Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Mhe. Hoja Mahiba akizungumza wakati akizindua Mradi wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto katika Kipindi cha Mlipuko wa Homa Kali ya Mapafu ‘COVID - 19’
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Mhe. Hoja Mahiba amezindua Mradi wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto katika Kipindi cha Mlipuko wa Homa Kali ya Mapafu ‘COVID - 19’ utakaotekelezwa katika kata 10 za halmashauri hiyo kwa ufadhili wa Shirika lisilo la kiserikali la Women Fund Tanzania (WFT).
Mradi huo utakaotekelezwa na Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga kwa kushirikiana na Mashirika matatu yasiyo ya kiserikali ambayo ni Investing in Childrean and Societies (ICS Africa), Thubutu Africa Initiatives (TAI) na Rafiki SDO umezinduliwa leo Jumanne Juni 30,2020 katika ukumbi wa Hospitali ya wilaya ya Shinyanga uliopo katika kata ya Iselamagazi.
Akizungumza wakati wa kufungua mradi huo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Mhe. Hoja Mahiba amesema suala la ukatili wa kijinsia ni suala mtambuka hivyo ni jukumu la kila mmoja kuhakikisha anapiga vita vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
“Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali tunaendelea na mapambano dhidi ya Corona,lakini tukiwa katika harakati hizo bado ukatili wa kijinsia unaendelea na inawezekana katika kipindi hiki tukawa na ukatili wa namna tofauti tofauti japokuwa katika mradi huu tutalenga zaidi kundi la wanawake na watoto”,alisema Mahiba.
“Niwashukuru sana Women Fund Tanzania kwa kutuwezesha ruzuku kupambana na ukatili wa kijinsia katika kipindi hiki cha Corona na tujipongeze wale tuliopata ruzuku, tukaitendee haki fedha tuliyopewa ili kuondokana na vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto. Naamini kabisa maeneo yaliyopata ruzuku yatatumika kama kata za mfano”,alisema Mahiba.
Naye Mratibu wa Mradi wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto kutoka Shirika la Women Fund Tanzania (WFT), Glory Mbia alisema shirika hilo linafanya kazi kwa kushirikiana na serikali ndiyo limetoa fedha za ruzuku kwa halmashauri ya Shinyanga katika jitihada za kupambana na athari zilizowakumba wanawake, mabinti na watoto katika kipindi cha mlipuko wa Corona kilichopelekea wanafunzi kukaa majumbani kwa zaidi ya miezi mitatu na baadhi ya shughuli za kila siku kubadilika.
“Yapo mengi yaliyojiri wakati wa COVID -19. Sisi tunalenga zaidi katika kipindi cha baada ya Corona,kuna maisha baada ya COVID -19 na tunajaribu kuangalia walengwa wetu ambao ni wanawake na watoto.Kuna changamoto gani walizipitia na hizo changamoto zinaweza kuwaathiri vipi nasi tunasaidiaje haya makundi ili yaweze kurudi katika maisha yao ya kawaida na kuishi katika hali iliyopo kwa mujibu wa miongozo inayotolewa na serikali”,alisema Mbia.
“Mwanzoni mwa Mwezi Aprili tulitoa matangazo watu waombe ruzuku,waliomba watu wengi nchi nzima. Mchakato ulifanyika kwa uhuru na uwazi kwa mujibu wa vigezo vilivyoainishwa wakati wa tangazo na kwa eneo letu hili la mradi tukafanikiwa kupata shirika la Rafiki SDO, Thubutu Africa Initiatives, ICS na halmashauri ya wilaya ya Shinyanga”,alisema Mbia.
Naye Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Edmund Ardon alisema lengo la Mradi wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto katika Kipindi cha Mlipuko wa Homa Kali ya Mapafu ‘COVID - 19’ utakaotekelezwa kuanzia Julai 1,2020 hadi Septemba 2020 ukigharimu takribani shilingi milioni 60 ni kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Alizitaja kata zitakazonufaika na mradi huo kuwa ni Bukene, Didia, Mwantini, Iselamagazi, Pangagichiza, Mwakitolyo, Salawe, Lyabukande, Lyabusalu na Solwa.
Nao Mameneja Miradi kutoka Mashirika yaliyopata Ruzuku, Paschalia Mbugani (Thubutu Africa Initiatives), Sabrina Majikata (ICS) na George Nyanda (Rafiki SDO) waliishukuru WFT kwa kuwapatia ruzuku na kueleza kuwa wamejipanga vizuri kuhakikisha mradi huo unatekelezwa kikamilifu.
Kikao kazi hicho cha Kutambulisha mradi kimehudhuriwa na wajumbe wa kamati ya watalaamu wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga (CMT),Maafisa Maendeleo ya Jamii kutoka kata 26 za halmashauri hiyo, Wajumbe wa kamati ya usimamizi wa mradi kutoka WFT,mashirika watekelezaji wa mradi na mashirika yanayofanya kazi za utetezi wa haki za wanawake na watoto.
ANGALIA PICHA ZA MATUKIO HAPA CHINI
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Mhe. Hoja Mahiba akizungumza leo Jumanne Juni 30,2020 wakati wa kuzindua Mradi wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto katika Kipindi cha Mlipuko wa Homa Kali ya Mapafu ‘COVID - 19’ utakaotekelezwa na Shirika la Investing in Childrean and Societies (ICS Africa), Thubutu Africa Initiatives (TAI) na Rafiki SDO katika kata 10 za halmashauri hiyo kwa ufadhili wa Shirika lisilo la kiserikali la Women Fund Tanzania (WFT). Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Mhe. Hoja Mahiba akiyahamasisha mashirika ya Investing in Childrean and Societies (ICS Africa), Thubutu Africa Initiatives (TAI) na Rafiki SDO kutumia vizuri fedha zilizotolewa na WFT kwa ajili ya Mradi wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto katika Kipindi cha Mlipuko wa Homa Kali ya Mapafu ‘COVID - 19’.
Wadau wa haki za wanawake na watoto wakimsikiliza Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Mhe. Hoja Mahiba wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto katika Kipindi cha Mlipuko wa Homa Kali ya Mapafu ‘COVID - 19’.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Mhe. Hoja Mahiba akiwataka wadau mbalimbali kushiriki katika mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia na kuwa mstari wa mbele kutoa taarifa za matukio ya ukatili pamoja na kutoa ushahidi pindi matukio ya ukatili yanapofanyika. Kushoto ni Afisa Maendeleo ya Jamii halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Deus Muhoja.
Mratibu wa Mradi wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto kutoka Shirika la Women Fund Tanzania (WFT), Glory Mbia akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto katika Kipindi cha Mlipuko wa Homa Kali ya Mapafu ‘COVID - 19’ utakaotekelezwa na Shirika la Investing in Childrean and Societies (ICS Africa), Thubutu Africa Initiatives (TAI) na Rafiki SDO kwa ufadhili wa Shirika lisilo la kiserikali la Women Fund Tanzania (WFT).
Mratibu wa Mradi wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto kutoka Shirika la Women Fund Tanzania (WFT), Glory Mbia akielezea namna shirika hilo linavyoshirikiana na serikali katika jitihada za kupambana na Corona kwa kuangalia kundi la wanawake na watoto.
Mjumbe wa kamati ya usimamizi wa mradi kutoka WFT, Irene Laulent kutoka kata ya Usanda katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga akiwahamasisha wazazi na walezi kukaa karibu na watoto wao wa kike na kueleza madhara ya kufanya ngono na kusaidia watoto pindi wanapofanyiwa vitendo vya ukatili.
Afisa Maendeleo ya Jamii halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Deus Muhoja akielezea namna watakavyotekeleza Mradi wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto katika Kipindi cha Mlipuko wa Homa Kali ya Mapafu ‘COVID - 19’ .
Wadau wa haki za wanawake na watoto wakiwa ukumbini wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto katika Kipindi cha Mlipuko wa Homa Kali ya Mapafu ‘COVID - 19’.
Wadau wa haki za wanawake na watoto wakiwa ukumbini wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto katika Kipindi cha Mlipuko wa Homa Kali ya Mapafu ‘COVID - 19’.
Wadau wa haki za wanawake na watoto wakiwa ukumbini wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto katika Kipindi cha Mlipuko wa Homa Kali ya Mapafu ‘COVID - 19’.
Wadau wa haki za wanawake na watoto wakiwa ukumbini wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto katika Kipindi cha Mlipuko wa Homa Kali ya Mapafu ‘COVID - 19’.
Meneja Miradi wa Shirika la ICS ,Sabrina Majikata akielezea namna shirika hilo lilivyojipanga kutekeleza Mradi wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto katika Kipindi cha Mlipuko wa Homa Kali ya Mapafu ‘COVID - 19’ katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Meneja Miradi kutoka Thubutu Africa Initiatives akielezea namna shirika hilo lilivyojipanga kutekeleza Mradi wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto katika Kipindi cha Mlipuko wa Homa Kali ya Mapafu ‘COVID - 19’ katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Wadau wakiwa ukumbini.
Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Edmund Ardon akielezea namna shirika hilo lilivyojipanga kutekeleza Mradi wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto katika Kipindi cha Mlipuko wa Homa Kali ya Mapafu ‘COVID - 19’ katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Mratibu wa Mradi wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto katika Kipindi cha Mlipuko wa Homa Kali ya Mapafu ‘COVID - 19’ kutoka Shirika la Rafiki SDO, George Nyanda akielezea namna watakavyotekeleza mradi huo katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Afisa Maendeleo ya Jamii kata ya Mwalukwa, Elypendo John akielezea umuhimu wa kuwapa elimu ya kutoa ushahidi waathirika wa vitendo vya ukatili wa kijinsia ili vitendo vya ukatili viweze kutokomezwa katika jamii.
Afisa Maendeleo ya Jamii kata ya Samuye, Magai Deogratius akichangia hoja wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto katika Kipindi cha Mlipuko wa Homa Kali ya Mapafu ‘COVID - 19’.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la AGAPE ACP, John Myola akielezea uzoefu kuhusu namna ya kutekeleza miradi mbalimbali inayohusu wanawake na watoto. Alisema katika kipindi cha ugonjwa wa Corona shirika hilo limetoa vifaa vya kujikinga na maambukizi dhidi ya Corona ,elimu kuhusu Corona pamoja na masuala ya ukatili wa kijinsia.
Wadau wa haki za wanawake na watoto wakiwa ukumbini.
Wadau wa haki za wanawake na watoto wakiwa ukumbini.
Wadau wa haki za wanawake na watoto wakiwa ukumbini.
Wadau wa haki za wanawake na watoto wakiwa ukumbini.
Wadau wa haki za wanawake na watoto wakiwa ukumbini.
Wadau wa haki za wanawake na watoto wakiwa ukumbini.
Wadau wa haki za wanawake na watoto wakiwa ukumbini.
Wadau wa haki za wanawake na watoto wakiwa ukumbini.
Wadau wa haki za wanawake na watoto wakiwa ukumbini.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog