Sunday, 11 August 2019

Kauli 12 Alizozitoa Waziri Mkuu Majaliwa Wakati wa Tukio la Kuwatambua Waliofariki kwa Moto Morogoro

1.Niko mbele yenu kumwakilisha Rais  Magufuli kuungana nanyi siku hii ya huzuni kubwa, Rais alipokea taarifa hii jana. Kwa taarifa mpaka sasa waliofariki ni 69, tumepata taarifa tukiwa hapa mwenzetu 1 aliyebebwa kwa Helikopta amekufa njiani.

2.Rais amepata taarifa hizi kwa masikito makubwa, ameendelea kuwaombea marehemu na majeruhi, amewaomba utulivu ndugu, jamaa, na marafiki mlioguswa na tukio hili, kwa uzito wa jambo hili amelitangazia taifa siku 3 za maombelezo kuanzia jana.

3.Yeye anaugeni mkubwa wa Marais 16 wanaoingia nchini kwa maandalizi ya mkutano wa SADC, kwa hiyo mtambue kwamba uzito wa kuwapokea wenzake pamoja na tatizo hili kubwa na kwa kuwa sisi wasaidizi wake tupo akaamua kunileta kwenu. 

4.Nimepita hapo hali si nzuri ndugu zetu wameungua sana, na iko hatari wengine tusiwafahamu kabisa, lakini hatutawanyima nafasi kuwatambua ndugu zetu, na kwa kuwa tulikuwa nao tangu jana asubuhi, tutawapa nafasi ya kuwatambua.

5.Kama una mashaka kuna ndugu yako humuoni tangu jana, tumekupa nafasi ya kuja kutoa taarifa, na tutakupima DNA, ili kutambua ndugu yake kwa sababu tumechukua vinasaba vya marehemu wote ili kuwatambua.

6.Nitaunda tume ianze kuchunguza kuanzia leo hadi Ijumaa, ichambue vizuri na hata kama mimi nitakuwa sijawajibika wanitaje, baada ya hapo serikali tutajua cha kufanya.

7.Manispaa kuna kitengo cha Fire, japo najua walikuja kwa kuzima, ila je walikuja baada ya muda gani? tumesisitiza umakini na uwajibikaji, nasikia tumeokoa mafuta sasa tumeokoa yakiwa yameisha? nitaunda tume wanijibu haya maswali madogo.

8.Hata kama mimi nimehusika wanitaje tu, hatuwezi likapita hivi. 

9.Ajali za aina hii Tanzania si mara ya kwanza ilitokea Mbeya niwasihi Watanzania ukiona gari limeanguka usilitumie kama fursa, ukawaokee binadamu walio pale. 

10. Je huu muda ambao walikutana hawa ndugu zetu waliotangulia mbele za haki kwa ajili kutoa mafuta, ni nani aliwazuia? mimi ninajua Trafiki huwa wanakuwa na haraka sana, ajali inapotokea, nani alihusika kuwazuia.? 

11.Vyombo vya habari mnaendelea kuhabarisha watanzania, kwenye vyombo vya habari tuelewane jambo moja kuhusu takwimu, jana zilikuwa zinachanganya msiseme suala la takwimu, anaeyeweza kusema ni Mkuu wa Mkoa. 

12.Naogopa msije mkaingia kwenye sheria ya takwimu, kuanzia sasa chukueni za Mkuu wa Mkoa, mlisababisha jana nikazungumza uongo nikiwa na wasomi wa Vyuo Vikuu, nikaona taarifa wako 100 ikaja nyingine 120, na mimi nikataja hiyo idadi.

 

 

 


Share:

LIVE: Tukio la Utambuzi na Kuaga Waliofariki Morogoro Kwa Ajali ya Moto

LIVE:    Tukio la Utambuzi  na Kuaga  Waliofariki Morogoro Kwa Ajali ya Moto


Share:

PICHA: Wananchi Wajitokeza kwa Wingi Kutambua Miili ya Wapendwa Wetu Waliofariki kwa Moto Morogoro

Wananchi wamejitokeza kwa katika viwanja vya Shule ya Sekondari ya Morogoro karibu kabisa na chumba cha kihifadhia maiti cha hospitali ya mkoa, ambapo zoezi la kutambua na  kuaga miili  ya waliofariki kwa ajali linafanyika.

Ajali hiyo ilitokea jana Jumamosi Agosti 10, 2019 katika kijiji cha Itigi, Msamvu mkoani Morogoro   baada ya lori la mafuta kupinduka na kuwaka moto muda mfupi baada ya watu kuanza kuchota mafuta.



Share:

Waziri Mkuu Atua Morogoro....Vifo Vyafika 68

Waziri Mkuu  Kassim Majaliwa ameungana na viongozi wengine wa vyama na Serikali mkoani Morogoro kwenye msiba wa kitaifa baada ya kutokea ajali ya moto iliyoua Watanzania 69 hadi leo Jumapili.

Kwa mujibu wa mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dk Stephen Kebwe amesema idadi hiyo imeongezeka kutoka vifo 64 vilivyoripotiwa hadi jana saa 10 jioni hadi vifo 69.

Ajali hiyo ilitokea jana Jumamosi Agosti 10, 2019 katika kijiji cha Itigi, Msamvu mkoani Morogoro   baada ya lori la mafuta kupinduka na kuwaka moto muda mfupi baada ya watu kuanza kuchota mafuta.


Share:

MSD Yakabidhi Madawa Mkoani Morogoro Kwa Ajili Ya Majeruhi Wa Ajali Ya Moto Wa Lori La Mafuta

Timu ya MSD ikiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa MSD Bw. Laurean Bwanakunu wakiwa sambamba na Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Mohamed Kambi, wamewatembelea majeruhi wa ajali ya moto, iliyosababishwa na mlipuko wa lori la mafuta waliolazwa katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro.

Pamoja na kuwajulia hali majeruhi hao, ujumbe huo pia umelenga kufuatilia na kufahamu misaada ya haraka ya kitabibu inayohitajika kwa sasa hospitalini hapo ili kusaidia majeruhi.

Aidha, wajumbe hao, wamewasilisha msaada wa dawa na vifaa tiba kwenye hospitali hiyo.


Share:

MSD YAKABIDHI MADAWA MKOANI MOROGORO KWA AJILI YA MAJERUHI WA AJALI YA MOTO WA LORI LA MAFUTA


Mkurugenzi Mkuu wa MSD Laurean Bwanakunu akiwa pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja na Shughuli za Kanda wa MSD Salome Mallamia na Meneja wa MSD Kanda ya Dar es Salaam inayohudumia mkoa wa Morogoro Celestine Haule wakiendelea kupokea dawa zaidi za kukabidhi hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Morogoro kwa ajili ya kuhudumia majeruhi

…………………………………………………

Timu ya MSD ikiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa MSD Bw. Laurean Bwanakunu wakiwa sambamba na Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Mohamed Kambi, wamewatembelea majeruhi wa ajali ya moto, iliyosababishwa na mlipuko wa lori la mafuta waliolazwa katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro.

Pamoja na kuwajulia hali majeruhi hao, ujumbe huo pia umelenga kufuatilia na kufahamu misaada ya haraka ya kitabibu inayohitajika kwa sasa hospitalini hapo ili kusaidia majeruhi.

Aidha, wajumbe hao, wamewasilisha msaada wa dawa na vifaa tiba kwenye hospitali hiyo.


Share:

Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Lataka majeruhi ajali ya moto Morogoro washitakiwe

Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) limeeleza kushtushwa na taarifa za vifo vya Watanzania zaidi ya 60 walioungua moto wakati wakichota mafuta kutoka katika lori lililopata ajali eneo la Msamvu, Morogoro, jana Agosti 10, 2019 likitaka waliojeruhia kushitakiwa watakapopona majeraha yao.

Taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari jana usiku Jumamosi na Kaimu Mwenyekiti Jukwaa hilo, Deodatus Balile ilisema vifo hivyo vimetokana na tabia mbaya iliyojengeka kwa baadhi ya watu kuchukulia ajali kama fursa ya kujipatia mali kwa njia haramu iliyoanza miaka ya hivi karibuni.

“Tumeshuhudia picha za watu waliofariki kwa kuungua moto zikirushwa kwenye mitandao ya kijamii kinyume cha maadili ya taaluma ya uandishi wa habari na upashanaji habari. Tunakemea tabia hii na kuitaka jamii iache mara moja tabia hii ya kinyama isiyo ya utu,” alisema Balile.

Balile pia alizungumzia watu zaidi ya 70 waliojeruhiwa katika ajali hiyo akisema wakipona wajiepushe na tabia hii ya uporaji.

“Ikilazimu, wote watakaopona katika ajali hii washitakiwe kwa mujibu wa sheria ili iwe fundisho kwao na wengine kuwa ikitokea ajali tunapaswa kusaidia majeruhi na kuokoa mali zao badala ya kupora,” alisema.


Share:

MAJERUHI WA AJALI YA MOTO MOROGORO WAANZA MATIBABU MUHIMBILI

Share:

MILIONI MIA MBILI ZATUMIKA KULETA MAENDELEO KATA YA KIHESA.

Share:

SERIKALI YAITAKA NIC KUCHANGIA PATO LA TAIFA KWA ZAIDI YA ASILIMIA TANO

 Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Shirika la Bima la Taifa- NIC, Dkt. Elirehema Doniye (kulia), akikabidhiwa rasmi ofisi hiyo na aliyekuwa Mkurugenzi wa Shirika hilo, Bw. Sam Kamanga, jijini Dar es Salaam.
 Aliyekuwa Mkurugenzi wa Shirika la Bima la Taifa- NIC, Bw. Sam Kamanga (kushoto), akitoa maelezo wakati wa kukabidhi rasmi ofisi kwa Mkurugenzi mpya wa Shirika hilo, Dkt. Dkt. Elirehema Doniye (wa pili kushoto).
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Khatibu Kazungu (kushoto) na Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Bima la Taifa- NIC, Bw. Laston Msongole, wakishuhudia makabidhiano ya ofisi kati ya aliyekuwa Mkurugenzi wa Shirika  la NIC. Bw. Sam Kamanga na Mkurugenzi Mtendaji mpya waShirika hilo, Dkt. Elirehema Doniye.
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Khatibu Kazungu (kushoto), akimpongeza Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Shirika la Bima Tanzania- NIC, Dkt. Elirehema Doniye, baada ya kukabidhiwa ofisi rasmi, jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Bima la Taifa- NIC, Bw. Laston Msongole (kulia) akizungumza jambo na Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Shirika hilo, Dkt. Elirehema Doniye, kabla ya kukabidhiwa rasmi Ofisi, jijini Dar es Salaam
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Khatibu Kazungu (kushoto), akipeana mkono na Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Bima la Taifa- NIC, Bw. Laston Msongole (kulia), baada ya kushuhudia makabidhiano ya ofisi kati ya aliyekuwa Mkurugenzi wa Shirika hilo, Bw. Sam Kamanga (hayupo pichani) na Mkurugenzi mpya , Dkt. Elirehema Doniye (katikati), jijini Dar es Salaam.
(Picha na Peter Haule, WFM, Dar es salaam)Na. Peter Haule, WFM, Dar es Salaam
Serikali imelitaka Shirika la Bima la Taifa- NIC kuhakikisha mchango wake unafikia zaidi ya asilimia tano katika pato taifa badala ya chini ya asilimia moja ya sasa ili kuweza kuchochea kasi ya ukuaji wa Sekta ya Fedha nchini. 
Hayo yamebainishwa Jijini Dar es Salaam na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Khatibu Kazungu, wakati akishuhudia kukabidhiwa rasmi Ofisi Mkurugenzi mpya wa Shirika la Bima la Taifa- NIC, Dkt. Elirehema Doniye.
Dkt. Kazungu amesema kuwa Shirika la NIC, linatakiwa kujipanga kimkakati kuwa chanzo kizuri cha mapato na kuhakikisha linawafikia wananchi wengi zaidi hususani katika Sekta ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi.
Aidha amelitaka Shirika la NIC kuhakikisha linajipanga kiushindani kutoa bima ya miradi yote mikubwa ya kimkakati inayotekelezwa na Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli. 
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya NIC, Bw. Laston Msongole, amesema kuwa Shirika hilo linawagusa watanzania wote kwa kuwa linatoa huduma zake Tanzania Bara na  Zanzibar.
Alisema kuwa Shirika la NIC, limeanza kufanya vizuri katika soko hivyo ni jukumu la Mkurugenzi mpya kuendeleza juhudi hizo kwa kuwa hapo awali lilikuwa miongoni mwa mashirika yaliyotakiwa kubinafsishwa, kwa kuona umuhimu wake Shirika hilo limebaki kuwa la wananchi na sasa linatakiwa kujiendesha kibiashara.
Naye Mkurugenzi mpya wa Shirika hilo Dkt. Elirehema Doniye, amesema kuwa anafanya jitihada kuhakikisha  Shirika hilo linaongeza ufanisi zaidi ili liweze kuchangia katika pato la Taifa kikamilifu kama alivyoelekeza, Naibu Katibu Mkuu, Dkt. Kazungu.
Alisema kuwa Shirika hilo linajiendesha kibiashara hivyo ni lazima watendaji kufanya kazi kwa nidhamu ya juu, kuwafikia wateja wadogo na wakubwa  na kwenda na kasi ya Serikali ya awamu ya tano.
Aidha aliyekuwa Mkurugenzi wa NIC, Bw. Sam Kamanga, amesema kuwa amemkabidhi Mkurugenzi mpya Shirika ambalo limeanza kufanya vizuri, kwa kuwa tayari kuna bima ya Kilimo ambayo itawafikia wananchi wengi, lakini pia  NIC imepata tuzo mbalimbali hivyo ni jukumu la uongozi mpya kuendeleza mafanikio hayo.
Mwisho
Share:

DC KASESELA ATATUA MGOGORO WA ARDHI WA FAMILIA YA MZEE MWENDA

Share:

Breaking : BODI YA SHIRECU YAVUNJWA KWA UBADHIRIFU WA FEDHA

Richard Luhende
Na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Bodi ya Chama Kikuu cha Ushirika mkoani Shinyanga (SHIRECU) inayoongozwa na Mwenyekiti wake Richard Luhende imevunnjwa kutokana na ubadhirifu wa shilingi millioni 8.9 pamoja na kutumia fedha zingine kinyume cha utaratibu ikiwemo kuweka mhasibu mkuu hewa aliyelipwa kiasi cha shilingi 770,000 ndani ya siku kumi.

Bodi hiyo imevunjwa rasmi jana Jumamosi Agosti 10,2019 na Mrajisi Msaidizi kutoka Vyama vya Ushirika Tanzania ,Josephat Kisamalala wakati akiongoza mkutano mkuu wa SHIRECU baada ya wajumbe 120 waliohudhuria kupiga kura ya kuwakubali au kuwakataa ambapo wajumbe 99 wakiikataa bodi hiyo kuendelea kuwaongoza.

Bodi hiyo ilikuwa ikiongozwa na Richard Luhende (Mwenyekiti), Enock Lyela (makamu mwenyekiti) na Donald Rogers,Dotto Kangoka na Jeremiah Kapolo(wajumbe).

Baada ya bodi hiyo kuvunjwa walichaguliwa majina ya wajumbe wapya saba watakaounda bodi wakiwa wajumbe watano pekee ili kuweza kufikisha mbali chama hicho.

Akifafanua zaidi, mkaguzi mwandamizi kutoka COASCO makao makuu Dodoma Gabriel Msuya alisema agizo la ukaguzi lilitoka kwenye ofisi ya mkuu wa mkoa kwa kuanzia tarehe 19 Novemba mwaka 2018 hadi tarehe 25 Novemba mwaka 2018 walibaini shilingi millioni 8,976,880 za ukarabati wa magari makubwa zilizotumika bila idhini ya mkutano mkuu na kibali cha mrajisi wa vyama vya ushirika.

Pia Msuya alisema katika zoezi la ukarabati wa majengo walibaini dosari kutoandikwa barua kwa mrajisi na shilingi 71,866,100/= zilitumika bila kuidhinishwa sanjari na mfanyakazi Paul Mainga kuwa katika nafasi ya uhasibu mkuu kinyume cha utaratibu na kulipwa kiasi cha shilingi 770,000/=.

Msuya alisema waliangalia uhalali wa fedha zilizotumika katika kulipia matangulizi ya matrekta matatu kiasi cha shilingi 36,000,000 ikiwa ilibaini vyama vitatu pekee vyenye viongozi wake wajumbe wa bodi ndiyo wangekuwa na uwezo wakupata matrekta hayo.


Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainabu Telack alisema kuwa SHIRECU sio taasisi ya mtu mmoja ,serikali iliamua kufufua vyama vya ushirika ili kuwasaidia wakulima na kusimamiwa na mkuu wa mkoa hivyo wajue wanaotenda maovu wako mlangoni mwa jeshi la polisi kwani unatakiwa uaminifu na uadilifu kwa watu wanaowasimamia.
Share:

Rais Magufuli Katangaza Siku Tatu za Maombolezo......Bendera Kupepea Nusu Mlingoti

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ametangaza siku 3 za Maombolezo ya Kitaifa kuanzia Jumamosi kufuatia vifo vya watu zaidi ya 60 vilivyosababishwa na ajali ya kuungua kwa moto wakati wakichota mafuta yaliyokuwa yakimwagika baada ya lori la mafuta kupinduka Mjini Morogoro.

Ajali hiyo imetokea jana majira ya saa 2 asubuhi ambapo lori lenye shehena ya mafuta ya petroli limepinduka jirani na Kituo Kikuu cha Mabasi cha Msamvu Mjini Morogoro wakati dereva alipokuwa akijaribu kumkwepa mwendesha pikipiki.

Pamoja na zaidi ya watu 60 kufariki dunia watu wengine takribani 70 wamejeruhiwa na wanapatiwa matibabu katika hospitali ya Mkoa wa Morogoro na Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam.

Rais Magufuli amemtuma Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa Majaliwa kumwakilisha katika mazishi ya Marehemu wa ajali hiyo yanayotarajiwa kuanza kesho Jumapili tarehe 11 Agosti, 2019.

Katika kipindi cha maombolezo bendera zote zitapeperushwa nusu mlingoti.



Share:

RAIS MAGUFULI ATANGAZA SIKU TATU ZA MAOMBOLEZO KITAIFA VIFO VYA WATU 60 MORO

Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya leo Jumapili 11 August

















Share:

Saturday, 10 August 2019

Maambukizi ya Fangasi katika Sehemu za Siri

Kati ya maambukizi yanayowasumbua wanawake wengi duniani ni maambukizi ya fangasi. Inakisiwa asilimia 75 ya wanawake wote duniani hupata maambukizi haya katika kipindi cha uhai wao.

Maambukizi ya fangasi katika sehemu za siri za mwanamke husababishwa na uwepo wa fangasi wanaojulikana kitaalamu kama Candida albicans. 

Maambukizi haya pia hujulikana kama yeast infection au thrush. Fangasi hupatikana kama vimelea vya kawaida katika mdomo, mpira wa kupitisha chakula sehemu inayojulikana kama pharynx, katika kibofu cha mkojo, uume na hata kwenye uke.

Mfumo mzuri wa kinga wa mwili pamoja aina fulani za bakteria wanaoishi pamoja na fangasi hawa husaidia sana katika kuthibiti maambukizi yanayoyosababishwa na aina hi ya fangasi. 
 
Nini hutokea?
Kwa kawaida, Candida albicans huishi kwenye uke na sehemu nyingine (kama zilivyoelezewa hapo juu) bila kusababisha madhara yoyote yale isipokuwa pale mazingira ya eneo husika yanapobadilika kama vile mabadiliko katika hali ya pH ya  eneo husika (ifahamike ya kwamba pH ya kawaida ndani ya  uke ni 4.0 - 4.5) au uwiano wake na vimelea  (microorganisms) wengine unapoharibiwa kutokana na sababu mbalimbali kama vile matumizi ya madawa aina ya antibiotics, kupungua kwa kinga mwilini kutokana na magonjwa mbalimbali n.k.

Maambukizi haya ya fangasi yanaweza kugawanywa katika sehemu kuu mbili
  1. Maambukizi yasiyo makali yaani uncomplicated thrush: Katika kundi hili, mgonjwa hupatwa na maambukizi  mara moja hadi nne kwa mwaka na dalili zake huwa si mbaya sana na maambukizi haya husababishwa na fangasi wa jamii hii ya Candida albicans.
  2. Maambukizi makali yaani complicated thrush: Katika kundi hili, mgonjwa hupatwa na maambukizi zaidi ya mara nne kwa mwaka, dalili zake kuwa mbaya zaidi au kama maambukizi  yatakuwa yametokea kipindi cha ujauzito, ugonjwa wa kisukari, upungufu wa kinga mwilini. Aina hii kusababishwa na vimelea vya aina nyingine tofauti na Candida albicans.
Vihatarishi
Watu walio katika hatari ya kupata maambukizi ya fangasi hawa ni  wale wenye

• Kutumia sana dawa aina ya detergents kwenye sehemu za siri au douches (vifaa vinavyotumiwa kusafishia uke kwa kutumia maji yaliyochanganywa na siki au antiseptic yoyote ile) kwa sababu hali husababisha kuharibika kwa uwiano wa fangasi na aina nyingine ya vinyemelezi kama bakteria aina ya lactobacilli

• Kutumia sana madawa aina ya antibiotics, steroids ambayo yana tabia ya kushusha kinga ya mwili

• Mabadiliko ya mfumo wa homoni mwilini ambayo husababisha mabadiliko katika s ehemu za siri na hivyo kufanya kuwepo kwa ukuaji wa kasi wa fangasi hawa

• Ujauzito (kutokana na kubadilika kwa mfumo wa homoni mwilini na kupungua kwa kinga ya mwili). Hata hivyo ieleweke hapa kuwa si kila mjamzito hupatwa na maambukizi haya.

• Matumizi ya dawa za kupanga uzazi (vidonge vya majira)

• Upungufu wa kinga mwilini kutokana na magonjwa sugu kama kisukari, saratani aina yoyote ile, ugonjwa aina ya mononucleosis na nk.

• Ugonjwa wa ukimwi (HIV/AIDS)

• Matibabu ya homoni (hormonal replacement therapy) kutokana na sababu mbalimbali

• Matibabu ya kusaidia kushika mimba kwa wale wenye matatizo ya uzazi (infertility treatment)

• Msongo wa mawazo (stress)

• Utapia mlo (malnutrition)

• Kuvaa nguo au mavazi yanayoleta joto sana sehemu za siri kwa muda mrefu kama nguo za kuogelea (swimwear), nguo za ndani (chupi)  zilizotengenezwa kwa kitambaa aina ya nylon, nguo za ndani zinazobana sana nk.

• Kujamiana kwa njia ya kawaida mara tu baada ya kujamiana  kupitia njia ya haja kubwa (anal sex) au matumizi ya vilainishi venye glycerin wakati wa kujamiana pia yamehusishwa na maambukizi haya.

• Kuvimba kwa tezi la koo (goiter)

• Saratani ya tezi la koo (thyroid cancer)

• Wanawake wenye umri wa miaka kati ya ishirini na thelathini wapo kwenye hatari kubwa ya kupata maambukizi haya wakati wale ambao wameshaacha kupata hedhi au wale ambao hawajaanza kupata hedhi kabisa hawako kwenye hatari kubwa.

Kwa wanaume vihatarishi  vya maambukizi haya ni

• Kujamiana na mwanamke mwenye tatizo hili au maambukizi haya

• Upungufu wa kinga mwilini

• Matumizi ya madawa aina ya antibiotics kwa muda mrefu bila ushauri wa daktari

• Magonjwa sugu kama kisukari, saratani ya aina yoyote ile na nk.

Dalili na viashiria kwa wanawake
• Kuwashwa  sehemu za siri  (kwenye tupu ya mwanamke)

• Kuhisi kuwaka moto sehemu za siri (burning sensation)

• Kufanya kama vidonda katika sehemu za siri (soreness)

• Maumivu wakati wa kujamiana (superficial dyspareunia)

• Maumivu  au usumbufu wakati wa kujisaidia haja ndogo (wakati mtu anakojoa)

• Kuvimba na kuwa rangi nyekundu kwa  mdomo wa nje wa tupu ya mwanamke (labia minora)

• Kutokwa na uchafu wa rangi nyeupe au nyeupe kijivu, unaoweza kuwa mwepesi, majimaji au mzito na ambao umefanana na jibini (cottage cheese like discharge) wenye muonekano unaojulikana pia kama curd-like appearance. Kwa kawaida, uchafu huu haumbatani na harufu yoyote isipokuwa panapokuwa na tatizo la ziada kama ugonjwa wa zinaa aina ya Bacteria vaginosis. Uchafu huu unaotoka hapa unaweza kuenea kwenye maeneo mengine yaliyokaribu na tupu ya mwanamke kama kwenye mitoki (groin area) au perineum na kusababisha kuharibika kwa ngozi katika sehemu hizo.

Dalili na viashiria hivi huwa mbaya zaidi wakati  mwanamke anapokaribia  kupata hedhi.

Dalili na viashiria kwa wanaume ni
• Kuwashwa sehemu za siri 
• Kuvimba na kuwa rangi nyekundu kwenye ncha ya uume
• Kuwepo kwa uchafu wa rangi nyeupe (kama nilivyoeleza hapo juu) kwenye sehemu ya juu ya uume.
• Kuwa na vidonda vidogo kwenye uume (sore on the glans)

Hata hivyo, mara nyingi wanaume hawaoneshi dalili zozote zile, ni vizuri kwa mwanamke kumueleza mwenza wake pale anapopata maambukizi haya ili naye pia apate kutibiwa. 
 

Matibabu
Matibabu ya fangasi huusisha dawa za kutibu fangasi (antifungal drugs) kama vile dawa za kupaka za topical Clotrimazole, topical Nystatin, Fluconazole au topical Ketoconazole. 

Wagonjwa wenye maambukizi yasiyo makali yaani uncomplicated vaginal candidiasis wanaweza kutumia dawa za kupaka (cream) kutoka dawa za fangasi za jamii ya -azole kama vile Butoconozale, Miconazole, Clotricomazole nk.

Ni vizuri kwa daktari kabla ya kumpa mgonjwa dawa hizi kumfahamisha kwa ufasaha jinsi ya kuzitumia na tahadhari anayotakiwa mgonjwa kuchukua.
 
Kinga ya maambukizi ya fangasi
• Kuosha sehemu ya siri kwa kutumia kitambaa kisafi kila siku na kuosha kuanzia mbele kuelekea nyuma, epuka kurudia ukishafika nyuma.

• Epuka matumizi ya sabuni zenye manukato, bubble baths, vaginal deodorant products, feminine hygiene, na bath powder.

• Vaa chupi ambazo hazibani sana na zilizotengenezwa kwa kutumia pamba au hariri (silk), epuka synthetic underwear.

• Epuka mavazi yoyote ya kubana kama jeans za kubana nk.

• Badilisha nguo za ndani (chupi) kila zinapopata unyevunyevu.

• Fua chupi zako kwa maji yenye nyuzi joto 90 na kuendelea.

• Tumia pad wakati tu unapozihitaji (kama umeingia kwenye mzunguko wako wa hedhi)

• Kula mlo wenye virutubisho vyote kamili (balanced diet)

• Epuka kufanya mapenzi  na mpenzi wako ambaye amepata maambukizi ya fangasi.

• Epuka kuoga  maji moto sana (hot baths) tumia maji ya uvuguvugu, hii kwa wale ambao wanaishi kwenye ukanda wa joto (tropical climate).

• Matumizi ya vifaa vya ngono (sex toys), vifaa vya upangaji uzazi (diaphragms, cervical caps) yanaweza kuleta kujirudia kwa maambukizi ya fangasi kama havitaoshwa  na kukaushwa vizuri baada ya kutumiwa.

• Baadhi ya tafiti zilizofanyika, zimethibitisha ya kwamba unywaji wa maziwa ya mtindi yenye live culture, husaidia kupunguza maambukizi ya fangasi.


Share:

Jinsi ya Kumtambua Mpenzi Tapeli na Muongo

Inawezekana upo katika uhusiano na tapeli wa mapenzi bila kujua, hiyo ni sumu na unachotakiwa kufanya sasa ni kuanza kumchunguza mpenzi wako mapema isije kuwa upo kwenye foleni!

Hakuna kitu kibaya kama kuwa katika foleni ya wapenzi kwa mpenzi mmoja, tena mbaya zaidi awe ni yule ambaye moyo wako umempenda kwa dhati.

Kumbuka, kuwa katika uhusiano na mtu ambaye haeleweki ni sawa na kukaribisha matatizo katika maisha yako, huna sababu ya kuishi kwa wasiwasi ukiwa hujui mpenzi wako anakuchukulia vipi.

Anza kumuwekea mitego mapema. Lakini katika mitego yako achana na simu yake kabisa, huna sababu ya kuchunguza simu yake lakini kama ni msaliti utajua tu, unafikiri atajificha mpaka lini?

Atafanya mambo yake gizani mpaka lini? Kuna siku utagundua na kumuacha aendelee na umalaya wake kama ameona ndiyo maisha. Usikubali kabisa kuwa katika penzi la kitumwa, penzi la kisaliti, kuwa na mtu ambaye anakuchanganya wa kazi gani zaidi ya kukupotezea muda na kukukaribishia machozi?

UTAMJUAJE MPENZI LAGHAI?
Hapa ndipo kwenye kazi, kwa bahati mbaya sana kama ikitokea ukampenda mtu sana hata kama akifanya mabaya kiasi gani unaweza usiyaone, kama wewe ni wa aina hii unapaswa kubadilika kifikra. Mwone wa kawaida, fanya uchunguzi wako polepole na kama ukiona moja kati ya mambo yafuatayo, ujue kuna kitu.

(a) Hataki ujulikane na rafiki zake
Hii ni kati ya alama walizonazo matapeli wa mapenzi, ni mtu wa kufanya mambo kwa upekee sana. Kila dakika hakaukiwi na neno nakupenda sana, lakini moyoni mwake hakuna alama hata moja ya mapenzi kwako.

Ni vigumu kumtambua mtu wa aina hii lakini chunguza kuhusu hili, hapendi kabisa kukukutanisha na rafiki zake na hata mkikutana nao kwa bahati mbaya basi hatakutambulisha na kama akikutambulisha hatakutambulisha kama mpenzi wake rasmi. Ataishia kusema ninyi ni marafiki mlioshibana!

Tangu lini mpenzi akatambulishwa kama rafiki? Mtu anapomtambulisha mpenzi wake humtambulisha kwa kujisikia furaha moyoni kwamba anamtambulisha mpenzi wake lakini inakuwaje kwako akutambulishe kama rafiki?

Baadaye utakapomuuliza hawezi kuwa na jibu la maana, atabaki kukuambia hata kama akikutambulisha kama rafiki jamaa ataelewa kuwa ni mpenzi wake, hii inaingia akilini kweli?

Hakuna ukweli kama huo ndugu zangu! Huo ni ulaghai na anaogopa kukutambulisha kama mpenzi maana tayari ameshaonwa akiwa na wapenzi wengine. Sasa kama ndivyo, atatambulisha wangapi? Aseme wewe ni nani? Amka ndugu yangu!

(b) Msiri kupitiliza
Hii ni alama nyingine waliyonayo wanaume wa aina ninayoielezea katika mada hii. Siku zote mambo yake ni kwa siri kubwa, kama mna ahadi ya kukutana, hataki muongozane, atakuambia mkutane moja kwa moja sehemu husika. Hata muda wa kuondoka atafanya kila njia ili kila mmoja aondoke mwenyewe na kama mkiondoka pamoja basi ujue ni usiku na hakuna atakayewaona.

Ikitokea akakubali kuongozana na wewe, hatapenda muongozane pamoja. Atalazimisha utangulie mbele yeye afuate nyuma, kwa nini? Kwa sababu anaogopa kujulikana kuwa yeye ni mpenzi wako na kama anaogopa anakupenda kweli? Mapenzi gani hayo yanafanywa kwa siri? Anakupotezea muda huyo.

(c) Hapendi ndugu wafahamiane
Mpenzi wa aina hii ni mjanja sana, kwanza kabisa atajifanya mtu mwenye ‘ubize’ sana, yote hii ni kukwepa kuwajua ndugu zako au wewe kuwajua ndugu zake! Wakati mwingine anakuwa hapendi ndugu zako na wake wakutane wakijua wazi kuwa nyie mna uhusiano, hili ni tatizo.

Hakuna uhusiano wenye heri na malengo ya kuishi pamoja siku zijazo ukawa wa kificho cha kiasi hicho. Kama ana nia na wewe basi atahakikisha anawafahamu baadhi ya ndugu zako na wewe unawafahamu baadhi ya ndugu zake, hayo ndiyo mapenzi ya kweli.

Mapenzi hayaishii kwa nyie wawili pekee bali hata kwa ndugu zenu. Mnapojuana inakuwa rahisi kusaidiana hata katika mambo mengine ya kawaida.

MWILI wako  una thamani kubwa sana, usiidharau jinsi yako, usijishushe kiasi hicho, huyo anayekupotezea muda na kukuchezea sasa hivi hana thamani kama huyo aliyeandaliwa kwa ajili yako. 

#Pakua App Yetu tukuhabarishe




Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger