Monday, 7 June 2021

TAWA Kanda Ya Magharibi Yakamata Bunduki 24 Na Meno Manne Ya Tembo Katika Doria Ya Kusaka Majangili

...


NA TIGANYA VINCENT

MAMLAKA ya ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania(TAWA) Kanda ya Magharibi imefanikiwa kukamata bunduki za aina mbalimbali 24 na meno ya tembo manne yenye uzito kilo 21.2 katika kipindi cha kuanzia mwezi Aprili hadi Juni mwaka huu.

Taarifa hizo zilitolewa jana mjini Tabora na Kamnda wa Uhifadhi wa Kanda ya Magharibi Bigilamungu Kagoma wakati wa mkutano na waandishi wa habari.

Alitaja aina za bunduki wanalizokamata kuwa ni SMG 1, Riffle 3, Shotgun 1 na gobore 19 ambazo zote hizo zilikuwa zikendesha vitendo vya ujangili katika Mapori mbalimbali ya Kanda ya Magharibi.

Kagoma alisema sanjari na hilo wamefanikiwa kuwakamata watuhumiwa 91 wa makosa mbalimbali yakiwemo ya kuingia hifadhini bila kibali , uwandaji wa wanyamapori, uvuvi haramu na uharibifu wa mazingira.

Kamanda huyo aliongeza kuwa baadhi ya Watuhumiwa wameshafikiwa Mahakamani na wengine wawili walikiri kosa na kulipa faini kwa mujibu wa Sheria ya Uhifadhi.

Aliongeza katika doria hizo pia wamefanikiwa kukamata risasi 38 za bunduki za aina mbalimbali na gololi 76 za gobole ambazo zilikuwa zipangwa kutumiaka katika ujangili katika mapori mbalimbai ya Kanda hiyo.

Kagoma alisema kuwa watumuhimwa wawili kati ya hao walikutwa katika pori la Akiba la Ugalla wakiwa wametoka kuwinda Boko wakiwa na Gobole.

Alitoa kwa wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa TAWA ili kuwabaini watu wanaoendesha ujangilili na hataimaye waweze kukamatwa na kufikishwa katika vyombo vya Sheria ikiwa ni hatua ya kukomesha vitendo hivyo.

Kagoma alitoa rai kwa Majangiri kuachana na vitendo vya kuwinda wanyama na kutafuta shughuli nyingine ya kuwaingizia kipato halali.

Alisema mwananachi ambaye andependa kushirikiana na TAWA katika kuwafichua Majangili kwa Kanda ya Magharibi anaweza kupiga simu namba 0800110048.

Katika hatua nyingine Kagoma alisema wanaendelea na jitihada za kufufua bustani ya wanayama ya Tabora iliyopo jirani na Hospitali ya Kitete kwa ajili kuvutia utalii wa ndani.

Aliwataka wakazi wa Kanda ya Magharibi kujenga utamaduni wa kutemelea vivutio vilivyopo vyawanayapori kwa kuwa gharama kwa Mtanzania ni shilingi 4,000/= kwa siku.

Aidha Kagoma alisema kuwa utaratibu wa kuanza maduka ya nyamapori kwa kanda ya Magharibi bado uko chini na kusema kuwa ni duka mmoja ambalo limeshaanzishwa na liko Katavi.




Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger