Wednesday, 1 December 2021

Wauza Madini Feki Wanaswa Sikonge


 Na Lucas Raphael,Tabora
Mwanamke mmoja mkazi wa mkoani wa Arusha amekamatwa na Jeshi la Polisi katika stendi ya mabasi wilayani Sikonge Mkoani Tabora kwa tuhuma za kukutwa na madini feki aina ya Dhahabu  waliyokuwa wakiwauzia wananchi wa kishrikiana na dereva wake .

Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari jana Kamanda wa Polisi Mkoani hapa ACP Richard Abwao alisema walimkamata Mariam Said, mkazi wa Arusha akiwa na dereva wake David George wakiwa na madini hayo waliyoyatumia kumtapeli mkazi wa kijiji cha Usunga wilayani humo aitwaye Edward.

Alibainisha kuwa watuhumiwa walikamatwa baada ya kumtapeli mkazi huyo kiasi cha sh 340,000 ambapo pia baada ya kukaguliwa walikutwa na kadi 5 za benki tofauti tofauti ambazo ni kadi za NMB 3, Posta 1na CRDB 1.

Vitu vinginevyo walivyokutwa navyo ni simu 4 aina ya iphone 6s plus, Tecno Spark 5 Air, Infinix hot 10 na Sam sung zinazodhaniwa kuwa za wizi.

Kamanda Abwao alibainisha kuwa madini hayo yamekamatwa kutokana na jitihada za Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na wananchi na vyombo vya ulinzi na usalama katika kuzuia, kutanzua na kupambana na uhalifu.

Aidha aliongeza kuwa katika kukabiliana na matukio ya uhalifu, mauaji, unyang’anyi wa kutumia silaha, ujambazi na uvunjaji Mkoani humo, Jeshi hilo limeendelea kufanya oparesheni mbalimbali katika wilaya zote.

Alitaja mafanikio ya oparesheni hiyo kwa mwezi huu kuwa ni kukamatwa watu 2 Khamis Baruti na Mohamed Shaban wakazi wa Izimbili wilayani Uyui kwa kukutwa na silaha aina ya gobore isiyo na namba za usajili iliyokuwa ikitumika kwenye uwindaji haramu.

Aidha walikamata silaha 2 aina gobore zilizosalimishwa na watu wasiojulikana katika kata za Kipanga na Mole ( Usanganya) wilayani Sikonge na silaha nyingine ilisalimishwa na mkazi wa Mibono John Matuzya katika Ofisi ya Mtendaji wa Kata ya Kiloleni akidai anatii sheria bila shuruti.

Kamanda alitoa wito kwa wananchi wanazomiliki silaha kinyume na utaratibu kuendelea kuzisalimisha ndani ya kipindi hiki cha msamaha wa Waziri wa Ulinzi vinginevyo watakamatwa, aliitaka jamii kuendelea kushirikiana na Jeshi hilo kwa kutoa taarifa za vitendo vya uhalifu na wahalifu.


Mwisho.


Share:

REA YATAMBULISHA WAKANDARASI NA KUKABIDHI MIKATABA YA MRADI WA KUSAMBAZA UMEME VIJIJI 216 SHINYANGA

Kaimu Mkurugenzi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Elineema Mkumbo (kushoto) akimkabidhi Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zuwena Omary Mikataba itakayotumiwa na Wakandarasi kutekeleza Mradi wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili unaotarajia kunufaisha vijiji 216 mkoani Shinyanga kwa gharama ya zaidi ya shilingi Bilioni 60.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Wakala wa Nishati Vijijini (Rural Energy Agency – REA) umetambulisha kwa uongozi wa Mkoa wa Shinyanga Wakandarasi wanaotekeleza Mradi wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili na kukabidhi Mikataba itakayotumiwa na Wakandarasi Kutekeleza Mradi huo unaotarajia kunufaisha vijiji 216 kwa gharama ya zaidi ya shilingi Bilioni 60.


Akizungumza leo Jumatano Desemba 1,2021 wakati wa kukabidhi Mikataba hiyo kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zuwena Omary , Kaimu Mkurugenzi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Elineema Mkumbo amewataja Wakandarasi watakaosimamia mradi wa usambazaji umeme wilayani Kahama, Shinyanga na Kishapu kuwa ni Suma JKT na Tontan Project Technology Co. Ltd.


Mhandisi Mkumbo amesema kutokana na maelekezo ya Serikali ni lazima vijiji vyote vinatakiwa kupatiwa huduma ya umeme ifikapo Mwezi Desemba mwaka 2022.


“Kwa niaba ya Bodi ya Nishati Vijijini, Menejimenti pamoja na Wafanyakazi wa REA tunakukabidhi Mikataba ya kupeleka umeme kwa uongozi wa Mkoa wa Shinyanga ili uendelee kutusaidia katika usimamizi wa mradi wa kupeleka umeme vijijini awamu ya tatu mzunguko wa pili katika mkoa wa Shinyanga. Kufuatia maelekezo ya Serikali ni lazima vijiji vyote vinapata umeme ifikapo Mwezi Desemba mwaka 2022”,amesema Mhandisi Mkumbo.


“Mradi huu tumeugawa katika mafungu mawili ili kuharakisha utekelezaji wake. Fungu la kwanza linaenda Wilaya ya Kahama ambapo gharama ya mradi ni shilingi Bilioni 39. Fungu la pili ni kwa ajili ya wilaya ya Kishapu na halmashauri ya Shinyanga ambapo gharama yake ni zaidi ya Bilioni 21. Hivyo kwa mkoa wa Shinyanga tuna zaidi ya Bilioni 60 ili kukamilisha upelekaji wa umeme katika vijiji”,ameongeza Mhandisi Mkumbo.


Amebainisha kuwa huwa kuna changamoto zinajitokeza wakati Wakandarasi wanapofika ‘Site’ kwa hiyo wameona wafanye maandalizi ya mapema kuziwahi hizo changamoto kabla hazijafika mbali hivyo wamekutana REA, TANESCO na Wakandarasi ili wajue changamoto ni zipi huku wakizingatia vipaumbele vya serikali.


“Pia ilikuwa ni lazima tuwatambulishe Wakandarasi wetu kwenye Uongozi wa Serikali ya Mkoa wa Shinyanga. Kwa hiyo tuna Kampuni ya Tontan Project Technology Co. Ltd ambayo itatekeleza mradi katika wilaya ya Kahama na SUMA JKT ambao watakuwa wilaya ya Kishapu na Shinyanga Vijijini”,amesema.


Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zuwena Omary ameelekeza kwamba Mkandarasi anapokwenda eneo lolote la mradi TANESCO lazima wawepo, uongozi wa eneo husika uwepo ili uweze kuainisha sehemu za kipaumbele na kuhakikisha REA inafuatilia.


“Wananchi wanasubiri sana huduma ya umeme kwa sababu umeme ni muhimu kwa maendeleo ya jamii kwani kila kila kazi inayofanyika inahitaji nishati ya umeme. Tunaamini kabisa kwamba umeme ukifika hata kasi ya maendeleo itakuwa kubwa. Serikali inasubiri umeme na tupo tayari kutoa ushirikiano utakaohitajika wakati Wakandarasi wakiwa ‘Site’ ,cha muhimu ni Mkandarasi awe mwepesi kutoa changamoto ambazo zitakazokuwepo kwenye maeneo ya mradi”,amesema Omary.


“Mara nyingi miradi ya umeme inapopita kunakuwa na changamoto ya mradi unapoelekea siyo kwenye mahitaji makubwa na ya lazima ya jamii, nendeni mkazichukue hizo changamoto na mzifanyie kazi,isitokee mradi unapelekwa maeneo ya mbali sana na kuacha vijiji vikubwa vyenye uhitaji mkubwa wa umeme, tuanze na hao wenye athari kubwa za kijamii na kimaendeleo”,amesema.

Amebainisha ili mradi huo ukamilike kwa wakati ni wajibu wa kila mmoja kuhakikisha anatimiza wajibu wake ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa kuhusu changamoto zinazojitokeza.


“Nina hakika kabisa kila mmoja, Mkandarasi, TANESCO, REA, Serikali ya mkoa wote tunataka kuhakikisha mradi unatekelezwa kwa wakati. Kinachotakiwa ni kila mmoja atimize wajibu wake,kila mmoja awe na wajibu wa kutoa taarifa kwa mwingine iwapo anahitaji msaada ‘Support’ wa changamoto anayokutana nayo”, amesema Mhe. Omary


Msimamizi wa Miradi ya REA - TANESCO Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Anthony Tarimo amesema mradi huo unatarajia kunufaisha vijiji 216 vya Mkoa wa Shinyanga na sasa wapo kwenye hatua za awali za utekelezaji wa mradi huu ikiwa ni pamoja na kuangalia namna ya kuingiza kwenye mradi vijiji 30 vilivyokuwa vimesalia kupatiwa umeme kwenye mipango iliyopita kwani serikali ilishatoa maagizo vipatiwe umeme kupitia Mradi huu mpya.


Naye Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Ukandarasi ya Tontan Project Technology Co. Ltd, Nasra Mwampashe ambao ni Wakandarasi wa Mradi huo wa REA wilaya ya Kahama wenye thamani ya shilingi Bilioni 39 ameahidi kuwa watatekeleza mradi huo kwa ufanisi na weledi mkubwa na kuhakikisha mradi unakamilika kwa wakati uliopangwa.


“Tukiwa Wakandarasi tunaishukuru sana Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutuamini na kutupatia huu mradi. Tunaahidi kufanya kazi kwa ufanisi na weledi wa hali ya juu kwa sababu uwezo tunao, nguvu tunayo, vifaa tunavyo na tumejipanga vilivyo kuhakikisha mradi unakamilika ndani ya muda tuliopangiwa”,amesema Mwampashe.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Kaimu Mkurugenzi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Elineema Mkumbo (kushoto) akimkabidhi Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zuwena Omary Mikataba itakayotumiwa na Wakandarasi kutekeleza Mradi wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili unaotarajia kunufaisha vijiji 216 mkoani Shinyanga. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kaimu Mkurugenzi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Elineema Mkumbo (kushoto) akimkabidhi Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zuwena Omary Mikataba itakayotumiwa na Wakandarasi kutekeleza Mradi wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili unaotarajia kunufaisha vijiji 216 mkoani Shinyanga.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zuwena Omary akionesha Mikataba itakayotumiwa na Wakandarasi kutekeleza Mradi wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili unaotarajia kunufaisha vijiji 216 mkoani Shinyanga kwa gharama ya zaidi ya shilingi Bilioni 60.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zuwena Omary akizungumza wakati Wakala wa Nishati Vijijini (Rural Energy Agency – REA) ukitambulisha kwa uongozi wa Mkoa wa Shinyanga Wakandarasi wanaotekeleza Mradi wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili na kukabidhi Mikataba itakayotumiwa na Wakandarasi Kutekeleza Mradi huo.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zuwena Omary akizungumza wakati Wakala wa Nishati Vijijini (Rural Energy Agency – REA) ukitambulisha kwa uongozi wa Mkoa wa Shinyanga Wakandarasi wanaotekeleza Mradi wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili na kukabidhi Mikataba itakayotumiwa na Wakandarasi Kutekeleza Mradi huo.
Kaimu Mkurugenzi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Elineema Mkumbo akizungumza wakati akitambulisha kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zuwena Omary Wakandarasi wanaotekeleza Mradi wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili na kukabidhi Mikataba itakayotumiwa na Wakandarasi Kutekeleza Mradi huo.
Kaimu Mkurugenzi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Elineema Mkumbo akizungumza wakati akitambulisha kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zuwena Omary Wakandarasi wanaotekeleza Mradi wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili na kukabidhi Mikataba itakayotumiwa na Wakandarasi Kutekeleza Mradi huo.
Kaimu Mkurugenzi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Elineema Mkumbo (katikati) akizungumza wakati akitambulisha kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zuwena Omary Wakandarasi wanaotekeleza Mradi wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili na kukabidhi Mikataba itakayotumiwa na Wakandarasi Kutekeleza Mradi huo.
Kaimu Mkurugenzi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Elineema Mkumbo akielezea namna walivyojipanga kutekeleza Mradi wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili  mkoani Shinyanga.
Msimamizi wa Miradi ya REA - TANESCO Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Anthony Tarimo akielezea namna vijiji 216 mkoani Shinyanga vitakavyonufaika na Mradi wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili.
Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Ukandarasi ya Tontan Project Technology Co. Ltd, Nasra Mwampashe akielezea namna walivyojipanga kutekeleza kwa ufanisi na weledi mkubwa Mradi wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili wilayani Kahama.

 Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog


Share:

Tanzania Yanadi Vivutio Vyake Vya Utalii Kwenye Mkutano Mkuu Wa 24 Wa Utalii Duniani Nchini Hispania


NA MWANDISHI MAALUM, MADRID, HISPANIA
UJUMBE wa Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro upo nchini Hispania, katika Jiji la Madrid kushiriki mkutano mkuu wa 24 wa Kimataifa wa Utalii Duniani ulioandaliwa na Shirika la Kimataifa  linaloshughulikia masuala ya Utalii Duniani ( UNWTO)

Katika mkutano huo wa siku nne ulioanza jana, unaotarajiwa kufunguliwa  rasmi leo hii Desemba Mosi, ambapo Waziri Ndumbaro akiwa katika jiji hili la Madrid, ameweka bayana mambo mbalimbali ambayo Tanzania itanufaika na mkutano huo.
 
Akizungumzia mambo hayo, Dkt. Ndumbaro amesema  ''katika  kuhakikisha kwamba tunaongeza idadi ya watalii kuitembelea Tanzania pamoja na mapato yatokanayo na Utalii, suala la kutangaza utalii wa Tanzania katika nyanja za kidunia ni suala ambalo haliepukiki ''

Ametaja moja ya kati ya maeneo ya  kutangaza Utalii huo, ni kuhudhuria mikutano mikubwa duniani ambayo Inahusisha masuala ya Utalii  ikiwemo kuja nchini Hispania ambako ndiko makao makuu ya utalii Duniani  katika jiji la Madrid, kwa ajili ya  kuhudhuria mkutano mkuu huu wa 24.

Ikiwa ni siku ya kwanza ya mkutano huo Tanzania ilipata fursa kadhaa ikiwemo kutumia  mkutano huu kutangaza vivutio vilivyopo Tanzania, kuwaambia dunia nzima  kwamba Tanzania  ipo salama na kuwataka watalii kuja kujionea vivutio vya utalii ilivyonanvyo

''Waje Tanzania wauone Mlima Kilimanjaro, waje Tanzania waione Serengeti, waje Tanzania waione Ngorongoro, waje Tanzania waone fukwe nzuri zenye mchanga mweupe zilizopo Zanzibar, waje Tanzania waone vivutio mbalimbali ambavyo tupo navyo.’’ Alisema Dkt. Ndumbaro.

Dkt. Ndumbaro aliongeza kuwa, katika suala la pili katika mkutano huo, Tanzania itasaini mkataba na UNWTO wa kuweza kuwa mwenyeji wa mkutano wa 65 wa Utalii Barani Afrika ambao utafanyika kati ya tarehe 6-8 Oktoba 2022 katika jiji la Arusha.

‘’Mkutano huu tunauleta kwa sababu ni fursa nyingine kwa  Tanzania, Tulishapewa kuwa mwenyeji wa mkutano wa utalii wa kanda ya Afrika  kule nchini Cape verde, lakini sasa tumekuja kusaini makubaliano ya kuwa wenyeji wa  mkutano huo, baada ya kusaini sasa tutakuwa na uhakika asilimia 100 na tumetengeneza ‘Post card’ ambapo kila mshiriki aliyekuja hapa tunampa post kadi hizi ambayo inasaidia sana kutangaza utalii wa Tanzania.’’ Alisema Dkt. Ndumbaro.

Aidha, alisema kuwa suala la tatu kwenye mkutano huo, Tanzania imekuwa  katikak  mstari wa mbele kupigania haki za Watalii ambapo watashiriki katika kufanikisha sheria ya Kimataifa inapitishwa.

‘’Jambo lingine ambalo tunalifanya katika mkutano huu, ni kupitisha sheria ya kutetea haki za watalii duniani pale inapotokea matatizo.. tumejifunza kutokana na kadhia ya UVIKO 19 kwamba nchi zilifunga mipaka, na baada ya nchi kufunga mipaka , watalii walikuwa wapo  kwenye nchi zingine na hawaweza kurudi.

‘’Sasa haki zao zilikuwa haziwezi kutetewa na sheria za kimataifa. Kwa hiyo sasa tunapitisha sheria ya kimataifa ya kutetea watalii katika mazingira ya dharura kama hayo. Ni sheria ambayo itaongeza heshima ya baishara ya utalii duniani, kwa sababu unapolinda haki ya mtalii, mtalii anajiona yupo salama zaidi kuja na kushiriki katika  nchi yako, Tanzania tumekuwa mstai wa mbele kuhakikisha sheria hiyo inapita.’’ Alisema Dkt. Ndumbaro.

Dkt. Ndumbaro alisema kuwa, mkutano huo una faida nyingi sana kwa nchi Tanzania, katika kuhakikisha kwamba tunatimiza idadi ya watalii milioni tano na mapato zaidi ya  bilioni sita.

‘’Tunatumia mkutano huu kama fursa ya sisi kuweza kutangaza utalii, lakini kama fursa ya kuwavuta wenzetu waje pia, tumepongezwa kwa namna ambavyo tumeweza kufanya onesho la kwanza la utalii katika nchi za Afrika Mashariki. Sisi tuliona dogo, lakini wenzetu huku katika nyanja za kimataifa tumepongezwa na nimesema kwamba kumbe kweli watanzania wanaweza kufanya mikutano kwa kiwango kikubwa zaidi’’ alisema Dkt. Ndumbaro.

Mkutano huo wa 24 wa Kimataifa wa Utalii duniani, ni wa siku nne, kuanzia jana Novemba 30 hadi 3 Desemba, ukijumuisha ujumbe mbalimbali wakiwemo Mawaziri wa Utalii, viongozi wakuu wanchi, Mashirika ya Kimataifa ya Serikali, binafsi, wadau wa Utalii  na watu mbalimbali waalikwa.

Mwisho.


Share:

Tanzania yafuzu kombe la Dunia mchezo wa soka kwa wenye ulemavu.


Na. John Mapepele
Waziri mwenye dhamana ya Michezo nchini. Mhe, Innocent Bashungwa leo Disemba 1, 2021 amewaongoza watanzania kuishangilia Timu ya Tanzania (Tembo Warriors) ambayo imefuzu na kuwa  timu ya kwanza miongoni mwa timu nne zinazoingia nusu fainali ya Soka ya Bara la Afrika kwa   wenye ulemavu (CANAF 2021) na hivyo kupata tiketi ya kushiriki  Mashindano ya Dunia  ya mchezo huo yatakayofanyika nchini Uturuki 2022 baada ya kuichapa timu ya Cameroon  mabao 5-0.

Timu ya Tanzania ambayo katika kipindi chote cha maandalizi imesimamiwa na  Kamati Maalum ya Kitaifa  chini ya Katibu Mkuu wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassani Abbasi ilianza vizuri  kutokana hamasa  iliyotolewa  na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe, Samia Suluhu Hasan.

Katika mechi zote za mashindano haya Tanzania imepoteza mechi moja tu ya Uganda mbayo ilifungwa goli 1-0, ambapo Tembo iliifunga timu ya Morocco 2-1 na Sierra Leone ambapo  tembo ilishinda  goli 1-0.


 Akizungumza na Waandishi wa Habari mara  baada ya mechi hii, Mhe. Bashungwa amewahakikishia kwamba Serikali itaendelea kuiisaidia  timu  hiyo ili iendelee  kufanya vizuri  maandalizi ya Kombe  la Dunia.

 Aidha, Dkt Abbasi amesema  kwa  kuwa  safari ya kuelekea  kombe la  dunia imekamilika kazi iliyobaki ni kuhakikisha kuwa  kombe  linabaki  Tanzania.

Magoli mawili ya Tanzania yamefungwa na  Alfan Kyanga dakika ya  2 na 15 , Ramadhan Chomole  dakika ya  18, na Frank Ngailo  dakika ya  36 na  44.

Mchezo huo pia umeshuhudiwa na  Rais wa Mashindano hayo duniani  Mateus Wildack.


Share:

Kamishna Mkuu TRA Awapongeza Wanamichezo Kwa Kuibuka Washindi Shimmuta


Na Mwandishi wetu
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania amewapongeza watumishi wa Mamlaka hiyo ambao ni wanamichezo kwa kuibuka washindi katika michuano ya SHIMMUTA iliyokuwa ikitimua vumbi hivi karibuni Mkoani Morogoro kwa kutwaa vikombe vitano vya ushindi katika michezo mbalimbali.

Akizungumza wakati wa mapokezi ya wanamichezo hao Bw. Kidata alisema kuwa, juhudi ambazo wamezifanya watumishi hao ni kielelezo cha kuwa na nidhamu na ushirikiano siyo tu katika majukumu yao ya kikazi bali hata baina yao wenyewe.

“Ushindi huu mliouleta unaonyesha dhahiri kwamba mnazingatia maadili ya msingi yanayotuongoza ambayo ni Weledi, Uwajibikaji na Uadilifu kwa sababu bila mambo haya matatu msingefanikiwa kuja na ushindi huu mkubwa, ninawapongeza sana,

Napenda kuwapa taarifa nzuri wanamichezo wote kwamba, nimetoa maagizo ya kufanya matengenezo ya uwanja wetu wa mazoezi uliopo eneo la Kurasini hapa Dar es Salaam na nimetoa maelekezo kwamba ifikapo Mwezi Juni, 2022 nikabidhiwe uwanja huo ili mpate uwanja mzuri wa kufanyia mazoezi,” alisema Bw. Kidata.

Katika mapokezi hayo Kamishna Mkuu Kidata alikuwa na mgeni wake Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato ya Uganda (URA) Bw. John Musinguzi ambaye aliitembelea TRA kwa ajili ya kufanya mazungumzo na mwenyeji wake Kamishna Mkuu wa TRA kuhusu masuala ya ushirikiano wa kimkakati hususani katika suala zima la ukusanyaji mapato ya Serikali.

Pamoja na kuwapongeza wanamichezo hao, Kamishna Mkuu huyo wa URA amesema kwamba, watafanya mazungumzo ili iandaliwe mechi ya kirafiki kati ya TRA na URA kwa lengo la kuimarisha afya ya mwili na kuongeza mahusiano mema baina ya ofisi zetu mbili.

“Hongereni kwa ushindi ambao mmeupata ila ningependa zaidi watumishi wa TRA wafanye mechi ya kirafiki na watumishi wa URA ili kujenga ushirikiano na kuimarisha afya zetu,” alisema Bw. Musinguzi

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Michezo wa TRA, Bw. Zahor Salum amemshukuru Kamishna Mkuu na menejimenti nzima ya TRA kwa kuwaruhusu, kuwaamini na kuwawezesha kushiriki michuano hiyo ya SHIMMUTA ambapo ameongeza kuwa bila kuwezeshwa na uongozi huo wasingeweza kupata ushindi huo mnono.

Mashindano ya SHIMMUTA ya mwaka huu yalianza tarehe 13 Novemba na kuhitimishwa tarehe 27 Novemba, 2021 yakishirikisha taasisi 44 za Serikali ambapo katika mashindano hayo, TRA imeibuka kidedea katika michezo mitano ambayo ni mpira wa miguu, bao, draft – Wanaume, draft – Wanawake pamoja na mchezo wa karata.


Share:

Zijue Sifa Za Camon 18 Premier Sifa Kuu Za Camon 18 Premier


Camon 18 inakuja na sifa mbalimbali kali, ila izi 5 ndizo zimeikonga nyoyo za watumiaji simu, zaidi wale wapenda simu janja(smartphone). TECNO CAMON 18 inakuja na kamera ya kisasa inakwenda kwa jina la GIMBAL CAMERA ambayo inauweza wa kuchukua video ikiwa clear bila kucheza cheza. Kwa mfano upo kwenye bodaboda au gari unaweza kurekodi video nzuri na kali.
       
Sifa kubwa nyengine kwenye kamera yake inauwezo wa kuzoom mara 60x zaidi. Hata kama kitu kipo mbali unazoom kwa ukaribu na picha ikatoka ikiwa na quality nzuri.
 

Ukiondoa uwezo wa kamera wa TECNO CAMON 18 pia simu hii na uwezo mkubwa wa kuhifadhi dokumenti, video, mziki na picha. Tofauti na matoleo ya zamani ya CAMON, simu hii ina kuja na 256GB ROM na RAM 8GB ya kurahisisha na pia kuongeza ufanisi wa kazi wa simu hii.

Pia simu ya TECNO CAMON 18 inakuja ikiwa na processor kubwa zaidi na pia ni ya kwanza Afrika kwa simu zenye kutumia processor za Media Tek. Ambapo simu hii ina Media Tek Helio G96. Kwa wale wapenda games hii simu inawafaa zaidi.


Unaweza kujiuliza mbona hatujataja uwezo wa betri wa CAMON 18? Simu hii inakuja na betri kubwa ya 4750mAh na uwezo wa kuchaji haraka 33W, ambapo utaweza kuchaji simu yako ndani ya dakika 30 ukajaza zaidi ya 64%. Pia inakuja na kioo cha kisasa AMOLED chenye refresh rate 120Hz ambapo kioo iki kinatunza chaji tofauti na vioo vya simu nyingine.                            


Simu ya TECNO CAMON 18 inapatikana katika maduka yote ya tecno Tanzania nzim. Ukinunua simu ya CAMON 18 unapata zawadi ya ear bud za Bluetooth au TECNO T301 papo hapo. Pia utaingia kwenye droo ya kupata zile zawadi kubwa ya tiketi za ndege mwaka mzima kutoa Air Tanzania na kifurushi cha dakika, SMS na GB kutoka Vodacom mwaka mzima, hii si ya kukosa. Kufahamu ofa na zawadi mbalimbali pindi ukinunua simu za TECNO tembelea kurasa zao za mitandano ya kijamii: https://bit.ly/3d12Xw6




Share:

Serikali Inashugulikia Hali Ya Upatikanaji Wa Mbolea Nchini - Majaliwa


WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema Serikali inaendelea na jitihada za kushughulikia hali ya upatikanaji wa mbolea nchini ili kukabiliana na uhaba uliojitokeza ambao umesababisha kuongezeka kwa bei.

Mheshimiwa Majaliwa amesema wakati Serikali inaendelea na jitihada hizo ni vyema pia wananchi wakatumia mbolea mbadala zinazopatikana nchini kama ya Minjingu ili kukabiliana na uhaba uliopo.

“Serikali inaendelea na jitihada mbalimbali, na hivi karibuni tuliitisha kikao na waagizaji wote wa mbolea nchini na tumewaomba kuingiza mbolea kutoka katika maeneo mbalimbali duniani, ingawa Serikali inaendelea kufanya mawasiliano na nchi rafiki ili zisaidie katika kukabiliana na uhaba uliojitokeza ambao umetokana na kusimama kwa uzalishaji wa mbolea kutokana na janga la Uviko 19 duniani.”

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo kwa nyakati tofauti leo (Jumanne, Novemba 30, 2021) akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Mbeya ambapo alipozungumza na wananchi eneo la la Kiwanja cha ndege cha zamani na alipokagua Ujenzi wa Shule ya Sekondari Mwashiwawala 

Waziri Mkuu ameuagiza uongozi wa mkoa huo kuendelea kuweka mipango ya kuboresha eneo la Uwanja wa ndege wa zamani wa Mbeya ambalo  Mkoa  umelitenga kwa ajili ya wafanyabiashara wadogo wadogo wa jiji hilo  kwa kutengeneza barabara na vizimba ili wafanyabiashara hao wafanye shughuli zao  katika mazingira rafiki.

“Ndugu zangu wafanya biashara, nataka niwaambie nia ya dhati ya Rais wetu Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ya kutaka kuboresha biashara nchini kwa makundi yote ya wafanyabiashara wadogo, wa kati na wawekezaji wakubwa na ametuagiza wasaidizi wake tuendelee kuweka mazingira rafiki kwa wafanyabiashara wote ili wapate tija kutoka katika biashara zao.”

Awali akiwasilisha taarifa ya wafanyabiasha wadogo (Machinga) Makamu Mwenyekiti wa Machinga Taifa Bw. Ernest Massanja ameipongeza Serikali kwa namna ilivyoratibu zoezi la kuwapanga wafanyabiashara wadogo katika maeneo mbalimbali nchini “Tunamshuruku sana Rais Samia kwa namna alivyosimamia zoezi hili, tuna imani naye katika uboreshwaji mazingira rafiki ya biashara kwa wamachinga”

Naye, Mbunge wa Mbeya Mjini Dkt.Tulia Ackson, ameiomba Serikali kuharakisha mchakato wa Ujenzi wa barabara ya njia nne kuanzia  eneo la Mlima Nyoka, Uyole hadi Mwanjelwa, ili kuondoa changamoto ya foleni katika barabara hiyo muhimu katika sekta ya usafirishaji.

Akijibu maombi ya  Mbunge wa Mbeya Mjini, Waziri Mkuu amewahakikishia wakazi wa Mbeya kuwa serikali iko katika hatua za awali za kukamilisha utaratibu wa ujenzi wa barabara hiyo, na pia amewasihi viongozi wa Mkoa wa Mbeya kuweka mikakati mizuri ya kuwawezesha wafanyabiashara wadogo kupata fursa za kifedha kutoka katika asilimia kumi ya fedha za Halmashauri ili kuwawezesha kukuza biashara zao.

Akifanya ukaguzi wa ujenzi wa madarasa manane katika Shule ya Sekondari ya Mwashiwawala, ambayo yanajengwa kwa fedha za Uviko 19, Waziri Mkuu ameupongeza Uongozi wa Mkoa wa Mbeya kwa kusimamia vyema miradi yote ambayo inajengwa  kwa fedha za serikali  hususan miradi ya Uviko 19 ambayo tayari Mkoa huo umeanza ujenzi na uko katika hatua za mwisho za ukamilishaji wake.

Akizngumza baada ya kutembelea kiwanda cha East African Starch Limited, kinachochakata na kuliongezea thamani zao la mahindi kwa kuzalisha bidhaa mbalimbali kama vile wanga, glucose, mafuta ya kupikia ya mahindi (Corn Oil) na Chakula cha Mifugo, Waziri Mkuu amemuhakikishia muwekezaji huyo kuwa Serikali itaendelea kumlinda na kuhakikisha anapata mafanikio katika uwekezaji wake.

“Serikali itaendelea kufuatilia kila hatua ya uwekezaji katika kiwanda hiki na mkandarasi aliyetaka kuhujumu ujenzi huu Serikali itaendelea kumfuatilia na kuhakikisha ujenzi wa kiwanda hiki unakamilia”.

Waziri Mkuu alihitimisha kwa kuushukuru na kuupongeza uongozi wa Mkoa wa Mbeya kwa usimamizu mzuri wa miradi yote ya Serikali, kujenga mahusiano mazuri kati ya viongozi wa serikali wabunge, wawekezaji na wananchi pamoja na utekelezaji wa miradi wenye viwango na ubora. Waziri Mkuu amemaliza ziara yake ya kikazi mkoani Mbeya ambayo ililenga kukagua miradi ya maendeleo na utekelezaji wa miradi ya kijamii.


(Mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,


Share:

Procurement Associate at SokoWatch

Procurement Associate   Dar Es Salaam, TZContractFMCG About Us: Sokowatch is transforming communities across Africa by revolutionizing access to essential goods and services. By connecting small shops to the digital economy, we fix inefficient supply chains and provide services previously unavailable to informal businesses. Sokowatch aims to provide everything a retailer needs, no wholesalers or […]

This post Procurement Associate at SokoWatch has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:

Sales and marketing Cum Assistant Accountant at Fastlink Safaris Limited

Sales and marketing Cum Assistant Accountant    Summary:  Fastlink Safaris Limited is looking for sales and marketing officer. Job Description:  This role includes research and development of various marketing strategies  for our products and services. You will implement marketing plans and work  to meet sales quotas. Tracking marketing and sales data and identifies areas of […]

This post Sales and marketing Cum Assistant Accountant at Fastlink Safaris Limited has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:

Head, Transactional & Liabilities Products at Stanbic Bank Tanzania Limited

Head, Transactional & Liabilities Products Overview Job ID: 57078 Job Sector: Banking Country: Tanzania Region/State/Province/District: Dar es Salaam Region Location: Dar es Salaam Job Details New role from Future Ready Transformation Job Purpose To design, advise and build fit-for-purpose product solutions for Liabilities and Transactional, in alignment with PBB AR Product and country strategies, whilst […]

This post Head, Transactional & Liabilities Products at Stanbic Bank Tanzania Limited has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:

Dereva aliesababisha ajali iliyoua Polisi ahukumiwa miaka minne jela


 Na Amiri Kilagalila,Njombe
ALIYEKUWA dereva wa basi la Sharon  lililosababisha ajali na  kusababisha vifo vya askari wanne wa Jeshi la Polisi mkoani Njombe na majeruhi saba, William Emmanuel (28)ahukukumiwa kifungo cha miaka minne jela na kufungiwa leseni yake kwa muda wa miaka miwili.

Akisoma hukumu hiyo jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Njombe Hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo Liad Shamshama akiwa na Wakili wa Serikali Andrew Mandwa amesema tukio hilo la ajali lilitokea Februari 2020 maeneo ya mlima wa polisi barabara kuu ya Njombe Songea  saa 12 alfajiri.

Amesema siku ya tukio dereva huyo alikuwa akiendesha basi aina ya Youtong hivyo alipofika maeneo ya mlima wa polisi alilipita  gari lingine sehemu ambayo haikutakiwa kufanya hivyo.Akiwa kwenye mwendo mkali dereva huyo aliligonga gari la polisi aina ya Land cruiser na kusababisha vifo vya askari hao.

"Pamoja na kupewa adhabu ya kutumikia kifungo cha miaka minne gerezani mshtakiwa pia amefungiwa leseni yake kwa kipindi cha miaka miwili kuanzia leo,"amesema Shamshama.Askari waliofariki kutokana na ajali hiyo ni Marianus Hamis Saidi,Heri Athumani Soka, Michael Ernest Mwandu na Dickson Kagoda Maijo.


Share:

Deputy Trial Manager at Mwanza Intervention Trials Unit

Deputy Trial Manager    The Mwanza Intervention Trials Unit (MITU) based at the National Institute for Medical Research campus in Mwanza, Tanzania is a collaborative research unit of the London School of Hygiene and Tropical Medicine and the National Institute for Medical Research. The mission of the Mwanza Intervention Trials Unit is to contribute to […]

This post Deputy Trial Manager at Mwanza Intervention Trials Unit has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:

Saccos Manager at Tumaini SACCOS

Saccos Manager   Tumaini SACCOS is a member based financial institution registered under COOPERATIVE SOCIETY ACT, with the Main objective of giving loans to members in accordance to Loan Policy. POSITION: SACCOS MANAGER Tumaini SACCOS is based in Arusha, is seeking to recruit suitably qualified candidate for the vacant positions of SACCOS MANAGER REPORTS TO: SACCOS […]

This post Saccos Manager at Tumaini SACCOS has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:

Drivers III at Ardhi University

Drivers III (2 positions)   Ardhi University has vacant positions in the Administrative cadre of Drivers on temporary basis. The University subscribes to the policy of an equal opportunity employer and therefore invites applications from candidates who are interested to work in a thriving University environment and have the requisite skills, qualifications and experience for the […]

This post Drivers III at Ardhi University has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:

TANZANIA YAFUZU KOMBE LA DUNIA MCHEZO WA SOKA KWA WENYE ULEMAVU



******************** 

Na. John Mapepele 

Waziri mwenye dhamana ya Michezo nchini. Mhe, Innocent Bashungwa leo Disemba 1, 2021 amewaongoza watanzania kuishangilia Timu ya Tanzania (Tembo Warriors) ambayo imefuzu na kuwa timu ya kwanza miongoni mwa timu nne zinazoingia nusu fainali ya Soka ya Bara la Afrika kwa wenye ulemavu (CANAF 2021) na hivyo kupata tiketi ya kushiriki Mashindano ya Dunia ya mchezo huo yatakayofanyika nchini Uturuki 2022 baada ya kuichapa timu ya Cameroon mabao 5-0. 

Timu ya Tanzania ambayo katika kipindi chote cha maandalizi imesimamiwa na Kamati Maalum ya Kitaifa chini ya Katibu Mkuu wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassani Abbasi ilianza vizuri kutokana hamasa iliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe, Samia Suluhu Hasan. 

Katika mechi zote za mashindano haya Tanzania imepoteza mechi moja tu ya Uganda mbayo ilifungwa goli 1-0, ambapo Tembo iliifunga timu ya Morocco 2-1 na Sierra Leone ambapo tembo ilishinda goli 1-0. 

Akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya mechi hii, Mhe. Bashungwa amewahakikishia kwamba Serikali itaendelea kuiisaidia timu hiyo ili iendelee kufanya vizuri maandalizi ya Kombe la Dunia. 

Aidha, Dkt Abbasi amesema kwa kuwa safari ya kuelekea kombe la dunia imekamilika kazi iliyobaki ni kuhakikisha kuwa kombe linabaki Tanzania. 

Magoli mawili ya Tanzania yamefungwa na Alfan Kyanga dakika ya 2 na 15 , Ramadhan Chomole dakika ya 18, na Frank Ngailo dakika ya 36 na 44. 

Mchezo huo pia umeshuhudiwa na Rais wa Mashindano hayo duniani Mateus Wildack.
Share:

Wachimbaji Madini Waaswa Kujikinga Dhidi Ya Maambukizi Ya Ukimwi- Waziri Biteko


 Na MWANDISHI WETU,TABORA
Katika kuelekea Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani, Waziri wa Madini Doto Biteko ameitumia fursa hiyo kuwaasa wachimbaji wote wa Madini Nchini kuhakikisha wanalinda afya zao kwa kujikinga na maambukizi ya virusi vya UKIMWI.
 

Waziri Biteko ameyasema hayo baada ya kutembelea mgodi wa wachimbaji wadogo wa Nsungwa uliopo wilayani Kaliua Mkoa wa Tabora ambako kumeibuka mfumuko wa Madini ya Dhahabu (Rush).
 

Aidha, Waziri Biteko amewataka wachimbaji hao kuhakikisha wanatunza akiba ya kipato wanachokipata na kutunza familia zao ikiwemo kuwekeza katika sekta nyingine hususan katika Sekta ya Biashara na Kilimo.
 

“Hela unayoipata usiidharau hata kama ni kidogo weka akiba ili ije ikusaidie kesho ukiwa huna nguvu, leo unanguvu unaingia duarani lakini baada ya miaka kadhaa hautaweza, utaitaji watu wa kukusaidia, nguvu ya leo uiweke akiba kwa ajili ya kesho ili ikusaidi kuwa na kesho nzuri usije ukawasumbua watu,” amesema Waziri Biteko.
 

Waziri Biteko amesema Wilaya ya Kaliua inafahamika kwa Kilimo cha Tumbaku ambapo kwa sasa umetokea mlipuko wa Madini ya Dhahabu katika eneo hilo na kusababisha Wilaya hiyo kuingia kwenye orodha ya Wilaya zinazochimba Madini ambapo amewataka Wachimbaji hao kuendelea kuwa watulivu na kufuata Sheria katika uchimbaji wao.
 

Pia, Waziri Biteko amesema haki zipo nyingi kuna Haki ya Ardhi, Haki ya Anga, Haki ya Madini na kadhalika, unaweza ukawa na shamba lakini mmiliki mkuu wa shamba hilo ni wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mwenye mamlaka ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kama kwenye shamba hilo kuna Madini hairuhusiwi yachimbwe mpaka kuwe na leseni katika eneo hilo.
 

“Yoyote anayepewa leseni ya Madini kazi yake ya kwanza ni kwenda kwa mwenye shamba sababu huwezi kuyachimba Madini mpaka ukubaliane na mwenye shamba na kuna makubaliano ya aina mbili ya kwanza ni kumlipa fidia mwenye shamba ili akupishe na aina ya pili ni mwenye shamba kuingia shea kwenye leseni husika,” amesema Waziri Biteko.
 

Pia, Waziri Biteko amewasisitiza wachimbaji wadogo kuachana na suala la kutorosha madini ambapo amewataka kuchimba kwa kufuata Sheria na kuhakikisha kodi ya Serikali inalipwa.
 

“Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anataka kuona Uchumi wa Madini unamilikiwa na Watanzania wa kawaida pia wachimbaji wote walioko sehemu mbalimbali ikiwemo Kaliua wanabadilisha maisha yao kwa rasilimali ambazo Mwenyezi Mungu amewabariki,” amesema Waziri Biteko.



Share:

Vijana Watakiwa Kujitokeza Kupima UKIMWI


NA.MWANDISHI WETU
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama amewaasa vijana kujitokeza kupima Virusi vya UKIMWI ili kujua hali zao na kuishi kwa malengo.

Ametoa kauli hiyo  Novemba 30, 2021 wakati akihutubia vijana katika kuadhimisha siku ya vijana katika kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani tarehe 01 Disemba, 2021 yatakayofanyika katika Uwanja ya Ruanda Nzovwe Jijini Mbeya. Kaulimbiu ya Maadhimisho kwa mwaka huu inasema “Zingatia Usawa. Tokemeza UKIMWI, Tokomeza Magonjwa ya Mlipuko”.

Alieleza kuwa, Kauli mbiu ya mwaka huu inalenga kutoa msukumo kwa Watanzania wote kujitokeza kwa ajili ya upimaji wa hiari wa VVU baada ya ushauri nasaha, ikiwa ni pamoja na kuanza kutumia dawa za kufubaza VVU (ARV) mapema kwa watakaogundulika kuwa na mambukizo ya VVU. Kauli mbiu hii inakwenda sambamba na jitihada za nchi katika kufikia malengo ya Kidunia ya Sifuri TATU ambayo tumeyaridhia.

Akieleza umuhimu wa kundi la vijana nchini, alisema ni kundi linalotegemewa kwa asilimi kubwa hivyo ni vyema wakawa na desturi za kupima hali zao ili kuishi kwa malengo na kutimiza ndoto zao.

“Vijana ndio nguzo katika ujenzi wa Taifa imara. Katika Taifa letu vijana ni zaidi ya asilimia 68 ya nguvu kazi ya Taifa letu, hii ni kwa mujibu wa takwimu za makadirio ya ongezeko la idadi ya watu nchini ambayo imeonesha kuwepo na ongezeko kubwa la vijana na watoto, hivyo hakuna namna tunayoweza kufanya shughuli za maendeleo pasipo kutambua nafasi ya vijana ndani ya jamii yetu na kufahamu vipaumbele vyao ikiwa ni pamoja na afya bora,”alisema waziri Mhagama.

Waziri Mhagama alisema utafiti wa Viashiria vya UKIMWI wa mwaka 2016/17 hapa nchini, ulibaini kuwa moja ya makundi yaliyo nyuma katika kufikia malengo yaliyowekwa ni kundi la VIJANA ambapo inaonesha vijana wengi wenye umri wa miaka 15 hadi 24 hawajui hali zao za maambukizo ukilinganisha na watu wenye umri mkubwa. Hali hii inapelekea vijana hawa kutoanza dawa za ARV mapema kwani hawajui hali zao na hivyo kutoweza kufubaza VVU.

“Nitoe rai kwa vijana wote nchini, tujitokeze kwa wingi katika huduma za upimaji wa VVU kwa hiari zitolewazo sehemu mbalimbali nchini, ili wale wote watakaogundulika kuwa wana maambukizo ya VVU waweze kuanza dawa za ARV mapema na hivyo kutimiza kwa vitendo kauli mbiu ya mwaka huu,”alisisitiza

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jukwaa la Vijana wanaoishi na VVU Nchini Bi. Pudenciana Mbwiliza akitoa salamu wakati wa maadhimisho hayo alieleza ni vyema vijana wakajitokeza kupima na kujua hali zao ili kuendelea kuunga mkono jitihada za mapambano haya.

Aidha akibainisha changamoto zao alisema ni wakati sahihi kuwa na mikakati ya kuendelea kutokomea vitendo vya kikatili na kuendelea kuwafikiwa vijana kupitia miradi mbalimbli inayotekelea afua za masuala ya UKIMWI nchini.

Pia alizitaja changamoto wanazokabiliana nazi ikiwemo ya kasi ya maambukizi mapya hasa kwa wasichana walio katika umri balee, unyanyapaa katika jamii hususan ule wa mtu binafsi, ukatili wa kijinsia, ufuasi hafifu wa utumiaji wa dawa za ARV, elimu duni kwa vijana walio mashuleni hasa katika shule za bweni, matumizi yasiyosahihi ya kondom na mwamko mdogo wa watu kujitokeza kupima na kujua hali zao.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge inayoshughulikia masuala ya UKIMWI Mhe. Fatma Taufiq alipongeza jitihada zinazofanywa na Serikali katika mapambano dhiti ya UKIMWI na kuahidi kuendeleza ushirikiano kadiri inavyotakiwa.

“Kweli bajeti tunayoipitisha bungeni inafanya kazi kwa haya tuliyoona na mwitikio huu wa vijana na kuona kundi hili linashirikishwa kwa namna kubwa na hii ni ya kupongeza sana. Naamini Taanziania bila UKIMWI inawezekana na Tanzania bila unyanyapaa inawezekana,”alieleza Mhe. Fatma

Aliongezea kwamba, Kamati itaendela kuishauri Serikali kuwa na sera na sheria imara kuhakikisha kundi ka vijana linapata fursa nzuri na kuone namna bora ya kuweka mipango thabiti ili kuendela kulivusha kundi hili.


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger