Na Michael Abel, Shinyanga.
Mahafali ya 56 Shule ya Awali na Msingi Jomu ya kuwaaga wahitimu wa darasa la saba yamefana, huku wazazi na walezi wakihimizwa malezi bora kwa watoto pindi wanapomaliza elimu ya msingi.
Mahafali hayo yaliyofanyika leo, Oktoba 2, 2026, yamehudhuriwa na mgeni rasmi, Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga, Mheshimiwa Mwanahamisi Munkunda, ambaye amewapongeza wahitimu kwa kuonesha nidhamu nzuri katika kipindi chao cha masomo.
Mheshimiwa Munkunda amewataka wahitimu hao wanaporejea katika familia na jamii zao kuendelea kuwa na nidhamu, bidii katika masomo na kujiepusha na matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii, akieleza kuwa mitaani wanakutana na mazingira yenye changamoto na
“Tusiogope kuzungumza na watoto wetu. Mafanikio ya mtoto ya baadaye yanajengwa na malezi bora. Tujitahidi kuwalea katika misingi ya dini na imani zetu. Kwa kufanya hivyo, tutaweza kujenga kizazi chenye maadili na maendeleo hapo baadaye,” amesema Mheshimiwa Munkunda.
Mheshimiwa Munkunda ameipongeza Shule ya Msingi Jomu kwa kufanya vizuri kitaaluma kwa miaka mitatu mfululizo, ambapo kiwango cha ufaulu kimeongezeka kutoka asilimia 80 hadi asilimia 95.
Katika kuunga mkono juhudi za shule hiyo, amechangia matofali 1,000 na mifuko 50 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa jiko la shule. Pia ametoa madaftari aina ya Counter Book 10 kwa wahitimu wote 43 pamoja na vifaa vya kujifunzia, huku akiahidi kusaidia kumaliza changamoto ya ukosefu wa viti na meza kwa walimu ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.
Kwa upande wake, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Jomu, Eva Vedasta, amewashukuru wazazi kwa kuwaamini na kuwapeleka watoto wao katika shule hiyo, akiahidi kuwa walimu wataendelea kutoa huduma bora ya elimu na kuhakikisha wanafunzi wanaendelea kufanya vizuri kitaaluma.
Awali, akisoma risala ya wahitimu kwa niaba ya wanafunzi wenzake, Maskrini Poclet, amesema shule hiyo imeendelea kufanya vizuri kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo, huku kiwango cha ufaulu kikiongezeka kutoka asilimia 80 hadi asilimia 95 ambapo kwa mwaka 2026 jumla ya wanafunzi 43 wamehitimu wasichana 31 na wavulana 12 na kuahidi kuendelea kufanya vizuri katika katokeo ya mwaka huu.
























0 comments:
Post a Comment