Ukiona mtu anaweza kufanya jambo lake bila uoga wa kuona wale wabishi na wakubwa zaidi yake kwenye hilo jambo nao wanafanya kwa wakati huo ni lazima ikupe maswali kidogo juu yake..Ndivyo ambavyo msanii anayekuja kwa kasi anavyowapa watu mshtuko na maswali baada ya kuachia ngoma yake inayokwenda kwa jina la BWEKA inapatikana hapa
jumatano ya wiki hii huku vyuma kama Diamond Platnumz,Harmonize na Ali Kiba nao wakiwa wametoa ngoma zao zinazozidi kushika chati kila siku.SALHA ambaye mbali na kuwa bado mchanga kwenye sanaa ya muziki ameonyesha kutokuogopeshwa na uwepo wa kazi za wasanii wakubwa sokoni kwa kuachilia nyundo yake kali ambayo kwa jinsi inavyozidi kupokelewa vizuri na wasikilizaji pamoja na vituo mbalimbali inatufanya tujiulize, je huyu ni gangwe mpya wa muziki wa Tanzania??Haikuishia hapo ambapo wasanii wakubwa pia kama Benpol wameonyesha wazi kuikubali BWEKA kwa kuitupia katika mtandao wake wa kijamii wa Instagram muda mchache tu baada ya kuiachilia..Kwa haraka picha anayotupa ni ya ujasiri mkubwa katika sanaa yake licha ya kuwa binti mdogo wa miaka 19 tu..BWEKA ambayo imepikwa kwa mtayarishaji Aloneym ni kati ya mishale ambayo mwanadada huyu mwenye sauti ya kipekee ameanza kuirusha akiwa chini ya menejimenti yake ya The Collective Live.Salha ambaye pia yupo kwenye maandalizi ya kuachia video ya ngoma hii hivi karibuni,anaweka wazi kuwa BWEKA ni moja tu kati ya ngoma zake kali ambao unapatikana sasa YouTube na anaamini watanzania wataupokea kwa mikono miwili na utawakonga nyoyo sana huku maandalizi ya video na mambo mengine ya kimuziki akiyatupia katika page yake ya instagram inayokwenda kwa jina la Salhaofficialtz
https://instagram.com/ salhaofficialtz Ninachoweza kusema tu kwasasa ni kuwa tasnia ya muziki imeongeza mwanajeshi mkali sana wa kike ambaye huko mbeleni tunamtabiria mambo makubwa sana..Kazi ni kwetu kuzidi kufuatilia kazi zake na kuona balaa lake.
Song link: https://youtu.be/ZI8XdkybUEA
Instagram: https://instagram.com/ salhaofficialtz
0 comments:
Post a Comment