Mbunge wa Ubungo (CHADEMA) Saed Kubenea amesema kuwa kitendo cha Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda kusema kuwa yeye na Mbunge wa Kibamba John Mnyika walitaka kujiunga na CCM, si kweli. Kubenea amesema kuwa hawakuongea vile na Rais bali walikuwa wakizungumza mambo mengine, na Makonda amesema yale ili kuwafurahisha wanachama wa chama cha mapinduzi waliokuwepo kwenye hafla ile. Kubenea amesema kuwa uchaguzi ujao watahakikisha kuwa wanashinda kwa kishindo hadi serikali inayoongozwa na CCM ishangae. “Nataka nimwambie tu RC Makonda kwamba katika uchaguzi unaokuja upinzani tutashinda zaidi kuliko…
Thursday, 20 December 2018
SERIKALI YA AWAMU YATANO IMEKUSUDIA KUIMARISHA SEKTA YA NISHATI NCHINI.
Na Mwandishi wetu Songea. Naibu waziri wa nishati ,Mheshimiwa Subira Mgalu amesema kuwa Serikali ya awamu ya Tano chini ya Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli imedhamiria kuimarisha sekta ya Nishati Nchini kwa kuanzisha miradi mbalimbali ya kuhakikisha Nchi inakua na Umeme wa Uhakika , na hilo limethibitika kwa kuanza mchakato wa ujenzi wa mradi wa umeme katika maporomoko ya mto Rufuji mkoani Njombe utakaozalisha megawats 358 kwa lengo la kuwa na umeme wa kutosha na wa gharama nafuu. Akizungumza na wananchi wakati akiwasha umeme…
RAIS MAGUFULI ASHANGAA UFUKWE WA COCO BEACH KUKOSA CHOO
Rais John Magufuli ameshangazwa na ufukwe wa Coco (Coco Beach) pembezoni mwa Bahari ya Hindi jijini Dar es Salaam kutokuwa na choo wakati eneo hilo zinakusanywa fedha kila siku.
Akizungumza leo Alhamisi Desemba 20, 2018 kabla ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa daraja la Selander jijini Dar es Salaam, Rais amedai magari yanayoegeshwa kando ya fukwe hiyo hulipiwa Sh2,000.
“Coco Beach panatia aibu. Ifike wakati tuzizungumzie aibu zetu pale hakuna hata choo, ndio nasikia wanajenga sasa,” amesema.
“Wanakusanya mapato kila siku hatujui hizo hela zinakwenda wapi na wanashindwa hata kujenga mabanda yaliyoboreshwa.”
Hata hivyo, amesema Jiji la Dar es Salaam limebadilika na kuwa na sifa ya kuwa jiji la kibiashara, kwamba anafurahi kuhamia Dodoma akiacha Dar es Salaam ikiwa katika hali hiyo.
MSD NA AGA KHANI WAKUBALIANA KUFANYA KAZI PAMOJA
Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Madawa Tanzania (MSD), Laurean Bwanakunu (kushoto) na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kanda ya Afrika Mashariki, wa Taasisi Aga Khan, Sulaiman Shahabuddin wakitiliana saini mkataba wa makubaliano ya Kiutendaji jijini Dar es Salaam Desemba 20 2018. Wanaoshuhudia (kulia) ni Meneja Msaidizi wa Kisheria wa Hospitali ya Aga Khan, Kieran Kitojo na Mwanasheria Mkuu wa MSD, Christopher Kamugisha. (Imeandaliwa na Robert Okanda)
Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Madawa Tanzania (MSD), Laurean Bwanakunu akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa hafla ya utiliaji saini makubaliano ya ushirikiano wa kiutendaji na Taasisi ya Taasisi Aga Khan. Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Huduma za Hospital ya Aga Khan, Lucy Kwayu.
Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Madawa Tanzania (MSD), Laurean Bwanakunu (kulia) na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kanda ya Afrika Mashariki, wa Taasisi Aga Khan, Sulaiman Shahabuddin wakiwa katika picha ya pamoja na maofisa wandamizi wa Taasisi waliohudhuria hafla hiyo.
RC KAGERA “WATAKAOHUJUMU ZOEZI LA VITAMBURISHO KUKIONA CHA MOTO”
Na: Mwandishi wetu Bukoba. Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti atekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli la kugawa vitambulisho kwa Wajasiliamli Wadogo ili waweze kufanya shughuli zao za ujasiliamali na kujiingizia kipato chao cha kila siku bila kusumbuliwa na mtu yeyote. Mhe.Gaguti ametekeleza agizo hilo la Rais Magufuli Desemba 20, 2018 katika Uwanja wa Uhuru (Maarufu kama Mayunga) Manispaa ya Bukoba ambapo amevigawa vitambulisho hivyo kwa Wakuu wa Wilaya zote za Mkoa wa Kagera na Halmashauri zake nane.…
RPC MUROTO AKIRI BIASHARA YA UKAHABA YAONGEZEKA KWA KASI JIJINI DODOMA
Msako unayoendeshwa na jeshi la polisi jijini Dodoma umeendelea katika maeneo mbalimbali ya jiji hilo na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa 64 wakiwemo wezi, makahaba na wauza madawa ya kulevya. Akizungumza jana na waandishi wa habari jijini Dodoma kuhusu kukamatwa kwa watuhumiwa 64 kati yao wakiwamo 11 wa ukahaba, Kamanda wa Polisi mkoani humo, Gilles Muroto, amesema kuwa jeshi hilo litaendelea kuwakamata watu hao kwa kuwa wanachafua taswira ya jiji hilo. Kamata kamata ya watu wanaofanya biashara ya kuuza miili yao, ilianza Oktoba 9, mwaka huu na kukamata makahaba 22, wanaume watano…
MMOMONYOKO WA MAADILI WATAJWA KUWA SABABU YA KUONGEZEKA UKATILI KWA WATOTO.
Na Amiry Kilagalila,Njombe. Utafiti wa mwaka 2009 unaonyesha kuwa asilimia 60% ya watoto wamefanyiwa ukatili wa aina mbali mbali ukiwemo wa kingono,wa kimwili au wa kihisia ambao kwa kiasi kikubwa umekuwa ukifanywa na wazazi hali inayopelekea kuwa na watoto wasio kuwa imara katika Taifa. Hayo yamezungumzwa na mkurugenzi msaidizi idara ya watoto bi.Grace Muwangwa wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo kwa wawezeshaji ngazi ya jamii kuhusu kitini cha elimu ya malezi kwa familia katika kuzuia ukatili dhidi ya watoto yaliyofanyika katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Njombe na kujumuisha…
DROO YA AFCON KUPANGWA LEO DAR
Droo ya upangaji wa makundi ya michuano ya mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya miaka 17 (AFCON) inatarajiwa kupangwa hii leo Jijini Dar es salaam.
Upangaji wa droo hiyo utafanyikia kuanzia saa 1:00 usiku katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City, ukiratibiwa na Shirikisho la Soka barani Afrika CAF na Shirikisho la Soka Tanzania TFF ambao ndiyo wenyeji wa michuano hiyo.
Timu zilizofuzu kushiriki michuano hiyo ni pamoja na Mwenyeji, Tanzania, Angola, Cameroon, Guinea, Morocco, Nigeria, Senegal and Uganda.
Fainali za michuano hiyo zinatarajia kufanyika kuanzia Aprili 14 hadi 28, 2019 ambapo timu zitakazofuzu hatua ya nusu fainali, zitaliwakilisha bara la Afrika katika michuano ya Dunia ya vijana chini ya miaka 17 itakayofanyika mwakani nchini Peru.
Chanzo - EATV
UCSAF WAZINDUA MNARA WA VODACOM USHETU KAHAMA
Muonekano wa Mnara unaomilikiwa na kampuni ya Vodacom uliozinduliwa katika halmashauri ya wilaya ya Ushetu.
Zaidi ya wananchi 50,000 kutoka kata tano za Halmashauri ya Ushetu Wilayani Kahama mkoani Shinyanga ambao walikuwa wanakabiliwa na changamoto ya mawasiliano kwa muda mrefu,hatimaye wamepata huduma hiyo kupitia mfuko wa mawasiliano kwa wote (UCSAF).
Wakizungumza jana katika hafla ya uzinduzi wa mnara unaomilikiwa na kampuni ya Vodacom ambao umejengwa na serikali kupitia mfuko wa mawasiliano kwa wote,wananchi hao walisema walikuwa wakitembea umbali mrefu kutafuta huduma ya mawasiliano kwa baadhi ya kata ambazo mtandao unakamata/unapatikana.
Mmoja wa wananchi hao Elias Zakaria mkazi wa kata ya Nyamilangano alisema walikuwa wakitembea umbali wa zaidi ya kilomita 100 kufika Kahama Mjini kutafuta huduma ya mawasiliano hali ambayo ilikuwa ikikwamisha shughuli za maendeleo katika maeneo yao.
Ofisa Mjendaji wa kijiji cha Nyamilangano Namana Shabani alisema walikuwa wanapata shida ya mawasiliano katika kuwaalika wajumbe wa serikali ya kijiji katika mikutano ya maendeleo ambapo njia iliyokuwa ikitumika ni barua au kuwafuata wajumbe nyumbani kwao.
“Tulikuwa tunapata shida kuwaalika wajumbe wa serikali ya kijiji na kata kuhudhuria kikao cha maendeleoa, na mfumo ambao tulikuwa tunautumia kuwapa taarifa ilikuwa ni kuwatumia barua ama kuwafuata nyumbani mjumbe mmoja baada ya mwingine hali ambayo ilikuwa inakwamisha shughuli za maendeleo kwenda kwa wakati”,alisema Shabani.
Hata hivyo, Katibu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote nchini (UCSAF) Justina Mashiba alisema mpaka sasa zaidi ya Minara 530 imeshafungwa katika kata mbalimbali nchi nzima na zaidi ya wananchi milioni nne wameshanufaika na huduma ya mawasiliano kwa wote vijijini.
Alisema mnamo tarehe 13 mwezi Disemba mwaka huu wameshasaini mikataba na makampuni ya simu kwa ajili ya ujenzi wa minara 173 katika maeneo ambayo yana changamoto ya mawasiliano nchini.
Naye mwenyekiti wa Mfuko huo Joseph Kilongola alisema wamekuwa walikijenga minara katika kata zenye mvuto wa kibiashara na kuongeza kuwa ifikapo mwaka 2020 kila sehemu zenye changamoto ya mawasiliano nchini zitakuwa zimepata huduma hiyo.
Kwa upande wake Meneja wa Kampuni ya Vodacom wilaya ya Kahama, Jovity Ikate alisema Halmashauri ya Ushetu ina jumla ya minara 10 kati hiyo minara miwili imejengwa na Serikali kwa asilimia 100 na kuwataka wananchi wa kata hizo kuchangamkia fursa za kibiashara kupitia huduma ya mawasiliano.
Naibu Waziri wa Ujenzi ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Ushetu Elias Kwandikwa alisema kupatikana kwa mnara huo kutasaidia kupunguza adha kwa wananchi na watumishi wa Halmashauri hiyo kusafiri umbali mrefu kufua huduma ya mawasiliano.
Aliongeza kuwa serikali kupitia mfuko huo itaendelea kutoa huduma ya mawasiliano katika maeneo yote ambayo yana changamoto ya huduma ya mawasiliano ili kuongeza chachu ya maendeleo katika kata na vijiji.
Na Salvatory Ntandu - Kahama
Naibu waziri wa Ujenzi Elias Kwandikwa akikata utepe ikiwa ni ishara ya kuuzindua mnara wa Vodacom katika kijiji cha Nyamilangano Halmashauri ya Ushetu mkoani Shinyanga.
Meneja wa Vodacom wilaya ya Kahama Jovin Ikate akisoma taarifa ya ujenzi wa Mnara huo katika hafla ya uzinduzi wa Mnara huo katika kijiji cha Nyamilangano.
Katibu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa wote nchini (UCSAF) akizungumza na Wananchi na viongozi waliohudhuria Hafla ya uzindunzi wa mnara wa Vodacom ambao umejengwa kwan ufadhili wa serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa wote.
AFRIKA KUSINI IMEAGIZA BI.GRACE MUGABE AKAMATWE
Waendesha mashtaka nchini Afrika Kusini wametoa amri ya kukamatwa kwa mke wa Rais wa zamani wa Zimbabwe, Grace Mugabe, kutokana na tuhuma za kumshambulia mwanamitindo Gabriela Engels mwaka 2017. Polisi nchini Afrika ya Kusini, imesema hatua hiyo imekuja baada ya mahakama kuibatilisha kinga yake ya kidiplomasia mwezi Julai. Utakumbuka, serikali ya Afrika Kusini ilikosolewa kwa kuruhusu Bi. Mugabe kuondoka nchini humo baada ya mashambulizi. Gabriella Engels alimshutumu mke huyo wa zamani wa Rais kwa kumpiga katika chumba kimoja cha hoteli mjini Johannesburg. Msemaji wa polisi,Vishnu Naidoo amesema hawezi kuthibitisha kuwa…
BIASHARA YA UKAHABA TISHIO DODOMA...POLISI WATAHADHARISHA ONGEZEKO MAAMBUKIZI YA VVU
Jeshi la Polisi mkoani Dodoma, limesema kasi ya biashara ya ukahaba inahatarisha usalama wa afya na kulifanya jiji hilo kuwa na ongezeko la maambukizi ya virusi vya Ukimwi.
Akizungumza jana na waandishi wa habari jiji Dododma kuhusu kukamatwa kwa watuhumiwa 64 kati yao wakiwamo 11 wa ukahaba, Kamanda wa Polisi mkoani humo, Gilles Muroto, alisema kuwa jeshi hilo litaendelea kuwakamata watu hao kwa kuwa wanachafua taswira ya jiji hilo.
Kamata kamata ya watu wanaofanya biashara hiyo, ilianza Oktoba 9, mwaka huu na kukamata makahaba 22, wanaume watano waliokuwa wakiwanunua pamoja na wamiliki wanne wa maeneo yanayoruhusu biashara hizo.
Aidha, Oktoba 31, mwaka huu, jeshi hilo liliwakamata watu wengine 17 wanaotuhumiwa kufanya biashara hiyo.
"Watuhumiwa hawa wote watafikishwa mahakamani na jeshi letu litaendelea na msako wa kuwakamata makahaba wote jijini Dodoma, Waziri Mkuu Majaliwa ndiye balozi wetu wa kupinga maambukizi mapya ya Ukimwi,hivyo hatuwezi kuendelea kuwavumilia hawa watu," alisema Muroto.
Alisema kumekuwa na ongezeko la biashara hiyo kwa kasi, hivyo ni vyema watu wakachukua tahadhari kujiepusha na ongezeko la maambukizi ya ugonjwa huo.
Chanzo - Nipashe
Picha : RAIS MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA UPANUZI WA BARABARA YA MOROGORO KUANZIA KIMARA – KIBAHA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifunua kitambaa na Viongozi mbalimbali wa Serikali na Vyama vya Kisiasa pamoja na Viongozi wa Dini kuashiria uwekaji rasmi wa jiwe la Msingi la Ujenzi wa Upanuzi wa barabara ya Morogoro Kuanzia Kimara hadi Kibaha yenye Urefu wa Kilometa 19.2 .Hafla iliyofanyika Kimara Jijini Dar es Salaam Desemba 19, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Job Ndugai mara baada ya kufunua kitambaa kuashiria uwekaji rasmi wa jiwe la Msingi la Ujenzi wa Upanuzi wa barabara ya Morogoro Kuanzia Kimara hadi Kibaha yenye Urefu wa Kilometa 19.2 .Hafla iliyofanyika Kimara Jijini Dar es Salaam Desemba 19, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihotubia Wananchi katika hafla ya uwekaji jiwe la Msingi la Ujenzi wa Upanuzi wa barabara ya Morogoro Kuanzia Kimara hadi Kibaha yenye Urefu wa Kilometa 19.2 .Hafla iliyofanyika Kimara Jijini Dar es Salaam Desemba 19, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Mtendaji Mkuu wa TANROADS Mhandisi Roberth Mfugale akitoa maelezo ya mradi wakati wa hafla ya uwekaji jiwe la Msingi la Ujenzi wa Upanuzi wa barabara ya Morogoro Kuanzia Kimara hadi Kibaha yenye Urefu wa Kilometa 19.2 .Hafla iliyofanyika Kimara Jijini Dar es Salaam Desemba 19, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikata Utepe na Viongozi mbalimbali wa Serikali na Vyama vya Kisiasa pamoja na Viongozi wa Dini wakati wa hafla ya uwekaji jiwe la Msingi la Ujenzi wa Upanuzi wa barabara ya Morogoro Kuanzia Kimara hadi Kibaha yenye Urefu wa Kilometa 19.2 .Hafla iliyofanyika Kimara Jijini Dar es Salaam Desemba 19, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na kumpongeza Mbunge wa Kibamba John Mnyika (CHADEMA) wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la Msingi la Ujenzi wa Upanuzi wa barabara ya Morogoro Kuanzia Kimara hadi Kibaha yenye Urefu wa Kilometa 19.2 .Hafla iliyofanyika Kimara Jijini Dar es Salaam Desemba 19, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na kumpongeza Mbunge wa Ubungo Said Kubenea (CHADEMA) wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la Msingi la Ujenzi wa Upanuzi wa barabara ya Morogoro Kuanzia Kimara hadi Kibaha yenye Urefu wa Kilometa 19.2 .Hafla iliyofanyika Kimara Jijini Dar es Salaam Desemba 19, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na kumpongeza Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es salaam Isaya Mwita wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la Msingi la Ujenzi wa Upanuzi wa barabara ya Morogoro Kuanzia Kimara hadi Kibaha yenye Urefu wa Kilometa 19.2 .Hafla iliyofanyika Kimara Jijini Dar es Salaam Desemba 19, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwenyekiti wa Kamati ya ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu Selemani Kakoso(Mb) alaipowasili katika hafla ya uwekaji wa jiwe la Msingi la Ujenzi wa Upanuzi wa barabara ya Morogoro Kuanzia Kimara hadi Kibaha yenye Urefu wa Kilometa 19.2 .Hafla iliyofanyika Kimara Jijini Dar es Salaam Desemba 19, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Wanachama wa Ccm Ramadhan Madabida,Erasto Kwirasa,Salum Madenge na Christopher Sanya ambao waliorejeshwa kwenye chama na NEC Desemba 18,2018 ,wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la Msingi la Ujenzi wa Upanuzi wa barabara ya Morogoro Kuanzia Kimara hadi Kibaha yenye Urefu wa Kilometa 19.2 .Hafla iliyofanyika Kimara Jijini Dar es Salaam.Desemba 19,2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amesimama na Spika wa Bunge Job Ndugai,Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isaack Kamwele,Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt.Agustino Mahiga,Waziri wa TAMISEMI Suleiman JaffoWazri wa Maji Profesa Makame Mbalawa,Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu Seleman Kakoso,Katibu Mkuu wa CCM Dkt.Bashiru Ally,Mkuu wa Mkoa wa DSM Paul Makonda pamoja na Viongozi wengine wakiimba wimbo wa Taifa wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la Msingi la Ujenzi wa Upanuzi wa barabara ya Morogoro Kuanzia Kimara hadi Kibaha yenye Urefu wa Kilometa 19.2 .Hafla iliyofanyika Kimara Jijini Dar es Salaam.Desemba 19,2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amesimama na Spika wa Bunge Job Ndugai,Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isaack Kamwele,Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt.Agustino Mahiga,Waziri wa TAMISEMI Suleiman JaffoWazri wa Maji Profesa Makame Mbalawa,Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu Seleman Kakoso,Katibu Mkuu wa CCM Dkt.Bashiru Ally,Mkuu wa Mkoa wa DSM Paul Makonda pamoja na Viongozi wengine wakipiga makofi mara baada ya kuimba wimbo wa Taifa wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la Msingi la Ujenzi wa Upanuzi wa barabara ya Morogoro Kuanzia Kimara hadi Kibaha yenye Urefu wa Kilometa 19.2 .Hafla iliyofanyika Kimara Jijini Dar es Salaam.Desemba 19,2018
Muonekano wa barabara ya Morogoro ambayo ipo katika hatua za ujenzi Kuanzia Kimara hadi Kibaha yenye Urefu wa Kilometa 19.2.
PICHA NA IKULU
MAMA APANDISHWA KIZIMBANI KWA KUUA MTOTO WAKE
Mwanamke mmoja Mkazi wa Mburahati NHC, Angelina Joseph (23), amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni kwa kosa la kumuua mtoto wake.
Mwendesha mashtaka wa Serikali, Ramadhan Mkimbo, amedai hayo leo Jumatano Desemba 19, mbele ya Hakimu Frank Moshi.
Amedai Novemba 5 mwaka huu, jijini Dar es Salaam, mshtakiwa kwa makusudi alisababisha kifo cha mtoto wake mchanga wa siku mbili.
Mshtakiwa hakutakiwa kujibu tuhuma hizo kutokana na Mahakama hiyo kutokuwa na uwezo wa kusikiliza kesi hiyo na kurudishwa rumande hadi Desemba 21, mwaka huu.
Na Aveline Kitomary - Mtanzania
ZAIDI YA WANAFUNZI 4,000 HATARINI KUKOSA MASOMO ILEMELA
Zaidi ya wanafunzi 4,000 waliohitimu darasa la saba mwaka huu na kufaulu, wako hatarini kukosa fursa ya kujiunga na kidato cha kwanza hapo mwakani kutokana na upungufu
Mbunge wa Jimbo la Ilemela ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angeline Mabula aliyasema hayo jana wakati akipokea mifuko 100 ya saruji kutoka benki ya Diamond Trust (DTB).
Dkt. Mabula alisema wanafunzi 8,350 wamefaulu mtihani wao wa darasa la saba lakini kuna upungufu wa vyumba 84 vya madarasa hivyo wenye uhakika wa kujiunga na elimu ya kidato cha kwanza ni wanafunzi takribani 4080. Wilaya ya Ilemela ilishika nafasi ya kwanza kwa ufaulu mkoani Mwanza na kitaifa nafasi ya sita.
Hivyo Dkt. Mabula alisema mifuko hiyo ya saruji kupitia taasisi yake ya The Angeline Foundation inayoshirikiana vyema na Halmashauri ya Ilemela, itasaidia kufyatua matofali kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa ili kuhakikisha wanafunzi waliofaulu wanapata nafasi ya kujiunga na masomo ya kidato cha kwanza ambapo aliwahimiza wadau wengine kuunga mkono juhudi hizo.
Naye Meneja wa DTB Tawi Kuu la Mwanza, Nabeel Alnoor alisema benki hiyo itaendelea kuwa mstari wa mbele katika kuchangia shughuli mbalimbali za maendeleo ya kijamii katika Mkoa Mwanza hususani katika sekta ya elimu na afya.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Kutoka kushoto ni Meneja Msaidizi DTB Tawi Kuu la Mwanza, Ezra Shandu, Meneja DTB Tawi Kuu la Mwanza, Nabeel Alnoor, Mbunge jimbo la Ilemela, Dkt. Angeline Mabula pamoja na Afisa Masoko DTB Tawi Kuu la Mwanza, Boniphace Mwita.
Mbunge jimbo la Ilemela, Dkt. Angeline Mabula akishiriki zoezi la kupanda miti iliyotolewa na Benki ya "DTB" katika Shule ya Msingi Kitangiri C.
Mbunge jimbo la Ilemela, Dkt. Angeline Mabula (wa pili kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Meneja Msaidizi DTB Tawi Kuu la Mwanza, Ezra Shandu (kushoto), Meneja DTB Tawi Kuu la Mwanza, Nabeel Alnoor ( wa pili kulia) na Afisa Masoko DTB Tawi Kuu la Mwanza, Boniphace Mwita (kulia).
Tazama BMG Online TV hapa chini
RAIS MAGUFULI ALIVYOPANGUA KAULI YA MNYIKA KUHUSU DEMOKRASIA NA VYUMA KUKAZA
Rais John Magufuli amemjibu mbunge wa Kibamba (Chadema), John Mnyika baada ya mbunge huyo kuhoji kuhusu demokrasia, vyuma kukaza na kuomba waliovunjiwa nyumba zao kupisha upanuzi wa barabara ya Morogoro kulipwa fidia.
Magufuli alitoa kauli hiyo jana Jumatano Desemba 19, 2018 muda mfupi kabla ya kuweka jiwe la msingi la upanuzi wa barabara ya Morogoro jijini Dar es Salaam katika eneo la Kimara Stop Over.
“Nilitegemea atakaposimama hapa angesema asanteni sana CCM, demokrasia ya namna gani anaitaka, hata kufunika midomo usiongee nayo ni demokrasia. Demokrasia siyo fujo, watu wafanye fujo mitaani wabomoe maduka halafu tuwaache eti kisa ni demokrasia? Haiwezekani. Demokaria ya kweli imehamia bungeni.
“Napenda kuwaambia ndugu zangu wa eneo hili la Kimara kuwa, ukivamia sehemu ya barabara ujue kabisa umetafuta umaskini, hivyo anayewaambia kua kuna fidia, mimi ninawaambia fidia haipo, narudia tena fidia haipo, fidia haipo.
Awali Mnyika alimuomba Rais Magufuli kuwalipa fidia wananchi waliyobomolewa nyumba zao katika eneo la Kimara kupisha upanuzi wa barabara hiyo, lakini Rais amesisitiza kuwa serikali haitalipa fidia kwa watu waliobomolewa nyumba zao kwa kuwa walikuwa wamejenga ndani ya hifadhi ya barabara.
“Wapo wanasema vyuma vimekaza, vitakaza kweli, asiyefanya kazi na asile, lazima tuwaambie ukweli hii ya vyuma vimekaza ni watu wanazushazusha. Wananchi wa Ubungo muache kulalamika vyuma vimekaza, mkatafute kazi ya hata ya kuchimba mtaro hivyo vyuma havitabana.
“Ninawaomba Watanzania wote, hebu tujiamni basi angalau kwa miaka mitano, nikishaondoka muache kujiamini, mfanye mnavyotaka. Kwa nchi inayojitambua hatuwezi kusubiri misaada, mtaji wa maskini ni nguvu zake mwenyewe, nchi hii sio katili.
"Tuheshimu Sheria zetu, nafahamu Sheria ni ngumu na ndiyo maana unakuta hata sheria za Mussa hatuziheshimu, usitamani mwanamke wa mtu unakuta kila mtu anatamani tu.
“Kuna watu wanasema eti ni kodi zetu, kwani zamani mlikuwa hamlipi kodi? Mmbona hazikujengwa? Kwa nini msiseme tu kuwa ni juhudi za Rais Magufuli?.
"Watu wamefariki kwa kushindwa kuwahi Muhimbili kwa ajili ya msongamano wa barabara hii, ndoa zimevunjika mtu anatumia sababu ya msongamano anarudi nyumbani usiku kumbe alikuwa pembeni anasema msongamano kumbe jamaa analiwa,” alisema Magufuli.
MWAKYEMBE APELEKA KWENYE VYOMBO VYA USALAMA MAJINA YA WANACHAMA WA YANGA
Waziri wa Habari Sanaa Utamaduni na Michezo, Dk. Harrison Mwanyembe amepeleka majina nane ya wanachama wa klabu ya Yanga kwenye vyombo vya usalama kwa ajili ya kuwachunguza.
Akisoma taarifa ya Waziri Mwakyembe kwa vyombo vya habari, Mkurugenzi wa Ufundi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Yusuph Singo amesema Mh. Mwakyembe hafurahishwi na vitendo vya wanachama hao.
Waziri Mwakyembe ameeleza kuwa wanachama hao wanaoongozwa na Bakili Makele, wanahamasisha wanachama wengine kupinga uchaguzi wa Yanga uliopangwa kufanyika Januari 13, 2019.
Taarifa hiyo imesema kuwa wanachama hao wakiongozwa na Bakili wanahamasisha wanachama kususia uchaguzi wakishinikiza kuwa Mwenyekiti wao Yusuph Manji bado yupo madarakani.
Wanachama hao ni:-
- Bakili Makele
- Mustaph Mohammed
- Said Bakari
- Shaban Mgonja
- Kitwana Kondo
- Boaz Kupilika
- David Sanare
- Edwin Kaisi.
Bakili ambaye alikuwa Mwenyekiti wa matawi ya Yanga huku Boaz akiwa Katibu wake walifungiwa kujihusisha na soka miaka mitano na faini ya milioni mbili na Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) kwa kosa hilo hilo wiki kadhaa zilizopita.