Wednesday, 19 May 2021

SHUHUDIA MAAJABU YA NG'OMBE WANAOOGELEA KAMA BINADAMU


Ng'ombe wakiogelea na binadamu
Jamii ya Njemps au Ilchamus

Mwandishi ni Kevin Anindo, Kaunti ya Nairobi.

Hii ni Afrika na Afrika kuna mengi ya kuvutia. Leo nakuangushia makala kuhusu mila ya zamani ya kabila la eneo la Ziwa Baringo linalohusishwa na biashara na maisha ya kabila lililo katika hatari ya kuangamia inakuwa kivutio halisi cha watalii, hasa kipindi hiki Kenya inapoendelea kushuhudia kuimarika zaidi kwa utalii wa ndani na kupungua kwa wageni au kusafiri nje kwa matajiri.

 Hili ni tukio la "ajabu" lisicho la kawaida la ng'ombe wanaoogelea wa Kisiwa cha Kokwa. Jamii ya wafugaji ya Njemps, kabila la dogo la Wamaasai ambalo idadi ya watu wake ni zaidi ya 30,000, hawana njia nyingine ya kuuza ng'ombe wao zaidi ya kusafirisha kila wiki kwenda sokoni katika mji wa Marigat.

Njemps ni moja ya jamii zinazotajwa kuwa maskini sana na wana mitumbwi ya miti ya asili ambayo hawawezi kuitumia kusafirishia ng'ombe wao hadi okoni, kwa hivyo kwa miaka mingi wamefundisha ng'ombe wao kuogelea kwenye maji ya ziwa kufikia ufukweni kutoka kisiwa hicho.

 Kwa muda baada ya hamu ya kushuhudia ng'ombe hao wakiogelea, tukio hilo sasa ni moja katika vivutio vya utalii huko Baringo na eneo jirani na mara nyingi ng'ombe hao husindikizwa na boti zilizobeba watalii na wao hufurahia kupiga picha na video hata kwa kutumia simu zao za rununu. 

Wakati mwingine, boti zile zile ambazo, kwa upande mwingine, labda zinamilikiwa na hoteli ambazo hutumika kushuhudia "kivutio hicho cha kabila hili" hutumiwa kuwabeba ng'ombe hao. 

Lakini ni vipi ng’ombe wanaojulikana kuwa waoga wa maji ya kina kirefu hufaulu kuogelea?

 Ingawa ng'ombe kwa kawaida ni mwogeleaji mzuri lakini inategemea mazingira, anaweza kuogelea vizuri-kama sio bora-kushinda mwanadamu. Maeneo mengine mfano hili tunalozungumzia, ng'ombe huogelea kwenye maji ya vina tofauti na ni sehemu ya maisha yao.

Mmoja wa wafugaji wa eneo hilo aliyezungumza na TUKO.co.ke alisema, "Walishaji mifugo wa Njemps hupeleka mifugo wao hadi kwenye ufukwe wa kisiwa hicho, kisha huwatupa majini ndama lakini wakiwa makini wasije wakazama au kusombwa.

"Kwa kuhofia kumpoteza ndama ng'ombe hufuata ili kuwaokoa na polepole watajifunza kuogelea.Wao huwarejesha ndama wao ufukweni na kisha tukio hilo hurejelewa mara kadha kwa kipindi fulani, mpaka watakapozoea kuogelea peke yao, bila kujali sana kuokoa watoto wao". 

Mazoea huwafanya ng'ombe kuwa tayari muda wote kuvuka mito peke yao kwa msaada mdogo. Lakini ni bora kufahamu kuwa, haimaanishi ng'ombe wanaoogolea wanaweza kuogelea tu bila kikomo.

 Ng'ombe wakianguka kwenye maji, wanahitaji njia ya kuwawezesha kutoka nje kabla ya kuchoka na labda kuzama. Nyakati nyingi, mito na maziwa huwa na maeneo yanayoteremkia fukweni ambayo huwasaidia ng,ombe walioingia kwenye maji hayo kutoka nje salama.

CHANZO - TUKO NEWS
Share:

WAKALA WA VIPIMO (WMA) WATEMBELEA VITUO VYA AFYA NA KUHAKIKI MIZANI


Muuguzi wa kituo cha afya mama na mtoto Chanika akimpima uzito mtoto pembeni wakiwa maafisa wa Wakala wa Vipimo (WMA) wakihakiki mizani hiyo kama ipo sahihi katika vipimo mara baada ya kutembelea katika kituo hicho kama kushiriki maadhimisho Siku ya Vipimo Duniani.
Maafisa wa Wakala wa Vipimo (WMA) wakihakiki mizani ya mtoto mdogo mara baada ya kutembelea katika kituo cha afya mama na mtoto Chanika kama kushiriki maadhimisho Siku ya Vipimo Duniani.
Maafisa wa Wakala wa Vipimo (WMA) wakihakiki mizani ya uzito mara baada ya kutembelea katika kituo cha afya mama na mtoto Chanika kama kushiriki maadhimisho Siku ya Vipimo Duniani.
Mama mjamzito akipimwa uzito.
Meneja wa Uhusiano kwa Umma wa Wakala wa Vipimo (WMA) Bi.Irene John akitoa elimu kwa wazazi kuhusu umuhimu wa mizani katika vituo vya afya mara baada ya kutembelea katika kituo cha afya mama na mtoto Chanika kama kushiriki maadhimisho Siku ya Vipimo Duniani.
Maafisa wa Wakala wa Vipimo (WMA) wakihakiki mizani inayopima uzito na urefu kwa wakati mmoja mara baada ya kutembelea katika kituo cha afya mama na mtoto Chanika kama kushiriki maadhimisho Siku ya Vipimo Duniani.
Mgonjwa akipima uzito
Maafisa wa Wakala wa Vipimo (WMA) wakihakiki mizani ya mtoto mchanga mara baada ya kutembelea katika kituo cha afya Buguruni kama kushiriki maadhimisho Siku ya Vipimo Duniani.

PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO

***************************

NA EMMANUEL MBATILO

Kuelekea siku ya Vipimo Duniani, Wakala wa Vipimo (WMA) wamezindua maadhimisho hayo kwa kutembelea vituo vya afya na hospitali katika eneo la Chanika na Buguruni kuhakiki mizani ambazo hutumika kwaajili ya vipimo.

Akizungumza mara baada ya kutembelea katika hospitali hizo, Meneja Wakala wa Vipimo Mkoa wa Ilala Bw.Saad Haruna amesema katika uhakiki walioufanya wamegundua mizani mingi bado inausahihi unaokubarika kwa matumizi.

Aidha Bw.Haruna amesema kuwa umhumu wa vipimo katika sekta ya afya ni pamoja na matumizi ya dawa kwani ili mgonjwa apate dawa sahihi anatakiwa kupimwa uzito ili apewe dozi kulingana na uzito wake.

"Vipimo kwa maana ya mizani ni muhimu katika sekta ya afya na sisi kwa kuliona hilo na kushirikiana na uongozi wa hospitali tumekuwa tukishirikiana nao katika uhakiki wa mizani kwenye hospitali za Ilala.Lakini hii si Ilala peke yake kwasababu Wakala wa Vipimo ina ofisi nchi nzima hivyo maadhimisho haya yamefanyika nchi zima katika mikoa na wilaya zote nchini". Amesema Bw.Haruna.

Kwa upande wake Muuguzi wa Kituo cha afya mama na mtoto Chanika Bi.Barry Fundi amewashukuru Wakala wa Vipimo kufika na kuhakiki mizani katika kituo hicho kwani kupitia hivyo kuna wapa mwangaza kuwa huduma wanazozitoa ni sahihi hata kwa vipimo vya dawa wanavyovitua kwa watoto kulingana na uzito kwa maana watoto wengi wanapewa matibabukulingana na uzito wao.

Nae fundi sanifu vifaa tiba katika kituo cha afya Buguruni Bw.Gidion Maganga amesema uhakiki wa mizani kwenye vipimo kwa maana inaongeza kitu katika matibabu yake ambapo itamsaidia kufahamu ni matumizi gani ya dawa anaweza kutumia na zisimletee madhara.

"Kuna wale ambao wanadharau mizani hizi ni hatari kwao kwasababu utakuja kupata dawa ambazo hazijaendana na uzito wao kitu ambacho kitaweza kukuletea madhara katika afya zao kwani hautakua unafahamu ni dozi gani unatakiwa kutumia". Amesema Bw.Maganga.

Maadhimisho haya hufanyika Mei 20 kila mwaka ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni "VIPIMO KATIKA SEKTA YA AFYA".

Share:

DRIVERS II (REGIONAL OFFICES)(RE-ADVERTISED) – 2 POST at LATRA

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

POST DRIVERS II (REGIONAL OFFICES)(RE-ADVERTISED) – 2 POST POST CATEGORY(S) ENGINEERING AND CONSTRUCTION HR & ADMINISTRATION EMPLOYER Land Transport Regulator Authority(LATRA) APPLICATION TIMELINE: 2021-05-18 2021-05-31 JOB SUMMARY N/A DUTIES AND RESPONSIBILITIES (i) To conduct pre-inspection and ensure cleanliness of the Authority’s vehicle prior to starting the engine and driving the vehicle; (ii) To drive the […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

Snr Admin Assistant at UNHCR

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

Eligible Applicants This position is advertised open to internal and external applicants. Procedures and Eligibility Interested applicants should consult the Administrative Instruction on Recruitment and Assignment of Locally Recruited Staff (RALS). Duties and Qualifications Senior Administrative Assistant Organizational Setting and Work Relationships The Senior Administrative Assistant will provide administrative support to the office where the […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

ARTISAN II At Tanzania Food and Nutrition Centre (TFNC)

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

POST: ARTISAN II – 1 POST POST CATEGORY(S): CREATIVE AND DESIGN ENGINEERING AND CONSTRUCTION EMPLOYER: Tanzania Food and Nutrition Centre (TFNC) APPLICATION TIMELINE: 2021-05-18 2021-05-31 JOB SUMMARY DUTIES AND RESPONSIBILITIES i.    To assist in operating printing machines; ii.    To sort and gather printed work; iii.    To operate both letter process and offset machines; iv.    To operate […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

Tazama Picha : RAIS SAMIA AWAAPISHA WAKUU WA MIKOA,KATIBU MKUU NA WATENDAJI WA TAASISI


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Amos Gabriel Makalla kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam katika hafla iliyofanyika leo tarehe 19 Mei, 2021 Ikulu Jijini Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Queen Cuthbert Sendiga kuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Stephen Nzohabonayo Kagaigai kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro katika hafla iliyofanyika leo tarehe 19 Mei, 2021 Ikulu Jijini Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Omary Tebweta Mgumba kuwa Mkuu wa Mkoa wa Songwe katika hafla iliyofanyika leo tarehe 19 Mei, 2021 Ikulu Jijini Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Mwanamvua Hoza Mrindoko kuwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Rosemary Staki Senyamule kuwa Mkuu wa Mkoa wa Geita
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuapisha David Zacharia Kafulila kuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu katika hafla iliyofanyika leo tarehe 19 Mei, 2021 Ikulu Jijini Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Brigedia Jenerali Charles Mang’era Mbuge kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera katika hafla iliyofanyika leo tarehe 19 Mei, 2021 Ikulu Jijini Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Charles Makongoro Nyerere kuwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara katika hafla iliyofanyika leo tarehe 19 Mei, 2021 Ikulu Jijini Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Brigedia Jenerali Wilbert Augustine Ibuge kuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma katika hafla iliyofanyika leo tarehe 19 Mei, 2021 Ikulu Jijini Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Nenelwa Joyce Mwihambi kuwa Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Balozi Joseph Edward Sokoine kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuapisha CP Salum Rashid Hamduni kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa PCCB
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Sylvester Antony Mwakitalu kuwa Mkurugenzi wa Mashitaka DPP
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Joseph Sebastian Pande kuwa Naibu Mkurugenzi wa Mashitaka
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Neema Mpembe Mwakalyelye kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa.

Viongozi wote walioapishwa Wakila Kiapo cha Maadili kwa Viongozi wa Umma Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Share:

Waziri Kalemani amsimamisha kazi Meneja TEHAMA TAESCO kisa ununuzi wa luku


Waziri wa Nishati Mh.Dkt.Medard Kalemani ameagiza kusimamishwa kazi kwa siku 10  watumishi watatu wa TANESCO akiwemo Meneja wa mfumo wa LUKU kwa kushindwa kutatua tatizo la LUKU lililojitokeza kwa siku tatu na kuleta  usumbufu kwa wananchi.

Waliosimamishwa kazi ni Meneja wa TEHAMA na huduma za biashara wa Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) Lonus Feruzi na Wasaidizi wake Frank Mushi na Idda Njau ili watoe maelezo kufuatia kuwepo kwa tatizo katika huduma ya manunuzi ya LUKU kupitia njia za kielektroniki na kusema endapo maelezo yao hayatojitosheleza wataondolewa kazini.

Kwa muda wa siku tatu, Wateja wa TANESCO wameshindwa kununua umeme wa LUKU kwa njia ya Kielekroniki hivyo kulilazimu Shirika hilo kuwaelekeza Wateja wake kununua umeme kwenye ofisi zake za Mikoa na Wilaya katika maeneo mbalimbali nchini.



Share:

Rais Samia Suluhu Hassan afanya mabadiliko kwa wakuu wa mikoa miwili


Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan  amefanya mabadiliko ya Uteuzi wa Wakuu wa mikoa wawili. 

John Mongella aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu atakuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha. David Kafulila aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha atakuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu

Rais Samia amesema hayo leo Jumatano, Mei 19, 2021 wakati akihutubia mara baada ya kumaliza kuwaapisha wakuu wa mikoa na wakuu wa taasisi, Ikulu jijini Dar es Salaam.

“Kuna mabadiliko madogo nimefanya, Kafulila nilimteua kuwa RC Arusha na Mongella kuwa RC Simiyu, nimeamua Mongella kwa sababu ulikuwa unaongoza Mkoa mkubwa basi ukawe RC Arusha na Kafulila kwa sababu ndio anaanza alikuwa RAS basi akawe RC Simiyu.

"Wote mlioapa na mlioteuliwa hongereni sana, nasema hongereni kwasababu Tanzania kuna Watu wengi na 15% wangefaa kuteuliwa lakini mmeteuliwa nyinyi, naamini mnapokwenda kufanya kazi zenu mtasimama na Mungu.

"Baada ya shughuli hizi za kuapishana na kupiga picha Wakuu wa Mikoa na Wateuliwa wengine mtarudi hapa na tutakuwa na kikao cha kazi kwahiyo kwasababu nina mambo mengi ya kuongea na nyinyi leo tuishie hapa tutakutana kwenye kikao cha kazi,” amesema Samia.



Share:

Officer, Integrated Middle Office (9 months contract) at Standard Chartered

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

About Standard Chartered  We are a leading international bank focused on helping people and companies prosper across Asia, Africa and the Middle East. To us, good performance is about much more than turning a profit.  It’s about showing how you embody our valued behaviours – do the right thing, better together and never settle – […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

Ukuaji Wa Michezo Ya Kubashiri Mtandaoni Nchini Tanzania

Michezo ya kubashiri ina kua  kwa kasi sana nchini Tanzania ni kutokana na hali ya mabadiliko ya ukuaji wa kiuchumi unao pambishwa na sera nzuri za uwekezaji za sasa kuwa rafiki kwa wekezaji kuwekeza katika michezo hii ya kubashiri.

Miaka kadhaa nyuma ilikuwa ni ngumu sana kwa michezo hii kuingia nchini kutokana na mifumo isiyo rafiki, na mwamko wa wananchi kuwa hafifu kutokana na sababu ya suala la utandawazi lilikuwa bado sana nchini, na kama ulikuwa umeingia basi uligusa familia chache ambazo kiuchumi ni bora.

Kuingia kwa sayansi na teknolojia na uwepesi wa upatikanaji wa vifaa wezeshi kucheza, kumeifanya Tanzania kupiga hatua zaidi na kuongezeka kwa idadi kubwa ya watu wanaojishughulisha na michezo hii ya kubashiri. Hali ya ukuaji inatiwa nguvu pia na uwepo wa Makampuni ya simu, laptop, tablate yanayozalisha vitendea kazi hivyo kupatikana kwa urahisi na kwa bei nafuu kabisa, hivyo kupelekea hata mtu wa uchumi mdogo kuweza kumiliki vitendea kazi hivyo.

 Kuwepo kwa  tovuti zinazoongoza kwa  dondoo za utabiri wa mpira wa miguu nchini Tanzania zikikiongozwa na tanzaniatips zinatoa chaguzi anuwai za mpira wa miguu, zilizotafitiwa kwa uangalifu na kuchambuliwa na timu zao za wataalam nguli wa kubashiri mpira wa miguu. Kutumia kanuni na hesabu za ubashiri na mifumo ya kieletroniki, wataalam wao uchagua uteuzi bora wa bashiri za mpira wa miguu kila siku.  Hivyo nakushauri kabla hujaweka mkeka wako hakikisha unatembelea tovuti ya Tanzaniatips ili upate dondoo za michezo na ubashiri.

Kwa Kuzingatia ligi kuu za mpira wa miguu ulimwenguni kote pamoja na Ligi Kuu Uingereza, Serie A na La Liga, wataalam na mifumo ya wavuti nyingi mtandaoni  huandaa takwimu na dondoo kwa wafuasi wao. Kisha wanachapisha chaguzi zao zilizotafitiwa kwenye wavuti zao ili uone na kubashiri, zote ikiwa ni BURE! Kwa baadhi ya makampuni na mengine niunachangia kwa gharama nafuuu.

Ushindani wa tovuti mtandaoni nao umepelekea kuwepo kwa ongezeko kubwa la ukuaji wa ubashiri mitandaoni, kwa kumrahisishia mchezaji kushinda na sio kukosa, hilo nalo limekuwa ni sababu kubwa kabisa. Kutoa dondoo za ubashiri kila mara, maboresho ya odds pia yamefanya watu wengi kushiri katika michezo hii ya kubashiri kwa lengo kubwa la kujitengenezea kipato ili kujikimu kimaisha.

Kuwa  na tovuti  bora mitandaoni za vidokezo vya utabiri wa mpira nchini Tanzania, na zinazofanya kazi masaa 24 kwa siku, siku saba (7) kwa wiki, zinakupa vidokezo na dondoo za ubashiri wa mpira wa miguu mtandaoni. Na pia zinazo zingatia ligi kuu zote za mpira wa miguu duniani kote zinazo chambua na kuleta dondoo za ubashiri wenye faida!

Dondoo za Utabiri unaoendana na wakati wa sasa kuhusu mpira wa miguu unatafitiwa kwa uangalifu, kuchambuliwa na kupitishwa kwako – ikiwa ni rahisi  kabisa kwa mchezaji kucheza na kujishindia mkwanja. Ukuaji pia umetegemea zaidi na ubora wa Makampuni katika kumrahisishia mchezaji kucheza pasipo kuangaika kwani taarifa na matokeo ya mechi utolewa mara kwa mra.



Share:

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE VIWANDA, BIASHARA NA MAZINGIRA YAIAGIZA TBS KUENDELEA KUBORESHA UTOAJI WA HUDUMA

 

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Prof. Kitila Mkumbo akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali yanayohusu TBS wakati wa semina ya kujenga uelewa na uwasilishaji taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira Bungeni Dodoma Mei 18,2021.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Dkt. Yusuph Ngenya akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya TBS kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira Bungeni Dodoma Mei 18,2021.

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe akijibu hoja mbalimbali zinazohusu Shirika la Viwango Tanzania (TBS) wakati wa semina ya kujenga uelewa kuhusu TBS kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira Bungeni Dodoma Mei 18,2021.

Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira Mhe. Askofu Josephat Gwajima akichangia hoja zinazohusu Shirika la Viwango Tanzania (TBS) wakati wa semina ya kujenga uelewa kuhusu TBS kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira Bungeni Dodoma Mei 18,2021.

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Prof. Kitila Mkumbo akijibu hoja mbalimbali zinazohusu Shirika la Viwango Tanzania (TBS) wakati wa semina ya kujenga uelewa kuhusu TBS kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira Bungeni Dodoma Mei 18,2021.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira Mhe. David Mwakiposa Kihenzile akiongoza semina ya kujenga uelewa na uwasilishwaji wa taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira Bungeni Dodoma, Mei 18,2021.

Meneja Udhibiti Ubora wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Bw. Gervas Mwanjabala akijibu maswali na hoja zilizoulizwa na wanakamati wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira wakati wa semina ya kujenga uelewa kuhusu TBS ,Bungeni Dodoma Mei 18,2021

.

Picha zote na Eliud Rwechungura


Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira imeliagiza Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kuendelea kuboresha utoaji wa huduma na utoaji wa elimu kwa wajasiliamali ili waweze kuzalisha bidhaa zenye ubora zitakazoendana na kuendana na kasi ya ukuaji wa viwanda na kuwezesha biashara shindani nchini.

Hayo yalisemwa leo na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda Biashara na Mazingira Mhe. David Kihenzile(Mb) wakati wa semina iliyolenga kuwajengea uelewa wajumbe wa Kamati hiyo kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Shirika hilo iliyofanyika leo tarehe Mei 18,2021 katika ukumbi wa Bunge jijini Dodoma.

Naye, Waziri wa Viwanda na Biashara. Mhe. Prof Kitila Mkumbo (Mb) wakati akijibu hoja, maoni na mapendekezo ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira alisema Serikali imeendelea kuiwezesha TBS kuboresha utoaji wa huduma zake.

Nao, Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda Biashara na Mazingira walitoa maoni na mapendekezo mbalimbali yaliyolenga kuboresha huduma na bidhaa zinazotolewa na TBS na utoaji wa elimu kwa umma kuhusu huduma hizo.

Maoni hayo yalijumuisha uboreshaji wa huduma ya ukaguzi wa magari yanayoingia nchini, udhibiti wa ubora wa chakula hususani nyama na nafaka, upimaji wa bidhaa zenye GMO zinazoingia nchini, vinasaba vya mafuta na utoaji wa nembo za ubora wa bidhaa mikoani ili kusogeza huduma hizo kwa wananchi katika maeneo husika.

Akiwaelimisha Wajumbe wa Kamati hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa TBS Dkt Yusuph Ngenya alisema TBS imepitia na kupunguza mchakato wa muda unaotumika kuandaa viwango ili kuendana na kasi ya ukuaji wa viwanda na kuwezesha biashara nchini.

Naye Meneja Udhibiti Ubora, Bw. Gervas Mwanjabala wakati akiwasilisha taarifa kwa Wajumbe wa Kamati hiyo, alisema TBS ina maabara tisa (9) zilizopo katika ofisi za Makao Makuu ya Shirika, Ubungo Dar es Salaam. Kati ya maabara tisa (9), maabara saba (7) zimehakikiwa na kupatiwa vyeti vya umahiri au ithibati (Accreditation), maabara hizo ni pamoja na Maabara ya Ugezi, Maabara ya Kemia ya Chakula, Maabara ya Maikrobaiolojia; Maabara ya Kemikali; Maabara ya Uhandisi Ujenzi; Maabara ya Uhandisi Mitambo; na Maabara ya Uhandisi Umeme

Aidha, Meneja huyo alisema kuwa TBS inaendelea kuboresha utoaji wa huduma kwa kutumia TEHAMA ili ziendane na wakati na kukidhi mahitaji ya wateja na inampango wa muda mfupi wa kuingia makubaliano na Maabara ya Taifa ya Udhibiti Ubora wa Samaki (NFQCL), Chuo cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela, Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA), Shirika la Utafiti wa Maendeleo ya Viwanda (TIRDO) na Maabara ya Maji Mwanza ili kukidhi ongezeko la uhitaji wa huduma za uchunguzi wa usalama na ubora wa bidhaa hasa za chakula

Shirika la Viwango Tanzania (TBS) lilianzishwa kwa juhudi za Serikali kama sehemu ya jitihada ya kuimarisha Miundombinu ya sekta ya Viwanda na Biashara ili kukuza uchumi wa Taifa. TBS ilianzishwa kwa Sheria ya Bunge Na. 3 ya Mwaka 1975 na kuanza rasmi tarehe 16 Aprili 1976 ambapo ilipewa jukumu la kuratibu uandaaji wa viwango na kusimamia utekelezaji wake.

Aidha, TBS iliongezewa uwezo mkubwa wa kusimamia shughuli za utayarishaji wa viwango na udhibiti wa ubora wa bidhaa kupitia Sheria ya Viwango Na.2 ya Mwaka 2009. Kufuatia mabadiliko ya Sheria ya Fedha Na.8 ya Mwaka 2019, Shirika liliongezewa majukumu mapya ya kusimamia usalama na ubora wa bidhaa za chakula na vipodozi

Share:

Waziri Wa Nishati Amewahimiza Wenye Viwanda Kuchangamkia Fursa Ya Matumizi Ya Gesi Asilia


Serikali kupitia Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), imetenga kiasi cha shilingi bilioni 28 kwa ajili ya uzalishaji wa gesi asilia kwenye viwanda ili kupunguza gharama za uzalishaji viwandani pamoja na matumizi ya majumbani.

Hayo yamebainishwa  Tarehe 18/05/2021 Wilayani Kibaha Mkoani Pwani na Waziri wa Nishati Mh. Dk.Merdard Kalemani wakati wa ziara ya kutembelea kiwanda cha BM Motors cha utengenezaji wa magari na kiwanda cha Kairuki Pharmacetical Industries cha utengenezaji wa dawa vilivyopo eneo la viwanda la Zegereni.

Dk.Kalemani alisema kuwa Tanzania ina kiasi cha gesi futi za ujazo tirioni 1.8 kwa ajili ya matumizi ya viwanda ambapo wanatarajia viwanda kuanza kutumia gesi ambayo itapunguza gharama za nishati ya umeme na kufanya bidhaa kuuzwa kwa bei nafuu.

“Nasisitiza viwanda vitumie gesi asilia maana matumizi yako chini sana ikilinganishwa na gesi iliyopo mpaka sasa hata tirioni 1 ya matumizi ya gesi haijafika,” alisema Dk.Kalemani.

Alisema kuwa pamoja na matumizi ya gesi asilia majumbani na kwenye magari bado matumizi yako chini sana ambapo kiasi cha gesi asilia ni futi za ujazo trilioni 57.5 na ipo ya kutosha hivyo wenye viwanda wajenge miumndombinu itakayotumia gesi kwenye viwanda vyao.

Dk. Kalemani ameliagiza Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC )kumaliza majadiliano ili baada ya miezi miwili au mitatu ujenzi uanze na kukamilika mwishoni mwa mwaka ili matumizi ya gesi asilia viwandani yaanze ili kuboresha upatikanaji wa Nishati ya umeme.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Biashara ya Mafuta na Gesi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Dk.Wellington Hudson alisema TPDC inatarajia kujenga vituo vitano vya (CNG) Compressed Natural Gas ambapo mojawapo ya kituo kitakuwa Kairuki Phamacetical Zegereni wilayani Kibaha mkoani Pwani.

Dk.Hudson aliendelea kusema kuwa gesi itakayotumika itakuwa kwenye mfumo wa kugandamizwa Compressed Natural Gas (CNG) ambapo mfumo huo utaweza kufikisha gesi mapema kwenye eneo hilo la viwanda wakati utaratibu wa mpango wa kujenga bomba ukiratibiwa.

“Katika kuhakikisha maeneo ya viwanda yanafikiwa na miundombinu ya usambazaji wa gesi asilia TPDC imewasiliana na uongozi wa mkoa wa Pwani na kupatiwa orodha ya viwanda vilivyoko Zegereni na Visiga ambapo mpango uliopo ni kuwapeleka wataalamu kutembelea viwanda hivyo ili kupata mahitaji ya nishati ya kila kiwanda na kuanisha mahitaji ya jumla ya miundombinu ya usambazaji wa gesi asilia,”alisema Hudson.

Alisema kuwa katika mwaka wa fedha 2020/2021 Serikali kupitia TPDC imetenga fedha kwa ajili ya miundombinu ya CNG ambapo ujenzi huo utahusisha ujenzi wa vituo vikuu viwili Dar es Salaam pamoja na vituo vitatu vya kupokelea gesi na kusambazwa kwa wateja wa mwisho ambao ni viwanda, magari, wazalishaji wa umeme na majumbani.

“Utekelezaji wa mradi wa CNG upo katika hatua za manunuzi ya wakandarasi wa ujenzi ili kazi ya ujenzi iweze kuanza na hatua hii imefikiwa baada ya kukamilisha usanifu wa mradi (Detailed Engineering Designs) mwezi Septemba mwaka 2020,”alisema Hudson.

Aidha alisema kuwa zabuni zilitangazwa Machi 30 mwaka 2021 na siku ya mwisho ya kupokea zabuni katika mfumo wa TANeps ni Mei 18 mkandarasi anatarajiwa kupatikana mwishoni mwa mwezi Juni na shughuli za ujenzi zinatarajiwa kukamilika Machi 2022.


Share:

Rais Samia ashiriki mkutano wa Wakuu wa Nchi na Mashirika ya Kimataifa kujadili namna ya kuokoa uchumi wa Afrika.



Share:

Waziri Kalemani Atoa Siku 10 Wakandarasi Kuanza Utekelezaji Mradi Wa Kumalizia Vijiji Visivyo Na Umeme


 Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Medard Kalemani ametoa muda wa siku 10 kwa wakandarasi walioshinda zabuni za kutekeleza Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme vijijini Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili kuanza kazi ya ujenzi wa miundombinu ya kusambaza umeme.


Waziri Kalemani alitoa agizo hilo tarehe 17/05/2021 wakati akizndua Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili katika Kijiji cha Mpakali kilichopo Wilaya ya Mbogwe katika Mkoa wa Geita.


Dkt. Kalemani alisema Serikali imetenga Shilingi bilioni 75.6 kwa ajili ya kupeleka umeme katika vijiji 97 ambavyo havina umeme katika Mkoa wa Geita. “Vijiji vyenye umeme ni 377 kati ya vijiji 474 n katika Wilaya ya Mbogwe vijiji visivyo na umeme ni 33 na tumewaletea mkandarasi atakayekamilisha kazi ya kupeleka umeme katika vijiji hivyo” alisema.


Aidha, alisisitiza kuwa Serikali imetoa muda wa miezi 18 kwa wakandarasi wanaotekeleza miradi ya kusambaza miundombinu ya umeme vijijini na kuwa muda huo hautaongezwa. Aliwataka REA kuwasimamia wakandarasi wakamilishe miradi kwa wakati kwa mujibu wa mikataba.


Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe, Martha MKupasi alisema kuwa Umeme ni nishati muhimu ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi na kuwa itasaidia katika kuboresha utoaji wa huduma za kijamii kama vile afya na elimu.


Naye Mbunge wa Jimbo la Mbogwe, Mhe. Nicodemus Maganga alisema kuwa upatikanaji wa nishati ya umeme katika jimbo hilo utafungua fursa ya uwekezaji wa viwanda vya kusindika mpunga, dengu na karanga ambazo zinalimwa ukanda huo.



Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger