Saturday, 16 November 2019

Wanafunzi Wachomana Visu Kisa Kumwagiana Maji Machafu Siku Ya Birthday

...
Mwanafunzi wa mwaka wa tatu katika Chuo cha Ufundi Trade Peramiho wilayani Songea, Grayson Maselin (23), amejeruhiwa na mwanafunzi mwenzake Mosses Ngole (23), kwa kuchomwa kisu shingoni baada ya kummwagia maji machafu siku ya kumbukizi ya kuzaliwa kwake (birthday).

Ngole, mwanafunzi wa mwaka wa nne katika chuo hicho, anadaiwa kumchoma kisu shingoni mwanafunzi mwenzake huyo na kumsababishia jeraha na kuvuja damu nyingi kwenye sherehe hiyo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Simon Maigwa, alidai tukio hilo lilitokea Jumatano majira ya saa saba mchana katika chuo hicho.

Alidai kuwa, siku ya tukio, Ngole alikuwa analazimishwa kumwagiwa maji na kupakwa matope na wanafunzi wenzake ndipo alipopandisha hasira na kufikia uamuzi wa kumchoma kisu mwanafunzi mwenzake huyo.

Kamanda Maigwa alidai mtuhumiwa anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kumjeruhi mwanafunzi mwenzake, ambaye kwa sasa amelazwa Hospitali ya Kanisa Peramiho.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger