Sunday, 2 February 2020

WASH Officer at UN High Commissioner for Refugees

Deadline Date: Thursday, 13 February 2020 Organization: UN High Commissioner for Refugees Country: United Republic of Tanzania City: Kibondo Organizational Setting and Work Relationships The WASH Officer will be responsible for provision of professional technical support and guidance on activities within the areas of Water, Sanitation & Hygiene (WASH) in the locations within the Areas of Responsibility (AoR).… Read More »

The post WASH Officer at UN High Commissioner for Refugees appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

ESTATE OFFICER II Job Vacancy at The Ngorongoro Conservation Area (NCA)

ESTATE OFFICER II Job Vacancy at The Ngorongoro Conservation Area (NCA) NGORONGORO CONSERVATION AREA AUTHORITY JOB ADVERTISEMENT The Ngorongoro Conservation Area (NCA) was established under National Parks Ordinance CAP. 412 of 1959. This unique area is currently managed by the Ngorongoro Conservation Area Authority (NCAA) pursuant to CAP 284 of 2002. It is under the Ministry of Natural… Read More »

The post ESTATE OFFICER II Job Vacancy at The Ngorongoro Conservation Area (NCA) appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

IT Adviser – Remote Job Vacancy at VSO Mtwara Tanzania

IT Adviser – Remote Job Vacancy at VSO Mtwara Tanzania   Role Overview To support implementation of project in Lindi and Mtwara by providing support on information gathering and key stakeholder engagement for the review of VSO-VETA’s online job platform “Kazi Connect”. Skills, Qualifications And Experience Competencies and Behaviour Whether You Want To Join Us As An Employee,… Read More »

The post IT Adviser – Remote Job Vacancy at VSO Mtwara Tanzania appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

MIILI 16 YA WAUMINI WALIOFARIKI WAKIKANYAGA MAFUTA YA UPAKO YATAMBULIWA...KUAGWA KESHO UWANJA WA MAJENGO

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira, amesema miili ya watu 20 waliofariki kwenye kongamano la Mtume na Nabii Mwamposa, itaagwa kesho Februari 3, 2020, kwenye viwanja vya Majengo mjini Moshi.  Amesema hadi sasa tayari miili 16 imeshatambuliwa.



Kwa upande wake Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini ,IGP Simon Sirro amewataka Watanzania kuwa  makini kwani kinyume na hapo itakuwa shida sana na kuongeza iko haja kamati za ulinzi na usalama za wilaya na mkoa kuanza kuyafuatilia makanisa yote nchini na hasa makanisa madogo madogo ambayo sasa yamekuwepo kila mahali.

"Sio kila padri, mchungaji basi anataka kuwachunga kondoo wake waende kuuona ufalme wa Mungu, wengine wanahangaika na utafutaji tu wa maisha.Sio kwamba nahukumu lakini kuna mambo ya kujifunza,"amesema

Kuhusu Polisi iwapo walikuwepo kwenye kongamano hilo la Mwamposa, IGP Sirro amesema ameshatoa maagizo kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimajaro kufuatilia na iwapo walikuwepo polisi lazima waulizwe imekuaje hadi watu wakapoteza maisha na wao wakiwepo, kwani sheria lazima ichukue mkondo wake. 


Share:

Picha : MUONEKANO WA UWANJA WA MAJENGO, MOSHI BAADA YA IBADA YA MTUME MWAMPOSA KUKANYAGA MAFUTA YA UPAKO


Uwanja wa majengo, Moshi unavyoonekana baada ya ibada ya jana iliyoongozwa na Mtume Boniface Mwamposa kugeuka vilio baada ya watu 20 kufariki dunia walipo kanyagana wakipita kwenye ‘mafuta ya upako’. 






Share:

MTUME BONIFACE MWAMPOSA ATIWA MBARONI


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene amesema wamemkamata Mtume Boniface Mwamposa Jijini Dar es salaam alipokuwa amekimbilia baada ya kutoroka mkoani Kilimanjaro kutokana na tukio waumini wake kugombea kukanyaga mafuta ya upako na kusababisha vifo vya watu 20.




Simbachawene ametoa pole kwa Familia ya Watu 20 waliopoteza maisha wakati wakitoka katika ibada hiyo  Mjini Moshi.

Amesema Wizara itaweka Kanuni na Taratibu kali za Usajili wa Taasisi zinazotoa Huduma za Maombezi(Ministries) ambazo baadhi zinavunja Sheria.


Share:

MTUME MWAMPOSA AAGA WAUMINI WAKE KUTII WITO WA JESHI LA POLISI MOSHI

 Kiongozi wa kanisa la Inuka Uangaze, Nabii na mtume Boniface Mwamposa amelazimika kusitisha ibada kwa ajili ya kuitikia wito wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Tanzania kulikotokea vifo vya waamini wake.

Mwamposa ambaye huendesha ibada zake katika eneo la Tanganyika Packers, leo Jumapili Februari 2, 2020, amelazimika kufupisha ibada ya kwanza na kuanza safari ya kuelekea Moshi alikoitwa na polisi.

Kawaida ibada hiyo huisha kati ya saa saba hadi saa nane mchana, lakini leo imeisha saa 4:30.

Mwamposa akiwa ameambatana na wasaidizi wake, aliondoka katika eneo hilo la Kanisa 4:30 leo asubuhi.
Share:

CCM KAHAMA WAADHIMISHA MIAKA 43 KUANZISHWA KWAKE KWA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO


Na Salvatory Ntandu - Malunde 1 blog 
Katika kuelekea katika maadhimisho ya miaka 43 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM ) kamati ya siasa ya CCM wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga imeanza kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo iliyotekelezwa na serikali ya awamu ya Tano katika halmashauri za Ushetu,Msalala na Mji wa Kahama.


Akizungumzia ziara hiyo ya kutembelea miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Ushetu, jana Febuari Mosi,2020 Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM wilaya ya Kahama Thomasi Myonga amesema ziara hiyo imelenga kukagua miradi iliyoainishwa na kutekelezwa na serikali ya awamu ya tano ambayo ipo katika ilani ya CCM.

"Leo Febuari mosi tumeanza kukagua miradi mbalimbali katika Halmashauri ya Ushetu ikiwemo ujenzi wa Hospitali ya wilaya,ujenzi wa Makao makuu ya halmashauri,madarasa,visima na mabweni katika shule mbalimbali.

“Tumeamua kuadhimisha miaka 43 ya chama chetu kwa kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM katika miradi mbalimbali ya maendeleo ili kubaini namna ilivyotekelezwa na kama kunakasoro tuweze kuziainisha kwaajili ya kupatiwa ufumbuzi wa haraka”,alisema Myonga.

Kwa upande wake Katibu wa Chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Kahama Emanuel Mbamange alisema watatembelea halmashauri zote mbili ili kukagua miradi yote ambayo imetekelezwa na serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dk John Pombe Magufuli ambayo imedhamiria kutatua kero za wananchi wanyonge.

Alifafanua kuwa maadhimisho ya miaka 43 ya CCM yamebeba kauli mbiu isemayo tumeahidi,tumetekeleza na tunaahidi tena kuchapa kazi kwa juhudi,ubunifu na maarifa zaidi ambapo yanaenda sambamba na kutekeleza shughuli mbalimbali za kimaendeleo zenye lengo la kusongeza huduma karibu kwa wananchi.

Awali akiikaribisha kamati ya siasa ya wilaya ya Kahama katika makao makuu ua Halmashauri hiyo nyamilangano, mwenyekiti wa Halmashauri ya ushetu Juma Ally Kimisha alisema kuwa halmashauri hiyo imetekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kwa asilimia 100 ambayo fedha zake zimeshatolewa na serikali kwa lengo la kuwasidia wananchi kupata huduma za kijamii,kwa mfano ujenzi wa zahanati vituo vya afya na miundombinu ya madarasa na barabara.

Share:

IDADI YA VIFO KUTOKANA NA VIRUSI VYA CORONA YAFIKA 304 CHINA


Idadi ya vifo kutokana na janga la virusi vya corona nchini China imefikia watu 304 kufikia jana usiku, baada ya watu 45 kufariki dunia katika siku iliyotangulia. 

Tume ya Afya nchini humo imesema vifo hivi vipya vilitokea katika mkoa wa Hubei, ambao ndio kitovu cha mlipuko wa virusi hivyo. 

Kote nchini China, kulikuwa na maambukizi mapya ya watu 2,590 jana Jumamosi na kufikisha 14,380 jumla ya idadi ya watu walioambukizwa mpaka sasa. 

China inaendelea kutengwa wakati hatua za kudhibiti usafiri duniani zikiendelea kuchukuliwa na kufutwa safari za ndege. 

Janga hilo limesababisha mataifa mengi kuwahamisha raia wao huku mashirika ya ndege yakisitisha safari kwenda nchini humo. 

Hatua hiyo pia inatishia kuathiri kwa kiasi kikubwa kushuka uchumi wa taifa hilo la pili kwa ukubwa kiuchumi duniani. 

Kumeripotiwa zaidi ya visa 130 vya maambukizi ya virusi vya corona katika karibu nchi nyingine 24 duniani.


Share:

Rais Magufuli kuapisha viongozi wa Wizara, Mahakama, Majeshi na Mikoa kesho Jumatatu tarehe 03 Februari, 2020 saa 3:15 asubuhi, Ikulu




Share:

Rais Magufuli Atuma Salamu Za Rambirambi Vifo Vya Watu 20 Waliofariki kwa Kukanyagana kisa mafuta ya Upako Moshi




Share:

MPINA ATOA SIKU 7 VIGOGO SERIKALINI KUKUTANA KUMALIZA DHULUMA KWA WAFUGAJI

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina akikagua mifugo 600 iliyolundikana kwenye zizi dogo lenye uwezo wa kuhifadhi ng'ombe 60 alipokwenda kukagua mifugo hiyo iliyokamatwa na Halmashauri ya Tanganyika Mkoa wa Katavi na kuwatoza faini ya shilingi milioni 60. Nyuma ni Daktari Mkuu wa Mifugo Tanzania, Profesa Hezron Nonga. Picha na Mpiga Wetu
 
NA MWANDISHI WETU, KATAVI

WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina ametoa siku saba kwa Daktari Mkuu wa Mifugo Tanzania (CVO), Kamishna wa Uhifadhi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) na Wakili Mkuu wa Serikali wakutane kutathmini na kuondoa dhuluma zinazoendelea kwa wafugaji pamoja na kuandaa kanuni na miongozo itakayoweka uwazi katika usimamizi wa Sheria za Misitu na Mifugo.

Mpina ametoa agizo hilo mwishoni mwa wiki baada ya Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi kutoza faini ya shilingi milioni 60 sawa na shilingi laki moja kwa kila ng’ombe baada ya ng’ombe 600 kukamatwa wakichungwa ndani ya  Msitu wa Tongwe Mashariki unaomilikiwa na halmashauri hiyo.

Waziri Mpina amefikia hatua hiyo baada ya kuwepo ukiukwaji mkubwa wa sheria na ukamataji holela wa mifugo unaofanywa kwenye baadhi ya Halmashauri, Hifadhi za Wanyama, Mapori ya Akiba ambapo mifugo inapokamatwa hunyimwa huduma muhimu ikiwemo malisho, maji, chanjo na dawa hali inayosababisha mifugo mingi kudhoofika na kufa.

Alibainisha manyanyaso mengine ni wafugaji kutozwa faini kubwa ambazo hazipo kwa mujibu wa sheria, kupigwa, mifugo kuibiwa, kupigwa risasi na mingine kuuzwa kwa njia ya  mnada kwa kisingizio cha kukosekana mmiliki wa mifugo hiyo huku idadi  inayotajwa mahakamani ni ndogo ikilinganishwa na mifugo iliyokamatwa.

Akizungumza mara baada ya kufika eneo ilikoshikiliwa mifugo hiyo umbali wa zaidi ya kilomita 50  kutoka barabara ya Mpanda- Kigoma, Waziri Mpina alihoji iweje Halmashauri hiyo iache kufuata sheria za nchi zinavyoelekeza kwa watu wanaoingiza mifugo na badala yake wakabuni faini ya kutoka kichwani kinyume cha Sheria na kuitafsiri hatua hiyo kuwa ni Unonevu, Rushwa, Wizi, Dhuluma na Manyanyaso kwa wafugaji.

Waziri Mpina alisema yeye kama msimamizi mkuu wa Sekta ya Mifugo nchini hawezi kumtetea mfugaji anayevunja sheria kwa kuingiza mifugo kwenye maeneo yaliyokatazwa kisheria lakini kilichomfanya kuingilia kati suala hilo ni kuvunjwa kwa Sheria ya Misitu Namba 14 ya mwaka 2002 inayoeleza bayana kwamba mtu atakayekutwa ametenda kosa ndani ya msitu atatozwa faini ya shilingi 30,000 na isiyozidi milioni moja.

“Kutoza hela ambayo haiko kwenye Sheria ni Wizi, ni Manyanyaso kwa wafugaji, Rushwa huwezi kutoza hela ya Serikali ambayo haiko kwenye kanuni yaani Serikali iache kusimamia sheria ifanyie kazi maamuzi ya vikao” alihoji Waziri Mpina.

Mmoja wa wachungaji hao Koye Mmela alilamikia kitendo cha kukamatwa na kushikiliwa msituni kwa siku sita mfululizo bila kufikishwa Mahakamani jambo walilolitaja ni uonevu mkubwa waliofanyiwa na askari waliokuwa doria.

Mwanasheria wa Halmashauri ya Tanganyika, Maraka Mrisho  alimweza Waziri Mpina kuwa faini hiyo ya milioni 60 haipo kwenye sheria yoyote bali ilitozwa kufuatia makubaliano ya kikao kilichowahusisha Maofisa wa Misitu wa halmashauri pamoja na Maofisa wa Wakala wa Huduma za Misitu (TFS) wa kanda hiyo na kubariki faini ya shilingi laki moja kwa kila ng’ombe.

Mrisho alisema kwa mujibu wa Sheria ya Misitu Namba Sheria ya Misitu Namba 14 ya Mwaka 2002, kifungu cha 84 Kifungu kidogo cha tano kinasema mtu yeyote atakayekutwa na kosa ndani ya misitu atatakiwa kulipa faini isiyopungua shilingi 30,000 na isiyozidi sh. Milioni 1 hivyo hakuna kifungu kinachozungumia kutoza faini ng’ombe.

Kwa upande wake Daktari Mkuu wa Mifugo Tanzania (CVO),  Profesa Hezron Nonga amesema waliokamata mifugo hiyo wamevunja Sheria ya Magonjwa ya Wanyama Namba 17 ya mwaka 2003, Sheria ya Ustawi wa Wanyama Namba 19 ya mwaka 2008 kutokana na ng’ombe 600 kulundikana kwenye zizi dogo linalotosha ng’ombe 60 tu hali iliyosababisha mifugo kukosa hewa na kufa, ndama kukanyagwa, kujeruhiwa na kufa.

Prof. Nonga alisema  ng’ombe hao wamefungiwa zizini muda mrefu bila maji wala malisho hali iliyopelekea afya zao kudhoofika, utaratibu wa ukamataji mifugo haukufuatwa kwa kuwa haukuhusisha daktari wa mifugo kama sheria inavyoelekeza huku mifugo hiyo ikinyimwa chanjo na tiba hivyo waliohusika na ukamataji huo walitakiwa kukamatwa na kushtakiwa kwa mujibu wa sheria hizo.

Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika, Rojaz Romuli alisema halmashauri hiyo haina bajeti ya kutibu mifugo pindi inapokamatwa msituni bali jukumu lao ni kulinda misitu isiharibiwe na wavamizi wakiwemo wafugaji na wawindaji haramu.

Hivyo baada ya mazungumzo ya kina ya kisheria na kubainika kulikuwa na ukiukwaji mkubwa wa sheria ndipo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Tanganyika, Rojazi Romuli akalazimika kubatilisha adhabu hiyo na kuwatoza faini ya shilingi milioni 11 badala ya shilingi milioni 60 ya hapo awali.

Kwa muda mrefu wafugaji wa Wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi wamekuwa wakilalamikia kunyanyaswa, kuteswa kupigwa faini kubwa na hata kuuwawa na kwamba malalamiko hayo yalishatolewa Rais Dk. John Magufuli alipofanya ziara mkoani Katavi mwaka jana.

Pia malalamiko ya aina hiyo yalitolewa kwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina na Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Juma Homera waliposhiriki uzinduzi uogeshaji mifugo Halmashauri ya Mpwimbwe mkoani  Katavi.

Homera alilazimika kuchukua hotuba nzima iliyojaa ya malalamiko ya wafugaji na kuikabidhi kwa Kamanda wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Katavi kwa hatua zaidi lakini bado Halmashauri ya  Tanganyika imeendeleza manyanyaso kwa wafugaji kwa kuwatoza faini kubwa ambazo haziko kwa mujibu wa sheria.

Share:

TMDA WAPONGEZA USAJILI WA MADUKA YA DAWA MUHIMU ZA BINADAMU NJOMBE

Kaimu meneja wa TMDA kanda ya nyanda za juu kusini,Anitha Mshighati akiendelea kutoa mafunzo kwa wataalamu/watendaji wa afya wa halmashauri za mkoa wa Njombe katika kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa chuo cha afya Kibena mjini Njombe mkoani humo.
Kaimu meneja wa TMDA kanda ya nyanda za juu kusini,Anitha Mshighati akiendelea kutoa mafunzo kwa wataalamu/watendaji wa afya wa halmashauri za mkoa wa Njombe katika kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa chuo cha afya Kibena mjini Njombe mkoani humo.
Baadhi ya wataalamu wa afya wakiwa makini kusikiliza,wakati wa kikao cha afya kilichofanyika mjini Njombe.
Katalina Revocat katibu tawala wa mkoa wa Njombe aliyekuwa mgeni rasmi akitoa hotuba ya ufunguzi wa kikao cha wataalamu wa afya na TMDA kilichofanyika katika ukumbi wa chuo cha afya kibena.
Kaimu meneja wa TMDA kanda ya nyanda za juu kusini, Anitha Mshighati wakati alipokuwa akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari
Dkt.Bumi Mwamasage mganga mkuu wa mkoa wa Njombe akizunguzmza na waandishi wa habari mara baada ya hotuba ya mgeni rasmi iliyotolewa kwa wataalamu wa afya na mamlaka ya dawa na vifaa tiba kanda ya nyanda za juu kusini.
**
Na Amiri Kilagalila-Njombe

Licha ya uwepo wa changamoto katika utoaji na utekekelezaji wa huduma za afya nchini,taarifa ya mamlaka ya dawa na vifaa tiba TMDA kanda ya nyanda za juu kusini inaonyesha utekelezaji mzuri katika usajili wa maduka ya dawa za binadamu mkoani Njombe huku moja pekee likibainika kuto kuwa na usajili.

Taarifa ya matokeo ya ukaguzi wa mwezi wa 7 mpaka wa 12 mwaka 2019 iliyosomwa katika kikao cha kawaida cha TMDA na wataalamu wa afya wa halmashauri za mkoa wa Njombe katika ukumbi wa chuo cha afya Kibena, kwa lengo la kuwaongezea uzoefu,inaonesha maduka matatu huku moja likiwa ni la dawa za binadamu na mawili ni dawa za mifugo hayakuwa na usajili pamoja na vibali vya kuendesha biashara huku wamiliki wakiagizwa kuomba usajili wa vibali ndani ya siku 14.

Aidha Idadi ya majengo ya afya yaliyokaguliwa katika kipindi hicho,kanda ilikagua jumla ya majengo 128 ikiwa hospitali 12,vituo vya afya 13,zahanati 4,famasi 9,maduka ya dawa muhimu 70,maduka ya dawa za mifugo 19 na maabara 1.

Anitha Mshighati ni kaimu meneja wa TMDA kanda ya nyanda za juu kusini,amasema wataendelea kukumbushana na kutoa elimu ili kuepusha ukiukwaji katika utoaji huduma.

“Tunataka kuhakikisha vile vitu ambavyo tumevisajili vinaendelea kuwepo sokoni na katika ubora ule ule maana sio kila wakati wakaguzi wanakuwepo wakati wa uhishaji wa bidhaa,kwa hiyo tunatakiwa kuhakikisha ubora tulioukubali unaendelea kuwepo katika nchi yetu”alisema Anitha Mshighati

Mganga mkuu wa mkoa wa Njombe Dkt.Bumi Mwamasage amesema ukaguzi hufanyika kila robo ya mwaka katika maduka yote ya dawa mkoani Njombe licha ya kuwepo kwa changamoto za ukiukwaji wa sheria huku hatua za kisheria zikiendelea kuchukuliwa kwa wanaobainika.

Katalina Revocati ni katibu tawala wa mkoa wa Njombe,ambaye alikuwa mgeni rasmi katika kikao hicho,ametoa rai kwa wakurugenzi wa halmashauri zote kuendelea kutekeleza majukumu ya udhibiti wa bidhaa za afya ili kulinda afya ya jamii.

“kumekuwa na changamoto mbali mbali ambazo zimekuwa zikijitokeza ambazo sisi sote tunatakiwa kuwa walinzi maswala haya ni kama vile halmashauri kuto kufanya kaguzi za mara kwa mara katika vituo vya kutolea huduma za afya na maduka ya dawa,kufuatilia dawa na vifaa tiba,hali hiyo inasababisha baadhi ya maduka na vituo vya afya kuendelea kuhifadhi dawa katika mazingira yasiyofaa hivyo kuhatarisha ubora wake”alisema Katalina Revocati

Baadhi ya washiriki katika kikao hicho wamekiri kupokea mafunzo na kwenda kuyatumia kikamilifu ili kuendelea kuboresha huduma ya afya kwa jamii.
Share:

POLISI TANZANIA YAMSAKA MTUME MWAMPOSA VIFO VYA WAUMINI 20 WAKIKANYAGA MAFUTA YA UPAKO


Mtume Boniface Mwamposa, kulia ni RPC Kilimanjaro Salum Hamduni

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro Salum Hamduni, amesema kuwa Jeshi la Polisi linaendelea kumsaka Mtume Boniface Mwamposa, aliyetoweka baada ya watu takribani 20 kufariki, wakati wakikimbilia kukanyaga mafuta ya upako katika kongamano lake lililofanyika mkoani humo.

Kamanda Hamduni amesema kuwa hadi sasa Jeshi hilo linawashikilia watu Saba kwa mahojiano zaidi kufuatia tukio hilo na kwamba jumla ya watu 20 walipoteza maisha huku wengine 16 wakijeruhiwa.

"Hatua tulizozichukua hadi sasa ni kuanza uchunguzi wa kujua ni nini hasa kilitokea na kupelekea vifo na majeruhi kwa hao waumini na tunawashikilia watu saba kwa mahojiano, Mchungaji Mwamposa tunamtafuta kwakuwa alitoweka mara baada ya hilo tukio kutokea" amesema Kamanda Hamduni.

Kwa mujibu wa Kamanda Hamduni jumla ya watu 20 walipoteza maisha siku ya jana ya Februari 1, 2020, katika viwanja vya Majengo Mjini Moshi, ambapo Watoto wa kike ni Wanne, Wanawake 15 na Mwanaume ni Mmoja, na majeruhi wamelazwa katika Hospitali ya Mawenzi.
Share:

RAIS MAGUFULI NA MKEWE WAMESHIRIKI MISA TAKATIFU DOMINIKA YA 04 MWAKA “A” KATIKA KANISA KATOLIKI LA MTAKATIFU PETRO PAROKIA YA OYSTERBAY DAR

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mkewe Janeth Magufuli pamoja na Waumini wengine wa Kanisa Katoliki wakishiriki Misa Takatifu Dominika ya 04 ya Mwaka “A” iliyofanyika katika kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es Salaam. Ibada iliyoongozwa na Paroko wa Parokia hiyo Padre Dkt. Alister Makubi, Febuari 02, 2020.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipiga makofi na mkewe Janeth Magufuli ya kuwapongeza viongozi wapya wa halmashauri ya Walei ngazi ya parokia kwa kuchaguliwa wakati wa Misa Takatifu Dominika ya 04 ya Mwaka “A” iliyofanyika katika kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es Salaam. Ibada iliyoongozwa na Paroko wa Parokia hiyo Padre Dkt. Alister Makubi, Febuari 02, 2020. 



Share:

RAIS MAGUFULI ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI VIFO VYA WATU 20 WAKIKANYAGA MAFUTA YA UPAKO MOSHI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametuma salamu za rambirambi kufuatia vifo vya Watu 20 waliofariki dunia Jumamosi Februari 1,2020 katika ibada ya mahuburi wakati wa harakati za kukanyaga mafuta ya upako kwenye kongamano la Mtume Boniface Mwamposa 'Buldoza' katika Viwanja vya Majengo Manispaa ya Moshi mkoani  Kilimanjaro.


Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili February 2

















Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger