Wednesday, 5 January 2022

ADAIWA KUMUUA MKE WAKE KWA KUMKATA KICHWA NAYE AJIUA JUU YA MTI


MICHAEL Methew mwenye umri wa miaka 33 mkazi wa Kijiji na Kata ya Mashete wilayani Nkasi Mkoa wa Rukwa anadaiwa kumuua mke wake kwa kumkata kichwa na kukitenganisha na kiwiliwili na kisha kujiua kwa kujinyonga kwa kutumia mnyororo aliokuwa akitumia kufungia ng'ombe wake.

Tukio hilo limetokea Januari 4,2022 majira ya saa 12:30 jioni katika Kijiji cha Mashete ndani ya Kata ya Mashete wilayani Nkasi mkoani Rukwa.

Afisa Mtendaji wa Kata ya Mashete, Bosko Wazamani akizungumzia tukio hilo amesema kuwa,chanzo cha mauaji hayo hakijafahamika.

Wazamani amesema,mpitanjia mmoja alifika katika nyumba yao na ndipo alipokuta mwili wa mwanamke huyo ukiwa umelazwa sakafuni.

Amesema kuwa, wanandoa hao walikuwa wakiishi peke yao nje ya mji, na walikuwa wameoana miezi michache iliyopita hivyo hawakuwa na mtoto isipokuwa mwanamke alikuwa na mtoto aliyezaa na mwanaume mwingine, hata hivyo hakuwa akiishi na mtoto huyo.

Mtendaji huyo amesema, baada ya uongozi wa kijiji kufika katika nyumba hiyo walikuta mwili wa mwanamke huyo ambaye jina lake bado halijafahamika ukiwa umetengenishwa na kichwa na pembeni kukiwa na shoka likilotapakaa damu alilotumia mume wake kufanya mauaji hayo.

Viongozi hao wa serikali ya kijiji na kata, walipoanza jitihada za kumtafuta mtuhumiwa, walikuta mwili wake ukiwa unaning'inia kwenye mti jirani na nyumba yake, huku akiwa amejinyonga kwa kutumia mnyororo anaofungia mifugo yake.

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi mkoani Rukwa, William Mwampaghale alikiri kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa chanzo cha mauaji hayo bado hakijafahamika kwa kuwa hakuna wa kumuhoji, lakini alisema kuwa polisi bado wanaendelea na uchunguzi.

Amesema kuwa, inadhaniwa huenda mwanamke aliyeuawa alikuwa na mawasiliano na mzazi mwenzake kitendo kilichosababisha wivu wa kimapenzi kwa mume wake mpya na kuamua kufanya mauaji hayo.

Kamanda huyo amewaasa wakazi wa mkoa wa Rukwa kuacha tabia za kujichukulia sheria mkononi badala yake wawe wanawahusisha ndugu, wazee wa kimila na viongozi wa kidini kutafuta suluhu katika changamoto za ndoa.
Share:

CCM DODOMA YAWATAKA WANA CCM KUACHA USALITI, MAJUNGU NA ROHO MBAYA...'RAIS NI MMOJA TU AHESHIMIWE'


 
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Dodoma,Dkt. Damas Mukkasa
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Dodoma, Dkt. Damas Mukkasa

Na Dotto Kwilasa,Malunde 1 blog,Dodoma

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma kimewataka baadhi ya wanachama na ambao sio wanachama wa chama hicho kuacha,usaliti,uzandiki, majungu,fitna na roho mbaya kwani Rais ni mmoja tu hivyo anatakiwa aheshimiwe.

Hatua hiyo imekuja kufuatia jana Rais Samia Suluhu Hassan kudai kwamba kuna baadhi ya wanachama wa chama hicho wamekuwa wakimsaliti katika suala la nchi kukopa.

Kupitia kauli ya Rais Samia, alisema lazima nchi ikope kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa madarasa kwakuwa fedha za tozo haziwezi kutekeleza mahitaji ya miradi hiyo.

Amesema mkopo ambao Serikali umeupata wa Sh trilioni 1.3 ni mzuri na haujawahi kutokea tangu nchi ipate Uhuru.

Akizungumza kwa niaba ya Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Dodoma leo Januari 5,2022, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Dodoma, Dkt. Damas Mukkasa kuhusu kumpongeza Rais kwa hotuba yake aliyoitoa Januari 4,2022 Jijini Dare-es-Salaam baada ya kupokea taarifa ya Mpango wa maendeleo wa ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya Uviko-19.

Mwenyekiti huyo wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Dodoma amemuomba Rais Samia kufanya kazi bila uoga na kuachana na baadhi ya watu ambao wana uchu wa madaraka.

Dkt. Mukassa ametoa wito kwa Wana CCM kuacha majungu,fitina na roho mbaya, kuacha kuharibiana kwani Rais ni mmoja na hivyo aheshimiwe.

Katika hatua nyingine amelaani makundi yanayowania Urais kwa mwaka 2025 kwani huo ni usaliti na tamaa na badala yake wamuunge mkono Rais katika utendaji kazi ili kuleta maendeleo.


Share:

Tuesday, 4 January 2022

RAIS SAMIA AMLIPUA SPIKA NDUGAI ..KUKOPA SIYO KIOJA..KINACHOSUMBUA NI STRESS YA 2025


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameeleza kushangazwa na kauli za Spika wa Bunge Job Ndugai kusimama hadharani na kukosoa mkopo wa Shilingi Trilioni 1.3 kutoka shirika la Fedha Duniani (IMF) wenye lengo la kuchochea mapambano dhidi ya UVIKO -19 wakati taarifa mbalimbali zinapitia kwenye bunge lake.

Akizungumza leo Jumanne Januari 4,2022 Jijini Dar es salaama wakati akipokea taarifa ya utekelezaji wa fedha hizo kwenye miradi mbalimbali ikiwemo elimu, afya,maji na miundombinu, Rais Samia ameonyesha kukerwa na kile alichokisema Spika wa Bunge, Job Ndugai kuhusu Serikali kukopakopa badala ya kujiendesha kwa pesa za ndani.

“Huwezi kufikiria mtu mliyemuamini, mshika mhimili, aende akasimame aseme yale. Ni stress ya 2025. Inashangaza kuona mtu mwenye uelewa, anasema kuna fedha ya tozo lakini kaenda kukopa, ya nini? Au kwa nini tunaendelea kutoa tozo wakati fedha ya mkopo ipo. Mawaziri tupeni hizo takwimu sasa hivi.

“Nitajitahidi kadiri ya uwezo wangu kutumia kila fursa nitakayoiona itakayoletwa ambayo naweza kuitumia kuleta maendeleo Tanzania nitaitumia. Sifanyi kwa ajili ya uchaguzi wa 2025, nafanya nimeapa kuleta maendeleo kwa Watanzania.

“Nawashukuru wenyeviti wa CCM kwa kusimama na kutetea mkopo ulioleta maendeleo kwenu. Walipotokea wakuhoji mlisimama mkajibu, mkijua kwamba kinachofanyika ni utekelezaji wa ilani. Sasa mna mambo ya kwenda kifua mbele kwa wananchi kuwaambia CCM imefanya.


“Hizi Fedha zitalipwa na wananchi kupitia tozo lakini wananchi wanatakiwa kuona matunda yake. “Na kwa maana hiyo ile hamu yao na tamanio lao la 2025 ‘somehow’ tamaa zinaondoka,” amesema Rais Samia.

"Tuna serikali ya kukopa kopa tangu uhuru.
Tumekopa kopa na maendeleo tuliyopata yanatokana na kukopa kopa..kukopa siyo kioja. Tutakopa mikopo isiyo na riba ili tupate maendeleo".
"Mtu na akili yake anasimama na anahoji kuhusu mikopo na tozo, sio lolote ni homa ya 2025, kwa mtu ambaye nilimtegemea kushirikiana naye kwenye maendeleo, sikutegemea kama angesimama na kusema maneno hayo. Huwezi kufikiria mtu mliyemuamini, mshika mhimili, aende akasimame aseme yale. Ni stress ya 2025", amesema Rais Samia.

"Kinachotokea sasa ni 2025 Fever, wasameheni...Haya ninayofanya sasa sifanyi kwa ajili ya mwaka 2025, nafanya kwa ajili ya maendeleo ya nchi...Tunachotazama sasa ni maendeleo kwa watanzania... Kelele za wanaopiga kelele hazinisumbui..mimi sivunjiki moyo, mimi nina moyo wangu, moyo wangu siyo wa glasi,ni wa nyama ulioumbwa na Mungu, hivyo sivunjiki moyo...Nishikeni mkono twende sote.

"Nataka niwaambie nitatoa list mpya ya Mawaziri hivi karibuni, wale wanaotaka kwenda na mimi nitaenda nao ila wale wanaotumika nitawapa nafasi wakatumike huko nje wanapopataka.  Wale ninaohisi wanaweza kwenda na mimi…nitakwenda nao. Lakini wale wote ninaohisi ndoto zao ni kule, na wanafanya kazi kwa ajili ya kule, nitawapa nafasi waende wakajitayarishe vizuri huko nje.

"Nilipopewa mamlaka haya kuna mtu alikuja na kunipa pole na hongera akasema mtu atakayekusumbua kwenye kazi yako na uongozi ni mtu shati la kijani mwenzako wala siyo wa upinzani ,Mpinzani atakutazama unafanya nini,ukimaliza hoja zao hawana maneno lakini shati wa kijani mwenzio anayetazama mbele  2025, 2030 huyu ndiyo atakusumbua , nataka niwaambie nicho kinachotokea kwa sababu  huwezi kufikiria mtu mnayemuamini anashikilia mhimili aende akasema hayo..Kinachosumbua ni Stress za mwaka 2025",ameongeza Rais Samia.

"Wakati mmenikabidhi huu mzigo, nilianza kusikia lugha zinasema serikali ya mpito, serikali ya mpito bungeni huko kwa kina Kassim. Nikarudi kwenye Katiba kuangalia serikali ya mpito imeandikwa wapi...sikuona. Nikasema 'anhaa, twendeni"- Rais Samia

“Wakatizama mtu aliyeshika kitabu kuapa, wakamfanyia tathmini, wakamfanyia yote waliyoyafanya wakampa ‘grade’ yake wakamuweka pale. Sasa yanayotokea hawaamini, kwamba yule mtu waliyempa ile thamani ndio anayafanya. Hawaamini. Uongozi huletwa na Mungu, aliyepangiwa ndiye atakayekaa"- Rais Samia

Share:

RAIS SAMIA ATANGAZA KUTEUA MAWAZIRI, WAKUU WA MIKOA WAPYA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema hivi karibuni atafanya mabadiliko ya viongozi mbalimbali wakiwemo Mawaziri, Makatibu Wakuu na Wakuu wa Mikoa.

Rais Samia ameyasema hayo leo Jumanne Januari 4,2022 Jijini Dar es salaama wakati akipokea taarifa ya utekelezaji wa fedha hizo kwenye miradi mbalimbali ikiwemo elimu, afya,maji na miundombinu.
Akizungumzia kuhusu mijadala inayoendelea juu ya serikali yake kukopa  kopa, Rais Samia amesema hizo kelele ni Presha 'Stres' za kuelekea uchaguzi mkuu 2025 hivyo ataweka pembeni ili wakutane mbele ya safari.

Amesema amewateua Wakuu wa Mikoa ili wamsaidie kuwaletea maendeleo wananchi.

"Wakuu wa mikoa nimekuwekeni nikiamini kule nilikowakasimia madaraka mtakwenda kusimamia kazi na wengine wote wakiwemo Makatibu Wakuu na Mawaziri",amesema.

"Nataka niwaambie nitatoa list mpya ya Mawaziri hivi karibuni, wale wanaotaka kwenda na mimi nitaenda nao ila wale wanaotumika nitawapa nafasi wakatumike huko nje wanapopataka. Wale ninaohisi wanaweza kwenda na mimi…nitakwenda nao. 

Lakini wale wote ninaohisi ndoto zao ni kule, na wanafanya kazi kwa ajili ya kule, nitawapa nafasi waende wakajitayarishe vizuri huko nje",amesema Rais Samia
Share:

Naibu Waziri Ummy Aeleza Mikakati Ya Serikali Ya Kuboresha Mazingira Ya Watu Wenye Ulemavu


NA. MWANDISHI WETU
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya watu wenye ulemavu Mhe. Ummy Nderiananga amesema Serikali itaendelea kuboresha mazingira ya watu wenye ulemavu ikiwemo ujenzi na ukarabati wa vyuo ili kuendelea kutatua changamoto wanazokutana nazo.

Ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais (Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi) Dkt.  Khalid Salum Mohamed alipomtembelea ofisini kwake Januari 03, 2022 ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi ya kujionea shughuli za watu wenye ulemavu katika visiwa vya Unguja na Pemba.

Naibu Ummy alibainisha kuwa, tayari serikali imetoa kiasi cha shilingi za kitanzania billion 8 kwa lengo ujenzi wa vyuo vya watu wenye ulemavu na ukarabati wa majengo chakavu ya kundi hilo nchini.

“Tunamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa kipaumbele katika kuhakikisha masuala ya watu wenye ulemavu yanazingatiwa ambapo ametoa shilingi bilioni 8 kwa ajili Ujenzi wa vyuo vipya viwili na ukarabati wa vyuo sita vya watu wenye ulemavu ili waweze kupata ujuzi kupitia elimu watakayopata na kuyafikia malengo yao”.alisisitiza Naibu Waziri Ummy

Aidha mikakati mingini ni pamoja na kuendelea kutoa vifaa saidizi kwa watu wenye mahitaji maalumu pamoja na kuhakikisha miundombinu inakuwa rafiki katika maeneo yanayowazunguka ili kuwapa nafasi ya kushiri vyema katika shughuli zao za kila siku.

“Serikali itaendelea kutenga bajeti ya kutosha, kuwawezesha vifaa saidizi, kuboresha miundombinu mbalimbali ili kuendana na hali zao pamoja na kuhakikisha haki na usawa kwa watu wenye ulemavu vinapewa kipaumbele kwa kuzingatia sheria ya watu wenye ulemavu Namba 9 ya Mwaka 2010,”alisema

Hata hivyo naibu Waziri Ummy alimhakikishia Dkt. Salim kuwa wataendelea kudumisha ushirikiano baina yao kwa lengo la kuendeleza jitihada za kuwahumia watu wenye ulemavu nchini.

“Watu wenye ulemavu waliopo Zanzibar na Bara ni kitu kimoja hata mazingira ya changamoto zao zinawiana ni vyema kuitumia fursa ya kuendelea kuzitatua changamoto hizo huku tukidumisha ushirikino,”alisisitiza

Kwa Upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais anayeshughulikia masuala ya Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi (SMZ) Dkt.  Khalid Salum Mohamed alieleza kuwa, wamendelea kuratibu masuala ya watu wenye ulemavu ikiwemo uwezeshwaji kiuchumi, upatikanaji wa elimu jumuishi pamoja na kuwajengea uwezo ili kujikwamua kiuchumi na kujiletea maendeleo.

“Kipekee nikupongeze kutenga muda wako kufika Zanzibar hii ni faraja kwa kuzingatia umuhimu wa masuala yanayowahusu watu weye ulemavu, tutaendelea kuboresha mshikamano ya kiutendaji baina yetu ili kuunga mkono juhudi za viongozi wetu,”alisema Dkt. Khalid


Share:

WAZIRI WA FEDHA : DENI LA TAIFA NI HIMILIFU...HAKUNA ATAKAYEGONGEWA MLANGO KUDAIWA


Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba, amesisitiza kuwa deni la taifa ni himilivu na kwamba hakuna Mtanzania yeyote atakayegongewa mlango wake ama kuamriwa kuuza mali yake ili kulipa deni la Taifa.

Dkt. Mwigulu amesema hayo leo Jumanne, Januari 4, 2022 wakati akiwasilisha ripoti ya matumizi ya Fedha za Maendeleo (Fedha za Uviko-19) mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, Ikulu jijini Dar es Salaam.


“Utekelezaji wa fedha imeendelea na kuongeza imani kwa Viongozi Wakuu wa IMF na kuamua kufuta masharti yote yaliyokuwa na riba kwa upande wa fedha zenye dirisha la ‘rapid financing instrument’ ambayo ilikuwa Dola za Kimarekani milioni 378.17 sawa na theluthi mbili ya mkopo wote.


“Napenda kutumia fursa hii kuufahamisha umma wa Watanzania kuwa mkopo wote wa Dola za Kimarekani 567.25 sawa na Trilioni 1.3 utakuwa mkopo usio na riba kabisa. Shirika la Fedha Duniani (IMF) limefuta masharti katika mkopo wa shilingi trilioni 1.3 na kwa maana hiyo, fedha tulizozichukua, baada ya kipindi cha mpito kupita tutazirudisha hizo hizo sh trilioni 1.3.


“Tathmini ya uhimilivu wa deni uliofanyika Novemba 2021 inaonesha deni letu ni himilivu kwa kipindi cha muda mfupi, wa kati na mrefu. Viashiria vinaonesha kuwa deni la serikali kwa uwiano wa pato la Taifa ni 31% ambapo ukomo wa kidunia ni 55%.


“Thamani ya sasa ya deni la nje kwa pato la Taifa ni 18.8%, ikilinganishwa na ukomo ambao ni 40%. Thamani ya sasa ya deni la nje kwa mauzo ya nje ni 142%, ikilinganishwa na ukomo ambao ni 180%.


“Mhe. Rais wale wasiotambua kuwa unafungua uchumi ili watoto wao wapate ajira wataendelea kuyaelewa haya unayofanya siku ukifungua uchumi, biashara zikakua watoto wao wakapata ajira. Mkopo anapewa mwenye chanzo cha kulipa.


“Kwa hiyo mkopo ni biashara, tajiri na tajiri wanafanya biashara, biashara ya kutumia fedha hizo. Kwa maana hiyo, tutaendelea kukopa ili tutekeleze miradi mikubwa kwa uharaka. Mkopo wa serikali yako wa kwanza ni huu wa trilioni 1.3 ambao hauna riba, mikopo mengine ya serikali ni ile ya Banki ya Dunia ambayo imesainiwa siku nyingi na ulipaji wake ni hadi pale itakapoiva.


“Watu wengine wakisikia neno mkopo wanashtuka, Mkopo sio Msaada, Mkopo anapewa mwenye chanzo cha kulipa , Maskini ambaye hana cha kulipa hapewi Mkopo..Kwa hiyo mkopo ni biashara, tajiri na tajiri wanafanya biashara, biashara ya kutumia fedha hizo. Kwa maana hiyo, tutaendelea kukopa ili kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kwa uharaka.


“Hakuna siku Mtanzania mmoja mmoja atagongewa mlangoni kwake kwamba unadaiwa fedha hizi kwa sababu nchi yako ilikopa, hakuna. Pia, Marais hawakopi, ni serikali. Hili si jambo la familia, ni jambo la serikali,” amesema Mwigulu.
Share:

AUA WATOTO WAKE NAYE KUJIUA KISA MUMEWE KUCHEPUKA




MWANAMKE mmoja, Hellen Vuyanzi (35) amejichoma moto yeye na watoto wake wawili kwa kinachodaiwa kuwa ni kutofautiana na mumewe kutokana na wivu wa mapenzi katika Kijiji cha Sirende eneo la bunge la Lugari.

Katika tukio hilo la siku ya Sikukuu ya Mwaka Mpya wa 2022 katika Kaunti Ndogo ya Lugari, Kakamega nchini Kenya inadaiwa kuwa mtoto wake wa tatu alinusurika katika mkasa huo baada ya kuruka nje ya nyumba kupitia dirishani.

Hellen aliripotiwa kuwa na ugomvi na mumewe na wakashauriwa na maofisa wa polisi wakiongozwa na Kamanda wa Kaunti Ndogo ya Lugari, Bernard Ngungu.

Kwa mujibu wa taarifa, baada ya kusuluhishwa, alirudi nyumbani lakini mume hakufanya hivyo ili kuepusha msuguano zaidi.

“Hellen alikuwa amemtuhumu mumewe kwa kuchepuka baada ya kubaini kuwa alikuwa na uhusiano na mwanamke mwingine,” alisema Kamanda Ngungu na kuongeza kuwa, huenda mwanamke huyo alinunua petroli na kuificha ndani ya nyumba kabla ya kutokea ugomvi na mumewe.

Jirani mmoja aliyekataa jina lake kutajwa, alisema wanandoa hao wamekuwa na ugomvi usioisha baada ya mwanamke huyo kuanza kumshuku mumewe. Vuyanzi walikuwa wameoana kwa miaka 12 na wenzi hao walikuwa na watoto watatu wenye umri wa miaka 11, 4 na 2.

Stephens Okila, shemeji wa marehemu, alisema alikuwa mbali na nyumbani wakati kaka yake alipompigia simu na kumwarifu kwamba aliambiwa kuwa nyumba yake inateketea.


“Tulikimbilia huko na kuthibitisha kuwa ni kweli. Kwa bahati mbaya, mke wake na watoto wawili wenye umri wa miaka 4 na 2 walikuwa tayari wamefia ndani ya nyumba. Mtoto wao mkubwa yeye alifanikiwa kujiokoa kupitia dirishani,” alisema Okila.

Okila alisema hafahamu kuhusu mzozo wowote kati ya mume na mke. “Ningesema kama kulikuwa na tatizo kati yao kwa sababu niko karibu na familia.” Ngungu alisema uchunguzi umeanzishwa kuhusu kifo cha mwanamke huyo na watoto wake.
Share:

SERIKALI YAONGEZA MIEZI 6 KUWASILISHA TAARIFA ZA WAMILIKI MANUFAA WA KAMPUNI


WAZIRI wa Viwanda na Biashara Prof.Kitila Mkumbo,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Januari 4,2022 jijini Dodoma wakati akitoa taarifa ya kuongeza muda wa kuwasilisha taarifa za wamiliki manufaa wa Kampuni (Beneficial Owners).Kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) Godfrey Nyaisa


WAZIRI wa Viwanda na Biashara Prof.Kitila Mkumbo, akitoa taarifa ya kuongeza muda wa kuwasilisha taarifa za wamiliki manufaa wa Kampuni (Beneficial Owners) leo Januari 4,2022 jijini Dodoma.


Kaimu Mkurugenzi Idara ya maendeleo ya Biashara kutoka Wizara ya Biashara na Viwanda Bw.Christopher Mramba,akimkaribisha Waziri wa Viwanda na Biashara Prof.Kitila Mkumbo,kutoa taarifa ya kuongeza muda wa kuwasilisha taarifa za wamiliki manufaa wa Kampuni (Beneficial Owners) leo Januari 4,2022 jijini Dodoma.


Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Makampuni na Majina ya biashara kutoka Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA),Meinrad Rweyamamu,akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) waliouliza maswali katika Mkutano wa Waziri wa Viwanda na Biashara Prof.Kitila Mkumbo, leo Januari 4,2022 jijini Dodoma.


Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) Godfrey Nyaisa ,akijibu Maswali ya waandishi wa habari (hawapo pichani) katika Mkutano wa Waziri wa Viwanda na Biashara Prof.Kitila Mkumbo, leo Januari 4,2022 jijini Dodoma.

................................................

Na Alex Sonna, Dodoma

Waziri wa Viwanda na Biashara, Prof.Kitila Mkumbo, ameongeza muda wa miezi sita kwa kampuni kuwasilisha taarifa za wamiliki manufaa wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA).

Hata hivyo, amesema kwa kampuni zitakazoshindwa kuwasilisha hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

Prof.Mkumbo ameyasema hayo leo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma kuhusu kuongeza muda wa miezi sita kwa ajili ya kuwasilishwa taarifa hizo.

Amesema awali taarifa hizo zilipaswa kuwa zimewasilishwa ifikapo Desemba 31, mwaka jana lakini kutokana na maombi ya wawekezaji kuhusu kuongeza muda, hivyo serikali imeongeza miezi sita ili kutoa nafasi kwa wamiliki hao kuwasilisha taarifa zao.

Waziri huyo amesema kampuni zilizowasilisha taarifa hizo hadi jana ni 14,026 sawa asilimia 14 ya matarajio.

Amefafanua kuwa kampuni zote nchini husajiliwa na BRELA na hupaswa kutoa taarifa kadhaa ikiwamo wamiliki manufaa wa kampuni na awali hazikulazimika kisheria kutoa taarifa za waliopo nyuma ya kampuni(wamiliki manufaa) lakini kwasasa ni lazima.

“Hawa wamiliki manufaa ndio wenye mtaji na wanaendesha kampuni, hivyo Benki ya Dunia na taasisi zingine kimataifa zimehimiza kueleza kwa uwazi umiliki wa kampuni,”amesema.

Amesema kutokana na umuhimu wa taarifa hizo na kwa mamlaka aliyonayo kisheria ameongeza muda huo hadi Juni 30, mwaka huu ili wamiliki wote watimize matakwa ya sheria.

“Niwahimize wamiliki wote watumie muda vizuri wa nyongeza na sheria ipo wazi kwa yule ambaye hatawasilisha taarifa zake hatua gani zitachukuliwa dhidi yake,katika kujenga mahusiano mema na wafanyabiashara tumekubaliana kuongeza muda huu,”amesema.

Naye, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Makampuni na Majina ya biashara kutoka BRELA,Meinrad Rweyamamu, amesema sheria ya makampuni imeweka utaratibu pale ambapo mtu atachelewesha kuwasilisha taarifa atakumbana na adhabu ya kulipa Sh.2500 kila mwezi.

“Kwa kila mwezi ambao atakuwa amechelewesha taarifa atapaswa kulipa kiasi hicho, sambamba na hilo ikibainika haikuwasilisha taarifa za wamiliki manufaa au kuwasilisha taarifa ambazo si za kweli Mahakama itaipiga adhabu kampuni hiyo ya faini kuanzia Sh.Milioni tano hadi 10,”amesema.

Amesema kampuni ambazo zimekuwa zikipeleka taarifa za mwaka ni zaidi ya 140,000 na kwamba bado kampuni nyingi hazipeleki taarifa zao BRELA hivyo wanatarajia kutoa taarifa ya kampuni zisizo hai ili zihuishe taarifa zao.
Share:

Live : RAIS SAMIA KATIKA HAFLA YA KUPOKEA TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA MATUMIZI WA FEDHA ZA UVIKO - 19

 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa mgeni rasmi katika hafla ya kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa matumizi ya fedha za maendeleo kwa ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya Virusi vya Korona (UVIKO-19) leo Januari 4,2022 Ikulu jijini Dar es Salaam.Tazama chini;
Share:

RAIS SAMIA AMJULIA HALI SHEIKH MKUU WA TANZANIA MUFTI ABUBAKAR BIN ZUBEIR


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimjulia hali Sheikh Mkuu wa Tanzania Mufti Abubakar Bin Zubeir anayepatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Jijini Dar es Salaam leo tarehe 04 Januari 2022.

PICHA NA IKULU
Share:

BROTHERHOOD SURVEY SERVICES CO.LTD WATANGAZA MRADI MPYA WA VIWANJA SHINYANGA MJINI....KIWANJA CHAKO KIPO KUANZIA LAKI 5 TU

Karibu Brotherhood Survey Services Company Limited!

Tuna mradi mpya sasa unaopatikana eneo la Mwalugoye kata ya Chibe Manispaa ya Shinyanga
Kwa bei nafuu kabisa.

Tunauza mita moja ya mraba shilingi 2,500/= za Kitanzania
Pamoja na hati miliki.

Tuna viwanja kuanzia bei ya laki 562,500/= na kuendelea kulingana na ukubwa wa kiwanja unavyoongezeka.

Tupo tayari kukuhudumia!!

Tunapatikana Mjini Shinyanga ghorofa ya kwanza katika Jengo la NSSF Mpya Pembezoni mwa Barabara ya Mwanza - Shinyanga (Eneo maarufu kwa jila la Level Four)

Wasiliana nasi : 0627030702 au 0677000021 au 0677000028


Share:

RAIS SAMIA ATEUA VIONGOZI MBALIMBALI LEO


Share:

Monday, 3 January 2022

MCHUNGAJI AWAVUA NGUO WANAWAKE ' LIVE' KANISANI..AWAPAKA MAFUTA YA UPAKO WAOLEWE

Haya ni maajabu ya fungua mwaka!, ama kweli  basi humu duniani hakuishi vituko kila kuchao. 

 Mchungaji wa kanisa moja nchini Ghana katika mitandao ya kijamii akiwavua nguo wanawake tena kanisani na kuwaogesha na kuwapaka mafuta huku ikidaiwa kwamba kufanya hivyo ni kuwapa upako wa ndoa akina mama hao.

Tukio la aina yake linadaiwa kufanyika siku ya mkesha wa mwaka mpya, Desemba 31, 2021 kuamkia Januari 1, 2022 kaninani hapo ambapo mchungaji huyo ambaye jina lake bado halijafahamika mara moja, amesema kuwa kuwaosha wanawake ni kuwasafisha, kuwaondolea mikosi na kuwapa upako hivyo kuwafanya wawe watakatifu.

Mchungaji huyo raia wa Ghana, amezua mjadala moto mtandaoni kwa kupeperusha video mubashara ya mkesha wa Mwaka Mpya akiwafanyia washirika wa kike tambiko ya kushangaza.

Katika video inayosambaa kama moto mtandaoni, pasta huyo anasikika akiwambia kondoo wake wajitokeze haraka kwa "kuoga takatifu" 

Baadhi ya washirika wanaonekana wakivua nguo zote na kubaki uchi wakiingia ndani ya beseni na baada ya kuogeshwa, pasta mwingine anaonyeshwa akiwapaka mafuta takatifu.

Pasta huyo pia anasikika akisema kuwa licha ya kufahamu kwamba hatua hiyo itazua utata, hana budi ila kuheshimu maagizo ya roho mtakatifu.


 


Pasta azindua chupi zenye picha yake


Huku mtumishi huyo akiwaogesha kondoo wake wa kike, mwingine nchini Nigeria amezindua chupi na sindiria zenye chapa ya picha yake ili kuwasaidia wanawake waseja wanaotamani kuolewa kuwavizia waume zao.

 Kulingana na pasta Dr J.S. Yusuf, ambaye ni mkuu wa Kanisa la Touch for Recovery Outreach International mjini Abuja, aliagizwa na Mungu kuzindua chupi hizo za 'baraka' ili kufungua milango ya ndoa Mwaka Mpya.

Mchungaji huyo alinukuu mstari kwenye kitabu cha Hesabu 23:20 unaosema “Tazama nimepokea amri ya kubariki, naye amebariki, wala siwezi kubadili.” 

Pia alisema kuwa chupi hizo zinapovaliwa na wanawake, zitawasaidia kupigana na magonjwa na kupata bahati njema ya kuwavizia wanaume ambao watawaoa.

 Itakumbukwa kwamba si mara ya kwanza kwa watumishi wa Mungu kufanya mambo ya kiajabu hususan wanaotokea katika mataifa ya magharibi mwa Afrika. 

Mhubiri ambaye ni raia wa Ghana, Osofo Acheampong, alitoa kauli nzito kwa kusema kwamba sio vibaya kwa mwanamume kuwa na mpango wa kando hata ingawa ni mume wa mtu.

Pasta Acheampong, anayesemekana kuwa kiongozi wa Kanisa la Kipentekosti la Sabato, alitoa maoni hayo kwenye mahojiano ya hivi punde huku akitoa mafungu ya Bibilia kuipa uzito kauli yake.
Share:

RAIS MWINYI AMTUMBUA MKURUGENZI MKUU WA SHIRIKA LA UTANGAZAJI ZANZIBAR



Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Zanzibar, Dk. Saleh Yusuf Mnemo.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Katibu Mkuu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi wa Zanzibar, Mhandisi Zena Said, utenguzi huo umeanza leo, Januari 3, 2022.
Share:

AHMED ALLY : NDOTO IMETIMIA KWENDA KUFANYA KAZI NDANI YA SIMBA SC




Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha Simba SC Ahmed Ally,  amezungumza kwa mara ya kwanza baada ya kupata wadhifa huo. Ahmed ameonesha furaha yake na tayari yuko njiani kuelekea Zanzibar kuungana na kikosi kwenye Mapinduzi Cup.

Alichokisema Ahmed; “Nimeipokea nafasi hii kwa uzito wa Dunia Nzima, ni habari njema, ni habari kubwa, ni habari nzuri kweli kweli, ni ndoto imetimia ya kwenda kufanya kazi ndani ya Simba SC, kwa hiyo uzito wa habari hii unaweza kusema ni uzito wa Dunia Nzima.

“Naimani mimi ni chaguo sahihi kwa klabu ya Simba na ndio maana mchakato wa kumtangaza Afisa Habari wa Simba SC ulikua mrefu, hii ilimaanisha Uongozi ulikua unatafuta mtu sahihi na mkweli na awe Simba SC,” amesema Ahmed Ally.
Share:

BWANYENYE KAMCHUKUA MKE WANGU

Tulikuwa tumeenda hospitalini kumpeleka mtoto wetu kufanyiwa vipimo vya Maleria Ijumaa iliyopita ndipo hili jambo lilipotokea. 


Mimi na kipenzi Aisha tulichukua bodaboda hadi mji wa Mbeya kuliko hiyo hospitali ya watoto, na tulipofika kisha tukaketi kwa kiti cha wageni kilichokuwa hapo kwa daktari ndipo niliona bwenyenye flani aliyekuwa amekalia karibu na bibi yangu akimuomba nambari ya simu. Niliacha tu apewe manaake nilijua hawataenda mbali naye.

 Kweli bibi yangu alikuwa na makosa kufanya dharau mbele yangu lakini nilipomuuliza mbona apeane namba nikiona aliniambia hata huyo bwenyenye akipiga simu yeye huwa hachukui simu za watu kama hao. 


Roho yangu ilichafuka siku hiyo hata bibi yangu alijua nimekasirika wakati wa usiku sababu sikumkaribia. Wiki moja baadaye bibi yangu alipokuwa kwa bafu nikachungulia simu yake na niliyoyaona Mungu ndiye anajua. Picha na video za mapenzi.


 Kwa picha moja huyo bwana amemtumia  picha yake ya utupu. Nilijua mimi na huyo bibi imeisha.

 Alipotoka bafuni mimi nilikaa tu kimya tu hadi asubuhi nikaelekea kwa Daktari mmoja niliyemfahamu tangu kitambo. Ni Daktari wa kienyeji anayeitwa Kiwanga. Nilipofika nilimuambia yote na akanipa kamti fulani. Aliniahidi kuwa baada ya siku moja tu huyo bwna atanitafuta kuomba msamaha. 


Kweli yalikuwa hivyo. Jamaa lilikuja kwangu likisema linachomeka kwa ‘mali’ yake na mimi huku nikijiambia kimoyo kuwa Daktari Kiwanga anafanya kazi. 


Bibi yangu naye sehemu yake nyeti pia ilianza kuuma maumivu makali. Ilifika mahali akajua ni mimi nimewaendea mahali kuwafunza funzo.


 Usiku n na mchana, aliniomba nimsamahe. Nilifanya hivyo na kasha nilimfukuza kutoka kwa boma langu huku huyo jamaa akinilipa milioni moja nimrudishie afya yake. Nilimpeleka kwa dakatri Kiwanga amtengeze.


 Bibi pia alitengenezwa. Kama unajua una matatizo na mambo ya mapenzi kwa nyumba yako tafadhali nakusihi pigia matabibu wa Kiwanga. Kiwanga Doctors ni shujaa wa mambo yote. Natoa wito kwa wenye shida za magonjwa, mapenzi, ndoa, biashara, kikazi na afya kuharakisha kuwatembelea madaktari wa Kiwanga. 


Tuvuti au Website yao ni:www.kiwangadoctors.com; Simu: +254 769404965 au wasiliana kwa barua pepe yaani Email kwa: kiwangadoctors@gmail.com. Si lazima usafiri hadi ofisi zao. Ongea nao kwa njia ya simu na utasaidika kwa haraka kama vile watu wengine wanavyopata usaidizi





Share:

BENKI YA CRDB YAZINDUA KAMPENI KUHAMASISHA WATANZANIA KUTUMIA HUDUMA NA BIDHAA BUNIFU CRDB



Benki ya CRDB imewataka Watanzania kutumia huduma na bidhaa bunifu zinazotolewa na benki hiyo kwa makundi mbalimbali ya wateja kufanikisha malengo waliyojiwekea katika mwaka huu mpya wa 2022. Hayo yamesemwa wakati wa uzinduzi wa kampeni ya “Unachostahili ni CRDB Bank” inayolenga katika kutoa elimu na kuwaonyesha Watanzania fursa mbalimbali zinazotolewa na Benki yao ya CRDB


Akizungumza katika uzinduzi wa kampeni hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela alisema Benki ya CRDB ikiwa benki ya kizalendo inatambua kuwa inawajibu wa kuwasaidia Watanzania na wadau wengine wa maendeleo nchini kutimiza malengo katika mwaka huu mpya 2022. Nsekela alisema kupitia kauli mbiu yake ya “Benki inayomsikiliza mteja”, Benki ya CRDB imekuwa ikisikiliza na kufanyia kazi mahitaji ya wateja ili kuwapa wanachostahili.
“Mwaka jana tulifanya utafiti maalum kufahamu mahitaji halisi ya wateja ambayo yamekuwa yakibadilika kila uchwao, utafiti ule ulienda sambamba na kupokea maoni ya namna bora ya kuwahudumia wateja. Ninajivunia kusema tumeweza kufanyia kazi maoni ya wateja na kuboresha sehemu kubwa ya huduma na bidhaa zetu ili kuweza kuwapa wanachostahili,” amesema Nsekela.


Nsekela alisema moja ya maeneo ambayo Benki hiyo imeyafanyia maboresho ni katika mtandao wa ufikishaji huduma za kibenki ambao unajumuisha mifumo ya kidijitali ikiwamo SimBanking, CRDB Wakala, TemboCard, na Internet banking ambayo inawawezesha wateja kupata huduma popote pale walipo. Hivi sasa wateja wa Benki ya CRDB wanaweza kupata zaidi ya asilimia 90 ya huduma kupitia njia hizo mbadala za upatikanaji wa huduma.
“Tunatambua wateja wanahitaji muda mwingi zaidi katika kufanya shughuli zao za kiuchumi, hivyo uboreshaji wa mifumo hii utawawezesha kufanya miamala yao kwa wakati na hivyo kuongeza ufanisi katika biashara na maeneo yao ya kazi hivyo kuongeza ufanisi,” amesema Nsekela huku akibainisha maboresho hayo yamesaidia kuongeza urahisi na unafuu wa kwa wateja.


Katika kampeni hiyo Benki ya CRDB pia imejipanga kuwaelimisha wateja juu ya huduma za uwezeshaji zinazotolewa na benki hiyo kupitia mikopo kwa makundi mbalimbali ya wateja ikiwamo wanafunzi, wafanyakazi, wajasiriamali, wakulima, wafanyabishara, makampuni na taasisi. “Niwahakikishie kuwa Benki yetu ina uwezo mkubwa kimtaji unaowezesha kutoa mikopo kwa makundi mbalimbali kwa gharama nafuu, hivyo niwasihi Watanzania kuchangamkia fursa zilizopo kufikia malengo yao.”
Nsekela alisema benki hiyo pia imejipanga kuendelea kushiriki kikamilifu katika miradi ya kimkakati ya Serikali huku akimpongeza Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendeleza utekelezaji wa miradi hiyo. “Ukubwa wa mizania yetu unatufanya tuwe na uwezo mkubwa wa kushiriki katika kuwezesha wadau wote wanaoshiriki katika miradi hii ikiwamo Serikali yenyewe, pamoja na wakandarasi na wazabuni,” amesema Nsekela.


Aidha, Nsekela alieleza kuwa katika kipindi cha kampeni hiyo wateja pia watakuwa wakielimishwa juu ya umuhimu wa kujiwekea akiba ili kufikia malengo kwa kutumia akaunti mbalimbali za benki hiyo. Benki ya CRDB ina akaunti zinazoongoza makundi mbalimbali ya wateja kuanzia akaunti za Junior Jumbo maalum ya watoto, wanafunzi - Scholar, wafanyakazi - Salary, wajasiriamali - Hodari, wafanyabiashara - Current, wakulima – FahariKilimo, Wanawake - Malkia na hata Wastaafu – Pension Account.


“Hizi ni baadhi tu ya fursa nyingi ambazo wateja na wadau wetu wanastahili ili kufikia malengo yao kwa mwaka huu 2022. Katika kipindi hiki cha kampeni tumejipanga kuhakikisha tunatoa huduma za daraja la kwanza kwa wateja wetu ili wawaeze kunufaika na fursa hizi zinazotolewa na benki yao.,” amesema Nsekela.
Naye Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa amesema benki hiyo itaendelea kutekeleza ahadi yake ya kumuweka kwanza mteja na kuwakaribisha Watanzania wote, wateja binafsi, makampuni, na taasisi kuchangamkia fursa hizo kufikia malengo yao. “Benki yetu ni imara na yenye kuaminika kwa ubunifu hapa nyumbani na nje ya nchi.


Nafikiri wote tumeona tulivyopokelewa vizuri hata nchi za jirani za Burundi na Congo, na inavyoaminika na Serikali kwa kuwa na mchango mkubwa kwenye kusaidia kujenga uchumi,” alisema Tully huku akiwataka wafanyabiashara wanaofanya biashara nan chi za jirani pia kutumia fursa zinazotolewa na benki hiyo.
Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Masoko, Benki ya CRDB, Joseline Kamuhanda aliwashukuru Watanzania kwa kuendelea kuichagua benki hiyo kuwa mtoa huduma wao na kuwaahidi benki hiyo itaendelea kuwapa wanachostahili kupitia bidhaa na huduma bunifu.


--
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger