Thursday, 2 July 2020

TCRA Yavipiga Faini Vyombo vya Habari Sita vya Utangazaji kwa kurusha maudhui katika muda ambao watoto hawapaswi kuangalia ama kusikiliza

Mamlaka  ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imevitoza faini ya Sh milioni 30 vyombo vya habari sita, kwa kukiuka kanuni na maadili ya utangazaji ikiwamo redio ya Clouds FM kuzungumzia supu ya pweza kuimarisha tendo la ndoa katika muda ambao wasikilizaji wanaweza kuwa watoto.

Mbali ya Clouds FM, vyombo vingine vilivyoadhibiwa ni East Africa Radio, na televisheni za Star, Sibuka, na Global Tv na Duma Tv.

Akisoma uamuzi huo jana jijini Dar es Salaam, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui ya TCRA, Joseph Mapunda alisema vyombo hivyo vilikiuka kanuni za mawasiliano kwa nyakati tofauti.

Mapunda alisema redio ya Clouds FM kupitia kipindi chake cha Jahazi, walihamasisha vitendo vya ngono, kwa kutumia supu ya pweza katika kuimarisha tendo la ndoa kwa muda ambao wasikilizaji wanaweza kuwa watoto.

Alisema baada ya kusikiliza utetezi wao, wanatozwa faini ya Sh milioni saba na kupewa onyo kali baada ya kuwatia hatiani kwa kosa hilo.

Katika shauri lingine, kituo cha Duma TV kimetozwa faini ya Sh milioni saba na kufungiwa kuchapisha maudhui kwa muda wa mwezi mmoja ili wajipange na kuzifahamu kanuni na kuzingatia weledi na maadili ya utangazaji.

Mapunda alisema Duma ilikutwa na hatia ya kukiuka kanuni kwa kuchapisha na kutangaza maudhui yenye lugha isiyo na staha na iliyo na udhalilishaji wa kijinsia kwa wanaume na wanawake.

Alisema redio ya East Africa imetozwa faini ya Sh milioni tatu na kupewa onyo kali kwa kukiuka kanuni hiyo, kwa kurusha maudhui ya kukashifu utendaji wa serikali kupitia uteuzi wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na kutumia lugha ya kashfa dhidi ya utendaji wake.

Vilevile Global Tv imetozwa Sh milioni saba na kupewa onyo kali, baada ya kupatikana na hatia ya kuchapisha picha ya mnato na kutangaza maudhui yasiyokuwa na lugha ya staha na yenye kushabikia vitendo vya mahusiano ya kimapenzi ya jinsia moja.

Mapunda alisema maudhui hayo, yangeweza kuwaumiza na kuwakwaza waumini wa dhebebu la Anglikana na Watanzania kwa ujumla. Pia, alisema Sibuka Tv inatozwa faini ya Sh milioni tatu baada ya kupatikana na hatia ya kushabikia mauaji ya kutisha katika muda, ambao watoto wanaweza kuwa sehemu kubwa ya watazamaji.


Share:

PAKUA APP YA MALUNDE 1 BLOG ILI TUWE TUNAKUMIA HABARI NA MATUKIO MOJA KWA MOJA KWENYE SIMU YAKO

Kuwa wa Kwanza kupata habari na matukio yanayojiri Tanzania na dunia kwa ujumla kwa kupakua/ kudownload App ya Malunde 1 blog tukuhabarishe masaa 24.


Tembea na dunia kiganjani mwako sasa.

Pakua App mpya ya Malunde 1 blog imeboreshwa zaidi ili kukidhi mahitaji ya wasomaji wetu. Hii ndiyo mpya kabisa,ina alama hii ↡↡
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Ni rahisi sana : Ingia Play store kisha Andika Malunde 1 blog halafu bonyeza Install

https://bit.ly/2Qb7qyF

Tafadhali fuata maelekezo hapo juu... Usikubali kukosa habari kizembe..Pakua app yetu Mpya ya Malunde1 blog Sasa
Share:

Msemaji wa Serikali atoa Siri 10 zilizopelekea Tanzania kuingia uchumi wa kati

Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi ametaja  siri 10 zilizopelekea Tanzania kuingia katika uchumi wa kati miaka mitano kabla ya lengo

Amesema Tanzania imekua miongoni mwa nchi 50 Duniani, nchi ya 24 kwa Afrika na ya pili kwa Afrika Mashariki kuingia katika uchumi wa kati, Uchumi wa kipato cha kati umehusishwa na nchi ambayo umasikini unapungua, uchumi imara unajengwa, uzalishaji viwandani unaimarika na wananchi wanapata maendeleo.

“Hii ni kali zaidi, tumewekeza katika maendeleo ya watu moja kwa moja, tukapimwa na benki ya Dunia tukaonekana tupo kwenye wastani wa kipato cha kati, Misingi kumi iliyotusaidia kuingia katika kipato cha kati ni amani na utulivu, mipango thabiti ya maendeleo, utekelezaji usioyumba, kufanya maamuzi magumu,azma ya kujitegemea, nidhamu katika matumizi”

==>>Msikilize hapo chini


Share:

Gari nne zagongana na kusababisha ajali Pwani

Gari nne yakiwemo malori mawili ya mafuta yamegongana na kusababisha ajali katika eneo la Mlandizi mkoani Pwani usiku wa kuamkia leo Julai 2.

Ajali hiyo imetokea majira ya saa 5 Usiku wa jana Julai Mosi, na kupelekea kifo cha mtu mmoja na majeruhi watatu ambao wote wamekimbizwa katika Hospitali ya Tumbi.

Akithibitisha taarifa hiyo, Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, Wankyo Nyigesa amemtaja marehemu kwa jina la Rahim Kurwa, huku akisisitiza kuwa abiria wanaotokea Dar es Salaam kwa kutumia barabara ya Morogoro watumie barabara ya Bagamoyo.

"Majeruhi wapo katika hospitali ya Tumbi pamoja na mwili wa marehemu lakini ninawashauri wasafiri wanaotokea Dar es Salaam watumie barabara ya Bagamoyo ili tuweze kuifungua hii barabara kwa sababu foleni ni kubwa sana", Kamanda Nyigesa

Credit: EATV


Share:

Jinsi Ya Kuondoa Kitambi Ndani Ya Siku Kumi Na Nne Kwa Kutumia Supu Ya Parachichi.

Ipo idadi  kubwa  duniani  ya  watu  wanao  kabiliwa  na  tatizo  la  kuwa  na  kitambi, wanawake  kwa  wanaume.

Kwa  mujibu  wa tafiti  mbalimbali  za  kitaalamu, kuwa  na  kitambi  ni  lugha  ya  mwili  ( body-language )  inayo  leta  ujumbe  kwako  kwamba  “ Mwili    wako  haupo  salama  tena “

Kama  una  kitambi   maana  yake  una  mafuta  yasiyo  hitajika  mwilini. Mwili  wako  unatumika  kuhifadhi  mafuta  usiyo  yahitajika.

Hali  hii  kitabibu  imaanisha  kwamba, ogani  nyinginezo  zilizomo  ndani  ya  mwili  wako  zinao gelea  kwenye  mafuta( fats  )  yasiyo  hitajika   yaliyomo ndani  ya  mwili  wako,  jambo  linalo  kuweka  katika  hatari  kubwa  sana  ya  kushambuliwa  na  magonjwa  hatari  kama  vile  shinikizo  kubwa  la  damu, matatizo  katika  moyo, kiharusi  na kisukari  na  kwa kutaja  machache.

Hivyo  basi  ili  kuondokana  na  hatari  hiyo, yakupasa   kupambana  kuondoa  hayo  mafuta  yasiyo  hitajika  mwilini  mwako.

Kusoma zaidi tembelea :
 


Share:

Primary Teacher Job Vacancy at Christ Church International School

Seeking enthusiastic teachers with a heart for missions! Now accepting applications for lower and upper primary lead teaching positions beginning August 2020. Applicants must be willing to teach on-campus in Tanzania or by distance learning using Google classroom (as deemed necessary by school management due to the coronavirus). The school is located in the foothills […]

The post Primary Teacher Job Vacancy at Christ Church International School appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Trainee Job vacancy at YARA Tanzania

About The Unit YARA Tanzania is duly registered company under the Laws of Tanzania as a subsidiary of Fertilizers Holdings AS. with headquarters in Dar es Salaam. The aim is developing a market concept that increase the number of farmers that use fertilizer in Tanzania including better knowledge in plant nutrition, improved distribution and logistics. […]

The post Trainee Job vacancy at YARA Tanzania appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

ASSISTANT PHARMACEUTICAL TECHNICIAN- 2 POSITIONS at Tanzania Red Cross Society

ASSISTANT PHARMACEUTICAL TECHNICIAN- 2 POSITIONS Duty Station: Nyarugusu Camp (Kasulu DC) and Mtendeli Camp (Kakonko DC) Reports to: PHARMACEUTICAL TECHNICIAN Age Limit: Not Above 50 Years MAJOR RESPONSIBILITIES  Supervises and coordinates the delivery of pharmaceutical care to patients of the hospital.  Distribution and monitoring of prescribed therapy which provide positive patient outcomes. All […]

The post ASSISTANT PHARMACEUTICAL TECHNICIAN- 2 POSITIONS at Tanzania Red Cross Society appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

5 FOOD DISTRIBUTORS at Tanzania Red Cross Society

FOOD DISTRIBUTOR – 5 POSITIONS Duty Station: Nyarugusu Camp (Kasulu Dc) and Mtendeli Camp (Kakonko Dc) Reports to: FOOD DISTRIBUTION SUPERVISOR Age Limit: Not Above 50 Years. MAJOR RESPONSIBILITIES  Supervision of Blanket Supplementary Feeding Programme (BSFP) to children 6-23 months during distribution  Provision of health nutrition education during BSFP distributions  Provision of […]

The post 5 FOOD DISTRIBUTORS at Tanzania Red Cross Society appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

2 FBM ASSISTANT DATA CLERKS at The Tanzania Red Cross Society

The Tanzania Red Cross Society is a voluntary humanitarian organization established as an independent National Society (NS) by an Act of Parliament No. 71 of December 1962 amended by Parliament of Tanzania 2019. Tanzania Red Cross Society was recognised and admitted to the membership of the International Federation of the Red Cross and Red Crescent […]

The post 2 FBM ASSISTANT DATA CLERKS at The Tanzania Red Cross Society appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

PHARMACEUTICAL ASSISTANT – DRUG DISPENSER (3-POSITIONS) at Tanzania Red Cross Society

PHARMACEUTICAL ASSISTANT – DRUG DISPENSER (3-POSITIONS) Duty Station: Nyarugusu Camp (Kasulu Dc) and Mtendeli Camp (Kakonko Dc) Reports to: PHARMACEUTICAL TECHNICIAN Age Limit: Not Above 50 Years MAJOR RESPONSIBILITIES  Distribution and monitoring of prescribed therapy which provide positive patient outcomes.  Dispensing of pharmaceutical products  Ensure efficiently and effectively Storage of pharmaceutical products […]

The post PHARMACEUTICAL ASSISTANT – DRUG DISPENSER (3-POSITIONS) at Tanzania Red Cross Society appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

2 FOOD BASKET MONITORING SUPERVISORS at The Tanzania Red Cross Society

The Tanzania Red Cross Society is a voluntary humanitarian organization established as an independent National Society (NS) by an Act of Parliament No. 71 of December 1962 amended by Parliament of Tanzania 2019. Tanzania Red Cross Society was recognised and admitted to the membership of the International Federation of the Red Cross and Red Crescent […]

The post 2 FOOD BASKET MONITORING SUPERVISORS at The Tanzania Red Cross Society appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Taarifa Kwa Umma Kutoka Mamlaka ya Mawasiliano -TCRA:Ufafanuzi wa URASIMISHAJI wa Laini za Ziada katika Mtandao Mmoja

1.0 UTANGULIZI
Kanuni za Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (Usajili wa Laini za Simu) za mwaka 2020, yaani “The Electronic and Postal Communications (SIM Card Registration) Regulations, 2020”, zimeainisha katika Kanuni ya 18 kuwa:-

18 (1) Mtu anayehitaji kumiliki na kutumia laini ya simu ataruhusiwa kusajili:-

(a) Kama ni mtu binafsi

    Idadi ya laini moja kwa kila mtoa huduma za mawasiliano kwa ajili ya kupiga simu za sauti, kutuma ujumbe mfupi pamoja na matumizi ya data;
    Idadi ya laini zisizozidi nne kwa kila mtoa huduma za mawasiliano

kwa matumizi ya mawasiliano kati ya mashine na mashine; na

(b) Kama ni Kampuni au Taasisi

    Idadi ya laini zisizozidi thelathini kwa kila mtoa huduma za mawasiliano kwa ajili ya kupiga simu za sauti, kutuma ujumbe mfupi pamoja na matumizi ya data;
    Idadi ya laini zisizozidi hamsini kwa kila mtoa huduma za mawasiliano kwa matumizi ya mawasiliano kati ya mashine na mashine.

(2) Laini zilizosajiliwa kwa matumizi yaliyoainishwa kwenye Kanuni 18 (1) (a) hazipaswi kutumiwa kwa kubadilishana (interchangebly).

(3) Bila kujali Kanuni ya 18 (1), Mtu binafsi, Kampuni au Taasisi inaweza kuruhusiwa kusajili na kumiliki laini zaidi ya zilizoainishwa kwa kuomba na kupata idhini kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania

(4) Mtu yeyote atakayekiuka masharti ya Kanuni hizi, atakuwa ametenda kosa la jinai.

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) inapenda kuutaarifu umma kwamba zoezi la kuomba idhini ya umiliki wa laini za simu zaidi ya moja katika mtandao mmoja linaendelea. Tunawashauri wamiliki wa laini za mawasiliano ya simu kuendelea kuhakiki usajili wa laini zao zote wanazomiliki.

2.0 KUTHIBITISHA IDADI YA LAINI ZILIZOSAJILIWA KUTUMIA KITAMBULISHO CHA TAIFA (NIDA)

2.1 Kila mmiliki wa laini ya simu anatakiwa kupiga namba *106# na kuangalia usajili wa laini anazomiliki na endapo atakuta namba ambayo haitambui na imesajiliwa kwa kutumia namba ya kitambulisho chake cha Taifa anashauriwa kuwasiliana na mtoa huduma wake ili azifunge mara moja kuepusha matumizi mabaya na kumsababishia usumbufu usiokuwa wa lazima utakaojitokeza.

2.2 Kwa wale ambao kwa sasa wanamiliki laini zaidi ya moja katika mtandao mmoja, mwisho wa kuhakiki laini zao itakuwa tarehe 31 Julai 2020.

2.3 Utaratibu wa kuomba idhini ya kumiliki laini mpya za ziada katika mtandao mmoja unaendelea na mteja anaweza kupata huduma hii kupitia kwa wakala au kwenye ofisi za watoa huduma ambapo kwa kutumia njia za kielektroniki mtoa huduma atawasilisha maombi ya mteja wake TCRA kwa idhini ya kusajili na kumiliki laini za ziada; mteja atapokea majibu ya maombi yake ndani ya takribani dakika tano.

3.0 URASIMISHAJI WA LAINI ULIZOTHIBITISHA

3.1 Urasimishaji wa laini za ziada kwa sasa unaweza kufanyika kwa wakala au kwenye ofisi za watoa huduma ambapo kwa kutumia njia za kielektroniki ambapo mtoa huduma atawasilisha maombi yake ya idhini ya kurasimisha laini za ziada TCRA na kupokea majibu ndani ya takribani dakika tano; au

3.2 Kwa kupitia namba *106# ambapo wewe mwenyewe utaweza kuomba idhini ya kurasimisha kutoka TCRA kupitia simu yako. Huduma hii ya kurasimisha kwa njia ya simu yako itaanza kutumika rasmi Agosti 1, 2020.

Imetolewa na:

Mkurugenzi Mkuu, 
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)




Share:

TAKUKURU wilaya ya Kiteto yasaidia kurejesha Mahindi ya Kijiji.

Na John Walter-Manyara
Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa  wilaya ya Kiteto mkoa wa  Manyara ,imefanikiwa kurejesha  mahindi gunia 45 katika kijiji cha Loltepes.

Mkuu wa TAKUKURU wilaya ya Kiteto Venance Sangawe amesema mahindi  hayo ni sehemu ya gunia 90 ambazo Takukuru  iliingilia kati kurejesha.

Sangawe amesema  diwani wa kata ya Sunya  aliemaliza muda wake, Musa Brayton na mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi  katika  kata hiyo Abdi  Puputo  walishindwa kutimiza masharti waliyokubaliana na kijiji  ya  kulipa mahindi hayo baada ya kulima shamba la kijiji  ekari tisini.

Ameongeza kuwa makubaliano kati ya watu hao na kijiji ilikuwa ni kulipa  gunia moja kwa kila ekari tangu mwaka 2017  hivyo kwa kushindwa kufanya hivyo Takukuru imeamua kuisaidia kijiji kurejesha mahindi hayo.

Akikabidhi mahindi hayo kwa mwenyekiti wa kijiji cha Loltepes Mkuu wa wilaya ya Kiteto Tumaini Magessa,  amewataka viongozi wa kijiji na shule kuhakikisha mahindi hayo yanatumika kwa ajili ya chakula cha wanafunzi wa shule za Loltepes na Loiborsoit zilizopo katika kijiji hicho.

Huo ni mwendelezo wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa mkoa wa Manyara katika kurejesha na kukabidhi mali kwa wahusika halali ili  kuondoa  migogoro isiyokuwa ya lazima.


Share:

Waziri Lukuvi Awashukia Viongozi Wapora Ardhi

Na Munir Shemweta, WANMM KATAVI
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amekerwa na tabia ya baadhi ya viongozi kuhusika kupora ardhi ya wananchi na kueleza kuwa muarobaini wa viongozi hao umefika kufuatia watendaji wa sekta ya ardhi kuhamishiwa Wizarani sambamba na kuanzishwa ofisi za ardhi katika mikao.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi alisema hayo wakati wa kuzindua ofisi ya ardhi mkoa Katavi wilayani Mpanda jana ikiwa ni mfululizo wa uzinduzi wa ofisi za ardhi kwenye mikoa mbalimbali nchini.

Alisema, wapo baadhi ya viongozi wa wilaya na mkoa ambao ni sehemu ya migogoro ya ardhi na wamekuwa wakitumia madaraka yao vibaya kwa kupora na kuuza ardhi za wananchi tabia aliyoieleza kuwa inamkera rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli.

Kwa mujibu wa Lukuvi, uanzishwaji ofisi za ardhi za mikoa pamoja na uhamishaji watendaji wa sekta ya ardhi kutoka TAMISEMI kuja Wizarani unatoa nguvu kwa watumishi wa sekta ya ardhi kutumia na  kusimamia sheria na kuonya viongozi kutojihusisha na kupora ardhi za wananchi na kubainisha kuwa ardhi itapangwa na kusimajiwa kwa mujibu wa sheria.

‘’ Kuna viongozi wa kuchaguliwa na wa kuteuliwa wanaotumia madaraka yao vibaya kwa kupora ardhi za wananchi, safari hii hakuna fursa maana watendaji wote wa sekta ya ardhi wako chini ya Wizara ya ardhi, madiwani hawawezi tena kuwaazimia  kuwafukuza.’’ alisema Lukuvi

Akizungumzia suala la upimaji ardhi katika mkoa wa Katavi, Lukuvi aliagiza hadi kufikia mwisho wa mwaka huu 2020 vijiji vyote katika mkoa huo viwe vimepimwa na kupatiwa hati za kijiji sambamba na wamiliki 15,000 waliokwama kupewa hati kutokana na urasimu kupatiwa hati zao na kuweka wazi kuwa, hivi sasa hakuna visingizio kwa kuwa vifaa kwa ajili ya upimaji vipo.

Agizo la Lukuvi linafuatia kuelezwa na Kamishna Msaidizi wa Ardhi mkoa wa Katavi Siyabumi Mwaipopo kuwa kati ya vijiji 172 vilivyopo kwenye mkoa wa Katavi ni vijiji vitatu tu ndivyo vilivyopimwa na kupatiwa hati za vijiji.

‘’Mwaka huu uwe wa mwisho kwa migogoro ya ardhi nchini kwani nyenzo zote zipo ikiwemo wataalamu pamoja na vifaa vifaa vya upimaji na nawataka viongozi wa wilaya na mkoa wasiwe sehemu ya migogoro’’ alisema Lukuvi.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula alisisitizia suala la ukusanyaji maduhuli ya serikali kupitia kodi ya pango la ardhi ambapo alisema ni muhimu wamiliki wa ardhi wakaepuka kuwa na malimbikizo ya kodi ya ardhi kwa kutii sheria ya kulipa kodi mujibu wa sheria.

Naye Mkuu wa mkoa wa Katavi Juma Homera mbali na kushukuru uamuzi wa kuanzisha ofisi ya ardhi katika mkoa wake, aliwataka wananchi wa Katavi kuitumia fursa ya kuwa na ofisi ya ardhi ya mkoa kupima ardhi na kumilikishwa na kusisitiza kuwa mkoa wake utaandaa opresheni maalum ya kupima ardhi katika mkoa mzima.

Uzinduzi ofisi ya ardhi mkoa wa Katavi uliambatana na makabidhiano ya vifaa mbalimbali ambapo Waziri Lukuvi alikabidhi gari lenye thamani ya shilingi milioni 150 pamoja na vifaa vya upimaji kwa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi kwa lengo la kurahisisha utendaji kazi wa sekta ya ardhi kwenye halmashauri hiyo.


Share:

Rais wa Urus Vladimir Putin ashinda kura ya maoni; atabakia madarakani hadi 2036

Rais wa Urus Vladimir Putin ameshinda kura ya maoni ambayo itamuwezesha kubakia madarakani hadi 2036

Putin mwenye  umri  wa  miaka  67, amekuwa  madarakani kama rais na  pia  waziri  mkuu  kwa  miongo  miwili  na  kwa  hivi  sasa  ni  rais aliyedumu  nchini Urusi kwa  kipindi  kirefu  zaidi

Kura ya maoni ilitaka  kuidhinishwa kwa mabadiliko ya katiba ambayo  yatamuwezesha Putin  kugombea  tena  katika  uchaguzi mara  mbili  zaidi  na  kuweza  kubakia  madarakani  hadi  akiwa  na umri  wa  miaka  83. Muhula  wake  wa  hivi  sasa  unamalizika miaka  minne  ijayo. Mwenyekiti wa  tume  ya  uchaguzi  ya  Urusi Ella Pamfilova  amesema.

Putin amejijengea umaarufu  kuwa  ni  mlinzi na  kiongozi  anayeweza kuleta  uthabiti  nchini humo, kinyume  na  hali  ya  kuyumba kwa uchumi na  kisiasa  katika  kipindi  baada  ya  iliyokuwa  jamhuri  ya kisovieti  katika  miaka  ya  1990 ambayo  imekuwa  kabla  ya kuingia  kwake  madarakani.

-DW


Share:

Waziri Wa Fedha Dr. Mpango Amtaka Mkandarasi Hospitali Ya Wilaya Ya Buhigwe - Kigoma Kuzingatia Ubora

Na. Josephine Majula na Peter Haule, WFM, Kigoma
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango, ameuagiza uongozi wa Mkoa wa Kigoma kumsimamia ipasavyo mkandarasi anayejenga Hospitali ya Wilaya ya Buhigwe mkoani humo, baada ya kutoridhishwa na ubora wa majengo ikilinganishwa na kiasi cha shilingi bilioni 2.4 zilizotumika mpaka hivi sasa kujenga moiundombinu ya Hospitali hiyo.

Dkt. Mpango alitoa agizo hilo wakati alipotembelea na kukagua Mradi wa Ujenzi wa Hospitali hiyo ya Wilaya ambayo licha ya miundombinu yake kutokamilika ipasavyo imeanza kutoa huduma kwa wananchi kuanzia mwezi Juni, 2020.

 “Ubora wa majengo hauendani na matarajio, inatakiwa iwe Hospitali ya Wilaya ya Kisasa kabisa hivyo muongeze usimamizi wa Mkandarasi, nitarudi tena hapa mwezi wa nane na mkandarasi afikishiwe salamu kuwa Waziri hakufurahishwa na ubora wa kazi kwa kuwa nikirudi nitaangali pia na thamani ya fedha kama fedha za wananchi zimewaletea kitu kinacholingana na fedha tulizotoa”, alieleza Dkt. Mpango.

Dkt. Mpango alisema kuwa fedha ya wananchi haitakiwi kuchezewa kwa kuwa wanatozwa kodi hivyo inatakiwa kurudi kwao kwa kuwaletea huduma ambazo zinafanana na thamani ya jasho lao.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe, Kanali Michael Ngayalina alisema atayafanyia kazi maelekezo ya Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mpango, na pia akamuomba kusaidia kuwezesha mradi huo kukamilika ili utoe huduma stahiki kwa wananchi kwa kuwa Waziri huyo amefika na kujionea hali halisi ya huduma zinazotolewa.

Aidha alimshukuru Dkt. Mpango kwa kuendelea kufanya ziara katika Wilaya hiyo na kukagua miradi inayopatiwa fedha na Serikali na kuchukua hatua zitakazowezesha kupata thamani ya fedha za miradi.

Naye Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Buhigwe, Bw. Fredrick Kanyondwi, alisema kuwa kiasi cha Sh. bilioni 2. 7 kilipokelewa kwa awamu nne na Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali hiyo ambayo imeanza kutoa huduma kuanzia Juni, 2020 kwa kutumia miundombinu iliyopo wakati ikisubiriwa kukamilika ili kutoa huduma kwa ufanisi.

Alisema ujenzi wa majengo ya Hospitali yametumia mfumo wa Force Acount ambapo jengo la Maabara limekamilika kwa asilimia 95, Mama na mtoto asilimia 87, utawala asilimia 99, jengo la wagonjwa wa nje asilimia 99 na majengo mengine kama la mionzi, jengo la dawa na kufulia ambayo kwa ujumla yametumia takribani Sh. bilioni 2.4.

Bw. Kanyondwi alisema kuwa bado kuna upungufu wa takribani Sh. milioni 200 baada ya  ya Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe kubaini upungufu wa Sh. milioni 500 ambapo mwezi Juni zilitolewa Sh. milioni Sh. milioni 300 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi huo na kusalia shilingi milioni 200 ambazo zinahitajika ili kukamilisha ujenzi huo.

MWISHO


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger