Thursday, 1 August 2019

Rais Magufuli atoa Maagizo kwa Waziri wa Viwanda na Biashara

Rais  Magufuli amemtaka Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa kusimamia wawekezaji wasisumbuliwe katika uwekezaji wa viwanda.

Rais Magufuli pia amewaomba Watendaji ndani ya Serikali kutowasumbua wafanyabiashara wanaotaka kuwekeza nchini.

Ametoa tamko hilo leo Alhamisi Agosti 1, alipokuwa akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Kiwanda cha Kusaga Nafaka cha 21st Century Food and Packaging, kilichopo Kurasini jijini Dar es Salaam, kinachomilikiwa na mfanyabiashara Mohamed Dewji (Mo Dewji).

“Watendaji ndani ya serikali pamoja na Waziri wa vianda yuko hapa, tusiwaumize vichwa wafanyabiashara wanaotaka kuwekeza katika nchi yetu, nimepata taarifa kuna baadhi ya wawekezaji wanawekewa masharti ya ajabu na wengine wanaombwa rushwa, sasa mnawazungusha kwanini hela ni yake haujamsaidia yeye anakuja kuwekeza ili watu wako wapate ajira,” amesema

“Waziri wa Biasha kama kuna watendaji wako ndani ya serikali bado hawajaona mwelekeo wa awamu ya tano wakae pembeni sisi tuendelee kwenda mbele kwani tunataka wawekezaji waje, akiwa na hela yake muoneshe eneo akajenge kiwanda chake na akishamaliza serikali itakusanya kodi, Tanesco watauza umeme, Dawasco watauza maji kwani hiyo ndiyo njia ya kuijenga nchi,”

“Waziri wewe ni kijana nenda ukafanye kazi kwa manufaa ya nchi, na mimi ninawaomba mkatangaze mema ya nchi yetu kwani serukali ya Tanzania ya awamu ya tano inapenda wawekezaji ndio maana tumefuta kodi zaidi ya 54 na sio rahisi kufanya hivyo lakini tunafanya kwa kuangali mbele,” amesema.


Share:

Baba Levo Ahukumiwa Kifungo cha Miezi Mitano Jela

Msanii wa Bongo Fleva na Diwani wa kata ya Mwanga Kaskazini, Manispaa ya Kigoma Ujiji, Revokatus Kipando maarufu kwa jina la Baba Levo amehukumiwa kifungo cha miezi mitano kwa kosa la kumshambulia Askari wa Usalama Barabarani Mkoani Kigoma.

Inadaiwa kuwa  Baba Levo alimshambulia askari anayefahamika kwa jina la Msafiri Ponera, akiwa eneo lake la kazi eneo la Kwabela baada  ya  mtuhumiwa kulazimisha kupita kwa pikipiki wakati askari huyo akiwaruhusu watembea kwa miguu, na baada ya hapo Baba Levo aliamua kumshambulia askari huyo.


Share:

Mo Dewji Ammwagia Sifa Rais Magufuli

Mkurugenzi wa Kampuni za Mohamed Enterprises Limited, Mohamed Dewji amempongeza Rais Magufuli kwa mageuzi makubwa kwa kipindi kifupi  cha uongozi wake.

Dewji ameyasema hayo leo akifungua kiwanda cha kusaga unga wa mahindi na ngano cha 21st Century Food Packaging kinachomilikiwa na Kampuni za Mohamed Enterprises Limited chenye uwezo wa kusaga tani 1,540 kwa siku

“Mheshimiwa Rais tunaamini kwamba wale wasiokuelewa leo watakuelewa baadae na wasioelewa lengo wataeleweshwa na matokeo ambayo tunaamini hayako mbali sana kwani mageuzi makubwa chini ya uongozi wako ndiyo yaliyotushawishi kuendelea kuwekeza nchini kama unavyoshuhudia leo hii,” amesema.

“Binafsi ninashuhudia kuimarika nidhamu kwa watumishi wa umma, mkazo mkubwa serikalini, kutekelezwa kwa miradi mbalimbali ya maendeleo, kupungua kwa rushwa na kushughulikiwa kwa migogoro ya ardhi nchini pia tumeguswa na namna ulivyoshugulikia matatizo ya wafanyabishara,” amesema.

Aidha amesema kiwanda hicho ni miongoni mwa viwanda vikubwa na vya kisasa kinachojihusisha na uzalishaji wa unga wa ngano na wa mahindi nchini, na kwamba kampuni ilianza uwekezaji 2005 na ilianza na kiwanda chenye uwezo mdogo wa kusaga tani 240 kwa siku pamoja na uwezo wa kuhifadhi tani 20 tu za nafaka.

“Hivi sasa kiwanda kimeboreshwa kwa kuwekeza kwenye mitambo mikubwa iliyogharimu jumla ya Sh. bilioni 105 na inatumia teknolojia ya kisasa zaidi, uwekezaji huu umefanyika chini ya awamu ya tano, leo tunashuhudia kiwanda cha mahindi chenye uwezo wa kusaga tani 300 kwa siku, kiwanda cha ngano chenye uwezo wa kusaga tani 1240 kwa siku, mitambo yenye uwezo wa kupokea tani 600 kwa saa za nafaka na uwezo wa kuhifadhi nafaka hadi tani elfu 50,” amesema.


Share:

Rais Magufuli amtaka Mo Dewji kujali maslahi ya wafanyakazi wake kama Anavyoijali Simba

Rais Magufuli amemtaka Mfanyabishara Mohamed Dewji (Mo Dewji), kuhakikisha anajali maslahi ya wafanyakazi wake kama anavyofanya katika Timu ya mpira wa miguu ya Simba Sports Club ambapo amemsihi kwamba wafanyakazi hao nao wanastahili kupata maslahi yao.

Ametoa ombi hilo leo Alhamisi Agosti 1, alipokuwa akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Kiwanda cha Kusaga Nafaka cha 21st Century Food and Packaging, kilichopo Kurasini jijini Dar es Salaam, kinachomilikiwa na mfanyabiashara huyo.

“Mohamed Dewji ninakupongeza sana katika hili na ninakuomba uwajali wananchi wanaofanya kazi hapa hasa maslahi yao kwahiyo unapokuwa unaangalia maslahi ya Simba uangalie pia masilahi ya wafanyakazi wa 21st century food and packaging,” amesema.

Aidha ameiataka Kampuni ya Metl Group iliyopo chini ya mfanyabishara huyo kuachana na utaratibu walionao wa kuagiza ngano kutoka nje ya nchi na badala yake kuanza kulima ngano nchini kwani kwa kufanya hivyo itasawadia Watanzania wanaohitaji ajira.

“Ninatoa wito kwa Kampuni ya Metl Group chini ya Mohamed Dewji, nilipokuwa ninapewa maelekezo nmeambiwa mahindi yanatoka Tanzania ambayo yanatengenezwa tani 300 kwa siku lakini ngano inayotengeneza tani 1400 kwa siku inaagizwa kutoka nje hii tuibadilishe,” amesema.

“Katika maisha yangu nilikua ninafahamu kulikuwa na mashamba makubwa sana ya ngano kule Manyara lakini sasa hivi hayatumiki na kuna wakati wawekezaji wakijaribu wanachomewa moto sasa nitoe wito hata kwa Kampuni yako muanze kulima ngano kwani mtakuwa mmesaidia Watanzania wengi,” amesema.


Share:

UDSM Entrepreneurship training for higher education graduates 2019

UDSM Entrepreneurship training for higher education graduates 2019-ujasiriamali, jifunze ujasiriamali, kanuni za ujasiriamali, jifunze ujasiriamali pdf, vitabu vya ujasiriamali pdf, changamoto za ujasiriamali, maana ya ujasiriamali ni nini, ujasiriamali in english, ujasiriamali maana yake nini, UDSM Entrepreneurship training for higher education graduates 2019. The Chancellor of the University of Dar es Salaam declares to all graduates of higher… Read More »

The post UDSM Entrepreneurship training for higher education graduates 2019 appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Internship Opportunities TBS-Tanzania Bureau of Standards (TBS)

Internship Opportunities TBS-Tanzania Bureau of Standards (TBS), tbs tanzania forms, tbs tanzania pvoc, tbs form, tanzania bureau of standards act, roles of tbs in procurement, about tbs, tbs address, tbs certification, Internship Opportunities, Nafasi za kazi tbs, nafasi za internship tbs tanzania 2019. Tanzania Bureau of Standards (TBS) is Tanzania’s sole Standards body, formerly established by the Standards… Read More »

The post Internship Opportunities TBS-Tanzania Bureau of Standards (TBS) appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

KARIBU INVO ENTERPRISES KWA USAFI WA OFISINI NA NYUMBANI

Share:

BABA AMKATA KOO MTOTO WAKE


Saidu Dan Iya raia wa Nigeria amemkata koo mwanaye wa kike aitwaye Zahra Saidu mwenye umri wa miaka 8.

Baba huyo ambaye anadaiwa kuwa na matatizo ya kisaikolojia baada ya kutumia madawa ya kulevya kwa muda mrefu, ambapo inadaiwa alimkaba mwanaye shingoni kisha kumkata koo kwa kutumia kisu.

Mama mzazi wa mtoto huyo Fadimatu Saidu ameeleza kuwa alipigiwa simu na jirani yake jana mchana baada ya kutokea kwa tukio hilo.

“Mimi ni mfanyakazi za ndani katika familia ya watu, Niliondoka asubuhi na kumuacha mwanangu akiwa amerudi kutoka shule akiwa na baba yake, lakini baadaye nilipigiwa simu na jirani yangu nirudi nyumbani ili kujionea tukio hili la jaribio la mauaji kwa mwanangu”, amesema mama wa mtoto huyo.

Baba huyo kwa sasa anashikiliwa na jeshi la Polisi na anashtakiwa kwa makosa mawili ya kihalifu ambayo ni kushambulia kwa kutumia silaha na kutoa vitisho vya kuuwa kwa mke wake.

Mtoto kwa sasa anapatiwa matibabu hospitalini na Daktari amesema kuna asilimia 50 za kupona au kupoteza maisha ila watatoa matibabu bila ya gharama zozote.
Share:

WAKONGWE WA YANGA SC NA PAMBA SC KUKUTANA KILELE WIKI YA MWANANCHI


Kuelekea kilele cha wiki ya Mwananchi mambo yanazidi kunoga huku Uongozi ya Klabu ya Yanga ukiendelea kuongeza ubunifu wenye lengo la kusherehesha siku hiyo ambayo itafanyika Siku ya Agosti 4 katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

Licha ya klabu hiyo ya Mitaa ya Jangwani kuendelea na wiki ya Mwananchi kwa kufanya Shughuli mbalimbali za Kijamiii,pia siku hiyo ya kilele cha Wiki ya Mwananchi utapigwa mchezo wa kirafiki utakaowakutanisha wachezaji wa zamani wa timu hiyo Dhidi ya wachezaji wa zamani wa Pamba Fc ya Jijini Mwanza.
 VIKOSI vitakavyocheza mchezo wa kirafiki siku ya kilele cha Mwanachi uwanja wa Taifa, Agosti 4

Share:

TETESI ZA SOKA ULAYA ALHAMISI


Manchester United bado hawajaamua kuhusu suala la kuhama kwa Paulo Dybala, huku mshambuliaji huyo wa Argentina , 25, akitarajia kujadili na Juventus juu ya hali yake ya baadae wiki hii . (Manchester Evening News)

Dybala ameiambia klabu ya United kuwa itatakiwa kumpa mkataba wenye thamani ya pauni £350,000 kila wiki ikiwa atakiunga nao. (Mail)

Rais wa kblabu ya Lille Gerard Lopez amethibitisha kuwa winga wa Ivory Coast Nicolas Pepe mwenye umri wa miaka 24 atauzwa kwa Arsenal kwa euro milioni 80. (RMC Sport - in French)Winga wa Ivory Coast Nicolas Pepe mwenye umri wa miaka 24 atauzwa kwa Arsenal

Napoli wamejipanga kwa dau la Euro milioni 60 kwa ajili ya winga wa Crystal Palace na mchezaji wa kimataifa wa Ivory Coast Wilfried Zaha baada ya kumkosa Pepe. (Mail)

Barcelona wanataka kumuuza Mbrazili Philippe Coutinho, lakini wanahofia kuwa kuwa hawajapata ofa yoyote kumuhusu mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 . (ESPN)

Arsenal imetengeneza dau la deni la mlinzi wa Juventus na Italia Daniele Rugani mwenye umri wa miaka 25 kwa ajili ya kuwa nae kwa misimu miwili. (Gazzetta dello Sport, via Sun)

Nahodha Laurent Koscielny, mwenye umri wa miaka 33, bado ameazimia kuondoka Arsenal msimu huu licha ya mazungumzo yanayoendelea baina yake na klabu hiyo.(Independent)Arsenal imetengeneza dau la deni la mlinzi wa Juventus na Italia Daniele Rugani

Arsenal wamejiandaa kumuacha mlinzi wao Mjerumani Shkodran Mustafi aondoke msimu huu, lakini Roma abado hawaweka dau kwa ajili yake licha ya kwamba wanahusishwa na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27.(Romanews, via Star)

Mkurugenzi wa michezo wa Bayern Munich Hasan Salihamidzic anasema kuwa Manchester City wanapaswa kuombwa msamaha baada ya meneja wa klabu Niko Kovac kusema kuwa timu hiyo ya Ligi ya Bundesliga imejipanga kusaini mkataba na winga wa Mjerumani Leroy Sanes mwanye umri wa miaka 23. (Sport Bild - in German)

Zenit St Petersburg wanatarajia kutangaza kusaini mkataba wa winga wa Barcelona Malcolm, mwenye umri wa miaka 22,baada ya klabu mbili kukubaliana kuhusu garamakatika kanda hiyo ya £36.5m na zaidi kwa ajili ya Mbrazili huyo. (Goal)Aston Villa ya wanamsaka mshambuliaji wa Brentford Mfaransa Neal Maupay

Manchester United wako tayari kukabiliana na Barcelona katika kumpata mshambuliaji wa klabu ya Marseille mwenye umri wa miaka 17 Mfaransa Lihadji msimu huu. (La Provence, via Mail)

Nia ya Aston Villa ya kumsaka mshambuliaji wa Brentford Mfaransa Neal Maupay imeongezeka zaidi baada ya Sheffield United kutafuta katika timu nyingine . (Birmingham Mail)

Sunderland watamrugusu kiungo wao wa kati na nahodha captain George Honeyman, mwenye umri wa miaka 24, kujiunga na kikosi cha Hull Citybadala ya kumkosa mhitimu wa shule ya soka kwa uhamisho wa bure msimu ujao. (Northern Echo)

Mchezaji mwenza wa Neymar katika kikosi cha Paris St-Germain Marco Verratti anakiri kuwa klabu hiyo lazima imuuze mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27- raia wa Brazil ikiwa hana raha katika Parc des Princes, licha ya kocha Thomas Tuchel wa kutaka mchezaji huyo abaki kikosini. (Express)Real Madrid wamemuambia mshambuliaji wa safu ya kati wa MColombia James Rodriguez kuwa atabaki Bernabeu

Juventus amethibitisha kuwa kumekuwa na ofa kwa ajili ya mshambuliaji wake raia wa Argentina Paulo Dybala, huku kukiwa na nia ya kumnunua mchezaji huyo kutoka kwa Manchester United na Tottenham ya kumnunua . (Mirror)

Mlinzi wa zamani wa Barcelona Carles Puyol, mwenye umri wa miaka 41, amesema kuwa alikataa mara mbili ombi la Real Madrid la kutaka ajiunge nao. (AS in Spanish)

Meneja wa Rangers Steven Gerrard amethibitisha kuwa uhamisho wa winga wa Liverpool Muingereza Ryan Kent, ambaye ana umri wa miaka 22, haupo na kwamba hawawezi kumudu uhamisho wake kudumu . (Daily Record)

CHANZO.BBC SWAHILI
Share:

AUAWA KWA KUPIGWA RISASI BAADA YA KUUA BABA YAKE NA KUJERUHI WATU SABA KWA PANGA TARIME


Na Asha Shaban - Mara.
Mtu mmoja anayefahamika kwa jina la Wambura Kisiri amemuua baba yake kwa kumkata kata kwa mapanga sehemu mblimbali za mwiliwake na kuwajeruhi watu wengine saba kwa panga katika sehemu mbalimbali za miili yao huko katika kijiji cha Kimusi kata ya Nyamwaga wilayani Tarime mkoani Mara.

Tukio hilo la kusikitisha limetokea Julai 29,2019 majira ya saa sita na nusu mchana huko katika kijiji cha Kimusi Senta ambapo mtuhumiwa alitoka nyumbani kwake na kwenda nyumbani kwa baba yake mzazi huku akiwa na mapanga mawili mkononi na kufika na kuanza kumkatakata kwa mapanga mzazi wake huyo.

Akielezea tukio hilo, Kamanda wa Polisi Kanda maalumu ya Tarime/Rorya Henery Mwaibambe alisema baba mzazi wa muuaji huyo anajulikana kwa jina la Kisiri Nyambari Kisiri alimaarufu Nyankongo (85)mkazi wa Kimusi aliuawa kwa kukatwa na panga kichwani,shingoni,tumboni na kwenye kiganja cha mkono wa kulia kwa kukiondoa chote.

"Aliuwawa kwa kukatwa panga na kijana wake ambaye baadae naye aliuawa kwa kupigwa risasi na polisi baada ya kushindwa kutii agizo la polisi la kumta kuacha kufanya fujo ",alieleza.

Alisema baada ya kumkatakata kwa mapanga baba yake pia alimfuata shangazi aitwaye Rhobi Nyambari (38) ambaye alijeruhiwa kwa kukatwa bega la kulia karibu na shingo,hali kadhalika kumjeruhi baba yake mdogo Marwa Nyambari (68) alijeruhiwa kwa kukatwa na panga kichwani.

Mwaibambe aliongeza kuwa baada ya tukio hilo kuendelea alijitokeza mtu mmoja ambaye ni jirani Chacha Hura (29) kwenda kutoa msaada na bahati mbaya naye alikatwa panga mgongoni.

Aidha wakati tukio hilo likiendelea kutendeka mtuhumiwa huyo alijeruhi watu wengine wanne lakini hawakupata madhara makubwa na taarifa zilifika kituo cha polisi ambapo askari walifika eneo la tukio kwa kwa ajili ya kumkamata mtuhumiwa ambapo alitaka kuendelea kuwaua wananchi wengine.

Alisema askari polisi walitumia mabomu ya machozi na risasi za moto ndipo mtuhumiwa huyo alijeruhiwa kwenye nyonga kwa lengo la kumpunguza nguvu ili asiendelee kuleta madhara na kurahisisha ukamataji wake pamoja na kumnyang’anya silaha alizokuwa nazo.

Kamanda Mwaibambe alieleza kuwa baada ya mtuhumiwa huyo kujeruhiwa alifariki dunia muda mfupi akiwa njiani kupelekwa hospitali ya wilaya ya Tarime kwa ajili ya kupatiwa matibabu na mwili wake umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali hiyo.

Mwaibambe alisema chanzo cha tukio hilo bado hakijafahamika na polisi wanachunguza chanzo cha tukio hilo ambapo alisema majeruhi wote katika tukio hilo wamelazwa katika kituo cha Afya cha Muriba na halizao zinaendelea vizuri.

Share:

HATIMA YA DHAMANA YA MWANDISHI WA HABARI ZA UCHUNGUZI ERICK KABENDERA KUJULIKANA AGOST 5


Mahakama ya Kisutu imekataa na imeutaka upande wa Serikali kuwasilisha kiapo kinzani  kabla ya August 5, 2019 kujibu hoja kuhusu kukamatwa kwa Mwanahabari Erick Kabendera. 


Wakili wake  Shilinde Swedy amewasilisha maombi ya kutaka Kabendera afikishwe Mahakamani kwasababu anashikiliwa  kwa zaidi ya masaa 24 tangu July 29.

Upande wa Jamhuri ulitaka kuwasilisha majibu ya kiapo kinzani  Agosti 7, mwaka huu, lakni Mahakama ikakataa.

Jamhuri wamekutana na kikwazo hicho leo Alhamisi saa tatu asubuhi mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustine Rwizile anayesikiliza maombi hayo.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon alidai maombi hayo yaliwafikia jana na leo shauri linakuja kwa mara ya kwanza hivyo anaomba apewe muda wa kuwasilisha kiapo cha majibu kinzani Agosti 7 mwaka huu kwa sababu kesho atakuwa Mahakama Kuu katika kesi nyingine.

Wakili wa mwombaji, Shilinde Swedy alidai mteja wake yuko chini ya ulinzi kwa zaidi ya saa 24, hajapata uwakilishi wa aina yoyote hivyo aliomba kesi ije Jumatatu.

Hakimu Rwizile alisema kwa kuwa maombi yamekuja chini ya hati ya dharura, muda ulioombwa na Jamhuri ni mrefu, hivyo maombi hayo yatasikilizwa Agosti 5, mwaka huu.

“Maombi yatasikilizwa Agosti 5, mwaka huu siku ya Jumatatu saa saba mchana, wajibu maombi watajibu wakati wowote kabla ya muda huo,” amesema Hakimu Rwizile.



Share:

LIVE: Rais Magufuli Akizindua Jengo La Tatu La Abiria Katika Uwanja Wa Ndege Wa Kimataifa Wa Julius Nyerere

Leo Agosti 01,2019 Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli anazindua rasmi Jengo la tatu la Abiria (Terminal III )katika Kiwanja cha ndege cha kimataifa  cha Mwalimu Julius Kambarage Nyerere


Tazama hapo chini


Share:

RAIS MAGUFULI AMTUMBUA MKURUGENZI WA HALMASHAURI

Rais Magufuli ametengua uteuzi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Morogoro Vijijini, Kayombe Rioba kwa utendaji usioridhisha wa miradi ya maendeleo hususani ujenzi wa Hospitali ya Wilaya.


Uamuzi wa kuondolewa kwa kiongozi huyo umetangazwa na Waziri wa nchi ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Seleman Jafo leo.

"Leo tarehe moja mwezi wa 8 mwaka 2019, Mh. Rais Magufuli amemtengua Mkurugenzi wa Halashauri ya Wilaya ya Morogoro Bwn. Kayombe Masoud Rioba kutokana na usimamizi usioridhisha wa miradi ya maendeleo hususani ujenzi wa Hospitali ya Wilaya," amesema leo Waziri Jafo.
Share:

CCM yashinda katika Uchaguzi wa Naibu Meya na Kaimu mwenyekiti wa Halmashauri mkoani Shinyanga

NA SALVATORY NTANDU
Diwani wa kata ya Igunda Halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama mkoani Shinyanga amechaguliwa kwa mara nyingine kuwa Makamo mwenyekiti wa Halmashauri hiyo katika Uchaguzi wa ndani wa  cha Chama cha Mapunduzi (CCM) kilichofanyika jana.

Uchaguzi huo umefanyika jana katika ofisi za CCM wilaya ya kahama ukiongozwa na Mwenyekiti wa uchaguzi huo Emmanuel Mbamange  ambaye pia ni katibu wa CCM wilaya ya Kahama na kusema kuwa mh, Katoto amepata kura 20 za ndio kutoka kwa madiwani wa Halmashauri hiyo waliohudhuria uchaguzi huo.

Amesema Halmashauri hiyo ina jumla ya madiwani 28 wa CCM lakini waliopiga kura ni 20 huku wengine wakiwa na udhuru mbalimbali na kusema kuwa uchaguzi huo ulikuwa huru na haki.

Baada ya kumalizika kwa uchaguzi huo Mh, Katoto amewashukuru madiwani wenzake na kuahidi kutoa ushirikiano kwao ili kuhakikisha Halmashauri ya Ushetu inapata maendeleo.

Katika Hatua nyingine  Diwani wa Kata ya Chibe manispaa ya Shinyanga John Kisandu (CCM) amechaguliwa kwa mara nyingine tena kuwa Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga, na kumshinda mpinzani wake Zena Gulamu (Chadema).


Uchaguzi huo wa Naibu Meya umefanyika jana kwenye mkutano mkuu wa mwaka wa baraza la madiwani wa kumchagua Naibu Meya pamoja na Kamati mbalimbali, ambazo zitasimamia utekelezaji wa maendeleo ya Manispaa hiyo, ikiwamo kamati ya fedha ya kudumu, uchumi, elimu na afya, miundombinu, ukimwi, maadili pamoja na Jumuiya ya Serikali za Mitaa (ALAT).

Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo, mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Geofrey Mwangulumbi, amesema John Kisandu kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) ameibuka mshindi kwa kupata kura 15, dhidi ya mpinzani wake Zena Gulam kutoka Chadema ambaye amepata kura tano ,ambapo wajumbe waliopiga kura walikuwa 20.

Akizungumza mara baada ya kupata ushindi huo, Kisandu ameomba ushirikiano kutoka kwa madiwani hao na kuwa kitu kimoja katika kuisimamia halmashauri kwa maslahi mapana ya wananchi na kuwaletea maendeleo.

Aidha madiwani hao wameendelea kujadili ajenda mbalimbali zikiwamo za afya, elimu, maji, miundombinu, fedha, kwa ajili ya mustakabali wa maendeleo ya manispaa hiyo.


Share:

TOUFIQ: Tanzania Kinara Katika Udahili Wa Wanafunzi Elimu Ya Awali Barani Afrika.

Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
IMEELEZWA kuwa Tanzania ni kinara katika suala la udahili wa wanafunzi katika elimu ya awali barani Afrika na hivyo kuifanya kupiga kubwa katika utekelezaji wa maelengo ya maendeleo endelevu(SDGs).  

Mafanikio hayo yanatokana na serikali kutoa elimu bure bila malipo ambao umechangia kuongeza udahili wa watoto wengi kupata fursa ya kupata elimu. 

Hayo yamebainishwa na Mbunge wa Viti maalum FATUMA TOUFIQ ambaye ni pia champion wa masuala ya SDGs bungeni wakati akitoa mrejesho kwa waandishi wa habari kuhusu mkutano aliohudhuriwa wa ‘High level political forum’ uliofanyika Umoja wa Mataifa(UN) hivi karibuni. 

Amesema katika mkutano huo waliwasilisha malengo 6 ya SDGs ambayo kwa ujumla wake Tanzania imefanya vizuri ikiwemo ujenzi wa miundombinu na kutoa wito kwa serikali. 

TOUFIQ ambaye pia ni Mkurugenzi wa Shirika linalojishughulisha na wanawake na watoto(Wowap), amesema katika mkutano huo alipelekwa kwa ufadhili kutoka Shirika la Equal Measure 2030 la nchini Marekani  linalojihusisha na masuala ya usawa wa kijinsia na kusaidia nchi zinazoendelea kufikia malengo hayo ili kuhakikisha kunakuwa kuna usawa kwenye mambo mbalimbali ikiwemo elimu. 

Mkutano huo ulikuwa kwa ajili ya utoaji taarifa jinsi nchi ilivyofanya katika utekelezaji wa SDGs na Tanzania ndio ilikuwa mara yake ya kwanza kutoa ripoti yake iliyowasilishwa na Waziri wa Fedha Dk.Philipo Mpango.


Share:

Rais Magufuli Kuzindua Uwanja wa ndege wa Julius Nyerere terminal 3 Leo

Rais John Magufuli leo Alhamisi Agosti Mosi, 2019, anatarajia kuzindua mradi wa upanuzi wa Uwanja wa ndege wa Julius Nyerere la terminal 3, ambao umetekelezwa kwa miaka6 kwa gharama ya Sh788.6 bilioni.

Mradi huo ulianza kujengwa 2013 na awali ulipangwa kutekelezwa kwa Sh705.3 bilioni lakini kutokana na kubadilika kwa taratibu za kikodi, mchoro wa mradi (Design) na gharama ya mradi huo iliongezeka kwa Sh85.3 bilioni.

Wakati mradi unaanza ulitarajiwa kuwa ungekamilika Desemba 2017, baadaye ukaongezewa mwaka mmoja hadi Desemba 2018, lakini haukukamilika badala yake umekamilika Mei, mwaka huu.

Kampuni iliyotekeleza mradi huo ni BAM International ya Uholanzi ambayo ndiyo iliyofanya kazi za kikandarasi na Arab Consulting Engineers (ACE) ya Misri, ilifanya kazi za ushauri.


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger