Sunday, 17 November 2019

Serikali yaamua kumfariji Binti ambae alifichwa kufariki kwa Wazazi Wake Wote na Ndugu Zake Watatu

...
Waziri wa Afya, Maendeleo Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu, ameeleza kuguswa na tukio la kupoteza wazazi wawili, na ndugu zake watatu lililomkuta mwanafunzi Anna Zambi ambaye amemaliza kidato cha 4 hivi karibuni ambapo Waziri Ummy ameahidi ataenda kumjulia hali mtoto huyo na kumpa salam za pole.

Ummy Mwalimu ametoa kauli hiyo kupitia ukurasa wake Twitter kufuatia jana mtoto huyo kupelekwa mahali ambapo wazazi wake na ndugu zake wamezikwa baada ya kufariki Dunia walipokuwa wakielekea kwenye Mahafali yake ambapo walifariki Dunia wakiwa mkoani Tanga kutokana na mafuriko ya maji.

Waziri Ummy ameandika kuwa; "Suala la mtoto Anna Zambi, Serikali kupitia Wizara ya Afya na Maendeleo ya Jamii tunachukua jukumu la kuratibu na kusimamia psychosocial support ya mtoto huyu pamoja na ustawi wake kwa ujumla, Katibu Mkuu Dkt. John Jingu leo ataitembelea familia yake iliyopo Goba” – Waziri Ummy

Wazazi walikuwa wakifahamika kwa majina ya Lingston Zambi na Winifrida Lyimo na wadogo zake watatu, Lulu, Andrew na Grace walikufa katika ajali hiyo baada ya gari walilokuwa wakisafiria kusombwa na maji kutokana na mvua kubwa iliyonyesha wilayani Handeni mkoani Tanga.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger