Sunday, 7 July 2019

Vijana wapewa elimu kuhusu kuanzisha biashara ili kujikwamua na uchumi

Na.Mwandishi Wetu-DSM
Vijana wapewa elimu kuhusu kuanzisha biashara ili kujikwamua na uchumi kwa  kuchangamkia fursa zilizoko kwenye maeneo yao na kujua umuhimu wa kodi katika biashara ili kuwezesha taifa kupata mapato na wao kupata faida. 

Akizungumza katika Semina ya Vijana iliyoandaliwa na Umoja wa Vijana Tanzania (TYVA), Afisa Elimu na Huduma kwa Walipa Kodi kutoka TRA, Isihaka Sharifu alisema kuwa Serikali imerekebisha baadhi ya Sheria za kodi hususani kwa vijana wanaofungua kampuni au biashara mpya. 

Sharifu alisema kuwa kwa sasa Sheria ya kodi imejikita kuwasaidia vijana wanaoanzisha kampuni na biashara mpya kwani imeweza kugusa msamaha wa kodi kwa miezi sita tofauti na awali ambapo biashara mpya zilikuwa zinalipiwa kodi baada ya miezi mitatu. 

“ Kwa sasa Sheria inasema ukiwa unafungua biashara yako au kampuni mpya kwa sasa unatakiwa kulipa kodi baada ya miezi sita, kwa hiyo hii itawasaidia vijana wengi ambao wanania ya kuanzisha biashara, nawasihi vijana wenzangu tumieni Fursa hiyo kujikwamua kiuchumi”, Alisema Sharifu. 

Katika Semina hiyo ambayo kauli mbiu yake ilikuwa ‘Nguvu ya Kodi’ Sharifu alipaeleza kuwa TRA inatekeleza maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano kuwakwamua vijana hasa wajasiriamali wadogo ambao wanafanya biashara zao kwenye maeneo mbalimbali hapa nchini. 

Alisema kuwa kodi inayotozwa kwa wafanya biashara wenye mauzo kuanzia milioni 0 hadi 100 imegawanyika katika makundi manne ambayo ni mauzo kuanzia 0 mpaka milioni 4 ambao hawatozwi kodi, mauzo ya milioni 4 mpaka 7.5 wanatozwa 100,000, milioni 7 mpaka 11 wanatozwa  250,000 na milioni 11 mpaka 14 wanatozwa 450,000 tofauti na hapo zamani ambapo walikuwa wanatozwa 546,000, kwa hiyo vijana wanatakiwa kuchangamkia fursa hiyo. 

Kwa upande wake, Afisa Vijana kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Temeke, Anna Marika alisema kuwa vijana wanatakiwa kuwa wazalendo kwa kutimiza wajibu wao kwenye suala la kulipa kodi kama Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. John Pombe Magufuli anavyoagiza. 

“Nimefurahi kwa Semina hii kwani watoa mada wamekuja na Mada nzuri zinazoelimisha ulipaji Kodi, wito wangu kwa vijana ni kwamba wanatakiwa kutimiza wajibu wao wa kulipa kodi kama Rais alivyoagiza kuchukua vitambulisho ili wasipate shida kwenye maeneo yao ya kufanyia Biashara”, Alisema Marika. 

Marika aliongeza kuwa kwa Wilaya ya Temeke wamejikita zaidi katika kuwasaidia vijana, wanawake na walemavu kujikwamua kimaisha kama Ofisi ya Rais –TAMISEMI ilivyoagiza kuwa asilimia 10 ya mapato ya halmashauri ijikite kwenye kuwasaidia vijana, wanawake na walemavu. 

Alisema Wilaya ya Temeke imetanga asilimia nne kwa vijana, asilimia  nne kwa wanawake na asilimia mbili kwa walemavu, huku wakilenga kuboresha utoaji wa huduma kwa kutoa vifaa vya kazi kwa vikundi mbalimbali kama vile pikipiki, Chelehani,vifaa vya mziki na magari ya kuzoa takataka na kusomba matofali. 

Alitolea mfano wa kikundi cha wanawake waliopewa chelehani 50 na wataanza kurejesha mikopo baada ya miaka miwili na wakimaliza mkopo vifaa vile vinakuwa mali ya kikundi. 

“Niombe sasa kwa wale vijana ambao mnaisha Temeke, haijarishi unatoka Wilaya gani hapa Dar es Salaam au mkoani, mkirudi kwenu kachangamkieni fursa hii ili kuwawezesha kujikimu kimaisha na kupata faida kubwa ya kuendesha uchumi wenu”, Alisistiza Marika.


Share:

Toa Mikunjo Usoni,Michirizi,Makovu, Kuza Nywele zako na Hawa Jamaa

Kessy_product_cosmetics:

            🍅🥒🍒👇

1- Kutoa Mvi Sugu Pia Zakuzala @130,000/

2-Kuza Nywele Na Kuzijaza Bila Kukatika@120,000/

3-Tengeneza Umbo Lako
4-Toa Mikunjo Uson Makonyanz(Ngozi Yakuzeeeka)90,000/

5-Toa Kitambi Na nyama Za pemben

6-Punguza Mwili Mzima @130,000/

7-Ongeza Unene Wa Mwili @100,000/

8-Towa Michirizi (Strech Mark)90,000/

9-Kutoa Alam, Chunusi,makovu Madoa@80,000/

10-Toa Ndevu Na Vinyweleo@100,000/

11-Ongeza Mguu Kam Bia@100,000/

12-Kama Umepoteza Hamu Yakula @100,000/

13-Towa Weusi Mapajani Mikononi@80,000/

14-Pata Mikanda Yakutowa Tumbo Kabisa *wakawaid@100,000/

*wenye Daw@150,000/

*waumeme@200,000/

15-Ngiri Ainazote@90,000/

16-Rudisha Nywele Kichwani(Kipara@15,000

17-Toa Harufu Sehem mbaya kwapani@100,000/

            🍍🍒🥬👇

Akikisha Unaongea Na Kessy Kwa Maelekezo

Tunapatikana Dar, K Koo,posta, Sinza

_+225_

0719955528

0756259180

0785371237

*Delivery  Popote Ulipo


Share:

Kigwangallah Ampa Makavu January Makamba...."Ni Dharau na Kujionesha tu"

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamis Kigwangalla ameonesha kutoridhishwa na kauli ya Waziri wa Mazingira, January Makamba akiieleza TANAPA kuwa hawawezi kuanza utaratibu wa kutumia magari maalumu ya umeme (Cable Cars), kwa ajili ya watalii wanaotembelea mlima Kilimanjaro.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Waziri Kigwangalla amehoji baadhi ya maswali kwenda kwenye mamlaka ya mazingira, akieleza kuwa watu hao wamekuwa wakishiriki zaidi kwenye makongamano na si uhalisia wa kulinda mazingira.

"Watu wa mazingira wanataka kuingilia kati mradi wa cable cars KILIMANJARO. Lengo letu ni kukuza utalii, kuongeza mapato na kuboresha experience ya watalii wetu nchini. Tusipokuwa wabunifu tunatukanwa kutokutumia vizuri vivutio vyetu, tukiamka wanakuja ‘speed governors’.

"Hivi kuna nchi ngapi zimeweka Cable Cars kwenye milima yake?, hizi haziharibu mazingira?, Cable inapita juu inaharibu mazingira gani?. Zaidi ya hekari 350,000 za misitu zinapotea kila mwaka nchini, ipi ni hatari kubwa?, watu wa mazingira wamechukua hatua gani zaidi ya makongamano tu?", amesema Kigwangalla.

Hivi karibuni wakati TANAPA ilieleza mpango wake wa kuja na namna mpya ya usafiri kwa watalii wanaotaka kwenda kutembelea mlima Kilimanjaro, Waziri wa Mazingira, January Makamba akasema suala hilo haliwezi kufanyika mpaka pale NEMC watakapo thibitisha.

"Inabidi watu wa Mazingira tupitishe na kutoa cheti kwanza kabla hawajaanza. Na tutafanya 'studies' ili kujua madhara kwa mazingira na uthabiti wa 'mitigation measures", alisema Makamba


Share:

Waziri Kamwelwe azindua treni ya Majaribio SGR

Na Grace Semfuko,MAELEZO.
Serikali imeanza mchakato wa ununuzi wa vichwa 22 vya treni, mabehewa 1,430 ya mizigo na Mabehewa 60 ya Abiria vitakavyotumika kwenye uendeshaji wa Reli ya kisasa ya SGR ambayo ujenzi wake unaendelea.

Yapi Merkez inajenga Reli ya SGR awamu ya kwanza kutoka Dar Es Salaam hadi Morogoro ambayo ujenzi wake umefikia asilimia 56 na awamu ya pili kutoka Morogoro hadi Makutupora Mkoani Singida ikiwa imefikia asilimia 52 zote zikiwa na urefu wa zaidi ya kilomita 722 na zinajengwa kwa gharama ya fedha za ndani shilingi Trilioni 7.2.

Hayo yalibainishwa na Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe wakati akizindua Safari ya kwanza ya majaribio ya Treni ya Wahandisi kwenye eneo la Soga lililopo Kibaha Mkoani Pwani.

Injinia Kamwelwe alisema mpango wa sasa wa Serikali ni kuwa na Seti tano za Treni  za SGR zitakazokuwa na behewa nane za abiria, mpango ambao unalenga kuimarisha  sekta ya usafirishaji wa reli.

“Ndugu zangu Watanzania, leo hii tumezindua majaribio ya njia ya reli yetu, hii inamaana kwamba tupo katika mipango ya kuhakikisha reli inakamilika kwa wakati, tumetembea kilomita 20 za majaribiop, reli ni salama kabisa, haina kikwazo,sasa tumeanza mchakato wa kununua vichwa vya treni 22 na mabehewa yake 60 ya Abiria na 1,430 ya Mizigo” alisema Waziri Kamwelwe.

Nae Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania TRC Masanja Kadogosa amesema zoezi la majaribio ya awali ya treni ya wahandisi ni hatua muhimu ya kuhakikisha reli hiyo inapitika bila kikwazo kwani inakagua na kuimarisha miundombinu ya reli hiyo.

Alisema zoezi hilo la awali limekuja kufuatia kukamilika kwa baadhi ya maeneo ya kupita treni kuanzia Soga Wilayani Kibaha Mkoani Pwani, kuelekea Morogoro na kuongeza kuwa treni rasmi kwa ajili ya kupita reli hiyo itawasili hivi karibuni.

Zoezi la majaribio ya uendeshaji wa Reli ya kihandisi ulishuhudiwa na Waziri Kamwelwe, Maafisa wa Shirika la Reli Tanzania TRC pamoja na Waandishi wa Habari ambao walitembea na treni hiyo kwa kilomita 20. 

Mwisho.


Share:

Halmashauri kuu CCM Njombe yatoa maagizo haya kwa serikali

Na Amiri kilagalila-Njombe
Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Njombe imetoa maelekezo kwa mkuu wa mkoa wa Njombe na Mkuu wa Wilaya ya Njombe kukutana haraka iwekezanavyo na wadau wa usafirishaji wa abiria mkoani humo ili kutatua changamoto inayowakumba wananchi wanaosafiri kwa mabasi kushindwa kushushwa  katikati ya mji wa Njombe baada ya stendi kuu mpya kuanza kufanya kazi.

Akizungumzia baadhi maazimio ya kikao cha  halmashauri kuu ya CCM mkoa wa Njombe iliyokutana siku chache zilizopita na kujadili utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2015/2020 kwa mwaka wa fedha 2018/19, katibu wa siasa na uenezi wa CCM mkoa wa Njombe, Erasto Ngole amesema CCM imesikia kilio cha wananchi juu ya adha wanayoipata abiria wanaposhindwa kushushwa na mabasi ya abiria katikati ya mji na hivyo imeagiza lazima kuwepo na kituo cha mabasi katikati ya mji wa Njombe.

“Chama cha mapinduzi mkoa wa Njombe tumempa maelekezo mkuu wa mkoa pamoja na mkuu wa wilaya na mkurugenzi wa halmashauri ya mji waite mkutano mkubwa wa wadau wanaohusika na usafiri,ili waweze kuangalia namna bora ya kuondoa haya manung’uniko,na sisi tumetoa mapendekezo kati kati ya mji lazima kuwe na kituo cha kushusha na kupakia abiria,haiwezekani kabisa mwananchi akapitishwa mjini kusiwe na kituo hata kimoja”alisema Ngole

Katika hatua nyingine kuhusu swala la vitambulisho vya ujasiriamali amesema chama kimetoa maelekezo  kwa serikali ya mkoa wa Njombe kuzingatia utaratibu wa ugawaji wa vitamburisho hivyo.

“Imeonekana kwa sasa yameorodheshwa makundi mbalimbali na watu wanagawiwa vitambulisho ili viishe,mheshimiwa Rais alisema wanaotakiwa kuwa na vitambulisho ni wafanyabiashara wadogo wadogo wenye mauzo chini ya milioni nne kwa mwaka kwa hiyo ni lazima tuzingatie hilo na halmashauri kuu ya mkoa imekazia hilo”aliongeza Ngole

Aidha kuhusu ujenzi wa barabara ya kiwango cha lami kutoka Njombe kuelekea tarafa ya Lupembe hadi mpakani na mkoa wa Morogoro, Ngole amesema chama cha mapinduzi kimeitaka serikali kuanza ujenzi wa barabara hiyo mara moja kwa sababu wananchi wanaoishi maeno hayo wamekuwa wakipata adha kubwa ya usafiri kutokana na miundombinu ya barabara kuwa mibovu.

Kwa upande wake mwenyekiti wa jumuia ya umoja wa vijana mkoa wa Njombe (UVCCM) Nehemia Tweve ametoa wito kwa vijana kuona fulsa mbali mbali zilizopo katika mkoa huo ikiwemo utalii licha ya kilimo na ufugaji ambazo zimezoeleka na wengi




Share:

Misri Yatupwa Nje Afcon Kwa Kuchapwa Bao 1-0 Na Afrika Kusini

Mabingwa watetezi Cameroon na wenyeji Misri wameyaaga mashindano Jumamosi Juni 6 baada ya kutolewa kwenye siku ya pili ya hatua ya mtoano.

Cameroon na Misri ndio waliocheza fainali ya Kombe la Maifa ya Afrika (Afcon) miaka miwili iliyopita ambapo Cameroon ilitwaa ubingwa.

Hata hivyo timu hizo mbili zimeyaaga mashindano baada ya Cameroon kufungwa 3-2 dhidi ya Nigeria jijini Alexandria.

Misri wamepigwa mbele ya mashabiki elfu sabini jijini Cairo na Afrika Kusini kwa goli moja tu lililofungwa na Thembinkosi Lorch katika dakika ya 85.

Afrika Kusini ambao walifuzu katika raundi ya mtoano kama timu ya tatu kwenye kundi lao baada ya kushinda mchezo mmoja tu haikupigiwa upatu katika mechi ya hiyo dhidi ya Misri inayoongozwa na mshambuliaji wa Liverpool Mo Salah.

Umakini wa safu ya ulinzi wa Afrika Kusini  ndio imekuwa chachu ya ushindi baada ya kuhimili vishindo na mikiki ya safu ya ushambuliaji ya Misri ambayo iliibuka na ushindi kwenye mechi zote tatu za makundi.


Share:

Iran Yatishia Kuitandika Kwa Makombora Uingereza

Mjumbe wa baraza la wataalamu wa Iran, Ayetullah Muhammed Ali Musevi, amesema Iran itajibu mapigo kwa makombora kutokana na kitendo cha uongozi wa Gibratar ambayo ni sehemu ya Uingereza, kuikamata meli ya mafuta ya Iran.

Akiongea na shirika la habari la Fars Musevi ameionya Uingereza kutokana na kitendo cha meli ya mafuta ya Iran kukamatwa katika mlango bahari ya Gibrata.

Musevi alikumbushia jinsi Iran ilivyoidungua ndege isiyoendeshwa na rubani ya Marekani baada ya kukiuka na kuingia katika anga la Iran bila ruhusa, kisha akasema kwamba kamwe Iran haitakubali kuonewa na kuhusiana na suala la meli yao kushikiliwa watatoa majibu muafaka.

Musevi alisema anatangaza waziwazi Uingereza ni budi iogope kushushiwa makombora na Iran.

Baada ya Uongozi wa Gibrata ambayo ipo chini ya Uingereza kuikamata meli ya mafuta ya Iran iliyokuwa ikipeleka shehena Syria siku ya alhamisi, Iran ilielekeza vitisho vya kuipiga kwa makombora Uingereza.


Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumapili 7 July















Share:

Lugola Asema Polisi Wanaoshirikiana Na Mafisadi Kudhulumu Ardhi Ya Wananchi Maskini, Dawa Yao Imeiva

Na Felix Mwagara, Mwibara (MOHA)
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amesema baadhi ya polisi wasiokuwa waaminifu nchini wanaoshirikiana na mafisadi kudhulumu ardhi ya wananchi maskini, sasa dawa yao imeiva. 

Akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kijiji cha Haruzale, Kata ya Nyamihyolo, Jimbo la Mwibara, Bunda akiwa katika ziara ya kutembelea miradi ya maendeleo jimboni mwake, Lugola amesema amepokea malalamiko mengi ya ardhi katika jimbo lake na sehemu mbalimbali nchini.

Amesema mafisadi wa ardhi hukimbilia kufungua kesi vituoni wakilazimisha kwa kutumia fedha ardhi iwe mali yao wakiwatumia polisi wasiokuwa waaminifu ili kufanikisha matwaka yao.

“Haiwezekani tabia hii ikachekewachekewa na kuonekana ni kawaida, nimekemea sana katika mikutano yangu hapa Mwibara na sehemu zinginezo hapa nchini, nitahakikisha napambana na mafisadi pamoja na polisi hao wasiokuwa waaminifu,” alisema Lugola.

Waziri Lugola alisema kila kukicha anapata malalamiko mengi kutoka sehemu mbalimbali nchini kuwa mafisadi wanaendelea kuwaonea wananchi maskini kwa kupora ardhi wakidai wao ndio wamiliki halali. Aliongeza kuwa, utumia polisi wasiokua waaminifu kuwakandamiza wananchi ambao hawana nguvu ya kifedha na kufanikiwa kudhulumu ardhi zao.

“Dawa yao ilikuwa jikoni, sasa imeiva, siwezi mwangusha Mheshimwa Rais Dkt. John Magufuli, Serikali hii haichezewi hata siku moja, sasa nitawashughulikia ipasavyo,” alisema Lugola.

Aidha, Lugola aliwataka wananchi wa Mwibara kuhifadhi vyakula vizuri ili kuepusha janga la njaa kwa hapo baadaye na kusababisha wananchi kuja kuteseka kwa ukosefu wa vyakula na kusababisha mateso katika familia. 

“Tutunzeni vyakula vyetu, msitumie hovyo, kuweni makini na matumizi ya vyakula, sitaki nije kuona mnateseka na njaa, hakikisheni mnatunza vyakula kwa ajili ya matumizi ya baadaye, ogopeni njaa kama ukoma,” alisema Lugola. 

Lugola ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo hilo, alifanya ukaguzi wa miradi ya maendeleo akikagua madarasa ya shule ya msingi pamoja na zahanati.


Share:

Rais Mstaafu Jakaya Kikwete Asifu Maonesho Ya 43 Ya Sababsaba Jijini Dar

RAIS Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Kikwete amezipongeza Wizara ya Viwanda na Biashara na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) kwa maandalizi mazuri ya Maonesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam yanayoendelea katika Viwanja vya Julius Nyerere.

Akizungumza  Jumamosi (Julai 6, 2019) mara baada ya kutembelea na kukagua mabanda mbalimbali ya washiriki wa Maonesho hayo, Rais Mstaafu Kikwete alisema hizo ni dalili njema kwa maonesho hayo kwa kuwa yamekuwa bora zaidi ya maonesho yaliyofanyika mwaka jana.

Aidha aliongeza kuwa maonesho ya mwaka huu, yameonesha dhamira ya dhati ya Serikali katika kujenga uchumi wake kupitia viwanda, kwa kuwa katika maonesho ya mwaka huu malighafi nyingi za kilimo zimepewa kipaumbele na wazalishaji wa bidhaa mbalimbali.

“Maonesho ya mwaka huu yamekuwa bora zaidi, kwani tumeshuhudia malighafi nyingi za kilimo zikipewa kipaumbele na hii imekuwa ni dalili njema na point (alama) tunayotakiwa kuifikia kwa sasa” alisema Kikwete.

Awali akitembelea Banda la Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Rais Mstafu Kikwete alilitaka jeshi hilo kuwa wabunifu kwa kuzalisha bidhaa bora zitakazoweza kutumika nje ya Tanzania hususani bidhaa za ngozi ikiwemo viatu vinavyozalishwa na Jeshi hilo.



Share:

Prof.Mbarawa kuzivunja bodi za mamlaka ya maji na kuwaondoa katika nyazifa wakurugenzi wazembe.

NA SALVATORY NTANDU
Serikali imesema  haitasita kuzivunja Bodi za Usimamizi wa Maji na kuwaondoa katika nyazifa,  Wakurugenzi wa Mamkala hizo watakaobainika  kushindwa kukusanya mapato na kusababisha kushindwa kujiendesha ikiwa ni pamoja nakukosekana kwa   huduma ya maji kwa wananchi.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Maji Prof. Makame Mbarawa jana wakati akizungumza na watumishi wa Mamkala ya majisafi na Usafi wa Mazingira mjini kahama(KUWASA) nakusema kuwa,mamlaka za maji  hapa nchini nyingi zinashindwa kujiendesha na kusababisha  kwa wananchi kukosha huduma hiyo muhimu.

Amesema ofisi yake inahitaji  kupata taarifa za ukusanyaji wa mapato(akra) kila baada ya miezi mitatu na nisipoyapata navunja bondi ya maji na kumuondoa mkurugenzi kwenye nafasi yake na kumpatia mwingine mwenye uwezo wa kukusanya mapato na kupeleka huduma ya maji kwa wananchi.

"Nimevunja bodi na kumuondoa mkurugenzi wa mamlaka ya maji Morogoro kutokana na kushindwa kukusanya mapato na kusababisha huduma ya maji kwa wananchi kukosekana, na nitafanya hivyo pia kwenye mamlaka ambazo zitashindwa kukusanya mapato bila kujali mwenyekiti wake wa bodi ni rafiki yangu" Amesema Prof.Mbalawa.

Hata hivyo Prof Mbarawa amesema mamlaka za maji zimekuwa zikisuasua kupeleka huduma ya maji hata kilometa mbili kwa wananchi na badala yake wamekuwa wakiomba fedha wizarani na huku wamekuwa wakitoa huduma na kukusanya mapato na kushindwa kutatua kero za wananchi.

Hata hivyo Prof. Mbarawa amesema adhima ya serikali ya awamu ya tano ni kuhakikisha ifikapo mwaka 2020  asilimia 85 ya vijiji vyote nchini view vinapata maji safi na salama hivyo kuzitaka mamlaka hizo kuongeza mitandao ya maji ili kuongeza mapato na kusogeza huduma hiyo kwa wananchi.

Nae Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mjini Kahama(KUWASA )Meja mstaafu Bahati Matala amesema, atahakikisha anaongeza mapato kwenye mamlaka yake kwa kupanua mtandao wa maji na kupunguza matumizi yasiyokuwa ya lazima.

Amefafanua kuwa, fedha itakayopatikana kwenye ukusanyaji wa akra za maji atahakikisha apeleka huduma ya maji kwa wananchi nakuongeza kwa wale wafanyakazi ambao watabainika kuwaunganishia huduma ya maji wateja kinyemela hata sita kuwaondoa kazini.


Share:

Rais Wa Kenya Uhuru Kenyatta Amaliza Ziara Yake Binafsi Ya Siku Mbili Chato Mkoani Geita Na Kurejea Nchini Kwake

Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta amerejea nchini kwake  baada ya kumaliza ziara ya siku mbili Tanzania.

Kenyatta ameondoka katika Uwanja wa Ndege wa Chato jana  mchana akisindikizwa na mwenyeji wake Rais wa Tanzania, John Magufuli.

Rais Kenyatta aliwasili Chato  Ijumaa ikiwa ni ziara yake binafsi baada ya kualikwa na Rais Magufuli.

Mara baada ya kuwasili alizungumza na wananchi akisisitiza umoja katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ili kuendeleza ushirikiano.

Pamoja na mambo mengine, kiongozi huyo alimjulia hali mama mzazi wa Rais Magufuli, Suzana.



Share:

Saturday, 6 July 2019

Isikupite Hii! 👉Naitwa Chief Karim Wa Sultan.....Ni Bingwa Na Mtabiri Wa Nyota

Isikupite hii! 👉Naitwa CHIEF KARIM WA SULTAN Kutoka- TANGA - TANZANIA: Ni Bingwa, Mnajimu na Mtabiri wa Nyota na Matatizo yote ya ndoa/mahusiano.

Natabiri nyota yako, Kung'alisha nyota, Kufungua nyota zako za mafanikio zilizo fungwa  na kusababisha usifanikiwe katika maisha yako, au unajikuta unafanya kazi/biashara unapata hela lakini pesa yako haikai yaani inapita tu katika mikono yako.

Nawezesha  NYOTA, ni UTAJIRI usio na kafara yoyote na ni UTAJIRI unaoendana na nyota yako tu.

Hakika watu wengi wanazidi kufanikiwa na kutimiza ndoto zao , Kulipwa haraka haki zako unazodai, Mvuto wa mapenzi, kumrudisha mpenzi, mme au mke aliyekuacha/kukutelekeza.

 Je unapata wapenzi/wachumba lakini wanakuacha bila kujua sababu? Nitakusaidia!

Kufungua kizazi chako kilichofungwa na kusababisha usipate mimba/mtoto au unashika mimba zinatoka/kuharibika na maumivu makali ya tumbo/chango.

 👉KWA TATIZO LOLOTE  LA KINYOTA WASILIANA NAMI 👉WhatsApp : 0763 103 527
au
👉PIGA SIMU  : 0716 681 318
👉 0688 745 790


NB 👉(KWA MWANAUME YOYOTE MWENYE TATIZO LA KUISHIWA AU KUPUNGUKIWA NGUVU ZA KIUME AU KAMA UMEATHIRIKA NA TATIZO LA KUPIGA PUNYETO TUWASILIANE POPOTE ULIPO)*{لَا يُؤَاخِذُكُمُ اللَّهُ بِاللَّغْوِ فِي أيْمَانِكُمْ وَلَٰكِنْ يُؤَاخِذُكُمْ بِمَا عَقَّدْتُمُ الْأَيْمَانَ ۖ فَكَفَّارَتُهُ إِطْعَامُ عَشَرَةِمَسَاكِينَ مِنْ أَوْسَطِ مَا تُطْعِمُونَ أَهْلِيكُمْ أَوْ كِسْوَتُهُمْ أَوْ تَحْرِيرُ رَقَبَةٍ ۖ فَمَنْ لَمْ يَجِدْ فَصِيَامُ ثَلَاثَةِ أَيَّامٍ ۚ ذَٰلِكَ كَفَّارَةُ أَيْمَانِكُمْ إِذَا حَلَفْتُمْ ۚ وَاحْفَظُوا أَيْمَانَكُمْ ۚ كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ اللَّهُ لَكُمْ آيَاتِهِ لَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ }* ﴿٨٩﴾ ✨WABILLAHHI TAWFIQ ASALLAM  ALAIKUM✨ 


Share:

Makamba Atoa Neno Mradi wa Magari ya Umeme Tanzania

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), January Makamba amesema ni lazima athari za usafiri wa magari ya umeme kwenye mazingira ziangaliwe kabla ya huduma hiyo kuanzishwa.

Makamba ametoa mwongozo huo kupitia ukurasa wake wa Twitter kufuatia taarifa ya TANAPA jana Julai 5, 2019 kwamba inajipanga kuleta usafiri wa magari ya umeme ili kurahisisha utalii.

Taarifa ya TANAPA ilieleza hivi, ''Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA), inatarajia kuanzisha usafiri mpya wa kutumia magari ya umeme yanayopita kwenye nyaya (Cable Cars), kupeleka watalii Mlima Kilimanjaro''.

Leo Julai 6, 2019 Waziri Makamba amesema ''Inabidi watu wa Mazingira tupitishe na kutoa cheti kwanza kabla hawajaanza. Na tutafanya studies ili kujua impact kwa mazingira na uthabiti wa mitigation measures''.


Share:

Mali za Freeman Mbowe Zapigwa Mnada

Mnada wa kuuza Vifaa na samani mbalimbali vya Kampuni ya Mbowe Limited, inayomilikiwa na Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe, umeonekana kufanikiwa kwa kiasi baada ya baadhi ya vifaa hivyo kununuliwa na kusalia vichache.

Mnada huo ulioendeshwa na Kampuni ya udalali ya Fosters Auctioneer & General Traders ya Dar Es Salaam, umefanyika leo Julai 6, 2019 chini ya dalali wa mahakama Joshua Mwaituka, kwenye ghala la Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) lililopo maeneo ya Bandari.

Akizungumza kuhusu mnada huo, Mwaituka amesema mwitikio wa wateja umekuwa ni mzuri na kwamba asilimia kubwa ya vifaa hivyo vimepata wateja,ambapo amevitaja vifaa vilivyonunuliwa ikiwa ni pamoja na taa, jukwaa, viti, kreti za bia, genereta,Mashine za kupozea na samani mbalimbali.

''Vitu vyote vimeuzwa kasoro makochi, na bei zake ni za kawaida na mwitikio wa watu ni mzuri wamefika tangu saa 2:00 asubuhi''

Kwa upande wake Meneja wa ukusanyaji Madeni kutoka NHC amesema mnada huo ni mwendelezo wa shirika hilo katika kudai deni la zaidi ya shilingi bilioni 1 na kwamba fedha zitakazopatikana kupitia mnada huo, zitaingizwa katika deni la kampuni hiyo na kiasi cha deni kitakachosalia wahusika watalipa kwa mujibu wa sheria.

Vifaa vilivyopigwa mnada vilikuwa vikitumika katika klabu ya Bilicanas,  vilichukuliwa na NHC Septemba mwaka 2016, baada ya mmiliki wake kushindwa kulipa deni la zaidi ya shilingi bilioni 1 alilokuwa anadaiwa kwa kutokulipa kodi kwa muda wa miaka 20.


Share:

Amber Rutty Afunguka Baada ya Video yake Chafu Kusambaa Jana

Binti aliyejipatia umarufu baada ya kuvuja kwa picha na video za utupu mitandaoni, Amber Rutty ameandika ujumbe mzito, na kuwachana wale wanaondelea kumfanya aonekane mbaya mitandaoni.

Amber rutty ameandika ujumbe huo kupitia ukurasa wake wa Instagram, baada ya kuendelea kuzagaa kwa video zake za faragha mitandaoni.

"😭😭😭😭😭Habar nasikitishwa sana na baadhi ya vitu vinavyofanywa na watu wanaotumia matumizi mabaya ya mitandao kwanjia ya kutaka nionekane mkosefu kila leo  ingawa pia najiskia vibaya kuona hata watu wanaotuzunguka nao kushindwa kuchunguza kiundani jambo hili  na kukumbuka swalazima lililowahi kutokea mpaka kupelekea mamlaka husika kutuchukulia hatua na tukajisalimisha kituoni tukasota sana segerea nampaka leo bado kesi ipo mahakaman kupitia hizo izo picha /video chafu wanazo zisambaza tena kwa mara nyingine tena  

sipo hapa kwa jili yakutaka kujua anaefanya ivi kusudio lake ni nini  kwasababu hata ukitazama mionekano yetu ya sasa nahizo video ukianza na mikono ya mmewangu davil mpaka vidolen ambapo amechora tattoos toka mwaka jana mwezi wa 12 napia atamimi ukijalibu kuniangalia the way nilivyo sasa na hzo video kuna utafauti mkubwa sana  

pengine furaha ya mtu anaefanya haya yote ni kuona ndoto zetu zinapotelea gizani  au kutaka kuona mmoja kati yetu kapoteza uhai  ukizingatia swala tayar lipo mahakaman toka October mwaka jana lakin bado leo hii wanayarudia kuyafufua hayo hayo, 

 kiukweli tumechanganyikiwa kiakili mpaka kiafya atupo sawa  ombiletu ni kuomba anaeusika na ili jambo tunaomba aache maramoja kuendelea kwasababu sisi ni binadamu maumivu /mateso tunayoyapitia kwakipindi hiki ni makubwa mno please please.😭😭😭😭"

Tukio la kuvuja kwa picha hizo mitandaoni zikimuonyesha Amber Rutty na mpenzi wake zilivuja mwezi wa kumi, mwaka jana.

Na siku ya jana ilisambaa tena video nyingine mitandaoni kati ya Amber Rutty na mume wake.


Share:

SBL yafanya ‘hafla kuipongeza Taifa Stars’ baada ya kurejea kutoka AFCON

Dar es Salaam, Julai 06, 2019: Kampuni inayoongoza kwa uzalishaji wa bia nchini Tanzania, Serengeti Breweries Limited (SBL), imeandaa hafla ya chakula cha mchana jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuipongeza Timu ya Taifa ya mpira wa miguu (Taifa Stars) baada ya kurejea kutoka nchini Misri ilipokwenda kushiriki kwenye fainali zinazoendelea za kombe la mataifa barani Afrika (AFCON 2019).

Licha ya kupoteza mechi zake tatu za hatua ya makundi na hivyo kushindwa kusonga mbele kwenye hatua zinazofuata za mashindano hayo, Taifa Stars inayodhaminiwa na SBL inastahili pongezi kwa kuweza kufuzu kushiriki fainali hizo za mashindano makubwa ya mpira wa miguu barani Afrika baada ya kushindwa kufanya hivyo kwa takribani miongo minne.

Akiongea kwenye hafla hiyo ambayo imefanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi wa Masoko wa SBL, Anitha Rwehumbiza amewashukuru wachezaji na viongozi wa Taifa Stars kwa kutimiza ndoto ya Tanzania kushiriki katika fainali za AFCON.

“Kitendo cha kuweza kufuzu kushiriki fainali za mashindano haya ni hatua moja kubwa mbele ikizingatiwa tumejaribu mara kadhaa bila kufanikiwa, hivyo basi kwa hatua ambayo tumeweza kufika, kila mmoja aliyeshiriki kuifikisha hapa timu anastahili pongezi”. Alisema Anitha huku akiongeza kuwa kiwango walichoonyesha Taifa Stars kilionekana ‘kuimarika zaidi’ licha ya matokeo kutoridhisha.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Tanzania (TFF), Kidao Wilfred ameishukuru SBL kwa mchango wake mkubwa kwenye timu ya taifa na kuongeza kuwa udhamini wa SBL kwa Taifa Stars umekuwa na mchango kubwa katika kuiwezesha timu kufanya vizuri katika mashindano mbalimbali yanayoikabili.

“Tutakutana na benchi la ufundi ili kufanya tathimini juu ya ushiriki wa timu yetu kwenye fainali za AFCON 2019, baada ya hapo tutakuja na mkakati kwa ajili ya mashindano yaliyoko mbele yetu ya kufuzu fainali za Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN)”. Alisema Kidao huku akidokeza kuwa timu imepata ‘funzo kubwa’ kule Cairo.

Taifa Stars inayodhaminiwa na SBL imeweza kushiriki katika fainali za AFCON 2019 kwa mara ya kwanza tangu mara ya wisho ilipofanikiwa kufuzu kucheza fainali hizo takribani miaka 39 iliyopita.

Stars ilipangwa kwenye kundi C ambalo lilijumuisha magwiji wawili wa soka barani Afrika (Senegal na Algeria) pamoja na Kenya.

…Mwisho…

Kuhusu SBL

Ikiwa imeanzishwa kama Associated Breweries mwaka 1988, Kampuni ya Bia Serengeti (SBL) ni moja ya kampuni kubwa za bia nchini Tanzania, ambapo aina zake za bia zinachangia zaidi ya asilimia 20 ya bidhaa hizo katika soko. SBL inaendesha viwanda vitatu vilivyopo Dar es Salaam, Mwanza na Moshi.

Tangu kuanzishwa kwa SBL mwaka 2002 biashara yake imekua na kuimarika zaidi na asilimia 51 ya hisa mwaka 2010 zilizochukuliwa na Kampuni ya Bia ya Afrika Mashariki (EABL) zimeshuhudia ongezeko la uwekezaji katika kukua zaidi na hivyo kusababisha kuongezeka kwa fursa zaidi za ajira kwa watu wa Tanzania.

Aina za bia zinazozalishwa na SBL ambazo zimepata tuzo kadhaa za kimataifa ni pamoja na Serengeti Premium Lager, Pilsner, Tusker Lager, Tusker Lite, Kibo Gold, Guinness stout, Uhuru na Kick.

SBL pia ni wazalishaji vinywaji vikali vinavyofahamika duniani kama vile Johnnie Walker Whisky, Smirnoff Vodka, Gordon’s Gin, Captain Morgan Rum na Baileys Irish Cream. ………………………………………………………

Kwa maelezo zaidi, wasiliana na; John Wanyancha SBL Corporate Relations Director Tel: 0692148857 Email: john.wanyancha@diageo.com
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger