Monday, 3 February 2020

BRELA YAJIDHATITI UTOAJI WA HUDUMA BORA KWA WADAU WAKE


Afisa Mtendaji Mkuu wa BRELA akiwa katika kikao cha kwanza na wafanyakazi tangu ateuliwe kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano BRELA Ofisi Kuu, Jijini Dar es Salaam.
**
Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) imeweka mikakati mizuri katika kuhakikisha kwamba wadau wake wanapata huduma yenye ubora.

Hayo yamebainishwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa BRELA, Bw. Godfrey Nyaisa katika kikao cha wafanyakazi kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano BRELA Ofisi Kuu, Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika kikao hicho Bw. Nyaisa amewataka wafayakazi kufanya kazi kwa bidii na kila mmoja kuwa tayari kusikiliza na kumsaidia mteja punde anapokutana naye.

“BRELA ni Taasisi ya Umma na msingi wake ni kutoa huduma kwa Watanzania wote katika hali ya haki na Usawa bila kujali tofauti za dini, kabila au siasa”, alisema Bw. Nyaisa.

Akizungumzia kuhusu maoni ya wadau kuhusu changamoto ya mfumo, Bw. Nyaisa amebainisha kwamba tayari suala la mfumo linafanyiwa kazi na punde suala hilo litabaki kuwa historia.

“Changamoto ya mfumo wa usajili imezungumzwa na wadau wengi, hivi sasa mfumo wa usajili unafanyiwa maboresho makubwa ili kurahisisha upatikanaji wa huduma za BRELA kwa njia ya mtandao.

Sambamba na hilo uelewa kwa wadau wengi juu ya matumizi ya mfumo huu bado upo chini, hivyo jitihada za ziada zimefanyika kuandaa kituo cha miito ya simu mahususi kwa ajili ya kutoa huduma kwa wadau wetu kwa ukaribu zaidi”.Alibainisha Bw. Nyaisa.

Aidha Bw. Nyaisa ametoa wito kwa wadau BRELA kuendelea kuhuisha taarifa za Makampuni na Majina ya Biashara yaliyosajiliwa nje ya mfumo wa mtandao wakati changamoto wanazokutana nazo zikiendelea kufanyiwa kazi.
Wafanyakazi wa BRELA wakifuatilia kwa umakini maelekezo ya Afisa Mtendaji Mkuu Bw. Godfrey Nyaisa (hayupo pichani) katika kikao cha wafanyakazi kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano BRELA Ofisi Kuu, Jijini Dar es Salaam.
Share:

KATIBU MKUU WA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA ADHAMIRIA KUTEKELEZA SERA YA TANZANIA YA VIWANDA


KatibuMkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Prof. Riziki Silas Shemdoe akiongea na Wakuu wa Taasisi zilizopo chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara.
KatibuMkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Prof. Riziki Silas Shemdoe akisalimia na Wakuu wa Taasisi zilizopo chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara.
Watendaji Wakuu wa Taasisi Mbalimbali wakimsikiliza Prof. Riziki Silas Shemdoe (Mbele kulia) Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara.
***
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Prof. Riziki Shemdoe ameweka bayana adhama yake ya kujikita katika utekelezaji wa sera ya Tanzania ya Viwanda.

Prof Shemdoe amebainisha hayo leo Januari 3, 2020 alipokutana na Watendaji Wakuu wa Taasisi na Wakala zilizo chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara kwenye kikao kilichofanyika katika ofisi ndogo ya Wizara iliyopo waterfront Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika kikao hicho amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kumuamini na kumpatia dhamana hiyo ambayo hakuitarajia.

“Namshukuru Mwenyezi MUNGU na Mhe. Rais John Pombe Magufuli kwa kuniamini na kuniteua kuwa Katibu mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara ambayo imebeba dhima ya kuwa na uchumi wa Viwanda”. Alisema Prof Shemdoe.

Aidha amewataka Watendaji Wakuu wa Taasisi na Wakala zilizo chini ya Wizara hiyo kujipanga kisawa sawa, kutambua wajibu mkubwa walionao kwa Tanzania na Zaidi ya yote kwenda na kasi ya Rais Magufuli.

“Ninachotaka kuwasisitiza ni kuwa Tufanye kazi ili kwenda na kasi ya Mhe. Rais wetu ambayo ni kuwa na Tanzania ya Viwanda. Tujue kuwa tumepewa jukumu kubwa sana hivyo yatupasa kushirikiana ili kuyafikia malengo ya Mhe. Rais ambayo anategemea katika Wizara yetu tuyafanye.

Nae Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo Dkt. Manege Ludovick amemshukuru Katibu Mkuu Mteule Prof. Shemdoe kwa niaba ya maafisa watendaji wakuu wa waliofika hapo na kumuahidi kumpa ushirikiano “ wewe ni Kiongozi wetu tunakuahidi kukupa ushirikiano ili kufikia malengo ya Wizara na nchi kwa ujumla ya kuwa na Tanzania ya viwanda.

Prof. Shemdoe ameapishwa leo rasmi na Rais Magufuli kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda ya Biashara ambapo kabla ya uteuzi huo alikua Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma.
Share:

RAIS DKT MAGUFULI AWAAPISHA VIONGOZI ALIOWATEUA HIVI KARIBUNI LEO IKULU JIJINI DAR ES SALAAM



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akishuhudia Jaji Kiongozi akimuapisha akimuapisha Bi. Shamira S. Sarwat kuwa Msajili wa Mahakama Kuu katika hafla iliyofanyika Ikulujijini Dar es salaam Februari 3, 2020
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Bi. Zena A. Saidi kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Nishati katika hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam Februari 3, 2020
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Profesa Riziki S. Shemdoe kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara katika  hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam Februari 3, 2020
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Bw. Christopher Kadio kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi katika  hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam Februari 3, 2020
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt. Hassan Abbas kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo katika  hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam Februari 3, 2020

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Bi. Mary G. Makondo kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi katika  hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam Februari 3, 2020
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Bw. Stephen Mashauri kuwa Katibu Tawala wa mkoa wa Ruvuma katika  hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam Februari 3, 2020
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Bw. Leonard R. Masanja kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati katika  hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam Februari 3, 2020
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Bw. Nathaniel M. Nhonge kuwa Kamishna wa Ardhi katika Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi katika  hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam Februari 3, 2020
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Bw. Wilbert M. Chuma kuwa Msajili Mkuu wa Mahakama katika hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam Februari 3, 2020
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Bw. Kelvin Mhina kuwa Msajili wa Mahakama ya Rufani katika hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam Februari 3, 2020
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Bw. Nathaniel M. Nhonge kuwa Kamishna wa Ardhi Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi katika  hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam Februari 3, 2020
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Jaji Dkt. Gerald Ndika kuwa Kamishna wa Tume ya Mahakama ya Utumishi wa Mahakama katika  hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar essalaam Februari 3, 2020
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha  Wakili Genoveva M. Kato kuwa Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Mahakama katika  hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam Februari 3, 2020
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Wakili Julius K. Bundala kuwa Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Mahakama  katika  hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam Februari 3, 2020
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimpandisha cheo Brigedia jenerali Suleiman M. Mzee kuwa Kamishna jenerali wa Magereza katika hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam Februari 3, 2020
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha  Brigedia jenerali Suleiman M. Mzee kuwa Kamishna jenerali wa Magereza katika hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam Februari 3, 2020
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimpandisha cheo  DCP John Masunga kuwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji katika  hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam Februari 3, 2020
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha DCP John Masunga kuwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji katika  hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam Februari 3, 2020.
Share:

Mbowe Amwandikia Barua Rais Magufuli.

Mwenyekiti wa Chadema Taifa Freeman Mbowe amemwandikia barua Rais wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli ili kumuomba alete utengamano wa kitaifa.

Akizungumza Makao Makuu ya Chadema Jijini Dar es Salaam leo,  Mbowe amesema kwa hali ilivyo sasa ikiwemo baadhi ya mataifa kuanza kuitenga Tanzania ni vema kukawa na maridhiano yatakayolifanya taifa hili kuwa lenye umoja na mshikamano.

Akifafanua Mwenyekiti huyo amesema, kuna ulazima Rais akaunda tume ya maridhiano ili kuepusha malalamiko kutoka kwa wananchi

Kuhusu uchaguzi wa Serikali za mitaa, Mbowe ametaka ufutwe na urudiwe.

"Kufutwa kwa uchaguzi huu kutahalalisha kuwa uchaguzi wa mwaka huu (uchaguzi mkuu) utakuwa huru na wa haki. Uchaguzi huu ukafanyike sambamba na uchaguzi wa madiwani, wabunge na Rais.” amesema Mbowe.


Share:

Waziri wa Kilimo: Mazao Yote Ya Kimkakati Yanasimamiwa Na Bodi Za Mazao Sio Ushirika

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameliarifu Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa mazao yote ya kimkakati yanasimamiwa na Bodi za Mazao husika sio vyama vya Ushirika.

Mhe Hasunga ameyasema hayo leo tarehe 3 Februari 2020 wakati akijibu maswali Bungeni ambapo amesisitiza kuwa vyama vya Ushirika vina jukumu la kukusanya mazao na kuyapeleka sokoni kwa ajili ya kuuza kwa niaba ya wanachama sio kusimamia uzalishaji.

Amesema kuwa jambo hilo litaendelea vivyo hivyo na kuwekewa mkakati wa kuimarishwa zaidi ili kuwasaidia wakulima kunufaika na kipato kinachotokana na tija katika uzalishaji wa mazao nchini.

“Tunataka mazao yote, pembejeo zote kuanzia (mbegu, mbolea, viuadudu) hivi vyote vitakuwa vinasambazwa na sekta binafsi katika maeneo yote sio serikali” Alikaririwa Mhe Hasunga

Kadhalika, amewataka wafanyabiashara kuchangamkia fursa hiyo ya kuuza viuatilifu kwani serikali inaendelea kuruhusu sekta binafsi kupeleka viuadudu kwenye mazao mbalimbali kama vile Korosho, Pamba, Kahawa na mazao mengine yote.

Ameongeza kuwa jukumu la serikali itakuwa ni kusimamia na kuratibu maendeleo ya mazao husika na namna ya kutafuta masoko lakini sio kusambaza pembejeo.

Mhe Hasunga amesema kuwa hiyo ni fursa kwa watanzania wote wanaotaka kufanya biashara hiyo kujitokeza kwa wingi.

Waziri Hasunga amesema kuwa baadhi ya viongozi wa vyama vya Ushirika waliingia kwenye biashara ya Tumbaku na kuuza zao hilo bila kufuata utaratibu hivyo kuathiri bei ambayo ingetokana na soko.

Amesema Kutokana na changamoto hiyo Wizara ya kilimo ilikabidhi taarifa ya uchunguzi kwenye uongozi wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ili kuwachukulia hatua viongozi wote waliokiuka maadili ya uongozi na wale ambao hawakusimamia mazao ipasavyo hivyo kusababisha hasara kwa wananchi na vyama vya Ushirika.

Zoezi hilo linaendelea nchi nzima kwani viongozi husika wanakamatwa na kuchukuliwa hatua ikiwemo kurejesha fedha walizopora.

MWISHO


Share:

Askari watatu wafariki dunia na wengine kujeruhiwa baada ya kupata ajali

Askari watatu wa Jeshi la Polisi Mkoani Njombe wamefariki dunia na wengine sita kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha magari matatu ikiwemo gari la polisi ambalo lilikuwa likipeleka askari Lindoni.

RPC Njombe Hamis Issa amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.



Share:

Rwanda na Uganda zakubaliana kubadilishana wafungwa

Serikali za Uganda na Rwanda, Jumapili zilikubaliana kubadilishana wafungwa, katika juhudi za kupunguza uhasama baina yao, baada ya kushutumiana kwa mda mrefu na kufanyiana ujasusi unaotajwa na wachambuzi kama wenye lengo la kutatiza amani ya kila upande.

Rais wa Rwanda Paul Kagame, na mwenzake wa Uganda Yoweri Museveni ambao walikuwa marafiki wakubwa sana kabla ya kutofautiana, walifikia makubaliano hayo katika kikao cha mjini Luanda, Angola.

Viongozi hao hao walisaini mkataba wa ushirikiano katika kurejesha hali ya utulivu baina yao, mwezi Agosti mwaka uliopita, lakini utekelezaji wake umekosa kasi ilivyiotarajiwa.

Japo hakuna taarifa zaidi zimetolewa kuhusu makubaliano ya jumapili, inafahamika kwamba viongozi hao wawili walikubaliana kubadilishana wafungwa katika kikao kitakachofanyika Februari 21, kwenye mpaka uliofungwa kati ya Rwanda na Uganda, mjini Katuna .

Kikao cha Angola kilisimamiwa na rais Joao Lourenco, na kuhudhuriwa na rais wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo Felix Tshisekedi.

Katika taarifa ya kurasa mbili yenye vipengele 8 iliyotolewa na ikulu ya rais wa Angola, viongozi hao waliahidi kushirikiana katika kuimarisha amani, utulivu, ujirani mwema na kuaminiana.

“Pande zote mbili zinatakiwa kujizuia na vitendo vinavyoweza kuleta hali ya kutoaminiana au uhasama, kuhusiana na madai ya kufadhili makundi yenye lengo la kutatiza serikali zake,” kinasema kipengele cha pili, aya ya saba ya taarifa hiyo fupi.

Wiki iliyopita, rais wa Rwanda Paul Kagame alisema kwamba hatashurutishwa kufungua mpaka kati ya Rwanda na Uganda hadi serikali ya rais Yoweri Museveni itakapotimiza matakwa ya serikali ya Rwanda ambayo ni pamoja na kuachilia huru raia wake wote wanaozuiliwa katika magereza ya Uganda.

Rwanda ilifunga mpaka wake mwezi Februari mwaka uliopita na kupiga marufuku biashara kati yake na Uganda.

Hakuna taarifa iliyotolewa iwapo Rwanda ipo tayari kufungua mpaka wa Katuna ili kuruhusu raia wake kuingia Uganda, au Kuruhsu bidhaa za Uganda kuingia Rwanda.

Rwanda inaishutumu Uganda kwa kufadhili makundi ya waasi yenye lengo la kupindua serikali ya rais Paul Kagame. 

-VOA


Share:

MATUSI YAMKERA SAMATTA

Mshambuliaji wa klabu ya Aston villa na timu ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars', Mbwana Samatta ameeleza masikitiko yake kufuatia maoni yasiyoridhisha ya Watanzania katika mitandaao ya kijamii.


Samatta amesema hayo kufuatia Watanzania kutoa maoni yasiyoridhisha yakiwemo matusi katika kurasa za klabu ya Aston Villa na kurasa za wachezaji wa timu hiyo, wakidai kuwa mchezaji wao hapewi nafasi nyingi uwanjani.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Samatta ameandika, "mashabiki wa soka Tanzania nafahamu kuwa mnanipenda kijana wenu na mnapenda nifanye vizuri katika timu yangu mpya, lakini nawaomba muache kutoa maneno ya kashfa au yenye mlengo mbaya katika kurasa za timu au wachezaji, binafsi sifurahishwi".


Share:

SAADAN YATUMIA BILIONI 1.1 KUSAIDIA MIRADI YA KIJAMII

Afisa Utalii wa Hifadhi ya Taifa ya Saadan Athuman Mbae akizungumza na waandishi wa habari 
Afisa Uhifadhi wa Kitengo cha Utalii Hifadhi ya Taifa ya Saadan Prisca Lyimo akielezea mikakati waliokuwa nayo
Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Saadani Martina Ngulei akizungumza kuhusu namna walivyonufaika na uwepo wa hifadhi hiyo
Afisa Utalii wa Hifadhi ya Taifa ya Saadan Athuman Mbae katikati akiwa na wageni kutoka mataifa mbalimbali waliotembelea hifadhi hiyo
Sehemu ya wageni wakifurahia utalii ndani ya hifadhi ya Taifa ya Saadan
Aina ya malazi yanayopatikana kwenye hifadhi ya Taifa ya Saadan kwa wageni wanaofika kutembelea vivutio mbalimbali
Mamba akiwa pembezoni mto Wami akiota jua kama alivyokutwa ambapo jamii ya Mamba wanapatikana pia kwenye hifadhi hiyo
Wanyama aina ya Viboko wakiwa kwenye maji ndani ya Mto Wami ambao umepita kwenye hifadhi hiyo ya Taifa ya Saadan kama wanavyoonekana
 Kundi la Wanyama aina ya Swala wakiwa ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Saadan

 Wanyama aina ya Pundamilia wakiwa ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Saadan
 Aina ya Makundi ya Ndege ambayo yamejenga kiota kwenye hifadhi ya Taifa ya Saadan ndani ya Mto Wami ambapo ndege hao huishi pamoja ambao huishi hapo kwa ajili ya kuijepusha na maadui zao
 Wanyama aina ya Pundamilia wakiwa ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Saadan
 Wanyama aina ya Twiga wakiwa ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Saadan
 Wanyama aina ya Ngiri wakila majani ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Saadan
 Mnyama Ngiri akiwa anakula majani karibu na bahari ya hindi kwenye Hifadhi ya Taifa ya Saadan
 Ndege aina ya Fundi Chuma akiwa ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Saadan
 Mtalii akifurahia upepo wa bahari ndani ya Taifa ya Saadan


Hifadhi ya Taifa ya Saadani imetumia kiasi zaidi ya sh Bil 1.1 kwa ajili ya miradi ya maendeleo kwenye vijiji 11 Kati ya 16 vinavyozunguka hifadhi hiyo kupitia mpango wa ujirani mwema.

Hayo yalisemwa na Afisa utalii wa hifadhi hiyo Athuman Mbae wakati akizungumza na waandishi wa habari walipotembelea hifadhi hiyo hivi karibuni kujionea shughuli za utalii.

Alisema kuwa jumla ya miradi 23 iliyoko kwenye sekta za Afya, Elimu, Maji na Mazingira imeweza kufadhiliwa na hifadhi hiyo kwa kushirikiana na wananchi.

"Tumekuwa tukishiriki katika miradi ya ujirani mwema ambapo hifadhi inachangia asilimia 90% huku wananchi wakichangia asilimia 10% kwa lengo la kuhakikisha wanaweza kuituza miradi hiyo"alisema Mbae.

Awali akizungumza Afisa Uhifadhi wa Kitengo cha Utalii Hifadhi ya Taifa ya Saadan Prisca Lyimo alisema kwamba alisema maboresho yaliyofanywa kwenye hifadhi hiyo na serikali ya awamu ya tano yamesaidia kuongeza idadi ya watalii wan je na ndani.

Alisema maboresho hayo yameongeza mwitikio wa watanzania kutembelea hifadhi za taifa kutokana na kuboresha miundombinu ufikaje wake huku watalii wanaweza kufika wakiwemo wa Zanznzar, Dar na Tanga na maeneo mengine hapa nchini.

“Bado tunaendelea kuhamasisha watanzania waone umuhimu wa kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo hapa nchini hususani hifadhi ya Kipekee ya Saadani inayopakana na Bahari ya Hindi”Alisema
 
Kwa upande wake Mtendaji wa Kijiji cha Saadani Martina Ngulei alisema kuwa hifadhi hiyo imeweza kusaidiana na wananchi katika kutatua kero mbalimbali ambazo zilikuwa zinatukabili.

"Hifadhi imeweza kutujengea nyumba ya Mwalimu,kusambaza maji kwenye nyumba za ibada sambamba na ujenzi wa choo chashule ambacho kilikuwa hakitumiki kwa muda mrefu kutokana na uchakavu"alisema Ngulei.

Nao baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Saadani wamesema kuwa kuishi kwa jirani na hifadhi kumekuwa ni neema kubwa kwao kwa kipato sambamba na fursa za biashara.

"Watalii wengine wakija wanaishi nje ya hifadhi hivyo tunapata kipato kwa kuwauzia chakula ikiwemo na malazi sambamba na kujifunza tamaduni za kwetu "alisemaAthuman Said.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger