Friday, 3 July 2020

ZOEZI LA UTAMBUZI KAYA MASKINI MANISPAA YA SHINYANGA MPANGO WA TASAF KIPINDI CHA PILI LATANGAZWA RASMI...MAAFISA WATENDAJI WAKUTANA

Mratibu wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini - TASAF Manispaa ya Shinyanga Octavina Kiwone.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Mratibu wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini - TASAF Manispaa ya Shinyanga Octavina Kiwone amewataka Maafisa Watendaji wa Mitaa,vijiji na kata katika Manispaa ya Shinyanga kusimamia kwa uadilifu na umakini zoezi la utambuzi wa kaya maskini ambazo zitaingia kwenye mpango wa kunusuru kaya maskini katika kipindi cha pili ulionza mwezi Juni,2020. 



Kiwone ametoa rai hiyo leo Ijumaa Julai 3,2020 wakati wa kikao kazi kilichokutanisha pamoja Maafisa Watendaji wa kata,vijiji na mitaa katika Manispaa ya Shinyanga kwa ajili ya kutoa maelekezo namna ya kutambua kaya maskini zitakazoingia kwenye mpango wa kunusuru kaya maskini katika kipindi cha pili. 

Kiwone alisema utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru kaya Maskini katika kipindi cha pili utakaodumu kwa kipindi cha miaka mitatu umeanza mwezi Juni 2020 ambapo zoezi la utambuzi katika Manispaa ya Shinyanga litafanyika kwa kipindi cha wiki mbili (kuanzia Julai 3 hadi Julai 20,2020). 

Alieleza kuwa zoezi la kutambua kaya maskini linalenga kaya maskini zilizosahaulika kwenye kipindi kilichopita lakini pia litahusisha mitaa na vijiji vyote katika Manispaa ya Shinyanga ambavyo havikuwepo kwenye mpango ambapo baada ya utambuzi huo wa awali ndipo serikali itajua inaenda kuhudumia walengwa wangapi na kutoa fedha kwa ajili ya kaya hizo. 

“Mpango huu wa kunusuru kaya maskini kipindi cha pili utagusa kata zote na Manispaa ya Shinyanga. Tunawasihi sana viongozi kwenye maeneo husika wasimamie zoezi hili kwa umakini na uadilifu mkubwa ili tupate kaya ambazo zina vigezo na zinastahili kuwepo kwenye mpango”,alisema Kiwone. 

“Hatutegemei kwenye eneo letu la Manispaa ya Shinyanga kupata kaya ambazo hazina sifa kuingia kwenye mpango. Kila mmoja atawajibika kwa nafasi yake kwa kufuata sheria, taratibu na kanuni zilizowekwa lakini pia watu wasifanye kwa matashi yao",alisema Kiwone. 

Alieleza kuwa ni haki ya kaya maskini kuhudumiwa siyo kwamba anapewa upendeleo ‘Favour’ au kwamba anapewa sadaka flani akibainisha kuwa hiyo ni fedha ya serikali inatakiwa iende kwa mtu stahiki na anayestahili kupata. 

Hata hivyo alisema baada ya utambuzi huo wa awali kufanyika kuna vyombo vingine vyenye dhamana vitarudi kwenye orodha ya kaya maskini zinakazopatikana ili kuhakiki kama waliopitishwa ni kweli ni kaya maskini zina vigezo na zinastahili kuingia katika mpango wa kunusuru kaya maskini. 

Alivitaja baadhi ya vigezo vinavyotakiwa katika mpango huo kuwa kaya zenye kipato duni zinazoshindwa kupata milo mitatu kwa siku,kaya yenye makazi duni, kaya yenye watoto wengi wanashindwa kuihudumia, kaya ambayo watoto wanashindwa kwenda shule kwa sababu hawana mahitaji ya shule au kwenda kliniki kwa sababu mbalimbali 

“Ni muda mzuri kwa wananchi pia kufahamu, wanapoitwa kwenye mikutano ya hadhara kwenye maeneo yao wafike ili wasikose haki yao ya msingi. 

Na kwa wananchi ‘makundi maalum’ ambao hawawezi kufika kwenye mikutano mfano watu wenye ulemavu,wazee maskini jamii iwataje. TASAF haiandikiwi mezani kupata orodha ya walengwa,orodha inapatikana kwenye mikutano ya hadhara,wakutambue kwamba wewe upo kwenye kaya maskini na mkutano uridhie kuwa kweli wewe ni kaya maskini”,alifafanua Kiwone.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mratibu wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini - TASAF Manispaa ya Shinyanga Octavina Kiwone akizungumza katika kikao kazi kilichokutanisha pamoja Maafisa Watendaji wa kata,vijiji na mitaa katika Manispaa ya Shinyanga kwa ajili ya kutoa maelekezo namna ya kutambua kaya maskini zitakazoingia kwenye mpango wa kunusuru kaya maskini katika kipindi cha pili kilichoanza mwezi Juni mwaka huu 2020 katika ukumbi wa Lewis Kalinjuna Manispaa ya Shinyanga leo Ijumaa Julai 3,2020 . Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mratibu wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini - TASAF Manispaa ya Shinyanga Octavina Kiwone akiwasisitiza Maafisa Watendaji wa Mitaa,vijiji na kata katika Manispaa ya Shinyanga kusimamia kwa uadilifu na umakini zoezi la utambuzi wa kaya maskini ambazo zitaingia kwenye mpango wa kunusuru kaya maskini katika kipindi cha pili ulionza mwezi Juni,2020. 
Mratibu wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini - TASAF Manispaa ya Shinyanga Octavina Kiwone akiwasihi Maafisa Watendaji wa Mitaa,vijiji na kata katika Manispaa ya Shinyanga kusimamia kwa uadilifu na umakini zoezi la utambuzi wa kaya maskini ambazo zitaingia kwenye mpango wa kunusuru kaya maskini katika kipindi cha pili ulionza mwezi Juni,2020. 
Maafisa Watendaji wa kata,vijiji na mitaa katika Manispaa ya Shinyanga wakiwa katika kikao cha kuelezwa namna ya kutambua kaya maskini zitakazoingia kwenye mpango wa kunusuru kaya maskini katika kipindi cha pili. 
Maafisa Watendaji wa kata,vijiji na mitaa katika Manispaa ya Shinyanga wakiwa katika kikao cha kuelezwa namna ya kutambua kaya maskini zitakazoingia kwenye mpango wa kunusuru kaya maskini katika kipindi cha pili. 
Maafisa Watendaji wa kata,vijiji na mitaa katika Manispaa ya Shinyanga wakiwa ukumbini.
Maafisa Watendaji wa kata,vijiji na mitaa katika Manispaa ya Shinyanga wakiwa ukumbini.
Maafisa Watendaji wa kata,vijiji na mitaa katika Manispaa ya Shinyanga wakiwa ukumbini.
Maafisa Watendaji wa kata,vijiji na mitaa katika Manispaa ya Shinyanga wakiwa ukumbini.
Maafisa Watendaji wa kata,vijiji na mitaa katika Manispaa ya Shinyanga wakiwa ukumbini.
Maafisa Watendaji wa kata,vijiji na mitaa katika Manispaa ya Shinyanga wakiwa ukumbini.
Maafisa Watendaji wa kata,vijiji na mitaa katika Manispaa ya Shinyanga wakiwa ukumbini.
Maafisa Watendaji wa kata,vijiji na mitaa katika Manispaa ya Shinyanga wakiwa ukumbini.
Maafisa Watendaji wa kata,vijiji na mitaa katika Manispaa ya Shinyanga wakiwa ukumbini.
Maafisa Watendaji wa kata,vijiji na mitaa katika Manispaa ya Shinyanga wakiwa ukumbini.
Maafisa Watendaji wa kata,vijiji na mitaa katika Manispaa ya Shinyanga wakiwa ukumbini.
Maafisa Watendaji wa kata,vijiji na mitaa katika Manispaa ya Shinyanga wakiwa ukumbini.
Maafisa Watendaji wa kata,vijiji na mitaa katika Manispaa ya Shinyanga wakiwa ukumbini.
Maafisa Watendaji wa kata,vijiji na mitaa katika Manispaa ya Shinyanga wakiwa ukumbini.
Maafisa Watendaji wa kata,vijiji na mitaa katika Manispaa ya Shinyanga wakiwa ukumbini.
Maafisa Watendaji wa kata,vijiji na mitaa katika Manispaa ya Shinyanga wakiwa ukumbini.
Maafisa Watendaji wa kata,vijiji na mitaa katika Manispaa ya Shinyanga wakiwa ukumbini.
 Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Share:

WAANDISHI WA HABARI WAPATA AJALI YA GARI KWENYE MSAFARA WA WAZIRI WA MADINI

George Binagi-GB Pazzo, BMG
Msafara wa Waziri wa Madini, Doto Biteko umepata ajali kwa kuhusisha gari lililokuwa limewabeba waandishi wa habari kukosa mwelekeo na kugonga kingo za barabara katika eneo la Murugunga, Kata ya Murusagamba, Wilaya ya Ngara mkoani Kagera.


Katika ajali hiyo, baadhi ya waandishi wamepata majeraha na kupatiwa huduma ya kwanza katika Kituo cha Afya Murusagamba na kisha kupelekwa mkoani Geita kwa uchunguzi zaidi.

Ajali hiyo imetokea mapema leo Julai 03, 2020 kwa kuhusisha gari aina ya Toyota Land Cruiser yenye nambari za usajili STL 3132 mali ya Wizara ya Madini huku Waandishia wa Habari waliokuwemo wakiwa ni Nazareth Ndekia (TBC), Emmanuel Ibrahim (Clouds), Victor Bariety  (Chanel Ten) pamoja na Salma Mrisho (Star TV).

"Vumbi limesababisha dereva ashindwe kutambua pale kuna kona . Amejitahidi kulimudu gari vinginevyo lingepinduka. Tunamshukuru Mungu tumetoka salama" amesema Emmanuel Ibrahim.

Kufuatia ajali hiyo, Waziri Biteko aliyekuwa ametembelea mgodi wa madini ya viwandani Manganizi (Manganese) Magamba ametoa pole na kuwaombea afya njema waandishi hao pamoja na dereva wao.

Akiwa katika mgodi wa Manganizi Magamba, Biteko amewaagiza Mafisa Madini katika mikoa yote nchini hadi kufikia Julai 15, 2020 wawe wamefanya sensa ya madini ya viwandani yanayosubiri vibali kwa ajili ya kusafirishwa nje ya nchi ili vibali hivyo vishughulikiwe.

Awali msimamizi wa mgodi wa Manganizi Magamba, Sarah Lusambagula amesema soko kubwa la madini ya Manganizi yanayotumika kwenye utengenezaji wa bidhaa za chuma liko nje ya nchi hivyo ameiomba Serikali kupitia Wizara ya Madini kusaidia upatikanaji wa kibali cha kuuza shehena ya madini ghafi aliyonayo kwani ikikaa muda mrefu inapoteza ubora.

Chanzo - BMG
Share:

WANANCHI KATA YA PUMA MKOANI SINGIDA WATENGENEZA MADAWATI YENYE THAMANI YA SH. MILIONI 3.4

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)  Wilaya ya Ikungi, mkoani Singida, Mika Likapakapa (kulia mwenye baraghashia) akikabidhi jana moja ya dawati kati ya 71 kwa Wazazi wa Kata ya Puma yaliyotengenezwa kwa ajili ya kukabiliana na changamoto ya kukaa chini kwa Wanafunzi wa Shule ya Msingi Puma. 

 Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)  Wilaya ya Ikungi, mkoani Singida, Mika Likapakapa, akiwa katika picha ya pamoja na Walimu wa Shule ya Msingi Puma baada ya kukabidhi madawati hayo.
 Wanafunzi wa Shule ya Msingi Puma wakiwa kwenye hafla ya kukabidhi madawati hayo.
  Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)  Wilaya ya Ikungi, mkoani Singida, Mika Likapakapa (katikati) , akiwa katika picha ya pamoja na Wanafunzi wa Shule ya Msingi Puma baada ya kukabidhi madawati hayo.


Wanafunzi wa Shule ya Msingi Puma wakiwa wamekaa kwenye  madawati hayo baada ya kukabidhiwa. 
  Wanafunzi wa Shule ya Msingi Puma wakiwa kwenye hafla ya kukabidhi madawati hayo.
 Viongozi wakiwa meza kuu kwenye hafla hiyo.
 Mwenyekiti wa Kamati ya  Shule ya Msingi Puma, Joseph Helman akizunguma kwenye hafla hiyo.
 Mwenyekiti wa Kijiji cha Puma, Samuel Mdimi akizunguma kwenye hafla hiyo.
 Afisa Utamaduni wa wilaya hiyo, Abubakar Kisuda akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo.
  Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Puma, Wenseslaus Masire  akizunguma kwenye hafla hiyo.
Mwenyekiti wa Kamati Maalumu iliyosimamia kutengeneza madawati hayo, Clemence Mande,  akizunguma kwenye hafla hiyo.

 Katibu wa Kamati ya hutengenezaji wa madawati hayo, Samsoni Masasi, akisoma taarifa.
 Wananchi wakiwa kwenye hafla hiyo.
Wajumbe wa Kamati Maalumu ya Kutengeneza madawati hayo wakitambulishwa.
Mwalimu, Christina Lyimo,  akizungumzia msaada wa madawati hayo.
 Mkazi wa Puma, Magreth Agustino, akizungumzia msaada wa madawati hayo.
Mwanafunzi Mariam Abdallah akizungumzia msaada wa madawati hayo.


Na Dotto Mwaibale, Singida

WANANCHI wa Kata ya Puma wilayani Ikungi mkoani Singida kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo wamefanikiwa kutengeneza madawati 71 yenye thamani ya sh.3,408,000 kwa ajili ya kupunguza changamoto ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Puma ya kukaa chini.

Hatua ya kutengeneza madawati hayo  ni kuunga mkono jitihada za Rais John Magufuli za kutoa elimu bure kuanzia shule za msingi hadi sekondari na kusoma katika mazingira bora.

Akizungumza jana wakati akipokea madawati hayo kutoka kwa kamati maalumu iliyosimamia hutengenezaji wake, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)  Wilaya ya Ikungi, Mika Likapakapa aliipongeza kamati hiyo, wananchi na viongozi mbalimbali kwa kufanikisha kazi hiyo.

Alisema kazi walioifanya ni kubwa mno na italeta faraja kwa wanafunzi baada ya kupata madawati hayo.

"Mimi kama kiongozi mkuu niliye ndani ya Wilaya ya Ikungi ninaye isimamia Serikali kwa hawa walioshiriki kufanya kazi hii tutawatambua kwa kuwapa vyeti vya utambuzi wa kazi hiyo jambo litakalo wasaidia kuwatia moyo" alisema Likapakapa.

Alisema katika utekelezaji wa kazi hiyo anajua walikumbana na changamoto mbalimbali ikiwamo za watu waliotoa ahadi kushindwa  kutoa fedha hizo ingawa watoto wao wapo shuleni hapo na watakaliaa madawati hayo.

Likapakapa alitumia mkutano huo kutoa sh.100,000 kama mchango wake wa kuunga mkono jitihada za wananchi hao katika shughuli za maendeleo.

Afisa Utamaduni wa wilaya hiyo, Abubakar Kisuda akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Justice Kijazi aliwashukuru wananchi hao kwa kazi hiyo ya kujitolea kwa moyo wa dhati na kuwa wazalendo.

Kisuda alisema mwaka 2015 katika utekelezaji wa ilani ya CCM wilaya hiyo ilitarajia kutengeneza madawati 5000 katika kipindi chote cha miaka mitano lakini hadi sasa wana asilimia 75 ya madawati yote waliyokusudia kuyatengeneza na ili kukamilisha mchakato wa kuyatengeneza ilihitajika nguvu kutoka kwa wananchi pamoja na wadau. 

"Puma imekuwa ni kijiji cha nne kati ya vijiji vilivyoweka jitihada za kutatua changamoto hii ya kutengeneza madawati." alisema Kisuda.

Alivitaja vijiji hivyo kuwa ni Unyahati, Nkhoire, Kisuluda na Puma na kuwa wazazi wote waliochangia kutengeneza madawati hayo wametimiza wajibu wao na wanakila sababu ya kupongezwa.

Kisuda alisema kwa muitikio huo waliouonesha halmashauri hiyo inawaahidi kuwapa kipaumbele katika miradi mbalimbali ya maendeleo kwenye shule hiyo kama walivyofanya mradi wa choo ambapo kuna shule zaidi ya 108 lakini wameipa shule ya Puma.

Alisema madawati 66 yaliyosalia kutengenezwa kati ya hayo 71 ambayo yapo tayari halmashauri hiyo itatoa mbao 20 ili kuyatengeneza ambapo alitoa mwito kwa wananchi hao kuendeleza jitihada hizo za shughuli za maendeleo katika kata hiyo.

Share:

DC MUHEZA AWATAKA VIONGOZI WA DINI KUHAMASISHA JAMII UNYWAJI WA DAWA ZA KUTOKOMEZA USUBI NA MINYOO YA TUMBO

 MKUU wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo akizungumza wakati akifungua kikao cha wajumbe wa kamati ya afya ya Msingi wilaya ya Muheza kulia ni Mganga Mkuu wa wilaya ya Muheza (DMO) Flora Kessy
 MKUU wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo akizungumza wakati akifungua kikao cha wajumbe wa kamati ya afya ya Msingi wilaya ya Muheza kulia ni Mganga Mkuu wa wilaya ya Muheza (DMO) Flora Kessy
 Mganga Mkuu wa wilaya ya Muheza (DMO) Flora Kessy akizungumza wakati wa kikao cha wajumbe wa kamati ya afya ya Msingi kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo


 Mratibu wa Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele wilayani Muheza Julias Mgeni akizungumza wakati wa kikao hicho
 Mratibu wa Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele wilayani Muheza Julias Mgeni akizungumza wakati wa kikao hicho
MRATIBU wa Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele Mkoa wa Tanga Dkt Rehema Maggid akizungumza katrika kikao hicho
 mmoja wa washiriki kwenye kikao hicho akichangia jambo
 sehemu ya wajumbe kwenye kikao hicho


MKUU wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga Mhandisi Mwanasha Tumbo amewataka viongozi wa dini wa taasisi za serikali na binafsi washirikiana kuwahamasisha jamii na wananchi wakijitokezea kwenye unywaji wa dawa za kutokomeza ugonjwa minyoo ya tumbo na usubi.

Mhandisi Mwanasha aliyasema hayo wakati akifungua kikao cha wajumbe wa kamati ya afya ya Msingi wilaya ya Muheza ambapo alisema kwamba kumekuwa na fikra potofu kwamba dawa hizo zinazuia uzazi au kusababisha kansa lengo kutokomeza ugonjwa wa m inyoo na tumbu na usubi.

Alisema kwa Sasa hawatoi dawa za kuzuia na kujikinga na matende kwa sababu wameweza kuudhibiti kwa asilimia kubwa ugonjwa huo huku akieleza mwengine uliokuwepo na sasa umekwisha ni mabusha kutokana na kufanya operesheni nyingi na umekwisha ,


Alitoa wito kwa jamii kama wapo wengine wenye matatizo hayo wajitokeza na kupatiwa matibabu na yaweze kwisha kabisa kwa jamii na hatimaye kuweza kuumaliza kabisa kwenye maeneo hayo.

Alisema kipindi cha nyumba walikuwa wanasumbuliwa na ugonjwa wa matendo na usubi mara nyingi hawayapewi kipambele wanakuwa hawafuatilii tiba matokeo yake wakawa wanaambukizana.

“Usubri upo hasa kandokandoi ya mito mtu anapata ugonjwa wa macho anaona ni ugonjwa wa kawaida lakini hivi sasa wamehakikisha wenye matende tunatoa kinga tiba kinga kama mtu anapata basi Kuhakikisha wadudu hao wanakufa”Alisema

“Lakini takribani muda mrefu wananchi wa muheza wamekuwa wakipewa dawa ya matende na wilaya ya Muheza vipimo vimefanyika na kuonekana ugonjwa huo umekwisha na jitihada hizohizo tunazielekeza kwenye usubi “Alisema DC Mhandisi Mwanasha

Mkuu huyo wa wilaya alisema kwamba hamasa hiyo kwa wananchi sasa ni kuhakikisha wanajitokeza waliokuwa na madhara na wasiokuwa nayo ili kuweza kupata kinga kwa sasa wamebakia asilimia 2.

Hata hivyo alisema kwa upande wa wanafunzi wana sumbuliwa na minyooo wameweka mikakati wanafunzi wote wahakikisha wanakunywa dawa za kuzuia minyoo ili kuweza kudhibiti.

“Lengo la Serikali chini ya Rais Dkt John Magufuli ni kuhakikisha wananchi wanakuwa na afya njema waweze kuendelea na shughuli za kiuchumi na kutekeleza kwa vitendo lakini pia na wanafunzi kusoma kwa bidii”Alisema Mkuu huyo wa wilaya.

Awali akizungumza Mratibu wa Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele wilayani Muheza Julias Mgeni alisema kwamba wilaya hiyo walianza kutokumeza magonjwa manne ambayo ni kichocho, usubi, mabusha na matende, minyoo ya tumbo.

Alisema kwa sasa kiwango cha maambukizi ya mabusha na matende kipo chini ya asilimia mbili hivyo haewaendelei tena kutoa dawa bali wanatoa elimu kwa walioathirika nalo ikiwemo upasuaji mabusha, matende wanatoa elimu.
Share:

Taarifa Kwa Umma Kutoka Mamlaka ya Mawasiliano -TCRA:Ufafanuzi wa URASIMISHAJI wa Laini za Ziada katika Mtandao Mmoja

1.0 UTANGULIZI
Kanuni za Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (Usajili wa Laini za Simu) za mwaka 2020, yaani “The Electronic and Postal Communications (SIM Card Registration) Regulations, 2020”, zimeainisha katika Kanuni ya 18 kuwa:-

18 (1) Mtu anayehitaji kumiliki na kutumia laini ya simu ataruhusiwa kusajili:-

(a) Kama ni mtu binafsi

    Idadi ya laini moja kwa kila mtoa huduma za mawasiliano kwa ajili ya kupiga simu za sauti, kutuma ujumbe mfupi pamoja na matumizi ya data;
    Idadi ya laini zisizozidi nne kwa kila mtoa huduma za mawasiliano

kwa matumizi ya mawasiliano kati ya mashine na mashine; na

(b) Kama ni Kampuni au Taasisi

    Idadi ya laini zisizozidi thelathini kwa kila mtoa huduma za mawasiliano kwa ajili ya kupiga simu za sauti, kutuma ujumbe mfupi pamoja na matumizi ya data;
    Idadi ya laini zisizozidi hamsini kwa kila mtoa huduma za mawasiliano kwa matumizi ya mawasiliano kati ya mashine na mashine.

(2) Laini zilizosajiliwa kwa matumizi yaliyoainishwa kwenye Kanuni 18 (1) (a) hazipaswi kutumiwa kwa kubadilishana (interchangebly).

(3) Bila kujali Kanuni ya 18 (1), Mtu binafsi, Kampuni au Taasisi inaweza kuruhusiwa kusajili na kumiliki laini zaidi ya zilizoainishwa kwa kuomba na kupata idhini kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania

(4) Mtu yeyote atakayekiuka masharti ya Kanuni hizi, atakuwa ametenda kosa la jinai.

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) inapenda kuutaarifu umma kwamba zoezi la kuomba idhini ya umiliki wa laini za simu zaidi ya moja katika mtandao mmoja linaendelea. Tunawashauri wamiliki wa laini za mawasiliano ya simu kuendelea kuhakiki usajili wa laini zao zote wanazomiliki.

2.0 KUTHIBITISHA IDADI YA LAINI ZILIZOSAJILIWA KUTUMIA KITAMBULISHO CHA TAIFA (NIDA)

2.1 Kila mmiliki wa laini ya simu anatakiwa kupiga namba *106# na kuangalia usajili wa laini anazomiliki na endapo atakuta namba ambayo haitambui na imesajiliwa kwa kutumia namba ya kitambulisho chake cha Taifa anashauriwa kuwasiliana na mtoa huduma wake ili azifunge mara moja kuepusha matumizi mabaya na kumsababishia usumbufu usiokuwa wa lazima utakaojitokeza.

2.2 Kwa wale ambao kwa sasa wanamiliki laini zaidi ya moja katika mtandao mmoja, mwisho wa kuhakiki laini zao itakuwa tarehe 31 Julai 2020.

2.3 Utaratibu wa kuomba idhini ya kumiliki laini mpya za ziada katika mtandao mmoja unaendelea na mteja anaweza kupata huduma hii kupitia kwa wakala au kwenye ofisi za watoa huduma ambapo kwa kutumia njia za kielektroniki mtoa huduma atawasilisha maombi ya mteja wake TCRA kwa idhini ya kusajili na kumiliki laini za ziada; mteja atapokea majibu ya maombi yake ndani ya takribani dakika tano.

3.0 URASIMISHAJI WA LAINI ULIZOTHIBITISHA

3.1 Urasimishaji wa laini za ziada kwa sasa unaweza kufanyika kwa wakala au kwenye ofisi za watoa huduma ambapo kwa kutumia njia za kielektroniki ambapo mtoa huduma atawasilisha maombi yake ya idhini ya kurasimisha laini za ziada TCRA na kupokea majibu ndani ya takribani dakika tano; au

3.2 Kwa kupitia namba *106# ambapo wewe mwenyewe utaweza kuomba idhini ya kurasimisha kutoka TCRA kupitia simu yako. Huduma hii ya kurasimisha kwa njia ya simu yako itaanza kutumika rasmi Agosti 1, 2020.

Imetolewa na:

Mkurugenzi Mkuu, 
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)




Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger