Wednesday, 4 March 2020

Picha : MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU AFUNGUA KONGAMANO KUADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI...AWATAKA WANAWAKE KUJITOSA UCHAGUZI MKUU 2020



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati wa Kongamano la Kuadhimisha na Kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani na Miaka 25 baada ya Mkutano wa Beijing linalofanyika katika Ukumbi wa Hyatt Regency Hotel Jijini Dar es salaam. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

****
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewataka Wanawake kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi mbalimbali za Uongozi ikiwemo Udiwani na Ubunge katika Uchaguzi Mkuu wa Tanzania mwaka 2020.

Mhe. Samia ametoa wito huo leo Jumatano Machi 4,2020 wakati akifungua Kongamano la Kuadhimisha na Kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani na Miaka 25 baada ya Mkutano wa Beijing linalofanyika katika Ukumbi wa Hyatt Regency Hotel Jijini Dar es salaam.

Alisema Mwaka 2020 ni mwaka wa uchaguzi hivyo ni vyema wanawake wakajitokeza kuwania nafasi za uongozi huku akiwataka wanawake kuacha tabia ya kubezana pale mwenzao anapojitokeza kugombea nafasi za uongozi.

“Huu ni mwaka wa uchaguzi,Wanawake tujitokeze katika majimbo,tujitokeze kwa wingi katika nafasi za udiwani na kisha tujaze kwa wingi fomu za viti maalumu. Tuhamasishe wanawake wajitokeze kugombea nafasi za uongozi”,alisema.

“Wanawake ni Jeshi kubwa katika kuleta usawa lakini cha kushangaza Mwanamke ndiyo wa kwanza kumponda mwenzie. Haya tuyaache,Ukiona mwanamke mwenzio kachukua fomu ya kugombea msaidie siyo kumponda.Mimi mwenyewe nimefikia hatua hii baada ya kushikwa mkono”,aliongeza.

Aliwaasa wanawake kushikamana kuiomba jamii kwa kuwashika mkono wanawake wenye sifa za kuwa viongozi ili kuhakikisha idadi ya wanawake katika meza za maamuzi inaongezeka hatimaye kufikia usawa wa kijinsia.

Alisema kuhusu suala la ushiriki wa wanawake katika meza ya maamuzi serikali imechukua hatua kadhaa ili kuondoa vizingiti vinavyowazuia wanawake wasishiriki kikamilifu katika meza ya maamuzi.

“Changamoto iliyopo ni uchache wa wanawake wenye uwezo wa kugombea nafasi mbalimbali iwe kwenye uongozi wa kisiasa,biashara,asasi za kiraia na sekta binafsi. Ni jukumu letu kama watetezi wa haki za wanawake kushawishi wanawake wenye uwezo kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi mbalimbali katika Nyanja tofauti”,alisema.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika lisilo la kiserikali la Women Fund Tanzania (WFT) Prof. Ruth Meena Prof. Meena kutoka WFT,alisema licha ya wanawake kuwa nguzo kuu ya Maendeleo katika kukuza uchumi wa nchi bado wanabeba mzigo mkubwa wa kulea na kuendeleza kizazi cha taifa bila nyenzo wezeshi katika kaya na jamii zao hali inayosababisha umaskini na ufukara wa dunia kuendelea kubeba sura ya mwanamke na msichana.

Prof. Meena kutoka WFT inayofanya shughuli za utetezi wa haki za wanawake na ujenzi wa tapo ya wanawake Tanzania,alisema pamoja na ongezeko la wanawake na wasichana katika uongozi na meza za maamuzi lakini bado ushiriki wao katika katika meza hizo za maamuzi haupo sawia katika Nyanja zote za kisiasa,kiuchumi na hata ki – ustawi wa jamii. 

“Pamoja na jitihada mbalimbali zinazofanyika kuleta mabadiliko kwenye sera na sheria za nchi,bado kuna mifumo kandamizi na ya kiubaguzi katika mifumo hi, hivyo kuna umuhimu wa uwajibikaji zaidi kwenye kubomoa mifumo kandamizi hususani mfume dume”,alisema. 

Kongamano la Kuadhimisha na Kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani na Miaka 25 baada ya Mkutano wa Beijing likiongozwa na Kauli mbiu ya ''Uwajibikaji wa uongozi kwenye kujenga kizazi cha usawa wa jinsia'' limeandaliwa na  Mtandao wa Wanawake na katiba, Uchaguzi na Uongozi kwa ufadhili wa Women Fund Tanzania, Global Affairs Canada, Embassy of Ireland, High Commission of Canada na WiLDAF. 

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati wa Kongamano la Kuadhimisha na Kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani na Miaka 25 baada ya Mkutano wa Beijing linalofanyika katika Ukumbi wa Hyatt Regency Hotel Jijini Dar es salaam. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwahamasisha wanawake kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi za uongozi katika Uchaguzi Mkuu wa Tanzania mwaka 2020.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika lisilo la kiserikali la Women Fund Tanzania (WFT) linalofanya shughuli za utetezi wa haki za wanawake na ujenzi wa tapo ya wanawake Tanzania, Prof. Ruth Meena akizungumza wakati wa Kongamano la Kuadhimisha na Kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani na Miaka 25 baada ya Mkutano wa Beijing.
Mwenyekiti wa Bodi ya WFT, Prof. Ruth Meena akizungumza wakati wa Kongamano la Kuadhimisha na Kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani na Miaka 25 baada ya Mkutano wa Beijing.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Lilian Liundi akizungumza wakati wa majadiliano kwenye Kongamano la Kuadhimisha na Kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani na Miaka 25 baada ya Mkutano wa Beijing.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Lilian Liundi akizungumza wakati wa majadiliano kwenye Kongamano la Kuadhimisha na Kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani na Miaka 25 baada ya Mkutano wa Beijing.
Mkurugenzi Mtendaji wa  Shirika la Msichana Initiative Rebeca Gyumi akizungumza wakati wa majadiliano kwenye Kongamano la Kuadhimisha na Kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani na Miaka 25 baada ya Mkutano wa Beijing.
Wadau wa haki za wanawake wakiwa kwenye kwenye Kongamano la Kuadhimisha na Kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani na Miaka 25 baada ya Mkutano wa Beijing.

Wadau wa haki za wanawake wakiwa kwenye Kongamano la Kuadhimisha na Kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani na Miaka 25 baada ya Mkutano wa Beijing.

Meneja Miradi wa shirika la Young Women Leadership (YWL) mkoani Shinyanga Veronica Massawe akichangia hoja 
kwenye Kongamano la Kuadhimisha na Kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani na Miaka 25 baada ya Mkutano wa Beijing.

Wadau wakiwa ukumbini.

Wadau wa haki za wanawake wakiwa kwenye kwenye Kongamano la Kuadhimisha na Kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani na Miaka 25 baada ya Mkutano wa Beijing.
Wadau wa haki za wanawake wakiwa kwenye kwenye Kongamano la Kuadhimisha na Kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani na Miaka 25 baada ya Mkutano wa Beijing.
Wadau wa haki za wanawake wakiwa kwenye kwenye Kongamano la Kuadhimisha na Kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani na Miaka 25 baada ya Mkutano wa Beijing.
Wadau wa haki za wanawake wakiwa kwenye kwenye Kongamano la Kuadhimisha na Kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani na Miaka 25 baada ya Mkutano wa Beijing.
Wadau wa haki za wanawake wakiwa kwenye kwenye Kongamano la Kuadhimisha na Kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani na Miaka 25 baada ya Mkutano wa Beijing.
Wadau wa haki za wanawake wakiwa kwenye kwenye Kongamano la Kuadhimisha na Kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani na Miaka 25 baada ya Mkutano wa Beijing.
Wadau wa haki za wanawake wakiwa kwenye kwenye Kongamano la Kuadhimisha na Kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani na Miaka 25 baada ya Mkutano wa Beijing.
Wadau wa haki za wanawake wakiwa kwenye kwenye Kongamano la Kuadhimisha na Kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani na Miaka 25 baada ya Mkutano wa Beijing.
Wadau wa haki za wanawake wakiwa kwenye kwenye Kongamano la Kuadhimisha na Kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani na Miaka 25 baada ya Mkutano wa Beijing.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipiga picha ya pamoja na washiriki wa Kongamano la Kuadhimisha na Kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani na Miaka 25 baada ya Mkutano wa Beijing linalofanyika katika Ukumbi wa Hyatt Regency Hotel Jijini Dar es salaam. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Share:

Maalim Seif Amkaribisha Membe Act-wazalendo

Mshauri Mkuu wa chama cha ACT- Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad amemkaribisha katika chama hicho aliyekuwa Mwanachama wa CCM, Bernard Membe huku akimtaka kutokuwa na masharti

Maalim Seif ametoa kauli hiyo leo Jumatano Machi 4, 2020 katika mahojiano na Gazeti la Mwananchi Communications Limited (MCL).

Membe na makatibu wakuu wawili wastaafu, Abdulrahman Kinana na Yusufu Makamba walifikishwa mbele ya kamati ndogo ya udhibiti na nidhamu kujibu mashtaka ya kinidhamu na kisha baadae kupewa adhabu huku Mzee Makamba akisamehewa.

 “Ya ndugu yangu Membe sisi chama chetu kitampokea yoyote atakayekuja mradi asije na masharti,” amesema Maalim Seif.

Alipoulizwa kuhusu kuomba msamaha ili arejee CCM, Maalim Seif  amesema angeweza kuomba msamaha tangu wakati wa Mwalimu Julius Nyerere akiwa Mwenyekiti wa CCM.

“Wakati huo kulikuwa na mawazo hayo kwamba tumewaonea hawa vijana tumewafukuza, kwamba wakiomba radhi tutawarejesha. Mimi nikasema sijasahau kitu CCM  nirudi kutafuta nini? Kwanza watuondoe, kwamba nitarudi CCM No, never. Sitorudi CCM,” amesema.

-Mwananchi


Share:

Watatu Watiwa Mbaroni Kwa tuhuma za wizi kwenye nyumba za kulala wageni Jijini Mbeya

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA
 
KUKAMATWA KWA WATUHUMIWA WA WIZI KWENYE NYUMBA ZA KULALA WAGENI.

Jeshi la Polisi mkoani Mbeya linawashikilia watuhumiwa watatu kwa tuhuma za wizi kwenye nyumba za kulala wageni [Guest House] ambao ni:-

1. WAMBURA DANIEL [47] Mkazi wa Kyabakari Mkoani Mara.

2. SELVANUS MATIKO [53] Mkazi wa Manyamanyama – Bunda.

3. JEREMIA KAKURU [45] Mkazi wa Ukerewe Nansio

Tukio hilo limetokea mnamo tarehe 29.02.2020 majira ya saa 13:00 mchana huko Stendi ya Ilomba, Kata ya Ilomba, Tarafa ya Iyunga, Jijini Mbeya.

Ni kwamba mnamo tarehe 29.02.2020 majira ya saa 06:00 asubuhi watuhumiwa wakiwa wamepanga katika moja ya nyumba za kulala wageni walimvizia mpangaji mmoja aitwaye RIZIKI MGWAMA [31] Mkazi wa Mafinga alipokwenda kuoga na kufunga chumba chake lakini watuhumiwa walifungua kufuli la chumba hicho kwa kutumia waya maalum na kisha kuingia ndani na kuiba begi ambalo ndani yake lilikuwa na vitu vifuatavyo:-

1. Laptop moja aina ya hp.
2. Simu ndogo aina ya Samsung
3. Power bank mbili
4. Nyaraka mbalimbali na vitambulisho vya kazi.

Watuhumiwa wamefikishwa Mahakama ya Mwanzo Mbeya Mjini CC.NO.140/2020 – Wizi kwenye Magesti.

KUKAMATWA KWA MTUHUMIWA WA UVUNJAJI.
Jeshi la Polisi mkoani Mbeya linamshikilia kijana mmoja aitwaye GIFT BRITHON [20] Mkazi wa Mapelele kwa tuhuma za kuhusika kwenye matukio ya uvunjaji na wizi wa mali mbalimbali.

Tukio hilo limetokea mnamo tarehe 03.03.2020 majira ya 21:00 usiku huko eneo la Mapelele, Kata ya Ilemi, Tarafa ya Sisimba, Jijini Mbeya baada ya Jeshi la Polisi kufanya msako na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa akiwa na vifaa mbalimbali vya kuvunjia ambao ni Nondo, Bisibisi, Patasi na Tindo.

Aidha mtuhumiwa baada ya kupekuliwa alikutwa na mali za wizi ambazo ni:-

1. Pikipiki moja MC 233 CEJ aina ya T-Better
2. TV Flat Screen mbili aina ya Samsung
3. Redio Sub Woofer moja [01].
4. Spika mbili [02]
5. Remote Control moja [01]
6. Vitenge doti kumi na tatu [13]
7. Sandals jozi mbili [02]

Mtuhumiwa amekiri kuhusika kwenye matukio ya uvunjaji na wizi katika maeneo mbalimbali hapa Mbeya na atafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi wa shauri hili kukamilika.

RAI YA JESHI LA POLISI KWA WAZAZI/WALEZI KUTOKANA NA MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linatoa rai kwa wazazi na walezi kuwa makini na watoto wao wadogo ikiwa ni pamoja na kuwawekea uangalizi mzuri kwa muda wote ili kuepuka madhara yanayoweza kuwapa watoto hao pindi wanapokuwa wenyewe.

Kwa kipindi cha hivi karibuni, kumekuwa na matukio ya watoto wadogo kufariki kutokana na kutumbukia katika visima vya maji, katika mabwawa ya maji, madimbwi yenye maji au katika mito pindi wanapovuka kuelekea Shuleni au wanapocheza.

Katika msimu huu wa mvua zinazoendelea kunyesha maeneo mbalimbali tayari zimeanza kuleta madhara kwa binadamu hasa watoto wadogo. Yapo mambo ya kuepuka hasa matumizi ya vifaa vya umeme kama vile redio, tv na simu za mkononi wakati mvua kubwa zinazoambatana na radi zikinyesha.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linatoa tahadhari kufuatia matukio ya kufa maji yanayosababishwa na uzembe wa kutovaa maboya wakati wanapoingia majini, mtoni au ziwani.

Aidha kufuatia mvua zinazonyesha nawasihi wazazi kuwapeleka watoto wadogo shuleni na kuwapokea ili kuwalinda dhidi ya madhara ya kutumbukia katika maji.
 
Pia tunatoa angalizo kwa watu wanaofanya shughuli za uchimbaji madini katika migodi, kuchukua tahadhari za kiusalama ili kuepuka ajali katika maeneo hayo hasa za kuangukiwa vifusi vya udongo hususani msimu wa huu wa mvua.

Tunapaswa kuchukua tahadhari kwa kufukia mashimo yasiyokuwa na dhahabu kwani ni hatari kwa watoto na watu wazima pindi yanapojaa maji.

Ni wito wetu Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kwa wazazi, walezi na jamii kwa ujumla kuzingatia ulinzi wa mtoto, malezi bora kwa mtoto na pia kuwasaidia watoto hasa kuwavusha katika maeneo yenye mito au maji mengi ili kuepuka madhara yanayoweza kuwapata. Pia ni kipindi cha kufukia mashimo, madimbwi yenye maji kwani ni hatari hasa kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali.


Share:

CHADEMA Wajutia Makosa ya 2015.....Baraza la Wazee Lamkataa Benard Membe

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema kinajutia uamuzi kiliochukua wakati wa kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, kuchukua wale waliokatwa kutoka CCM ambao sasa wamerejea katika chama chao cha zamani.

Akizungumza ofisi za Makao Makuu ya Chadema jana, Mwenyekiti wa Baraza la Wazee la Chadema (Bazecha), Hashim Juma alisema pamoja na heshima aliyonayo kwa aliyekuwa mgombea wa Ukawa mwaka 2015, Edward Lowassa, lakini tathmini ya baraza hilo imeonyesha hakuwa na msaada mkubwa kwenye chama.

“Kwa kweli katika Uchaguzi Mkuu wa 2015 tuliweka mgombea dhaifu ambaye kwanza alishindwa kulinda kura zetu kwa sababu ya u-CCM wake ambao hakuuvua wakati huo.

“Lakini pia ndani ya Ukawa tulisimamisha mgombea mwenza ambaye pia hakuwa mwana Chadema, hivyo hakuwa na uchungu na chama chetu.

“Kwa hiyo, hatutaki kuona makosa tuliyoyafanya mwaka 2015 yakijirudia mwaka huu, hasa baada ya kukijenga chama nchi nzima kuanzia ngazi ya chini kabisa, kazi tuliyoifanya kwa miaka miwili.

“Ni wazi kwamba tayari kuna mmoja wa viongozi wakuu wa chama, ambaye ana uchungu na chama, aliyeko nje ya nchi kwa sasa, ambaye ameshaeleza utayari wake wa kuwania urais iwapo atateuliwa na chama kwa hiyo huyo ndiye tunayemuunga mkono,” alisema Juma.

Mwenyekiti huyo wa Bazecha alisisitiza kuwa kwa sasa hawako tayari kutumika kama njia ya baadhi ya wanasiasa kutaka kutimiza mahitaji yao binafsi kwa kuingia katika chama hicho na wakikosa wanachokihitaji wanarejea kule walikotoka, kama walivyofanya baadhi ya wanasiasa walioingia Chadema kisha kurejea CCM baada ya kushindwa kutimiza malengo yao binafsi.

Alisema japokuwa baraza hilo halina mamlaka ya Kamati Kuu ya chama, wala ya mkutano mkuu, baraza hilo linatamka wazi kwamba haliko tayari kuona uongozi wa chama hicho ukizungumza suala la kumpokea Bernard Membe, aliyekuwa mwanachama wa CCM ambaye Kamati Kuu ya chama chake imeridhia kwa kauli moja kumvua uanachama.

“Sisi kama wazee tumemridhia na tunampa baraka zetu zote Lissu, kwa hivyo Mheshimiwa Membe tunamtakia kila la kheri na kama atakwenda chama kingine, tutashukuru na tutafurahi kwa sababu kwa vyovyote vile anakwenda kuzigawa kura za CCM.

“Ni kwa sababu, Membe hawezi kuchukua kura hata moja ya Chadema, ataondoka na kundi kubwa la CCM kama Lowasa hivyo atapata kura za chama atachoenda pamoja na za CCM.” amesema Mzee Hashimu. 


Wakati huo huo Mzee Hashimu ameeleza, msimamo wa baraza hilo ni kupigania Tume Huru ya Uchaguzi ili uchaguzi wa tarehe 25 Oktoba 2020 uwe wa huru na haki.


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger