Monday, 3 February 2020

SAADAN YATUMIA BILIONI 1.1 KUSAIDIA MIRADI YA KIJAMII

Afisa Utalii wa Hifadhi ya Taifa ya Saadan Athuman Mbae akizungumza na waandishi wa habari 
Afisa Uhifadhi wa Kitengo cha Utalii Hifadhi ya Taifa ya Saadan Prisca Lyimo akielezea mikakati waliokuwa nayo
Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Saadani Martina Ngulei akizungumza kuhusu namna walivyonufaika na uwepo wa hifadhi hiyo
Afisa Utalii wa Hifadhi ya Taifa ya Saadan Athuman Mbae katikati akiwa na wageni kutoka mataifa mbalimbali waliotembelea hifadhi hiyo
Sehemu ya wageni wakifurahia utalii ndani ya hifadhi ya Taifa ya Saadan
Aina ya malazi yanayopatikana kwenye hifadhi ya Taifa ya Saadan kwa wageni wanaofika kutembelea vivutio mbalimbali
Mamba akiwa pembezoni mto Wami akiota jua kama alivyokutwa ambapo jamii ya Mamba wanapatikana pia kwenye hifadhi hiyo
Wanyama aina ya Viboko wakiwa kwenye maji ndani ya Mto Wami ambao umepita kwenye hifadhi hiyo ya Taifa ya Saadan kama wanavyoonekana
 Kundi la Wanyama aina ya Swala wakiwa ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Saadan

 Wanyama aina ya Pundamilia wakiwa ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Saadan
 Aina ya Makundi ya Ndege ambayo yamejenga kiota kwenye hifadhi ya Taifa ya Saadan ndani ya Mto Wami ambapo ndege hao huishi pamoja ambao huishi hapo kwa ajili ya kuijepusha na maadui zao
 Wanyama aina ya Pundamilia wakiwa ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Saadan
 Wanyama aina ya Twiga wakiwa ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Saadan
 Wanyama aina ya Ngiri wakila majani ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Saadan
 Mnyama Ngiri akiwa anakula majani karibu na bahari ya hindi kwenye Hifadhi ya Taifa ya Saadan
 Ndege aina ya Fundi Chuma akiwa ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Saadan
 Mtalii akifurahia upepo wa bahari ndani ya Taifa ya Saadan


Hifadhi ya Taifa ya Saadani imetumia kiasi zaidi ya sh Bil 1.1 kwa ajili ya miradi ya maendeleo kwenye vijiji 11 Kati ya 16 vinavyozunguka hifadhi hiyo kupitia mpango wa ujirani mwema.

Hayo yalisemwa na Afisa utalii wa hifadhi hiyo Athuman Mbae wakati akizungumza na waandishi wa habari walipotembelea hifadhi hiyo hivi karibuni kujionea shughuli za utalii.

Alisema kuwa jumla ya miradi 23 iliyoko kwenye sekta za Afya, Elimu, Maji na Mazingira imeweza kufadhiliwa na hifadhi hiyo kwa kushirikiana na wananchi.

"Tumekuwa tukishiriki katika miradi ya ujirani mwema ambapo hifadhi inachangia asilimia 90% huku wananchi wakichangia asilimia 10% kwa lengo la kuhakikisha wanaweza kuituza miradi hiyo"alisema Mbae.

Awali akizungumza Afisa Uhifadhi wa Kitengo cha Utalii Hifadhi ya Taifa ya Saadan Prisca Lyimo alisema kwamba alisema maboresho yaliyofanywa kwenye hifadhi hiyo na serikali ya awamu ya tano yamesaidia kuongeza idadi ya watalii wan je na ndani.

Alisema maboresho hayo yameongeza mwitikio wa watanzania kutembelea hifadhi za taifa kutokana na kuboresha miundombinu ufikaje wake huku watalii wanaweza kufika wakiwemo wa Zanznzar, Dar na Tanga na maeneo mengine hapa nchini.

“Bado tunaendelea kuhamasisha watanzania waone umuhimu wa kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo hapa nchini hususani hifadhi ya Kipekee ya Saadani inayopakana na Bahari ya Hindi”Alisema
 
Kwa upande wake Mtendaji wa Kijiji cha Saadani Martina Ngulei alisema kuwa hifadhi hiyo imeweza kusaidiana na wananchi katika kutatua kero mbalimbali ambazo zilikuwa zinatukabili.

"Hifadhi imeweza kutujengea nyumba ya Mwalimu,kusambaza maji kwenye nyumba za ibada sambamba na ujenzi wa choo chashule ambacho kilikuwa hakitumiki kwa muda mrefu kutokana na uchakavu"alisema Ngulei.

Nao baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Saadani wamesema kuwa kuishi kwa jirani na hifadhi kumekuwa ni neema kubwa kwao kwa kipato sambamba na fursa za biashara.

"Watalii wengine wakija wanaishi nje ya hifadhi hivyo tunapata kipato kwa kuwauzia chakula ikiwemo na malazi sambamba na kujifunza tamaduni za kwetu "alisemaAthuman Said.
Share:

Serikali Yachukua Hatua Za Makusudi Kuhakikisha Mbolea Zinapatikana Za Kutosha-MGUMBA

Na Mathias Canal, Wizara ya kilimo-Dodoma
Kutokana na kuwepo kwa upungufu wa pembejeo nchini, Serikali imechukua hatua mbalimbali za kuhakikisha pembejeo zinapatikana kwa wingi ili kutosheleza mahitaji ya ndani ya nchi.

Hatua hizo ni pamoja na; kutoa vibali kwa wasambazaji wakubwa wa mbolea kuagiza nje ya mfumo wa BPS kutokana na mahitaji ya wakulima na soko ambapo tani 200,000 zimeagizwa na hadi kufikia tarehe 30 Januari, 2020; Kutoa kibali cha kuagiza tani 45,000 kwa Umoja wa wasambazaji na wauzaji wa pembejeo za kilimo; na kuagiza mbolea tani 43,000 kwa kutumia mfumo wa BPS ambapo mbolea hiyo imeanza kusambaza nchini tangu tarehe 28 Januari, 2020.

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba (Mb) ameyasema hayo tarehe 3 Januari 2020 bungeni Jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Kavuu Mhe Dkt. Pudeciana Wilfred Kikwembe aliyetaka kufahamu serikali ina mpango gani juu ya ucheleweshwaji wa pembejeo za kilimo hasa mbegu na mbolea ambazo huwasababishia wakulima hasara.

Mhe Mgumba amesema kuwa Serikali kwa kushirikiana na wadau inaendelea kuboresha mifumo ya uzalishaji, udhibiti na usambazaji wa pembejeo nchini ambapo sekta ya Umma na binafsi zitashirikishwa na kuhamasishwa kuzalisha pembejeo nchini ili kukidhi mahitaji.

Kuhusu upungufu wa mbolea nchini Mhe Mgumba amesema kuwa umechangiwa na sababu mbalimbali ikiwemo kuchelewa kupatikana kwa mahitaji kutoka kwa Makampuni ya mbolea hapa nchini, kuongezeka kwa matumizi ya mbolea kutokana na bei nzuri ya mazao kwa msimu wa 2018/2019; kuongezeka kwa kilimo cha kibiashara baada ya Serikali kuwahakikishia wakulima kuwa haitafunga mipaka na kuingilia upangaji wa bei za mazao ya kilimo na kuwepo kwa mvua nyingi ambazo zimesababisha kuongezeka kwa viwango vya matumizi ya mbolea kwa wakulima.

Katika msimu wa 2019/2020 upatikanaji wa pembejeo zikiwemo mbegu bora hadi kufikia Desemba, 2019 ni tani 71,155.13. Kati ya hizo, tani 58,509.9 zimezalishwa nchini, tani 5,175.79 zimeingizwa kutoka nje ya nchi na tani 7,469.44 ni bakaa ya msimu 2018/2019.

Aidha, upatikanaji wa mbolea hadi kufikia tarehe 30 Januari, 2020 ni tani 410,499 zikijumuisha tani 92,328 za UREA na tani 84,311 za DAP. Kati ya hizo tani 225,417 zimeingizwa kutoka nje ya nchi, tani 16,685 zimezalishwa ndani ya nchi na tani 168,397 ni bakaa ya msimu wa 2018/2019.


Share:

Serikali Kuendelea Kufuatilia Dawa Za Kuulia Wadudu Wanaoharibu Pamba-BASHE

Na Mathias Canal, Wizara ya kilimo-Dodoma
Serikali imewahakikishia wakulima wa Pamba nchini kuwa itaendelea kufuatilia upatikanaji wa viuadudu vya zao la pamba na kuhakikisha vinawafikia wakulima kwa wakati.

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Hussein Bashe ameyasema hayo tarehe 3 Februari 2020 wakati akijibu swali la swali la Mbunge wa Jimbo la Geita Vijijini Mhe Joseph Kasheku Msukuma aliyetaka kufahamu serikali inampango gani kupeleka dawa za kuuwa wadudu wa Pamba kwani zinazopatikana huwa ni chache.

Bashe amesema kuwa kama sehemu ya utekelezaji wa hamasa za kilimo cha Pamba, katika msimu wa kilimo wa mwaka 2017/2018 eneo la ekari 1,488,406 lililimwa na kuzalisha kiasi cha tani 132,961. Chupa milioni 4.6 za viuadudu zenye thamani ya shilingi bilioni 16.8 na vinyunyizi 15,300 vyenye thamni ya shillingi milioni 462 vilinunuliwa na kusambazwa mwaka huo.

Aidha, katika msimu wa 2018/2019 eneo la ekari 1,865,000 lililimwa na kuzalisha kiasi cha tani 222,725 ambapo chupa  milioni 6 za viuadudu vyenye thamani ya shilingi bilioni 29 na vinyunyizi 23,000 vyenye thamani ya shilling bilioni  1.8 vilinunuliwa.

Vilevile, katika msimu wa 2019/2020 eneo la ekari 1,786,890 lililimwa na kuzalisha kiasi cha tani 350,473 ambapo chupa milioni 8.2 zenye thamani ya shilingi bilioni 41 na vinyunyizi 20,000 vyenye thamani ya shillingi bilioni 1.6 vilinunuliwa.

Mhe Bashe amesema kuwa katika msimu wa 2017/2018 jumla ya ekapaki 965,300 na vinyunyizi 3,302 vilisambazwa katika Mkoa wa Geita. Aidha, jumla ya ekapaki 736,345 na vinyunyizi 3,020 vilisambazwa katika mkoa huo katika msimu wa 2018/2019. Kwa msimu wa 2019/2020 Mkoa wa Geita umekwisha kusambaziwa kiasi cha ekapaki 8,748 na usambazaji bado unaendelea.

Bashe amesema, si sahihi kusema kuwa Serikali inahamasisha kilimo cha pamba  ikiwa haina uwezo wa kupeleka sumu za kuulia wadudu na hata  zinapopatikana huwa ni chache. Serikali inaendelea kuhamasisha kilimo cha mazao likiwemo zao la pamba ili kuongeza tija na uzalishaji wa mazao kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.

Akizungumzia uchache wa viuadudu vya zao la pamba Mhe Bashe amesema kuwa umechangiwa na baadhi ya wakulima kutumia viuadudu katika kupulizia mazao mengine kama vile mahindi na viazi vitamu ili kudhibiti viwavijeshi vamizi.

Vilevile, amesema kuwa kukosekana kwa uaminifu kwa baadhi ya viongozi wa vijiji katika baadhi ya maeneo ukiwemo Mkoa wa Geita ambapo viuadudu havikupelekwa kwa wakulima na badala yake kuuzwa katika maduka ya pembejeo kinyume na taratibu za usambazaji wa viuadudu vya zao la pamba.

Ameongeza kuwa Watu zaidi ya 12 walikamatwa na kati yao 9 walifunguliwa mashtaka ambapo watu nane (8) walihukumiwa kifungo cha miezi sita jela kila mmoja.


Share:

EBENEZER TV YAMWAGA NAFASI ZA AJIRA...SOMA HAPA UOMBE MARA MOJA


Ebenezer Television ni kituo kipya cha habari ambacho kinatarajia kuanza kurusha matangazo yake kutokea Mikocheni Dar es Salaam. Kituo kinahitaji wafanyakazi katika Nyanja zifauatazo;

A.    NAFASI ZA AJIRA

1.     Mhariri Mkuu – Nafasi moja (1)
-        Awe na Shahada ya Uandishi wa Habari au Mawasiliano ya umma
-        Awe na uzoefu usiopungua miaka mitatu katika nafasi hiyo
-        Awe amelelewa katika maadili ya kikristo.
-        Awe na uwezo wa kusimamia uzalishaji wa vipindi
-        Awe amehitimu katika vyuo vikuu vinavyotambulika na serikali.

2.     Wazalishaji vipindi – Nafasi tatu (3)
-        Awe ana kiwango cha chini cha Stashahada kutoka Chuo kinachotambulika.
-        Awe na uzoefu usiopungua miaka miwili katika nafasi hiyo

3.     Waandishi wa Habari – Nafasi tatu (3)
-        Awe ana kiwango cha chini cha Stashahada kutoka Chuo kinachotambulika.
-        Awe na uzoefu usiopungua miaka miwili katika nafasi hiyo

4.     Wahariri wa picha nyongefu na wasanifu – Nafasi mbili (2)
-        Awe na Stashahada kwenye uandishi wa habari, uhariri picha au ubunifu wa matangazo.
-        Awe na uzoefu usiopungua miaka miwili.

5.     Wapiga picha nyongefu – Nafasi nne (3)
-        Wawe na elimu kuanzia Astashahada katika upigaji picha nyongefu
-        Awe na ujuzi wa sauti za picha nyongefu
-        Awe na uzoefu usiopungua miaka miwili.

6.     Warusha Matangazo – Nafasi tatu (3)
-        Awe na Stashahada katika teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT)
-        Au Stashahada katika teknolojia ya mawasilianao na elektroniki
-        Awe na uwezo wa kutatua matatizo ya kiufundi
-        Awe na uwezo wa kushauri vifaa bora kutokana na teknolojia

7.     Wasoma Habari – Nafasi tatu (3)
-        Awe na elimu isiyo chini ya Astashahada ya Uandishi wa Habari au sifa inayofanana na hiyo.
-        Awe na uzoefu usiopungua miaka miwili katika fani husika

8.     Mkutubi – Nafasi moja (1)
-        Awe na elimu isiyo chini ya Astashahada ya utunzaji kumbu kumbu
-        Awe ana ujuzi wa kutunza vielelezo vya sauti na picha nyongefu
-        Uzoefu wa zaidi ya mwaka mmoja.

9.     Msimamizi wa vipindi – Nafasi moja (1)
-        Awe na elimu isiyopungua astashahada ya uandaaji na usimamizi wa vipindi
-        Awe anajua kupanga ratiba za vipindi katika kituo cha runinga.
-        Awe anajua kupanga utaratibu wa matukio ya kitaifa au kikanisa yatakayotokea.
-        Awe anajua kupanga na kuratibu matangazo ya biashara katikati ya vipindi pale endapo tangazo litakuja.

10. Mratibu wa maudhui mtandaoni – Nafasi moja (1)
-        Awe na elimu isiyopungua Astashahada
-        Awe na uzoefu wa mitandao ya kijamii
-        Mwenye ujuzi wa mifumo ya kielectronika na komputa

11. Msimamizi wa Utawala – Nafasi moja (1)
-        Awe na elimu ya shahada ya awali katika Uongozi yaani (Public Administration, Leadership and Governance.
-        Mwenye ujuzi wa habari na Mawasiliano atapewa kipaumbele
-        Awe amelelewa katika maadili ya dini ya KIKRISTO
-        Awe tayari kufanya kazi nyingine zinazoendana na nafasi hyo
-        Awe na uwezo wa kufanya tathmini ya wafanyakazi waliopo na kushauri Uongozi njia bora ya kuboresha.
-        Uzoefu wa miaka miwili katika nafasi kama hyo

12. Mhasibu – Nafasi moja (1)
-        Awe na elimu ya shahada ya awali katika masuala ya fedha
-        Awe amelelewa katika maadili ya kikristo
-        Awe na uelewa katika masoko na biashara
-        Awe na uzoefu wa miaka miwili
-        Awe amelelewa katika maadili ya KIKRISTO

13. Fundi sanifu wa umeme – Nafasi moja (1)
-        Awe na stashahada ya umeme katika chuo kinachotambulika
-        Awe na uzoefu wa vifaa vya electronics na sauti
-        Awe anaufahamu umeme wa phase moja na phase tatu
-        Awe na uwezo wa kufuatilia tatizo la umeme na kulitatua
-        Awe na ujuzi wa kuunganisha na kuwasha generator.



B.    NAFASI  ZA WAKURUFUNZI (INTERNS)
1.     Waandishi wa Habari – Nafasi tatu (3)
2.     Mhariri wa picha – Nafasi mbili (2)
3.     Msaidizi wa msimamizi wa vipindi – Nafasi mbili (1)
4.     Mrusha Matangazo – Nafasi mbili (2)
5.     Wapiga picha – Nafasi mbili (2)
6.     Wakutubi – Nafasi mbili (1)
7.     Waandaaji vipindi – Nafasi mbili (2)

-        Wawe na ujuzi katika fani husika uzoefu si lazima AU awe mwanafunzi anayetarajia kumaliza masomo katika fani husika

C.    Watendaji wa kujitolea (Volunteers)
1.     Wapiga picha – Nafasi 1
2.     Wahariri picha – Nafasi 3
3.     Waandaaji vipindi – Nafasi 4
4.     Afisa Masoko – Nafasi 3


Maombi yote yaliyo ambatanishwa na nakala za vyeti na CV yatumwe kwa;
Mratibu wa Mradi - Ebenezer Television
S.L.P 4067
Shule Kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma
Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam.
Dar es Salaam.

AU


Kwa barua pepe ebztvtz@gmail.com katika mfumo wa PDF na viambatanisho vyote viwe katika nakala moja. Mwisho wa kutuma maombi ni February 12, 2020.
Share:

DKT. ABBAS KUENDELEA KUWA MSEMAJI WA SERIKALI


Rais  Magufuli ametaja sababu ya kumteua Dk Hassan Abbasi kuwa katibu mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo akisema ni kutokana na kufanya kazi nzuri ya kuisemea Serikali bila kuchoka. Kabla ya uteuzi huo, Dk Abbasi alikuwa msemaji mkuu wa Serikali.

“Dk Abbas amefanya kazi nzuri kama msemaji wa Serikali, hakuchoka aliisemea vizuri Serikali, ningependa aendelee tu kuwa msemaji wa Serikali lakini mahali mtu anapotakiwa kupata promosheni, usimnyime promosheni.

“Ndiyo maana tumemteua awe katibu mkuu wa wizara hiyo na kwa sasa hivi ataendelea kuwa msemaji wa Serikali mpaka tutakapopata mwingine na atakuwa anasema sasa akiwa mkubwa zaidi,” amesema Magufuli.


Share:

Shambulio la nzige Afrika, Somalia yatangaza janga la taifa

Somalia imekuwa nchi ya kwanza ya Pembe ya Afrika kutangaza kuwa, wimbi la nzige waliovamia nchi hiyo ni janga na kwamba kupambana na janga hilo ni jambo la dharura kitaifa.

Wizara ya Kilimo ya Somalia ilisema jana (Jumapili) kwamba wimbi kubwa la nzige waliovamia maeneo ya jangwani ni hatari kubwa kwa nchi hiyo ambayo tayari ina mazingira mabaya ya usalama wa chakula.

Taarifa ya wizara hiyo imeongeza kuwa, chakula cha wanadamu na mifugo yao kiko hatarini Somalia. Wimbi la nzige walioivamia nchi hiyo ni kubwa na wanaangamiza kiwango kikubwa cha mazao, mimea na majani.

Wizara hiyo imesema, tahadhari ya taifa iliyotangazwa na wizara hiyo inalenga kuhamasisha juhudi zaidi za kupambana na janga hilo na kuomba mataifa kuisaidia Somalia kwani kuvamiwa na nzige wakati huu wa kabla ya mwezi Aprili ambacho ni kipindi cha mavuno ni jambo hatari sana.

Nzige ni jamii ya panzi na wanapovamia shamba huangamiza kila kitu na kusababisha kutokea janga la njaa.

Waziri wa Kilimo wa Somalia, Said Hussein Iid amesema kuwa, kama hatua hazitachukuliwa hivi sasa, basi nchi hiyo itakumbwa na upungufu mkubwa wa chakula ambao itashindwa kukabiliana nao. Amesema, wametoa tahadhari hiyo kama njia ya kulinda usalama wa chakula kwa wananchi wa Somalia.


Share:

LIVE: Rais Magufuli Akiwaapisha Viongozi Mbalimbali Aliowateua IKULU Dar

LIVE:  Rais Magufuli Akiwaapisha Viongozi Mbalimbali Aliowateua IKULU Dar


Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano February 3

















Share:

Sunday, 2 February 2020

WASH Officer at UN High Commissioner for Refugees

Deadline Date: Thursday, 13 February 2020 Organization: UN High Commissioner for Refugees Country: United Republic of Tanzania City: Kibondo Organizational Setting and Work Relationships The WASH Officer will be responsible for provision of professional technical support and guidance on activities within the areas of Water, Sanitation & Hygiene (WASH) in the locations within the Areas of Responsibility (AoR).… Read More »

The post WASH Officer at UN High Commissioner for Refugees appeared first on Udahiliportal.com.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger