Monday, 9 March 2020

Picha : MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI MKOA WA SHINYANGA RAHA MTUPU...SHUHUDIA HAPA

Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) ameongoza Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani mkoa wa Shinyanga ambayo yamefanyika Machi 8,2020 katika kata ya Iselamagazi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga. 

Akizungumza katika maadhimisho hayo yenye Kauli mbiu “Kizazi cha Usawa kwa Maendeleo ya Tanzania ya sasa na ya baadae”, Mhe. Azza aliwataka wanawake kuelekea uchaguzi mkuu wa Tanzania 2020 wachague viongozi waadilifu,wawajibikaji na wenye nia ya kuleta mabadiliko. 

“Nina imani kubwa wanawake mtajitokeza kwa wingi kugombea nafasi za uongozi katika Uchaguzi Mkuu”,alisema  Mhe. Azza. 

“ Naomba niwakumbushe kuwa mwanamke ni fursa katika uchumi wa kaya apewe kipaumbele katika maamuzi ya familia na jamii. Wakati ni sasa chukua hatua,mwanamke simama chukua nafasi kwa maendeleo endelevu ya Tanzania ya sasa nay a baadae”,alisema Mhe. Azza. 

Alisema licha ya serikali kuendelea na mikakati mbalimbali ya kumuinua mwanamke lakini bado eneo la mila na desturi gandamizi,potofu na zenye madhara kuwa ni kikwazo cha kufikia maendeleo ya 50 kwa 50 hususani katika uchumi wa viwanda. 

Mbunge huyo,alitumia fursa hiyo kuwapongeza wanafunzi na walimu wa shule ya Msingi Ilobi iliyopo wilayani Kishapu kwa kufanya vizuri katika mtihani wa kuhitimu darasa la saba mwaka 2019 na kuuletea mkoa wa Shinyanga heshima ambapo kati ya wanafunzi bora wa kike, watano walitoka katika shule ya Ilobi. 

“Shule ya msingi Ilobi wameuletea heshima kubwa mkoa wa Shinyanga. Wanafunzi na walimu wa shuli hii wanahitaji kupewa motisha na shule zingine zikajifunze pale wanafanya nini. Binafsi niliwapatia Kompyuta na Printer yake kama motisha kwao”,alisema Azza. 

Maadhimisho ya Siku ya Wanawake duniani mkoa wa Shinyanga yalianza kwa maandamano ya wadau wa haki za wanawake, ambapo Wanawake wameonesha ujuzi wao na vipaji kwa kuendesha magari, mitambo mikubwa ya kutengeneza miundombinu ya barabara pamoja na gwaride ya Wanawake askari lengo ni kuwatia motisha ya kuachana na mila na desturi za ukandamizaji wa Wanawake na Mtoto wa kike. 

Mgeni rasmi Azza Hilal pia alikabidhi taulo laini za kike zenye thamani ya shilingi milioni 7.7 kwa ajili ya wanafunzi wa kike wanaotarajia kumaliza elimu ya darasa la saba 2020. 

Matukio mengine ni pamoja na Mhe.Azza Kuzindua Timu ya Wanawake mpira wa miguu mkoa wa Shinyanga ‘Shinyanga Super Queen’, kukabidhi Vifaa vya kazi’ Aproni’ kwa Mama Lishe 300 na shilingi 500,000/= kwa mwanamke mwenye ulemavu. 

Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Shinyanga,Tedson Ngwale aliwataka wadau waliofanikisha maadhimisho ya siku ya wanawake mkoa wa Shinyanga kuwa ni pamoja na shirika la World Vision, VSO,CUAMM,Thubutu Africa Initiatives,Rafiki SDO, Life Water International ,Pathfinder,USAID Tulonge Afya,RUDI,YADEE,TANESCO,IBA,TANROADS,TEMESA,ICS,AGAPE,VODACOM,Benki ya CRDB na Kampuni ya Jambo Food Products Ltd.
ANGALIA PICHA ZA MATUKIO HAPA CHINI
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akizungumza kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani mkoa wa Shinyanga ambayo yamefanyika Machi 8,2020 katika kata ya Iselamagazi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akizungumza kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani mkoa wa Shinyanga ambayo yamefanyika Machi 8,2020 katika kata ya Iselamagazi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga. 

Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, James Bwana akizungumza kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani mkoa wa Shinyanga ambayo yamefanyika Machi 8,2020 katika kata ya Iselamagazi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga. 
Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Shinyanga, Tedson Ngwale akizungumza kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani mkoa wa Shinyanga ambayo yamefanyika Machi 8,2020 katika kata ya Iselamagazi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga,Mhe. Hoja Mahiba akizungumza kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani mkoa wa Shinyanga ambayo yamefanyika Machi 8,2020 katika kata ya Iselamagazi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Wadau wakiwa kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.
Wadau wa haki za wanawake wakiwa kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.

Wa pili kushoto ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) na viongozi mbalimbali wakiwasili kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani mkoa wa Shinyanga ambayo yamefanyika Machi 8,2020 katika kata ya Iselamagazi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga. 
Mgeni rasmi Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akikagua kikundi cha wanawake/vijana wa kike wanaojihusisha na masuala ya ujenzi wa nyumba.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akiwa katika banda la Benki ya CRDB.
Afisa wa Benki ya CRDB akimuelezea Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) kuhusu huduma zinazotolewa na Benki ya CRDB.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akiwa katika banda la USAID Tulonge Afya.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) na viongozi mbalimbali wakipokea maandamano ya wadau wa haki za wanawake kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani mkoa wa Shinyanga ambayo yamefanyika Machi 8,2020 katika kata ya Iselamagazi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga. 
Askari polisi wanawake wakiwa kwenye maandamano wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.
Askari polisi wanawake wakiwa kwenye maandamano wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.
Wafanyakazi wa Benki ya CRDB wakiwa kwenye maandamano wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani mkoa wa Shinyanga.
Wanawake wakiwa katika maandamano.
Wanawake wakiwa kwenye maandamano.
Wanawake wanaoendesha magari na mitambo ya kuchonga barabara wakiwa kwenye maandamano.
Wanawake wanaoendesha magari na mitambo ya kuchonga barabara wakiwa kwenye maandamano.
Maandamano yanaendelea.
Wadau wakiendelea na maandamano.
World Vision wakiwa kwenye maandamano.
Maandamano yanaendelea.
Maandamano yanaendelea.
Maandamano yanaendelea.
Maandamano yanaendelea.
Maandamano yanaendelea.
Maandamano yanaendelea.
Maandamano yanaendelea.
Wadau wakiwa kwenye eneo la tukio.

Burudani ya ngoma ikiendelea.
Wadau wakiwa kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani mkoa wa Shinyanga ambayo yamefanyika Machi 8,2020 katika kata ya Iselamagazi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Mgeni rasmi Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) na viongozi wengine wakielekea katika uwanja wa Iselamagazi kwa ajili ya Kuzindua Rasmi Timu ya Wanawake ya mpira wa miguu ya 'Shinyanga Super Queen'.
Wachezaji wa timu za wanawake ' Ngokolo Secondary' kulia na Shinyanga Super Queen wakiwa uwanjani kabla ya kuanza mchezo wa Kuzindua Rasmi Timu ya Wanawake ya mpira wa miguu ya 'Shinyanga Super Queen'.
Mgeni rasmi Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akisalimiana na wachezaji wa Timu ya Wanawake mkoa wa Shinyanga ' Shinyanga Super Queen'
Mgeni rasmi Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akizindua  Timu ya Wanawake mkoa wa Shinyanga ' Shinyanga Super Queen' kwa kurusha mpira.
Mchezo kati ya Shinyanga Super Queen' na Ngokolo ukiendelea ambapo dakika 30 za mchezo zilimalizika kwa timu ya Shinyanga Super Queen Kuichapa Ngokolo Secondary bao 3 -0.
Wadau wakifuatilia mtanange kati ya Shinyanga Super Queen' na Ngokolo ukiendelea ambapo dakika 30 za mchezo zilimalizika kwa timu ya Shinyanga Super Queen Kuichapa Ngokolo Secondary bao 3 -0.
Wadau wakifuatilia mtanange kati ya Shinyanga Super Queen' na Ngokolo ukiendelea ambapo dakika 30 za mchezo zilimalizika kwa timu ya Shinyanga Super Queen Kuichapa Ngokolo Secondary bao 3 -0.
Wadau wakifuatilia mtanange kati ya Shinyanga Super Queen' na Ngokolo ukiendelea ambapo dakika 30 za mchezo zilimalizika kwa timu ya Shinyanga Super Queen Kuichapa Ngokolo Secondary bao 3 -0.
Wadau wakiwa kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani mkoa wa Shinyanga ambayo yamefanyika Machi 8,2020 katika kata ya Iselamagazi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Wadau wakiwa kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani mkoa wa Shinyanga ambayo yamefanyika Machi 8,2020 katika kata ya Iselamagazi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Wadau wakiwa kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani mkoa wa Shinyanga ambayo yamefanyika Machi 8,2020 katika kata ya Iselamagazi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Maafisa wa Shirika la World Vision wakiwa kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani mkoa wa Shinyanga ambayo yamefanyika Machi 8,2020 katika kata ya Iselamagazi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Mgeni rasmi Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akikabidhi zawadi ya mbuzi wawili kwa Mariam Amos mkazi wa Lyabusalu kwa kuwa mshindi wa kwanza mbio za baiskeli kuzunguka uwanja wa mpira mara nne.
Mgeni rasmi Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akikabidhi zawadi ya mbuzi wawili kwa Eunice Emmanuel mkazi wa Mwambasha kwa kuwa mshindi wa pili mbio za baiskeli kuzunguka uwanja wa mpira mara nne.
 Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake duniani mkoa wa Shinyanga.
Wadau wakiwa kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani mkoa wa Shinyanga ambayo yamefanyika Machi 8,2020 katika kata ya Iselamagazi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Wadau wakiwa kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani mkoa wa Shinyanga ambayo yamefanyika Machi 8,2020 katika kata ya Iselamagazi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Wadau wakiwa kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani mkoa wa Shinyanga ambayo yamefanyika Machi 8,2020 katika kata ya Iselamagazi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Wadau wakiwa kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani mkoa wa Shinyanga ambayo yamefanyika Machi 8,2020 katika kata ya Iselamagazi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akicheza muziki na wanawake wakati nyimbo kuhusu wanawake zikipigwa kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani mkoa wa Shinyanga ambayo yamefanyika Machi 8,2020 katika kata ya Iselamagazi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga. 

Wanawake wakicheza muziki wakati nyimbo kuhusu wanawake zikipigwa kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani mkoa wa Shinyanga ambayo yamefanyika Machi 8,2020 katika kata ya Iselamagazi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga. 
Wadau wakiwa kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani mkoa wa Shinyanga ambayo yamefanyika Machi 8,2020 katika kata ya Iselamagazi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Wadau wakiwa kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani mkoa wa Shinyanga ambayo yamefanyika Machi 8,2020 katika kata ya Iselamagazi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Wadau wa haki za wanawake na watoto wakiwa kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani mkoa wa Shinyanga ambayo yamefanyika Machi 8,2020 katika kata ya Iselamagazi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga. 

Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akionesha shilingi 500,000/= zilizotolewa na zilizotolewa na Kampuni ya Utengenezaji na Usambazaji wa Vinywaji baridi ‘Jambo Food Products Limited’ kwa ajili ya  Mwanamke mwenye ulemavu Bi.Happiness Kwigema anayejishughulisha na biashara ya pipi na sabuni za kufulia Mjini Shinyanga. Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Jambo Food Products Limited’,Esme Salum.
Wanafunzi na wadau wakiwa eneo la tukio.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akipiga picha ya pamoja na baadhi ya Mama Lishe katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga baada ya kuwakabidhi vifaa vya kazi 'Aproni'.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akipiga picha ya kumbukumbu na Mama Lishe na Wakurugenzi/Wawakilishi wa wakurugenzi wa halmashauri za wilaya 6 za mkoa wa Shinyanga waliopokea  Aproni na watakwenda kuzigawa kwa Mama Lishe waliopo katika halmashauri zao.
Wanafunzi wakiwa kwenye eneo la tukio.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akielezea namna alivyoshirikiana na wadau mbalimbali kufanikisha kupatikana kwa taulo laini za kike kwa ajili ya wanafunzi wa kike wanaotarajia kumaliza elimu ya darasa la saba mwaka 2020 zenye thamani ya shilingi Milioni 7.7. Kushoto ni sehemu ya maboksi 66 yenye taulo hizo laini za kike.
Afisa Masoko Benki ya CRDB tawi la Shinyanga Mwanahamisi Iddi akionesha risti ya malipo ya fedha iliyotolewa na Benki ya CRDB na kuchangia kufanikisha kupatikana kwa taulo laini za kike kwa ajili ya wanafunzi wa kike wanaotarajia kumaliza elimu ya darasa la saba mwaka 2020 zenye thamani ya shilingi Milioni 7.7 zilizotolewa na wadau mbalimbali mkoa wa Shinyanga waliomuunga Mkono Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga.  Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Jambo Food Products Limited, Esme Salum.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akiwa ameshikilia Taulo laini za kike na wanafunzi wanaosoma darasa la saba katika shule mbalimbali katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akipiga picha ya pamoja na baadhi ya wadau mbalimbali waliofanikisha kupatikana kwa  Taulo laini za kike ‘ Pedi’ zenye thamani ya shilingi milioni 7.7 kwa ajili ya wanafunzi 780 wanaotarajia kuhitimu elimu ya darasa la saba mwaka 2020 kutoka shule 30 mkoa wa Shinyanga.
Wadau wakiwa eneo la tukio.
Maafisa kutoka Shirika la World Vision wakionesha ishara ya usawa la Kijinsia kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake duniani mkoa wa Shinyanga.
Mc Mzungu Mweusi (kushoto) na MC Elipendo John wakiendelea kutoa maelekezo mbalimbali kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani mkoa wa Shinyanga ambayo yamefanyika Machi 8,2020 katika kata ya Iselamagazi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga. 
Wadau wakiwa kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani mkoa wa Shinyanga ambayo yamefanyika Machi 8,2020 katika kata ya Iselamagazi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga. 
Wadau wakiwa kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani mkoa wa Shinyanga ambayo yamefanyika Machi 8,2020 katika kata ya Iselamagazi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga. 
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Share:

Picha : WORLD VISION YASHIRIKI MAADHIMISHO SIKU YA WANAWAKE DUNIANI...YAHAMASISHA KLINIKI KWA WAJAWAZITO, MATUMIZI YA MAZIWA YA MBUZI

Kushoto ni Afisa Lishe Mradi wa ENRICH unaotekelezwa na Shirika la World Vision , Stella Mbuya  na Afisa Jinsia na Utetezi wa Shirika la World Vision kupitia mradi wa ENRICH, Magreth Mambali wakionesha alama ya Usawa wa Kijinsia.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Wanawake wajawazito wamekumbushwa umuhimu wa kuhudhuria Kliniki angalau mara nne katika kipindi chote cha ujauzito ili waweze kupata huduma zote za msingi ili wajifungue salama kupunguza vifo vya uzazi vya mama na mtoto. 

Rai hiyo imetolewa na Afisa Lishe Mradi wa ENRICH unaotekelezwa na Shirika la World Vision katika mikoa ya Shinyanga na Singida, Stella Mbuya wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Mkoa wa Shinyanga yaliyofanyika Machi 8,2020 katika kata ya Iselamagazi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga. 

Mbuya alisema endapo mama mjamzito atahudhuria kliniki itamsadia kupata huduma zote za msingi katika kipindi chote cha ujauzito ili aweze kujifungua salama ili kupunguza vifo vya uzazi na mtoto ambavyo pia husababishwa na Lishe duni. 

“World Vision kupitia mradi wetu wa ENRICH,tunahamasisha akina mama kula vyakula kwa kuzingatia mlo kamili unaoundwa na makundi matano ya chakula ili kuimarisha afya ya uzazi na lishe kwa mama na mtoto aliyepo tumboni”,alisema Mbuya. 

“World Vision pia tunaendelea kuwahamasisha matumizi ya maziwa ya mbuzi kwa sababu maziwa ya mbuzi yana uwiano wa virutubishi/viini lishe vilivyopo kwenye maziwa ya mbuzi yanakaribiana sana na maziwa ya binadamu tofauti na wanyama wengine ama maziwa ya kopo”,alisema Mbuya. 

Mbuya aliwakumbusha akina mama wajawazito kutumia vidonge vya madini chuma na Asidi ya Foliki ‘Folic acid sambamba na viazi lishe na mboga za majani yakiwemo matembele kwa ajili ya kuongeza damu mwilini ili kukabiliana na vifo vinavyotokana na upungufu wa damu. 

Kwa upande wake,Afisa Jinsia na Utetezi wa Shirika la World Vision kupitia mradi wa ENRICH unaofadhiliwa na serikali ya Canada, Magreth Mambali aliwataka wanawake kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi za uongozi katika uchaguzi mkuu 2020 unaohusika Madiwani, Wabunge na Rais. 

“Tunapoelekea kwenye uchaguzi Mkuu,World Vision tunasisitiza kumpa mwanamke nafasi katika nyanja zote ikiwemo kiuchumi na kisiasa.Tunapenda mwanamke ashiriki katika ngazi za maamuzi kuanzia ngazi ya familia mpaka taifa kwa sababu wanawake tunaweza na tumeshuhudia wanawake wengi wanafanya vizuri katika masuala ya uongozi,Mfano Mzuri ni mama yetu Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan”,alieleza Mambali. 

Mambali aliitaka jamii kuwalinda watoto wa kike dhidi ya mimba na ndoa za utotoni na kutomaliza masomo shuleni akibainisha kuwa mlinzi wa kwanza wa mtoto wa kike ni jamii inayomzunguka. 

Katika hatua nyingine alifafanua kuwa,World Vision kupitia mradi wa ENRICH inatekeleza afua zake kwa kuunda vikundi mbalimbali ikiwemo vikundi vya ‘Baba wanaojali’ ambao wamepata mafunzo ya kuwa baba wanaojali familia zao na kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto. 

Alivitaja vikundi vingine kuwa ni VICOBA kwa wanawake,klabu za afya ya uzazi kwa vijana katika shule za msingi na sekondari na vikundi vya Sauti ya Umma na Utendaji ambavyo vinajihusisha na utoaji elimu kwa wanawake juu ya umuhimu wa kuhudhuria kliniki na kujifungulia katika vituo vya afya. 

Kwa upande Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Shinyanga, Tedson Ngwale aliwapongeza World Vision kwa kuendelea kushirikiana na serikali kuhamasisha wanawake kuzingatia lishe ili kupunguza vifo vitokanavyo na lishe duni. 

Naye Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) alitoa wito kwa wazazi na walezi kupeleka watoto shule na kutowaozesha wangali wadogo huku akiwahamasisha wanawake kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi za uongozi katika uchaguzi mkuu 2020. 

Kauli mbiu ya Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani Machi 8,2020 ni “Kizazi cha Usawa kwa Maendeleo ya Tanzania ya sasa na ya baadae”.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (katikati) akipokea maandamano ya wadau mbalimbali wa haki za wanawake na watoto wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Mkoa wa Shinyanga yaliyofanyika Machi 8,2020 katika kata ya Iselamagazi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.Kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Mhe. Hoja Mahiba. Kushoto ni Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Kaimu ni James Bwana. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Maafisa kutoka Shirika la World Vision kupitia Mradi wa ENRICH wakiwa wamebeba bango lenye ujumbe wa ' Mlinde Mtoto wa kike, Mpe Mwanamke Nafasi' na Kauli Mbiu ya Siku ya Wanawake Duniani mwaka 2020 ' “Kizazi cha Usawa kwa Maendeleo ya Tanzania ya sasa na ya baadae”.
Askari polisi wanawake wakiwa kwenye maandamano wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Mkoa wa Shinyanga yaliyofanyika katika kata ya Iselamagazi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akizungumza kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Mkoa wa Shinyanga ambapo alitoa wito kwa wazazi na walezi kupeleka watoto shule na kutowaozesha wangali wadogo.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akizungumza kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Mkoa wa Shinyanga na kuwahamasisha wanawake kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi za uongozi katika uchaguzi mkuu 2020. 
Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Shinyanga, Tedson Ngwale akilipongeza shirika la World Vision kwa kuendelea kushirikiana na serikali kuhamasisha wanawake kuzingatia lishe ili kupunguza vifo vitokanavyo na lishe duni. 
Maafisa kutoka Shirika la World Vision kupitia Mradi wa ENRICH wakiwa na  matembele na viazi lishe,wameshikilia vipeperushi kwenye banda lao la maonesho kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Mkoa wa Shinyanga yaliyofanyika katika kata ya Iselamagazi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Maafisa kutoka Shirika la World Vision kupitia Mradi wa ENRICH wakiwa wameshikilia vipeperushi kwenye banda lao la maonesho kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Mkoa wa Shinyanga yaliyofanyika katika kata ya Iselamagazi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Viazi Lishe vikiwa kwenye banda la World Vision kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Mkoa wa Shinyanga yaliyofanyika katika kata ya Iselamagazi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga
Afisa Lishe Mradi wa ENRICH unaotekelezwa na Shirika la World Vision katika mikoa ya Shinyanga na Singida, Stella Mbuya akionesha mboga za majani 'matembele' ambayo akina mama wajawazito wanashauriwa kutumia ili kukabiliana na tatizo la upungufu wa damu.
Maafisa kutoka Shirika la World Vision kupitia Mradi wa ENRICH wakiwa na mbuzi kwenye bando lao la maonesho wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Mkoa wa Shinyanga yaliyofanyika katika kata ya Iselamagazi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Maafisa kutoka Shirika la World Vision kupitia Mradi wa ENRICH wakionesha alama ya Usawa wa Kijinsia wakati Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Mkoa wa Shinyanga yaliyofanyika katika kata ya Iselamagazi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Maafisa kutoka Shirika la World Vision kupitia Mradi wa ENRICH wakionesha alama ya Usawa wa Kijinsia wakati Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Mkoa wa Shinyanga yaliyofanyika katika kata ya Iselamagazi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Share:

Sunday, 8 March 2020

Picha : KAMPUNI YA JAMBO YAMCHANGIA SHILINGI 500,000/= KUONGEZA MTAJI MWANAMKE SHUJAA MWENYE ULEMAVU

Kampuni ya Utengenezaji na Usambazaji wa Vinywaji baridi ‘Jambo Food Products Limited’ ya mkoani Shinyanga imemsaidia mtaji wa shilingi 500,000/= Mwanamke mwenye ulemavu Happiness Kwigema anayejishughulisha na biashara ya pipi na sabuni za kufulia Mjini Shinyanga.

Fedha hizo Taslimu zimekabidhiwa na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) kwenye Maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani ambayo katika mkoa wa Shinyanga yaliyofanyika katika kijiji cha Iselamagazi kata ya Iselamagazi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Jambo Food Products Limited’,Esme Salum amesema Jambo imeguswa na kujituma kwa mwanamke huyo ‘Mama Shujaa Happiness na kuamua kumpatia shilingi Laki 5 ili aongeze mtaji katika biashara anazozifanya.

“Happiness Kwigema ni mwanamke mwenye ulemavu lakini anajituma katika kazi,anajishughulisha na biashara ndogo ndogo ili kujipatia kipato.Kwetu tunamuona ni Mama Shujaa,tumeamua kumchangia shilingi 500,000/=”,alisema Salum.

Alisema katika kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani Jambo mbali na kumchangia Bi. Happiness Kwigema pia wameshiriki maadhimisho ya siku ya wanawake duniani kwa kuchangia katoni 20 za maji,Shilingi milioni 1 kwa ajili ya Taulo za kike kwa wanafunzi wa kike wanaotarajia kufanya mtihani wa Darasa la saba mwaka 2020.
Soma pia : MBUNGE AZZA HILAL AKABIDHI TAULO ZA KIKE 'PEDI' ZA MIL 7.8 KWA WANAFUNZI WA KIKE DARASA LA SABA 2020

"Katika kushiriki kikamilifu katika kumuenzi Mwanamke na kutambua mchango wake katika ajira, katika Kiwanda cha Jambo Food Products Ltd tunazingatia sana usawa wa kijinsia kwani mpaka sasa wastani wa ajira zetu Kiwandani ni 45% wanawake na 55% wanaume, lakini lengo letu likiwa ni kufikia 50%  kwa 50%",alisema Mkurugenzi wa Kampuni ya Jambo.

 "Kwa mara ya kwanza kwa sasa kiwandani tumeajiri Machine Operators wanawake, Mafundi umeme na Mafundi magari, lakini pia kwa kuwa tuna mpango wa kufungua viwanda vingine vipya vya asali, biscuits, pipi na ice cream tutaajiri pia Engiiners wanawake. Ikumbukwe kwa miaka mingi baadhi ya kazi zilionekana kufanywa na wanaume tu kutokana na Mila na Desturi gandamizi. Ni imani yetu sura hii itatoa hamasa kubwa kwa Jamii",aliongeza Salum.

Kwa Upande wake Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad ambaye alikuwa Mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani mkoa wa Shinyanga, amempongeza Bi. Happiness Kwigema kwa kujituma kufanya shughuli za kumwingizia kipato na kuwashauri wanawake wengine kuiga mfano wa Happiness kwa kufanya kazi za kuwaingizia kipato.

Mhe. Azza pia ameipongeza Kampuni ya Jambo kwa michango inayoendelea kuitoa katika jamii akibainisha kuwa Jambo wamekuwa wadau wazuri wa maendeleo mkoani Shinyanga.
Kushoto ni Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Shinyanga ,Tedson Ngwale akimtambulisha Bi. Happiness Kwigema (kulia), Mwanamke mwenye ulemavu Shujaa anayejituma katika kazi ambaye amekabidhiwa shilingi 500,000/= na Kampuni ya Vinywaji Jambo Food Products Ltd kwa ajili ya kuongeza mtaji wake wa kuuza pipi na sabuni za kufulia. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mgeni rasmi kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Mkoa wa Shinyanga ambaye ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (katikati) akizungumza wakati wa Kukabidhi shilingi 500,000/= za mtaji zilizotolewa na Kampuni ya Utengenezaji na Usambazaji wa Vinywaji baridi ‘Jambo Food Products Limited’ kwa Mwanamke mwenye ulemavu Happiness Kwigema anayejishughulisha na biashara ya pipi na sabuni za kufulia Mjini Shinyanga.

Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akionesha shilingi 500,000/= zilizotolewa na zilizotolewa na Kampuni ya Utengenezaji na Usambazaji wa Vinywaji baridi ‘Jambo Food Products Limited’ kwa ajili ya  Mwanamke mwenye ulemavu Bi.Happiness Kwigema anayejishughulisha na biashara ya pipi na sabuni za kufulia Mjini Shinyanga. Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Jambo Food Products Limited’,Esme Salum.
Kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Jambo Food Products Limited’,Esme Salum akinyoosha mkono wakati Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akionesha shilingi 500,000/= zilizotolewa na zilizotolewa na Kampuni ya Utengenezaji na Usambazaji wa Vinywaji baridi ‘Jambo Food Products Limited’ kwa ajili ya  Mwanamke mwenye ulemavu Bi.Happiness Kwigema.
Bi.Happiness Kwigema akishukuru baada ya kukabidhiwa shilingi 500,000/= zilizotolewa na Kampuni ya Jambo Food Products Limited’ ili zimsaidie kuongeza mtaji wa biashara anazofanya.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Jambo Food Products Limited’,Esme Salum na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM)  pamoja na viongozi mbalimbali wakipiga picha na Bi. Happiness Kwigema.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive

Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger