Wednesday, 21 August 2019

Waliofariki kwa ajali ya moto Morogoro wafikia 100

Idadi ya waliofariki kutokana na ajali ya moto wa lori la mafuta mkoani Morogoro, Agosti 10, 2019 imefikia 100.

Hii inatokana na majeruhi mwingine mmoja kufariki jana usiku Jumanne wakati akiendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini  Dar es Salaam.

Kifo hicho kimekuwa cha tatu kwa siku ya jana Jumanne ambapo hadi saa 10 jioni ya jana Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dk Stephen Kabwe alisema majeruhi wawili kati ya 18 walikuwa wamefariki.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa MNH, Aminiel Aligaesha amewataja waliofariki ni Mazoya Sahani, Khasim Marjani na Ramadhani Magwila.

Amesema majeruhi waliobaki katika hospitali hiyo waliolazwa chumba cha uangalizi maalum (ICU) ni 13 na wawili wametolewa ICU na kulazwa wodi ya Sewahaji.


Share:

Jaji Mkuu wa Tanzania Kuongoza Jopo la Majaji Watatu Kusikiliza Mashauri 29 ya Rufaa Iringa

Na Lusako Mwang’onda, Mahakama Kuu – Iringa
Jumla ya mashauri 29 yanatarajiwa kusikilizwa mkoani Iringa katika kikao maalum ‘session’ ya Mahakama ya Rufani chini ya jopo la Wahe. Majaji watatu likiongozwa na Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Profesa Ibrahim Juma.

Akizungumzia kuhusu kikao hicho ‘session’ mapema Agosti 19, 2019, Naibu Msajili wa Mahakama ya Rufani, Mhe. Eddie Fussi amesema kuwa katika kikao hicho kuna jumla ya mashauri ya rufaa za jinai ishirini na tano (25), rufaa za madai mbili (2) na maombi ya madai mawili (2)

Mhe. Fussi ameongeza kuwa kati ya mashauri hayo ishirini na tisa (29); matatu (3) ni ya zamani (backlogs) na ishirini na sita (26) ni ya muda wa kati na mapya (back stopping).

Kikao hiki cha Mahakama ya Rufani kilichoanza wiki iliyopita ni cha pili (II) kufanyika ndani ya mwaka huu. Majaji wengine waliopo katika jopo hilo ni pamoja na Mhe. Richard Mziray, Mhe. Rehema Mkuye na Mhe. Ignas Kitusi.

Kikao hicho kinatarajiwa kukamilika Agosti 30 mwaka huu na mara baada ya kukamilika kwa kikao hicho, Mhe. Jaji Mkuu anatarajia kufanya ziara ya kikazi kwenye Mahakama zote za mikoa ya Iringa na Njombe, ambapo atakagua maendeleo ya shughuli mbalimbali za kimahakama na kuzungumza na watumishi.


Share:

Waganga Wakuu Wa Mikoa Na halmashauri Watakiwa Kuimarisha Lishe

Na.Catherine Sungura,WAMJW-Dodoma
Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri nchini wametakiwa kuweka mikakati ya kuimarisha hali ya lishe katika ngazi ya jamii ili kupunguza hali ya udumavu kwa jamii.

Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri wa Afya, Maendleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Dkt. Faustine Ndugulile kwenye kikao kazi cha Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri unaofanyika jijini hapo.

Dkt. Ndugulile amesema kuwa ili kuwe na taifa lisilo na kiwango cha chini cha hali ya lishe waganga wakuu hao lazima wapange mikakati ambayo itaanzia ngazi ya jamii ili wananchi waweze kuelewa umuhimu wa lishe bora na inayostahili kwa familia hivyo wanapaswa kufanya kazi kwa weledi ili mikakati hiyo ifanikiwe.

Hata hivyo alisisitiza watoa huduma kutoa huduma bora kwa wananchi kwa kuimarisha huduma za afya katika maeneo yao ili wananchi wanaoenda kupata huduma wapate huduma hizo kwa haki na usawa” na katika hili ni vyema mwananchi anayekuja kupata huduna ni vyema aridhike na huduma anayopata katika vituo vyetu vyote nchini”.Alisema Dkt. Ndugulile.

Aidha, Dkt. Ndugulile aliwataka waganga wakuu hao kusimamia utendaji wa kazi katika maeneo yao ili kuweza kutoa huduma bora za afya kwa jamii“inasikitisha kuona mama mjamzito anafariki kwenye kituo cha afya kwa ajili ya uzembe au kutokupata huduma sahii jambo hili halikubariki”.

Kikao kazi cha waganga wakuu wa mikoa na halmashauri mwaka huu kinafanyika jijini hapa ambapo kilifunguliwa na mgeni rasmi ambaye ni Waziri wa ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Suleiman Jafo na kauli mbiu ya kikao hicho ni “Uwajibikaji ni nguzo muhimu katika utoaji huduma bora za afya kuelekea uchumi wa kati na utakua wa siku tano.


Share:

Serikali: Uhalifu Wapungua Nchini

Na Mwandishi Wetu
Serikali imesema katika kipindi cha Januari hadi Juni mwaka huu nchi imeendelea kuwa katika amani na utulivu huku uhalifu ukipungua kwa asilimia 2.2 kwa makosa makubwa ya jinai ukilinganisha na kipindi kama hicho kwa mwaka uliopita hali inayopelekea wananchi kuendelea na shughuli za kiuchumi kwa amani na usalama.


Hayo yamesemwa leo jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni wakati akisoma taarifa ya Serikali mbele ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, iliyohusu Hali ya Ulinzi na Usalama wa Raia na Mali zao kwa Kipindi cha mwezi Januari hadi Juni mwaka huu ikiwemo utekelezaji wa dhana ya Ulinzi Shirikishi.

“Kuanzia Januari hadi Juni ndani ya mwaka huu jumla ya makosa makubwa ya jinai yaliyoripotiwa katika vituo vya polisi nchi nzima yalikuwa 28,252 tofauti na kipindi kama hiki mwaka uliopita ambapo makosa 28,889 yaliripotiwa vituoni, tukiangalia vizuri hesabu zetu ndani ya mwaka huu tumepunguza makosa 637 hii yote inatokana na juhudi za askari wetu na utekelezaji wa dhana ya ulinzi shirikishi” alisema Masauni

Naibu Waziri Masauni ameyataja makosa hayo makubwa ya jinai kuwa ni Makosa dhidi ya binadamu, Makosa dhidi ya Maadili ya Jamii, Makosa ya kuwania mali na Makosa ya Uhalifu wa Kifedha

Akizungumzia makosa ya usalama barabarani Naibu Waziri Masauni amesema kumekuwepo na mafanikio katika kupunguza makosa ya usalama barabarani hali inayochagizwa na usimamiaji wa sheria na kutoa elimu ya usalama barabarani kwa watumiaji wa vyombo vya moto na watembea kwa miguu..

“Takwimu za makosa ya ajali za barabarani katika kipindi cha Januari hadi Juni mwaka huu zinaonesha kuwepo kwa jumla ya makosa 1,610 yaliyoripotiwa ikilinganishwa na makosa 2,200 mwaka uliopita huku takwimu zikiweka wazi makosa 590 kupungua katika vipindi hivyo viwili” alisema Masauni

Alisema kutokana na kupungua kwa makosa ya barabarani hata idadi ya ajali zilipungua hali iliyopelekea kupungua kwa vifo kwani mwaka jana watu 1,051 walifariki tofauti na mwaka huu ambapo kuanzia mwezi Januari mpaka Juni watu 781 walipoteza maisha.

Akizungumza wakati wa kikao hicho Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro alisema mafanikio hayo ya kupungua kwa uhalifu nchini yamechangiwa pia na matumizi ya teknolojia katika kupambana na uhalifu huku akiwaonya wahalifu kutafuta shughuli nyingine ya kufanya.

“Tunatumia vifaa maalumu ikiwepo drones katika kudhibiti uhalifu japo kwasababu za kiintelijinsia hatuwezi kusema ziko ngapi na maeneo gani muhimu tunawaasa wahalifu kuacha mipango yao ya kuvuruga amani ya nchi hii nawahakikishia hawatabaki salama,tunataka wananchi wafanye shughuli zao za kiuchumi” alisema IGP Sirro

Vikao vya Kamati za Bunge zinaendelea jijini Dodoma huku wizara mbalimbali zikiwasilisha taarifa zao kwa kamati hizo huku vikao vya Bunge vikitarajiwa kuanza mwanzoni mwa mwezi ujao.



Share:

Waziri Kabudi afungua rasmi kikao kazi maalum cha Mabalozi

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi amewataka Mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania nje kuongeza jitihada katika kuhamasisha wawekezaji, wafanyabiashara na watalii kuja nchini ikiwa ni utekelezaji wa Diplomasia ya Uchumi.

Waziri Kabudi ameyasema hayo  tarehe 20 Agosti 2019 wakati akifungua rasmi kikao kazi maalum cha Mabalozi kinachofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Julius Nyerere kuanzia tarehe 20 hadi 23 Agosti 2019.

Mhe. Waziri Kabudi alisema kuwa, Mabalozi ambao wana jukumu kubwa la kusimamia maslahi ya nchi kwenye nchi mbalimbali duniani, wameendelea kufanya kazi nzuri katika katika kuhakikisha dhana ya diplomasia ya uchumi inafikiwa na kwamaba matokeo ya jitihada hizo ni pamoja na kuongezeka kwa watalii, wawekezaji na wafanyabiashara nchini. P.ia kuongezeka kwa fursa za ufadhili wa masomo na ajira kwa Watanzania kwenye nchi mbalimbali

“Hii ni mara yangu ya kwanza kukutana nanyi Waheshimiwa Mabalozi tangu niteuliwe na Mhe. Rais kwenye wadhifa huu. Nazipongeza jitihada zenu katika utekeelzaji wa diplomasia ya uchumi kwani matokeo tunayaona kwa biashara kuongezeka hapa nchini watalii na hata wawekezaji. Hivyo nataka mwongeze jitihada Zaidi ili nchi yetu ifikie azma ya kuwa nchi ya uchumi wa kati na viwanda ifikapo mwaka 2025” alisema Mhe. Kabudi”.

Aidha, Mhe. Waziri Kabudi alitoa rai kwa Mabalozi kuendelea kuwahamasisha Watanzania waishio nje (Diaspora) kujiandikisha na kuanzisha jumuiya zao ili kwa namna moja au nyingine na wao washiriki kuchangia maendeleo hapa nchini.

Akizungumzia changamoto mbalimbali zinazowakabili Mabalozi hao ikiwa ni pamoja na uchakavu wa baadhi ya majengo ya balozi, Mhe. Kabudi alieleza kuwa Wizara inaendelea kutafuta suluhisho la kudumu kwa changamoto hizo.

Akizungumza kwa niaba ya Mabalozi, Kiongozi wa Mabalozi hao, Mhe. Naimi Aziz, Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia alipongeza jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano kwa kuanzisha na kukamilisha miradi mbalimbali ya maendeleo ambayo Mabalozi walipata fursa ya kuitembelea. Alisema kuwa, miradi hiyo ni chachu ya maendeleo katika kuifikisha Tanzania kwenye uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

Tunaipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kwa kuanzisha miradi mikubwa ya kimkakati. Tumepata fursa ya kujionea miradi hiyo ikiwemo ile ya ujenzi wa barabara, reli na umeme. Kimsingi miradi hii inalenga kumwondolea umaskini Mtanzania kwa vile itarahisha usafirishaji na kumwezessha mkulima kusafirisha kwa urahisi mazao yake kutoka sehemu moja kwenda nyingine kupitia miundombinu hiyo.

Pia aliipongeza Serikali kupitia Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa kufanikisha Mkutano wa 39 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kufanyika nchini kwa mafaniko makubwa.

Imetolewa na:

Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dar es Salaam
20 Agosti 2019


Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatano 21 August

























Share:

Tuesday, 20 August 2019

Polisi Iringa Wamshikilia Mwanamke Aliyekutwa Akiwa Kifua Wazi, Ungo Katika Paa La Nyumba Ya Mchungaji

Na Datus Mahendeka, Jeshi la Polisi
JESHI la Polisi Mkoa wa Iringa linamshikilia na kumhoji mwanamke Kabula Masunga(41), anayedaiwa kufanya ushirikiana baada yakukutwa kwenye paa la nyumba ya Mchungaji Jeremia Charles saa 11 alfajiri.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa Juma Bwire amesema leo Agosti 20,2019 kuwa mwanamke huyo anatuhumiwa kufanya ushirikina huo eneo la Isele Ilula wilayani Kilolo mkoani Iringa na kusababisha taharuki kwa wakazi wa maeneo hayo.

Amefafanua mwanamke huyo ambaye ni mpagani na mkazi wa Morogoro alikutwa akiwa katika mazingira hayo akiwa amejifunga mavazi ya rangi nyekundu na nyeusi lakini kifua aliacha wazi.

"Pia alikutwa akiwa na ungo uliyofungwa kitambaa ya rangi nyeusi na nyekundu.Amekutwa pia na pembe la ng'ombe na alijifunga hirizi mikononi. Mwanamke huyo alikuwa na wenzake wanne inaodaiwa alikuwa anasafiri nao kwa kutumia ungo,"amesema .

Kamanda Bwire amesema kwa sasa wanaendelea kumhoji zaidi ili kufahamu lengo la kufanya ushirikina huo.


Share:

Okoa Ndoa Yako Na Afya Yako Sasa Kwa Kutumia Dawa Bora Ya Nguvu Za Kiume Na Kisukari

Ni dawa zilizopimwa na mkemia na kupewa no 341/VOL,XV/36 na TFDA no 0127/F/F/1819/ MTINJETINJE ni dawa ya kisukari .....Hurudisha kongosho katika hali ya kawaidi hata kama limefeli haijalishi unatumia vidonge au sindano za insulin, itaifanya sukari kuwa normal

SUPER MAJINJA ni dawa inayotibu nguvu za kiume yani matatizo yafatayo (1) kushindwa kurudia tendo na mwili kuchoka (2)kuwai kufika kabla ya  mwenzi wako (3)maumbile ya kiume kulegea na kusinyaa (4)maumbile ya kiume  kuingia ndani na kuwa mafupi kwa wale walio jichua (5)miuungurumo ya tumbo,ngiri,kukosa choo,kiuno kuuma

ACHA KUONGOPEWA SASA DAWA HIZI NI TOFAUTI NA ULIZOWAI KUTUMIA

NJOO OFISINI KWANGU MBAGALA KARIBU NA BENK YA KCB NA mwanza yupo wakala piga simu ya DR AGU whatsapp 0783185060. 0620113431


Share:

Je, Wewe ni Mwathirika wa Kujichua?... Soma Hapa

🔖Asilimia 45-80 ya wanaume wapo tofauti na wengine kwa kutowatimizia vyema wake au wapenz wao na kuwasababishia kutoka nje ya mahusiano yao.
------------------
🔖NINI CHANZO CHA HAYO?

📌Kupiga punyeto
,Ngiri,

Vidonda vya tumbo,

📌Korodani moja kuvimba,

📌 Msongo wa mawazo,

📌Presha, Magonjwa ya zinaa,

 ðŸ“ŒKufanyiwa tohara
ukiwa na umri mkubwa,

📌Kisukari.
------------------

💉DR. KHAFIZ Sasa anakuletea tiba sahihi ya tatizo la Nguvu za kiume.na maumbile mafupi
-------------------

💊MUJARABU :Hii hutibu na kuponya kabisa tatizo la Nguvu za kiume, utakuwa na uwezo wa kufanya tendo la ndoa zaidi ya mara tatu bila kuchoka 
------------------
📌inazalisha homoni kwa mwingi na kuku fanya uwe nambegu nyingi zenye vimeleo vyauzazi vilivo koma
------------------
📌 itakufanya uchelewe kufika kileleni kwa mda wa dk 20-45. Dawa hii imechanganywa na miti 18,Hata wazee wenye umri mkubwa wa zaidi ya miaka 85 wanapona kabisa okoa mahusiano yako, ndoa yako sasa.
------------------
📌TIBA YA KUDUMU

 -----------------
📌TUMIALEO UWONE MAJABU YAKE

------------------
🌠Pia tunadawa za Kupandisha nyota , Uzazi, Pumu, Malaria sugu, miguu kuwaka moto, Kaswende, Kisonono  na mvuto wa mpenzi.bishara na zindiko
--------------------
 ðŸ’‰DR.KHAFIZ ANAPATIKANA DAR-ES-SALAM SM 0716948950 kwa wale wa mikoani mingine huduma hii utaipata popote ulipo.


Share:

Katibu Mkuu Mifugo Asisitiza Ukusanyaji Mapato.

Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Profesa Elisante Ole Gabriel, amezitaka taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo kuimarisha ukusanyaji wa mapato kwa njia ya kielektroniki ili zitoe gawio serikalini.

Profesa Gabriel, ameyasema hayo jijini Dodoma katika kikao cha majadiliano kati ya wataalamu wa sekta za Mifugo na uvuvi na wataalamu kutoka taasisi binafsi ya Trade Mark East Africa yenye lengo la kusaidia uboreshaji wa mifumo ya ukusanyaji wa mapato ya serikali kwa njia ya kielekroniki.

Amesema lengo ni kuhakikisha Tanzania inainuka kiuchumi kupitia kudhibiti mapato kwani kumekuwepo na upotevu mkubwa wa mapato uliotokana na kukosekana kwa njia imara za ukusanyaji.

Profesa Gabriel, ametolea mfano mnada wa Maswa ambao kabla ya udhibiti wa mapato ulikuwa ukikusanya sh. 756,000 kwa siku na baada ya udhibiti yameongezeka na kufikia sh. 7,028,000 kwa siku.

Kwa upande wa mnada wa Halmashauri ya Bariadi, mkoani Simiyu, Profesa Gabriel amesema kabla ulikuwa ukikusanya sh. Milioni 2,500,000 na baada yameongezeka hadi sh. 3,000,000 kwa siku na kufikia shilingi 14,950,000 kwa siku.

Aidha amewataka wataalamu hao baada ya kuwa na mifumo imara ya ukusanyaji wa mapato, pia kutafuta namna nyingine bora za kuongeza wigo wa ukusanyaji mapato, akitolea mfano utalii kwenye sekta za Mifugo na Uvuvi nchini.

Ameongeza kwa kusisitiza suala la elimu kutolewa kwa wafugaji na Wavuvi ambao ndiyo wadau wakuu wa sekta za mifugo na uvivu.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkazi wa Trade Mark East Africa nchini, John Ulanga, amesema haijawahi kutokea katika taasisi zote walizofanya nazo kazi kuona utayari na ushirikiano kama walioupata kwa wizara ya mifugo na uvuvi.

Amesema lazima kuwepo na utayari wa kubadilika fikra katika utendaji ndani ya Wizara na taasisi zake vinginevyo mifumo hiyo haitakuwa na faida yoyote.


Share:

PICHA: Rais Pombe Magufuli Atembelea Mamlaka Ya Maabara Ya Mkemia Mkuu Wa Serikali Jijini Dar Es Salaam Leo

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametembelea na kukagua utendaji kazi wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali iliyopo karibu na Hospitali Kuu ya Taasisi ya Saratani Ocean road Jijini Dar es salaam pamoja na kuzungumza na wafanyakazi wa Ofisi hiyo.



Share:

MWENGE WA UHURU KUZINDUA MIRADI YA SH. BILIONI 1.162 WILAYANI IKUNGI


Mwenge wa Uhuru unaotarajiwa kuwasili wilayani Ikungi mkoani Singida kesho asubuhi utazindua miradi ya maendeleo yenye thamani ya zaidi ya sh. bilioni 1.162 .


Taarifa hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya hiyo Edward Mpogolo wakati akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusu ukimbizaji wa mwenge wa Uhuru katika wilaya yake.

Mpogolo alisema mara baada ya kuwasili kwa mwenge huo na kupokelewa Kijiji cha Mkiwa patazinduliwa madarasa mawili ya Shule ya Msingi Darajani na kisha kuelekea kutembelea mradi wa upimaji wa virusi vya na elimu ya uchaguzi wa Serikali za mitaa uliopo katika Kijiji cha Issuna.

" Baada ya kutembelea mradi huo wa kijiji cha Issuna watakwenda kuweka jiwe la msingi ujenzi wa mnara wa kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere utakao jengwa Ikungi mjini",alisema Mpogolo.

Alisema baada ya hapo watakwenda kuweka jiwe la msingi wa mtandao wa maji Kijiji cha Ighuna pamoja na kutembelea mapambano dhidi ya dawa za kulevya Kituo cha Polisi cha Puma.

Aliongeza kuwa baada ya hapo watakwenda kukagua ujenzi wa Kituo cha Afya cha Sepuka na kufuatiwa na usomaji wa risala ya utii eneo la mkesha wa mwenge Uwanja wa Ofisi ya Mtendaji Kata ya Sepuka.

Mpogolo amewaomba wananchi wa wilaya hiyo kujitokeza kwa wingi kuupokea mwenge huo na kushuhudiwa miradi hiyo itakapo kuwa ikizinduliwa.

Na Dotto Mwaibale, Singida
Share:

Ziara ya Biteko Lindi : Kampuni ya Indiana yajisalimisha

Na Issa Mtuwa Dodoma
Kufuatia ziara aliyofanya Waziri wa Madini Doto Biteko mkoani Lindi na Mtwara hususani wilaya ya Nachingwea na kuibua sintofahamu juu ya Kampuni ya Ngwena Ltd kuhusu ushirika wake na Kampuni ya Indiana kutoka Australia, suala hilo limefanya Uongozi wa Kampuni ya Indiana kupitia Mkurugenzi wake Bob Adam kuja nchini kukutana na Waziri wa Madini ili kujadili kuhusu ushirika wao na Ngwena Ltd.
 
Agosti 19, 2019 Waziri Biteko amekutana na kuzungumza na mkurugenzi huyo kuhusu ushirika wao wa kuunganisha kampuni hizo bila kuijulisha wizara. 
 
Waziri Biteko amembana mwekezaji huyo kwa hoja tatu zilizopelekea kutopatikana  majibu ya moja kwa moja kutokana na kuto kuwepo kwa mwakilishi wa upande wa pili wa  kampuni ya Ngwena Ltd. 
 
Hoja hizo ambazo waziri Biteko alitaka kufahamu kutoka kwa kampuni ya Indiana ni; mosi, makubaliano kati ya Indiana na Ngwena hayana taarifa kwa Wizara, ni kwa nini waliamua kuunganisha bila kuijulisha Wizara wakati kampuni moja ni ya Kitanzania na nyingine ni ya kigeni... Mbili, Wizara inataka kuona makubaliano yao ya kimaslahi (fair deal) baina ya pande zote ili pia wizara ijue serikali inafaidikaje? Na tatu, kampuni husika zinatunzaje shehena kubwa ya sampuli za madini bila kuijulisha Taasisi ya  Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) ambayo ndio yenye dhamana ya utunzaji? 
 
Aidha, waziri Biteko aliendelea kuibana kampuni hiyo ya Indiana kupitia mkurugenzi wake huyo kwa kumuuliza uhusika wake katika kampuni ya Ngwena Ltd huku Mkurugenzi wa huduma za Sheria wa Wizara ya Madini Edwin Igenge akimhoji ni tangu lini ushirika wake na Ngwena ulianza? Je, ni kabla au baada ya marekebisho ya Sheria ya Mwaka 2017? 
 
Akitoa majibu kwa baadhi ya hoja na maswali, Bob Adam amesema Indiana ndio inayomiliki Ngwena Ltd na kufadhili kifedha na masuala mengine. Kuhusu kabla au baada ya marekebisho ya sheria ya 2017 Adam hakuwa na uhakika wa moja kwa moja na alisema mpaka arejee kwenye nyaraka ili ajiridhshe.
 
“Kampuni yetu ndio inayo miliki Ngwena Ltd kwa maana Indiana inamiliki 60% ya hisa zote na ndio maana ninasema Indiana inamiliki Ngwena,” amesema Bob Adam.
 
Kutokana na hoja tatu za msingi kutopatiwa majibu ya kuridhisha kwa kukosekana kwa Uongozi wa Ngwena Ltd katika kikao hicho, Waziri Biteko ametaka kupangwa kwa tarehe nyingine huku akimtaka Adam kurudi tena nchini   akiwa na uongozi wa Ngwena Ltd ili kufahamu kiundani juu ya makubaliano yao kwani mpaka sasa kampuni inayotambuliwa na wizara ni Ngwena Ltd na siyo Indiana. 
 
Wiki iliyopita Waziri wa Madini alifanya ziara mkoani Lindi wilaya ya Nachingwea na kutembelea eneo la Nditi ambalo kampuni ya Ngwena Ltd imewekeza, moja ya mambo aliyokutana nayo ni uwepo wa makubaliano (Joint-Venture) kati ya kampuni ya Ngwena Ltd na Indiana kutoka Australia kinyume cha sheria na uwepo wa shehena kubwa ya sampuli za madini zilizohifadhiwa kinyume cha sheria.


Share:

Ufahamu Ugonjwa Wa Ngiri Na Tiba Yake

Tatizo la Ngiri Linavyosababisha Upungufu wa Nguvu za Kiume na Maumbile Kusinyaa, Dalili zake Hizi Hapa..Makala
51 minutes ago

Ngiri au Hernia ni aina ya ugonjwa ambao unampata mtu baada ya misuli au kuta za tishu mwilini zinazoshikiria au kubeba viungo (organs) fulani mwilini kupoteza uimara wake au kuwa na uwazi (Opening) na hivyo kusababisha viungo hivyo kutoshikiriwa ipasavyo katika sehemu vinapostahili kuwepo.

Katika mwili wa binadamu, maeneo ambayo tatizo hili hutokea mara kwa mara ni maeneo ya tumboni, katika eneo la kinena, eneo la paja kwa juu na pia ngiri inaweza kutokea katika eneo ambalo mtu alifanyiwa upasuaji (operesheni).

Dalili za Ngiri
Tumbo kuunguruma, kiuno kuuma, kupata choo kama cha mbuzi, kushindwa kufanya tendo la ndoa, mishipa ya uume kulegea, kutokuwa na hamu ya kulundia tendo la ndoa, korondani moja kuvimba, mgongo kuuma.

Dalili zingine za ugojwa wa ngiri ni pamoja na;

Uvimbe unaoteremka kuingia ndani ya korodani unaojulikana kitaalamu kama Direct Scoratal inguinal Hernia.


Uvimbe unaojitokeza tumboni na kuteremka hadi ndani ya korodani, uvimbe huu hauumi na unaweza kurudishwa kwa urahisi iwapo mgonjwa atalala chali na kusukuma kwa vidole, uvimbe huu.


Na pindi ukikubali kurudi ndani ndipo unapoitwa Reduible direct scrotal inguinal hernia.


Na pia endapo utashindikana kurudi tumboni ndipo unapoitwa Irreduible direct scrotal inguinal hernia.


Ugojwa huu wa ngiri unaweza kutibika

Mpate mpenzi wako unayempenda na kumfunga mume,mke mpenzi asitoke kwa mwingine .

Kwa Ushauri na Msaada wa Wasaliana na  0714006521


Share:

Mitambo Ya Kunyanyulia Mizigo Ya Ujenzi mkubwa wa umeme wa Julius Nyerere Hydro Power Project (JN HPP). Yazinduliwa Rasmi Fuga

Na.Paschal Dotto-MAELEZO
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe.Atashasta Nditiye amazindua Rasmi Vifaa vya Kunyanyulia Makontena ya Mizigo na Vifaa vizito vya utekelezaji wa ujenzi wa Mradi mkubwa wa umeme wa Julius Nyerere Hydro Power Project (JN HPP).

Akizungumza jana katika stesheni ya fuga, Waziri Nditiye alisema kuwa Serikali imenunua vifaa hivyo ambavyo ni Reach Stacker 2 zenye uwezo wa kunyanyua tani 45, Mobile crane yenye uwezo wa tani 15 na Forklift 2 zenye uwezo wa tani 5 na zimegharimu Tzs Bilioni 3.5

“Vifaa hivi vimenunuliwa na Serikali ili kuiwezesha TAZARA kutekeleza majukumu iliyopewa ya upokeaji makontena ya mizigo mizito ya ujenzi wa bwawa la kufua umeme la JN HPP, katika mto Rufiji, mradi utakozalisha Megawati 2,115 na kuiwezesha Tanzania kufikia uchumi wa viwanda”, Naibu Waziri Nditiye.

Aidha, Waziri Nditiye alisema kuwa Serikali itaendelea kuishika mkono TAZARA ili kuhakikisha inafanya kazi ufanisi mkubwa kwenye utekelezaji wa mradi wa kufua umeme  JN HPP na ndiyo maana imetoa Tsh. Bilioni 10 ili kununua Traction Motors 42 kwa ajili ya vichwa saba vya treni za masafa marefu na sogeza ambazo zitaanza kuwasili mwezi oktaoba.

Waziri Nditiye aliongeza kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inawahakikishia wafanyakazi wa Mamlaka ya Reli Tanzania na Zambia (TAZARA)kuwa itaendelea kulipa mishahara yote kwa kipindi chote cha mwaka wa fedha 2019/2020 na tayari imetanga kiasi cha shilingi bilioni 14.9 zimetengwa.

Kwa upande wake Meneja Mkuu wa Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) alisema kuwa ni  jambo kubwa na heshima kwa Mamlaka hiyo kupewa majukumu ya kupoea mizigo ya utekelezaji wa ujenzi wa Mradi wa Umeme JN HPP.

“Napenda kusema kuwa Serikali ya Tanzania, Chini ya Rais Dkt.John Pombe Magufuli, ilituamini na kutupatia kiasi cha Shilingi Bilioni tano ili kukarabati stesheni ya Fuga kwa kujenga Stendi ya kupokea na kusafirisha mizigo, kununua vifaa vitakavyosaidia kunyanyua mizigo hiyo kwa ufanisi mkubwa”, Mhandisi. Bruno Chingandu.

Mhandisi Chingandu alisema kuwa vifaa hivyo viyakuwa na uwezo mkubwa wa kutosheleza mahitaji ya kupokea mizigo ya ujenzi wa mradi mkubwa wa kihistoria wa kufua umeme  wa JN HPP, kwani tani kati ya 5 mpaka 45 zitanayanyuliwa na vifaa hivyo.

Aidha, Mhandisi Chingandu alisema kuwa Serikali imetekeleza kwa vitendo ununuzi wa Traction motor 42 kwa ajili ya treni ya masafa marefu kwa kutoa Tsh.Bilioni 10, hivyo itaiwezesha TAZARA kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi mkubwa na kuliwezesha Shirika hili kurejera tena katika utendaji mkubwa.
 
Naye Meneja wa TAZARA Mkoa wa Tanzania, Fuad Abbdalah, alisema kwamba Serikali imewapatia Fedha za ujenzi na ununuzi wa vifaa ni heshima kubwa kwa Shirika hilo kwani limeingia kwenye historia ya mageuzi ya Serikali ya Awamu ya Tano.

“Leo tunashuhudia kitendo kikubwa cha kuzindua hizi mashine tano za kunyanyulia mizigo mizito ya ujenzi wa Mradi wa kihistoria wa JN HPP, Mashine hizi zina uwezo mkubwa wa kunyanyua Tani 5 mpaka 45, uwezo stahiki kabisa kuhudumia mizigo yote inayohitajika kwenye mradi wa umeme mto Rufiji”; Fuad Abbdalah, Meneja TAZARA mkoa wa Tanzania 

Fuad aliongeza kuwa Serikali imeliamini Shirika hilo na Rais wa Jamhuri ya Muungano ameahidi kurudisha uafanisi wa utendaji wake na katika ziara yake ya kwenda kuzindua Mradi wa umeme JN HPP alisema  atahakikisha anashirikiana na Rais wa Zambia ili kurudisha heshima ya TAZARA.

Kwa upande wake Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt.Hassan Abbasi alisema Serikali imetekeza ukarabati wa stesheni ya kupokea na kushushia mizigo ya Fuga itayosaidia ujenzi wa Mradi wa Umeme wa JN HPP kufanikiwa kwa haraka Zaidi.

“Tunatekeleza Uboreshaji huu wa Stesheni ya Fuga, tumeleta mitambo ya kisasa mikubwa kabisa ambayo imedhaminiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ajili ya kuhudumia ujenzi wa bwawa la kufua umeme JN HPP, kwa hiyo mitambo hii imefika, inafanya kazi na inasambazwa na Kampuni ya kizawa”, Dkt.Abbasi.

Mwisho.



Share:

WADAIWA SUGU WA BENKI YA TIB WATAKIWA KUREJESHA FEDHA

Na. Peter Haule, WFM, Dar es Salaam

Serikali imeitaka Benki ya TIB kuhakikisha inawafuatilia kwa karibu wadaiwa sugu wote wa Benki hiyo ili waweze kurejesha fedha wanazodaiwa ili kuongeza ukwasi wa taasisi.

Hayo yameelezwa jijiji Dar es Salaam na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Khatibu Kazungu, alipofanya ziara katika Benki hiyo ikiwa ni sehemu ya ufuatiliaji wa utekelezaji wa bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2018/19 katika taasisi zilizopo chini ya Wizara ya Fedha na Mipango ili kujua changamoto na njia za kuzitatua kwa mwaka wa fedha 2019/20.

Dkt. Kazungu amesema, wadaiwa sugu wanaodaiwa na Benki ya TIB warejeshe fedha walizochukua ili kuongeza ukwasi wa Benki hiyo na kuendelea kukidhi vigezo vya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) inavyoviangalia katika kudhibiti taasisi za kibenki nchini.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya TIB, Bw. Charles Singili, alisema kuwa ni vizuri watu wazingatie mikataba wanayoingia na Benki wakati wa kukopa fedha, kwa kujenga nidhamu ya matumizi ili kuzitumia katika lengo husika na kukuza uchumi wa mlengwa hatimaye kuzirudisha kwa wakati ili kutoa fursa kwa wengine kunufaika na mikopo hiyo.

“Benki ya TIB ni taasisi ya Serikali na ni ya kisera, imeundwa mahususi kwa ajili ya kuchochea maendeleo ya uwekezaji wa ndani ya nchi hususani katika kufanikisha utekelezaji wa miradi ya Serikali na miradi ya sekta binafsi”, alieleza Bw. Singili.

Bw. Singili alisema kuwa, Benki ya TIB ilianzishwa ili kukabiliana na uhitaji wa mitaji ya muda mrefu kwa kuwa benki nyingi nchini ni za kibiashara na mitaji inayotoa kwa wateja wake ni ya muda mfupi.

Alisema kuwa mikopo inayotolewa na benki hiyo inaendana na ajenda ya Serikali ya kuboresha miundombinu wezeshi pamoja na uwekezaji kwenye viwanda, hivyo ajenda hiyo haiwezi kufikiwa kwa mikopo ya mitaji ya muda mfupi.

“Ukitazama Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka mitano 2016/17 hadi 2020/21 kwa fedha iliyopangwa kwa ajili ya kutekeleza mpango huo haiwezi kupatikana kutokana na  makusanyo ya kodi pekee hivyo kuna kila sababu kwa taasisi hii kama Benki ya Maendeleo kuangalia njia mbadala hususani kupitia kwenye masoko ya mitaji ili kusaidia juhudi za Serikali katika upatikanaji wa fedha hizo”, aliongeza Bw. Singili.

Bw. Singili ameahidi kuyafanyia kazi maagizo ya Naibu Katibu Mkuu, Dkt. Kazungu, hususani katika kukabiliana na mikopo chechefu kwa kuongeza nguvu katika kuwafuatilia wadaiwa sugu.

Aidha amempongeza Naibu Katibu Mkuu huyo, kwa kufanya ziara za kiutendaji katika taasisi yake, kwa kuwa zinasaidia katika kubadilishana mawazo na kujua matarajio na changamoto za taasisi katika mtazamo wa pamoja wa kuzitatua.

Mwisho


Share:

CPB Yampongeza Rais Magufuli Kwa Kuchaguliwa Kuwa Mwenyekiti Mpya Wa SADC

Salamu  za pongezi za kuchaguliwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kuwa Mwenyekiti Mpya wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika SADC zimeendelea kumiminika leo Agosti 20, 2019 ambapo Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB) nayo imetoa salamu zake za pongezi.

"Bodi ya Wakurugenzi na Menejimenti ya Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB) tunatoa pongezi nyingi kwako Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti Mpya wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika SADC kwenye kikao cha 39 cha Wakuu wa Nchi za SADC jijini Dar es Salaam 2019.

Tunakutakia Mheshimiwa Rais kazi njema na yenye ufanisi katika kutekeelza majukumu hayo mapya." Taarifa hiyo imesema.

Katika kikao cha kihistoria cha siku mbili kilichofanyika jijini Dar es Salaam Agosti 17 na 18, 2019, Wakuu hao wa Nchi walimchagua Dkt. Magufuli kuwa Mwenyekiti wa SADC kwa kipoindi cha mwaka mmoja ambapo aliyekuwa Mwenyekiti wa SADC Mhe. Dkt. Hage Gengob, ambaye ni Rais wa Namibia alimkabidhi uenyekiti huo.




Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger