zaidi ya miaka 25.

Dkt. Ashatu Kijaji sasa ni Waziri mpya wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara akihamishwa kutoka Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na anachukua nafasi ya Prof. Kitila Mkubo na Geoffrey Mwambe(Uwekezaji) ambao wameachwa nje baraza jipya.

Nape Nnauye ndiye Waziri mpya wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, alikotoka Dkt Kijaji. Nape aliwahi kuongoza Wizara ya Habari na kuondolewa mwaka 2017 na Rais John Magufuli aliyefariki dunia Machi 17, 2021.

Mawaziri waliobakia katika nafasi zao ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberatha Mulamula; Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba; Waziri wa Nishati, January Mkamba; Waziri wa Madini, Doto Biteko; Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro; Waziri wa Maji, Jumaa Aweso; Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa; Waziri wa Ulinzi, Stegomena Tax; na Waziri Ofisi ya Rais - Kazi Maalum, George Mkuchika.







 

Share:

RAIS SAMIA ATEUA KATIBU TAWALA WA MKOA WA KILIMANJARO



Share:

Breaking News : RAIS SAMIA ATEUA WAPYA MAWAZIRI, MAKATIBU WAKUU NA MANAIBU MAKATIBU WAKUU...HAWA HAPA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko Madogo katika Baraza la Mawaziri, Makatibu Wakuu, Manaibu Makatibu Wakuu.

Akitangaza mabadiliko hayo leo Jumamosi Januari 8, 2021 Ikulu jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Hussein Kattanga amesema Rais Samia amefanya mabadiliko ya muundo katika Wizara tatu.

Mawaziri wapya watano walioteuliwa ni Nape Nnauye (Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari), Hamad Masauni (Mambo ya Ndani), Dk Pindi Chana (Sera Bunge na Uratibu), Anjelina Mabula (Ardhi) na Husein Bashe (Kilimo).

Rais Samia pia ameteua manaibu waziri wapya katika wizara tano.

Manaibu waziri hao wapya walioteuliwa ni pamoja na Anthony Mavunde (Kilimo), Jumanne Sagini (Mambo ya Ndani) Dkt.  Lemomo Kiruswa (Madini), Ridhiwani Kikwete (Ardhi) na Atupele Mwakibete (Ujenzi na Uchukuzi).

Tazama Video Hapa chini

Ofisi ya Rais Ikulu
Waziri wa Nchi Kazi Maalum – Kapeni Geroge Mkuchika

Waziri wa Utumishi – Jenista Mhagama

Naibu Waziri Utumishi – Deogratius John Ndejembi

TAMISEMI

Waziri – Innocent Bashungwa

Naibu Waziri – David Silinde

Naibu Waziri – Festo Dugange

Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira

Waziri – Suleimani Jafo
Naibu Waziri – Hamis Hamis

 

Sera Bunge
Pindi Chana
Nderiananga

Wizara ya Kazi Ajira

Waziri – Ndalichako waziri

Wizara ya Ulinzi –

Wizara ya Sheria na Katiba
Waziri –  George Simbachawene
Naibu Waziri – Godfrey Mizengo Mizengo Pinda

Wizara ya Kilimo
Waziri – Hussein Bashe
Naibu Waziri – Anthony Mavunde

Wizara ya Uvuvi
Waziri – Mashimba Ndaki
Naibu Waziri – Abdallah Hamisi Ulega

Wizara ya Ardhi
Waziri – Angelina Mabula
Naibu Waziri – Ridhiwani Kikwete

Rais Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri.

Akitangaza mabadiliko hayo leo Jumamosi Januari 8, 2021 Ikulu jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Hussein Kattanga amesema Rais amefanya mabadiliko ya muundo katika wizara tatu.

Rais Samia amefanya mabadiliko hayo ikiwa anatimiza ahadi yake ya kufanya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri.

Ofisi ya Rais Ikulu
Waziri wa Nchi Kazi Maalum – Kapeni Geroge Mkuchika

Waziri wa Utumishi – Jenista Mhagama

Naibu Waziri Utumishi – Deogratius John Ndejembi

TAMISEMI

Waziri – Innocent Bashungwa

Naibu Waziri – David Silinde

Naibu Waziri – Dugange

Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira

Waziri – Suleimani Jafo

Naibu Waziri – Hamis Hamis

Wizara ya Kazi Ajira

Waziri – Ndalichako

Naibu Waziri – Patrobas Katambi

Wizara ya Fedha

Waziri – Mwigulu Mwigulu
Naibu Waziri – Chande

Wizara ya Ulinzi

Waziri – Stergomena Tax

Wizara ya Sheria na Katiba
Waziri –  George Simbachawene
Naibu Waziri – Godfrey Mizengo Mizengo Pinda

Wizara ya Kilimo
Waziri – Hussein Bashe
Naibu Waziri – Anthony Mavunde

Wizara ya Uvuvi
Waziri – Mashimba Ndaki
Naibu Waziri – Abdallah Hamisi Ulega

Wizara ya Ardhi
Waziri – Angelina Mabula
Naibu Waziri – Ridhiwani Kikwete

Wizara ya Mambo ya Ndani

Waziri  – Mhandisi Hamad Masauni
Naibu Waziri – Sagini Jumanne Abdallah

Wizara ya Mambo ya Nje
Waziri – Liberata Mulamula
Naibu Waziri – Mbaruku

Wizara ya Maliasili
Waziri – Dkt. Damas Ndumbaro
Naibu Waziri – Mary Masanja

Wizara ya Nishati
Waziri – January Makamba
Naibu Waziri – Steven Byabato

Wizara ya Madini
Waziri – Dkt. Dotto Biteko
Naibu Waziri – Kiluswa

Ujenzi
Mbarawa
Atupele Mwakibete
Godtlfrey Kasekenya

Viwanda
Kijaji
Kigahe

Afya
Ummy Mwalimu
Ole Mollel

Elimu
Mkenda
Kipanga

Maendeleo ya jamii
Gwajima dorothy
Mwanaidi Hamis

Maji
Jumaa aweso
Mahundi

Utamaduni
Mchengerwa
Gekul

Share:

RAIS SAMIA AMTEUA NAPE NNAUYE KUWA WAZIRI WA HABARI TANZANIA


Rais Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri na Makatibu Wakuu na Manaibu Makatibu Wakuu.

Akitangaza mabadiliko hayo leo Jumamosi Januari 8, 2021 Ikulu jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Hussein Kattanga amesema Nape Nnauye ameteuliwa kuwa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.

Mawaziri wapya watano walioteuliwa ni Nape Nnauye (Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari), Hamad Masauni (Mambo ya Ndani), Dk Pindi Chana (Sera Bunge na Uratibu), Anjelina Mabula (Ardhi) na Husein Bashe (Kilimo).

Rais Samia pia ameteua manaibu waziri wapya katika wizara tano.

Manaibu waziri hao wapya walioteuliwa ni pamoja na Anthony Mavunde (Kilimo), Jumanne Sagini (Mambo ya Ndani) Dkt.  Lemomo Kiruswa (Madini), Ridhiwani Kikwete (Ardhi) na Atupele Mwakibete (Ujenzi na Uchukuzi).

*************

Ofisi ya Rais Ikulu
Waziri wa Nchi Kazi Maalum – Kapeni Geroge Mkuchika

Waziri wa Utumishi – Jenista Mhagama

Naibu Waziri Utumishi – Deogratius John Ndejembi

TAMISEMI

Waziri – Innocent Bashungwa

Naibu Waziri – David Silinde

Naibu Waziri – Festo Dugange

Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira

Waziri – Suleimani Jafo
Naibu Waziri – Hamis Hamis

 

Sera Bunge
Pindi Chana
Nderiananga

Wizara ya Kazi Ajira

Waziri – Ndalichako waziri

Wizara ya Ulinzi –

Wizara ya Sheria na Katiba
Waziri –  George Simbachawene
Naibu Waziri – Godfrey Mizengo Mizengo Pinda

Wizara ya Kilimo
Waziri – Hussein Bashe
Naibu Waziri – Anthony Mavunde

Wizara ya Uvuvi
Waziri – Mashimba Ndaki
Naibu Waziri – Abdallah Hamisi Ulega

Wizara ya Ardhi
Waziri – Angelina Mabula
Naibu Waziri – Ridhiwani Kikwete

Rais Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri.

Akitangaza mabadiliko hayo leo Jumamosi Januari 8, 2021 Ikulu jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Hussein Kattanga amesema Rais amefanya mabadiliko ya muundo katika wizara tatu.

Rais Samia amefanya mabadiliko hayo ikiwa anatimiza ahadi yake ya kufanya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri.

Ofisi ya Rais Ikulu
Waziri wa Nchi Kazi Maalum – Kapeni Geroge Mkuchika

Waziri wa Utumishi – Jenista Mhagama

Naibu Waziri Utumishi – Deogratius John Ndejembi

TAMISEMI

Waziri – Innocent Bashungwa

Naibu Waziri – David Silinde

Naibu Waziri – Dugange

Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira

Waziri – Suleimani Jafo

Naibu Waziri – Hamis Hamis

Wizara ya Kazi Ajira

Waziri – Ndalichako

Naibu Waziri – Patrobas Katambi

Wizara ya Fedha

Waziri – Mwigulu Mwigulu
Naibu Waziri – Chande

Wizara ya Ulinzi

Waziri – Stergomena Tax

Wizara ya Sheria na Katiba
Waziri –  George Simbachawene
Naibu Waziri – Godfrey Mizengo Mizengo Pinda

Wizara ya Kilimo
Waziri – Hussein Bashe
Naibu Waziri – Anthony Mavunde

Wizara ya Uvuvi
Waziri – Mashimba Ndaki
Naibu Waziri – Abdallah Hamisi Ulega

Wizara ya Ardhi
Waziri – Angelina Mabula
Naibu Waziri – Ridhiwani Kikwete

Wizara ya Mambo ya Ndani

Waziri  – Mhandisi Hamad Masauni
Naibu Waziri – Sagini Jumanne Abdallah

Wizara ya Mambo ya Nje
Waziri – Liberata Mulamula
Naibu Waziri – Mbaruku

Wizara ya Maliasili
Waziri – Dkt. Damas Ndumbaro
Naibu Waziri – Mary Masanja

Wizara ya Nishati
Waziri – January Makamba
Naibu Waziri – Steven Byabato

Wizara ya Madini
Waziri – Dkt. Dotto Biteko
Naibu Waziri – Kiluswa

Ujenzi
Mbarawa
Atupele Mwakibete
Godtlfrey Kasekenya

Viwanda
Kijaji
Kigahe

Afya
Ummy Mwalimu
Ole Mollel

Elimu
Mkenda
Kipanga

Maendeleo ya jamii
Gwajima dorothy
Mwanaidi Hamis

Maji
Jumaa aweso
Mahundi

Utamaduni
Mchengerwa
Gekul

Share:

BABU AJIUA KWA KUJINYONGA UGWETO SHINYANGA


Mwanaume aliyefahamika kwa jina la Magesa Mahona anayekadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka 60 na 65 mkazi wa mtaa wa Ugweto manispaa ya Shinyanga amefariki dunia kwa kujinyonga katika nyumba yake majira ya usiku.

Mwili wa marehemu uligunduliwa na familia yake leo asubuhi Jumamosi Januari  8,2022 baada ya kukutwa ukining’inia. Kamanda wa polisi mkoani Shinyanga, ACP George Kyando amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.


Share:

UKILOST MKEKA UNALIPWA: SOMA HAPA JINSI YA KUOMBA BONUS UKILOST MKEKA WAKO

Habari njema kwa wadau wakubeti ambao hupoteza mikeka yao mara kwa mara hapa nitakueleza namna ya kuomba utumiwe bonus  kama malipo ya mikeka yako uliyopoteza

Ofa hii inapatikana ndani ya kampuni ya kubet ya 22bet

Masharti ya kupata bonus hii,

👉 Ni lazima uwe umejisajili na >>22bet>>

👉Uwe umepoteza angalau mikeka 20 mfululizo

👉Katika timu zote ulizopoteza  timu ziziwe na ods juu ya 3.0 maana kuna watu watachagua timu yenye ods 12 ili walost makusudi na kuomba bonus.

👉Mikeka yote uliyolost iwe imewekwa ndani ya siku 30 sio zaidi ya hapo.

👉 Kila mkeka uliolost  stake yake ianzie $2 sawa na kama 4700 

👉Kumbuka  unatakiwa kuomba bonus hii kwa account moja tu, ikiwa unamiliki zaidi ya account 1 hutopewa na watagundua kupitia IP adress

Does your series of losing bets meet all the requirements? Then email us at support@22bet.com  account number and putting "Series of losing bets" in the subject line.

Kama umetimiza vigezo hivyo tuma barua pepe, na sehemu ya subject jaza account namba yako  na idadi ya mikeka uliyopoteza  utapokea malipo yako ndani ya muda mfupi, kumbuka email itumwe   kwenda  support@22bet.com  

   kUJISAJILI NA 22BET BOFYA >>>HAPA>>


Share:

KAMATA BONUS YA SIKU YAKO YA KUZALIWA NA 22BET TANZANIA

 

Kampuni ya kubet ya 22BET hutoa bonus kwa kila mteja wake anayeadhimisha siku yake ya kuzaliwa, unachotakiwa ni kujisajili na kuset tarehe yako ya kuzaliwa na pia uwe unatumia mtandao huo kuweka mkeka wako mara kwa mara, itakapofika siku yako kulingana na tarehe uliyoweka, utatumiwa bonus yako katika account yako. bonus hiyo hutofautiana baina ya mteja mmoja na mwingine kulingana na utumiaji wako.

KUJIUNGA NA 22BET BOFYA <<<HAPA>> NA UJAZE TAARIFA ZAKO











Share:

Friday, 7 January 2022

WABUNGE WA TANZANIA WAITWA BUNGENI SAA CHACHE BAADA YA SPIKA NDUGAI KUJIUZULU


Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Nenelwa Mwihambi leo Ijumaa, Januari 7, 2022 amesema baada ya Job Ndugai kujiuzulu nafasi ya Uspika kwa sasa taratibu za uchaguzi wa kujaza nafasi hiyo zinaendelea na kwamba kwa mujibu wa sheria kiti cha Spika kinapokuwa wazi hakuna shughuli yoyote itakayotekelezwa katika Bunge isipokuwa Uchaguzi wa Spika.

Katika taarifa yake, Mwihambi amesema Kamati zilizokuwa zikutane kianzia Januari 10, 2022 na Januari 17, 2022 hazitokutana kwa wakati huo na badala yake zitakutana wakati wa Mkutano wa Sita wa Bunge Februari 1-11, 2022 kwa utaratibu wa tarehe zitakazotangazwa na hivyo Wabunge wameombwa kufika Dodoma Januari 31, 2022.
Share:

MASTAA 17 KUONDOKA MANCHESTER UNITED


Manchester United ipo katika wakati mgumu hasa kutokana na kudaiwa kuwa kuna wimbi kubwa la wachezaji wanataka kuondoka wakati huu wa Januari au mwishoni mwa msimu huu.

Kwa ufupi ni kuwa kuna hali tete ndani ya Old Trafford, ambapo inaelezwa kuwa kuna wachezaji takribani 17 ambao wanaweza kuondoka.

Morali ndani ya klabu hiyo ipo chini licha ya kuwa kuna ujio wa Kocha Ralf Rangnick ambaye ameshindwa kuamsha morali tangu kuondoka kwa Ole Gunnar Solskjaer. Baadhi ya wachezaji wanaoweza kuondoka kwa asilimia kubwa ni wale ambao hawana furaha na mikataba yao inaelekea mwishoni.

Baadhi ya wachezaji wanaotajwa kuwa wapo njiani kuondoka ni Anthony Martial, Paul Pogba, Edinson Cavani,Jesse Lingard, Juan Mata, Donny van de Beek, Dean Henderson, Eric Bailly na Phil Jones. Wengine ni Nemanja Matic, Fred, Diogo Dalot na Axel Tuanzebe.
Share:

WIZARA YA ARDHI YAZINDUA KITUO CHA MAWASILIANO KWA WATEJA

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akizindua Kituo cha Mawasiliano kwa Wateja cha Wizara ya Ardhi leo tarehe 7 Januari 2022 jijini Dodoma. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi Mary Makondo. Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akipata maelezo kutoka kwa Afisa Ardhi David Malisa kuhusiana na namna ya Kituo cha Mawasiliano kwa Wateja cha Wizara ya Ardhi kinavyopokea malalamiko ya Wateja alipokizindua leo tarehe 7 Januari 2022 jijini Dodoma. Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akifuatilia upokeaji malalamiko ya wananchi kwenye kituo cha Mawasiliano kwa Wateja cha Wizara ya Ardhi mara baada ya kukizindua leo tarehe 7 Januari 2022 jijini Dodoma. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi Mary Makondo. Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akiangalia ndege ya kuchukua picha za anga (Drons) kwa ajili ya uandaaji ramani za msingi za upimaji leo tarehe 7 Januari 2022 jijini Dodoma. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi Mary Makondo.

********************************

Na Munir Shemweta, WANMM DODOMA

Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi imezindua kituo cha Mawasiliano kwa Wateja kwa lengo la kuondoa kero za wananchi katika masuala ya ardhi.

Uzinduzi wa kituo hicho umefanywa leo tarehe 7 Januari 2022 na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi katika ofisi za Wizara zilizopo Mtumba jijini Dodoma.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kituo hicho, Waziri Lukuvi alisema, kwa kutumia maendeleo ya teknolojia ya mawasiliano na habari yaliyopo sasa wizara yake imeona zipo baadhi ya huduma za ardhi zinazoweza kutolewa kwa njia ya simu na mitandao ya kijamii ambazo hazimlazimu mwananchi kufika ofisi za ardhi.

‘’Wizara imeanzisha kituo cha Mawasiliano kwa Wateja kitakachotoa huduma ya mawasiliano moja kwa moja na mwananchi kwa kutumia simu na ujumbe wa maneno kupitia Whatsup ambapo majibu au ufafanuzi utatolewa kwa wananchi na wataalamu wa ardhi’ alisema Lukuvi

Kwa mujibu wa Lukuvi, Kituo hicho cha Mawasiliano kwa Wateja kina wataalamu wabobezi katika masuala ya ardhi waliopata mafunzo yakinifu ya kuifanya kazi ya kutoa huduma kwa wateja kwa weledi na kutoa majibu kwa wakati.

Aidha, Waziri Lukuvi alitumia fursa ya uzinduzi wa kituo hicho kuwataka wananchi kukitumia kituo cha Mawasiliano kwa Wateja cha Wizara ya Ardhi kuwasilisha kero mbalimbali zikiwemo za matapeli wa ardhi, watumishi wa sekta ya ardhi wasio waaminifu pamoja na wale madalali wanaochukua fedha za wapangaji na kusisitiza kuwa, anayepaswa kutoa fedha kwa madalali ni mwenye nyumba na siyo mpangaji.

Aliongeza kwa kusema, kupitia kituo hicho mwananchi atalazimika kupiga simu na kuongea moja kwa moja na watoa huduma kupitia namba 0739-646-885 au kutuma ujumbe wa maneno kupitia mtandao wa Whatsup kwa namba hizo. Kituo hicho kitakuwa wazi siku za kazi kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 9:00 alasiri kwa ajili ya kutoia huduma kwa wananchi.

‘’Ni matumaini yangu kituo hiki kitatoa fursa kwa wananchi kupata huduma za ardhi kwa haraka, kwa ufanisi na kwa gharama nafuu kwa kuwa mwananchi hatakazimika kufika ofisi za ardhi endapo huduma anayohitaji anaweza kuipata kupitia simu.

Alitoa rai kwa wananchi kukitumia kituo hicho kwa kupiga simu na kutuma ujumbe wa maneno kupitia namba ya simu iliyotangazwa na kutumia tovuti ya wizara kupata huduma kwa urahisi bila usumbufu ili kuepuka gharama za kusafiri sambamba na kutumia muda mwingi kufuata huduma hizo ofisi za wizara makao makuu, ofisi za ardhi za mikoa na halmashauri.

Uanzishwaji Kituo cha Mawasiliano kwa Wateja ni moja ya mikakati mbalimbali ya Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuhakikisdha huduma kwa wateja wa ardhi zinaboreshwa na zionatolewa kwa weledi na ufanisi mkubwa.
Share:

Thursday, 6 January 2022

Breaking : SPIKA JOB NDUGAI AJIUZULU


Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai ametangaza kujiuzulu wadhifa wake huo ndani ya Bunge leo Alhamisi, Januri 6, 2022 kutokana na fukuto la kisiasa linaoendelea kufuatia kauli yake aliyoitoa kuhusu Rais Samia Suluhu kukopa Tsh trilioni 1.3.


"Naomba kutoa taarifa kwa umma wa Watanzania kuwa leo Tarehe 6 Januari 2022 nimeandika barua kwenda kwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kujiuzulu nafasi ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,uamuzi huu ni binafsi na hiari na nimeufanya kwa kuzingatia na kujali maslahi mapana zaidi ya Taifa langu,Serikali na Chama cha CCM", - Mhe.Job Ndugai 
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger