Monday, 3 May 2021
Sunday, 2 May 2021
CHANGAMOTO YA UPOTEVU WA MAZAO YA UVUVI YAANZA KUPATIWA MAJIBU
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega akizungumza na wanakijiji cha Songosongo kilichopo Wilaya ya Kilwa Mkoani Lindi, wakati wa hafla fupi ya kukabidhi kituo cha kuzalisha barafu kilichojengwa na Mfuko wa Uhifadhi wa Mazingira Duniani (WWF), kwa ufadhili wa Climateworks Foundation na kuipongeza WWF kwa kuyafanyia kazi maono ya serikali ya kuhifadhi mazao ya uvuvi ambayo yamekuwa yakiharibika kutokana na kukosekana kwa nyenzo za kuyahifadhi ikiwemo barafu.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (kushoto) akipeana mkono na Mkurugenzi Mkazi wa Mfuko wa Uhifadhi wa Mazingira Duniani (WWF), kwa Tanzania, Dkt. Amani Ngusaru mara baada ya Dkt. Ngusaru kuzungumzia mradi wa miaka miwili wa WWF katika kijiji cha Songosongo kilichopo Wilaya ya Kilwa Mkoani Lindi, uliowezesha kupatikana Tani 91,000 za samaki aina ya pweza zenye thamani ya Shilingi Milioni 458, wakati wa hafla fupi ya kukabidhi kituo cha kuzalisha barafu kijijini hapo.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI) Dkt. Ishmael Kimirei akizungumza na wanakijiji cha Songosongo (hawapo pichani) kilichopo Wilaya ya Kilwa Mkoani Lindi, wakati wa hafla fupi ya kukabidhi kituo cha kuzalisha barafu kilichojengwa na Mfuko wa Uhifadhi wa Mazingira Duniani (WWF), kwa ufadhili wa Climateworks Foundation na kuwaasa wanakijiji hao kuhakikisha uvunaji wa samaki aina ya pweza unakuwa endelevu na kutumia vyema kituo hicho ili kiwe na tija katika kuzuia upotevu wa mazao ya uvuvi.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (kushoto) akimshuhudia Mkurugenzi Mkazi wa Mfuko wa Uhifadhi wa Mazingira Duniani (WWF), kwa Tanzania, Dkt. Amani Ngusaru na viongozi wa Halmashauri ya Wilaya na Kijiji cha Songosongo katika utiaji saini wa makabidhiano ya kituo cha kuzalisha barafu kilichopo Kijiji cha Songosongo Wilaya ya Kilwa Mkoani Lindi, wakati wa hafla fupi ya kukabidhi kituo hicho.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega akiwasha moja ya mitambo ya kuzalisha barafu ikiwa ni ishara ya kuanza rasmi kutumika kwa kituo cha kuzalisha barafu kilichojengwa na Mfuko wa Uhifadhi wa Mazingira Duniani (WWF), kwa ufadhili wa Climateworks Foundation katika Kijiji cha Songosongo kilichopo Wilaya ya Kilwa Mkoani Lindi, wakati wa hafla fupi ya kukabidhi kituo hicho.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega akiangalia ubora wa barafu iliyozalishwa na moja ya mitambo iliyopo kwenye kituo cha kuzalisha barafu katika kijiji cha Songosongo kilichopo Wilaya ya Kilwa Mkoani Lindi. Kushoto kwake ni Mkurugenzi Mkazi wa Mfuko wa Uhifadhi wa Mazingira Duniani (WWF) Dkt. Amani Ngusaru ambapo kituo hicho kimejengwa na WWF kwa ufadhili wa Climateworks Foundation.
Muonekano wa kituo cha kuzalisha barafu kilichopo Kijiji cha Songosongo Wilaya ya Kilwa Mkoani Lindi, kilichojengwa na Mfuko wa Uhifadhi wa Mazingira Duniani (WWF), kwa ufadhili wa Climateworks Foundation kwa thamani ya Shilingi Milioni 424 na kina uwezo wa kuzalisha barafu Tani 1.4 kwa saa 24.
NABII JOSHUA AMSHUKURU MUNGU KUEPUSHA KIMBUNGA JOBO TANZANIA
PASTA AGEUZA BAA 'NIGHT CLUB' KUWA KANISA MARIDADI LA KUABUDIA
TBS YAKUTANA NA WADAU ZAIDI YA 300 WA MCHELE KANDA YA ZIWA...YAWAPA SIRI YA VIWANGO, UBORA NA USALAMA WA BIDHAA
SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limewataka wajasiriamali wanaojihusisha na usindikaji, uchakataji, ufungashaji na uuzaji wa mchele kulipa uzito suala la viwango, ubora na usalama wa bidhaa ili kuweza kuongeza tija.
Wito huo ulitolewa juzi (Ijumaa) na Meneja Mafunzo na Utafiti wa TBS, Hamisi Sudi Mwanasala, wakati akifungua mafunzo kwa wajasiriamali wanaojihusisha na usindikaji, uchakataji, ufungashaji na uuzaji wa mchele katika Wilaya ya Sengerema, mkoani Mwanza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo, Dkt. Yusuf Ngenya.
Mafunzo hayo yaliyoanza Aprili 27, mwaka huu yamefanyika katika wilaya nne kwa nyakati tofauti za Kahama, Bukombe, Katoro, wilayani Geita na kuhitimishwa Sengerema. Mafunzo hayo yametolewa kwa washiriki zaidi ya 300 katika wilaya hizo.
Katika mafunzo hayo washiriki walipewa elimu kuhusu TBS na majukumu yake, kanuni bora za uzalishaji, matakwa ya viwango, namna bora ya uhifadhi, ufungashaji na teknolojia ya vifungashio na taarifa za msingi kwenye vifungashio.
Aidha, Sudi alisema washiriki hao walielimishwa juu ya taratibu za usajili wa bidhaa za vyakula, vipodozi na majengo, kazi ambazo hapo awali zilikuwa zikifanywa na iliyokuwa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA).
Kwa mujibu wa Sudi, Shirika hilo limeandaa mafunzo hayo ikiwa ni utekelezaji wa makubaliano ya kikao kilichofanyika Sirari,mkoani Mara, ambacho kiliridhia TBS,itoe mafunzo kwa wajasiriamali wanaosindika, kuzalisha, kufungasha na kuuza mchele katika kanda nzima ya Ziwa.
Alisema wametiwa moyo na mwitikio na ushirikiano mzuri walioupata katika Wilaya zote Kahama,Bukombe,Sengerema na mji mdogo Katoro Geita wakati wa maandalizi ya mafunzo haya.
Alisisitiza kwamba mafunzo hayo ni uthibitisho wa azma ya Serikali katika kufanikisha malengo ya Tanzania viwanda.
"Na kwa sababu hiyo tuliona muelekeo mzuri wa usimamizi wa Serikali ya awamu ya tano ambao umeweza kututoa katika uchumi wa chini na sasa tumeingia uchumi wa ngazi ya kati na Awamu ya Sita Kazi inaendelea," alisema.
Alitoa wito kwa waliopata mafunzo hayo waweze kuyatumia watakaporejea kwenye shughuli zao. Aliahidi kuwa TBS itaendelea kutoa mafunzo ya namna hiyo kwa wazalishaji, wauzaji na wadau wote wa mchele.
Wakizungumzia mafunzo hayo, washiriki waliipongeza TBS kwa kutoa mafunzo hayo hasa kwa kuzingatia kwamba yametolewa wakati muafaka wa mavuno ya mpunga. Wametoa wito kwa shirika hilo kuhakikisha mafunzo hayo yanakuwa endelevu.
JAMAA ANUSURIKA KIFO KWA KUANGUKIWA MTI AKIJISAIDIA
SUPER – NHESHA: Dawa Bora Ya Kutibu Tatizo La Kisukari
Ni dawa ya kutibu tatizo la sukari au jina la kitaalamu (Diabetes Mellitus) ni kundi la magonjwa yanayohusiana na ufanyaji kazi wa mwili ambapo Mtu anakuwa na kiwango kikubwa cha sukari aina ya Glucose katika mwili kutokana na mwili wake kukosa uwezo wa kutengeneza Insulin ya kutosha au seli za mwili wake kutumia insulin iliyopo au pengine mwili kuwa na matatizo yote kwa pamoja na kupelekea mgonjwa wa sukari kupata haja ndogo mara kwa mara (Polyuria) uhisi kiu kila wakati (Polydipsia) Na (Polyphagia).
AINA YA KISUKARI
Kuna aina chache tofauti za ugonjwa wa kisukari (1) ni ugonjwa wa Auto hii aina mgonjwa wa Auto hushambulia mfumo wa kinga na kuharibu seli katika kongosho ambako insulin huzalishwa asilimia 10% ya watu wenye ungonjwa wa kisukari wanayo aina hii (Auto).
AINA YA PILI
Hii hutokea wakati mwili wako unakuwa sugu kwa insulin na sukari hujenga katika damu yako hii husababishwa na kuwa na sukari nyingi kwenye damu yako kuliko kawaida.
CHANZO CHA UGONJWA SUKARI
Viko vyanzo vingi mbalimbali vya sukari
1. Shinikizo la damu (B.P)
2. Viwango vya juu vya triglyceride (mafuta)
3. Lishe yenye mafuta mengi na wanga
4. Utumiaji mkubwa wa pombe kupita kiasi
5. Ulaji wa vyakula vyenye sukari nyingi
6. Mtindo wa maisha usiofaa kiafya
7. Uzito na unene uliozidi
8. Kutofanya mazoezi
9. Umri
10. Kurith
UNAJUAJE KUWA UNADALILI ZA KISUKARI
1. Kusikia njaa mara kwa mara
2. Kusikia kiu mara kwa mara
3. Kupungua uzito
4. Maono machafu
5. Uchovu mara kwa mara
6. Ukipata kidonda hakiponi
7. Kushuka kwa kinga mwili
DALILI ZA KISUKARI KWA MWANAUME
Mbali na dalili za jumla za ugonjwa wa sukari wanaume wenye tatizo hilo wanakuwa na upungufu wa nguvu za kiume na kushindwa kufanya tendo la ndoa uume hushindwa kusimama misuri hulegea na kusinyaa, maumivu ya mgongo, kiuno, tumbo kujaa gesi na kuunguruma, kupata choo kama cha mbuzi
DALILI ZA WANAWAKE
Wanawake wenye ugonjwa wa sukari wanaweza pia kuwa na dalili kama vile maambukizi kwa njia ya mkojo (U.T.I) maambukizi ya gonzi kukakamaa
TIBA YA MAGONJWA YA SUKARI
Ugonjwa wa sukari unatibika bila kujali ni mda gani umepata hilo tatizo wengi wamekata tama na kuwa wabishi amini tatizo hili linatibika vizuri sana wengi wemepona.
Tumia dawa ya SUPER-NHESHAambayo ni dawa ya miti shamba yaani (asilia) ambayo humfanya mtu kupona na kuimalika kabisa.
Tutakuelekeza pia mfumo wa mtindo wa maisha utakao takiwa kutumia ili kutoluhusu tatizo hilo kurudi tena.
BABU MADUHU ANAPATIKANA MAGOMENI MOROCCO/KANISANI NJIA PANDA YA KWENDA SINZA SIMU: 0652 102 152/0788 330 105/ 0755 684 297 NYOTE MNAKARIBISHWA PIA TUNATUMA MIKOANI WHATAPPS NO 0652 102 152
Watahiniwa 90, 025 Kidato cha Sita Kuanza Mitihani ya Kesho
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) Dkt. Charles Msonde, amesema kuwa mitihani ya kidato cha sita Tanzania Bara na Visiwani itaanza kesho Mei 3 hadi Mei 25, 2021.
Taarifa hiyo ameitoa hii leo Mei 2, 2021, jijini Dar es Salaam na kuongeza kuwa licha ya mitihani hiyo pia itafanyika mitihani ya ualimu, ambapo vituo katika shule za sekondari ni 804, vituo vya watahiniwa wa kujitegemea 248 na kwa upande wa vyuo vya ualimu viko 75 kwa Tanzania Bara na Zanzibar.
"Jumla ya watahiniwa 90, 025 ndiyo waliosajiliwa kufanya mtihani huo wa kidato cha sita na kati yao watahiniwa wa shule wako 81,343 na wakujitegemea wako 8,682, na kati ya watahiniwa hao wa shule wanaume ni 46,233 na wanawake 35,110", ameeleza Dkt. Msonde
Bunge La Somalia lapiga kura kumfutia Rais muda wa nyongeza
Wabunge wa Somalia wamepiga kura kwa kauli moja kufuta nyongeza ya miaka miwili kwenye muhula wa rais Mohamed Abdullahi Mohamed waliyoidhinisha mwezi uliopita baada ya kuzuka mvutano mkubwa kuhusu suala hilo.
Zoezi la kura hiyo lilirushwa moja kwa moja na televisheni nchini humo na lilifanyika muda mfupi baada ya rais Mohammed kulihutubia bunge na kutangaza nia ya kuitisha uchaguziwa bunge uliocheleweshwa.
Mgogoro wa kisiasa umeibua wasiwasi kuwa Waasi wa Al Shabaab wanaweza kutumia nafasi hiyo kuhatarisha hali ya usalama ikiwa Vikosi vya Serikali vitagawanyika.
Watu 60,000 hadi 100,000 walilazimika kukimbia makazi yao kufuatia mapigano ambayo yalichochea hofu ya vita kati ya vikundi vinavyomuunga mkono Rais na vinavyompinga.
Korea Kaskazini yapuuza pendekezo la kufanya mazungumzo na Marekani
Korea Kaskazini imepuuza wazo la kufanya mazungumzo na Marekani siku moja baada ya utawala mjini Washington kusema uko tayari kwa majadiliano ya kidiplomasia kuhusu Pyongyang kuachana na mradi wake wa nyuklia.
Wizara ya mambo ya kigeni ya Korea Kaskazini imesema haiko tayari kufanya mazungumzo na taifa linalotumia diplomasia "bandia" kuficha matendo yake ya uchokozi.
Taifa hilo pia limemtahadharisha Rais Joe Biden wa Marekani dhidi ya kuchukua kile imekitaja kuwa "msimamo uliopitwa na wakati" na kuonya kuwa Washington itapata madhara kwa kuichokoza Korea Kaskazini.
Matamshi kutoka Pyongyang yanatolewa siku kadhaa tangu rais Biden alipoliambia bunge la Marekani kuwa utawala wake utatumia diplomasia pamoja na msimamo usioyumba kudhibiti malengo ya nyuklia ya Korea Kaskazini.
DW
Vijana Wahimizwa Kujiamini Na Kujitambua Kupambana Na VVU /UKIMWI
Mwandishi Wetu Dodoma
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii) Dkt. John Jingu, amewataka Vijana balehe hususani wasichana kujitambua na kujiamini kuwa wao ni nyezo muhimu ya Kupambana na changamoto za maisha ikiwemo maambukizi ya Virusi vya Ukimwi
Dkt. Jingu ametoa rai hiyo jijini Dodoma wakati akifunga Mkutano wa mwaka wa wadau wanaotekeleza Afua za VVU na Ukimwi zinazolenga wasichana balehe na wanawake Vijana.
"Naomba wasichana mjitambue na kujiamini kwani ni nyenzo muhimu ya kutatua Changamoto zinazoendana na umri wenu.Jiamini unaweza kupambana na changamoto,ukilegea kidogo ukiteleza unaharibu ramani ya maisha yako,"amesema.
Amesema endapo wakijitambua hawatakuwa tayari kurubuniwa itakuwa rahisi kwenu kukataa vishawishi, hakikisheni mnasema hapana na maana ya kusema hapana ni kuepuka marafiki wabaya na wenye ushawishi mbovu, vitu vizuri huwa vinachukua muda msiwe na papara na kikubwa mlinde ndoto zenu msizipoteze.
Katibu Mkuu huyo amevitaka vyuo na shule hapa nchini kuanzisha madawati ya Jinsia ili wanaopata changamoto na kufanyiwa vitendo vya ukatili waweze kufika kwenye madawati hayo na kupatiwa msaada.
Dkt. Jingu pia ametumia fursa hiyo kusisitiza umuhimu wa nguzo Kuu Sita za Ajenda ya kitaifa ya kuwekeza katika Afya ya Maendeleo kwa Vijana Balehe ambazo ni kuzuia maambukizi ya Virusi vya Ukimwi kwa Vijana, kutokomeza mimba katika umri mdogo, kuzuia ukatili wa kimwili na kisaiklojia na kuboresha lishe miongoni mwa vijana Balehe.
Nguzo nyingine ni kuhakikisha watoto wanapelekwa shule na kumaliza masomo yao na kuwawezesha Vijana Balehe kupata fursa za kiuchumi kwa kuajiriwa na kuajiriwa.
Pia Dkt.Jingu amewataka vyuo na shule kuwajengea uwezo vijana ili kukabiliana na changamoto huku alisisitiza mashirika Yasiyo ya Kiserikali na Taasisi mbalimbali kuendelee kulilinda na kulisaidia kundi hili na kikubwa tuwekeze kwenye uwekezaji kiuchumi.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania Dkt. Leonard Maboko amesema ni nia ya Serikali kufikisha Afua za mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI kwa kuwezesha vijana kupata fursa za mitaji na ajira ili kuondokana na changamoto za kukubana na vishawishi.
Dkt. Masoko amefafanua kuwa maabukizi ya Ukimwi kitaifa ni wastani wa asilimia 4.7 kiwango alichosema kitapungua kwa kuwalinda vijana walio katika umri hatarishi.
Amesema asilimia 40 ya watu wenye maambukizi ya VVU ni vijana kati ya umri wa miaka 15 na 24 na asilimia 80 vijana hao ni wasichana.
Naye mmoja wa wawakilishi wa Wasichana Balehe na Wanawake Vijana Mariana Mathias kutoka Mkoani Mbeya ameishukuru Serikali na wadau kuja na afua mbalimbali zinazolenga kuwasaidia Wasichana Balehe na Wanawake Vijana katika kuoambana na maambukizi ya VVU na UKIMWI kwani imewasaidia vijana wengi akiwemo yeye kujiamini na kujitambua.
“Mimi ni mfano niliwezeshwa kutoa elimu ya fani ya urembo na kupewa vifaa wezeshi vinavyonisaidia kuendesha maisha yangu ya kila siku na hata kuendesha maisha ya familia yangu” alisema Mariana
Mwisho