Tuesday, 5 May 2020

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne May 05





















Share:

Monday, 4 May 2020

Wenye Virusi Vya Corona Nchini Kenya Wafika 490 Baada ya Wengine 25 Kuongezeka

Kenya imethibitisha maambukizi mapya 25 ya virusi vya Corona na kufikisha 490 waliothibitishwa kuwa na virusi hivyo kufikia sasa.

Wizara ya afya inasema kuwa visa 15 vinatoka jijini Nairobi na 10 kutoka kaunti ya Mombasa.

Wote wakiwa ni wakenya ambao hawana historia ya kusafiri nje ya nchi.

Naibu waziri wa afya Dkt Mercy Mwangangi anasema kuwa sampuli 1012 zilifanyiwa vipimo katika muda was aa 24 zilizopita.

Aidha watu 6 zaidi wamepona na kuruhusiwa kuondoka hospitalini na kufikisha 173 waliopona kufikia sasa.


Share:

WATOA HUDUMA ZA AFYA SHINYANGA WAPEWA MAFUNZO NAMNA YA KUHUDUMIA WASHUKIWA NA WAGONJWA WA CORONA

Jumla ya watoa huduma za afya 56 kutoka kwenye vituo vya afya vya umma na watu binafsi wilaya ya Shinyanga na Kishapu wamepatiwa mafunzo ya namna ya kutoa matibabu kwa washukiwa na wagonjwa watakaobainika kuwa na Maambukizi ya Virusi vya Corona (COVID 19).

Mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga kwa ufadhili wa Shirika la Lifewater International yamefanyika leo Jumatatu Mei 4,2020 katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga.

Afisa Afya Mkoa wa Shinyanga Neema Simba amesema mafunzo hayo yatakayofanyika kwa muda wa siku mbili yanalenga kuwajengea uwezo watoa huduma za afya wawe tayari kuhudumia washukiwa wa ugonjwa wa Corona.

“Tunawashukuru Lifewater International kwa ufadhili wa mafunzo haya ambayo yamekutanisha watoa huduma za afya kutoka kwenye vituo vya afya vya umma na binafsi katika Halmashauri ya wilaya ya Kishapu, Shinyanga na Manispaa ya Shinyanga”,ameongeza Bi. Neema.

Naye Meneja wa Shirika la Lifewater International mkoa wa Shinyanga, Benety Malima amesema watoa huduma za afya ni kundi ambalo linatakiwa kuangaliwa kwa jicho la pekee kwani wapo hatarini kupata maambukizi ya COVID 19 hivyo ni vyema wakajengewa uelewa wa kutosha kuhusu ugonjwa wa Corona.

“Lifewater International tumeamua kufadhili mafunzo haya kwani tunaamini sekta ya afya ni sekta ambayo ipo mstari wa mbele zaidi katika mapambano dhidi ya maambukizi ya Virusi vya Corona. Watoa huduma za afya ndiyo wapo mstari wa mbele katika kuhudumia washukiwa na wagonjwa wa Covid 19”,amesema Malima.

Kwa upande wake, Mratibu wa Huduma za Matibabu Mkoa wa Shinyanga Dkt. Daniel Mzee amesema miongoni mwa mada zitakazofundishwa katika mafunzo hayo ni pamoja na Utambuzi wa washukiwa na wagonjwa wa Corona na namna ya kuchukua tahadhari kwenye maeneo yao ya kazi ili wasipate maambukizi.

Amesema pia watoa huduma wa afya watafundishwa namna ya kufanya matumizi sahihi ya vifaa vya kujikinga na maambukizi (Personal Protective Equipment - PPE) pamoja na namna ya kuvaa nguo/vazi maalumu linalotumika kuhudumia mshukiwa/mgonjwa wa Corona.
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Afisa Afya Mkoa wa Shinyanga Neema Simba akizungumza leo Jumatatu Mei 4,2020 wakati  wa mafunzo kwa watoa huduma za afya kutoka kwenye vituo vya afya vya umma na watu binafsi wilaya ya Shinyanga na Kishapu yenye lengo la kuwajengea uwezo watoa huduma za afya namna ya kutoa matibabu kwa washukiwa na wagonjwa watakaobainika kuwa na Maambukizi ya Virusi vya Corona (COVID 19). Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mratibu wa Huduma za Matibabu Mkoa wa Shinyanga Dkt. Daniel Mzee akizungumza wakati wa mafunzo  kwa watoa huduma za afya wilaya ya Shinyanga na Kishapu ambapo amesema miongoni mwa mada zitakazofundishwa katika mafunzo hayo ni pamoja na Utambuzi wa washukiwa na wagonjwa wa Corona,namna ya kuchukua tahadhari kwenye maeneo yao ya kazi ili wasipate maambukizi,matumizi sahihi ya vifaa vya kujikinga na maambukizi (PPE) pamoja na namna ya kuvaa nguo/vazi maalumu linalotumika kuhudumia mshukiwa/mgonjwa wa Corona.
Meneja wa Shirika la Lifewater International mkoa wa Shinyanga, Benety Malima akizungumza wakati wa mafunzo kwa watoa huduma za afya ambapo amesema watoa huduma za afya ni kundi ambalo linatakiwa kuangaliwa kwa jicho la pekee kwani wapo hatarini kupata maambukizi ya COVID 19 hivyo ni vyema wakajengewa uelewa wa kutosha kuhusu ugonjwa wa Corona.
Watoa huduma za afya wakiwa ukumbini.
Watoa huduma za afya wakiwa ukumbini.
Katibu wa Afya Mkoa wa Shinyanga William Mambo akizungumza wakati wa mafunzo hayo.
Katibu wa Afya Mkoa wa Shinyanga William Mambo akizungumza wakati wa mafunzo hayo.
Watoa huduma za afya wakiwa ukumbini.
Mwezeshaji katika mafunzo hayo Dkt. Geofrey Mboye akitoa mada kuhusu COVID 19.
Mwezeshaji katika mafunzo hayo Dkt. Geofrey Mboye akitoa mada kuhusu COVID 19.
Watoa huduma za afya wakiwa ukumbini.
Afisa Afya Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Musa Makungu akitoa mada kuhusu COVID 19
Mafunzo yanaendelea.
Mafunzo yanaendelea.
Mafunzo yanaendelea.
Watoa huduma za afya wakiwa ukumbini.
Mafunzo yanaendelea.
 Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Share:

Wadau Wachangia Sh. Milioni 150 Kukabiliana Na Corona

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama amepokea msaada wa hundi tatu zenye thamani ya sh. milioni 150 zilizotolewa na kampuni tatu zinazozalisha nguzo za umeme nchini kwa ajili ya kusaidia mapambano dhidi ya homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya Corona (COVID- 19).

Waziri amepokea michango hiyo kwa niaba ya Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa leo tarehe 4 Mei, 2020 katika Ofisi ya Waziri Mkuu Mlimwa, Jijini Dodoma. Michango hiyo imetolewa na kampuni Mufindi Woodpoles Plant and Timber Ltd, Qwihaya General Enterprises Co Ltd na Poles (T) Ltd ambapo kila kampuni imetoa sh. milioni 50.

Akizungumza wakati wa kupokea michango hiyo Waziri Mhagama aliwapongeza viongozi wa kampuni hizo kwa kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuhakikisha inapambana na janga la ugonjwa wa COVID-19.

“Nawashukuru sana kwa niaba ya Serikali na hii inaonesha uzalendo, utayari na kuhakikisha kila Mtanzania anakuwa ni sehemu ya mapambano hayo kwa vitendo,”alieleza Waziri Mhagama.

Pia, Waziri Mhagama alitumia fursa hiyo kuwasihi wakandarasi wengine pamoja na Watanzania kuendelea kushirikiana na Serikali kwa kujitolea kwa hali na mali ili kuwezesha katika kukabiliana na janga hilo.

“Tunatoa wito kwa Watanzania wote kuona umuhimu na kuguswa na janga hili kwa kuchangia kwa kadiri inavyofaa ili kuendeleza uzalendo kwa hali ya kujali na kuonesha utayari ili kudumisha hali ya utamaduni uliopo tangu awali wa umoja na mshikamano ,”alisema Waziri Mhagama. 

Aliwahakikishia wadau hao kuwa, michango hiyo itatumika kwa malengo yaliyokusudiwa na kuwaeleza kuwa imefika katika eneo salama.

Awali, Waziri wa Nishati Dkt. Medadi Kalemani aliwapongeza viongozi wa kampuni hizo kwa michanga waliyoitoa kwa Serikali ambayo inakwenda kuongeza nguvu katika kukabiliana na ugonjwa wa COVID-19.

“Niwapongeze wakandarasi hawa kwa kuonesha nia ya kushiriki katika mapambano haya na wito wangu kila anayeguswa na janga hili ni faraja kubwa mnayoitoa kwa Serikalini katika kuhudumia na kusaidia katika kipindi hiki. Pia nawaomba wakandarasi wengine waige, ”alisema Dkt. Kalemani.  

IMETOLEWA NA:
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
OFISI YA WAZIRI MKUU



Share:

Serikali Yasema Demokrasia itaendelea kuheshimiwa nchini

Na Eleuteri Mangi, WHUSM, Dodoma
Serikali inaendelea na zoezi la Kidemokrasia la wananchi kuboresha taarifa za wananchi kwenye Daftari la Kudumu la Mpiga Kura ambazo zitatumika kwenye Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Mdiwani unaotarajiwa kufanyika Oktoba 2020.

Msemaji Mkuu wa Serikali na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Hassan Abbasi ameongoza zoezi hilo kwa Makatibu Wakuu leo Mei 04, 2020 hapa jijini Dodoma kuhakiki na kuhuisha taarifa zao katika ikizingatiwa leo ni siku ya mwisho kwa zoezi hilo nchini kote.

“Serikali inaendelea kukamilisha kuboresha Daftari la Kudumu la Mpiga Kura, Serikali zoezi hili ni muhimu sana kwa nchi yetu ikizingatiwa ni la kidemokrasia licha ya kwamba nchi yetu na dunia nzima inapitia kwenye changamoto tuliyonayo ya COVID-19” alisema Dkt. Abbasi.

Ameongeza kuwa Demokrasia itaendelea kuheshimiwa nchini kwa sababu ni kitu muhimu sana na viongozi hao pamoja na wananchi waliojiandikisha kutumia haki yao ya Kikatiba kuchagua viongozi wao.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome amesema kuwa Wizara yake inajukumu la kuhamasisha mambo mbalimbali ikiwemo elimu ya haki ya Mpiga kura.

“Nchi yetu imepiga hatua kubwa sana katika demokrasia kiasi kwamba tunajivunia hatua tuliyofika ni nzuri na demokrasia imekuwa ni ya kweli hakuna mwaka ambao tumevuka miaka mitano hatujafanya uchaguzi na wanannchi wamekuwa wakijitokeza kwa wingi kuwachagua viongozi wao” alisema Prof. Mchome.

Lengo la elimu ya mpiga kura ni kuwahamasisha wananchi kutumia haki yao ya kikatiba katika kujitokeza na kushiriki kuchagua viongozi wao watakao waongoza ili kujenga Demokrasia na Utawala Bora nchini hatua inaanza kwa wananachi kijiandikisha kwenye Daftari la Kudumu la Mpiga Kura ambalo linaratibiwa na kusimamiwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).


Share:

Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo Ataka Mbinu Mbadala Ya Karantini Kwa Wageni Kutoka Nje Ya Mkoa Kuinua Sekta Ya Utalii

Na Ahmed Mahmoud,,Arusha
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amesema ataishauri serikali kuangalia uwezekano wa kuondoa utaratibu wa sasa wa kuwaweka kwenye karantini ya siku 14 wageni wote wanaoingia mkoani hapa kwa shughuli za utalii  ili kuepusha kuwakatisha tamaa.
 
Gambo amelazimika kutoa kauli hiyo mapema leo wakati akipokea msaada wa Lita 500 za vitakasa mikono kutoka kampuni ya bia nchini, TBL na kueleza kwamba njia sahihi ya kuendelea kuchapa kazi ni pamoja na kuruhusu watalii walioonyesha nia kuingia nchini kama njia moja wapo ya kuvutia utalii .
 
Alisema wapo wageni wengi walioonyesha nia ya kutembelea vivutio mbalimbali mkoani hapa ila wanakumbwa na kikwazo cha Karantini jambo linalowakatisha tamaa na hivyo ameonelea ipo haja ya kuishauri serikali kubadilisha kipengere hicho ili kuangalia namna nzuri zaidi itakayowapendeza watalii bila kueneza maambukizo ya Korona.
 
Amesema sekta ya utalii ni muhimu sana kwa ustawi wa mkoa wa Arusha hivyo ameonelea ipo haja kwa watalii walioonyesha nia yakuingia nchini kuanzia mwezi juni mwaka huu kupewa utaratibu mpya wa maambukizi ya ugonjwa wa Korona badala ya kuwekwa kwenye Karantini ambayo huwapotezea muda na kuwaongezea gharama zaidi.
 
“Tunafikiria mkoa wa Arusha kuishauri  serikali ili kile kipengere cha Karantini iweze kukiondoa ili kuepuka kuwakatisha tamaa watalii walioonyesha nia ya kuja mkoani hapa kuanzia mwezi juni mwaka huu”Amesema Gambo
 
Katika hatua nyingine Gambo alisema kuwa mkoa wa Arusha utaendelea kutoa elimu kwa wananchi sanjari na kuwaondoa hofu ikiwemo kuondoa misongamano isiyo ya lazima kwa kuweka utaratibu wa mazishi kwa watu wasiozidi 10  na kuwa sio kila anayefariki basi amefariki wa Ugonjwa wa Covid 19.
 
Awali Meneja Uzalishaji wa kiwanda Cha bia cha TBL ,Joseph Mwaikasu alisema kampuni imeona uhitaji wa jamii na kuunga Juhudi za Serikali za kukabiliana na Ugonjwa wa homa Kali ya mapafu Covid 19 kwani hata wafanyakazi wao idadi kubwa ni wakazi wa mkoa wa Arusha.
 
Alisema kuwa wataendelea kuunga mkono juhudi za Serikali kwa kuhakikisha waendelea kusaidia katikamapambano dhidi ya janga hili hatari
 
Kwa upande wake Katibu Tawala wa mkoa wa Arusha Richard Kwitega alizipongeza baadhi ya Taasisi na mashirika mbalimbali ambayo yamekuwa yakitoa vifaa kwa ajili ya kupambana na Ugonjwa huo na kutaka wengine kuendelea kujitokeza kusaidia.


Share:

Serikali Yawataka Wafanya Kazi Wa Saluni Wachukue Tahadhari Dhidi Ya Maambukizi Ya Corona

Na WAMJW – DSM
Serikali kupitia Wizara ya Afya imetoa wito kwa Wafanya kazi katika maeneo ya saluni kuchukua tahadhari ili kujikinga dhidi ya maambukizi ya homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya Corona katika maeneo yao.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Kitengo cha maji na usafi wa mazingira, Wizara ya Afya, Ndg. Anyitike Mwakitalima wakati akitoa elimu kwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam kuhusu kuchukua tahadhari za kujikinga dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona.

“Kwa wale ambao wanasafisha nywele, kucha, wanafanya masaji, wanaosuka nywele, mchukue tahadhari kwasababu mpo katika hatari kubwa sana ya kuambukizwa lakini vile vile kuambukiza watu wengine maambukizi ya virusi vya Corona” alisema

Aliendelea kusema kuwa, Serikali inaendelea kuwakumbusha wafanya kazi wote katika maeneo ya saluni kuhakikisha wanaepuka msongamano pindi wanapokuwa katika majukumu yao, huku akisisitiza ni muhimu kwa kinyozi kuvaa Barakoa pindi ananyoa.

“Tunawakumbusha tena, kwa upendo kabisa, Tunawakumbusha muepuke msongamano ndani, awepo mtu anaenyoa na anaenyolewa na yule ambae ananyoa ahakikishe muda wote amevaa Barakoa, tunawaambia hivi kwasababu tunawapenda” alisema.

Kwa upande wake, Sfaff sergeant (S/Sgt ) Valentine Ngowi, amewataka madereva wote wa vyombo vya moto hususan bodaboda na bajaj kuhakikisha wanavitakasa vyombo vyao vya usafiri kwa sabuni mara kwa mara ili kuua maambukizi ya virusi vya Corona endapo vitakuwepo.

Nae, Balozi wa kampeni ya Mikoni safi, Tanzania salama, Msanii Mrisho Mpoto (Mjomba) amesisitiza kuwa ili kupambana na ugonjwa huu watu wasichoke kunawa mikono kwa sabuni na maji safi yanayotiririka ili kuepuka kupata maambukizi ya virusi vya Corona.

Uhamasishaji huu unafanywa kupitia kampeni hii ya “Mikono safi, Tanzania salama” inaratibiwa na Wizara ya Afya, kwa kushirikiana na Shirika lisilo la kiserikali la Project CLEAR kwa kushirikiana na Msanii Mrisho Mpoto (Mjomba) kutoka Mjomba Theatre Gallery unaendelea katika Jiji la Dar es Salaam.


Share:

Je? Umeachwa na mke/ mume/mchumba na bado unampenda ?

Je? Umeachwa na mke/ mume/mchumba na bado unampenda ? Kuna mtu unamtaka unashindwa kumwambia? 

Ipo dawa ya kumvuta  mume, mke ,mchumba na mtu yoyote unaye muhitaji katika mahusiano na kumfanya atimize unachokiitaji kutoka kwakwe na kumfunga asiwe na mtu mwingine zaidi yako hata kama yupo mbali ndani ya masaa .(2) tu na kukutafufuta yeye mwenyewe  .

Unamatatizo ya kushika mimba ? Na ukishishika zinaharibika?dawa zipo . 

PIA.TUNAYO DAWA YA ASILI YA NGUVU ZA KIUME YENYE KUTIBU MATATIZO MATATU KWA WAKATI MMOJA (1)nguvu za kiume ,(2) Kuongeza maumbile (3)kuchelewa kufika  kilelen.

Yajue .matatizo yanayosababisha upungufu wa nguvu za kiume .
(1)ngiri ya kupanda na kushuka 
(2)korodani moja kuvimba 
(3)tumbo kuunguruma,kujaa ges.
(4)kisukari 
(5)presha
(6)kiuno kuuma 
(7)kutopata choo 

 Tunatibu kisukari Suki (14)vidonda vya tumbo siku(30) mmiguu kufa ngazi,kuwaka moto .anapandikiza nyota ya kushinda bahati  na sibu ,kusafisha nyota kukupa mvuto wa ajabu ,kutoa nuksi na mifungo mbalimbali zindiko za nyumba na biashara  Peter za bahati .huzuia chuma ulete kwenye biashara .hurudisha Mali zilizopotea anao uwezo wa kumurudisha alie mbali au alie chukuliwa msukule :humaliza kesi ya aina yoyote ndan ya siku .(4)PIA TUNATIBU.BUSHA BILA OPRESHEN. 

Kwa mawasiliano tupigie No.0747100745( Namba hii pia iko Whatsapp)

Share:

Mkurugenzi wa Maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii asimamishwa kazi......Waziri Ummy Aunda Tume Ya Uchunguzi Wa Mwenendo Wa Maabara Ya Taifa




Share:

Taarifa Kwa Umma Kutoka Jeshi La Polisi Jijini Mwanza

Jeshi la polisi (m) Mwanza linawashikilia watuhumiwa 13 kwa tuhuma za kujihusisha na makosa mbalimbali baada ya kufanya operation kali ya kuzuia vitendo vya uhalifu na kuwakamata baadhi ya watu wanaojihusisha na vitendo hivyo.

Tukio la kwanza-; kukamatwa kwa watuhumiwa wa mauaji yaliyohusisha ramli chonganishi.

Tarehe 02.05.2020 majira ya 02:00hrs usiku katika kitongoji cha Imalange, kijiji cha Mwanangwa, wilaya ya Misungwi, mkoa wa Mwanza, alikamatwa mtuhumiwa wa kosa la mauaji aitwaye rodha shabani, miaka 27, msukuma na mkazi wa kijiji cha Mwankali, ambaye baada ya kuhojiwa kwa kina alikiri kuhusika na mauaji ya bibi kizee Ndebeto Tabitha Kakula, miaka 78, msukuma, mkulima na mkazi wa kijiji cha Mwankali, aliyeuawa tarehe 29.04.2020 majira ya 08:20hrs, kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali ambacho baadae ilibainika kuwa ni panga sehemu ya shingoni upande wa kulia wakati akitoka kisimani kuchota maji. Tukio hilo lilitokea baada ya  mganga wa kienyeji aitwaye Muhangwa Paul  kumpigia  ramli chonganishi  mtuhumiwa aliyemuua   bibi kizee huyo  kwa madai aliwaroga watoto wake wawili na kusababisha vifo vyao. 

Upelezi umewezesha kukamatwa kwa mganga huyo wa kienyeji na panga lililotu–mika kwenye uhalifu huo limepatikana.  Upelelezi wa shauri hili umekamilika kwa asilimia 90 na watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani haraka iwezekanavyo.

Tukio la pili; – kukamatwa kwa mama aliye telekeza watoto kwenye mazingira hatarishi ya majaluba ya mpunga.

Tarehe 29.4.2020 majira ya 06:00hrs asubuhi huko Nyakato,  wilaya ya Ilemela,  mwanamke aitwaye Happines Mafuru, miaka 23, mjita, mkulima na mkazi wa Nyamhongolo, alikamatwa kuhusiana na tukio la kutelekeza watoto wawili lililotokea tarehe 27.04.2020 majira ya 05:00hrs katika mashamba ya mpunga (majaruba), tukio hilo lilitokea mtaa wa mtakuja, nyamhongolo, wilaya ya ilemela, ambapo watoto hao walitelekezwa. Majina ya watoto ni 1. Kelvin mathias, umri mwaka mmoja na miezi 7 na 2. Anastazia mathia, umri miezi 4. Watoto wanaendelea vizuri,  hospitali ya rufaa ya bugando.

Jeshi la polisi linaendelea na upelelezi wa kina ili kujua mazingira ya tukio husika yakoje ikiwa ni pamoja na kuendelea kumsaka mzazi mwenzake aliyetoroka.Baada ya tukio hili.

Tukio la tatu:-
Jeshi la polisi mkoa wa Mwanza katika kipindi cha kuanzia mwezi march, 2020 hadi mwezi april 2020, katika maeneo ya jiji la mwanza, liliendesha operesheni kali dhidi ya wahalifu wa matukio ya uvunjaji wa nyumba usiku na wizi wa vifaa vya nyumbani vya ki elektronik, ambapo katika operesheni hiyo watuhumiwa 7, pamoja na flat tv 30, mota za machine 2, deki 2, subwoofer 2 na vifaa vya kuvunjia kama vile nyundo, shoka, nondo, simu 30,tindo, spana, plaizi,  baruti na vifaa vya kulipulia vimekamatwa.

Watuhumiwa wanaoshikiliwa ni;-
  1.     Juma said miaka 35, muha, mkazi wa kirumba.
  2.     Saitoti makokoyo, miaka 28, masai, mkazi wa bwiru.
  3.     Kelvin irizikiwa, miaka 32, muha, mkazi wa bwiru.
  4.     Hussein masoud, miaka 42, mnyamwezi, mkazi wa isevya –tabora.
  5.     Kiroba heka, miaka 38, msukuma, mkazi wa nakatunguru.
  6.     Kudra melikiadi, miaka 23, mjita, mkazi wa nakatunguru.
  7.     Busumbilo charles, miaka 25, mjita, mkazi wa kamkoko.
  8.      Simon deonatus @ killer, namagubo.
  9.     Ally bakari, miaka 24, mjita, mkazi wa mdoe.
Jeshi la polisi linaendelea na upelelezi wa mashauri hayo, mara baada ya kukamilika watuhumiwa watafikishwa mahakamani. Aidha linawataka wananchi wote waliowahi kuibiwa tv na vifaa vingine vilivyotajwa wafike kituo cha polisi kati  ilemela na nyakato kwa utambuzi.

Jeshi la polisi mkoa wa mwanza linaendelea kuwashukuru wananchi wote wanaoendelea  kutoa taarifa za wahalifu na uhalifu ili wakamatwe na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria. Pia linawataka wanachi kuacha kujihusisha na vitendo vya imani potofu za kishirikina kwani hazina ustawi kwa jamii.

Imetolewa na:
Muliro Jumanne Muliro -; ACP
Kamanda wa polisi (m) Mwanza
04 may, 2020


Share:

Kamanda Wa Polisi Afanya Ukaguzi Wa Kushtukiza Stendi Kuu Ya Mabasi Mbeya

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi ULRICH MATEI leo tarehe 04.05.2020 majira ya saa 05:00 Alfajiri amefanya ukaguzi wa kushtukiza wa Mabasi ya Abiria yanayofanya safari kwenda mikoa mbalimbali kabla ya kuanza safari kwa lengo la kuangalia usalama wa vyombo hivyo vya usafiri pamoja na kujiridhisha na usimamizi na utekelezaji wa maelekezo yake kwa wakaguzi wa magari waliopo Stendi Kuu.

Katika ukaguzi huo alikuta Mabasi matatu ya abiria yenye namba za usajili T.619 CQV aina ya Scania Mali ya Kampuni ya Isamilo Express linalofanya safari kati Mbeya – Mwanza ambalo tairi zake zilikuwa zimeisha na lilikuwa na tatizo kwenye mfumo wa breki, Basi namba T.420 DNM aina ya Toyota Coaster Mali ya Kampuni ya Amazon Tour Express linalofanya safari kati ya Mbeya – Sumbawanga tairi zake zilikuwa zimeisha na Basi namba T.606 DLQ aina ya Euchre Mali ya Kampuni ya Gitu Express pia tairi zake zilikuwa zimeisha.

Kutokana na matatizo hayo, Kamanda MATEI alizuia mabasi hayo kuendelea na safari hadi yatakapofanyiwa marekebisho ikiwa ni pamoja na kuwekewa tairi mpya. Uongozi wa Kampuni ya Isamilo Express ulileta basi jingine la kampuni hiyo na abiria kuhamia kwenye basi hilo na kuanza safari, pia basi la kampuni ya Amazon Tour Express lilibadilishwa tairi na kuruhusiwa kuendelea na safari.

Aidha Kamanda MATEI amekagua usalama wa abiria kabla ya kuanza safari hasa kipindi hiki cha uwepo wa ugonjwa wa Homa Kali ya Mapafu [COVID 19] na kuwataka Madereva, Abiria na Uongozi wa Stendi Kuu ya Mabasi Mbeya kuhakikisha kila mmoja anafuata maelekezo yanayotolewa na Viongozi Wakuu wa Nchi pamoja na Wizara ya Afya hususani kuvaa barakoa, kunawa mikono kwa maji tiririka yenye sabuni au vitakasa mikono [Sanitizer] ili kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa Homa Kali ya Mapafu.

Aidha Kamanda MATEI ametoa wito kwa wamiliki wa vyombo vya usafiri kuhakikisha wanafanya matengenezo mara kwa mara ya vyombo hivyo kabla na baada ya safari ili kujiridhisha juu ya usalama wake. Pia amewataka abiria kutoa taarifa za mienendo ya mabasi hayo kwa Jeshi la Polisi kupitia namba za simu ili hatua stahiki zichukuliwe dhidi ya madereva wanaokiuka sheria, kanuni na taratibu za usalama barabarani.


Share:

Corona Yafuta tofauti ya Daimond na Clouds Media ......Kusaga Aagiza nyimbo yake Ipigwe Redioni

CEO wa Clouds Media Group Joseph Kusaga amezindua kampeni ya BONGE LA MPAMBANAJI ambayo ni maalum kwa ajili ya kuwawezesha Wahudumu wa Afya Tanzania kwa vifaa tiba na mahitaji mengine kwenye vita hii dhidi ya kirusi cha corona.

Wakati akihojiwa na Power Breakfast ya Clouds FM Kusaga akasema anao Wapambanaji wenzake ambao wako tayari kuungana na yeye na miongoni mwao ni Vodacom, Tigo na Diamond Platnumz ambaye alimpigia simu LIVE na kuzungumza kwenye Power Breakfast.

Akiongea kwenye PB Diamond amesema “Kwanza nimpongeze CEO Kusaga kwa kuweka nguvu zake kwenye hilo sio kila Mtu mwenye moyo huo, mimi pia nitaweka mchango wangu hapo na kama unavyofahamu tayari pia upande wangu nimeanza kulipia kodi familia zilizokwama kutokana na hii corona”

Baada ya kuzungumzia Bonge la Mpambanaji, CEO Kusaga alimtaka Diamond achague wimbo wake ili uchezwe kwenye PB kuwaamsha Wapambanaji wote ambapo mara ya kwanza alipendekeza apigwe Msanii wake mpya @officialzuchu lakini baada ya Jo kusisitiza kuwa ngoma ya Diamond ndiyo inatakiwa, Platnumz alichagua yope remix na ikapigwa.


Share:

Wenye Virusi Vya Corona Uganda Wafika 89 Baada ya Mmoja Kuongezeka

Wizara ya Afya Uganda imesema kuna ongezeko la mgonjwa mmoja wa corona na kufanya jumla ya maambukizi kufikia 89


Waliopona corona Uganda ni Watu 52 na hakuna kifo

Rais  wa nchi hiyo Yoweri Museveni leo jioni atalihutubia Taifa hilo kuhusu hatua zaidi baada ya siku 21 za lock down kukamilika kesho.




Share:

Maambukizi Ya Virusi Vya Corona Yapindukia milioni 3.5 Duniani Kote

Maambukizi ya virusi vya Corona duniani yamepindukia milioni 3.5 leo Jumatatu, wakati idadi ya vifo vinavyosababishwa na janga hilo imeongezeka hadi zaidi ya 245,000, ingawa viwango vya maambukizi mapya na vifo vimepungua ikilinganishwa na mwezi uliopita, kulingana na ripoti ya shirika la habari la Reuters.

Visa vingi vilivyothibitishwa katika siku za hivi karibuni viliripotiwa katika ukanda wa Amerika ya Kaskazini na nchi za Ulaya, ingawa idadi ya kila siku ya maambukizi mapya inaongezeka katika ukanda wa Amerika ya Kusini, Afrika na Urusi.

Duniani kote, visa vipya 84,004 viligunduliwa ndani ya masaa 24 yaliyopita, shirika la habari la Reuters limebaini, huku likijikita katika takwimu rasmi zilizotolewa na kila, idadi ambayo inafanya jumla ya visa duniani kote kufikia zaidi ya milioni 3.5.

Vifo vinavyotokana na mlipuko wa Covid-19, ugonjwa unaosababisha matatizo ya kupumua vimefikia jumla ya 245,992.

-RFI


Share:

Teknolojia inavyotuwezesha kuendesha maisha na biashara

Hali inaonesha kwamba, nchi nyingi duniani zimeathirika na homa ya kirusi cha korona na athari hizi huenda zikabaki katika maisha ya watu kwa muda mrefu.  
 
Mbali na njia mbalimbali za kupambana na maambukizi kama kufunga shule na kuzuia mikusanyiko, Watanzania wengi pia sasa wanatumia njia za kidijitali zaidi kuwasiliana na kuendesha maisha na shughuli zao za kila siku kwa sababu maisha lazima yaendelee. Ama kweli sasa kuungana kidijitali limekuwa jambo muhimu sana. 
 
Mawasiliano ya kidijitali yameleta ahueni sana. Mfano wapo watu ambao hawataweza kuwatembelea ndugu, jamaa na marafiki kama walivyozoea lakini sasa wanaweza kuwasiliana kwa simu na kubaki wamoja na wapendwa wao. Jambo hili linaelezwa kuwa ni muhimu kwa afya ya akili. 
 
Teknolojia ya kidijitali imekuwa si tu ya faida kwa mawasialiano ya mtu mmoja mmoja na familia bali pia kwa biashara. Imesaidia biashara hizi kuendelea kutoa huduma kupitia mtandao wa intaneti ikiwemo kuwasiliana na wateja, huduma za masoko na malipo kidijitali. 

Kwa bahati nzuri kampuni za mawasiliano ya simu ziko mstari wa mbele kuwezesha sisi kubaki tumeungana kidijitali. Kampuni ya Tigo kwa mfano ina huduma ya Mfano mmojawapo ni kampuni ya Tigo ambayo ina router ya intaneti nyumbani (Home Internet Router) ambayo inasaidia familia kuwasiliana kwa kuipa mtandao bora wa intaneti. Kwa upande wa maofisi nao wana huduma ya intaneti kwa ofisi (Office Internet) ambayo husaidia ofisi kuendelea kubaki pamoja na kufanya kazi kidijitali. 

Katika nyakati hizi za changamoto, kubaki tumeungana kidijitali na kuendelea na maisha na shughuli zetu ni jambo muhimu kuliko wakati wowote ule.


Share:

Colombia yakanusha kuhusika na majaribio ya mapinduzi ya kisiasa nchini Venezuela

Wizara ya mambo ya nje ya Colombia imetoa taarifa ikikanusha Colombia kuhusika na majaribio ya mapinduzi ya kisiasa nchini Venezuela.

 Waziri wa mambo ya nje wa Venezuela Bw. Nestor Reverol amesema mamluki wa Colombia walijaribu kutekeleza shughuli za kimabavu na kufanya mapinduzi kutoka pwani ya jimbo la La Guaira, kaskazini mwa nchi hiyo.

 Kikosi cha usalama cha Venezuela kimepambana na magaidi hao, na kuwaua na kuwakamata baadhi yao. 

-CRI


Share:

JITIBU TATIZO LA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME KWA KUTUMIA FULL POWER.. UUME MDOGO ZAT 50 NDIYO SULUHISHO




Zati 50
Full Power


Sababu za upungufu wa nguvu za kiume na maumbile madogo ya uume:

⇒Ngiri,


⇒Henia


⇒Kisukari


⇒Tumbo kujaa gesi

⇒Kutopata choo vizuri


⇒Utumiaji madawa kwa muda mrefu


⇒Unywaji wa pombe kupita kiasi


⇒Msongo wa mawazo 

⇮⇒Haya yote hupelekea mwili kutokuzalisha homoni ya gesrtogine au kuwa chache na kushindwa kupata mzunguko mzuri wa damu na vichocheo vingine kama madini ya zinki ambayo hukufanya kuwa na msisimko  na kufanya kuwa na muda  mrefu na nguvu za kutosha.

ZAT 50

⇨ Inarutubisha maumbile ya uume  na kunenepesha urefu nchi 6,unene sentimita 4

⇨Dawa hii ni ya kutibu kabisa tatizo hilo.


FULL POWER

⇨Ni dawa ya vidonge ya miti shamba inaongeza nguvu za kiume na kutibu kabisa tatizo hilo.

⇨Inaongeza hamu ya tendo la ndoa
⇨Inakufanya uchelewe kufika kileleni zaidi ya Dakika 30 na kurudia tendo zaidi ya mara nne na zaidi.

Pia tunatibu Magonjwa mengine Kama

Matatizo ya pumu,Bawasiri, vidonga vya tumbo,Kisukari,Magonjwa sugu ya zinaaa,Kaswende,U.T.I , kiuno,miguu kuwaka moto, Fangasi sehemu za Siri, kupunguza unene wa mwili,tumbo kuunguruma,kujaa gesi, matatizo ya uzazi kwa wanawake, kurutubisha mbegu za uzazi kwa akina baba, matatizo ya meno tunatibu bila kungoa

Kliniki yetu inapatikana Zanzibar, Dar es salaam na Shinyanga.

Wasiliana nasi kwa simu namba 071770 22 27
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger