Saturday, 2 November 2019

Lugola: Siku za mtu anayejiita Kigogo kwenye mitandao ya kijamii zinahesabika

Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola, amesema kuwa hivi karibuni Jeshi la Polisi litamtia nguvuni mtu anayejiita kigogo kupitia ukurasa wa Twitter.

Ametoa kauli hiyo leo Novemba 2, 2019 katika mkutano na wanahabari wakati akitoa tathimini ya hali ya usalama hapa nchini kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, ambapo amesema kuwa muda si mrefu polisi watamtia nguvuni mtu huyo.

"Kalenda inazo tarehe, utahesabu mwezi mfupi na mrefu, nataka niwaambie kwa kifupi siku za huyo Kigogo zinahesabika na hana siku nyingi", amesema Waziri Lugola.

Aidha katika hatua nyingine, Waziri Lugola ametoa wito kwa wananchi kuendelea kuwa na utulivu na amani na kutoa onyo kwa yeyote atakayekuwa na mpango wa kuvuruga uchaguzi ama kampeni basi atatumbukizwa kwenye gari lenye maji ya kuwashawasha.

''Niwaonye wanasiasa, siasa za majitaka na lugha ya matusi zinazoudhi wengine, Jeshi la Polisi limejipanga vizuri ikiwa ni pamoja na kuwashusha kwenye majukwaa ili wasiendelee kumwaga sumu inayohatarisha amani kwa wananchi", amesema.

"Ole wake yule mwenye mpango wa kuvuruga kampeni au uchaguzi tutamshughulikia, tuna magari ya washawasha, wakorofi na watakaoleta fujo watawashwawashwa kweli, hatutawamwagia tu bali wakorofi kabisa tutawatumbukiza na kuwakogesha kwenye hayo maji yanayowashawasha'', ameongeza Kangi Lugola.


Share:

Diamond Platnumz Amjibu Ali Kiba

Diamond Platnumz amezungumzia kilichoandikwa na msanii mwenzake, Ali Kiba katika mtandao wake wa  kijamii wa Instagram saa chache baada ya  kumualika kushiriki tamasha la Wasafi litakalofanyika Novemba 9, 2019.

Akizungumza jana Ijumaa Novemba Mosi, 2019 katika televisheni ya Wasafi ,Diamond alisema hakujua Ali Kiba alilenga nini, akibainisha kuwa hawezi kuwa na chuki naye.


“Alikiba ni kaka yangu, amenizidi umri na alianza muziki kabla yangu. Sijui aliandika vile akimaanisha nini, yeye na mimi ni miongoni mwa tunaoiletea sifa nchi kupitia muziki, upinzani wetu ni kwenye muziki tu, simchukii na nina imani naye pia hanichukii.

“Mimi nimetokea maisha ya chini sana ila Mwenyezi Mungu amenibariki ndio maana niliwashika mkono watu wengine ikiwemo Harmonize, tamanio la WASAFI ni kuona vijana tunapeana support na kumuunga mkono kwenye vitu ambavyo anavifanya.

“Mtu anavyofanikiwa na kuanza kushika mkono vijana wengine ni jambo zuri, furaha yangu ni kuona vijana wengi wa Tanzania wenye talent wanafanikiwa, pengine na mimi nisingemshika mkono, watu wasingeona kipaji chake.

”Nimefanya kazi nyingi za Kushikiana na wasanii, nina collabo nyingi ndani hadi natamani nizitaje, nina ngoma inakuja na Swaelee, kuna nyingine nimefanya na Steff London.

“Wasafi Festival itaanza mapema na kutakuwa na mashindano ya kuimba, Mshindi atapata Tsh. Millioni 10 na nafasi ya kusainiwa WCB Wasafi, kutakuwa na mashindano ya Dancers ambapo washindi pia watapata zawadi ya Tsh. Million 10 na nafasi ya kufanya kazi na wasanii wa WCB.

“Juzi tu hapa nilishinda Tuzo ya Mtumbuizaji bora Siku ya Festival nitatumbuiza kweli na hapa Nipo na Mh. Makonda Siwezi kumuangusha kwenye mkoa wake,” amesema Diamond.


Share:

Yanga Yateua Wakurugenzi Wapya Watatu




Share:

Kampuni ya Nyanza Yapigwa Marufuku Dar

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,  Paul Makonda ametaka umakini katika utoaji wa tenda za ujenzi wa miradi mbalimbali ili kuepuka dosari.

Makonda ameayasema hayo leo, Jumamosi, Novemba 2, 2019, wakati akiwa kwenye ziara ya kukagua miradi ya kimkakati inayoendelea katika wilaya za Ilala na Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Aidha, Makonda ametoa agizo kuwa Kampuni ya Nyanza inayosimamia mradi wa ujenzi wa Daraja la Mto Kivule isipewe tenda yoyote baada ya kukamilisha mradi huo, kutokana na kushindwa kukamilisha baadhi ya miradi ambayo wamewahi kupewa. Hata hivyo, Mkandarasi huyo tayari, ameanza ujenzi wa mradi huo baada ya kusikia RC Makonda anakwenda huko.

“Huyu mkandarasi huu uwe mradi wake wa mwisho katika Jiji la Dar es Salaam. Kama mnakumbuka hata Temeke aliwahi kufanya uzembe wa namna hii, vifaa hana vya kutosha kazi yenyewe haieleweki, tunataka Makandarasi wenye kasi kutekeleza miradi ya maendeleo,” amesem Makonda.

Amesema baadhi ya Makandarasi wanapewa tenda na kuishia kulipa madeni yanayowakabili kutokana na fedha wanazoingiziwa kukatwa na kusababisha miradi kutokamilika kwa wakati.

“Mnapotoa hizi tenda mjiridhishe wengine ndio kama hawa ambao hadi leo kazi hazionekani,  pia msiwape kazi kwa rushwa mtashindwa kusimamia miradi hii muhimu kwa wananchi,” amesema Makonda


Hivi karibuni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda, alitoa agizo la kuwekwa rumande kwa mkandarasi huyo kutokana na kusuasua kwa ujenzi huo.

Kwa upande mwingine, Mkandarasi anayejenga Machinjio ya Kisasa ya Vingunguti, Elisante Ulomi amesema, mradi wa machinjio ukikamilika utaongeza pato la Taifa kwa kuwa kila kitu kitakachoptoakana na zao la mifugo kitauzwa kwa mfano pembe, damu, ngozi, kwato na nyama ambapo Serikali itakusanya mapato na wananchi watafanya biashara kirahisi katika mazingira rafiki.

Katika hatua nyingine Makonda amelipongeza Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kutokana na kasi ya utekelezaji wa mradi wa Machinjio ya kisasa katika eneo la Vingunguti jijini Dar es Salaam.


Share:

Serikali Kuendelea Kutatua Changamoto Sekta Ya Usafirishaji

NA; MWANDISHI WETU
Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kuendelea kutatua changamoto zinazoikabili sekta ya usafirishaji hapa nchini ili iweze kuongeza mchango wake katika kukuza uchumi.

Akizungumza Novemba 1, 2019 Jijini Dodoma wakati wa mkutano wa pamoja kati ya Vyama vya Madereva na Vyama vya Wamiliki wa Vyombo vya Usafirishaji, Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama amesema kuwa dhamira ya Serikali ni kujenga mazingira wezeshi kati ya wadau wote wa sekta ya usafirishaji hapa nchini wakiwemo madereva na wamiliki wa vyombo vya usafirishaji.

“Moja ya maazimio ya mkutano wetu wa leo ni kuwataka wamiliki wa vyombo vya usafiri ambao hawajatoa mikata ya ajira kwa madereva wao waanze kutoa mikataba ya ajira iliyoboreshwa suala hilo lianze kutekelezwa mara moja kwa kuwa ni takwa la kisheria na sio jambo la hiari” Alisisitiza Mhagama

Kutolewa kwa mikataba hiyo ni matokeo ya makubaliano yaliyofikiwa kati ya pande hizo mwaka 2017 yakitaka kuwepo kwa mikataba ya ajira iliyoboreshwa kwa madereva wote itakayoleta ustawi wa maslahi ya pande hizo na Taifa kwa ujumla.

Alifafanua kuwa mkutano huo umefanikisha kufikiwa kwa maazimio ya pamoja kati ya Serikali, wamiliki na madereva kupitia viongozi wa makundi hayo ili kuchochea ustawi wa sekta hiyo na kuondoa hali ya malalamiko na mapungufu yaliyobainika katika ukaguzi uliofanyika mwezi Julai na Agosti 2019 kwa lengo la kuona namna sheria za kazi  zinavyozingatiwa.

Azimio jingine ni kuendelea kutoa elimu kwa makundi hayo kupitia vyama vya wamiliki na madereva ili kupunguza au kuondoa changamoto zilizopo hasa zilizoibuliwa katika ukaguzi uliofanyika hivi karibuni.

Aidha, Waziri Mhagama ameviagiza vyama vya wamiliki wa vyombo vya usafirishaji kuhakikisha wanaruhusu wafanyakazi kuanzisha matawi ya vyama vya wafanyakazi kwa Makapuni ambayo hayajafanya hivyo bado.

“Vyama vya wafanyakazi vinasaidia sana kuleta tija na ufanisi katika maeneo ya kazi maana wafanyakazi hutumia vyombo hivyo kushauriana namna bora ya kutatua changamoto zinazowakabili,” alisema Mhagama

Katika hatua nyingine Waziri Mhagama aliwataka madereva na wamiliki wa vyombo hivyo kuendelea kuzingatia sheria na kuthamini utu na heshima pande zote mbili, Serikali itachukua hatua kwa yeyote atakayekiuka misingi hiyo.

Kwa upande wake Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri mkuu Kazi, Vijna na Ajira Mhe. Antony Mavunde amesema kuwa maazimio yaliyofikiwa katika mkutano huo yatasaidia kutatua changamoto zilizoibuliwa na madereva na wamiliki wa vyombo vya usafirishaji.

Mkutano wa wadau wa sekta ya usafirishaji umefanyika Jijini Dodoma ukishirikisha Wizara zinazohusika na masuala ya uckuzi na Ujenzi.

=MWISHO=


Share:

MBARAWA AFANYA ZIARA WILAYANI HANDENI ILI KUONA NAMNA YA KUWANUSURU WANANCHI ELFU 55.

Share:

Maswali 15 Yanayoulizwa Mara kwa Mara Kwenye Usaili ( Interviews ) na Namna ya Kuyajibu

Usail wa ajira (interviews) husababisha hofu na msongo wa mawazo kwa vijana wengi kabla au baada ya kutoka chumba cha usaili.

Tatizo hilo hutokana na hofu inayojenga wakati wa kujibu maswali unayoulizwa  na watu ambao wamekuzunguka wakati wa kufanyiwa usaili.

Njia moja ya kuzuia hii kutokea ni kufuatilia mfumo wa kujibu maswali.

Ifuatayo ni orodha yetu ya maswali 15 yanayoulizwa mara kwa mara kwenye interviews( Usaili) na namna ya kuyajibu;

▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬ 

1.Jitambulishe(Wewe ni Nani?)
Mara nyingi hili ni swali ambalo mtahiniwa huulizwa mara tu aingiapo kwenye chumba cha usaili. Kwa bahati mbaya watahiniwa wengi hudhani kuwa waajiri hutamani kujua majina yao. Hapana, majina yako wanayafahamu na pengine hata taarifa za ziada. Katika swali hili waajiri uhitaji kujua sifa zako zihusianazo na ajira zitakazo dhihirisha kuwa wewe ni mtu sahihi.

Mfano mtu anaweza kujibu hivi, “Jina langu ni Mti Mkavu, ni Mhitimu wa Shahada ya Masoko ya Chuo Kikuu Dodoma. Ni mtu makini, mbunifu, mchapa kazi na ninayependa watu. Pamoja na hayo ninao ujuzi usio na shaka kwenye masuala ya mawasiliano. Uwezo wangu unadhihirishwa na mrejesho ambao huwa na upata kwa kila mtu ninaye fanya naye kazi”.

Katika swali hili ni muhimu kujua kuwa halihitaji wewe kuzungumzia mambo yasiyo husiana na kazi na ajira. Kwenu mpo wa ngapi,jina la mama yako, mkoa unaotoka, kabila, kazi ya baba au mama yako havihitajiki katika taarifa unazotakiwa. 


2.Kwanini upewe ajira kwetu? | au unaweza ukaulizwa Kwa nini unahisi wewe ni mtu sahihi kwa kazi hii na siyo mwingine?

Kumbuka kuwa usaili wa kazi unahusisha ushindani hivyo swali hili linataka uoneshe utofauti ulionao. Katika kujibu swali hili zingatia mahitaji ya kazi husika kujenga hoja kwani hata kama una utofauti wa aina gani kama hautasaidia katika kufikia  malengo ya taasisi bado itakuwa ni kazi bure.

Mfano, “ Siyo kwamba mimi ni mchapakazi na mbobezi katika uhasibu pekee lakini pia ni mtu ambaye ninaweza kufanya shughuli zangu bila kusimamiwa. Mimi ni mtu wa matokeo hivyo kwa kila ambacho hufanya hulenga kutimiza malengo kwa wakati na kufikia viwango stahiki. 


"Ubora wangu unathibitishwa na tuzo kadhaa nilizowahi kupata ikiwemo mfanyakazi bora wa mwezi mara nne nilipokuwa nikifanya kazi na na Magogo Media. Hii inathibitisha kuwa mkinipa fursa hii hamtakuwa mnajaribu bali mtakuwa mnafanya maamuzi sahihi”.

3.Unajua nini kuhusu sisi?
Siku zote maandalizi ya usaili yanaenda sambamba na kutafuta taarifa sahihi za taasisi husika. Hivyo ni vyema kuhakikisha kuwa taarifa unazotoa hapa ni sahihi na muhimu katika kudhirisha kuwa ulishafanya utafiti wa kutosha kuhusu taasisi husika.

Mfano, “ Benki yenu ilianzishwa mwaka 1987 ina maono ya kuwa benki bora kuliko zote nchini kwa kutoa huduma za kifedha zinazo aminika na kufikia maeneo mengi nchini. Kwa sasa benki yenu ina matawi 700 na ATMs 500 huku ikiwa na mpango wa kufungua matawi mengine Kigoma hivi karibuni. 


Endapo mtanipa fursa ya kufanya kazi na nyinyi nitahakikisha natumia vyema uwezo wangu katika masuala ya masoko ili kuongeza wateja na kuhaikisha huduma bora mnayotoa inafahamika kwa watu wengi.”

4. Ni vitu gani unavyojivunia?
Katika swali hili waajiri huhitaji kujua mambo kadhaa ambayo unayaona kama mtaji mkubwa katika utendaji kazi. Ni vyema kukumbuka kuwa mambo utakayo yataja hapa ni yale yenye umuhimu katika kuongeza ufanisi au ubora katika kazi husika kwani kila kazi inamahitaji yake ya tofauti na kazi nyingine.

Kwa mfano, “mambo makuu mawili ninayojivunia ni ujuzi na uwezo katika huduma kwa wateja na kujisimamia katika majukumu yangu. Kila ninapowahudumia wateja huwa napokea mrejesho chanya juu ya namna wanavyoridhishwa na huduma yangu hivyo kutamani kuhudumiwa nami tena.


Hii hunifanya nijione kuwa mtu muhimu sana katika taasisi yoyote ninayofanya nayo kazi. Pia, uwezo wangu katika kufanya shughuli bila kusimamiwa au chini ya usimamizi mdogo unanifanya niwe mtu wa kuaminiwa na kutegemewa katika kufanya shughuli zangu.Haya ni baadhi ya mambo mengi yanayonifanya mimi kuwa mtu wa tofauti. Nina amini hamtaacha fursa ya kufanya kazi nami”
 

5.Udhaifu wako ni upi?
Hili ni moja ya maswali ambayo watainiwa wengi huyachukia na kuyaona kama yana lengo la kuwatafutia sababu za kuwanyima kazi. Wengine kwa lengo la kuonesha ukamilifu huthubu kusema kuwa hawana udhaifu wowote-usithubutu kusema hivyo. Kila mtu ana udhaifu wake kwani hakuna aliye mkamilifu.

Suala la msingi ni kujua namna ya kujibu suali hili. Mambo ya kuzingatia ni pamoja na kuchagua udhaifu ambao hauta athiri utendaji wako na pili hakikisha udhaifu huo unahusiana na ujuzi na sio tabia. 


Ujuzi ni rahisi kuutafuata lakini kubadilisha tabia ni ngumu zaidi hivyo usiseme kuwa wewe ni mvivu,mdokozi, na mengineyo ya kitabia. Na unapotaja udhaifu wowote kumbuka kuonesha jitihada ambazo umeshazifanya ili kudhibiti udhaifu huo.

Kwa mfano, kwa kazi ya uhasibu mtu anaweza sema, “Udhaifu nilio nao ni masuala ya ‘graphic designing’ niligundua hili nilipohitaji kuandaa tangazo kwa ajili ya ofisi niliyokuwa nikifanya nayo kazi. Hata hivyo, nimeanza kujifunza mwenyewe kupitia mtandao wa internet na naona napata mabadiliko chanya kila leo”.

Kwa jibu hili ni dhahiri kabisa graphic designing siyo mahitaji muhimu ya kazi ya uhasibu hivyo haita athiti utendaji wa kazi.


6. Kwa nini uliacha kazi yako ya mwanzo?
Hapa unahitajikua makini sana, kumbuka na epuka kuzungumza vibaya kuhusu muajiri yeyote kabla au sasa au uwezo wa muajiri. 


Hapa unaweza ukawajibu tu kwamba;" Kwa sababu ya kuboresha na kuongeza ujuzi, pia natafuta fursa bora zaidi."

7.Unatarajia kupata nini kutokana na kufanya kazi hapa? au unaweza ukaulizwa | Baada ya miaka mitatu wewe mwenyewe utakua wapi?
Ongelea unachotumaini kutimiza ila kuwa mkweli. Pia usiongee kwa ujumla. Chagua kitu maalum ambalo ni muhimu kwa kampuni alafu ilenge. Ila, uwe wazi kwa kusema itachukua muda kujifunza zaidi kuhusu kampuni ili kufanikiwa zaidi.

Kwa mfano; “Nikiwa mwalimu wa kiingereza, lengo langu ni kuongeza asilimia ya wanafunzi wanaofaulu mtihani wa taifa kuwa 85% ya darasa yangu. Najua itachukua muda kujua vizuri changamoto za wanafunzi ila, naamini nitafanikiwa”


Ni vizuri kusema kwamba unatumaini kuona uwajibikaji zaidi  katika kampuni hiyo na kuongeza thamani katika kampuni kwa mchango wako. 

8.Kwanini umekaa muda mrefu bila kupata ajira?

Wajibu kwamba; "Nilikuwa najiendeleza katika taaluma yangu "


9. Eleza namna unavyoweza kujisimamia mwenyewe
Wajibu kwamba: Nitakuwa nafanya kazi niliyopewa nikishirkiana na wasimamizi wangu na viongozi juu ya namna ya kumaliza kazi kabla ya muda uliopangwa.


10. Kitu gani kinakukera miongoni mwa wafanyakazi wenzako?

Wajibu kwamba; "Naamini katika kufanya kazi kwa pamoja. Hata kama nikikerwa na kitu chochote, huwa najaribu kuepuka isipokuwa kama ni kitu cha binafsi."

11.Unategemea kufanya kazi kwa muda gani kama ukipewa ajira?

Wajibu:Kwa muda mrefu kama nitaendelea kuongeza kitu katika taaluma yangu.

12:Je, mwenyewe unajiona kufanikiwa?

Wajibu: Ndio, ukiachana na uwezo wa taaluma yangu, nadhani nimepata watu sahihi wa kufanya nao kazi.

13. Uwezo wako ni upi katika kazi?
Wajibu: Mimi huwa naelewa na kufundishika kwa haraka na ni mchapakazi wa kweli.

14,Unapenda nafasi au cheo gani katika timu unayofanya nayo kazi?
Wajibu: Haijalishi hadi nitakapojifunza kitu kipya kwa kila mradi au kazi.

15.Je, unaswali lolote kwetu? 

Mwishoni wa interview, ni kawaida kwa mwajiri kuuliza kama una maswali kwao. Ukipewa nafasi hii, usiulizie mshaara na faida zingine. Badala yake, uliza:
  1.     Maadili ya kampuni
  2.     Aina ya uongozi
  3.     Wafanyakazi wenzako
  4.     Chochote ambacho hukuelewa kuhusu kazi hiyo.
  5.     Watakupa jibu baada ya muda gani?
==>>USIFANYE HAYA MAKOSA KATIKA SWALI HILO:
- Je, kuna fursa ya kukua / kupandishwa ngazi?
- Nitapata siku ngapi za likizo?

- waajiliwa wanafaidika vipi na kampuni hii. 

==>Tiba bora ya msongo wa interview ni kujiandaa
Ingawa interview inaweza ikakupa misongo mingi, ukijiandaa vizuri Utashangazwa na mafanikio yako.

Interview ni nafasi yako ya mwisho kumvutia mwajiri, na vidokezo vilivyoelezwa hapo juu vitakusaidia na hilo.

Kumbuka, hamna haja ya kuwa na wasiwasi ukiwa umejiandaa. 


Nakutakia Mafanikio mema kwenye Interview
▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬

👉Sasa, kwa kuwa umeshajua jinsi ya kujibu vizuri maswali ya Interview, anza kutafuta kazi unayoitaka kwa kubofya hapo chini. 


Hilo ni Jukwaa Maalumu la Ajira zote za Serikali, Makampuni Binafsi n.k. Kuna Nafasi za Kazi zaidi ya 7000 kwa ajili yako.

👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇
http://ajirazote.com/jobs


▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬ 

Bonyeza <<HAPA>> ujiunge na Group letu la Telegram ili upate makala mbalimbali kama hizi pamoja na matangazo ya Ajira, Scholarships


Share:

Mchunguzi Mkuu TAKUKURU Amwandikia Barua DPP Kukiri Makosa Yake

Mchunguzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Cosmas Batanyika (44) anayekabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi ikiwamo kushawishi rushwa ya zaidi ya Sh. milioni 300, kupokea na kutakatisha Dola za Marekani 20,000 amedai mahakamani amemwandikia barua Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) ya kukiri makosa yake.

Batanyika alitoa madai hayo jana kesi yake ilipopangwa kwa ajili ya kutajwa mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi, Kevini Mhina, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam.

Wakili wa Serikali, Glory Mwenda, alidai kuwa kesi hiyo imepangwa kwa ajili ya kutajwa na kwamba upelelezi haujakamilika.

Hata hivyo, mshtakiwa alidai kuwa amemwandikia barua DPP na kwenye makubaliano anasubiri majibu ndugu zake wanafuatilia.

Hakimu Mhina alisema kesi hiyo itatajwa tena Novemba 15, mwaka huu na mshtakiwa ataendelea kukaa mahabusu


Share:

Aliyemtishia Mwenzake Kumuua kwa Bastola Akamatwa

Kamanda wa Polisi Kinondoni, Mussa Taibu amesema wamemkamata Shabani Hamis Said ambaye anadaiwa kumtishia kwa Bastola dereva wa lori Venance John maeneo ya Mabwe Pande, saa 3 asubuhi, October 30, 2019.

Amesema baada ya lori la mchanga  alilokuwa anaendesha Venance kukwama bila kupata msaada wa haraka, akatokea mshtakiwa Shabani Hamis akiwa anaendesha gari lake aina ya Subaru na kumtaka dereva huyo ampishe ili apite na  akamjibu hawezi kumpisha kwa sababu amekwama katika mchanga.

Baadae wananchi wakatokea na kumpa msaada wa kumkwamua na kuondoka lakini alipofika mbele mshtakiwa alimzuia dereva huyo wa lori na kuanza kumtupia maneno kisha wakaanza kujibizana na kufikia hatua ya mshitakiwa kuamua kutoa Bastola na kutishia kumuua Venance.


Share:

Waziri Kigwangalla Aaigiza Maboresho Ya Huduma Mlima Kilimanjaro.

Na. Aron Msigwa – WMU, ARUSHA.
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla ameliagiza Shirika la Hifadhi za Taifa nchini (TANAPA) lifanye maboresho ya miundombinu ya huduma za dharula na uokoaji ndani ya hifadhi ya mlima Kilimanjaro ili kuogeza usalama wa watalii wanaokweda 2kupanda mlima huo.

Pia, amelitaka shirika hilo liedelee kuboresha miudombinu ya malazi katika hifadhi hiyo ili iweze kuendana na mahitaji ya sasa ya wapanda mlima na kuangalia uwezekano wa kutafuta wawekezaji watakaojenga hoteli za kisasa kwa lengo la kuvutia watalii wengi zaidi.

Dkt.Kigwangalla ametoa maagizo hayo alipokutana na kufanya mazungumzo na Menejimenti ya TANAPA na Wakuu wa Kanda wa Shirika hilo jijiini Arusha.

Amesema hatua hiyo imekuja kufuatia changamoto mbalimbali alizokutana nazo wakati akipada mlima Kilimanjaro Septemba, 28 mwaka huu, akiwa ameambatana na kundi la Wasanii na wadau mbalimbali kutoka taasisi za umma na binafsi.

Dkt. Kigwangalla ameieleza Menejimenti hiyo kuwa katika zoezi lake la kupanda mlima Kilimanjaro kuna changamoto alizibaini zikiwemo za kukosekana kwa miudombinu ya kutosha ya huduma za uokoaji na malazi ambazo zinatakiwa kufanyiwa kazi kwa haraka ili kuongeza ufanisi na idadi ya watalii wanaopanda mlima huo.

Kufuatia hali hiyo ameiagiza TANAPA ianze kuboresha huduma za dharula na uokoaji pia ijenge vituo vya kutolea tiba na huduma ya kwanza mlimani vitakavyokuwa na wataalam wa kuhudumia watalii wanaopata matatizo wakiwa mlimani pia kuboresha huduma za malazi katika baadhi njia za mlima huo.

Dkt.Kigwangalla amesema changamoto hizo zikitatuliwa kwa haraka zitauwezesha mlima huo kupata idadi kubwa ya watalii kuliko ilivyo sasa na kuiogezea serikali mapato.

Kuhusu uboreshaji wa huduma za uokoaji (Rescue services) kwa watalii wanaopanda mlima Kilimanjaro ameiagiza TANAPA ifanye utaratibu wa kuazisha huduma ya viberege maalum (Zip line) vitakavyokua vinatumika kushusha wapada mlima watakaokua wakipata matatizo ya kiafya kwa haraka hata wakati wa hali mbaya ya hewa.

“Suala la matumizi ya “Zip line” mliongezee nguvu ya kulitekeleza, hii itakua njia rahisi ya uokoaji na itawajengea ujasiri wapada mlima waelewe kwamba hata kama watapata shida yoyote ya kiafya wakati wa kupanda mlima wanajua wana uhakika wa usalama wa maisha yao hata pale ambapo hali ya hewa ni mbaya na helikopta haiwezi kutua mlimani” Amesisitiza Dkt. Kigwangalla.

Amesema uwepo wa huduma hiyo ya kisasa ya kushusha watalii wanaopata chagamoto za kiafya itawezesha watalii kupata huduma mlimani kupitia vituo vya kutolea huduma ya kwanza vitakavyojegwa mlimani ambavyo vitakua na wataalam wenye mafumzo watakaokuwa na jukumu la kutoa huduma muda wote.

Kuhusu uboreshaji wa huduma ya malazi mlimani Dkt. Kigwangalla ameonesha kuridhishwa na hatua zinazoendelea kuchukuliwa na TANAPA kuboresha miundombinu ya malazi mlimani na kuitaka iangalie uwezekano wa  kuhamasisha wawekezaji wakubwa kwenye ujenzi wa hoteli za kisasa. 

Amesema uwepo wa hoteli hizo pamoja na mambo mengine utaongeza siku za watalii kukaa mlimani akitoa mfano wa hoteli nzuri na za kisasa zilizojengwa katika milima ya Alaps ambazo zinatembelewa na watu maarufu kutoka maeneo mbalimbali duniani.

Kufuatia maagizo hayo, Kamishna wa uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA), Dkt. Allan Kijazi amesema kuwa TANAPA inaendelea kufanya maboresho kwenye maeneo ya kulala wageni ili yaweze kwenda na wakati pia yawe na uwezo wa kupokea wageni wengi pia kuishirikisha sekta binafsi katika utoaji wa huduma mlimani.

Amesema kazi ya kuainisha maeneo kwa ajili ya ujenzi wa hoteli za kisasa inaendelea na kwa kuanzia maeneo manne yamekwishaainishwa kwa ajili ya uwekezaji na kuongeza kuwa baadhi ya wawekezaji wamekwishajitokeza na kuonesha nia ya kujenga hoteli za kisasa katika mlima huo.

Kuhusu uboreshaji wa huduma za ukoaji mlimani amesema kwa sasa kuna maeneo yana miundombinu ya barabara zinazowezwsha magari ya kubebea wagonjwa kufika katika baadhi ya maeneo na kutoa huduma ya uokoaji.

 Pia amesema wamekua wakitumia helikopta kutoa huduma za uokoaji licha ya huduma hiyo kushindwa kufanyika kazi wakati wa hali mbaya ya hewa na hivyo kulazimika kutumia machela za matairi zinazoendeshwa na watu kuhudumia watalii wanaopata matatizo ya kiafya.

Aidha, Dkt. Kijazi amesema TANAPA inaendelea kufanya maboresho ya huduma za dharula na uokoaji na itawasilisha kwake taarifa ya utekelezaji itakayoainisha mpango wa ujenzi wa njia za kisasa zitakazotumia viberenge maalum vya uokoaji vitakavyokua vikipita kwenye waya (Zip line) ili kazi ya ujenzi wa njia hizo ianze mara moja.


Share:

Ofisi Ya Makamu Wa Rais Kwa Kushirikiana Na Wizara Ya Viwanda Na Biashara Yakutana Na Wazalishaji, Wasambazaji Na Wauzaji Wa Mifuko Mbadala Wa Plastiki.

Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kushirikiana na Wizara ya Viwanda na Biashara imeandaa kikao kilichowakutanisha Wazalishaji, Wauzaji na Wasambazaji wa mifuko mbadala wa plastiki. 

Kikao hiko kimefanyika katika Ukumbi wa Mwalimu Julius Kmbarage Nyerere (JNICC) jijini Dar Es Salaama Lengo la Kikao hiko ni kusikiliza hoja na changamoto mbalimbali kutoka kwa Wazalishaji, Wauzaji na Wasambazaji wa mifuko hiyo, na hivyo basi kuwezesha Serikali kuzipatia changamoto hizo uvumbuzi.

Akiongea katika Kikao hiko Mgeni Rasmi ambaye ni Mkurugenzi wa Viwanda kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara Bw. Leo Lyayuka alisema kuwa zoezi zima la upigaji marufuku mifuko ya plastiki limefanikiwa kwa kiasi kikubwa na lilifanyika kwa weledi hali iliyopelekea kutokua na malalamiko yoyote kutoka kwa wananchi.

“Kwenye mafanikio yoyote hapakosi changamoto, vivohivyo, kwenye zoezi hili, ingawa tumepata mafanikio makubwa lakini kuna changamoto ambazo zimejitokeza na kama zisipotafutiwa ufumbuzi wa haraka zitaharibu na kurudisha nyuma mafanikio makubwa yaliyopatikana. Kwahiyo kikao chetu kitajikita katika kuzibaini changamoto zote na kupendekeza mapendekezo namna ya kutatua”.Alisema Bwana Lyayuka.

Naye Mkurugenzi Msaidizi toka Ofisi ya Makamu wa Rais Bi Kemilembe Mutasa alisema kuwa Kikao hiko kina lengo la kujenga uelewa wa pamoja kuhusu utekelezaji wa katazo la mifuko ya plastiki, kuibua changamoto za utekelezaji na namna ya kukabiliana na changamoto husika hususani katika masuala yafuatayo:- Viwango vya ubora vinavyotakiwa vya mifuko mbadala wa plastiki, Hali ya uzalishaji na usambazaji wa mifuko mbadala wa plastiki, Uzalishaji na upatikanaji wa malighafi kwa ajili ya mifuko mbadala wa plastiki, Viwango vya ubora wa mifuko mbadala na Changamoto zinazojitokeza katika uzalishaji wa mifuko mbadala wa plastiki.

Ofisi ya Makamu wa Rais imekua ikiandaa vikao kama hivyo mara nyingi ili kuweza kupata maoni na changamoto juu ya uzalishaji, usambazaji na biashara ya mifuko mbadala wa plastiki kwa pamoja.


Share:

Wabadhilifu, Wezi wa Dawa za Serikali Wapewa ONYO Tena

Na. Atley Kuni- TAMISEMI
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Dkt. Dorothy Gwajima, ameapa kwamba moto dhidi ya wabadhilifu wa dawa aliouwasha katika zoezi la ufuatiliaji hautazimika wala kupoa, huku akiwaomba wananchi kutoa ushirikiano wa karibu kwa kuwafichua watu/mtu yeyote atakayebainika kuhujumu jitihada za serikali.

Gwajima ametoa kauli hiyo ikiwa ni mara ya pili kurudia wito huo mbele ya Makatibu Tawala wa Mikoa, wataalamu Wafamasia kutoka mikoa 13 na wadau wa maendeleo Global Supply chain, waliokutana mjini Dodoma kwenye ukumbi wa Mikutano wa OR-TAMISEMI katika kikao kazi cha tathmini ya mbinu mpya ya kuimarisha takwimu za bidhaa za afya.

Akizungumza katika kikao hicho Gwajima amesema, vita hiyo wataweza kuishinda kwa kuunganisha nguvu na wananchi kutoka maeneo yote nchini.

“Niwaombe wanachi kuwa mstari wa mbele kufichua wale wote mtakaowabaini wanahujumu suala la dawa kwani vita hiyo siyo ya mtu mmoja mmoja wala serikali peke yake bali ni ya jamii nzima” alisema Gwajima na kuongeza kuwa, “wapo watu wanaotambua nani ni adui wao katika vita hivi ndiyo maana jana nimeona kwenye Jamiiforum wakinipa pole na kunipongeza, lakini nasema lazima tutembee na wananchi katika hili.” alisisitiza kiongozi huyo.

Gwajima alisema inashangaza unafika kwenye kituo ambacho kina wafamasia wasiopungua sita (6) lakini unakuta kitabu cha kupokelea dawa (ledger) hakijahuishwa kwa zaidi ya miezi 5, hii ni hali ya hatari sana, suala hilo halivumiki na wala hawezi kukubaliana nalo.

“Viongozi wangu Makatibu Tawala, mnaelewa tunatekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi ya 2015-2020, hivyo fuatilieni hili hadi kwenye stoo za kutunzia dawa lakini pia ombeni taarifa na ingieni kwenye mikutano yao muone kile wanachokijadili maana humo hakuna zuio lolote kwa kuwa taarifa zinazojadiliwa humo sio siri za mgonjwa, sasa wasije wakajifichia kwenye mwamvuli wa taarifa za kitabibu kwa kuwahadaa eti siri za Mgonjwa?” Alihoji na alikemea  

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Global Supply Chain Tukay Mavere aliwataka wachumi, watawala wa fedha pamoja na watumiaji wa mfumo wa eLMIS kukaa pamoja na kuja na mbinu mbadala za kudhibiti hali ya dawa na upatikanaji wake na kutoa mrejesho wa kile ambacho serikali imewekeza.

“Lengo la mfumo huu tunataka tuwe tunachukua jambo, tunalichakata na kisha tunalitolea majibu kwa wakati sio kungoja muda uende, aidha hii inakuwa ni zoezi endelevu katika utendaji wa siku kwa siku kama mfumo ulivyo, hivyo tumeitana ili tuwe na uwelewa wa pamoja juu ya hili tunalokusudia kulifanikisha” alisema Mavere.

Kwa upande wao washiriki wa warsha hiyo wameipongeza serikali na wadau kuja na mfumo huo, kwani ni matumaini yao utakuwa suluhu ya yale wanayofanyia kazi kila siku.

“Kama Naibu Katibu Mkuu alivyosema, mfumo huu utasaidia kuondoa ziada ya dawa inayosababisha upotevu wa pesa kutokana na kuchina kwa Bidhaa zilizoingizwa bila takwimu sahihi, vema sasa kila mmoja wetu akitoka hapa awe mstari wa mbele katika kuutumia mfumo kwenye utendaji wake.” alisema, Msalika Makungu Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora.

Katika kikao hicho cha siku mbili pamoja na mambo mengine yatakayojitokeza, wataalam watajifunza kupata takwimu sahihi kwa ajili ya kufanyia maoteo kwa kuwa mfumo unaanzia chini kwenye huduma kwenda juu, hivyo itakuwa ni fursa ya kuwajengea uwezo timu za uratibu wa afya za Mikoa na Wilaya, kupata taarifa sahihi na kufanya ugawaji wa dawa kulingana na mahitaji na kuondokana na tatizo la dawa kwenye maeneo yenye dawa nyingi.

Mambo mengine ni kufanya bajeti kulingana na rasilimali zilizopo lakini pia kuwezesha kufanya usimamizi kwa njia ya mtandao Online Supervision.

Katika kikao hicho, Wataalamu hao walikumbushwa juu ya viapo vyao kwa kuongozwa na kiapo mbele ya Naibu Katibu Mkuu huku wakiwa wamenyoosha mikono juu na kuapa kwamba, watakuwa chachu ya mapambano dhidi ya ubadhilifu wa dawa na endapo wakishindwa basi wawe tayari kuachia nyadhifa zao hata kwa kutuma ujumbe wa maandishi kwenye mtandao wa kundi sogozi (WhatsApp) kuhusu  kuachia madaraka waliyonayo.


Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumamosi November 2





















Share:

Friday, 1 November 2019

KIJANA ALIYEFUNGWA MINYORORO CHUMBANI AFUNGULIWA SHINYANGA


Kijana wa miaka 26, mkazi wa Old Shinyanga katika Manispaa ya Shinyanga, aliyekuwa amefungwa minyororo chumbani kwa miezi miwili, Shadrack Johanes amefunguliwa na kufanyiwa usafi, kuvishwa nguo na kuanza kupatiwa matibabu ya afya ya akili.


Shadrack Johanes, alifunguliwa minyororo hiyo jana mara baada ya Nipashe kuripoti habari kuhusu ukatili uliokuwa unafanywa dhidi ya na ndugu zake.

Kwa miezi miwili alikuwa amefungwa minyororo mikono na miguu akiwa mtupu huku akila chakula kwenye chumba ambacho alikuwa anajisaidia haja kubwa na ndogo.

Ofisa Ustawi wa Jamii Manispaa ya Shinyanga, Panuela Samwel, alisema kijana huyo amefunguliwa minyororo hiyo na serikali itatoa matibabu kwake bila malipo.

Panuela Samwel ameongeza kuwa, wameambiwa na wataalamu wa afya kuwa matibabu ya kijana huyo yanatarajiwa kuchukua muda wa miezi sita hadi mwaka mzima. Ofisa huyo wa serikali alisema kama kijana huyo hatapona, watampatia rufani kwenda jijini Dodoma kupatiwa matibabu kwenye Hospitali ya Mirembe jijini Dodoma.

”Tukio alilofanyiwa kijana huyu ni la kinyama sana, nashukuru vyombo vya habari kwa kuliibua, bila ninyi huenda kijana huyu angefia ndani. Sisi sasa kama serikali, tutamtibu kijana huyu bure kabisa, na leo (jana) anaanza kupatiwa dawa ambayo itachukua muda wa miezi sita hadi mwaka mzima.” amesema Panuela Samwel ambaye ni Ofisa Ustawi wa Jamii Manispaa ya Shinyanga.

Akiwa kwenye familia ya kijana huyo jana, ofisa huyo aliitaka isimnyanyapae tena, badala yake imweke kwenye mazingira mazuri pasi na kumfunga minyororo.

Mratibu wa Magonjwa ya Afya ya Akili, Brigita Nyangare, alisema kijana huyo hana tatizo kubwa sana la akili kwa kuwa ana bado ana uwezo wa kuongea na hajapoteza kumbukumbu.

Alisema atakuwa karibu na kijana huyo muda wote wa matibabu yake na atakuwa anafuatilia anavyoishi nyumbani hadi pale atakapojiridhisha amepona.

Akizungumza kwa shida, Johanes aliwaomba ndugu zake wasimfungie ndani tena. Ndugu wa kijana hauyo waliomba msamaha kutokana na kumfungia na kuahidi kufuata maagizo waliyopewa na serikali.
Share:

ALIYESHIRIKI KUTUNGA SHERIA YA KUZUIA UZINZI AFUMANIWA AKIHONDOMOLA MKE WA MTU


Mwanaume mmoja nchini Indonesia ambaye alishiriki kwa kiasi kikubwa kuandaa Muswada wa sheria ya kupinga vitendo vya uzinifu nchini humo amekamatwa akizini na mke wa mtu.

Mukhlis bin Mudammad ni mmoja kati ya wwanachama wa baraza la wanatheolojia ambalo lilisaidia kutunga sheria za Kiisilamu kupinga vitendo vya zinaa pamoja na baadhi ya makosa mengi, lakini alijikuta akicharazwa viboko 28 hadharani mbele ya kadamnasi ya watu hapo jana siku ya Alhamisi katika Mkoa wa Aceh, Besar kufuatia kufumaniwa uzinzi na Mke wa mtu.

Tukio hilo linamfanya, Mukhlis bin Mudammad mwenye umri wa miaka 46, kuwa kiongozi wa kwanza wa baraza hilo kuadhibiwa na sheria hizo baada ya kukutwa na hatia.

Mukhlis pamoja na mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 33, ambao wote wawili ni wanandoa wamepatika na hatia ya kuchepuka na kuzisaliti ndoa zao kupitia mahaka ya Mkoawa Aceh ya ekhtilat baada ya kufumwa wakifanya vitendo hivyo ndani ya gari katika fukwe mwezi uliyopita.
Share:

IDRIS ARIPOTI TENA POLISI MAKOSA YA MTANDAO...ANATUHUMIWA KUSAMBAZA UONGO NA KUJIFANYA RAIS

Na Pamela Chilongola, Mwananchi 
 Mchekeshaji na mshindi wa shindano la Big Brother 2014, Idris Sultan ameripoti kituo cha polisi kati leo Ijumaa Novemba Mosi, 2019 na kuhojiwa kwa dakika 30 na kutakiwa kuripoti tena Jumatano Novemba 6, 2019.

Jana asubuhi, Idris aliripoti kituoni hapo na kuhojiwa kwa saa tano na kupekuliwa nyumbani kwake, usiku aliachiwa kwa dhamana akitakiwa kuripoti tena leo saa 2 asubuhi, jambo ambalo amelitekeleza.

“Idris ameripoti kituoni saa 2:00 asubuhi na kuhojiwa kwa dakika 30. Wamechukua simu zake kwa uchunguzi na kutakiwa kuripoti tena Jumatano ijayo (Novemba 6, 2019).”

“Wamemueleza kuwa kosa lake ni kusambaza habari za uongo chini ya kifungu cha 16 cha sheria ya makosa ya mtandao. Kosa la pili ni kujifanya Rais chini ya kifungu cha 15 cha makosa ya mtandao,” amesema, Benedict Ishabakaki ambaye ni mwanasheria wa mchekeshaji huyo.

Jana alipopekuliwa nyumbani kwake polisi walichukua kompyuta mpakato kwa ajili ya uchunguzi, aliporudishwa kituoni kabla ya kupewa dhamana alipelekwa kitengo cha makosa ya mtandaoni.

Juzi mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alimtaka Idris kuripoti polisi baada ya kuweka picha yenye sura yake huku akiwa ameketi katika kiti chenye nembo ya Taifa.

Pia, Idris aliweka picha nyingine inayoonyesha sura ya Rais John Magufuli akiwa amesimama huku amevaa suruali yenye mikanda inayoshikizwa mabegani.

Hata hivyo, dakika chache baada ya Makonda kumtaka msanii huyo kuripoti polisi, waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla aliahidi kumuwekea dhamana iwapo angekamatwa.

Ilivyokuwa
Via>>Mwananchi

Share:

AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUMJERUHI ASKARI POLISI KWA KUTUMIA PAKA 'NYAU'

Vyombo vya habari vya Urusi vimeripoti kuwa mwanaume mmoja mjini Moscow anakabiliwa na kifungo cha miaka mitano kwa kosa la kumtumia paka 'nyau' kama silaha yake.

Mtuhumiwa huyo Gennady Shcherbakov anatuhumiwa kwa kumrushia polisi paka wakati ambapo polisi alikuwa ameenda kuthibiti kelele ambazo zilikuwa katika makazi ya watu.

Bwana Shcherbakov, 59, anakabiliwa na kosa la jinai la unyanyasaji dhidi ya polisi.

Kesi hiyo ilifunguliwa siku ya jumatano, ambapo ilikuwa ni kipindi cha zaidi ya mwaka tangu tukio hilo litokee , imeripotiwa na chaneli ya Telegram Baza

Tuhuma hizo zilikuwaje?

Kwa mujibu wa televisheni ya taifa ya Urusi, tarehe 4 oktoba 2018, bwana Shcherbakov alikuwa amekuwa anapiga kelele katika makazi ya watu huko Moscow.

Anadaiwa kuwa alikuwa amelewa sana.

Wakazi wa eneo hilo waliripoti kuhusu usumbufu aliokuwa anasababisha.

Mara baada ya polisi kufika katika eneo hilo kumzuia asiendelee kufanya fujo , bwana Shcherbakov aligoma kutoa ushirikiano kwa polisi na hata kujibu maswali aliyokuwa akiulizwa.

Badala yake bwana Shcherbakov anadaiwa kuwa alimnyanyua paka ambaye alikuwa karibu yake na kumrushia polisi.

Mnyama huyo anaripotiwa kuwa alimjeruhi polisi.

Bwana Shcherbakov, ambaye hakuwa mkazi wa eneo hilo, anakanusha kuhusika na tukio hilo na hata kutumia paka kama silaha.

Yeye anadai kuwa paka huyo alimrukia polisi mwenyewe bila kurushwa au kusukumwa na mtu yeyote.

Kesi hiyo imewekwa kwenye kifungu cha 318 , kwa kosa la uhalifu wa jinai wa kutumia vurugu dhidi ya asifa wa umma.

Haijafahamika kwa nini kesi hiyo imechukua muda mrefu kufunguliwa kama kosa la jinai na hata hawajaeleza nini kitamkuta paka aliyehusika

 Chanzo - BBC
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger