Thursday, 5 December 2019

Picha : AGAPE, POLISI WAADHIMISHA SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA




Shirika lisilo la kiserikali Agape Aids Cotrol Program la mkoani Shinyanga, limefanya maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia  kwa kupinga vitendo vya ubakaji, ulawiti, mimba na ndoa za utotoni, pamoja na kutoa lugha chafu za matusi kwa wafanyabiashara wanawake sokoni.


Maadhimisho hayo ambayo kilele chake ni Desemba 10 mwaka huu, yamefanyika kwenye viwanja vya Zimamoto Shinyanga mjini leo Desemba 5,2019  ambapo mgeni rasmi alikuwa Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Sophia Jongo.

Akizungumza kwenye maadhimisho hayo ,Kamanda Jongo, ametoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Shinyanga kuacha tabia ya kuwafanyia vitendo vya ukatili watoto wadogo, ikiwemo ubakaji, ulawiti, vipigo, kuwapa mimba pamoja na kuwaozesha ndoa za utotoni.

Amesema mkoa wa Shinyanga unashika nafasi ya tano kitaifa dhidi ya matukio ya ubakaji, ikiwamo wanafunzi kupewa ujauzito pamoja na kuozeshwa ndoa za utotoni, jambo ambalo linauchafua mkoa, na hivyo kuwataka wananchi waachane na matukio hayo ili watoto wapate kusoma kwa bidii na kuweza kutimiza ndoto zao.

“Nayapongeza sana mashirika haya ambayo siyo ya kiserikali likiwamo la Eguality For Growth (EFG) pamoja na Shirika la Agape, kwa kazi nzuri sana ambayo wanayoifanya mkoani hapa kwa kupambana kutokomeza matukio ya ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto,”amesema Jongo.

“Pia naomba waendelee na mapambano haya ya kutokomeza ukatili huu wa kijinsia, kwa kutoa elimu kwa wananchi pamoja na wanafunzi dhidi ya madhara haya ya kufanya ukatili, ambapo mkoa wetu unaongoza kwa matukio ya ubakaji watoto na tunashika nafasi ya tano kitaifa,”ameongeza.

Naye mkurugenzi wa Shirika la Agape John Myola, amesema Shirika hilo limekuwa likijihusisha na miradi mbalimbali ya kupinga ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto, ikiwemo miradi ya kupinga mimba na ndoa za utotoni, pamoja na ukatili dhidi ya wanawake sokoni.

Pia amelipogeza Jeshi la Polisi kwa kushirikiana vyema na Shirika hilo la Agape dhidi ya mapambano ya matukio ya ukatili, ambapo wao wanapokuwa wakitoa taarifa za matukio hayo, polisi hufika mara moja kwenye eneo la tukio na kumkamata mtuhumiwa.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la Equality For Growth kutoka Jijini Dar es salaam Jane Majigita, ametoa wito kwa wananchi pamoja na watoto, wawe wanatoa taarifa za matukio ya ukatili wa kijinsia, ili yafanyiwe kazi na wahusika kuchukuliwa hatua kali za kisheria, hali ambayo itapunguza matukio hayo.

Aidha kauli mbiu ya maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia mwaka huu inasema "Kizazi Chenye Usawa, Simama Dhidi ya Ubakaji".

TAZAMA MATUKIO KATIKA PICHA HAPA CHINI

Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Shinyanga Sophia Jongo akizungumza leo Desemba 5,2019 kwenye maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia,ambapo kilele chake kitafanyika Desemba 10 mwaka huu. Picha zote na Marco Maduhu - Malunde 1 blog

Mkurugenzi wa Shirika la Agape mkoani Shinyanga John Myola akizungumza kwenye maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia.

Mkurugenzi wa Shirika la Equality For Growth (EFG) kutoka Jijini dar es salaam Jane Majigita, akizungumza kwenye maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia.

Mkuu wa kituo cha Polisi wilaya ya Shinyanga Grace Salia akizungumza kwenye maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia

Afisa Maendeleo ya Jamii manispaa ya Shinyanga Anjel Mwaipopo akizungumza kwenye maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia.

Wanafunzi pamoja na Askari Polisi wakiwa kwenye maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kwenye viwanja vya Zimamoto Shinyanga Mjini.

Wanafunzi pamoja na askari polisi wakiwa kwenye maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kwenye viwanja vya Zimamoto Shinyanga Mjini.

Wanafunzi pamoja na askari Polisi wakiwa kwenye maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kwenye viwanja vya Zimamoto Shinyanga Mjini.

Wazazi wakiwa kwenye maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia.

Watumishi wa Serikali na Askari Polisi wakiwa kwenye maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia.

Wanafunzi wakiwa kwenye maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia.

Wanafunzi wakiwa kwenye maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia.

Jeshi la Zimamoto na uokoaji wakitoa elimu ya majanga ya moto namna ya kutumia kifaa cha kuzimia moto kwenye maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia.

Wanafunzi kutoka Shule ya Msingi Mwenge wakitoa burudani.

Kikundi cha Ngoma kutoka Mwawaza kikitoa burudani.

Burudani ikiendelea kutolewa kwenye maadhimisho hayo ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kwa kucheza na nyoka.

Kiongozi wa kikundi cha ngoma, Mahona Mtoba, akitoa burudani Meza kuu.

Awali wanafunzi wakiandamana kutoka Bwalo la Polisi hadi kwenye viwanja vya Zimamoto kwa ajili ya kuadhimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia.

Maandamano yakiendelea.

Wanafunzi wakionyesha mabango yenye ujumbe mbalimbali.

Mgeni Rasmi akipokea maandamano pamoja na meza kuu.

Kaimu kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Shinyanga Sophia Jongo, akitoa zawadi ya vifaa vya shule kwa ajili ya wanafunzi wenye uhitaji katika shule ya Sekondari Uhuru, akimkabidhi mwalimu wao.

Kaimu kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Shinyanga Sophia Jongo, akitoa zawadi ya vifaa vya shule kwa ajili ya wanafunzi wenye uhitaji katika shule ya Msingi Mwenge, akimkabidhi mwalimu wao.

Mgeni rasmi kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Sophia Jongo akipiga picha ya pamoja na wafanyakazi kutoka Shirika la Agape, pamoja na mkurugenzi wa Shirika la EFG, Jane Majigita (wa kwanza mkono wa kushoto aliyekaa kwenye kiti).

Mgeni rasmi kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Sophia Jongo akipiga picha ya pamoja na kikundi cha ngoma.

Picha zote na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog.

Share:

BINTI AFARIKI AKIMUOKOA MWANAUME KWENYE MTO ULIOJAA MAJI

Waokoaji nchini Kenya wameuopoa mwili wa kijana mmoja aliyekufa maji alipokuwa akijaribu kumuokoa mwananume ambaye alikuwa akiomba usaidizi alipokuwa akivuka mto uliokuwa umefurika.

Anna Nduku mwenye umri wa miaka 19 alianguka katika mto Kandisi karibu na eneo la Ongata Rongai , viungani vya mji mkuu wa Nairobi siku ya Jumanne.

Ni miongoni mwa zaidi ya watu 130 ambao wamefariki kutokana na mafuriko yanayosababishwa na mvua kubwa ambayo imekuwa ikinyesha tangu siku ya Jumanne.

Bi Nduku alikuwa akijibu kilio cha mwanaume aliyekuwa akining'inia katika eneo moja la daraja ambalo liikuwa likijengwa.

Mwanaume huyo aliokolewa lakini yeye akaanguka katika mto huo alipojaribu kumuokoa.

Mamake Nduku, Elizabeth Mutuku, alikuwa karibu wakati ajali hiyo ilipotokea.

''Nilimuona akijaribu kujitoa katika maji nikajaribu kumuokoa. Nilimwita Anna Anna! Nilitaka kumrushia kijiti ili kujaribu kumvuta lakini mto huo ulikuwa umejaa maji hivyo basi alikuwa akirushwa kutoka eneo moja hadi jingine kabla ya kusombwa na maji hayo''.

Mto huo ulikuwa umefurika kutokana na mvua kubwa inayonyesha ambayo ilianza siku ya Jumatatu.

Ni baadhi ya mvua zilizoripotiwa katika eneo la Afrika mashariki katika wiki za hivi karibuni.

Wakazi wanasema kwamba hii ni miongoni mwa ajali za hivi karibuni ambazo zimefanya watu kadhaa kusombwa na maji katika kipindi cha miaka miwili iliopita.

Daraja la zamani liliondolewa mwaka 2017 na daraja jipya bado halijakamilishwa. Hatua hiyo imewafanya wakaazi kupitia maji kwa kutumia mawe wanayokanyaga ili kuvuka mto huo.

Dada yake Nduku , Maryam Zenneth, amelaumu serikali za mitaa kwa kushindwa kumaliza daraja hilo ambalo ni kiunganishi muhimu kati ya kijiji chake na mji wa soko wa Ongata Rongai.

''Watu wengi wanafariki na wao wanatazama watu wakiendelea kupoteza maisha'' , aliiambia BBC huku akiwa amejawa na hasira.

''Wanakuja na kuomboleza nawe lakini hawachukui hatua yoyote, leo ni dada yangu kesho atakuwa nani''?

''Daraja hilo ndio barabara kuu miongoni mwa watoto wanaokwenda shule. Kwa nini waliliondoa daraja lililokuwepo ili kuanza kujenga jipya na hawalimalizi kulijenga''?Watu hupanda katika daraja hilo ambalo halijakamilisha ili kujaribu kuvuka mto huo

Serikali ya mitaa katika eneo hilo bado haijatoa tamko lolote . Akikumbuka kuhusu maisha ya mwanawe, mamake amesalia akiwa amevunjika moyo. 'Nina huzuni, pengine angekuwa kiongozi wa siku zijazo ama hata mwalimu. Kupoteza maisha kama hayo kutokana na daraja ni uchungu mwingi."

Mvua zaidi inatarajiwa kunyesha katika taifa hilo katika siku zijazo , na serikali inawashauri watu wanaoishi katika maeneo ambayo yametabiriwa kuathiriwa vibaya kuhamia katika maeneo salama.

Maeneo mengine katika eneo hilo , watu sita wamefariki mashariki mwa Uganda kufuatia maporomoko ya ardhi baada ya mvua kunyesha kwa siku mbili mfululizo na kufikia sasa takriban watu 50 hawajulikani waliko.
Share:

MSHINDI WA PROMOSHENI YA TIGO CHEMSHA BONGO 2019 AKABIDHIWA GARI LAKE


Mkazi wa Zanzibar, Shaban Khamis Ali(49) akifurahia mara baada ya kukabidhiwa gari yake aina Renault Kwid yenye thamani ya 23m/- baada ya kuibuka mshindi wa promosheni ya Tigo Chemsha Bongo 2019.  
BAHATI IMEMUANGUKIA Mzee Shaban Khamis kutoka Zanzibar kushinda Gari aina ya Renault Kwid. Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Pwani, Joseph Mutalemwa, amempongeza Mzee Shaban kwa kutumia fursa ya #TigoFiesta2019 Chemsha Bongo vizuri 
Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Pwani, Joseph Mutalemwa,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kumkabidhi zawadi Mshindi wa promosheni ya Tigo Chemsha Bongo 2019 
“Kuna vitu vikitokea kwenye maisha yako inakuwa ngumu kuficha hisia zako. Nashukuru TIGO kwa kuleta mchezo huu wa #TigoChemshaBongo nilicheza nikiamini nitashinda pesa lakini nimeambulia zawadi kubwa kabisa ya gari” ,Mzee Shaban Khamis
Dar es Salaam Desemba 5 2019.Mkazi wa Zanzibar, Shaban Khamis Ali(49) amekabidhiwa rasmi gari yake aina ya Renault Kwid yenye thamani ya 23m/- baada ya kuibuka mshindi wa promosheni ya Tigo Chemsha Bongo 2019.
Promosheni hiyo iliyodumu kwa siku 90 kuanzia tarehe 4 Agosti hadi 14 Novemba 2019 na wateja wa Tigo walipata nafasi ya kujishindia zawadi za pesa taslim kila siku na droo ya mwisho mshindi alikuwa anajinyakulia zawadi ya gari. Promosheni hii ilishuhudia washindi 90 kila siku waliojishindia Tshs 100,000 na washindi wengine 90 waliojishinda Tshs 50,000. Pia tuliwapa washindi 12 kili wiki kwa mda wa wiki 12, Tshs 1,000,000.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo Shabaan alisema “Wakati napigiwa simu,nilikuwa nyumbani najipanga kutoka kuenda katika mihangaiko yangu ya kibiashara, basi nilipopata ile taarifa kwamba nimeibuka mshindi nilifurahi sana kwani sikutegemea kabisa kuwa ningeibuka mshindi katika promosheni hii, habari hizi naziona kama ndoto kwangu, nashukuru Tigo kwa kunifungia mwaka vizuri na kutimiza ndoto yangu ya kumiliki gari, kwani itanisaidia katika mizunguko yangu ya kibiashara “alisema kwa furaha.

Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Pwani, Joseph Mutalemwa, alimpongeza mshindi huyo na kutumia fursa hiyo kuwashukuru wateja wote wa kampuni ambao walishiriki na baadhi yao kujishindia zawadi mbalimbali ikiwemo zawadi za fedha taslimu ambayo yalitolewa na kampuni hiyo.

“Tunayo furaha kubwa katika kipindi hiki tunachoelekea katika msimu wa sikukuu kumkabidhi mshindi wetu wa gari ya aina Renault Kwid,yenye thamani ya 23m/-, gari hili ni jipya kabisa,. Tunawashukuru wateja wetu nchi nzima walioshiriki kwenye promosheni hii ya miezi mitatu ambayo imemalizika mwishoni mwa mwezi wa Novemba 2019”,alisema Mutalemwa.

Aliongeza kuwa, promosheni hii ambayo ilianza jijini Mwanza katika msimu wa Tigo Fiesta 2019-Saizi Yako imepata mafanikio makubwa kutokana na wateja wengi kujitokeza kushiriki na baadhi yao kufanikiwa kujishindia zawadi(fedha taslim) mbalimbali na hivyo Tigo kufanikisha lengo lake ambalo lilikuwa ni kuwashukuru wateja kwa kuiunga mkono kampuni kupitia kununua bidhaa zake mbalimbali.

Mutalemwa aliwashukuru wateja wote wa Tigo kwa kuendelea kuunga mkono kampuni na kuahidi kuwa promosheni mbalimbali za kunufaisha wateja wa kampuni hiyo zinatendelea kubuniwa katika siku za usoni.

Share:

TAMISEMI-Over 50,000 pupils miss out on Form One selection for 2020

A total of 58,699 who passed the Primary School Leaving Examinations in 2019 have not been selected to join Form One in 2020 due to lack of classrooms. The minister of Local Government Seleman Jafo made the announcement today in Dodoma saying those are affected amounted to 7.73 per cent. “This means that 701,737 pupils equivalent to 92.27… Read More »

The post TAMISEMI-Over 50,000 pupils miss out on Form One selection for 2020 appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Majina wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza 2020

Wanafunzi 701,038 sawa na asilimia 92.27 waliofaulu mtihani wa darasa la saba mwaka 2019 wamechaguliwa kuendelea na kidato cha kwanza mwaka 2020.

Wanafunzi  58,699 hawajapata nafasi kutokana na uhaba wa vyumba vya madarasa huku ikiagizwa ujenzi wa madarasa ufanyike mapema ili waweze kuendelea na masomo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Alhamisi Desemba 5, 2019 Waziri wa Tamisemi, Selemani Jafo amesema waliokosa nafasi wanatoka katika Mikoa 13 nchini huku Mkoa wa Kigoma ukiwa na idadi kubwa ya wanafunzi 12,092. 

Majina ya wanafunzi waliochaguliwa kidato cha kwanza 2020

“Wanafunzi 701,038 sawa na asilimia 92.27 watajiunga moja kwa moja kidato cha kwanza Januari 2020 na kati yao  wanafunzi 3,145 sawa na asilimia 0.41 watajiunga na shule za bweni.”

“Kati ya waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza wavulana ni 335, 513 na wasichana ni 365, 525,” amesema Jafo.

Waziri Jafo amesema hadi Februari 2020 madarasa yawe yamekamilika ili wanafunzi wajiunge mapema shuleni.

Majina ya wanafunzi waliochaguliwa kidato cha kwanza 2020


Share:

Kabendera atakiwa kwenda mwenyewe kwa DPP ili kujua Hatima Yake

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeuambia upande wa utetezi katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili Mwandishi wa Habari, Erick Kabendera kuwa waende wenyewe kwa Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP) ili kujua hatma ya barua ya Kabendera ya makubaliano ya kuomba msamaha na kukiri kosa.

Hatua hiyo imefikiwa wakati kesi hiyo ilipoitwa Mahakamani hapo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Janet Mtega kwa ajili ya kutajwa na kudaiwa kuwa upelelezi bado haujakamilika hivyo upande wa utetezi wakawasilisha hoja zao.

Wakili wa Utetezi, Jebrah Kambole amesema Oktoba 11,2019 waliitaarifu Mahakama juu ya Kabendera kuandika barua ya kuomba msahama na kukiri kosa kwenda kwa DPP lakini mpaka leo ni miezi miwili hawajapata mrejesho wowote kutoka kwa DPP na Mtuhumiwa bado yuko gerezani na ni mgonjwa.

Kufuatia hoja hizo, Hakimu Mtega ameutaka upande wa utetezi waende wenyewe kufuatilia jalada la kesi kwa DPP ili wajue kinachoendelea na ameiahirisha kesi hiyo hadi itakapotajwa tena Desemba 18, mwaka huu.


Share:

3 NUTRITIONISTS at Doctors with Africa CUAMM Trustees

VACANCY FOR 3 NUTRITIONISTS  Background Doctors with Africa CUAMM Trustees: Doctors with Africa CUAMM Trustees is a non-for-profit entity, dealing with health issue. It was founded in 1987 and its headquarter is in Dar es Salaam, CUAMM focuses on supporting health system, strengthening projects tailored to the specific needs of the countries where the organization carries out projects.… Read More »

The post 3 NUTRITIONISTS at Doctors with Africa CUAMM Trustees appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Relationship Officer (50 posts) at AccessBank Tanzania (ABT)

CAREER OPPORTUNITY:  Relationship Officer (50 posts)  AccessBank Tanzania (ABT) is a commercial bank with a special focus on microfinance and SME. With very strong international shareholders such as AccessHolding, International Finance Corporation (World Bank), KfW, African Development Bank and MicroVest. ABT’s vision is to be committed to the development of financial systems that support social progress by rendering… Read More »

The post Relationship Officer (50 posts) at AccessBank Tanzania (ABT) appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Sikonge Wapigwa Marufuku Kulima Pamba Hadi Serikali Itakapotoa Tamko La Kuwaruhusu

NA TIGANYA VINCENT
WAKULIMA wilayani Sikonge ambao wanataka kulima zao la pamba wametakiwa kuwa wavumilivu hadi hapo utafiti utakapokamika ili Serikali ijiridhishe kama tishio la mdudu aina ya funza mwekundu halipo katika maeneo jirani yaliyopigwa marufuku kulima zao hilo.

Ushauri huo umetolewa juzi wilayani Sikonge na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wakati wa kikao robo ya kwanza cha Baraza la Madiwani.

Alisema kwamba Wizara iliweka karantini kwa Wilaya zinazopakana na mikoa ya Rukwa na Mbeya kutolima pamba kutokana na kuwepo funza wekundu wanaoshambulia zao hilo.

Mkuu wa Mkoa alisema hawezi kuruhusu watu walime hadi hapo wataalamu wa Wizara waje wajiridhishe na watoe tamko kuhusiana kutokuwepo kwa tishio la mdudu huyo.

Katika agizo lake Mkuu wa Mkoa aliwataka Madiwani wasiende kuwahamasisha wananchi kulima zao la pamba kabla hawajapata msimamo wa Serikali ili wasijekupata hasara.

Mwanri alisema kitendo cha kuruhusu kulimwa kwa zao hilo kabla ya matokeo ya wataalamu hayajatoka  kunaweza kusababisha hasara kubwa katika maeneo ya ndani na nje ya Mkoa wa Tabora ambapo funza huyo mwekundu anaweza kusabambaa hata katika maeneo ambayo alikuwa hayupo.

Awali Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge Peter Nzalalila aliishauri Serikali iwaruhusu walime  pamba kama zao mbadala ya tumbaku ambayo inapigwa vita kimataifa.

Aliomba Serikali iwaruhusu kulima pamba kwa kuwa maeneo ya jirani zao ambayo yalikuwa yamepigwa marufuku wameanza kulima na wana vyama vya Msingi vya zao hilo.

Nzalalila alisema wakazi wengi wamehamasika kulima pamba wanachosubiri kibali ili waweze kushiriki kilimo hicho kwa ajili ya kuondokana na umaskini.

Katika hatua nyingine Madiwani na Viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge wametakiwa kutumia mvua zinazoendelea kunyesha kuwahimiza wananchi kujielekeza katika kulima kwa kuzingatia kanuni za kilimo bora.

Alisema hatua hiyo itasaidia kuzalisha chakula na mazao ya biashara ya kutosha ambayo yatawasaidia kujiongezea kipato na kuboresha maisha yao.

Mkuu huyo wa Mkoa aliongeza kuwa kwa kutambua umuhimu wa kipindi hiki ndio maana amesimamisha kwa muda likizo za Maafisa Ugani na Kilimo ili waweze kutoa ushauri utakaomsaidia mkulima kulima kisasa.

Mwisho


Share:

Dk Kalemani : “Marufuku Nyumba Za Tembe na zilizoezekwa kwa Nyasi Kutowekwa Umeme “

NA SALVATORY NTANDU
Serikali imesema itachukua hatua kali za kisheria kwa wakandarasi wanaotekeleza miradi  ya  REA katika maeneo mbalimbali hapa nchini watakaobainika kuzibagua nyumba za tembe na zilizoezekwa kwa majani kwa kukataa kuzipatia nishati ya umeme nyumba hizo licha ya  wamiliki wake kulipia gharama za huduma hiyo.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Nishati Dk Medadi Kalemani kwenye ziara ya siku mmoja ya kukagua utekelezaji wa mradi wa REA katika Halmashauri za Ushetu na Msalala mkoani Shinyanga na  kupokea malalamiko ya wananchi kutopatiwa huduma hiyo kwa kigezo cha nyumba zao kutokuwa na ubora.

“Akibainika mkandarasi akifanya ubaguzi kwa wenye nyumba za tembe na nyasi ambao wamelipia gharama za kuunganishiwa umeme serikali haita mvumilia tutamchukulia hatua kali za kisheria”alisema Dk Kalemani.

Katika hatua nyingine DK KALEMANI ametoa siku 30 kwa Mkandarasi Kampuni ya ANGELIQUE INTERNATIONAL.LTD anayetekeleza mradi wa REA katika halmashauri ya Ushetu kuhakikisha anakamilisha kuweka umeme katika vijiji 54 kama mkataba wake unavyoelekeza.

“Kasi yako ya ujenzi wa mradi huu hairidhishi ukishindwa kutimiza ndani ya siku hizo nilizokupa hatua dhidi yako zitachukuliwa hebu ongeza wafanyakazi na vifaa ili kwenda sambamba na masharti ya mkataba wako”aliseme Dk Kalemani.

Fortunata Maila ni mkazi wa Igunda katika Halmashauri ya Ushetu ni miongoni mwa wanufauika na Mradi wa REA awamu ya Tatu amesema tangu huduma hiyo imeanza kutolewa wamenufaika kwa kuanzisha miradi ya ujasiriamali kama vile uzaji wa barafu vinyaji baridi kama vile soda na maji.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Kahama Anamringi Macha amesema kukamilika kwa mradi wa umeme katika Halmshauri hizo utatoa fursa nyingi za kujiajiri sambamba na kuwataka wananchi kuhakikisha wanailinda miundombinu hiyo ili iweze kudumu kwani imetumia fedha nyingi za serikali.


Share:

Wizara Ya Mifugo Na Uvuvi Kinara Kuelekea Uchumi Wa Viwanda

Na. Edward Kondela
Wizara ya Mifugo na Uvuvi imepongezwa kwa kuwa moja ya wizara ambazo ni vinara katika kusimamia na kutekeleza azma ya serikali ya awamu ya tano kuelekea uchumi wa kati unaotegemea viwanda kwa kusimamia uanzishwaji wa viwanda vinavyotegemea malighafi za mifugo.

Akizungumza jana (04.12.2019) kwenye mkutano wa mashauriano kati ya serikali na wawekezaji Mkoani Morogoro, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki, amesema uanzishwaji wa viwanda vya kusindika maziwa ni moja ya vipaumbele katika ofisi ya waziri mkuu jambo ambalo limekuwa likisimamiwa vyema na Wizara ya Mifugo na Uvuvi ambapo viwanda kadhaa vimeanzishwa na vingine vinaendelea kuanzishwa vikiwemo vya kuchakata ngozi.

Mhe. Kairuki ambaye ni mwenyekiti wa mikutano hiyo inayofanyika katika mikoa ya Morogoro, Pwani na Dar es Salaam ikishirikisha wizara 13 wakiwemo mawaziri na naibu mawaziri amesema wizara yake itahakikisha inaendelea kushirikiana na wizara nyingine katika kuweka mazingira bora zaidi ya wawekezaji ili kuanzishwa kwa viwanda vingi zaidi hali ambayo itakuza uchumi wa nchi na wananchi.

Awali akizungumza kwenye mkutano huo Mkoani Morogoro kuhusu sekta ya mifugo, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega amesema wizara tayari imeanza matumizi ya mizani katika minada ya mpakani na upili ili wafugaji waweze kuuza mifugo yao kwa kupimwa uzito badala ya kukadiria hali ambayo imekuwa ikiwafanya wafugaji kutopata faida kulingana na muda na gharama ambazo wanatumia kutunza mifugo yao.

“Tayari tumeanzisha hili sasa wafugaji wanauza mifugo yao kwa kupimwa uzito, tunataka tufike mahali baada ya kuwa na mizani ni kuwa na bei ya nyama kwa kilogramu ili mfugaji aweze kupata faida kwa kuuza mfugo wake, badala ya kuuza kwa kukadiria wakati mfugaji anahangaika zaidi ya miaka minne hadi mitano kutunza mfugo wake.” Amesema Mhe. Ulega

Mhe. Ulega amesema kuhusu maeneo ya malisho ya mifugo, wizara inaboresha sheria ili ardhi iliyotengwa kwa ajili ya ufugaji na malisho ilindwe na sheria isiwe rahisi ardhi hiyo kubadilishwa matumizi mengine.

Aidha amefafanua kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Magufuli amefanya jambo kubwa kwa kutoa maelekezo ya kutazamwa maeneo nchini ambayo yanaweza kutumika kwa ajili ya ufugaji na kilimo, ambapo wizara kupitia maeneo ya Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO) imetoa kiasi kikubwa maeneo ya malisho kwa wafugaji wanaoweza kukodi kwa muda mfupi ili mifugo yao iweze kupata maeneo ya malisho ya uhakika.

Naibu waziri huyo ametoa rai kwa wafugaji na wizara kushirikiana ili kuhakikisha viwanda vya kusindika maziwa kutozalisha bidhaa chini ya malengo yao kutokana na uhaba wa maziwa kutoka kwa wafugaji kwa kuwa ushirikiano huo utaiwezesha wizara kuyafikia masoko na kuwawezesha wafugaji kupata huduma ya kuweza kufanya shughuli zao na kusisitiza wafugaji wa Mkoa wa Morogoro kujiunga katika ushirika.

“Kiwanda cha Tanga Fresh kimefanikiwa kwa kuwa kina ushirika na kinamilikiwa na Chama Kikuu cha Ushirika cha Wafugaji wa Ng’ombe wa Maziwa Mkoa wa Tanga (TDCU) ambacho kina hisa zaidi ya asilimia 40 katika kiwanda hicho wafugaji wa hapa Mkoani Morogoro nanyi pia mjiunge katika ushirika na viwanda vya hapa visikose malighafi ya maziwa kwa ajili ya kusindika.” Amesema Mhe. Ulega

Kuhusu uanzishwaji wa viwanda nchini vinavyotegemea malighafi ya mifugo Naibu Waziri Ulega amesema kuna takriban viwanda vitano vya kuchakata nyama vinavyojengwa nchini nzima na kwamba uwepo wa viwanda hivyo vitachangia matumizi sahihi ya reli ya kisasa (SGR) kwa kuwa utakuwepo utaratibu wa reli ya mizigo ambapo pia mifugo itasafirishwa na kuwataka wananchi kuendelea kufanya shughuli mbalimbali za uzalishaji ili kutumia fursa zilizopo.

Katika kudhibiti magonjwa ya mifugo, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi akizungumza kwenye mkutano huo wa mashauriano kati ya serikali na wawekezaji Mkoani Morogoro, amefafanua kuwa serikali imefanya kazi kubwa katika madawa ambapo Kituo cha Kuzalisha Chanjo Tanzania (TVI) katika kipindi cha miaka minne kimeweza kubaini magonjwa 11 ya kipaumbele ambapo tayari chanjo sita ikiwemo ya ugonjwa wa mdondo ambao umekuwa ukiathiri wafugaji wa kuku tayari zinazalishwa na kupatikana kote nchini.

Amebainisha pia serikali ya awamu ya tano kuanzia mwaka wa fedha 2018/2019 imetoa dawa ya ruzuku kwa majosho yote yanayofanya kazi nchini nzima na mwaka huu 2019/2020 imeendelea kutoa ili mifugo iweze kuogeshwa kudhibiti magonjwa na kufafanua kuwa mkakati wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi ni kufanya ukaguzi wa kila mara kubaini ubora wa dawa za mifugo zilizopo madukani na kwamba itakuwa inadhibiti dawa ili wafugaji wasiendelee kuuziwa dawa zisizo sahihi na ambazo hazifai kwa matumizi ya mifugo yao.

Katika sekta ya uvuvi naibu waziri huyo amesema serikali ina kituo cha muda mrefu cha Kingolwira kilichopo Mkoani Morogoro ambacho kinazalisha vifaranga vya samaki ambao wanapatikana kwa bei nafuu zikiwemo pia huduma za kitaalamu, hivyo kuwataka wananchi kukitumia kituo hicho ili kukuza uchumi wao kwa kufuga samaki kwa kuwa Tanzania inazalisha samaki Tani 350,000 hadi 400,000 lakini mahitaji ni Tani 800,000 kwa mwaka.

“Sasa hivi tumeweka mkakati mkubwa wa kuzuia samaki kutoka nje ya nchi ili wananchi waweze kuchangamkia fursa katika sekta ya uvuvi kwa kufuga samaki na kufidia soko lililopelea la Tani 400,000 hivyo ni vyema mchangamkie fursa hii.” Amesema Mhe. Ulega

Kufuatia migogoro ya ardhi kati ya wakulima na wafugaji ambayo ilijitokeza miaka iliyopita Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro Mhe. Mohamed Utaly amewaambia wajumbe wa mkutano huo kuwa migogoro ya namna hiyo imeisha katika wilaya hiyo kutokana na juhudi mbalimbali ambazo zimefanywa na serikali kwa kushirikiana na wananchi.

Mkutano wa mashauriano kati ya serikali na wawekezaji Mkoani Morogoro, ambao ulikuwa chini ya mwenyekiti Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki, umehudhuriwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Mendeleo Mhe. William Lukuvi, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega, Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Josephat Kandege, Naibu Waziri wa Madini Mhe. Stanslaus Nyongo, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Sima, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Costantine Kanyasu, Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Subira Mgalu, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Vijana na Ajira) Mhe. Anthony Mavunde.

Mkutano huo umehudhuriwa pia na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Loatha Sanare pamoja na watendaji kutoka taasisi na mashirika yaliyo chini ya wizara hizo pamoja na wafanyabiashara wa Mkoa wa Morogoro.


Share:

Wizara Yafungua Dawati Mashuleni Mkoani Rukwa Kutokomeza Ukatili Kwa Watoto

Na Mwandishi wetu Rukwa.
Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii kwa kushirikiana na Mkoa wa Rukwa imefungua Madawati ya watoto kwa baadhi ya Shule za Msingi na Sekondari katika Manispaa ya Sekondari kwa lengo la kupambana na ukatili dhidi ya Watoto ikiwemo mimba za utotoni.

Mkurugenzi Msaidizi anayeshughulikia masuala ya watoto kutoka Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Bw. Sebastian Kitiku akiongea na wanafunzi wa shule za Msingi Chem chem na Lukewile zote Manispaa ya Sumbawanga ameutaja Mkoa wa Rukwa kuwa na changamoto kubwa ya mimba za utotoni.

Aidha Bw. Kitiku amewataka watoto shuleni hapo kulitumia Dawati  la Watoto Shuleni hapo ipasavyo ili liweze kuwa masaada mkubwa kwa wanafunzi wanaokumbana na vitendo vya ukatili na kuwataka kutokuwa waoga wa kutoa taarifa ili kuwawezesha walimu wa malezi shuleni hapo kuweza kuangalia namna bora ya kulifanyia kazi taio hilo.

 Bw. Kitiku ameongeza kuwa watoto wanatakiwa kupewa haki zote kama ilivyo kwa watu wazima akizitaja haki hizo kuwa haki ya kulindwa, haki ya kuendelezwa, Afya, kutobaguliwa na kushirikishwa kama ilivyobainishwa katika Sera ya Taifa ya Mtoto ya Mwaka 2008.

Aidha Mkurugenzi huyo amewataka watoto hao kutoa taarifa katika Dawati la Jinsia la Jeshi la Polisi lakini pia kutumia mtandao wa simu ya bure ya 116 ili kuweza kupewa msaada wa haraka pindi watakapobaini kuwa wanafanyiwa vitendo vya ukatili ambavyo amevitaja kuwa ulawiti na ubakaji, kazi ngumu kwa watoto pamoja na utumikishwaji watoto manyumbani kwa maana ya ukatili wa kingono na kimwili.

Dwati la watoto katika shule hizo limefanyika kwa wanafunzi husika kuchagua wawakilishi wao ndani ya Dawati lakini pia wanafunzi hao baada ya kuelimishwa pia wamewachagua walimu ambao wanawaamini kuwa walezi hao ambao kimsingi watafanya kazi kwa karibu sana na Dawati la Jinisia shuleni hapo.

Zoezi la uanzishwaji Dawati la Watoto shuleni pia limefanyika shule ya Sekondari Kilimani Maweni iliyoko nje kidogo ya mji wa Sumbawanga na Wizara kwa kushirikiana na uongozi wa shule na mkoa wameongoza wanafunzi shuleni hapo kuchagua wawalilishi wao wa Dawati lakini pia wamechagua walimu wawili kuwa walimu wa malezi shuleni hapo.

Wataalam wa Wizara ya Afya Idara Kuu Mawendeleo ya Jamii wako Mkoani Rukwa kushirikiana na Mkoa huo katika juhudi zake za kutokomeza vitendo vya ukatili dhidi ya watoto na mkoa ni miongoni mwa mikoa yenye kiwango cha juu Kitaifa kuwa na idadi kubwa ya mimba za utotoni.  


Share:

Ahukumiwa Kifungo Cha Mwaka Mmoja Jela Au Faini Ya Milioni Mbili Kwa Kukutwa Na Viuatilifu Visivyo Sajiliwa

Na innocent Natai, Morogoro
Mahakama ya Wilaya ya  Ifakara Mkoani Morogoro imemuhukumu kutumikia kifungo cha mwaka mmoja jela au faini ya shilingi Milioni Mbili pamoja na kuviteketeza viuatilifu kwa gharama zake mwenyewe, Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Yerusalem Mwamaja miaka 49 (Mhehe) baada ya kupatikana na hatia ya kupatikana na viuatiliafu visivyo sajiliwa

Hukumu hiyo imetolewa  Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Binge Njaga Mashabara, baada ya kujiridhisha na hoja za mashahidi watatu wa upande mshtaka, bila kuacha shaka yeyote.

Hakimu Mashabara alisema vitendo kama hivyo vinawasababishia hasara wakulima na seikali kwa ujumla ukiachilia mbali kuendelea kusababisha madhara kwa mazingira na kwa Afya za binadamu wanyama na mimea. Hivyo alitoa adhabu hiyo ili iwe onyo na fundisho kwa wote wenye tabia kama hizo.

Awali, Wakili wa Serikali, alidai kuwa hakukuwa na kumbukumbu za mashtaka ya nyuma dhidi ya mshatakiwa na hivyo kuiomba Mahakama kutoa adhabu kali ili iwe onyo na fundisho kwa wote wenye tabia kama hizo.

Katika utetezi wake Yerusalem Mwamaja alikubali mashtaka na aliomba apunguziwe adhabu kwani ni mara yake ya kwanza kufanya kitendo hicho na hata rudia.

Akizungumzia hukumu hiyo baada ya kutoka Mahakamani hapo Bw Solomon Shedrack Mungure amabaye ni Mkurugenzi wa Viuatilifu kutoka ofisi ya TPRI Dar es Saalam ameipongeza Mahakama hiyo kwa adahabu iliyotoa kwani itakuwa ni fundisho kwa wengine wenye tabia za kufanya biashara za viuatilifu visivyo Sajiliwa.

Aidha ametoa rahi kwa wauzaji na wasambazaji wa Viuatilifu nchi nzima wenye tabia za kuuza na kusambaza viuatilifu visivyo sajiliwa na kukaguliwa na TPRI kuacha mara moja kwani zoezi la ukaguzi na kuwabaini watu kama hao halikomi ni la kila siku na kila saa hivyo watakamatwa mara moja na kuwafikisha mahakamani.

Aidha amehitimisha kwa kusema kuwa kuuza au kusambaza viuatilifu bila kwa na elimu pia ni kosa kwani kunaweza kumsababishia madhara msambazaji au muuzaji wakati wa ufanyaji biashara bila kuwa na elimu ya namna bora na salama ya kufanya biahara hiyo, hivyo ni vyema wasio na taaluma hiyo kuacha kufanya biashara hizo mara moja na wafuate kanuni na taratibu za kupata mafunzo na kibali cha kufanya biashara hizo.


Share:

CUF kurejesha ofisi zake zote zilizochukuliwa na chama cha ACT Wazalendo

Chama cha Wananchi CUF kimesema kuwa kimeazimia kurejesha ofisi zake zote zilizochukuliwa na chama cha ACT Wazalendo hususan Visiwani Zanzibar.

Kauli hiyo imetolewa jana jijini Dar es Salaama na Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini wa chama hicho, Mussa Haji Kombo, ambaye alisema kuwa ofisi hizo ni mali ya CUF hivyo ni lazima wazirejeshe.

“Kwa kuwa baraza Kuu la Uongozi la Taifa la CUF limeazimia kurejesha ofisi  zake zilizoporwa na ACT kupitia kikao chake cha hivi karibuni sisi viongozi tutazirejesha na tupo tayari kwa lolote na wala hatuna hofu na vitisho vya Maalim Seif na wafuasi wake.
 
Katika hatua nyingine, Kombo alimtuhumu Maalim Seif kuwa ni mbaguzi na mwenye kupandikiza chuki miongoni mwa jamii ya watanzania.


Share:

Mkurugenzi wa Kampuni ya SKOL, Vicent Massawe Aaanguka na Kuzimia Baada ya Kubanwa na Waziri Jafo

Mkurugenzi wa Kampuni ya SKOL, Vicent Massawe ameishiwa nguvu na kuanguka ghafla baada ya Waziri Jafo kumpa siku 26 kukamilisha Mradi wa Barabara ya Swaswa, Dodoma kwa kiwango cha lami(KM1.8) na kuagiza akishindwa kukamilisha asipewe tena kazi Tamisemi.

Tukio hilo limetokea jana  Jumatano Desemba 4, 2019 baada ya Jafo  kutembelea ujenzi wa barabara hiyo yenye urefu wa kilomita nane iliyotakiwa kukamilika Agosti lakini ukaongezwa muda hadi Oktoba, 2019.

Kutokana na kuchelewa huko mkandarasi huyo  amekatwa Sh80 milioni na Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (Tarura).

Licha ya kujitetea kuwa wamejenga katika miradi mingi nchini ikiwemo katika jimbo la Kisarawe ambalo mbunge wake ni waziri huyo wa Tamisemi, waziri huyo alikataa na kubainisha kuwa uwezo wa kampuni hiyo ni mdogo.


Share:

Video : NG'WANA MALINGITA - BHASHABHIKI

Hii hapa video ya msanii Amos Ng'wana Malingita inaitwa Bhashabhiki.

Share:

Video Mpya : NGELELA - MOTO GWA MBELELE

Nakualika kutazama video ya Manju Ngelela inaitwa Moto Gwa Mbelele...Itazame hapa chini

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger