Saturday, 6 July 2019

SBL yafanya ‘hafla kuipongeza Taifa Stars’ baada ya kurejea kutoka AFCON

...
Dar es Salaam, Julai 06, 2019: Kampuni inayoongoza kwa uzalishaji wa bia nchini Tanzania, Serengeti Breweries Limited (SBL), imeandaa hafla ya chakula cha mchana jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuipongeza Timu ya Taifa ya mpira wa miguu (Taifa Stars) baada ya kurejea kutoka nchini Misri ilipokwenda kushiriki kwenye fainali zinazoendelea za kombe la mataifa barani Afrika (AFCON 2019).

Licha ya kupoteza mechi zake tatu za hatua ya makundi na hivyo kushindwa kusonga mbele kwenye hatua zinazofuata za mashindano hayo, Taifa Stars inayodhaminiwa na SBL inastahili pongezi kwa kuweza kufuzu kushiriki fainali hizo za mashindano makubwa ya mpira wa miguu barani Afrika baada ya kushindwa kufanya hivyo kwa takribani miongo minne.

Akiongea kwenye hafla hiyo ambayo imefanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi wa Masoko wa SBL, Anitha Rwehumbiza amewashukuru wachezaji na viongozi wa Taifa Stars kwa kutimiza ndoto ya Tanzania kushiriki katika fainali za AFCON.

“Kitendo cha kuweza kufuzu kushiriki fainali za mashindano haya ni hatua moja kubwa mbele ikizingatiwa tumejaribu mara kadhaa bila kufanikiwa, hivyo basi kwa hatua ambayo tumeweza kufika, kila mmoja aliyeshiriki kuifikisha hapa timu anastahili pongezi”. Alisema Anitha huku akiongeza kuwa kiwango walichoonyesha Taifa Stars kilionekana ‘kuimarika zaidi’ licha ya matokeo kutoridhisha.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Tanzania (TFF), Kidao Wilfred ameishukuru SBL kwa mchango wake mkubwa kwenye timu ya taifa na kuongeza kuwa udhamini wa SBL kwa Taifa Stars umekuwa na mchango kubwa katika kuiwezesha timu kufanya vizuri katika mashindano mbalimbali yanayoikabili.

“Tutakutana na benchi la ufundi ili kufanya tathimini juu ya ushiriki wa timu yetu kwenye fainali za AFCON 2019, baada ya hapo tutakuja na mkakati kwa ajili ya mashindano yaliyoko mbele yetu ya kufuzu fainali za Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN)”. Alisema Kidao huku akidokeza kuwa timu imepata ‘funzo kubwa’ kule Cairo.

Taifa Stars inayodhaminiwa na SBL imeweza kushiriki katika fainali za AFCON 2019 kwa mara ya kwanza tangu mara ya wisho ilipofanikiwa kufuzu kucheza fainali hizo takribani miaka 39 iliyopita.

Stars ilipangwa kwenye kundi C ambalo lilijumuisha magwiji wawili wa soka barani Afrika (Senegal na Algeria) pamoja na Kenya.

…Mwisho…

Kuhusu SBL

Ikiwa imeanzishwa kama Associated Breweries mwaka 1988, Kampuni ya Bia Serengeti (SBL) ni moja ya kampuni kubwa za bia nchini Tanzania, ambapo aina zake za bia zinachangia zaidi ya asilimia 20 ya bidhaa hizo katika soko. SBL inaendesha viwanda vitatu vilivyopo Dar es Salaam, Mwanza na Moshi.

Tangu kuanzishwa kwa SBL mwaka 2002 biashara yake imekua na kuimarika zaidi na asilimia 51 ya hisa mwaka 2010 zilizochukuliwa na Kampuni ya Bia ya Afrika Mashariki (EABL) zimeshuhudia ongezeko la uwekezaji katika kukua zaidi na hivyo kusababisha kuongezeka kwa fursa zaidi za ajira kwa watu wa Tanzania.

Aina za bia zinazozalishwa na SBL ambazo zimepata tuzo kadhaa za kimataifa ni pamoja na Serengeti Premium Lager, Pilsner, Tusker Lager, Tusker Lite, Kibo Gold, Guinness stout, Uhuru na Kick.

SBL pia ni wazalishaji vinywaji vikali vinavyofahamika duniani kama vile Johnnie Walker Whisky, Smirnoff Vodka, Gordon’s Gin, Captain Morgan Rum na Baileys Irish Cream. ………………………………………………………

Kwa maelezo zaidi, wasiliana na; John Wanyancha SBL Corporate Relations Director Tel: 0692148857 Email: john.wanyancha@diageo.com
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger