Wednesday, 3 June 2020

TRAINING ASSISTANT II (BAMBOO PRODUCTS) – 1 POST at SMALL INDUSTRIES DEVELOPMENT ORGANIZATION (SIDO

TRAINING ASSISTANT II (BAMBOO PRODUCTS) – 1 POST at SMALL INDUSTRIES DEVELOPMENT ORGANIZATION (SIDO POST TRAINING ASSISTANT II (BAMBOO PRODUCTS) – 1 POST POST CATEGORY(S) FARMING AND AGRIBUSINESS EMPLOYER SMALL INDUSTRIES DEVELOPMENT ORGANIZATION (SIDO) APPLICATION TIMELINE: 2020-05-20 2020-06-04 JOB SUMMARY N/A DUTIES AND RESPONSIBILITIES i.Conducts  on-the-job  training,  classes,  or  training  sessions  to  teach  and  demonstrate principles, techniques, procedures,… Read More »

The post TRAINING ASSISTANT II (BAMBOO PRODUCTS) – 1 POST at SMALL INDUSTRIES DEVELOPMENT ORGANIZATION (SIDO appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Unicef Jobs: Immunization Specialist,(NOC),Temporary Appointment (9 Months),Zanzibar,Tanzania

Immunization Specialist, Zanzibar, Tanzania Organization: Unicef Country: Tanzania City: Zanzibar, Tanzania Office: UNICEF Zanzibar Grade: NO-C Closing date: Thursday, 11 June 2020 Immunization Specialist,(NOC),Temporary Appointment (9 Months),Zanzibar,Tanzania #00113571 Job no: 531809 Position type: Temporary Appointment Location: Tanzania,Uni.Re Division/Equivalent: Nairobi Regn’l(ESARO) School/Unit: United Republic of Tanzania Department/Office: Zanzibar, United Rep. of Tanzania Categories: Child Protection, NO-3, Early Childhood Development, Expanded Programme Immunization, Programme Management UNICEF works in some of the world’s toughest… Read More »

The post Unicef Jobs: Immunization Specialist,(NOC),Temporary Appointment (9 Months),Zanzibar,Tanzania appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

ARTISAN (MASONRY) II – 1 POST at Mzumbe University

ARTISAN (MASONRY) II – 1 POST Employer: Mzumbe University   POST DETAILS POST ARTISAN (MASONRY) II – 1 POST POST CATEGORY(S) ENGINEERING AND CONSTRUCTION EMPLOYER Mzumbe University APPLICATION TIMELINE: 2020-06-01 2020-06-14 JOB SUMMARY N/A DUTIES AND RESPONSIBILITIES i.    To perform more challenging craft jobs under close supervision; ii.    To perform routine technical cleaning of the work environment; iii.   … Read More »

The post ARTISAN (MASONRY) II – 1 POST at Mzumbe University appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Head of Education Job vacancy at Plan International, Dar es Salaam

Head of Education, Dar es Salaam Organization: Plan International Country: Tanzania City: Dar es Salaam, Tanzania Office: Plan International Dar es Salaam, Tanzania Closing date: Sunday, 7 June 2020 The Organisation Plan International is an independent development and humanitarian organisation that advances children’s rights and equality for girls. We believe in the power and potential of every child. But this is often… Read More »

The post Head of Education Job vacancy at Plan International, Dar es Salaam appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

PATH Jobs: Strategic Information Management and Advocacy Officer, Tools for Integrated Management of Childhood Illness. (10049), Dar es Salaam, Tanzania

Strategic Information Management and Advocacy Officer, Tools for Integrated Management of Childhood Illness. (10049), Dar es Salaam, Tanzania Organization: Program for Appropriate Technology in Health (PATH) Country: Tanzania City: Dar es Salaam, Tanzania Office: PATH Tanzania Dar es Salaam Tracking Code 10049 Job Description Please include a cover letter with your resume describing your interest in the position and how you meet… Read More »

The post PATH Jobs: Strategic Information Management and Advocacy Officer, Tools for Integrated Management of Childhood Illness. (10049), Dar es Salaam, Tanzania appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

IntraHealth: Senior Advisor – Health Workforce Strengthening, Dar es Salaam, Tanzania

Senior Advisor – Health Workforce Strengthening, Dar es Salaam, Tanzania Organization: IntraHealth International Country: Tanzania City: Dar es Salaam, Tanzania Office: IntraHealth International Dar es Salaam Why Join IntraHealth? IntraHealth International is a global health nonprofit that has worked for 40 years in over 100 countries. We improve the performance of health workers and strengthen the systems in which they work so… Read More »

The post IntraHealth: Senior Advisor – Health Workforce Strengthening, Dar es Salaam, Tanzania appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

UNICEF Jobs: Individual National Consultant -To Develop the Decentralization by Devolution Support Programme 2 (DbDSP) 2020-2025, Zanzibar, Tanzania

Individual National Consultant -To Develop the Decentralization by Devolution Support Programme 2 (DbDSP) 2020-2025, Zanzibar, Tanzania Organization: Unicef Country: Tanzania City: Zanzibar, Tanzania Office: UNICEF Zanzibar Closing date: Sunday, 7 June 2020 Individual National Consultant -To Develop The Zanzibar Decentralization by Devolution Support Programme 2 (DbDSP) 2020-2025 Job no: 531868 Position type: Consultancy Location: Tanzania,Uni.Re Division/Equivalent: Nairobi Regn’l(ESARO) School/Unit: United Republic of Tanzania Department/Office: Zanzibar, United Rep. of Tanzania… Read More »

The post UNICEF Jobs: Individual National Consultant -To Develop the Decentralization by Devolution Support Programme 2 (DbDSP) 2020-2025, Zanzibar, Tanzania appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

UNICEF:Individual Consultant – Providing technical support to UNICEF Social Policy team (Remote), Dar es Salaam, Tanzania

Individual Consultant – Providing technical support to UNICEF Social Policy team (Remote), Dar es Salaam, Tanzania Organization: Unicef Country: Tanzania City: Dar es Salaam, Tanzania Office: UNICEF Tanzania Closing date: Sunday, 7 June 2020 Individual Consultant -Providing technical support to UNICEF Tanzania Social Policy team (Remote) Job no: 531984 Position type: Consultancy Location: Tanzania,Uni.Re Division/Equivalent: Nairobi Regn’l(ESARO) School/Unit: United Republic of Tanzania Department/Office: Dar Es Salaam, United Rep. of… Read More »

The post UNICEF:Individual Consultant – Providing technical support to UNICEF Social Policy team (Remote), Dar es Salaam, Tanzania appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

WAZIRI WA ELIMU ATOA SIKU TATU KWA VYUO VIKUU WAPEWE FEDHA ZA KUJIKIMU


Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof Joyce Ndalichako ametoa muda wa hadi kufika Ijumaa wiki hii ambayo itakuwa Juni 5, 2020, vyuo vyote vya elimu ya juu hapa nchini viwe vimemaliza kuwapa fedha za kujikimu wanafunzi wote na si vinginevyo.

Amesema hayo leo Juni 6, 2020 wakati akizungumza baada ya kukabidhi magari manne kwa chuo cha taifa cha usafirishaji (NIT).

Ndalichako amesema, serikali haitakuwa na mswalia mtume katika hili kwa kuwa tayari ilishatoa fedha hizo na hakuna sababu ya kuchelewa kuwapa wanafunzi fedha hizo

"Hakuna sababu ya kuwacheleweshea fedha wanafunzi wakati serikali imeshatoa Sh.bil 122.Rais alishatoa maelekezo na lazima yatekelezwe.Sasa ole wao vyuo vitakavyokuwa havijatekeleza agizo .Suala la wanafunzi kukataa kusaini siyo kweli, hatutakuwa na msalia mtume.

"Ifikapo Ijumaa wiki hii wanafunzi wote wa vyuo vikuu wawe wameshapata fedha zao za kujikimu, hatutakuwa na msamaha kwa vyuo ambavyo vitakuwa havijatekeleza agizo hilo.

"Kama kutakuwa na wanafunzi ambao watakuwa hawajasaini fedha za kujikimu achaneni nao, wapeni ambao wameshaini"-Waziri wa elimu, Prof. Joyce Ndalichako

Vyuo vimefunguliwa Juni 1, 2020 baada ya kusimama  kutokana na janga la Corona. Serikali tayari imeshathibitisha kuingiza fedha za mikopo kwa wanafunzi hivyo kuacha jukumu kwa vyuo kukamilisha kuwapatia wanafunzi.



Share:

GGML YATOA MILIONI 100 UJENZI WA CHUO KIKUU HURIA – GEITA


Makamu Rais wa GGML, Simon Shayo
Na Mwandishi Wetu
Katika kukuza sekta ya elimu ya juu nchini, Kampuni ya Geita Gold Mining Ltd. (GGML) kupitia sera yake ya uwajibikaji kwa jamii imetoa kiasi cha Sh milioni 100 kusaidia ujenzi wa Kituo cha Chuo Kikuu Open University cha Mkoa wa Geita. 

Awamu ya kwanza ya mradi huo inajumuisha ujenzi wa jengo la utawala linalojumuisha chumba mikutano cha viongozi, maktaba, chumba cha maabara ya kompyuta na ofisi nyingine tano. 

Pia kiasi hicho cha pesa kilichotolewa na GGML ni kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya ujenzi na malipo ya mafundi ujenzi. 

Akizungumzia mradi huo, Makamu Rais - Maendeleo Endelevu katika kampuni hiyo, Simon Shayo alisema uwezeshaji huu unatarajiwa kufaidisha wanafunzi 500 wanaotokea katika vituo vitatu vya Mkoa wa Geita ambavyo ni Chato, Nyang’wale na Geita mjini. 

Alisema GGML kwa kushirikiana na wananchi imeamua kuunga mkono juhudi za serikali kufadhili mradi huo kwani mbali na kuongeza mazingira bora ya upatikanaji wa elimu pia utazalisha wahitimu bora wenye weledi ndani ya jamii wataokuwa na uwezo wa kusukuma gurudumu la maendeleo ya Taifa mbele kwa kupitia elimu waliyoipata. 

Alisema Chuo cha Open University - Geita, kama vilivyo vyuo vingine kimekuwa kikifanya shughuli zake katika majengo ya kukodi ambayo hutumika kama madarasa na ofisi za utawala. 

“Mradi huu unaifanya Geita kuwa mkoa wa (1, 2, 3) katika ukanda wa ziwa na wa (2, 10, 20) nchini Tanzania kunufaika na miundombinu inayomilikiwa wa Open University. 

"Kwa ufadhili huu, tuna hakika kwamba chuo kikuu kitapunguza gharama za uendeshaji na kuboresha ufanisi. Zaidi ya hayo itaunda uhusiano mzuri kati ya wanafunzi kutoka Geita na vyuo vingine 30 vya Open University Tanzania. Mradi huu moja kwa moja unasaidia Serikali kufikia lengo la 4 la maendeleo endelevu (SDGs), ambalo ni upatikanaji wa elimu bora ifikapo 2030 kama ilivyotarajiwa ”alisema Shayo. 

Aidha, Mkurugenzi wa Open University Geita, Ally Abdu aliishukuru GGML kwa msaada huo ambao unaongeza mazingira mazuri ya kusoma na kukidhi idadi ya wanafunzi wa elimu ya juu ambao wanaongezeka kila mwaka. 

"Malengo ya Chuo kikuu huria ni kutoa elimu inayofaa na yenye ubora, elimu iliyo rahisi kupatikana na nafuu kwa njia ya mtandao. Elimu iliyojitosheleza kwa tafiti zenye kutoa suluhu ya matatizo ndani ya jamii kwa maendeleo ya uchumi wa Tanzania na dunia kwa ujumla. 

“Kupitia msaada huu wa GGML, sasa tuna uhakika kwamba tutapunguza gharama zetu za uendeshaji na kuboresha ubora wa elimu katika tawi letu la Geita, " alisema Ally. 

Hata hivyo, Shayo aliongeza kuwa kufuatia marekebisho ya Sheria ya Madini mwaka 2017, Kampuni ya Dhahabu ya Geita kupitia mpango wake wa uwajibikaji kwa jamii imeungana na serikali za mitaa za Geita kutekeleza miradi ya jamii yenye thamani ya Sh bilioni 18 katika Mkoa wa Geita. 

“Kabla ya marekebisho GGML ilikuwa imewekeza kihistoria katika miradi endelevu ya kimkakati kwa jamii ikiwa ni pamoja na shule ya Sekondari ya Wasichana ya Nyankumbu, mradi wa maji safi wa mji wa Geita na mradi wa Kilimanjaro Challenge unaolenga kutokomeza maambukizi ya VVU/UKIMWI nchini,” alisema. 

Share:

Mtangazaji Maarufu wa Clouds FM Hamisi Mandi (B Dozen ) atimkia E-FM

Aliyekuwa mtangazaji wa kituo cha Redio cha Clouds FM Hamis Mandi maarufu B Dozen amejiunga na Kituo cha redio cha EFM- Tanzania

Mandi ambaye anafahamika zaidi kwa jina la utangazaji la B-Dozen (The Navigator, Msafiri) kwa muda mrefu alikuwa akiongoza kipindi cha XXL cha Clouds FM, pamoja na vingine.

Kupitia ukurasa wao wa Instagram, E-FM wameandika mbobezi huyo wa utangazaji amejiunga nao, na kwamba kinachofuata ni kupaa juu, na kuhakikisha mafanikio zaidi kwa Tanzania.


Share:

WASIOSHIRIKI MISIBA SASA KUCHARAZWA VIBOKO

Diwani wa Kata ya Mwangata, Manispaa ya Iringa, Edward Nguvu


Na Zuhura Zukheir, Iringa
Wakazi wa Kata ya Mwangata, Manispaa ya Iringa wamepongeza uamuzi wa Diwani wa Kata ya Mwangata, Edward Nguvu kutaka watu wasiohudhuria misibani wacharazwe viboko ili iwe fundisho kwa wengine.

Akizungumza na Majira kwa niaba ya wananchi wenzake, mmoja wa wananchi hao amesema hivi sasa kumekuwa na tabia ya waombolezaji kwenye kata hiyo kuchagua misiba, jambo ambalo halikubaliki hata kidogo.

Mwananchi huyo ambaye hakutaka jina lake kutochapishwa gazetini amesema zamani mwitikio wa wananchi kushiriki misibani ulikuwa mkubwa, lakini sasa hivi ni kinyume, ndiyo maana wanaunga ushauri wa diwani wao.

Diwani Nguvu alishauri watu hao wawe wanacharazwa viboko jana alipohudhuria mazishi ya mkazi wa kata hiyo, Wilbart Mgongolwa yaliyofanyika katika makaburi ya Mlolo Mjini hapa.

Amesema baadhi ya watu wamekuwa wakiendekeza majukumu yao ya kimaisha na kutojihusisha na shida za kijamii kama kushiriki shughuli za misiba na mazishi

Ameongeza kwamba vijana wamekuwa wakikimbilia kwenye misiba ya jamaa zao kwa kwenda kuchimba kaburi, huku misiba mingine wakiachiwa wahusika wenyewe hali inayoelezwa kuleta mpasuko ndani ya jamii.

Ametolea mfano msiba wa Wilbert Mgongolwa, Diwani Nguvu alisema watu wengi hawakuhudhuria katika msiba huo kwa dharau au kutokuwa na msukumo kutoka kwa viongozi wa mtaa.

Amesema kufuatia kuwepo kwa watu wasioshiriki shughuli za misiba wala kutembelea wagonjwa kwa makusudi hivi sasa ipo haja kwa Serikali ya Mtaa kuanza utaratibu wa kuwacharaza viboko wale wote wanaobaki nyumbani bila kuwa na udhuru wowote.

“Sasa hivi imejitokeza tabia ya dharau na watu kutokwenda misibani kwa makusudi, sasa tabia hii inabidi ikomeshwe kwa nguvu zote, nashauri wenyeviti mliopo kwenye kata yangu anzisheni utaratibu wa kuwacharaza bakora wale wote wasiohudhuria msibani ili kesho wao wawe wa kwanza kufika,”amesema Nguvu.
Share:

FAMILIA YASHEREHEKEA KIFO CHA BIBI WA MIAKA 126 MOSHI


Kushoto ni Bibi Susana Mmari wakati wa uhai wake, kulia ni mazishi yake.

Hivi karibuni kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii, zilisambaa video na picha zikionesha watu wakisherehekea kifo cha Bibi mmoja aliyejulikana kwa jina la Susana Benjamin Mmari, aliyefariki na umri wa miaka 126, kilichotokea Mei 27 na kuzikwa Mei 30, 2020, huko Old Moshi Kidia.

Mmoja wa wajukuu wa Bibi huyo, anayejulikana kwa jina la Noel Mmari na kusema kuwa waliamua kuugeuza msiba huo kama sherehe, kwa sababu ilikuwa ni shukrani kwa Mungu kutokana na Neema kubwa aliyowapa kupitia maisha ya Bibi yao.

"Bibi alikuwa na watoto sita, wakiume 4 na wanawake walikuwa 2, na wawili tayari walishafariki, kaacha wajukuu 97, vitukuu 370, hivyo jumla ameacha uzao wa watu 586, tulimzika kwa shangwe kwa sababu afya yake mwishoni ilikuwa kama anateseka, kwahiyo kitendo cha kutwaliwa tukaona tukisikitika tutamkosea Mungu, sababu katupa Neema ambayo tunatakiwa kumshukuru siyo kusikitika" amesema Noel.

Aidha Noel amesimulia Bibi Suzana alikuwa ni wa aina gani, "Bibi alikuwa akiamka asubuhi anaenda shamba na alichokuwa anakilima ndiyo hicho hicho alikuwa anakula na wanaye na wajukuu na mimi alinilea baada ya kumaliza chuo na kupata kazi, ilibidi nimchukue niishi naye, kwahiyo amefariki akiwa kwenye mikono yangu, mimi ni miongozi mwa wajukuu zake wadogo, nina miaka 40 sasa".

Chanzo- EATV
Share:

Daladala Dar Ruksa Kusimamisha Wanafunzi Wanne

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, ameagiza daladala za mkoa huo, ziruhusu wanafunzi wanne kusimama ili kuondoa changamoto ya usafiri.

Makonda alitoa agizo hilo jana jijini Dar es Salaam wakati akipokea vifaa tiba na vifaa vya ujenzi na kueleza kuwa, agizo hilo la kubeba wanafunzi lianze mara moja.

“Sitaki kusikia mwanafunzi anaachwa eti konda na dereva wanasema wanabeba abiria kulingana na viti, wabebwe ili waende kwenye masomo,” alisema.

Alisema daladala litakalokuwa limebeba wanafunzi wasiozidi wanne, trafiki haruhusiwi kulikamata, lakini kama amesimamisha abiria wachukue hatua.

Pia, alisema alitoa maelekezo ya bodaboda na bajaji kuingia katikati ya jiji kubeba abiria, lakini kuna mtu mmoja ameanza kuwakamata na kumweleza kuwa hakuna Mkuu wa Mkoa mwingine.

“Hakuna Mkuu wa Mkoa mwingine, nipo na bado nipo, bodaboda, bajaji mnaendelea kuingia katikati ya mji kuendelea na shughuli zenu za kiuchumi kama nilivyoelekeza kauli hii sijaitengua na hakuna mwingine wa kuitengua katika mkoa huu labda mamlaka nyingine kutoka juu yangu,” alisema.


Share:

DC Macha Awatoa Hofu Wanafunzi Wa Kidato Cha Sita Kuhusiana Na Covid 19

SALVATORY NTANDU
Serikali wilayani Kahama mkoani Shinyanga imewatoa hofu wanafunzi wa kidato cha sita walioanza masomo June Mosi mwaka huu katika shule sita zilizopo wilayani humo kuhusiana na ugonjwa wa homa kali ya Mapafu inayosababishwa na Virusi vya Corona.

Pia imewataka kuchukua tahadhari kwa kuhakikisha wanazingatia maelekezo ya wataalamu wa afya yaliyotolewa na Wizara ya Afya katika kipindi hiki ambacho wanajiandaa na  mitihani ya  mwisho ya Taifa inayotarajia kufanyika hivi karibuni.

Wanafunzi nikutoka shule za sekondari, Busoka, Anderleck, John Paul, Mwendakulima,  Mwalimu Nyerere na Dakama na kuwataka walimu wa shule hizo kuhakikisha kila darasa linakuwa na ndoo za kunawia mikono,Vitakasa mikono pamoja na matumizi ya Barakoa wakati wa masomo.

Anamringi Macha ni mkuu wa wilaya ya Kahama, aliyabainisha hayo June 2 Mwaka huu katika ziara ya kukagua maandalizi ya Mapokezi ya wanafunzi wa kidato cha sita kuhusiana na namna viongozi wa shule hizo walivyotekelza maagizo ya serikali ya kujikinga na ugonjwa wa Covid 19 kwa wanafunzi.

Aidha Macha alisema kuwa Ugonjwa wa Corona bado upo lakini hapa nchini maambukizi yameshuka ukilinganisha na hapo awali,na kuwataka wanafunzi kutokuwa na hofu juu ya ugonjwa huo na badala yake wajikite na maandalizi ya mitihani yao ya Mwisho.

“ Wanafunzi wangu msiazimane barakoa na muache tabia za kutembeleana katika mabweni nyakati za usiku,kumbukeni moja ya sababu ya kuambukizana kwa ugonjwa huu ni kuazimana,nguo,barakoa,kugusana na kutonawa mikono,”alisema Macha.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Msalala, Simon Berege alisema kuwa,watahakikisha wanawapatia wanafunzi huduma zote katika kipindi hiki cha mitihani ikiwemo, chakula na malazi ili waweze kufanya vizuri katika mitihani yao ya Mwisho.

“Walimu wapo tayari kuwasaidia kwa masomo yote na hakuna mwanafunzi ambaye ataruhusiwa kwenda kuzurura nje ya maeneo ya shule tumejipanga vizuri na ndoo,vitakasa mikono na sabuni zipo kwa wingi hivyo tunaamini watamaliza mitihani yao salama,”alisema Berege.

Mwisho.


Share:

Mtoto Afariki Kwa Kushambuliwa Na Fisi Shinyanga, RPC Atoa Wito Kwa Wazazi

SALVATORY NTANDU
Wazazi na Walezi Mkoani Shinyanga wametakiwa kuchukua tahadhari kwa watoto wao dhidi ya  wanyama aina ya Fisi ambao wamekuwa wakionekana katika maeneo mbalimbali  na kusababisha madhara kwao ikiwemo ya vifo.

Kauli hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba June 2 wakati akizungumza na vyombo vya habari kuhusiana na tukio la kushambuliwa  hadi kufariki dunia kwa mtoto wa miaka miwili na nusu  aliyehamika kwa jina la Charles Christian katika kitongoji cha Mwagala kata ya Ibadakuli.

Amesema  tukio hilo limetokea June Mosi mwaka huu majira ya saa moja usiku akiwa anacheza na watoto wenzake nje ya nyumba yao alijeruhiwa kwa kung'atwa na fisi sehemu za usoni na kisha kuburuzwa umbali wa mita 50 ndipo wananchi walipoamua kumfukuza akamuachia na kukimbia baada ya kuzidi kwa kelele za wananchi hao.

“Wanyama hawa wamekuwa wakizurura ovyo hivyo ni Budi kila mzazi /Mlezi kuhakikisha watoto wao wanakuwa salama na kwani matukio ya watu kushambuliwa na fisi ama mifugo yamekuwa ni mengi hivyo chukueni Tahadhari,”alisema Magiligimba.

Amefafanua kuwa  Charles  alifariki dunia akiwa njiani akisafirishwa kwenda katika hospitali ya rufaa ya kanda ya  Bugando jijini Mwanza  kwa matibabu na mwili wake  umehifadhiwa katika hospitali ya rufaa mkoa wa Shinyanga kwaajili ya kukabidhiwa ndugu zake kwaajili ya Matibabu.

Mwisho.


Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano June 3



















Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger