Friday, 20 March 2020

Dereva Wa Basi La Isamilo Afariki Dunia Akiwa Safarini

Dereva wa Basi la Isamilo lenye namba za usajili T609 CQB Scania linalofanya safari zake kutoka Mwanza kwenda Mbeya Sebastian Mathias (43) mkazi wa Mwanza amefariki dunia wakati akiendelea na safari kutoka Mbeya kwenda Mwanza.           

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga, Deborah Magiligimba amesema tukio hilo limetokea leo Ijumaa Machi 20,2020 saa nne asubuhi.

Kamanda Magiligimba amesema Sebastian wakati akitoka Mbeya kwenda Mwanza alikuwa akijisikia vibaya walipofika Singida ndipo hali yake ilibadilika wakawa wamebadilishana na dereva mwenzake.

"Sebastian alitoka Mwanza kwenda Mbeya akiwa anajisikia vibaya. Huwa wapo madereva wawili,wameenda hadi Mbeya,wakati wanatoka Mbeya kwenda Mwanza Sebastian alikuwa anaendelea kujisikia vibaya, walipofika Singida akawa anajisikia vibaya zaidi ndipo akabadilishana na yule dereva mwenzake",amesema Kamanda Magiligimba.

"Wamefika Tinde leo saa nne asubuhi akawa amezidiwa sana, wakambeba kwenda kwenye Kituo cha Afya Tinde,baada ya kumfikisha,Daktari akabaini kuwa tayari Sebastian Mathias alikuwa amefariki dunia",ameeleza Kamanda Magiligimba

Amesema kwa kuwa gari lina madereva wawili, dereva mwingine ameendelea na safari kwenda Mwanza na maiti imehifadhiwa katika kituo cha afya cha Tinde.


Share:

Wanaume waliombaka mwanamke ndani ya basi wanyongwa India

India imewanyonga hadi kufa wanaume wanne walioshitakiwa kwa kosa la kumbaka na kumuua mwanafunzi mmoja ndani ya basi mnamo mwaka 2012. 

Mwanamke huyo aliyekuwa na miaka 23 alibakwa wakati basi lilipokuwa likiendelea na safari mjini New Delhi. 

Watu hao wamenyongwa mapema hii leo katika gereza la Tohar Jail mjini New Delhi hii ikiwa ni kulingana na shirika kubwa la habari nchini humo la Press Trust of India, lililonukuu mamlaka za gereza. 

Wanaume hao walimbaka mwanamke huyo aliyekuwa akitokea kutazama sinema na kumuumiza vibaya kwenye sehemu zake za siri kwa kutumia kipande cha chuma. 

Tukio hilo baya kabisa liliibua maandamano kote nchini India na kuwachochea wabunge kuongeza ukali wa adhabu dhidi ya kesi za unyanyasaji wa kingono. 

Adhabu ya mwisho ya kunyongwa ilitolewa mwaka 2013 nchini India.

-DW


Share:

Mkutano wa kilele wa G7 wafutwa kwa sababu ya corona

Serikali ya Marekani imefuta mkutano wa ana kwa ana wa kilele wa wakuu wa kundi la mataifa yaliostawi zaidi kiviwanda duniani G7 uliokuwa umepangwa kufanyika mwezi Juni kutokana na janga la mripuko wa virusi vya corona. 

Badala yake viongozi hao wa serikali na mataifa saba watazungumza kwa njia ya video. 

Viongozi wa ngazi ya juu wa mataifa yaliostawi zaidi kiviwanda duniani ya Uingereza, Canada, Ufaransa, Ujerumani, Italia, Japan na Marekani, hukutana mara moja kwa mwaka kujadili masuala muhimu ya kidunia. 

Mwaka huu rais wa Marekani Donald Trump ndiye alipaswa kuwa mwenyeji wa mkutano huo.


Share:

Wizara ya Mambo ya Nje Yakutana Na Kamati Ya Bunge Yawasilisha Taarifa Ya Utekelezaji Kwa Mwaka 2019/2020

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imekutana na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama na kuwasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti ya Wizara kwa Mwaka wa Fedha wa 2019/2020.

Akiwasilisha taarifa ya Wizara, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi amesema Wizara katika kuhakikisha inatekeleza majukumu yake kwa ufanisi na kuzingatia maoni na ushauri wa Kamati ya Bunge imeanzisha Kitengo cha Usimamizi wa Majengo ambacho kitakuwa chini ya Mkurugenzi Msaidizi katika Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu.

Amesema pamoja na kuanzishwa kwa Kitengo hicho Wizara imeendelea kushirikiana na Wakala wa Majengo ya Serikali (TBA) katika kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa ufanisi huku wakifuata sheria na taratibu zilizopo.

Amesema uamuzi wa kuanzishwa kwa kitengo hicho unatokana na ushauri uliotolewa na Kamati hiyo uliyoitaka Wizara kuhakikisha mipango ya ujenzi wa majengo ya ofisi na makazi ya Balozi mbalimbali nje ya nchi unasimamiwa kitaalamu na kwa ufanisi mkubwa.

“Uamuzi huu umetokana na ushauri ambao Kamati hii iliutoa kwa Wizara katika kuhakikisha suala la ujenzi wa majengo ya Balozi zetu unasimamiwa kitaalamu na kwa ufanisi,” alisema Prof. Kabudi.

Mhe. Waziri amesema Wizara inaendelea na mipango ya kuwashirikisha Watanzania waishio ughaibuni katika mipango na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchininikiwa ni pamoja na kuwawekea mazingira rafiki ya kuchangia maendeleo na kusaidia ndugu na jamaa zao waliopo nchini na kufanya uchambuzi wa mazingira ya ushirikishwaji wao na kuangalia masuala ya kisheria, kitaasisi ushirikiano na sekta binafsi takwimu za Watanzania waishio ughaibuni na uwezo na hamasa ya kuchangia maendeleo ya nchi.


Share:

Corona yasitisha uchaguzi wa viongozi wa CWT Ngazi za wilaya

Na Amiri kilagalila,Njombe
Kutokana na tishio la ugonjwa wa Corona (COVID 19) unaeoendelea kuenea nchi nyingi Duniani huku Tanzania ikifikia wagonjwa 6 mpaka sasa kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na waziri wa afya maendeleo ya jamii, jinsia na watoto  Ummy Mwalimu.

Katibu wa chama cha walimu CWT mkoa wa Njombe Mwalimu Fraten Kwaison amesema kutokana na agizo la serikali kuwataka watanzania kutokujihusisha na mikusanyiko isiyokuwa ya lazima pamoja na njia nyingine zinazowezesha kujikinga na maambukizi ya virusi vya COVID 19,chama hicho kimesitisha uchaguzi wa viongozi ngazi ya wilaya ambao ulitarajiwa kufanyika kuanzia machi 21-28  2020 kwa kuwa unakutanisha watu Zaidi ya 100.

“Kwa ngazi ya wilaya uchaguzi wetu ungefanyika tarehe 21 mpaka 28 ya mwezi huu wa tatu sasa baada ya tangazo kutoka tumesitisha,na tumesitisha kwasababu mikutano hii inayofanyika ni mikubwa na inakwenda takribani watu 100 na kuendelea,kwa hiyo kwa tangazo lililotolewa na serikali ilikuwa ni muhimu sana kusitisha”alisema Kwaison

Aidha Kwaison amesema chaguzi nyingine upande wa shule mahali pa kazi upande wa shule za misingi,sekondari,vyuo vya ualimu na vyuo vya maendeleo ya wananchi uchaguzi umekwisha fanyika lakini kwa ngazi ya wilaya umeahirishwa kutokana na kutii agizo la serikali.

Vile vile amesema kwa upande wa maandalizi ya sherehe za mei mosi chama kinaendelea kukusanya michango kwa wadau kwa kuwa watu wamekwishaainishwa na sherehe hizo zitafanyika kutokana na muelekeo wa serikali.

“Kwasababu watu walishaainishwa kazi iliyobakia ni kuwapelekea barua kwenye ofisi zao na manyumbani  kwao kwasababu tarehe ambayo tulikusudia michango kukamilika ni tarehe 17 mwezi wa 4 kila mmoja awe amejua cha kuchangia,kwa hiyo utekelezaji huo unaendelea kwa upande wa Mei mosi,na serikali ikitoa muelekeo na nini cha kufanya basi sherehe itaendelea kufanyika ila hatuwezi kukaa tukaacha kukusanya hiyo michango wakisema hitafanyika hiyo ni kitu kingine”alisema tena Fraten Kwaison

Katika hatua nyingine Bwana Kwaison ametoa wito kwa wazazi na walezi kuwalinda watoto kwa kuwa shule zimefungwa kwa dharula na sasa wapo mikononi mwao hivyo ni wajibu wa wazazi na wanafunzi kujilinda kwa kipindi hiki cha kufungwa shule kwa dharula kutokana na ugonjwa wa COVID 19.

“Kwa sasa watoto wako mazingira huru na wamekwenda kwa jamii,ninaomba wazazi wasiwaache watoto huru ila wawadhibiti vizuri ili warudi shuleni wakiwa salama na ukizingatia mitaani kuna mambo mengi,lakini kubwa kwenye hili la CORONA tunaendelea kukumbasha mpaka huku majumbani ni lazima tujikinge kweli kweli”alisema tena Kwaison.

Serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania imetoa utaratibu mbali mbali ikiwemo kufunga shule za awali mpaka vyuo vikuu na vya kati,pamoja na kuzuia mikusanyiko isiyo kuwa ya lazima ili kuzuia na kupambana na maambukizi ya virusi vya Corona (COVID 19) huku mpaka serikali ikiwa imetangaza takribani watu 6 kukumbwa na virusi hivyo.




Share:

Wizara ipo tayari kumpa ushirikiano Chidbenz- Naibu Waziri Shonza

Na Anitha Jonas – WHUSM
Naibu Waziri Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza amwaahidi ushirikiano msanii wa bongofleva nchini Rashid Abdallah maarufu Chidbenz.

Mheshimiwa Shonza ametoa kauli hiyo leo jijini Dodoma alipofanya kikao na msanii huyo ambapo Chid benz alimuhakikishia kuwa kwa sasa amebadilika na anataka kuwaonyesha watanzania amefanikiwa kujikwamua katika matumizi ya madawa ya kulevya na hataki tena kurudi huko kwani anazaidi ya miezi mitatu sasa hajatumia madawa hayo kabisa.

“Kati ya wasanii wenye kukubalika na mashabiki zao wewe Chid benz ni mmoja wao na mashabiki zako ni wengi hivyo ningependa kukuona kwanzia sasa unalijenga zaidi jina lako kwa kuonyesha kuwa umebadilika,katika kipindi hichi nitafurahi zaidi kukuona unasonga mbele na hurudi tena katika matumizi ya madawa ya kulevya wizara ipo pamoja na wewe kukusaidia wakati wowote ,”alisema Mhe.Shonza.

Akiendelea kuzungumza katika kikao hicho mheshimiwa Shonza alimsisitiza msanii huyo kuwaonyesha watanzania kuwa anaweza na hata akipewa nafasi anaweza kujitumia vyema na kuonyesha juhudi yake katika kufanya kazi na kuwa mbunifu katika kufanya kazi zake za usanii.

Naye Msanii huyo wa Bongofleva Chid benz alieleza kuwa kwa sasa hautarudi nyuma tena sababu tayari amekwisha acha kutumia matumizi ya madawa hayo na ninaelewa bahati haiji mara mbili lakini kwangu naiona imekuja zaidi ya mara moja kwa maana ya kuwa nimekuwa nimekuwa na anguka nainuka narudi kwa mashabiki wananipokea nakuendelea kukubali muziki wangu hakika najiona niwakati wa kuwafurahisha zaidi mashabiki na sitawaangusha.

“Ombi langu kwa serikali ni kupata ushirikiano na mapema wiki ijayo ninatarajia kutoa wimbo wangu mmoja uitwao Beautiful ambao nimeuiamba nikisifu uzuri wa mwanamke na kufuatia janga la Corona ninamwahidi mheshimiwa Naibu Waziri kuwa nitatunga wimbo kwa ajili ya Corona ,”Chid benz.

Pamoja na hayo nae Chid benz alitoa wito kwa watanzania kuacha kufanya mzaha katika mitandao ya jamii kuhusu suala la ugongwa Corona sababu hili ni tatizo ni janga linalosumbua dunia kwa sasa hivyo jambo la msingi ni kuzingatia maelekezo yaliyotolewa na serikali kutoka kwa wataalamu wa afya.


Share:

Idris Sultani na meneja wake wapandishwa kizimbani Mahakama ya Kisutu

Mchekeshaji maarufu nchini Tanzania, Idris Sultani (27) na wenzake wawili, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam kujibu shtaka moja la kuchapisha maudhui mtandaoni bila kuwa na leseni kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Sultani(27) ambaye ni mfanyabiashara na mkazi wa Mbezi Beach na wenzake wamesomewa shtaka lao, leo Ijumaa Machi 20, 2020, mahakamani hapo.

Mbali na Sultani, washtakiwa wengine ni mfanyabiashara Doctor Ulimwengu (28) mkazi wa Mbezi Beach na Isihaka Mwinyimvua (22) ambaye ni msanii na mkazi wa Gongolamboto.

Washtakiwa hao wamesomea shtaka lao na wakili wa Serikali, Batilda Mushi mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi.

Wakili Mushi alidai washtakiwa wote wanakabiliwa na kesi ya jinai namba 60/2020.

Amedai washtakiwa wanadaiwa kutenda kosa hilo kati ya Machi 8, 2016 na Machi 13, 2020 katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam.

Inadaiwa siku hiyo ya tukio, kwa kutumia online Tv inayojulikana kwa jina la Loko  Motion, walichapisha maudhui katika mtandao huo bila ya kuwa na kibali kutoka TCRA, jambo ambalo ni kinyume cha sheria.

Washtakiwa baada ya kusomewa shtaka hilo, walikana na upande wa mashtaka ulidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.

Hakimu Shaidi, alitoa masharti ya dhamana ambayo, kila mshtakiwa alitakiwa  kuwa na mdhamini mmoja atakayesaini bondi ya Sh 8milioni.

Pia, mdhamini huyo anatakiwa kuwa na barua inayotambulika kisheria na kitambulisho cha Taifa.

Washtakiwa wote wametimiza masharti ya dhamana na hakimu Shaidi, ameahirisha kesi hiyo hadi April 21, 2020 itakapotajwa.


Share:

Tume ya Ushindani (FCC) yaonya upandishaji bei vifaa vya kujikinga corona

Tume ya Ushindani (FCC) nchini Tanzania imewapa onyo waingizaji, wazalishaji, wasambazaji na wauzaji wa jumla na rejareja wa bidhaa za kujikinga na maambukizi ya virusi ya corona ikisema ni kinyume cha sheria ya ushindani.

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa tume hiyo, jana Ijumaa Machi 19,2020 imesema kumekuwa na malalamiko ya wananchi kuhusu upatikanaji wa bidhaa hizo ambazo ni pamoja na dawa za kutakasa mikono na maeneo yanayoweza kuguswa kwa mikono (Hand Sanitizers), barakoa (face masks) na Vizuizi vya mikono (gloves).

“Baada ya Serikali kutangaza kuwa virusi vya corona vimeingia nchini na kutolewa kwa miongozo ya namna ya kujikinga na maambukizi, wananchi wamejitokeza kwa wingi kununua bidhaa za kujikinga dhidi ya maambukizi ya virusi hivyo.”

“Tume imepokea malalamiko juu ya uhaba na kuongezeka kwa kasi kwa bei za bidhaa hizo,” imesema sehemu ya taarifa ya tume hiyo.



Share:

Wizara Ya Afya Yasema Hakuna Maambukizi Mapya Ya Virusi Vya Corona.....Wagonjwa Ni Walewale 6




Share:

Staa wa muziki wa Soukous kutoka DR Congo, Aurlus Mabélé Afariki Dunia

Staa na nguli wa muziki wa Soukous kutoka DR Congo, Aurlus Mabélé amefariki Dunia akiwa na umri wa miaka 67. 

Chanzo cha kifo chake bado hakijawekwa wazi lakini Mabélé alikuwa akisumbuliwa na Saratani (cancer) kwa muda mrefu.
 
Kwa mujibu wa mwanamuziki Nyboma Mwandido, Mabele amefariki usiku wa kuamkia leo katika Hospitali moja jijini Paris Ufaransa.

Nyboma amesema Mabele alilazwa hospitalini Alhamis Machi 19, 2020 usiku.

Sababu rasmi ya kifo chake bado haijawekwa wazi huku vyanzo mbalimbali vikieleza huenda ni Corona na vingine vikisema ni mshtuko.


Share:

Jafo Aingilia Kati Sakata Wanafunzi Waliokosa Usafiri Baada ya Shule Kufungwa Kisa Corona

Mwandishi wetu OR-TAMISEMI
WAZIRI wa Nchi,Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Mhe. Selemani Jafo ameagiza Wakuu wa Wilaya,Wakurugenzi na Wakuu wa shule nchini,kuhakikisha wanafunzi waliokosa usafiri wanasafirishwa badala ya kuwaacha wakizagaa kwenye vituo vya mabasi.

Waziri Jafo ametoa agizo hilo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari, jijini Dodoma kutokana na baadhi ya maeneo wanafunzi wakionekana kupata adha ya usafiri licha ya serikali kutoa maelekezo ya namna ya kuwasafirisha wanafunzi hao hadi makwao.

Amesema serikali kupitia Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ilitoa maelekezo ya kufunga shule zote na vyuo vikuu kwa kipindi cha siku 30  kutokana na ugonjwa wa Corona na Katibu Mkuu alishaandika barua kupitia Ofisi za Wakuu wa Mikoa kwamba uwekwe utaratibu mzuri kwa vijana hao kuanzia Machi 17-20 wa kuwasafirisha hadi makwao kwa usalama na amani.

Waziri. Jafo  amesema  agizo hilo lilitolewa kwa viongozi hao kusimamia  vizuri zoezi hilo lakini baadhi ya maeneo utaratibu haukwenda vizuri hadi leo wanafunzi wa bweni wameruhusiwa kwenda vituoni kutafuta magari wenyewe na hivyo kusababisha wanafunzi kutangatanga sana.

“Tumesikia kwenye maeneo ya Moshi na Morogoro tumeona wanafunzi wa Dakawa wakitangatanga kituo cha mabasi Msamvu na Maeneo mengine, katika hili halikubaliki hata kidogo,”amesema Mhe. Jafo

Ametoa pongezi kwa Mkuu wa Shule ya Kilakala iliyopo Morogoro na Mkuu wa Shule ya Dodoma Sekondari kwa kuweka utaratibu mzuri wa kusafirisha wanafunzi hao.

“Kilakala alihakikisha wanafunzi wake wote anawakodia mabasi yanawachukua shuleni na hadi leo(jana) alikuwa amebaki na wanafunzi 30 wanaoenda Mkoa wa Manyara, Kiteto na Simanyiro ambao anawasafirisha, pia Dodoma yeye hata wanafunzi wasiokuwa na nauli alikodi magari kuwasafirisha bila nauli na kuwataka wazazi watume kwake nauli hizo ili alipe gharama za usafiri,”amesisitiza Mhe. Jafo

Aidha ameagiza viongozi hao wahakikishe wanafunzi ambao hawajapata usafiri hadi sasa waratibu na kuwasafirisha kwenda majumbani kwao kwa salama na amani na hatarajii kuona wakitangatanga kwenye maeneo yao.




Share:

Naibu Waziri Mabula Aingilia Kati Mgogoro Kati Ya Mapadri Na DC Ukerewe

Na Munir Shemweta, WANMM UKEREWE
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ameagiza kufanyika utambuzi wa mipaka sambamba na kuweka alama katika eneo lenye mgogoro wa ardhi kati ya Kanisa Katoliki, wananchi na shule ya msingi ya Kagunguli iliyopo wilaya ya Ukerewe mkoa wa Mwanza

Uamuzi huo unafuatia kuibuka mgogoro kati ya Mapadri wa Kanisa Katoliki na Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Cornel Magembe kuhusu umiliki wa sehemu ya eneo la shule ya msingi Kagunguli jambo lililosababisha Mapadri kuandika waraka wa kutoshirikiana na mkuu huyo wa wilaya.

Akizungumza katika kikao cha utatuzi wa mgogoro huo uliohusisha Mapadri, Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya na Serikali ya Kijiji  jana wilayani Ukerewe mkoani Mwanza Dkt Mabula alisema maamuzi yote yaliyotolewa nje ya utaratibu kuhusiana na mgogoro huo ni batili na usubiriwe utambuzi wa mipaka ya eneo lenye mgogoro.

‘’ Wizara itatuma timu ya wataalamu ili kutafuta ufumbuzi wa mgogoro kwa kubainisha na kutambua mipaka ya hapa eneo Kagunguli na kuja na ufumbuzi wa kudumu’’ alisema Dkt Mabula.

Aidha, Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ameagiza kupatiwa barua za maeneo yote ya taasisi za dini yenye migogoro mikubwa ya ardhi ili iweze kushughulikiwa na kubainisha kuwa katika kuishughulikia migogoro hiyo timu ya wataalamu itatumwa katika maeneo husika kwa lengo la kubainisha uhalali wa pande zenye migogoro.

Alimtaka Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Ukerewe Estar Chaula kujiandaa kugharamia wataalamu watakaokwenda kubainisha mipaka yenye mgogoro katika halmashauri yake kwa kuwa halmashauri ndizo zenye jukumu la kupanga maeneo yake.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mary Makondo alisema kitakachofanywa na wizara yake sasa kuhusiana na mgogoro huo ni kwenda kufufua mipaka na kuanisha matumizi ya eneo hilo ambapo alisisitiza kuwa ni vizuri maeneo yote ya umma yakawekewa mipaka yenye alama zinazoonekana.

Mkuu wa wilaya ya Ukerewe Cornel Magembe aliweka wazi kuwa, mgogoro uliopo katika eneo linalohusisha shule ya Sekondari Kagunguli inayomilikiwa na Kanisa Katoliki umechochewa kwa kiasi kikubwa na Mkuu wa shule ya Sekondari Kagunguli Padri Johanes Nawachi kwa kile anachodai padre huyo eneo la shule yake kuvamiwa.

Hata hivyo, Magembe alisema katika kutafuta suluhu ya mgogoro huo aliagiza Kanisa Katoliki kuwasilisha Hati ya umiliki eneo lake, huku serikali ya kijiji nayo ikitakiwa kuwasilisha muhtasari wa kijiji kuhusiana na kutolewa sehemu ya eneo sambamba na nyumba tatu za walimu wa shule ya msingi Kagunguli kubaki kama zilivyo ndipo afanye maamuzi kuhusiana na mgogoro huo.

Alisema, kilichofanywa na Mapadri wa Kanisa Katoliki kuandika waraka wa kutoshirikiana naye ni uchochezi kwa waumini wa kanisa hilo na serikali na kubainisha kuwa hali hiyo imesababishwa na msimamo wake wa kuhakikisha maeneo ya serikali yanalindwa.

Kwa upande wake Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Kagunguli Padri Johanes Nawachi alisema kumekuwa na mahusiano mabaya baina yake na Mkuu wa wilaya ya Ukerewe Cornel Magembe baada ya kuanza zoezi la kupanda miti eneo alilodai kumilikiwa na kanisa Katoliki na kuhusisha pia maeneo ya nyumba tatu za walimu wa shule ya msingi Kagunguli.


Share:

Breaking : DEREVA WA BASI LA ISAMILO AFARIKI DUNIA AKIENDELEA NA SAFARI KWENYE BASI



Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Dereva wa Basi la Isamilo lenye namba za usajili T609 CQB Scania linalofanya safari zake kutoka Mwanza kwenda Mbeya Sebastian Mathias (43) mkazi wa Mwanza amefariki dunia wakati akiendelea na safari kutoka Mbeya kwenda Mwanza.

Akizungumza na Malunde 1 blog, Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga ACP Deborah Magiligimba amesema tukio hilo limetokea leo Ijumaa Machi 20,2020 majira ya saa nne asubuhi.

"Sebastian alitoka Mwanza kwenda Mbeya akiwa anajisikia vibaya. Huwa wapo madereva wawili wameenda hadi Mbeya,wakati wanatoka Mbeya kwenda Mwanza alikuwa anaendelea kujisikia vibaya, walipofika Singida akawa anajisikia vibaya zaidi ndipo akabadilishana na yule dereva mwenzake",amesema Kamanda Magiligimba.

"Wamefika Tinde saa nne asubuhi akawa amezidiwa sana, wakambeba kwenda kwenye Kituo cha Afya Tinde,baada ya kumfikisha,Daktari akabaini kuwa tayari Sebastian Mathias alikuwa amefariki dunia",ameeleza Kamanda Magiligimba.

Amesema kwa kuwa gari lina madereva wawili,dereva mwingine ameendelea na safari kwenda Mwanza.

Share:

DOWNLOAD - PAKUA APP YA MALUNDE 1 BLOG ...TUWE TUNAKUTUMIA HABARI ZOTE BURE MOJA KWA MOJA KWENYE SIMU YAKO

Kuwa wa Kwanza kupata habari na matukio yanayojiri Tanzania na dunia kwa ujumla kwa kupakua/ kudownload App ya Malunde 1 blog tukuhabarishe masaa 24.

Tembea na dunia kiganjani mwako sasa.

Pakua App mpya ya Malunde 1 blog imeboreshwa zaidi ili kukidhi mahitaji ya wasomaji wetu. Hii ndiyo mpya kabisa,ina alama hii ↡↡
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Ni rahisi sana : Ingia Play store kisha Andika Malunde 1 blog halafu bonyeza Install

https://bit.ly/2Qb7qyF

Tafadhali fuata maelekezo hapo juu... Usikubali kukosa habari kizembe..Pakua app yetu Mpya ya Malunde1 blog Sasa
Share:

Lipumba aitaka serikali kufunga mipaka. Kukabiliana na Corona.....IGP Sirro Amjibu

Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba ameiomba serikali kuhakikisha inafunga mipaka haraka kuzuia wageni wanaoingia nchini ambao nchi zao zimekumbwa na maambukizi ya virusi vya corona.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana Alhamisi Machi 19, Profesa Lipumba alisema kuendelea kuacha mipaka hiyo bila udhibiti wa wageni hao ni kuendelea kuhatarisha usalama wa afya za wananchi.

Alisema ni vema kukaongezwa uwezo wa vipimo na wataalamu wa kutosha ili kuwabaini wasafiri wanaoingia nchini wanaotoka sehemu mbalimbali za nchi.

“Wakati sasa umefika wa serikali kuamua kufanya uamuzi wa kufunga mipaka yetu, kuweka wataalam na vifaa vya kutosha kwani ugonjwa huu ni hatari na ukiendelea kuingia hapa nchini hali itakuwa mbaya zaidi kwakuwa hata mataifa tajiri wanahangaika nao,”amesema Profesa Lipumba.

Profesa Lipumba ameongeza kuwa wataalamu wasiishie kupima tu kiasi cha joto bali ni vizuri wakajiridhisha zaidi kwa kuchunguza afya ya wasafiri hao.

Hata hivyo Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Tanzania (IGP) Simon Sirro amesema jeshi hilo limejipanga imara kwenye mipaka ili kuhakikisha kwamba watu wanaoingia nchini wanafuata utaratibu na endapo wakibainika kuwa na viashiria vya virusi vya Corona basi hatua zinachukuliwa kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa.
 

IGP Sirro amesema kwa sasa hakuna haja ya kufungwa kwa mipaka lakini kama kutakuwa na sababu ya moja kwa moja vyombo vya usalama vilivyopo katika mipaka vitashauri lakini kutokana na Intelijensia walizozipata hakuna tishio kubwa kiasi hicho mpaka kufikia kufungwa mipaka.

"Sasa elimu tumeshaipata kilichobaki ni sisi watanzania kutekeleza hiyo elimu ambayo tumeipata, manaake ukiipata hiyo elimu, usipoitumia hiyo elimu ukabaki kufanya mambo yako ya zamani mwisho wa siku utaangamiza jamii ya Watanzania" Alisema.


Share:

Idadi ya watu waliofariki dunia kutokana na Corona nchini Italia yazidi ile ya China

Serikali ya Italia ilitangaza jana usiku kwamba idadi ya watu walioaga dunia kutokana na ugonjwa wa COVID-19 (corona) nchini humo imefikia 3,405.

Taarifa iliyotolewa na serikali ya Italia imesema kuwa kesi nyingine mpya za maambukizi ya watu 5322 pia zilisajiliwa katika masaa 24 yaliyopita nchini humo na kuongeza kuwa, hadi kufikia jana jioni watu 41,035 walikuwa wameambukizwa virusi vya corona.

Takwimu hizo za kufariki dunia watu 3,405 nchini Italia kutokana na virusi vya corona zinaonyesha kuwa idadi ya watu waliouawa na virusi hivyo nchini humo sasa imepita ile ya waliouawa na virusi hivyo nchini China ambao walikuwa watu 3,245.

Kutokana na kasi kubwa ya maambukizi ya virusi vya corona, Jumanne iliyopita Waziri Mkuu wa Italia, Giuseppe Conte alitangaza karantini katika maeneo yote ya nchi hiyo yenye idadi ya watu milioni 60.

Jumatano iliyopita peke yake, watu 475 waliaga dunia nchini Italia kutokana na virusi vya corona na idadi hiyo ndiyo ya juu na kubwa zaidi ya wahanga wa virusi hivyo kutokea siku moja katika upeo wa dunia nzima.


Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa March 20





















Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger