Sunday, 6 June 2021

KUMBE TB JOSHUA ALIJITABIRIA KIFO CHAKE WIKI HII, TAZAMA VIDEO YAKE HAPA



Video ya muhubiri maarufu TB Joshua akitabiri kwamba hataweza kusherehekea siku yake ya kuzaliwa Juni 12,2021 kama kawaida imeibuka kwenye mtandao wa kijamii.

Haya yanajiri baada ya Mhubiri huyo maarufu mwenye umri wa miaka 57, kupumua pumzi yake ya mwisho Jumamosi, Juni 5,2021 lakini bado chanzo cha kifo chake hakijafichuliwa. 

Kulingana na video hiyo ambayo ilichapishwa kwenye Twitter Alhamisi, Juni 3,2021 mtumishi huyo wa Mungu alikuwa anatazamiwa kusherehekea siku yake ya kuzaliwa akitimia umri wa miaka 58 Jumamosi, Juni 12,2021.

Hata hivyo, pasta huyo Mnigeria alisema kutokana na sababu zisizoweza kuepukika ambazo hakuzitaja, alisema hatasherehekea siku hiyo. "Kwa watu wote kote ulimwenguni Juni 12, inakaribia na kama mjuavyo mimi ni mtu wa watu, kwa hivyo shida ya mmoja ni ya kila mtu. Kama ilivyo, unaweza kutambua kuwa haikuwa rahisi kwangu kusherehekea siku yangu ya kuzaliwa. Watu ambao wanataka kuja wamezuiwa na hali hiyo," alisema Joshua. 

Badala yake aliamua kufunga na kuomba kwa ajili ya siku hiyo spesheli. Wakati wa siku hiyo, aliwahimiza wafuasi wake kuwakumbuka wasiojiweza. Taarifa katika ukurasa wake wa Facebook zilisema alifariki Jumamosi baada ya kumtumikia Bwana kwa kipindi kirefu.

 "Mnamo Jumamosi, Juni 5, 2021. Nabii TB Joshua alizungumza kwenye mkutano wa Emmanuel TV Partners kuhusu wakati wa kuja hapa kufanya maombi na wakati wa kurudi nyumbani kwa ibada," taarifa hiyo ilisema.

"Mungu amemchukua mtumishi wake Nabii TB Joshua nyumbani kama inavyotakikana. Siku zake za mwisho duniani zilikuwa za huduma kwa Mungu. Hili ndilo alizaliwa kufanya, na alifariki akifanya hivyo," taarifa iliongeza. 



HUYU NDIYE TB JOSHUA..MHUBIRI MWENYE MIUJIZA MINGI ALIYEKAA TUMBONI KWA MAMA YAKE MIEZI 15

 

Share:

TIGO WAPANDA MITI 500 KUADHIMISHA SIKU YA MAZINGIRA

 

Mkurugenzi wa Tigo, Simon Karikari akipanda miti katika viwanja vya Half London, Hai, Kilimanjaro Tunaadhimisha Maadhimisho ya siku ya mazingira duniani yenye kauli mbiu “Kurejesha Mfumo wa Ikolojia” kwa kupitia mkakati wetu wa #TigoGreenForKili tunarejesha mazingira mazuri yanayozunguka Ml. Kilimanjaro kwa kupanda miti 28,000 mwaka huu.

KILIMANJARO YETU: Urithi wetu uko mikononi mwetu, tunapanda miti kuhakikisha theruji ya mlima huu mrefu barani Afrika haipotei kutokana na shughuli na mabadiliko ya tabia nchi.

Jackson Haule- Mwakilishi kutoka NEMC akipanda Mti kama mkakati wa kurejesha mazingira salama mkoa wa Kilimanjaro.

Wafanyakazi wa Kampuni ya Northern Engineering wakipanda Miti kama ishara ya kurejesha hadhi ya Ml Kilimanjaro na kuifanya Kilimanjaro ya kijani ten

Mkurugenzi wa Tigo, Simon Karikari akipanda miti katika viwanja vya Half London, Hai, Kilimanjaro

Tunaadhimisha Maadhimisho ya siku ya mazingira duniani yenye kauli mbiu “Kurejesha Mfumo wa Ikolojia” kwa kupitia mkakati wetu wa #TigoGreenForKili tunarejesha mazingira mazuri yanayozunguka Ml. Kilimanjaro kwa kupanda miti 28,000 mwaka huu.



HATUNA BUDI “Mabadiliko ya tabia ya nchi na shughuli za kibinadamu yameathiri Mazingira ya Mlima Kilimanjaro hivyo hatuna budi kuchukua tahadhari ndio mana kupitia #TigoGreenForKili tutaweza Kurejesha Mfumo wa Ikologia”.
Asifiwe James - Mkurugenzi @voewofo




LENGO KUU “Dhima ya mwaka huu #SikuYaMazingiraDuniani yenye kauli mbiu Kurejesha Mfumo wa Ikolojia, inaendana na mkakati wetu wenye lengo la kurejesha hadhi ya mlima Mrefu barani Afrika kupitia mkakati wa #TigoGreenForKili kupanda miti 28,000 mwaka huu” Mkurugenzi wa Tigo, Simon Karikari



“Mazingira ni muhimu & ni chanzo cha uhai wetu, hatuna budi kuyatunzq ili yatutunze hasa kupitia mkakati huu ambao @tigo_tanzania wamekuja nao” Jackson Haule- Mwakilishi kutoka NEMC

AHADI YETU KWENU: “Tunawahakikishia kuilinda vyema miti hii 500 tutakayoipanda katika viwanja vya Half London ili kwa pamoja tuweze kuifanya Kilimanjaro iwe ya kijani tena.” Mkurugenzi wa mamlaka ya Mji wa hai, Noel Nnko
Tumeanza rasmi maadhimisho ya siku ya mazingira duniani yenye kauli mbiu “Kurejesha Mfumo wa Ikolojia”. Kupitia mkakati wa #TigoGreenForKili 
tumedhamiria kurejesha mazingira mazuri yanayozunguka Ml. Kilimanjaro kwa kupanda miti 28,000 mwaka huu. Kupitia michango mbalimbali kutoka kwa wadau mbalimbali tumeweza na tunaendelea kupanda miti katika maeneo mbalimbali mkoa wa Kilimanjaro.

.
Tunapongeza & kuwashukuru wadau wetu wote walioitikia wito huu


 
Share:

SALMA BINTI MZURI ALIONEKANA KAMA ALIKUWA NA UJAUZITO

Share:

HUYU NDIYE TB JOSHUA..MHUBIRI MWENYE MIUJIZA MINGI ALIYEKAA TUMBONI KWA MAMA YAKE MIEZI 15


Maelezo ya picha,TB Joshua
Mfahamu Temitope Balogun JoshuaJe maarufu TB Joshua

Habari za kifo cha Temitope Balogun Joshua ambaye ni maarufu kwa jina T.B Joshua zimewashangaza raia wengi wa Nigeria na dunia kwa ujumla.

Kanisa lake la Sinagogi la mataifa yote SCOAN ambalo lilianzishwa na muhubiri huyo lilithibitisha habari za kuhuzunisha za kifo chake Jumapili alfajiri likisema:.


Muhubiri TB Joshua anaacha sifa za huduma na kujitolea kwa ufalme wa Mungu ambao utaendelea kuwepo kwa vizazi vijavyo.

Wosia wa T.B Joshua

Muhubiri TB Joshua ni raia wa Nigeria kiongozi na mwanzilishi wa kanisa la SCOAN ambalo limekuwa likirusha matangazo yake mubashara katika runinga ya Emmanuel TV mjini Lagos kusini mwa Nigeria.

Alizaliwa kama Temitope Balogun Joshua mnamo tarehe 12 mwezi Juni ,1963 katika jimbo la Ondo nchini Nigeria.

Kulingana na Mtandao wa kanisa lake la SCOAN , Joshua alikuwa ndani ya tumbo la mamake kwa miezi 15 kabla ya kuzaliwa kwake.

Joshua alisomea katika shule ya msingi ya St. Stephen Anglican {Ikare-Akoko, Nigeria 1971-1977} lakini aliwacha shule alipojiunga na shule ya upili baada ya mwaka mmoja na kufanya kazi katika shamba moja la kuku.

Akiwa shuleni alijulikana kama muhubiri mdogo kutokana na alivyokuwa akiipenda Biblia na uwezo wa kutabiri matukio yaliofanyika katika jamii yake , kulingana na mtandao wa SCOAN.

Alianzisha kanisa la SCOAN mwaka 1987 akiwa na waumini wachache kabla ya kanisa hilo kupanuka hadi kimataifa.

Mwaka 2009 TB Joshua alianzisha klabu ya kandanda kwa jina My people FC katika juhudi za kuwasaidia vijana.

Wanachama wawili wa timu hiyo Sani Emmanuel na Ogenyi Onazi walichezea Nigeria Golden mwaka 2009, katika kombe la dunia la wachezaji wasiozidi umri wa miaka 17.

Tayari wachezaji watatu wamepata ufadhili Ulaya kuwa wachezaji wa kulipwa nchini Sweden.

Kulingana na jarida la Forbes 2011 , Temitope Joshua ni muhubiri wa tatu tajiri nchini Nigeria akiwa na thamani ya $15m.

Utata wa TB Joshua

Baadhi ya watu wamekuwa wakimkosoa kutokana na idadi ya miujiza yake anayofanya katika mikutano yake.

Baraza la makanisa ya Pentecostal nchini Nigeria PFN , chini ya mwavuli wa makanisa ya Pentecostal nchini Nigeria hayakubaliani na kanisa la muhubiri huyo wakimtaja TB Joshua kuwa kibaraka.

Christ Okote muhubiri wa kanisa maarufu nchini Nigeria alimshutumu Joshua kwa kuwa 'mganga'

Wakosoaji wake wa Kikristo wanasema kwamba mbinu zinazotumiwa na Joshua haziendani na zile za biblia.

Chanzo  - BBC Swahili

Share:

WAFANYAKAZI BARRICK WAADHIMISHA SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI 2021 KWA VITENDO

Katika maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani 2021, yaliyofanyika mwishoni mwa wiki, Wafanyakazi wa kampuni ya Barrick nchini, walishiriki kusafisha na kupanda miti katika maeneo ya kuzunguka migodi na kufanya uhamasishaji kwa jamii kutunza mazingira.
Wafanyakazi wa mgodi wa Barrick wa North Mara wakishiriki zoezi la kupanda miti katika maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani
Wafanyakazi wa mgodi wa Barrick wa North Mara wakishiriki zoezi la kupanda miti katika maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani
Wafanyakazi wa Barrick-North Mara wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumaliza zoezi la kusafisha mazingira na kupanda miti katika maeneo ya mgodi kuadhimisha siku ya Mazingira Duniani mwishoni mwa wiki.
Share:

STEPHEN MASELE AMLILIA TB JOSHUA

 

Aliyekuwa Makamu wa Rais wa Kwanza wa Bunge la Afrika (PAP) ,Stephen Masele ametuma salamu za rambirambi kufuatia kifo cha Mhubiri wa kimataifa, Temitope Balogun Joshua maarufu TB Joshua.

TB Joshua ni mwanzilishi wa kanisa la Synagogue Church of All Nations (Scoan) na kituo cha televisheni cha Emmanuel TV ambacho amekuwa akikitumia katika mahubiri yake.

Share:

MHUBIRI MAARUFU TB JOSHUA AFARIKI DUNIA


Mhubiri wa kimataifa, Temitope Balogun Joshua maarufu TB Joshua amefariki dunia jana Jumamosi Juni 5, 2021 nchini Nigeria.

TB Joshua ni mwanzilishi wa kanisa la Synagogue Church of All Nations (Scoan) na kituo cha televisheni cha Emmanuel TV ambacho amekuwa akikitumia katika mahubiri yake na kuwavutia watu wa mataifa mbalimbali.

Taarifa iliyotolewa na kanisa lake la Scoan inaeleza kwamba TB Joshua alifariki muda mfupi baada ya kutoa huduma katika kanisa hilo Jumamosi.

Taarifa hiyo ilisema: Mungu amechukua maisha ya mhudumu wake TB Joshua kulingana na uwezo wake. Amefariki akimuhudumia Mungu.

Taarifa hiyo imetaja sura moja katika biblia inayosema : Mungu muweza hawezi kufanya lolote bila kutoa mipango yake kwa watume wako. " - Amos 3: 7

"Mungu amemuita nyumbani Nabii TB Joshua kwa mapenzi yake. Nyakati zake za mwisho hapa duniani alizitumia katika huduma ya Mungu. Hiki ndio kitu alichozaliwa kukifanya, alikiishi na kukifia," inaeleza taarifa hiyo.

Hata hivyo, taarifa hiyo haijaeleza chanzo cha kifo chake huku ikiwataka waumini kumwombea mhubiri huyo na kuwapa nafasi wanafamilia kuomboleza kifo cha mpendwa wao.


Siku ya Jumamosi tarahe 5 Juni 2021, mtume TB Joshua alizungumza katika mkutano wa runinga ya Emmanuel.
alisema 'kila jambo na wakati wake, kuna wakati wa kuja hapa kwa maombi na wakati wa kurudi nyumbani baada ya ibada'."

TB Joshua alizaliwa mwaka 1963 na mpaka anakutwa na mauti alikuwa na umri wa miaka 58.

Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI JUNI 6,2021












Share:

Saturday, 5 June 2021

Tume Ya Pamoja Tanzania Na Msumbiji Zajadili Masuala Ya Ulinzi, Usalama Na Amani


Na Mwandishi wetu, Dar

Tume ya pamoja ya Ulinzi na Usalama ya Tanzania na Msumbiji imekutana kujadili  masuala ya ulinzi na usalama kati ya Mataifa hayo.

 

Akiufungua Mkutano huo wa tatu wa Tume ya pamoja ya ulinzi na usalama kati ya Tanzania na Msumbiji Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula, amesema mkutano huo ni wa muhimu kwakuwa unatoa fursa ya kuangalia namna ya kukabiliana na matukio yanayotishia ulinzi na usalama yamejitokeza kusini mwa Tanzania na kaskazini mwa Msumbiji ili kwa pamoja kupata suluhisho la kudumu.

 

“Mkutano wa leo pia utatoa fursa ya kuangalia masuala ya Ulinzi na Usalama, masuala ya mtambuka ambayo ni pamoja na umaskini na utawala bora katika nchi zetu mbili, kikao hiki ni muhimu sana kwani kitarudisha imani kwa wananchi na kuonesha kuwa hatujalala hadi hali itengamae kule Msumbiji,” Amesema Balozi Mulamula

Balozi Mulamula ameongeza kuwa, anaamini kupitia majadiliano yaliyoanza kuanzia tarehe 3 Juni kwa ngazi ya Wataalamu / Makatibu Wakuu hadi leo terehe 5 Juni mkutano wa ngazi ya Mawaziri utapitia mapendekezo ya vikao vya awali kuweza kuchukua maamuzi katika maeneo masuala ya ulinzi, usalama na usalama wa jamiii.

Ujumbe wa Msumbiji umeongozwa na Waziri wa Ulinzi wa Msumbiji Mhe Jaime Augusto Neto na kuainisha masuala jumuishi kuhusu ulinzi na usalama na kwamba ni Imani yake kuwa kikao hicho kitatoka na maazimio ya utekelezaji ili kuwa na mtangamano imara.

 

Katika tukio jingine Umoja wa Ulaya umesema unaunga mkono hatua za muendelezo na mabadiliko ya sera za kijamii na maendeleo yanayofanywa Nchini,chini ya uongozi wa Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan na kwamba unapongeza hatua hizo.

 

Akizungumza kwa niaba ya mabalozi wa Jumuiya ya Ulaya hapa Nchini katika kikao kazi walichokiandaa Jijini Dar es Salaam,Balozi wa Umoja huo Mhe Manfredo Fanti ameongeza kuwa matamko ya Rais Samia kuhusu ushirikiano kati ya Tanzania na Jumuiya za Kimataifa,sekta binafsi,uhuru wa kujieleza,haki za binadamu na utawala bora yanatia moyo.

 

“Matamko na maelekezo ya Mhe. Rais Samia kuhusu ushirikiano kati ya Tanzania na Jumuiya za Kimataifa,sekta binafsi,uhuru wa kujieleza,haki za binadamu na utawala bora yanatia moyo na kutuhamasisha kuwashawishi wawekezaji na wafanyabiashara kuja kuwekeza Tanzania,” Amesema Balozi Fanti. 

 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula amesema mkutano huo ulikuwa ni wa muhimu kwa kuwa unaweka misingi ya kuaminiana na kuimarisha mahusiano kati ya Tanzania na Umoja huo ili kuweka mazingira bora ya Mabalozi hao kuhamasisha wawekezaji na wafanyabiashara kutoka katika Mataifa yao kuja kuwekeza hapa nchini.



Share:

JAMAA MATATNI BAADA YA KUNASWA LIVE AKIPAKUA ASALI YA JIRANI YAKE...AAMRISHWA ACHANGIE MAHARI

Jamaa mmoja kutoka eneo la Seme, Kisumu nchini Kenya amejikuta pabaya na kulazimishwa kuchangia mahari baada ya kunaswa peupe akipakua asali kutoka kwa mzinga wa jirani yake. 

Penyenye zinasema kuwa jamaa amenaswa akila uroda na mke wa jirani ambaye alipowasili nyumbani na kugundua kilichokuwa kikiendelea alifunga mlango kwa nje kumzuia mshukiwa kuponyoka.

“Jamani leo nimeshika. Njooni muone,” mwenye nyumba alipiga mayowe kuwaita watu kulingana na Taifa Leo. 

Punde si punde boma lilifurika watu. “Jirani yangu yumo ndani. Nimempata hadharani kitandani na mke wangu,” jamaa alieleza.

 Duru zinaarifu kwamba umati huo ulichacha kwa hasira na kumtaka jamaa afungue mlango ili wampe kichapo mwizi huyo wa mapenzi.

 “Sifungui mlango. Nawasubiri wazee waje kisha waamue hii kesi,” jamaa alidai.

Muda mfupi baadaye wazee waliwasili naye mwenye nyumba akawaeleza kila kitu.

Baada ya wazee kutulia mlango ulifunguliwa. Mara tu mlango huo ulipofunguliwa wanaume waliokuwa wamefika bomani humo kujionea kisanga hicho walimrukia na kuanza kumzaba jirani huyo makofi.

 “Huyu ni jirani yangu. Nimekuwa nikishuku kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na mke wangu,” jamaa aliwaarifu wazee. Inasemekana kimya kilitawala huku kila mmoja akitaka kupata uhondo.

“Nikiondoka kwa boma huwa napata habari kwamba mke wangu huonekana naye kila mahali, sio sokoni, sio wakitoka gesti fulani,” mwenye boma alisema huku vicheko vikishamiri.

“Leo nimempata mwenyewe juu ya mzinga. Kile ninataka wazee waamue ni kwamba achangie kulipa mahari kwa kuwa ni wazi tunachovya asali kutoka mzinga mmoja,” jamaa alisema.

 Penyenye zinasema kuwa jamaa alijaribu kuomba msamaha lakini hakuna aliyetaka kumsikia. 

“Hii tabia umekuwa ukiifanya kwa muda. Faini unayopigwa kwa sasa ni wewe kuchangia mahari. Mahari hayo unaitoa leo,” jamaa alifokewa huku akibaki mdomo wazi. 

“Ng’ombe watatu ambao umefuga walete sasa hivi,” kijogoo aliamrishwa.

Share:

SERIKALI YATOA UFAFANUZI JUU YA MWANAFUNZI ALIYEVAA MABANGO SHINYANGA MJINI "HAKUCHAGULIWA ECA NA HANA SIFA ZA PCB"

 

Mwanafunzi Josephat John, aliyekuwa anasoma kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Kom iliyopo Manispaa ya Shinyanga, akiwa amevaa mabango na kujifunika maboksi 

****

Mwanafunzi Josephat John hakuchaguliwa ECA na hakuwa na sifa za kuchaguliwa PCB

OR-TAMISEMI,DODOMA

Mwanafunzi Josephat John aliyekuwa anasoma kidato cha nne shule ya Sekondari Kom iliyopo kwenye Manispaa ya Shinyanga alizua taharuki baada ya kujianika juani huku akiwa amevaa mabango yenye ujumbe wa kupinga kuchaguliwa masomo ya biashara (ECA) ambayo anadai hajawahi kusomea kwani yeye amesoma masomo ya Sayansi(PCB)

Mwanafunzi huyu amepata Div II:21 na masomo ya sayansi anayodai amesomea amepata DCC yenye jumla ya pointi 10. Mwisho wa pointi za wanafunzi waliopangiwa Tahasusi hii ni 8 sawa na BCC, hivyo mwanafunzi huyu hajakidhi vigezo vya kuchaguliwa katika Tahasusi hii ya PCB kulingana na idadi ya nafasi zilizopo mwaka huu.

Hata hivyo Mwanafunzi huyu hajapangiwa Tahasusi ya Biashara (ECA) kama anavyodai, bali amepangiwa kusoma Stashahada Maalumu ya Ualimu kwa Masomo ya Physicis na Hesabu katika chuo cha Ualimu Songea ambapo ni miongoni mwa Maeneo aliyochagua katika machaguo ya vyuo alianza na Ufundi, Afya kisha Elimu.

OR TAMISEMI inaendelea kumtafuta mwanafunzi huyu ili iweze kufahamu nia na shida ambayo amekumbana nayo mpaka kufikia kufanya kitendo hiki.

OR TAMISEMI inaendelea kusisitiza kama kuna mzazi au mlezi yoyote anahitaji ufafanuzi wowote awasiliane na kituo chetu cha huduma kwa wateja kwa kupiga simu namba 0735-160201 na 0262-160201 kuandika barua pepe kwenye anwani yetu huduma@tamisemi.go.tz


Share:

RAS MWALUKO AELEZA AJIPANGA KUPIGANIA ELIMU YA MTOTO WA KIKE


Katibu Tawala mpya wa Mkoa wa Singida Dorothy Mwaluko akizungumza kwenye hafla ya makabidhiano ya ofisi iliyofanyika jana Mkoani Singida.

Na Edina Alex Singida
Katibu Tawala Mpya wa Mkoa wa Singida Bi. Dorothy Mwaluko amekabidhiwa rasmi ofisi na mtangulizi wake Dkt. Angelina Lutambi huku akiahidi kusimamia kidete elimu ya mtoto wa kike.

Akizungumza kwenye hafla ya makabidhiano hayo jana, Mwaluko pamoja na mambo mengine ameomba ushirikiano kutoka kwa watendaji wote mkoani Singida ili kusukuma kasi ya maendeleo lakini zaidi kuleta ustawi kwenye eneo la elimu na maboresho ndani ya sekta ya afya.

"Kitaaluma mimi ni mwalimu,na kipaumbele changu hasa ni masomo ya sayansi, natamani na nitasimamia kuhakikisha watoto wa kike wanasoma masomo haya kwa mafanikio makubwa",alisema katibu Tawala na akaongeza;

"Kwenye elimu msitarajie kunidanganya na atakayekwenda kinyume hatutaelewana,".

Aidha kwenye eneo la afya ameomba kila mtendaji kuwajibika ipasavyo ili matarajio ya wanasingida yazidi kudhihirika kupitia serikali inayoongozwa na Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Kwa upande wake aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida Dkt Lutambi ambaye kwa sasa amehamishiwa Mkoa wa Mbeya, pamoja na mambo mengine amemueleza Mwaluko kuwa hali ya uchumi wa Mkoa inaendelea kuimarika siku hadi siku.

Hata hivyo ameshauri kuwepo kwa msukumo mkubwa na usimamizi kwenye utekelezaji wa sheria ya fedha za serikali za mitaa hasa kupitia tangazo la serikali namba 286 la April 5, 2019 ambalo lilielekeza asilimia 10 ya fedha za mfuko wa Wanawake,Vijana na wenye ulemavu zitolewe ipavyo.

"Utoaji wa fedha hizo mpaka sasa bado haufanyiki kulingana na sheria inavyoelekeza, hivyo msukumo mkubwa na usimamizi vinahitajika sana ili kutoa fursa kwa makundi hayo kunufaika", alisema.
Aliyekuwa Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dkt. Angelina Lutambi kulia akimkabidhi nyaraka Katibu Tawala mpya wa mkoa huo Dorothy Mwaluko kwenye hafla ya makabidhiano ya ofisi iliyofanyika jana Mkoani Singida.
Aliyekuwa Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dkt. Angelina Lutambi akizungumza kwenye hafla ya makabidhiano ya ofisi iliyofanyika jana Mkoani Singida.
Share:

TUTUMIE NISHATI MBADALA KUHIFADHI MAZINGIRA - WAZIRI NDAKI

 

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh. Mashimba Ndaki akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kufika kwenye banda la Wizara tarehe 03.06.2021 na kujionea shughuli zinazofanywa na Sekta ya Mifugo na Uvuvi  Katika utunzaji na uhifadhi wa Mazingira kwenye Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani inayofanyika katika Viwanja vya Jakaya Kikwete Convention Centre, Dodoma

Nahodha Mwandamizi kutoka Idara ya Uvuvi Bw. Dickson Stowa akitoa maelezo kwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh. Mashimba Ndaki juu ya Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira kwa kutumia Zana za Uvuvi tarehe 03.06.2021 kwenye Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani inayofanyika katika Viwanja vya Jakaya Kikwete Convention Centre, Dodoma.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh. Mashimba Ndaki akipatiwa maelezo ya namna ya kuandaa udongo wa kuoteshea miche kwa ajili ya kutunza Mazingira na Mkurugenzi Mkuu wa mradi wa "The Young World Feeders" Bw. Ray Peter alipotembelea banda la Wizara ya Kilimo tarehe 03.06.2021 kwenye Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani inayofanyika katika Viwanja vya Jakaya Kikwete Convention Centre, Dodoma
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh. Mashimba Ndaki akipewa elimu na Mratibu wa Miradi ya Uhifadhi wa Wanyama Pori Bw. Rich Katondo juu ya Wananchi kujikinga na mazao yao ili Kupunguza migogoro kati ya Hifadhi ya wanayama pori na mifugo leo tarehe 03.06.2021 kwenye Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani inayofanyika katika Viwanja vya Jakaya Kikwete Convention Centre, Dodoma

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.Mashimba Ndaki amesisisitiza wananchi kutumia nishati mbadala ili kuhifadhi na kutunza mazingira kwenye Sekta ya Mifugo na Uvuvi

Waziri Ndaki ameyasema hayo leo tarehe 03.06.2021 alipotembelea baadhi ya mabanda kwenye Maadhimisho ya Siku ya Mazingira inayofanyika Katika Viwanja vya Jakaya Kikwete Convetion Centre ,Jijini Dodoma na kusisitiza elimu zaid juu ya nishati mbadala      Kwa Wananchi ili kutunza Mazingira vizuri.

“Tujali sana kutunza mazingira tunapofanya shughuli za kiuchumi na kijamii, kwenye shughuli za kufuga na kuvua lazima tujali kuhifadhi mazingira, tusipohifadhi mazingira tutakosa na mazalia ya samaki na samaki watakosa chakula”,amesema Waziri Ndaki.

Mhe. Ndaki amesema kuwa ili shughuli zetu za ufugaji na uvuvi ziweze kuendelea tuhifadhi kwenye maeneo ya nchi kavu, bahari , mito, maziwa na maeneo ya misitu ili ziweze kuwa endelevu.

“Watanzania tutunze mazingira ya nchi yetu ili yaweze kututunza”alimalizia Waziri Ndaki alipokuwa akihitimisha wito wake kwa Wananchi .

Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi Huduma za Ugani (Sekta ya Mifugo) Dkt. Kejeri Gillah amesema kuwa, wafugaji wazingatie namna bora ya kufuga mifugo yao, kuhifadhi na kutunza mazingira vizuri.

“Kabla ya kupanda malisho ni vizuri kujua mbegu inayostahimili ikolojia na wafugaji wazingatie malisho yanayostahimili  katika maeneo husika”, alisema Dkt. Gillah.

Aidha, Dkt. Gilla amebainisha kuwa watu wanapochinja Mifugo yao takataka zinazotokana na Mifugo hiyo inaenda kuchafua mazingira, hivyo tunashauri wafugaji kuzingatia namna bora ya kutunza Mifugo na mazingira.

Naye, Mkuu wa kitengo cha mazingira (Sekta ya uvuvi) Bw. Melton Kalinga, amesema kuwa lengo la maonesho haya ni kutumia zana za uvuvi rafiki kwa mazingira kwa ajili ya kutunza viumbe hai majini, hususani samaki.

Aidha, Nahodha Mwandamizi kutoka Idara  ya Uvuvi Dickson Stoah ameongeza kuwa, uharibifu wa mazingira unatokana na Utumiaji wa zana haramu majini na hivyo kuathiri mfumo mzima wa viumbe maji.

Kwa upande wa Wadau wa mazingira waliokuwa wanatembelea mabanda, baadhi ya washiriki wameipongeza Serikali kwa kuweka Maadhimisho hayo kwa ajili ya kuelimisha na kujifunza juu ya uhifadhi na utunzaji wa mazingira kwa kutumia nishati mbadala kuongoa mfumo wa ikolojia.

Maadhimisho ya siku ya mazingira Duniani yatahitimishwa tarehe 05.06.2021 Jijini Dodoma Katika Viwanja vya Jakaya Kikwete Convetion Centre ambapo kauli Mbiu yake ikiwa inasema “Tutumie Nishati Mbadala kuongoa mfumo wa Ikolojia”.


Share:

SEKTA ZA MIFUGO TANZANIA BARA NA ZANZIBAR ZAIMARISHA USHIRIKIANO.


*Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Prof. Elisante Ole Gabriel akizungumza na wataalam wa Sekta ya Mifugo wa Serikali ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar pamoja na waandishi wa habari (hawapo pichani)  wakati wa kikao cha wataalam wa Sekta ya Mifugo kilichofanyika kwenye ukumbi wa TVLA Jijini Dar es, (04/06/2021)*

*Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Umwagiliaji Maliasili na Mifugo Zanzibar Bi. Maryam Juma Saadalla akiongea wakati wa kufunga kikao cha  ushirikiano cha wataalam wa Sekta ya Mifugo wa Serikali ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kilichofanyika kwenye ukumbi wa TVLA Jijini Dar es Salaam. (04//06/2021)*

*Makatibu wakuu wa Sekta ya Mifugo (wa pili kutoka kushoto mbele ni Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Elisante Ole Gabriel, wa tatu kutoka kushoto ni Katibu Mkuu, Wizara ya Kilimo Umwagiliaji Maliasili na Mifugo Zanzibar Bi. Maryam Juma Saadalla wakiwa kwenye picha ya pamoja na wataalam wa Sekta hiyo mara baada ya kikao  cha ushirikiano Kati ya Serikali hizo mbili kilichofanyika kwenye ukumbi wa TVLA Jijini Dar es Salaam (04/06/2021).*


Wizara ya Mifugo na Uvuvi na Wizara ya Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo Zanzibar zimekubaliana kuendeleza ushirikiano na kutatua changamoto za  kiutendaji katika ngazi za idara na taasisi zikiwemo Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI)   na Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Zanzibar (ZALIRI).

Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi  Prof. Elisante Ole Gabriel alisema hayo wakati wa mapitio ya taarifa ya kikao cha wataalam wa sekta ya Mifugo wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kilichofanyika Juni 04, 2021 Jijini Dar es salaam.

Alisema utaandaliwa mkakati wa pamoja wa mawasiliano katika sekta hizo za pande mbili ili wadau pia watambue ushirikiano huo ambao umelenga kukuza uzalishaji katika sekta ya Mifugo hapa nchini.

Alisema pamoja na mambo mengine wataangalia namna ya kuwepo kwa urahisi wa utekelezaji wa vibali vya mazao ya mifugo ili vibali ambavyo vimetolewa Zanzibar vitambulike bara na vilivyotolewa bara vitambulike Zanzibar.

"Utaandaliwa mkakati wa pamoja wa mawasiliano katika sekta hizi za pande mbili ili wadau pia watambue ushirikiano huo ambao umelenga kukuza uzalishaji katika sekta ya Mifugo  nchini pamoja na kuwepo kwa urahisi wa utekelezaji wa vibali vya mazao ya mifugo" alisema Prof. Elisante

Aliongeza kuwa uamuzi huo umekusudia kuboresha mazingira ya kufanyia biashara ili kuleta manufaa ya kiuchumi kwa muungano na kwamba utaratibu na kukuza ubora wa wataalam wa mifugo.

Kadhalika alibainisha suala la tozo ya maziwa yaliyokuwa yakitoka Zanzibar (maziwa ya unga) ambapo mnufaika wa nafuu ya tozo hiyo ni Azam kwa makubaliano ya kuhakikisha anawezesha wazalishaji wa maziwa Zanzibar kuendelea na waliazimia aendelee na tozo iliyoazimiwa.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo Zanzibar Maryam Juma Sadalla alisema matayarisho ya sheria ya mifugo ni muhimu lifanyike kwa wakati kama walivyokubaliana ili kukuza sekta ya mifugo  Nchini.

Alisema kukamilika kwa sheria hiyo kutasaidi kuwepo kwa udhibiti wa magonjwa ya mlipuko ambayo yamekuwa yakisumbua mifugo hasa homa ya mafua ya ndege ambayo imekuwa changamoto kubwa kwa upande wa Zanzibar

“Nashukuru hatua iliyochukuliwa kuendeleza sekta yetu ya kilimo ambayo imeleta faraja kwa kutuongezea ajira kwa vijana ambao wamepata fursa ya kuzalisha vifaranga kupitia vibali maalum kwa sababu ya changamoto ya mafua ya  ndege” alisema Bi. Maryam.


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger