Sunday, 8 November 2020

FULL POWER, ZATI 50 NI KIBOKO YA TATIZO LA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME NA UUME MDOGO

Zati 50
Full Power
Sababu za upungufu wa nguvu za kiume na maumbile madogo ya uume:

⇒Ngiri,

⇒Henia

⇒Kisukari

⇒Tumbo kujaa gesi

⇒Kutopata choo vizuri

⇒Utumiaji madawa kwa muda mrefu

⇒Unywaji wa pombe kupita kiasi

⇒Msongo wa mawazo 

⇮⇒Haya yote hupelekea mwili kutokuzalisha homoni ya gesrtogine au kuwa chache na kushindwa kupata mzunguko mzuri wa damu na vichocheo vingine kama madini ya zinki ambayo hukufanya kuwa na msisimko  na kufanya kuwa na muda  mrefu na nguvu za kutosha.

FULL POWER

⇨Ni dawa ya vidonge ya miti shamba inaongeza nguvu za kiume na kutibu kabisa tatizo hilo.

⇨Inaongeza hamu ya tendo la ndoa

⇨Inakufanya uchelewe kufika kileleni zaidi ya Dakika 30 na kurudia tendo zaidi ya mara nne na zaidi.

Zati 50

⇨ Inarutubisha maumbile ya uume  na kunenepesha urefu nchi 6,unene sentimita 4

⇨Dawa hii ni ya kutibu kabisa tatizo hilo.

Pia tunatibu Magonjwa mengine Kama

Matatizo ya pumu,Bawasiri, vidonga vya tumbo,Kisukari,Magonjwa sugu ya zinaa,Kaswende,U.T.I , kiuno,miguu kuwaka moto, Fangasi sehemu za Siri, kupunguza unene wa mwili,tumbo kuunguruma,kujaa gesi, matatizo ya uzazi kwa wanawake, kurutubisha mbegu za uzazi kwa akina baba, matatizo ya meno tunatibu bila kungoa

Kliniki yetu inapatikana Zanzibar, Dar es salaam na Shinyanga.

Wasiliana nasi kwa simu namba 071770 22 27
Share:

Joe Biden Ashinda Urais wa Marekani

Hatimaye na baada ya siku nne za vuta nikuvute, vyombo vya habari vya Marekani vimetangaza kuwa mgombea urais kwa tiketi ya chama cha Democratic, Joe Biden ndiye aliyechaguliwa na Wamarekani kuwa rais wa 46 wa nchi hiyo.

Ripoti zinasema kuwa Biden ameshinda kura 290 za wajumbe wa Electoral College baada ya kumpiku mpinzani wake, Donald Trump katika majimbo ya Pennsylvania na Nevada. Biden alihitajia kura 270 tu  kati ya 538 za wajumbe wa Electoral College ili atangazwe mshindi.

Timu ya kampeni za uchaguzi ya Donald Trump imesema bado ni mapema kumtangaza Joe Biden kuwa mshindi wa uchaguzi wa rais wa tarehe 3 Novemba na kusisitiza kuwa, itawasilisha mashtaka mahakamani dhidi ya jinsi zoezi la uchaguzi wa rais wa Marekani lilivyofanyika. 

Hata hivyo, kwa kutilia maanani ufa na tofauti kubwa iliyopo baina ya kura za wananchi na zile za wajumbe wa Electoral College za washindani hao wawili ni vigumu sana kuona matokeo yaliyotangazwa na vyombo vikuu vya habari vya Marekani yakibadilika kwa maslahi ya Donald Trump. 

Hivyo, tunaweza kusema kuwa, Biden ndiye atakayeshika hatamu za uongozi wa Marekani tarehe 20 Januari mwakani baada ya kipindi cha Donald Trump kumalizika rasmi.

Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili Novemba 8

Share:

Saturday, 7 November 2020

JOE BIDEN ASHINDA UCHAGUZI URAIS MAREKANI...TRUMP OUT

Joe Biden ameshinda uchaguzi wa Marekani na kuwa rais mteule wa Marekani baada ya kumshinda Donald Trump.

Bw. Biden ameshinda katika jimbo muhimu la Pennsylvania, akijizolea kura zaidi ya 270 zilizohitajika ili kunyakua kiti cha White House.

Kampeni ya Trump imeonesha mgombea wao hana mpango wa kukubali matokeo ya uchaguzi huo.

Matokeo hayo yanamfanya Trump kuwa rais wa kwanza kutumikia awamu moja madarakani tangu miaka ya 1990.

Uchaguzi huu umeshuhudia watu wengi wakijitokeza kupiga kura tangu miaka ya 1900. Bwana Biden ameshinda zaidi ya kura milioni 73 mpaka sasa, idadi ya juu kuwahi kutokea kwa mgombea yoyote yule Marekani. Trump akipata kura zaidi ya milioni 70 akishika nafasi ya pili kwa idadi kubwa katika historia ya Marekani.

Rais Trump alijitangaza mshindi wa uchaguzi wakati kura zikiendelea kuhesabiwa. Wakati wote amedai kuwa zoezi la kuhesabu kura limekuwa na dosari, lakini hajawasilisha ushahidi wowote kuhusu madai yake.

Kampeni yake imefungua kesi katika majimbo mbalimbali mapema Ijumaa, wakati Biden alipokuwa akikaribia kunyakua ushindi, alisema : ''uchaguzi huu haujakwisha.''

Chanzo -BBC Swahili
Share:

SIMBA, YANGA WATUNISHIANA MISULI

Mchezo kati ya Yanga na Simba umemalizika katika Uwanja wa Mkapa  kwa timu hizo kutoka sare ya kufungana bao 1-1

Share:

CCM yawapitisha Ndugai, Dk. Tulia kuwania Uspika

Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimeteua majina mawili ya wanachama wake, watakaogombea Uspika na Naibu Spika wa Bunge la 12 la Tanzania.

Pia, chama hicho, kimeteua jina moja la mwanachama wa chama hicho kuwania Uspika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.

 Uteuzi huo umefanywa na kikao cha kamati kuu ya CCM kilichokutana juzi Alhamisi jijini Dodoma tarehe 5 Novemba 2020 chini ya Mwenyekiti wa chama hicho, Rais John Magufuli.

Walioteuliwa ni; Job Ndugai kuwa mgombea Uspika na Dk. Tulia Ackosn kugombea Naibu Spika wa Bunge  la Tanzania.

Share:

POLISI, ZIMAMOTO WACHUNGUZA MOTO WA AJABU KAHAMA MJINI ..."UNAJIWASHA NA KUUNGUZA MAGODORO"

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP, Debora Magiligimba akizungumza na waandishi wa habari leo Jumamosi Novemba 7,2020 akitoa taarifa kuhusu matukio mbalimbali yaliyojiri mkoani Shinyanga. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP, Debora Magiligimba akizungumza na waandishi wa habari leo Jumamosi Novemba 7,2020 akitoa taarifa kuhusu matukio mbalimbali yaliyojiri mkoani Shinyanga.

 Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Umesikia kuhusu ile taarifa ya moto wa ajabu unaojiwasha na kuunguza magodoro,nguo na mito ya makochi ya watu Mjini Kahama??.... Sasa Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga kwa kushirikiana na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wanafanya uchunguzi kuhusu tukio hilo katika kitongoji cha Hongwa mtaa wa Shunu Mjini Kahama ambalo limezua gumzo.

Habari kutoka eneo la tukio zinasema ,moto huo wa ajabu unaohusishwa na imani za kishirikina umekuwa ukiunguza vitu vya ndani ya nyumba pekee kwenye nyumba ambazo hazina umeme tena nyakati za mchana tu. 

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari leo, Novemba 7,2020 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, ACP Debora Magiligimba amesema Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na jeshi la Zimamoto na Uokoaji wanaendelea na uchunguzi kuhusu tukio hilo la moto kutokea na kuharibu mali nyumbani kwa Joseph Kioja Dida na majirani zake 8 katika mtaa wa Shunu Mjini Kahama. 

Akisimulia kuhusu tukio hilo, Kamanda Magiligimba amesema mnamo Novemba 4,2020 majira ya saa mbili kamili usiku Joseph Kioja Dida (34) dereva pikipiki ‘bodaboda’ mkazi wa mtaa wa Shunu Mjini Kahama alifika kituo cha Polisi Kahama na kutoa taarifa kwamba huko nyumbani kwake kwa nyakati tofauti kumekuwa na tukio la kutatanisha la moto. 

“Joseph Kioja Dida alisema moto huo umetoa takribani mara 30 na kuharibu/kuunguza mali mbalimbali za nyumbani hasa magodoro,mito ya makochi,nguo na bidhaa za dukani analomiliki nyumbani kwake tangu mwezi Agosti 2019 hadi sasa. 

Hata hivyo hakuwahi kuripoti polisi wala Zimamoto kutokana na sababu za mazingira na namna moto huo unavyotokea bila kuwashwa na mtu yeyote akiamini kwamba moto huo unatokana na imani za kishirikina mpaka tarehe 04.11.2020 alivyoenda kutoa taarifa kituo cha polisi Kahama”,anasimulia Kamanda Magiligimba. 

Kamanda huyo amesema, Kutokana na moto huo, Joseph Kioja Dida amepata hasara ya vitu mbalimbali kuungua na kuharibika vinavyokadiriwa kuwa na thamani ya jumla ya shilingi Milioni 2. 

“Inasadikiwa kila mtu aliyenunua bidhaa kutoka dukani kwake mara baada ya kufika nyumbani moto huo hutokea na kuunguza bidhaa hizo. Hali hiyo imesababisha wapangaji kuhama kutoka kwenye nyumba yake kwenda kupanga sehemu zingine na watu wengine kuacha kununua bidhaa kutoka dukani kwake”,amesema Kamanda Magiligimba. 

“Hata hivyo pamoja na wapangaji hao kuhama,moto huo umeendelea kutokea nyumbani kwa majirani na kuunguza vitu mbalimbali yakiwemo Magodoro,nguo za watoto,mito ya makochi”,ameongeza. 

Amewataja majirani walioathirika na moto huo kuwa ni Adam Jackson ambapo moto huo uliunguza godoro lenye thamani ya shilingi 150,000/=, Anna Kachwele godoro na nguo za watoto zenye thamani ya shilingi 180,000/=, Benadetha John godoro,mito ya makochi na vitu mbalimbali vyenye thamani ya shilingi Milioni Moja na Emmanuel Bundala, magodoro matatu na nguo za watoto zenye thamani ya shilingi milioni 1 na laki 5. 

Wengine ni Saji Swalehe,godoro na nguo vyenye thamani ya shilingi 180,000/=, Joseph Masoud,godoro lenye thamani ya shilingi 80,000/= na Betri la Solar lenye thamani ya shilingi 50,000=, Teresia Nesphory,godoro na mito vyenye thamani ya shilingi 250,000/= na Laurent Charles, godoro lenye thamani ya shilingi 80,000/=. 

Kamanda Magiligimba amesema uchunguzi wa awali unaonesha kuwa matukio hayo ya moto huo hutokea wakati wa mchana na nyumba hizo hazina umeme. 

Share:

Mkutano Wa Bunge La 12 Kuanza Rasmi Novemba 10,2020 Jijini Dodoma

 KATIBU  wa Bunge Steven Kagaigai  ametangaza kuwa Bunge la 12 kuanza rasmi Novemba 10 mwaka huu jijini Dodoma huku akiwataka wabunge wa kuchaguliwa na kuteuliwa kufika katika ofisi za Bunge wakiwa na nyaraka mbalimbali kwa ajili ya kujisajili.

Wito huo ameutoa leo jijini Dodoma kwa waandishi wa habari jijini Dodoma, Kagaigai  amesema kuwa  kikao hicho kimeitishwa baada ya Tangazo la Rais lililotolewa Novemba 5, mwaka huu kwenye gazeti la serikali toleo maalum namba 942A

Share:

MUUGUZI, DAKTARI MBARONI KWA WIZI WA MASHINE ZA MIL. 26 CHUMBA CHA UPASUAJI HOSPITALI YA RUFAA SHINYANGA

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba sehemu ya vifaa tiba mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni 26 vilivyoibiwa katika Chumba cha Upasuaji katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Shinyanga.

Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga linamshikilia Mtumishi wa Idara ya Chumba cha Upasuaji katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga Madaraka Joseph (32) na Mmiliki wa Suka Wazazi Dispensary, Dk. Suka Charles kwa tuhuma ya wizi wa vifaa tiba zikiwemo mashine za kuangalia wagonjwa zenye thamani ya shilingi milioni 26 katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga. 

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari leo,Jumamosi Novemba 7,2020, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba amesema wizi huo umetokea Oktoba 13,2020 majira ya saa 10 jioni katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Shinyanga. 

Kamanda Magiligimba amesema Oktoba 13,2020 kulitokea wizi wa mashine mbili za kuangalia wagonjwa katika chumba cha upasuaji aina ya EDAN 1M8 na DATA SCOP 1 zenye thamani ya shilingi milioni 26 mali ya Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Shinyanga. 

“Kufuatia tukio hilo, Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga likaanza uchunguzi wake mara moja na kubaini kuwa mtuhumiwa Madaraka Joseph, Muuguzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga na mkazi wa Mageuzi Mjini Shinyanga ambaye ni Mtumishi wa Idara ya Chumba cha Upasuaji ndiye aliyeziiba mashine hizo na kwenda Kuuza kwa Dk. Suka Charles ambaye ni Mmiliki wa Suka Dispensary iliyopo wilayani Kahama ambaye ni mkazi wa Buzuka Mjini Shinyanga na makazi mengine wilayani Kahama”,ameeleza Kamanda Magiligimba. 

“Muuguzi huyo wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, Madaraka Joseph aliuza mashine hizo kwa Suka Charles kwa makubaliano ya Shilingi Milioni 4 ambapo alishatanguliziwa shilingi milioni 2”,amesema Kamanda Magiligimba. 

Kamanda huyo wa polisi amesema baadae Suka Charles alikamatwa na upekuzi ulifanyika nyumbani kwake maeneo ya Mhongolo wilayani Kahama na kufanikiwa kupata mashine hizo (EDAN 1M8 na DATA SCOP 1) zikiwa na vifaa vyake. 

Amevitaja vifaa hivyo kuwa ni Patient Monitor mbili, BP mashine accessories 5,cable wires accessories 7,medical molecular sieve,Oxygen Concentrator na Oxygen Concentrator Intesty. 

Kamanda Magiligimba amesema watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika. 

Ametoa wito kwa watumishi kuacha tabia ya wizi wa mali za umma zinazotokana na tama ya mafanikio ya muda mfupi ambapo hupelekea wananchi kukosa huduma hivyo kuibebesha lawama serikali. 

Hata hivyo amesema Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga litaendelea kuchukua hatua kali za kisheria kwa mtu yeyote au watumishi wa serikali watakaobanika kufanya uhalifu wa aina yoyote ile.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba akitoa taarifa kwa vyombo vya habari leo Jumamosi Novemba 7,2020 kuhusu wizi wa vifaa tiba uliotokea Oktoba 13,2020 majira ya saa 10 jioni katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Shinyanga. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba sehemu ya vifaa tiba mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni 26 vilivyoibiwa katika Chumba cha Upasuaji katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Shinyanga.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba sehemu ya vifaa tiba mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni 26 vilivyoibiwa katika Chumba cha Upasuaji katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Shinyanga.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba sehemu ya vifaa tiba mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni 26 vilivyoibiwa katika Chumba cha Upasuaji katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Shinyanga.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba sehemu ya vifaa tiba mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni 26 vilivyoibiwa katika Chumba cha Upasuaji katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Shinyanga.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba vifaa tiba mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni 26 vilivyoibiwa katika Chumba cha Upasuaji katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Shinyanga.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba sehemu ya vifaa tiba mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni 26 vilivyoibiwa katika Chumba cha Upasuaji katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Shinyanga.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba sehemu ya vifaa tiba mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni 26 vilivyoibiwa katika Chumba cha Upasuaji katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Shinyanga.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba sehemu ya vifaa tiba mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni 26 vilivyoibiwa katika Chumba cha Upasuaji katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Shinyanga.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba sehemu ya vifaa tiba mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni 26 vilivyoibiwa katika Chumba cha Upasuaji katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Shinyanga.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba sehemu ya vifaa tiba mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni 26 vilivyoibiwa katika Chumba cha Upasuaji katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Shinyanga.
Muonekano wa sehemu ya vifaa tiba mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni 26 vilivyoibiwa katika Chumba cha Upasuaji katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Shinyanga.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Share:

Wanafuzi waboreshewa vyoo kujikinga na magonjwa ya mlipuko.

Samirah Yusuph.
Maswa. Kukamilika kwa ujenzi wa matundu ya vyoo katika shule za msingi wilayani Maswa imetajwa kuwa ni moja ya sababu za kutokomeza magonjwa ya mlipuko wilayani hapo.
Ujenzi uliogharim kiasi cha shilingi milioni 178.7 kukamilisha matundu 125 katika shule saba za msingi  itakuwa ni msaada kwa wanafunzi na jamii katika kujilinda na magonjwa hayo kwa matumizi sahihi ya vyoo.

Ambapo mkurugenzi mtendaji wa wilaya hiyo Fedrick Sagamiko alisema ujenzi umekamilika kwa asilimia 95, mradi uliotekelezwa kupitia programu ya Afya na Elimu  shuleni (SWASH) katika awamu ya kwanza, alisema:

“Ni mradi wa benki ya dunia lakini upo chini ya usimamizi wa ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa (TAMISEMI)  mradi huo unatekelezwa katika shule ambazo zilikuwa na changamoto ya vyoo kwa wanafunzi pamoja na walimu".

Sagamiko Alizitaja shule hizo kuwa ni Jija A matundu (20), Malampaka(33), Mandang'ombe(7), Maswa(30), Mwabulimbu(15), Mwashegeshi(9) na Sangamwalugesha(11).

Katika ujenzi huo kuna mambo ya msingi ambayo yamezingatiwa ambayo ni elimu,afya na maji kwa lengo la kutunza mazingira na kuwa msafi ili kujiepusha na magonjwa ya mlipuko yanayotokana na uchafu.

Alisema kuwa wamehakikisha vyoo hivyo vinakuwa na mfumo wa maji ili mtumiaji mara baada ya kutumia ananawa mikono na kuwa msafi na hivyo kujiepusha na aina yoyote ya magonjwa yanayotokana na uchafu na kuongeza kuwa:

"Ujenzi wa vyoo hivyo umechangiwa na wananchi wa maeneo husika huku akiwashukuru kwa kujitoa katika kushiriki na kuhakikisha vyoo hivyo vinakamilika".

Awali Afisa Elimu Msingi wilaya ya Maswa Saimon Bujimu, alihakikisha kuwa kwa ushirikiano na wakala wa maji wilayani hapo wataweza kutatua changamoto ya maji katika shule hizo ili  kuhakikisha wanafunzi wanasoma katika mazingira safi na salama".

MWISHO.

Share:

PLANNING/DEVELOPMENT ENGINEER (5 POSTS) at ATCL

Air Tanzania Company Limited (atcl) is in the process of revamping its operations and has introduced new equipment to its fleet as part of implementation of its five years Corporate Strategic Plan (2017/2018-2021/2022. In line with this expansion, the Company is also making some reforms in Engineering and Maintenance section to accommodate the business needs. […]

The post PLANNING/DEVELOPMENT ENGINEER (5 POSTS) at ATCL appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Cabin Crew (5 Posts) at ATCL

Air Tanzania Company Limited (ATCL) is in the process of revamping its operations and has introduced new equipment to its fleet as part of implementation of its five years Corporate Strategic Plan (2017/2018-2021/2022). In line with this expan­sion, the Company is also making some reforms in its structure, internal operations and staffing to accommodate the […]

The post Cabin Crew (5 Posts) at ATCL appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Communication specialist Volunteer at VSO

VSO is the world’s leading international development organisation that works through volunteers to fight poverty. Working in 24 countries around the world, our unique role in international development is to place committed volunteers with carefully selected organisations where their skills can have the greatest impact. As a VSO volunteer you’ll live and work in some […]

The post Communication specialist Volunteer at VSO appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Driver at VSO November

VSO is the world’s leading international development organisation that works through volunteers to fight poverty. Working in 24 countries around the world, our unique role in international development is to place committed volunteers with carefully selected organisations where their skills can have the greatest impact. Our extraordinary volunteers live and work in some of the […]

The post Driver at VSO November appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Project MEAL Officer at VSO

VSO is the world’s leading international development organisation that works through volunteers to fight poverty. Working in 24 countries around the world, our unique role in international development is to place committed volunteers with carefully selected organisations where their skills can have the greatest impact. Our extraordinary volunteers live and work in some of the […]

The post Project MEAL Officer at VSO appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Distribution Driver at Coca-Cola Kwanza (Tanzania)

Job Title Distribution Driver Function Logistics, Warehouse & Distribution Company Coca-Cola Kwanza (Tanzania) Job Type Permanent Location – Country Tanzania Location – Province Not Applicable Location – Town / City Dar es Salaam   Job Description Coca-Cola Kwanza Ltd has an exciting opportunity in Logistics department. We are looking for a 05 talented individual with […]

The post Distribution Driver at Coca-Cola Kwanza (Tanzania) appeared first on Udahiliportal.com.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive

Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger