Monday, 18 November 2019

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatatu November 18



















Share:

Sunday, 17 November 2019

DAKTARI MATATANI KWA KUWAFUNGA VIZAZI WANAWAKE 126 BILA RIDHAA YAO

Daktari mmoja anatuhumiwa kwa kufanya upasuaji kwa wanawake na kutoa viungo bila ridhaa zao, mmoja wa wagonjwa wake amemtuhumu na kumfikisha mahakamani.

Amefikishwa katika mahakama huko Virginia nchini Marekani.

Dr Javaid Perwaiz dakatari bingwa wa kina mama, amewadanganya wanawake kuhusu afya zao na kuwasababishia majeraha makubwa, kwa mjibu wa shirika la upepelezi la marekani FBI.

Tangu kukamatwa kwake tarehe 8 novemba , zaidi ya wanawake 126 wameripoti na kulalamika kuhusu tabia zake.

Siku ya alhamisi , jaji wa mahakama alitoa amri ya kukamatwa kwa Dr Perwaiz wakati akisibiri hukumu yake.

Kwa mujibu wa hati ya kukamatwa ya FBI Dr.Perwaiz anatuhumiwa kutoa majibu ya uongo ya kiafya na kufanya upasuaji usio wa lazima kwa wagonjwa wake na bila ridhaa zao.

Amefanya upasuaji wa kutoa sehemu za uzazi za wanawake bila ridhaa zao pamoja na kufunga uzazi. Daktari huyo ana ofisi mbili eneo la Chesapeake, jimbo la Virginia nchini Marekani.

Kwa mujibu wa taarifa zilizofikishwa mahakamani, katika kipindi cha mwaka 2014-18 Dr Perwaiz amefanya upasuaji kwa asilimia 40 ya wanawake wanaopokea matibabu wakiwa na kipato cha chini.

Katika kundi la wagonjwa wanawake 510,asilimia 42 walifanyiwa angalau upasuaji wa aina mbili.

Shirika la upepelezi la FBI lilipewa taarifa kwa mara ya kwanza mwaka 2018 na muuguzi ambae alisikia kutoka kwa mgonjwa mmoja.

''Wagonjwa wanasema kuwa walikua wakisikia Dr Perwaiz akitaja sana kuhusu saratani na kuwatisha waweze kufanyiwa upasuaji'' anasema Afisa wa FBI Desiree Maxwell.Daktari huyu amekua akiwafunga vizazi wanawake bila ridhaa zao.

Wakili wa Dr Perwaiz hakujibu baada ya kutafutwa na BBC siku ya Alhamisi.

Dr Perwaiz amesoma masomo yake ya utabibu huko Pakistani na alipata leseni ya kufanya kazi Virginia Marekani mwaka 1980.

Mwaka 1982 alipoteza sifa zake za kufanya kazi katika hospitali huko Maryland kutokana na maamuzi mabaya ya kitabibu.

Kwa mujibu wa FBI alifanyiwa uchunguzi mara ya kwanza na bodi ya madaktari wa Virginia kwa kufanya upasuaji bila kuwa na maamuzi yasiyo na weledi wa kitaaluma.

Baada ya kukubali hatia ya kukwepa kodi 1996, alinyang'anywa leseni kwa miaka miwili.
Chanzo - BBC
Share:

Kampeni Ya Elimu Kwa Mlipakodi Yawafikia Wafanyabiashara Zaidi Ya 700 Morogoro

Na Veronica Kazimoto
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imewafikia na kuwaelimisha wafanyabiashara zaidi ya 700 kupitia kampeni ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi iliyofanyika mkoani Morogoro.

Lengo la kampeni hiyo ilikuwa ni kutoa elimu kuhusu masuala mbalimbali ya kodi pamoja na kusikiliza malalamiko, changamoto na maoni kutoka kwa wafanyabiashara hao.

Akizungumza mara baada ya kukamilika kwa kampeni hiyo mwishoni mwa wiki, Afisa Msimamizi wa Kodi Mkuu wa TRA, Julius Mjenga amesema kuwa, mamlaka hiyo ililenga kuwafikia wafanyabiasha 500 lakini kutokana na mwitikio mkubwa, TRA imefanikiwa kuvuka lengo hilo na kuwafikia zaidi ya 700.

“Wiki hii moja ya elimu kwa mlipakodi, tuliwalenga wafanyabiashara wa wilayani ambapo kumekuwa na changamoto ya kutokupata elimu ya kodi kwa wakati. Nashukuru tumefanikiwa kwa kiasi kikubwa kwa sababu tumeweza kuwaelimisha wafanyabiashara 774 katika kampeni hii”, alisema Mjenga.

Mjenga ameongeza kuwa “Tumefika karibu wilaya zote za mkoa huu wa Morogoro ambazo ni Malinyi, Ulanga, Kilosa, Mvomero, Kilombero na Gairo na kila mahali tulipopita tumepata mwitikio mkubwa kutoka kwa wafanyabiashara na wananchi mbalimbali.”

Kwa upande wa wafanyabiashara waliotembelewa na TRA, wameishukuru mamlaka hiyo kwa kuwaelimisha masuala mbalimbali yanayohusu kodi na kuomba elimu hiyo iwe endelevu.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, baadhi ya wafanyabiashara hao wamesema kuwa, TRA ya sasa sio ile ya zamani kwa sababu sasa hivi maafisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania wamekuwa karibu na walipakodi na siku hizi hawana tabia ya kufunga biashara zao.

“Zamani mtu alikuwa akisikia watu wa TRA wanakuja, anafunga duka anaondoka lakini siku hizi, TRA wamekuwa marafiki, wanatuelimisha na wala hawafungi biashara zetu, kwakweli tunashukuru sana,” alisema Eleonora Kisimba, mfanyabiashara wa duka la nguo wa wilayani Mvomero.

Naye Stanphord Mjumbe ambaye ni mfanyabiashara wa duka la vifaa vya ujenzi wilayani Gairo mkoani hapa alisema kuwa, kampeni ya elimu kwa mlipakodi ifanyike mara kwa mara kwa sababu wafanyabiashara walio wengi hususani wadogo hawajasoma hivyo wanahitaji kuelimishwa zaidi juu ya haki na wajibu wao katika ulipaji kodi.

“Sisi wafanyabiashara wadogo, tulio wengi hatujasoma hivyo tunahitaji elimu hii angalau kwa mwaka mara tatu ili tuweze kuelewa kwa kina haya mambo ya ulipaji kodi maana wakati mwingine tunakuwa hatujui haki zetu,” alisisitiza Mjumbe.

Aidha, wafanyabiashara hao wameiomba Mamlaka ya Mapato Tanzania kurejesha Kodi ya Zuio kwa wamiliki wa majengo kwa kuwa baadhi yao hawataki wapangaji kuzuia asimilia kumi na kuiwasilisha TRA.

Vilevile, wameomba kuelimishwa jinsi ya kulipa kodi ya mapato kwa awamu mara tu wanapokadiriwa kodi hususani kwa wafanyabiashara wapya kwani wengi wao wanapitiliza tarehe za kulipa kodi hiyo kwa kukosa uelewa.

Kampeni ya huduma na elimu kwa mlipakodi imemalizika tarehe 17 Novemba, 2019 na ilifanyika katika Mikoa ya Morogoro na Pwani ambapo wafanyabiashara wamepata fursa ya kutembelewa katika maduka yao na wengine walihudhuria semina kwa ajili ya kuelimishwa masuala mbalimbali yanayohusu kodi.

Mwisho.


Share:

Serikali yaamua kumfariji Binti ambae alifichwa kufariki kwa Wazazi Wake Wote na Ndugu Zake Watatu

Waziri wa Afya, Maendeleo Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu, ameeleza kuguswa na tukio la kupoteza wazazi wawili, na ndugu zake watatu lililomkuta mwanafunzi Anna Zambi ambaye amemaliza kidato cha 4 hivi karibuni ambapo Waziri Ummy ameahidi ataenda kumjulia hali mtoto huyo na kumpa salam za pole.

Ummy Mwalimu ametoa kauli hiyo kupitia ukurasa wake Twitter kufuatia jana mtoto huyo kupelekwa mahali ambapo wazazi wake na ndugu zake wamezikwa baada ya kufariki Dunia walipokuwa wakielekea kwenye Mahafali yake ambapo walifariki Dunia wakiwa mkoani Tanga kutokana na mafuriko ya maji.

Waziri Ummy ameandika kuwa; "Suala la mtoto Anna Zambi, Serikali kupitia Wizara ya Afya na Maendeleo ya Jamii tunachukua jukumu la kuratibu na kusimamia psychosocial support ya mtoto huyu pamoja na ustawi wake kwa ujumla, Katibu Mkuu Dkt. John Jingu leo ataitembelea familia yake iliyopo Goba” – Waziri Ummy

Wazazi walikuwa wakifahamika kwa majina ya Lingston Zambi na Winifrida Lyimo na wadogo zake watatu, Lulu, Andrew na Grace walikufa katika ajali hiyo baada ya gari walilokuwa wakisafiria kusombwa na maji kutokana na mvua kubwa iliyonyesha wilayani Handeni mkoani Tanga.


Share:

Wanajeshi wa China wasafisha mitaa ya Hong Kong Iliyokuwa Imefungwa na Waandamanaji

Wanajeshi wa China wametoka jana katika kambi zao mjini Hong Kong na kwenda mitaani kusaidia kuisafisha na kuondoa vifusi na vizuizi vilivyowachwa na waandamanaji.

Lilikuwa tukio lisilo la kawaida kwa Jeshi la China kuingia katika mitaa ya jimbo hilo lenye mamlaka ya ndani, ambalo kushindwa kwa serikali yake kumaliza maandamano yaliyodumu kwa zaidi ya miezi mitano kumezusha uvumi kuwa China huenda ikawatumia wanajeshi wake kisiwani humo.

Serikali ya Hong Kong imesema haikuomba msaada wa jeshi katika shughuli ya usafishaji, ikiielezea kuwa shughuli ya kujitolea ya kijamii. Wengi wa waandamanaji wanaoipinga serikali waliondoka kwenye vyuo vikuu vya Hong Kong baada ya kuvidhibiti kwa karibu wiki moja.


Share:

TIGO YAZINDUA DUKA JIPYA KIGOMA MJINI



Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Ziwa, Uthmaan Madati akizungumza mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali Mstaafu, Emmanuel Maganga wakati wa uzinduzi wa Duka la Tigo ‘Tigo Shop’ mkoani Kigoma.
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali Mstaafu, Emmanuel Maganga akizungumza na wakazi wa Kigoma pamoja na wafanyakazi wa Kampuni ya Tigo wakati wa uzinduzi wa duka la Tigo Mkoani Kigoma, Kulia ni Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Ziwa, Uthmaan Madati. 
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali Mstaafu, Emmanuel Maganga akikata utepe wakati wa uzinduzi wa duka jipya la Tigo ‘Tigo Shop’ mkoani Kigoma. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Ziwa, Uthmaan Madati.
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali Mstaafu, Emmanuel Maganga akihakiki utendaji kazi wa mfumo wa kusajili namba za simu kwa alama za vidole katika duka jipya la Tigo lililopo eneo la Lubengela Mkoani Kigoma jana mara baada ya kuzindua duka hilo.Kulia ni Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Ziwa, Uthmaan Madati. 
 ****

Kigoma. Novemba 16, 2019. Wateja wa Tigo Mkoani Kigoma wataweza kupata huduma zilizoboreshwa zaidi katika duka jipya ‘Tigo Shop’ lililozinduliwa leo mkoani humo.

Duka hilo jipya litakuwa sehemu maalumu kwaajili ya wateja kujionea na kufanya majaribio ya bidhaa na huduma mbalimbali mpya na za kidigitali kama Tigo Pesa zitolewazo na kampuni hiyo.

Wateja pia wataweza kupata huduma ya kusajili upya namba za simu kwa mfumo wa alama za vidole.

Akizungumza wakati wa  hafla ya uzinduzi, Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Ziwa, Uthmaan Madati alisema “Ufunguzi wa duka hili ni utekelezaji wa mkakati wa Tigo wa kufikisha huduma karibu na wateja na tunaamini kuwa duka hili litatoa fursa za biashara kwa wateja na kuchochea ukuaji wa uchumi mkoani hapa,” alisema Karembo.

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali mstaafu Emmanuel Maganga aliipongeza Tigo kwa 
Kwa jitihada zake za kuhakikisha wateja wanapata huduma zenye viwango vya kimataifa maeneo yote ya nchi.

“Duka hili jipya litakuwa chachu katika uboreshaji wa huduma za mawasiliano hapa mkoani Kigoma.Mkoa huu una wakazi wachapa kazi na wafanyabiashara ambao wanatamani kujikwamua kiuchumi hivyo hii ni fursa muhimu kwao,” alisema.

Aliongeza “Hii ni faraja kuona kwamba sasa huduma za Tigo zitapatikana kwa urahisi zaidi na hii itasaidia kufungua fursa nyingi za kiuchumi.”

Duka hilo linalopatikana katika mtaa wa Lubengela Kigoma Mjini, ni la kwanza mkoani humo na litakuwa likitoa huduma sambamba na dawati la wateja lililopo Wilayani Kasulu.

 “Duka hili limewekwa katika eneo hili kimkakati ili kufikika kwa urahisi kwa wakazi wa Kigoma na maeneo jirani na mipakani,” alisema Madati.

Duka hilo linaifanya Tigo kuongeza kasi ya usambazaji wa huduma zake maeneo mbalimbali ya nchi ili kufikia wateja wake zaidi ya 11.6 milioni jambo linalofungua milango kwa wateja kufurahia huduma za kidigitali zinazotolewa na kampuni hiyo.
Mwisho//








Share:

Bodi Ya Rea Yampa Siku 14 Mkandarasi Wa Umeme Mkoani Simiyu Kujirekebisha

Na Teresia Mhagama, Simiyu
Bodi ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) imempa siku 14 mkandarasi wa umeme vijijini mkoani Simiyu kuongeza kasi ya usambazaji umeme katika vijiji alivyopangiwa la sivyo Bodi hiyo haitasita kuchukua hatua mbalimbali za kimkataba ikiwemo ya kusitisha mkataba.

Mwenyekiti wa Bodi ya REA, Wakili Julius Kalolo  alisema hayo tarehe 16 Novemba, 2019 wilayani Busega mkoani Simiyu mara baada ya kukagua kazi ya usambazaji umeme katika Vijiji mbalimbali vya wilaya ya Bariadi na Busega akiwa amembatana na Mjumbe wa Bodi hiyo, Dkt Andrew Komba na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mhandisi Amos Maganga.

” Bodi haijaridhishwa na kasi ya mkandarasi huyu kwani amepewa kazi ya kupeleka umeme katika vijiji 152 vya Mkoa wa Simiyu lakini mpaka sasa amesambaza katika vijiji 54 ambayo ni takribani asilimia 30 tu ya kazi anayopaswa kufanya hivyo tumempa siku 14 aonyeshe mabadiliko la sivyo tutachukua hatua.” Alisema

Wakili Kalolo alieleza kuwa, Serikali imetimiza jukumu la kutoa malipo kwa mkandarasi huyo ili kazi ya usambazaji umeme ifanyike kwa kasi hivyo visingizio vya ucheleweshaji wa kazi havikubaliki kwani kwa mujibu wa mkataba wa mkandarasi huyo anapaswa kumaliza kazi mwezi Aprili mwaka 2020.

Aidha, alimwagiza mkandarasi huyo kampuni ya Whitecity Guangdong JV, kuwasilisha mpango kazi wake kwa Bodi hiyo, Mameneja wa TANESCO mkoani Simiyu pamoja Ofisi ya Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu ili kuweza kufuatilia kwa karibu utekelezaji wa kazi anazofanya.

Awali Bodi hiyo ilikutana na Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Jumanne Sagini ambapo, Mjumbe wa Bodi ya REA, Dkt. Andrew Komba alitoa shukrani kwa viongozi wa mkoa wa Simiyu kwa kufuatilia utekelezaji wa kazi ya usambazaji umeme vijijini.

Aidha, aliomba kasi hiyo iongezeke ili Mradi wa usambazaji umeme vijijini wa Awamu ya Tatu, Mzunguko wa Kwanza (REA III) ukamilike kwa wakati.

Alisema kuwa, msukumo wa kuwafuatilia wakandarasi unahitajika ili kutimiza lengo la Serikali  la kupeleka umeme katika vijiji vyote vilivyopo katika mpango  wa REA III mzunguko wa kwanza ifikapo mwezi Disemba mwaka huu.

Aidha alitoa wito kwa viongozi wa Serikali katika  ngazi mbalimbali za mkoa, kuhamasisha wananchi kujiunga na huduma ya umeme kwani Serikali imefanya uwekezaji mkubwa katika kuwasambazia umeme wananchi hivyo wanapaswa kuunganisha umeme kwa wingi na kuutumia katika shughuli za kiuchumi na kijamii


Share:

Biteko Ang’aka Kuhusu Mishahara ya Watanzania Migodini Na Issa Mtuwa – Geita

Waziri wa Madini Doto Biteko pamoja na kuupongeza uongozi wa mgodi wa dhahabu wa Geita “GGM” katika  mambo mengi leo tarehe 16/11/2019 alikuwa “mbogo” kwa uongozi huo kuhusu suala la mishahara wanayolipwa Watanzania ambapo amebaini kutokuwepo kwa usawa. 
 
Biteko amesema anaumizwa sana na jambo la malipo ya mishahara kati ya Watanzania na wageni licha ya kulingana kwa sifa, ujuzi na elimu na wakati mwingine mtazania anasifa zaidi kuliko mgeni lakini bado mtanzania analipwa chini kuliko yule mgeni.  

Kutokana na hali hiyo, Biteko ameuagiza uongozi wa GGM kuwasilisha orodha ya malipo ya mishahara ya wafanyakazi wote (Payroll) kwa Kamishna wa Madini Mhandisi David Mulabwa wiki ijayo. Biteko alianza kuhoji idadi ya idara zilizopo na zinaongozwa na akina nani huku akiuliza kuna watu wangapi wa kigeni katika idara hizo na majukumu yako.  

“Sheria ya madini hasa sheria ya Local content inatoa muongozo ni namna gani na wakati gani mgodi unaweza kumuajiri mtaalamu wa fani fulani kutoka nje endapo hakuna mtanzania wa kuweza kushika wadhifa huo” amesema Biteko.  

Ameongea hayo wakati akiongea na uongozi wa mgodi wa GGM mkoani geita alipotembelea mgodini hapo kwa ziara maalum ya kikazi kwa lengo la kufuatilia na kukagua uendeshaji wa shughuli za mgodi huo, ufuatilia na kuangalia utekelezaji wa malalamiko ya wananchi na malipo ya ushuru wa Halmashauri (Service Levy) ambapo mgodi huo unawajibika katika malipo hayo. 

Aidha, Biteko amekwenda kujiridhishi katika masuala mbalimbali ambayo kamati maalumu aliyoiunda kwenda mgodini hapo kwa ajili ya kuangalia na kukagua ili ajiridhishe kabla ya kutoa idhini ya kuruhusu mgodi huo kuanza uchimbaji wa chini kwa chini (Underground) kufuatia maombi ya mgodi huo kwa waziri. 

Kwa mujibu wa kifungu cha 40 cha marekebisho ya sheria ya madini ya mwaka 2017  hairuhusu uchimbaji wa chini kwa chini kwa mwekezaji au mgodi mpaka apate idhini (Kibali) ya waziri mwenye dhamana ya Madini ambapo Waziri alianisha mambo mengi ya kuzingatiwa na mgodi kabla hawajaruhusiwa. 

Biteko ameendelea kusisitiza kauli yake ya mara kwa mara kuwa raslimali hizi ziwe neema kwa wananchi na sio mateso. Kauli hiyo ameitoa kufuatia malalamiko ya wananchi wapatao 350 ambao makazi yao yalipitiwa na tetemeko wakati wa milipuko mbalimbali mgodini hapo wakati wa ulipuaji wa miamba. 

Ameongeza kuwa hadi kufikia mwisho mwaka huu ukurasa wa suala la malipo ya fidia ya suala hili liwe limefungwa na kwamba wenye malalamiko wote wapeleke kwa Mkuu wa Wilaya Geita kuanzia tarehe 18-23/11/2019. 

Kwa upande wa uongozi wa mgodi ukiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Mgodi Richard  Jordanson na Makamu Mkurugenzi Mtendaji Simon Shayo kwa nyakati tofauti wametoa shukrani kwa ujio wa Waziri kwenye mgodi wao ikiwa ni mara yake ya kwanza kutembelea tangu alipoteuliwa kuwa Waziri wa Madini.  

Wameongeza kuwa mgodi wao upo mstari wa mbele kutekeleza maagizo ya serikali na kwamba wanapenda kuwa msistari mbele na wawe wa kwanza katika kuchangia sehemu kubwa itakayo changia pato (GDP) la taifa kwa upande wa madini. 

Shayo amemwambia waziri kuwa mambo mengi aliyoyasema Waziri kama vile; mpango wa ufukiaji mashimo baada ya mgodi kufungwa, ulipaji wa ushuru wa Halmashauri za wilaya (Service levy), mchakato wa ulipaji wa fidia ya wananchi na utekelezaji wa sheria ya local content vinatekelezwa baadhi vimeshakamilishwa na baadhi vipo kwenye taratibu za kukamishwa.  

Akiwa kwenye mgodi wa RZ unaomilikiwa na mwekezaji kutoka china anae fahamika kwa jina la “Lyuu” amemtaka mwekezaji huyo kwa kufanya kazi zake kwa kuzingatia sheria zote zikiwemo za madini, kazi na utoaji wa mikataba ya ajira na makato ya NSSF kwa wafanyakazi wake na kuiwasilisha kwa mamlaka husika.  

“Lyuu” amesema ameshukuru waziri kutembelea mgodi kwake na amepokea maelekezo ambayo ameyakubali na kuahidi kuyatekeleza. Wakati wakati huo huo wafanayakazi walipo mgodini hapo amewataka kuwa waaminifu na kuepuka vitendo vihovu kwa mwekezaji. 


Share:

WAZIRI MPINA AZINDUA AGENDA ZA UTAFITI NA KUIBUA TAFITI ZILIZOFICHWA MAKABATINI

 Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Agenda ya Kitaifa za Utafiti wa Mifugo, Uvuvi na Ukuzaji wa Viumbe Maji ya mwaka 2020-2025 katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA mjini Morogoro wengine wanaoshuhudia ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Loata Ole Sanare, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdalah Ulega na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu SUA, Profesa Raphael Chibunda. Picha na Mpiga Picha Wetu
 Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina akimkabidhi Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Wavuvi Wadogo Dar es Salaam, Feisal Mohamed Ally Agenda ya Kitaifa za Utafiti wa Mifugo, Uvuvi na Ukuzaji wa Viumbe Maji ya mwaka 2020-2025 baada ya kuizindua katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA mjini Morogoro. Wengine Katikati ni Katibu Mkuu Mifugo, Prof. Elisante Ole Gabriel na Katibu Mkuu Uvuvi, Dk. Rashid Tamatamah Picha na Mpiga Picha Wetu
 Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina akionesha kitabu cha Agenda ya Kitaifa ya Utafiti wa Mifugo muda mfupi baada ya uzinduzi wa Agenda ya Kitaifa za Utafiti wa Mifugo, Uvuvi na Ukuzaji wa Viumbe Maji ya mwaka 2020-2025 katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA mjini Morogoro wengine wanaoshuhudia ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Loata Ole Sanare, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdalah Ulega na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu SUA, Profesa Raphael Chibunda. Picha na Mpiga Picha Wetu.

 Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina akimkabidhi Mdau wa Ufugaji Samaki kwenye Vizimba –Ziwa Victoria, Said Mecky Sadiq Agenda ya Kitaifa za Utafiti wa Mifugo, Uvuvi na Ukuzaji wa Viumbe Maji ya mwaka 2020-2025 baada kuizindua katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA, Mjini Morogoro. Katikati ni Katibu Mkuu Mifugo, Prof. Elisante Ole Gabriel. Picha na Mpiga Picha
 Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Loata Ole Sanare Agenda ya Kitaifa za Utafiti wa Mifugo, Uvuvi na Ukuzaji wa Viumbe Maji ya mwaka 2020-2025 baada kuizindua katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA, Mjini Morogoro. Wengine ni Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdalah Ulega na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu SUA, Profesa Raphael Chibunda. Picha na Mpiga Picha Wetu.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina akiwa katika picha ya pamoja na Wafugaji na Wadau wa Ufugaji wa Samaki kwenye Mabwawa kutoka Jimbo la Kisesa Wilaya ya Meatu Mkoa wa Simiyu huku wakionesha kitabu cha Agenda ya Kitaifa za Utafiti wa Mifugo, Uvuvi na Ukuzaji wa Viumbe Maji ya mwaka 2020-2025 baada kuzinduliwa katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA, Mjini Morogoro

Na Mwandishi Wetu, Morogoro

WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina amezindua Agenda ya Kitaifa ya Utafiti wa Mifugo, Uvuvi na Ukuzaji wa Viumbe Maji ya mwaka 2020-2025 na kutangaza kuzifumua na kuziibua tafiti zote  zilizofanywa na wasomi na kutelekezwa kwenye makabati miaka ya nyuma na kuziingiza kwenye mfumo rasmi wa matumizi ili kuleta mageuzi makubwa ya kiuchumi na maendeleo.

Pia agenda hizo zitaleta msisimko mpya wa kufanya utafiti nchini na kuleta mageuzi makubwa ya kiuchumi na maendeleo tofauti na ilivyokuwa kipindi cha nyuma ambapo tafiti nyingi zilifanywa na kutelekezwa kwenye makabati na watafiti mbalimbali wakiwemo Wanafunzi wa Shahada ya Uzamili (Masters Degree)  na Shahada ya Uzamivu (PHD) katika vyuo vikuu mbalimbali.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa agenda hizo kitaifa katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA),  Kampasi ya Mazimbu mjini Morogoro, Waziri Mpina aliziagiza Taasisi ya Utafiti wa Mifugo(TALIRI) na Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi(TAFIRI) kubadilika ili kufanya tafiti kwa vigezo vilivyowekwa na kuleta mabadiliko chanya katika sekta za mifugo na uvuvi nchini.

Waziri Mpina alisema chimbuko la kuandaliwa kwa ajenda hizo za utafiti ni baada ya kubaini kuwa ajenda zilizokuwepo awali za Mifugo na Uvuvi zilishindwa kuibua na kuzitumia tafiti zilizofanywa kuchochea mabadiliko kwenye sekta hiyo muhimu ya uzalishaji.

Pia ajenda za utafiti zilizokuwepo za Mifugo na Uvuvi hazikuwa na utaratibu wa kuzitambua, kuziorodhesha na kuzitumia tafiti zinazofanywa na Wanafunzi wa Shahada ya Uzamili (Masters Degree) na Uzamivu (PHD) lakini sasa ajenda za utafiti zilizozinduliwa zimeweka utaratibu wa namna ya kuzitambua, kuziorodhesha na kuzitumia tafiti za wasomi hao.

“Haiwezekani tafiti za wasomi wa kiwango cha juu kiasi hicho wanazozifanya wakati wa kukamilisha masomo yao ziishie kupata alama za ufaulu na kutupwa kwenye makabati, Leo kila mhitimu atalazimika kuandaa policy brief ambayo itawezesha watumiaji na Serikali kurekebisha au kuandaa Sera na Sheria” alisema Waziri Mpina.

Aliongeza kuwa Ajenda za Utafiti zilizokuwepo za Mifugo na Uvuvi hazikuwa na utaratibu wa kuweka Kanuni ambazo zitahakikisha kuwa utekelezaji  wa ajenda za utafiti unafanyika, lakini ajenda za utafiti iliyotangazwa inaweka Kanuni zitakazotoa mwongozo na usimamizi wa utekelezaji na wajibu wa kila mhusika.

Aidha Waziri Mpina alibainisha kuwa ajenda za utafiti zilizokuwepo za Mifugo na Uvuvi hazikuwa na utaratibu wa kuwaunganisha Watafiti wa Mifugo na Uvuvi nchini, na hivyo kupelekea kila mmoja kufanya utafiti kivyake hali iliyosababisha jambo moja kufanyiwa utafiti na mtafiti zaidi ya mmoja na kukosa jukwaa la kuratibu na kuchambua tafiti zinazofanywa nchini.

“Agenda ninayoizindua leo inakwenda kujumuisha watafiti na wataalam mbalimbali waliobobea katika fani za mifugo, uvuvi na ukuzaji wa viumbe maji ili kuyapitia matokeo ya utafiti, teknolojia zilizoibuliwa na utafiti na kuzisambaza kwa watumiaji kwa manufaa ya Taifa” alisema Waziri Mpina

Pia Waziri Mpina alibainisha mapungufu mengine yaliyomo kwenye ajenda za utafiti zilizokuwepo za Mifugo na Uvuvi ni pamoja na kutoweka msingi mzuri wa kusimamia Watafiti na kufanya tafiti kulingana na mahitaji ya soko badala yake  Taasisi za Utafiti na Watafiti kufanya tafiti nyingi za nje na mambo muhimu ya wananchi yanayohitaji kufanyiwa utafiti kutelekezwa.

“Leo hii agenda ninazozizindua zimeweka utaratibu wa kuzingatia vipaumbele vya kitaifa, kupanua mtandao wa utafiti  na kufanya tafiti zote kulingana na mahitaji ya wananchi.  Mfano katika maeneo ya nyama, maziwa, samaki, ngozi, chakula cha samaki na mifugo, magonjwa, malisho na migogoro” alisema Mpina.

Aidha dosari nyingine zilizokuwepo kwenye ajenda za utafiti zilizokuwepo za Mifugo na Uvuvi ni kutojumuisha katika vipaumbele masuala mengi muhimu yenye changamoto nyingi ikiwemo  Mitaala na hali ya ajira.

Mpina alisema mitaala inapoanzishwa haifanyiwi utafiti wa mara kwa mara matokeo yake mafunzo yanayotolewa sio yale yanayohitajika katika soko la ajira huku Wanafunzi wanaohitimu mafunzo hawajulikani wanakwenda wapi baada ya kuhitimu na hakuna mfumo wowote wa uratibu.

“Ukienda kwa wafugaji wanaofuga na kuchunga sio hao waliosomea mifugo, ukienda kwa Wavuvi na Ukuzaji viumbe maji wanaovua na kufuga si hao waliosomea taaluma hizo, ukienda viwandani vilevile”alisema Mpina.

Pia Masoko na Biashara, Uongezaji wa mnyororo wa thamani wa mazao ya mifugo na uvuvi (Livestock & Fisheries value chain & value addition), agenda iliyopita ilizingatia uzalishaji pekee bila kuangalia upande wa soko wakati vitu hivi vinakwenda kwa pamoja kwani hakuna uzalishaji bila soko.

Waziri Mpina pia alisema licha ya kushamiri kwa migogoro ya wafugaji na watumiaji wengine wa ardhi na eneo hilo kugubikwa na changamoto nyingi  ikiwemo  mifugo kutaifishwa, kupigwa risasi, kufilisiwa, kuuwawa kwa watu na mifugo  na kupigwa faini kubwa kiasi cha kutishia uendelevu wa sekta lakini eneo hili halikujumuishwa katika Agenda ya utafiti iliyopita.

Pia masuala mtambuka, afya ya wanyama na magonjwa ya afya ya jamii (Zoonotic Diseases) ambapo hivi sasa asilimia 60 ya magonjwa yasiyoambukiza yanatokana na mazao ya mifugo, malisho, nyanda za malisho na vyakula vya mifugo na samaki, uvuvi endelevu katika maji ya asili (Uvuvi Haramu na utoroshaji wa mazao ya uvuvi)  ambayo nayo hayakuzingatiwa katika agenda za utafiti zilizopita .

Hivyo Waziri Mpina aliwahakikishia watanzania kuwa Wizara yake itaendelea kushirikiana na wadau wote kuhakikisha kuwa matokeo ya tafiti zinazofanywa zinawafikia walengwa kwa wakati ili tafiti hizo ziongeze tija na kipato kwa watuamiaji na Taifa kwa ujumla. 
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), Profesa Raphael Chibunda alimhakikishia Waziri Mpina kuwa kwa niaba ya watafiti wa Chuo kikuu hicho watatakwenda kuwa sehemu ya utekelezaji wa agenda hizo.
Share:

RAIS MHE. DKT. MAGUFULI NA MKEWE JANETH MAGUFULI WAMESHIRIKI MISA TAKATIFU DOMINIKA YA 33 MWAKA “C” KATIKA KANISA KATOLIKI LA MTAKATIFU PETRO PAROKIA YA OYSTERBAY JIJINI DAR ES SALAAM. NOVEMBA 17, 2019

Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumapili November 17




Share:

NIDA Yasema Apps Za Kitambulisho Cha Taifa Zinazosambaa Mitandaoni Ni Batili




Share:

Saturday, 16 November 2019

GANGWE MPYA KWENYE GAME??




Ukiona mtu anaweza kufanya jambo lake bila uoga wa kuona wale wabishi na wakubwa zaidi yake kwenye hilo jambo nao wanafanya kwa wakati huo ni lazima ikupe maswali kidogo juu yake..Ndivyo ambavyo msanii anayekuja kwa kasi anavyowapa watu mshtuko na maswali  baada ya kuachia ngoma yake inayokwenda kwa jina la BWEKA inapatikana hapa 

 jumatano ya wiki hii huku vyuma kama Diamond Platnumz,Harmonize na Ali Kiba nao wakiwa wametoa ngoma zao zinazozidi kushika chati kila siku.SALHA ambaye mbali na kuwa bado mchanga kwenye sanaa ya muziki ameonyesha kutokuogopeshwa na uwepo wa kazi za wasanii wakubwa  sokoni kwa kuachilia nyundo yake kali ambayo kwa jinsi inavyozidi kupokelewa vizuri na wasikilizaji pamoja na vituo mbalimbali inatufanya tujiulize, je huyu ni gangwe mpya wa  muziki wa Tanzania??Haikuishia hapo ambapo wasanii wakubwa pia kama Benpol wameonyesha wazi kuikubali BWEKA kwa kuitupia katika mtandao wake wa kijamii wa Instagram muda mchache tu baada ya kuiachilia..Kwa haraka picha anayotupa ni ya ujasiri mkubwa katika sanaa yake licha ya kuwa binti mdogo wa miaka 19 tu..BWEKA ambayo imepikwa kwa mtayarishaji Aloneym  ni kati ya mishale ambayo mwanadada huyu mwenye sauti ya kipekee ameanza kuirusha akiwa chini ya menejimenti yake ya The Collective Live.Salha ambaye pia yupo kwenye maandalizi ya kuachia video ya ngoma hii hivi karibuni,anaweka wazi kuwa BWEKA ni moja tu kati ya ngoma zake kali ambao unapatikana sasa YouTube na anaamini watanzania wataupokea kwa mikono miwili na utawakonga nyoyo sana huku maandalizi ya video na mambo mengine ya kimuziki akiyatupia katika page yake ya instagram inayokwenda kwa jina la Salhaofficialtz 

https://instagram.com/salhaofficialtz Ninachoweza kusema tu kwasasa ni kuwa tasnia ya muziki imeongeza mwanajeshi mkali sana wa kike ambaye huko mbeleni tunamtabiria mambo makubwa sana..Kazi ni kwetu kuzidi kufuatilia kazi zake na kuona balaa lake.





Share:

Wanafunzi Wachomana Visu Kisa Kumwagiana Maji Machafu Siku Ya Birthday

Mwanafunzi wa mwaka wa tatu katika Chuo cha Ufundi Trade Peramiho wilayani Songea, Grayson Maselin (23), amejeruhiwa na mwanafunzi mwenzake Mosses Ngole (23), kwa kuchomwa kisu shingoni baada ya kummwagia maji machafu siku ya kumbukizi ya kuzaliwa kwake (birthday).

Ngole, mwanafunzi wa mwaka wa nne katika chuo hicho, anadaiwa kumchoma kisu shingoni mwanafunzi mwenzake huyo na kumsababishia jeraha na kuvuja damu nyingi kwenye sherehe hiyo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Simon Maigwa, alidai tukio hilo lilitokea Jumatano majira ya saa saba mchana katika chuo hicho.

Alidai kuwa, siku ya tukio, Ngole alikuwa analazimishwa kumwagiwa maji na kupakwa matope na wanafunzi wenzake ndipo alipopandisha hasira na kufikia uamuzi wa kumchoma kisu mwanafunzi mwenzake huyo.

Kamanda Maigwa alidai mtuhumiwa anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kumjeruhi mwanafunzi mwenzake, ambaye kwa sasa amelazwa Hospitali ya Kanisa Peramiho.


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger