Monday, 7 June 2021

TAWA Kanda Ya Magharibi Yakamata Bunduki 24 Na Meno Manne Ya Tembo Katika Doria Ya Kusaka Majangili


NA TIGANYA VINCENT

MAMLAKA ya ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania(TAWA) Kanda ya Magharibi imefanikiwa kukamata bunduki za aina mbalimbali 24 na meno ya tembo manne yenye uzito kilo 21.2 katika kipindi cha kuanzia mwezi Aprili hadi Juni mwaka huu.

Taarifa hizo zilitolewa jana mjini Tabora na Kamnda wa Uhifadhi wa Kanda ya Magharibi Bigilamungu Kagoma wakati wa mkutano na waandishi wa habari.

Alitaja aina za bunduki wanalizokamata kuwa ni SMG 1, Riffle 3, Shotgun 1 na gobore 19 ambazo zote hizo zilikuwa zikendesha vitendo vya ujangili katika Mapori mbalimbali ya Kanda ya Magharibi.

Kagoma alisema sanjari na hilo wamefanikiwa kuwakamata watuhumiwa 91 wa makosa mbalimbali yakiwemo ya kuingia hifadhini bila kibali , uwandaji wa wanyamapori, uvuvi haramu na uharibifu wa mazingira.

Kamanda huyo aliongeza kuwa baadhi ya Watuhumiwa wameshafikiwa Mahakamani na wengine wawili walikiri kosa na kulipa faini kwa mujibu wa Sheria ya Uhifadhi.

Aliongeza katika doria hizo pia wamefanikiwa kukamata risasi 38 za bunduki za aina mbalimbali na gololi 76 za gobole ambazo zilikuwa zipangwa kutumiaka katika ujangili katika mapori mbalimbai ya Kanda hiyo.

Kagoma alisema kuwa watumuhimwa wawili kati ya hao walikutwa katika pori la Akiba la Ugalla wakiwa wametoka kuwinda Boko wakiwa na Gobole.

Alitoa kwa wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa TAWA ili kuwabaini watu wanaoendesha ujangilili na hataimaye waweze kukamatwa na kufikishwa katika vyombo vya Sheria ikiwa ni hatua ya kukomesha vitendo hivyo.

Kagoma alitoa rai kwa Majangiri kuachana na vitendo vya kuwinda wanyama na kutafuta shughuli nyingine ya kuwaingizia kipato halali.

Alisema mwananachi ambaye andependa kushirikiana na TAWA katika kuwafichua Majangili kwa Kanda ya Magharibi anaweza kupiga simu namba 0800110048.

Katika hatua nyingine Kagoma alisema wanaendelea na jitihada za kufufua bustani ya wanayama ya Tabora iliyopo jirani na Hospitali ya Kitete kwa ajili kuvutia utalii wa ndani.

Aliwataka wakazi wa Kanda ya Magharibi kujenga utamaduni wa kutemelea vivutio vilivyopo vyawanayapori kwa kuwa gharama kwa Mtanzania ni shilingi 4,000/= kwa siku.

Aidha Kagoma alisema kuwa utaratibu wa kuanza maduka ya nyamapori kwa kanda ya Magharibi bado uko chini na kusema kuwa ni duka mmoja ambalo limeshaanzishwa na liko Katavi.




Share:

Waziri Mkenda Aitaka Tfra Kuandaa Mkakati Wa Upatikanaji Wa Mbolea Kwa Bei Nafuu


Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dar es salaam
Bodi na Menejimenti ya Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) imetakiwa kuanisha mkakati wa upatikanaji wa mbolea nchini kwa bei nafuu.

Waziri wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda ametoa rai hiyo wakati akizungumza kwenye kikao kazi alipotembelea taasisi hiyo kujionea hali ya utendaji na upatikanaji wa mbolea wakati akiwa katika ziara ya kikazi ya siku moja Jijini Dar es salaam.


Pamoja na kuandaa mkakati wa urahisishaji wa upatikanaji wa mbolea, Pia Waziri Mkenda ameitaka taasisi hiyo kuandaa mkakati wa uanzishwaji wa viwanda vipya vya mbolea ili kuongeza uzalishaji wa pembejeo hiyo hapa hapa nchini.

Waziri Mkenda, amesema Bodi na Menejimenti ya Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea, ina jukumu kubwa la kuhakikisha kuwa uzalishaji wa ndani wa mbolea, unapewa kipaumbele na kwa kuongeza uanzishwaji wa viwanda vipya; mbolea itakuwa ikipatikana kwa urahisi, nafuu na kila Mkulima atamudu kuinunua na kuitumia.

Prof Mkenda ameongeza kuwa Bodi na Menejimenti ya TFRA ibuni mkakati wa namna bora ya kuongeza uwekezaji hapa hapa nchini, kwa kuwa hilo ndiyo suluhisho la kweli katika kuwahakikishia Wakulima wengi wadogo unafuu bei.


Kadhalika, amewataka Watumishi wa TFRA kuongeza udhibiti kwenye usimamizi wa ubora wa mbolea hususan kwenye mikoa yenye matumizi makubwa ya mbolea.
MWISHO





Share:

Dkt.ndugulile Ahimiza Uboreshaji Wa Mifumo Mbalimbali Ya Usimamizi Wa Huduma Za Mawasiliano


Na Mwandishi Wetu
SERIKALI imehimiza uboreshaji wa Mifumo mbalimbali ya usimamizi wa huduma za Mawasiliano ili kuhakikisha kunakuwa na Usalama na Ubora wa Huduma Nchini.

Akizungumza katika ziara ya kutembelea mifumo hiyo kwenye Taasisi ya Udhibiti, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), jijini Dar Es salaam, , Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Dkt. Faustine E. Ndugulile (Mb) amesema Wananchi wanatarajia kupata huduma bora zenye usalama.

“Upatikanaji wa huduma Bora, za Uhakika na Salama nijambo la msingi sana kwa ajili ya maendeleo ya Wananchi na Taifa” amesema Mhe. Ndugulile.

Katika ziara hiyo Mhe. Ndugulile alipokelewa na Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Dkt. Jabiri K. Bakari na Menejimenti alipotembelea mifumo ya udhibiti wa Mawasiliano.

Dkt. Ndugulile aliipongeza TCRA kwa ubunifu wa kujenga Mifumo Wezeshi kwa huduma mbali-mbali za Mawasiliano Nchini, ambapo alisema uboreshaji wake nimuhimu sana.

Baadhi ya mifumo aliyotembelea Mhe. Waziri ni Mfumo wa Usimalizi na Udhibiti wa Masafa ya Redio na Televisheni na Kituo cha Kuratibu Majanga ya Kimtandao (TZ-CERT). TZ-CERT pia itatoa ushuri wa kitaalam-namna bora wa kudhibiti na kupambana ya majanga mbali-mbali ya Kimtandao kwa Taasisi na makampuni mbali-mbali hapa Nchini.

Mhe. Waziri pia alitembelea Kituo cha Huduma kwa Wateja ambapo alihimiza TCRA kuendeza kushirikiana na Taasisi zingine zikiwemo za Kiudhibiti kama Bank Kuu ya Tanzania (BOT).


Share:

Baraza La Madiwani Busega Lataka Uwepo wa Mahakama ya Wilaya; Lashauri Marekebisho Stendi ya Wilaya


Baraza la madiwani halmashauri ya Wilaya ya Busega limetaka uwepo wa Mahakama ya Wilaya Busega. Hayo yamesemwa na wajumbe wa baraza hilo wakati wa kikao cha baraza la madiwani robo ya tatu lililofanyika tarehe 04 Juni 2021 ukumbi wa Silisos.

Diwani kata ya Nyasimo Mhe. Mickness Mahela amehoji kuhusu suala la uwepo wa Mahakama wilayani Busega, akisema kwamba imekuwa kero kubwa kwa wakazi wa Busega wanapotaka kupata huduma ya mahakama, kwani inawalazimu kwenda Wilaya jirani ya Bariadi kupata huduma hiyo.

“Wilaya ya Busega ina takribani miaka tisa kwasasa, hivyo uwepo wa mahakama ni muhimu kwa wananchi wetu” aliongeza Mhe. Bi. Mickness Mahela. Wajumbe wa baraza hilo wamekiri kwamba uwepo wa mahakama ni suala lisilopingika, huku wakidai kwamba wilaya inahitaji mahakama ili kuondoa kero ya wakazi na wananchi wa Busega.

Akitoa ufafanuzi wa suala la uwepo wa mahakama wilayani Busega, mwakilishi kutoka Ofisi ya Mkuu wa wilaya Busega Bw. David Pallangyo anasema kwamba ni suala ambalo Ofisi ya Mkuu wa Wilaya imekua ikifuatilia kwa ukaribu na inaendelea na ufutiliaji. Kwa upande mwingine ameeleza kwamba licha ya watumishi wa mahakama kupangiwa kufanyia kazi zao wakiwa Busega lakini bado wanafanyia kazi zao wilayani Bariadi.

Aidha, hoja ya matengenezo ya magari iliibuliwa na wajumbe huku wakitaka uwepo wa gereji ya halmasuri ili kuwa na ufanisi wa matengenezo ya magari hayo kuliko kupeleka magari hayo kwa Wakala wa Ufundi wa Umeme na utengenezaji wa Magari ya Serikali (TEMESA). Akitoa ufafanuzi wa suala hilo Mkurugenzi Mtendaji Bw. Anderson Kabuko licha ya changamoto ya TEMESA, lakini tayari marekebisho na matengenezo madogo yanafanyika kwa baadhi ya magari na kazi hiyo inafanywa na fundi wa halmashauri.

Suala la stendi ya Wilaya ambayo imeanza kufanya kazi mwanzoni mwa mwezi wa tano mwaka huu, pia limepata wasaa wa kujadiliwa na baraza hilo. Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Busega Bw. Anderson Kabuko amesema tayari halmashauri imevunja mkataba na mkandarasi wa awali ambae alikuwa akijenga stendi hiyo kutokana na kutofikia ubora wa ujenzi, na tayari utaratibu unafanyika ili kumpata mkandarasi mwingine. Baraza hilo limetaka ujenzi wa wa stendi hiyo uboreshwe hasa njia za kupita magari ili kuondoa usumbufu na kero.

Akiahirisha kikao cha baraza hilo, Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Busega Mhe. Sundi Muniwe, ametaka kuendelea kwa juhudi ujenzi wa stendi ya Wilaya, na kuagiza kwamba kwasasa hatuhitaji mkandarasi, mhandisi wa ujenzi kwa kushirikiana na Meneja wa TARURA kufanya kazi ya ujenzi kuendelea na ujenzi wa stendi ya Wilaya, Nyashimo. Kwa upande mwingine ameomba viongozi wa mkoa kufuatilia suala la mahakama ili wilaya ya Busega iweze kupata mahakama.   




Share:

Gardener at AUMS

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

African Underground Mining Services (AUMS) is an international leader in mechanised hard rock underground mining. AUMS is part of Perenti (Formerly the Ausdrill Group), an ASX 200 company and Australia’s second largest integrated mining services provider. We are a global leader in hard rock underground mining; together with Barminco we operate across Africa in Tanzania, […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

Service Crew at AUMS

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

African Underground Mining Services (AUMS) is an international leader in mechanised hard rock underground mining. AUMS is part of Perenti (Formerly the Ausdrill Group), an ASX 200 company and Australia’s second largest integrated mining services provider. We are a global leader in hard rock underground mining; together with Barminco we operate across Africa in Tanzania, […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

Underground Charge Up Operator at AUMS

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

African Underground Mining Services (AUMS) is an international leader in mechanised hard rock underground mining. AUMS is part of Perenti (Formerly the Ausdrill Group), an ASX 200 company and Australia’s second largest integrated mining services provider. We are a global leader in hard rock underground mining; together with Barminco we operate across Africa in Tanzania, […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

Nipper at AUMS

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

African Underground Mining Services (AUMS) is an international leader in mechanised hard rock underground mining. AUMS is part of Perenti (Formerly the Ausdrill Group), an ASX 200 company and Australia’s second largest integrated mining services provider. We are a global leader in hard rock underground mining; together with Barminco we operate across Africa in Tanzania, […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

UG First Line Leader at North Mara Gold Mine Limited

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

POSITION DESCRIPTION: North Mara Gold Mine Limited is seeking to recruit One (1) UG First Line Leader to join Underground Mining Production team. The successful candidate will be responsible for supervision of the mine crews, to ensure safety is managed, and overall performance is monitored and efficient. Ensure that any non-conforming items (Quality and quantity) are immediately isolated and reported for […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

Agronomist Operation at Kilombero Sugar Company Ltd

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

Kilombero Sugar Company Limited (KSCL), the largest producer of sugar in the country operating cohesively with Extra Neutral Alcohol Distillery is seeking to recruit a dynamic, visionary and result oriented person to fill the position of Agronomist Operation at Estate Agriculture Department reporting to Agriculture Optimisation Manager. Role Intent Provide direction and technical guidance on crop varieties, […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

Board Members Vacancies at CRDB

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

BOARD MEMBERS VACANCIES CRDB Bank Burundi S.A. is 100% owned by CRDB BANK PLC and operates in Burundi and is inviting applications from qualified candidates to fill the existing vacant positions for the Board of Directors. CRDB BANK PLC is the leading bank, wholly owned private commercial Bank operating in Tanzania and Burundi. The Bank […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

Client Service Officer at Citi Bank

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

Our employees are energetic and dedicated individuals who work in a fast-paced and challenging position that relies on the ability to think and react quickly, formulate creative solutions to pressing problems, and serve clients with dedication. Our employees serve as the human voice and personality behind the Citi brand as they provide quality customer service […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATATU MEI 7,2021















































Share:

DC AWATAKA WAMILIKI WA VIWANDA KUZINGATIA MIONGOZO YA OSHA


Kaimu Mtendaji Mkuu wa OSHA, Khadija Mwenda, akizungumza na viongozi wa kiwanda cha Nondo cha Fujian Hexingwang, alipotembelea kiwanda hicho kilichopo Mkuranga Mkoani Pwani. Lengo la ziara hiyo ilikuwa ni kufuatilia utekelezaji wa maagizo ya kuboresha mazingira ya kazi ambayo yalitolewa na Taasisi yake baada ya kufanya ukaguzi na kubaini mapungufu katika mifumo ya kuwalinda wafanyakazi ambapo walikifunga kiwanda hicho na kuwataka wamiliki kufanya maboresho ya mifumo ya kuwalinda wafanyakazi dhidi ya ajali na magonjwa yatokanayo na kazi.
Mfanyakazi wa kiwanda cha Nondo cha Fujian Hexingwang, akionyesha jinsi ya kuendesha mtambo wa kisasa kwa ajili ya kupakia malighafi kwenye majiko ya kuyeyushia chuma kinachotumika kutengeneza nondo. Mtambo huo ambao unaendeshwa kwa kutumia rimoti (remote control) ni sehemu ya maboresho katika mifumo wa usalama na afya kutokana na maelekezo yaliyotolewa na wakaguzi wa OSHA katika kiwanda hicho hivi karibuni.
Kaimu Mtendaji Mkuu wa OSHA, Khadija Mwenda (mwenye kofia nyeupe), akisikiliza maelezo kutoka kwa mkalimani wa viongozi wa kiwanda cha Nondo cha Fujian Hexingwang (ambao ni Raia wa China), alipotembelea kiwanda hicho kilichopo Mkuranga Mkoani Pwani. Lengo la ziara hiyo ilikuwa ni kufuatilia utekelezaji wa maagizo ya kuboresha mazingira ya kazi ambayo yalitolewa na Taasisi yake baada ya kufanya ukaguzi na kubaini mapungufu katika mifumo ya kuwalinda wafanyakazi.
Kaimu Mtendaji Mkuu wa OSHA, Khadija Mwenda (mwenye kofia nyeupe),, akizungumza na wafanyakazi wa kiwanda cha Nondo cha Fujian Hexingwang, alipotembelea kiwanda hicho kilichopo Mkuranga Mkoani Pwani. Lengo la ziara hiyo ilikuwa ni kufuatilia utekelezaji wa maagizo ya kuboresha mazingira ya kazi ambayo yalitolewa na Taasisi yake baada ya kufanya ukaguzi na kubaini mapungufu katika mifumo ya kuwalinda wafanyakazi.

Mkuu wa Wilaya Mkuranga, Filbert Sanga (mwenye fulana ya kijivu), akizungumza na Kaimu Mtendaji Mkuu wa OSHA, Khadija Mwenda, ambaye alimtembelea ofisini kwake akiwa ameambatana na Kaimu Meneja wa OSHA-Kanda ya Pwani, George Chali. Mazungumzo hayo yalifanyika muda mfupi kabla ya viongozi hao kutembelea kiwanda cha Nondo cha Fujian Hexingwang kilichopo Mkuranga Mkoani Pwani kwa lengo la kufuatilia utekelezaji wa maagizo ya kuboresha mazingira ya kazi ambayo yalitolewa na OSHA ili kufungua kiwanda hicho ambacho kilifungwa kuruhusu maboresho tajwa kufanyika.

**


Na Mwandishi Wetu     

Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Filbert Sanga, ametoa wito kwa wamiliki wa maeneo ya kazi hususan viwanda katika Wilayani ya Mkuranga Mkoani Pwani kuhakikisha wanatoa ushirikiano kwa Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) ili Mamlaka hiyo iweze kuwaongoza katika kuboresha mazingira yao ya kazi. 

Sanga ameyasema hayo  ofisini kwake alipotembelewa na Kaimu Mtendaji Mkuu wa OSHA, Khadija Mwenda, ambaye alifanya ziara katika Kiwanda cha Fujian Hexingwang kwa lengo la kufuatilia utekelezaji wa maelekezo ya kuboresha mifumo ya usalama na afya katika kiwanda hicho yaliyotolewa awali na wataalam kutoka OSHA.

“Nawashukuru OSHA kutembelea kiwanda chetu cha Fujian Hexingwang kinachozalisha nondo na kuchukua hatua kufuatia ajali iliyotokea mwezi uliopita. Naomba ziara hizi ziendelee pia kwenye viwanda vyote vilivyopo wilayani kwetu ili kuhakikisha kwamba wamiliki wa viwanda wanafuata na kutekeleza maelekezo yote yanayohusu uboreshaji wa usalama na afya kwa wafanyakazi,” aliosema Sanga.

Naye Kaimu Mtendaji Mkuu wa OSHA, Khadija Mwenda, akiongea baada ya kukagua maboresho yaliyofanyika katika kiwanda hicho, amesema Taasisi yake imeridhishwa na maboresho ya awali yaliyofanyika  na hivyo kuondoa hati ya zuio la kufanya uzalishaji iliyotolewa hapo awali ambapo wametoa hati ya maboresho (improvement notice). 

 “Tumejionea maboresho mengi ambayo kiwanda hiki kimejitahidi kuyafanya ikiwemo kufunga mashine (Feeder scooper trolley) ambazo zitasaidia kazi zilizokuwa zinafanywa na wafanyakazi, sasa kazi hizo zitafanywa na mashine na hivyo kupunguza hatari ya ajali kwenye eneo hilo, alifafanua Mwenda na kuongeza:

“Agizo lingine ambalo tunaona utekelezaji wake umefanyika ni pamoja na kuweka mtaalamu wa utambuzi wa vyuma ambavyo vinaweza kusababisha milipuko. Hii itasaidia sana kuhakikisha vyuma vinavyoenda kwenye moto ili kuzalisha uji ambao unatengeneza nondo ni vile tu ambavyo vinastahili kuchomwa. Aidha, wamefanya maboresho katika utoaji wa vifaa kinga stahiki kwa wafanyakazi.” 

Kufuatia maboresho hayo, Kiongozi huyo Mkuu wa OSHA, amesema wameoandoa hati ya zuio walilolitoa katika kiwanda hicho baada ya kusababisha ajali na kuwapatia hati ya maboresho (improvement notice).

Aidha,  ameutaka uongozi wa kiwanda hicho kuendelea kuboresha zaidi eneo lao la kazi na kuhakisha wanawasiliana na mamlaka  nyingine za serikali ambazo zilipita kwenye kiwanda hicho, kuangalia utekelezaji wa maboresho yaliyofanyika ili kiwanda hicho kiendelee na uzalishaji.

Meneja wa Kiwanda cha Fujian Hexingwang, XU XINGDA, ameishukuru OSHA kwa ushirikiano na maelekezo ambayo wamekuwa wakiyatoa katika kuhakikisha kwamba wafanyakazi wa kiwanda hicho wanafanya kazi katika mazingira salama. 

Kwa upande wao wafanyakazi wa kiwanda hicho, wameishukuru OSHA na uongozi wa kiwanda chao kwa jitihada ambazo wamezifanya katika kuhakikisha kiwanda hicho kinaboresha mazingira ya kufanyia kazi. 

Mwezi uliopita, ajali ilitokea katika kiwanda cha Fujian Hexing wang kutokana na mlipuko katika majiko ya kuyeyushia vyuma chakavu na kupelekea vifo vya wafanyakazi wawili. Kufuatia ajali hiyo, OSHA ilifanya uchunguzi wa ajali na kubaini chanzo chake na hivyo kuelekeza kiwanda hicho kufanya maboresho katika mifumo yake ya usalama na afya mahali pa kazi. 

Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani ni miongoni mwa Wilaya zenye viwanda vingi katika mkoa wa Pwani ambapo inakadiriwa kuwa na viwanda vipatavyo 130. 


Share:

JINSI NILIVYOLINDA BIASHARA YANGU KUTOKANA NA KUATHIRIKA WAKATI WA CORONA WAFANYABIASHARA WENGINE WAKIZAMA

Share:

Sunday, 6 June 2021

MBUNGE MPINA ATAKA BUNGE KUWAWAJIBISHA MAWAZIRI WALIOVUNJA KATIBA

 

Mbunge wa Jimbo la Kisesa, Luhaga Mpina akichangia bajeti ya Wizara ya Maliasili na Utalii Bungeni Dodoma na kuitaka Serikali kuwawajibisha viongozi waliokaidi amri ya Mahakama kuhusu mifugo 6,000 iliyokamatwa na Mahakama kuamuru kurejeshewa wamiliki wake ambapo Serikali imekubali kusimamia haki hiyo.

MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina ameliomba Bunge kuwawajibisha Waziri wa Maliasili na Utalii, Waziri wa Katiba na Sheria, Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali (DPP) kwa kitendo cha kudharau Mahakama iliyoamuru wafugaji wa maeneo mbalimbali nchini walioshinda kesi mahakamani warudishiwe mifugo yao 6,000 iliyokamatwa na na Serikali.

Akichangia hotuba ya Makadirio ya mapato na Matumizi ya Wizara ya Malisiali na Utalii kwa mwaka wa fedha 2021/2022 bungeni Dodoma, Mpina amesema hadi leo viongozi hao wamekataa kutii amri hiyo ya Mahakama na kuwadhulumu haki wananchi hao na kwa makusudi wamevunja Katiba ibara ya 107A (i) inayoitaja Mahakama kuwa ndio yenye kauli ya mwisho ya utoaji haki.

“Suala la wafugaji walioshinda kesi mahakamani lakini Serikali imekaidi kurudisha mifugo yao, katika Pori la Akiba la  Maswa na WMA ya Makao ng’ombe walikamatwa 1,739 walipoenda kwenye Mahakama Kuu Shinyanga wafugaji hao walishinda, wakaenda kwenye Mahakama ya Rufaa Tabora wakashinda ngombe jumla ya 1,739 mpaka leo hii hawajarejeshwa na Serikali” alisema Mpina.

Mpina alisema kuwa Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma kwa kesi ya Jinai 136 ya mwaka 2017 ng’ombe 466 walikamatwa katika Pori la akiba la Swagaswaga ambapo ni ng’ombe 113 tu walirudishwa lakini wengine wote katika 466 hawajarudishwa mpaka sasa.

“Pori la Akiba la Muyowosi ambako ng’ombe 216 walikamatwa mpaka leo hawajarudishwa na Serikali katika ile hesabu ya ng’ombe 6,000 hii ni mifano tu Mh. Mwenyekiti ya wafugaji wetu ambao wameshashinda kesi mahakamani lakini Serikali haijarudisha mifugo yao”alihoji Mpina

Pia Mpina alisisitiza kuwa sio mara ya kwanza kulizungumza suala hilo bungeni kwani hata wakati wa hotuba ya Waziri Mkuu alilizungumza suala hilo kwa uchungu mkubwa akiamini Serikali italizingatia.

“Nilizungumza wakati nachangia hotuba ya Mh. Waziri Mkuu hapa kwa uchungu mkubwa nikijua kwamba Serikali italichukulia hili maanani lakini nimesoma hotuba ya Waziri hakuna hata mstari mmoja alipozungumzia juu ya mifugo hawa, Mh. Mwenyekiti wewe unajua kwamba haki inatolewa na chombo gani nanukuu kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ibara ya 107A(i) Mamlaka yenye kauli ya mwisho ya utoaji wa haki katika Jamhuri ya Muungano  itakuwa ni Mahakama” alisema Mpina

Mpina alihoji iweje Mahakama imeshaamua ng’ombe warudishwe kwa wahusika lakini Serikali hawajarudisha mpaka leo ng’ombe hao wa wafugaji jambo lilioacha huzuni na umasikini mkubwa kwa wananchi hao.

“Waziri wa Malisiali na Utalii hajarudisha mifugo ya wananchi, Waziri wa Katiba na Sheria amekataa kurudisha mifugo ya wananchi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali amekataa kurudisha mifugo ya wananchi, Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali (DPP) amekataa kurudisha mifugo ya wananchi hawa wote Mh. Mwenyekiti wamevunja Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambao wao wameapa kuitetea na kuilinda” alisema Mpina.

Mpina alihoji tayari wananchi hawa wameshinda kesi Mahakamani, Mahakama za Kuu zimeamua mifugo warudishwe, Mahakama ya rufaa imeamua mifugo warudishwe nani tena mtoa haki mwingine ambaye anasubiriwa.

“Mh. Mwenyekiti naomba Bunge lako liamua leo hatma ya mifugo ya wananchi hawa irudishwe kwa wananchi ambao wamepata mateso makubwa sana kwa muda mrefu na Serikali imeshindwa kurudisha mifugo yao hawa Mawaziri wamevunja Katiba ya Jamhuri ya Muungano Ibara ya 107A(i) na Kama Katiba ya Jamhuri ya Muungano imevunjwa na mawaziri hawa Mh. Mwenyekiti Bunge lako lichukue nafasi”alisema Mpina.

Akihitimisha bajeti ya Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kujibu hoja za wabunge kuhusu bajeti hiyo, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Damas Ndumbaro ameliambia Bunge kuwa wafugaji wote walioshinda kesi Mahakamani watarudishiwa mifugo yao kama hukumu zilivyoelekeza.

“Mh. Naibu Spika imeongelewa hapa watu wameshinda kesi lakini mifugo yao haijulikani ilipo hawajakabidhiwa Mh Naibu Spika nchi hii inaongozwa na utawala wa sheria na sheria inatafsiriwa Mahakamani mtu akienda mahakamani ameshinda kesi lazima apate kile alichokishinda mahakamani” alisema Waziri Ndumbaro.

Hivyo Waziri Ndumbaro akaahidi kupitia Bunge kuwa Serikali itafuatilia kwa karibu kesi zote ili kila mmoja aweze kupata haki inayostahili.

“Mimi niwaahidi waheshimiwa wabunge na niliahidi bunge lako tukufu tutafuatilia kesi zote hizi ili haki za wale walioshinda kesi mahakamani zisipotee, nimelichukua jambo hilo kwa umakini wa hali ya juu na niwaahidi tutakwenda kutekeleza”alisema Waziri Ndumbaro.

Bunge limepitisha Bajeti ya Wizara ya Maliasili na Utalii kwa mwaka wa fedha wa 2021/2022 ya jumla ya sh 571,623,424,000.

Share:

MATUKIO KATIKA PICHA WAKATI WA BUNGE LA KUPITISHA BAJETI YA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII KWA MWAKA 2021/2022

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja akiwa katika picha mbalimbali za pamoja na Wabunge, Mwenyekiti wa UWT, Bi. Helen Bogohe ambaye aliwaongoza Wenyeviti na Makatibu wa Wilaya wa umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) wanaotokea mkoani Mwanza mara baada ya uwasilishwaji wa Bajeti ya Wizara ya Maliasili na Utalii kwa mwaka 2021/2022 katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jijini Dodoma.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger