Sunday, 1 November 2020
POLISI SHINYANGA WAONYA WATAKAOTHUBUTU KUANDAMANA KUPINGA MATOKEO YA UCHAGUZI
NEC YAMKABIDHI MAGUFULI CHETI CHA USHINDI KITI CHA URAIS TANZANIA
Dkt. Magufuli na Dkt. Mwinyi kuapishwa wiki ijayo
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole amesema shughuli ya kuapishwa kwa Rais Mteule wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi na Rais Mteule wa Jamhuri ya Muungano, Dkt. John Magufuli zitafanyika wiki ijayo.
Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi ndogo za chama hicho jijini Dar es Salaam Polepole amesema Dkt. Mwinyi ambaye alishinda katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 28, 2020 ataapishwa Novemba 2, 2020 katika Uwanja vya Amani Zanzibar kuwa Rais wa awamu ya nane wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar baada ya rais Dkt. Ali Mohamed Shein kumaliza muda wake.
Siku mbili zimepita tangu Tume ya ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) kumtangaza Dkt. Mwinyi kuwa mshindi wa kiti cha urais kwa kujipatia kura 380,02 sawa na asilimia 76.27 ya kura zote halali.
Kwa upande wa Rais Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli, Polepole amebainisha kuwa shughuli ya kuapishwa kwake kuongoza dola kwa muhula itafanyika Novemba 5, 2020 katika Uwanja wa Jamhuri Dodoma.
Dkt. Magufuli alitangazwa kuwa mshindi baada ya kupata kura 12,516,252 sawa na asilimia 84.4 ya kura zote halali.
Katibu mkuu huyo amewashukuru Watanzania wote kwa kuendelea kukiamini Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kukipatia ushindi wa kishindo, hivyo kuwataka kujitokeza kwa wingi katika matukio hayo muhimu la kuapishwa kwa viongozi wateule.
Polisi yatoa onyo wanaotaka kuandamana
Kamishna wa Operesheni na Mafunzo, CP Liberatus Sabas, amesema kuwa jeshi la polisi halitamvumilia mtu yeyote awe kiongozi wa chama au mfuasi, atakayefanya maandamano batili na kama kuna yeyote ambaye hakuridhika na matokeo afuate taratibu za kisheria kudai haki zao kama zipo.
CP Sabas ametoa kauli hiyo hii Oktoba 31,2020, na kuwasihi akina mama kuongea na watoto wao kwamba, wasithubutu kushiriki katika maandamano hayo na wasije wakarubuniwa na watu ambao hawana nia nzuri na Taifa.
"Nasisitiza kwamba jeshi la polisi halitakuwa na simile kwa yeyote atakayejihusisha na chokochoko hizi ambazo tunaziona zinaanza kuanzishwa na watu hawa ambao hawalitakii mema Taifa hili, nawaomba akina mama mkanye mwanao kwa sababu mwisho wa siku mtoto atakapopata matatizo atakulilia mama, sasa kabla matatizo hayajamfika nakuomba mkanye mwanao", amesema CP Sabas.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Aboubakar Kunenge atoa onyo kwa waliopanga kufanya vurugu Dar
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Aboubakar Kunenge ametoa onyo kwa watu au vikundi vya watu vilivyopanga kufanya vurugu mkoani kwake na kueleza kuwa sheria itachukua mkondo wake kwa yeyote atakayejaribu kuvuruga amani.
Kunenge ametoa onyo hilo wakati wa Uzinduzi wa Baraza la Wafanyakazi wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC).
Mkuu huyo wa mkoa ameongeza kuwa jiji lipo kwenye hali ya amani na utulivu huku usalama ukiwa umeimarishwa.
RC SHIGELLA APIGA MARUFUKU MAANDAMANO NA MIKUSANYIKO
madereva wa pikipiki maarufu bodaboda waliokusanyika kwa ajili ya kumpongeza Rais Dkt John Magufuli kwa kuchaguliwa tena kuongoza Tanzania kwa kipindi kingine cha miaka mitano kushoto Katibu wa kikundi cha Tanga One cha wilaya ya Tanga Omari Ahmed MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella akizungumza
madereva wa pikipiki maarufu bodaboda waliokusanyika kwa ajili ya kumpongeza Rais Dkt John Magufuli kwa kuchaguliwa tena kuongoza Tanzania kwa kipindi kingine cha miaka mitano kushoto Katibu wa kikundi cha Tanga One cha wilaya ya Tanga Omari Ahmed
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella kulia akiteta jamboi na viongozi waendesha pilkipiki bodaboda Jijini Tanga cha Tanga One wakati akipokea maandamano yao waliokusanyika uwanja wa Lamore kwa ajili ya kumpongeza Rais Dkt John Magufuli kwa kupata ushindi katika uchaguzi mkuu uliofanyika Octoba 28 mwaka huu KATIBU Mwenezi wa CCM wilaya ya Tanga Lupakisyo Kapange akizungumza
MKUU wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigella amepiga marufuku aina yoyote ya maandamano na mikusanyiko huku akiwataka wananchi kuendelea kujikita kwenye shughuli za kimaendeleo kwa maslahi mapana ya Taifa kutokana na kwamba uchaguzi umekwisha na walioshindwa wakubali matokeo.
RC Shigella aliyasema hayo wakati madereva wa pikipiki maarufu bodaboda waliokusanyika kwa ajili ya kumpongeza Rais Dkt John Magufuli kwa kuchaguliwa tena kuongoza Tanzania kwa kipindi kingine cha miaka mitano.
Alisema kwamba amepokea maandamano hayo ili atumie nafasi hiyo kuwatangazia wananchi kwamba serikali hairuhusu mikusanyiko yoyote katika kipindi hiki ambacho uchaguzi umemalizika.
Hatua ya Mkuu huyo wa Mkoa kupiga marufuku maandamano au mikusanyiko yoyote imekuja kutokana na uwepo wa tetesi kwamba wafuasi wa baadhi ya vyama vya upinzani wanaandaa maandamano ya kupinga matokeo ya uchaguzi huo.
Awali akisoma risala ya umoja wa waendesha bodaboda kikundi cha Tanga One cha wilaya ya Tanga iliyosomwa na Katibu wao Omari Ahmed alisema wanampongeza Rais Dkt John Magufuli kwa ushindi walioupata na kwamba wana matumaini kwamba sasa wana uhakika wa kufanya kazi zao kwa utulivu.
Alisema wanampongeza kwa dhati Rais Magufuli kwa kuibuka na ushindi wa kishindo kwani walikuwa wanamuombea kila wakati katika mchakato huo wa kuwania nafasi hiyo.
“Lakini tunapongeza vyombo vya ulinzi na usalama kwa kuhakikisha amani ya Taigfa inakuwa shwari wakati wote huu wa uchaguzi na umekwisha sasa tunaangalia maendeleo zaidi na kauli mbiu ya Rais Dkt Magufuli hapa kazi tu”Alisema
Hata hivyo alisema wao bodaboda kwa niaba ya wenzao wanaombi kwa Rais wanaomba aendelee kuwakumbuka watu wa Tanga huku wakiomba wakati akiapishwa waalikwe watu 10 wa bodaboda waende kushuhudia tukio hilo.
Electronics Technician at Fastlink Safaris
Electronics Technician Fastlink Safaris Engineering & Technology Dar es Salaam|Full Time IT & Telecoms Job Summary We are looking for electronic technicians for our mobile repair shops to set up, maintain, and repair electronic systems and devices. Minimum Qualification: Diploma Experience Level: Entry level Experience Length: 1 year Job Description This role requires hands-on experience […]
The post Electronics Technician at Fastlink Safaris appeared first on Udahiliportal.com.
Site Roll Out Manager at TIGO Tanzania
Site Roll Out Manager Job Country: Tanzania JOB PURPOSE To deliver a steady throughput of on air sites to the Head of Operations within a specified budget and according to specifications following MIC policies and processes that are given to the network roll out team. WE LEAD AND CONTRIBUTE. by connecting, by owning, by delivering, by […]
The post Site Roll Out Manager at TIGO Tanzania appeared first on Udahiliportal.com.
Finance Manager at Natural Extracts Industries
Finance Manager Natural Extracts Industries Ltd Accounting, Auditing & Finance Arusha & Moshi|Full Time Manufacturing & Warehousing Job Summary NEI is looking for a Finance Manager to oversee overall finance operations and liaising with senior stakeholders such as Board Directors Minimum Qualification: Bachelor Experience Level: Senior level Experience Length: 6 years Job Description Overall responsibility […]
The post Finance Manager at Natural Extracts Industries appeared first on Udahiliportal.com.
Customer Service Agents at WinPrincess
CUSTOMER SERVICE AGENTS POSTS(4) JOB Description Handling and replying to customer inquiries through live chats, phone calls, social media interaction with customers Maintaining customer relations. Providing feedback to Supervisor/ Head on customer’s needs/feedbacks. Preparing and generating reports/relating customer’s queries. Researching into customer’s queries/concerns into the systems. Assist players with specifics about promotions, loyalty programs, and […]
The post Customer Service Agents at WinPrincess appeared first on Udahiliportal.com.
Portfolio and Analytics Manager at Standard Chartered Bank
Portfolio and Analytics Manager Standard Chartered Bank Dar es Salaam, Dar es Salaam, Tanzania About Standard Chartered We are a leading international bank focused on helping people and companies prosper across Asia, Africa and the Middle East. To us, good performance is about much more than turning a profit. It’s about showing how you embody […]
The post Portfolio and Analytics Manager at Standard Chartered Bank appeared first on Udahiliportal.com.
Manager Alliance and Partnerships at Standard Chartered Bank
Manager Alliance and Partnerships Standard Chartered Bank Dar es Salaam, Dar es Salaam, Tanzania About Standard Chartered We are a leading international bank focused on helping people and companies prosper across Asia, Africa and the Middle East. To us, good performance is about much more than turning a profit. It’s about showing how you embody […]
The post Manager Alliance and Partnerships at Standard Chartered Bank appeared first on Udahiliportal.com.
Senior Sales Manager at Standard Chartered Bank
Senior Sales Manager Standard Chartered Bank Dar es Salaam, Dar es Salaam, Tanzania About Standard Chartered We are a leading international bank focused on helping people and companies prosper across Asia, Africa and the Middle East. To us, good performance is about much more than turning a profit. It’s about showing how you embody our […]
The post Senior Sales Manager at Standard Chartered Bank appeared first on Udahiliportal.com.
MARUCO second round selected applicants 2020/2021
The Marian University College MARUCO second round selected applicants 2020/2021 are the names of students who have passed the Second-round admission selection stage and successfully approved by TCU to join undergraduate studies at Marian University College (MARUCO) for the 2020/2021 academic year second round application window. The Marian University College MARUCO second round applications and […]
The post MARUCO second round selected applicants 2020/2021 appeared first on Udahiliportal.com.
Saturday, 31 October 2020
Tanzia : MUIGIZAJI MAARUFU WA FILAMU YA JAMES BOND AFARIKI DUNIA
"Wote tunafanyia kazi kuelewa tukio hili kubwa kwa kuwa ndio kwanza limetokea," aliongeza, akielezea kifo cha baba yake kuwa ni "pigo kwa watu wote duniani ambao walifurahia zawadi aliyokuwa nayo kama muigizaji.
Hafla ya heshima za mwisho kwa Connery itakayofanyika baadaye, kwa mujibu wa ofisa habari wake.
Lakini ilikuwa ni sinema maarufu ya 007, aliyoigiza akitumia Kiingereza chenye lafudhi ya Scotland akiigiza kama mpelelezi aliyekuwa na leseni ya kuua, iliyompatia umaarufu mkubwa duniani kote.
Alikuwa ni muigizaji wa kwanza kutoa maneno yasiyosahaulika ya "Bond, James Bond" na aliigiza filamu sita zilizotokana na mtunzi wa vitabu vya hadithi, Ian Fleming.
"Alikuwa na siku zote ataendelea kukumbukwa kama James Bond halisi," walisema watayarishaji filamu maarufu, Michael G. Wilson na Barbara Broccoli.
Mara kadhaa , mcheza sinema huyo kutoka Scotland alipigiwa kura na mashabiki ya kuwa muigizaji bora wa nafasi ya Bond, akiwashinda waigizaji wengine kama Daniel Craig wa sasa na Roger Moore.