Wednesday, 19 December 2018

SALUM MWALIMU : NIMEKAMATWA,NIMEPIGWA NA KUDHALILISHWA


Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA (Zanzibar), Salum Mwalimu.

Baada ya Polisi mjini Mafinga mkoani Iringa Jumapili ya Disemba 16, kumkamata na baadaye kumwachia, Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA (Zanzibar), Salum Mwalimu, mwenyewe amefunguka kuwa kilichofanyika ni uonevu dhidi ya demokrasia.

Akizungumza na www.eatv.tv, Mwalimu amesema kuwa kinachodaiwa na aliyetoa agizo la kukamatwa kwake kuhusiana na kutokuwa na kibali cha kufanya mkutano wa ndani hakikuwa sahihi kwa mujibu wa sheria.

Mwalimu amesema kitendo alichofanyiwa kilikuwa cha udhalilishaji na uonevu kwani, hakuwa na kosa lolote ambalo alitenda na kuongeza kuwa hata mikutano ya hadhara ya kisiasa huwa hakuna kibali bali taarifa.

"Sisi sio wajinga kuwa tunavunja sheria makusudi, kama sheria hiyo ipo tungeifuata kama tunavyofanya kwingine, nimekamatwa, nimepigwa na kudhalilishwa bila sababu za msingi", amesema Mwalimu.

Salum Mwalimu alikamatwa wakati akijiandaa kushiriki kikao cha ndani cha chama hicho, na baadaye kuachiwa bila masharti yoyote kutoka kwa Jeshi la Polisi.

Chanzo- EATV
Share:

RAISI ASEMA WALIOBOMOLEWA NYUMBA ZAO HAKUNA FIDIA

Rais John Magufuli amesema waliobomolewa nyumba kupisha upanuzi wa barabara ya Morogoro eneo la Kimara hadi Mbezi jijini Dar es Salaam hawatalipwa fidia kwa kuwa walijenga katika eneo la hifadhi ya barabara.

Rais Magufuli ametoa ufafanuzi huo leo Jumatano Desemba 19, 2018 katika hafla ya uwekaji jiwe la msingi la upanuzi wa barabara hiyo inayofanyika eneo la Kimara Stop Over.

Huku akirejea mara tatu kusema "hakuna fidia", Magufuli amesema hata wakienda mahakamani hakuna fidia.

“Niwambie tu wananchi kuwa ukisogelea barabara madhara yake ni umasikini, hata mimi sijafurahishwa na hii bomoabomoa kwa kuwa wapo ndugu zangu nyumba zao zimebomolewa,” amesema.

"Ni vyema kuwaambia ukweli kesi hii hata wakienda wapi hawawezi kushinda."
Share:

AMA KWELI YANGA NI TIMU YA WANANCHI,MASHABIKI TENA WAIMWAGIA MAMILIONI HAYA

KAMA ulikuwa uamini kama YANGA ni timu ya Wananchi basi amini hii baaada ya wanachama wa klabu ya Yanga Kuamua kuwekeza nguvu zao kwa kuichangia timu kiasi cha shilingi za kitanzania, milioni 8. Mabingwa hao wa Historia ambao wamefika jana salama kwenye Jiji la Arusha jana kwa ajili ya kumenyana na Afrika Lyoni . Wanachama na wadau hao wenye mapenzi ya dhati na Yanga, wametoa kiasi hicho cha pesa kwa ajili ya kuipa hamasa na kuisaidia baadhi ya gharama za kutumia kwa kipindi cha siku tatu ambazo itakuwa mkoani humo.…

Source

Share:

MTIBWA SUGAR KUJENGA UWANJA MKUBWA WA SOKA

Klabu ya soka ya Mtibwa Sugar imetangaza nia yake ya kujenga uwanja wa kisasa na mkubwa wa soka, ambao utakuwa na uwezo wa kubeba mashabiki wengi zaidi.


Hayo yamezungumzwa na Mkurugenzi wa klabu hiyo, Jamal Bayser ambapo amesema kuwa wameamua kuwafuata mashabiki wao na wapenda soka kwa kuwajengea uwanja karibu na makazi yao.

"Dhumuni letu hasa ziadi ni kujenga uwanja ambao utakuwa karibu zaidi kule na wananchi, kule kuna maeneo wanaita Mabawa, ni eneo ambalo wananchi wengi wa Madizini pale wanaweza kutembea kidogo kuliko kule Manungu ambako ni ni mbali kwao," amesema Mkurugenzi huyo wa Mtibwa.

Mtibwa Sugar inajiandaa kwaajili ya mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya KCCA ya Uganda utakaopigwa wikiendi hii Jijini Dar es salaam.

Katika mchezo wa kwanza uliofayika mjini Kampala Uganda wikiendi iliyopita, Mtibwa Sugar ilifungwa kwa mabao 3-0, ambapo katika mchezo wa marudiano inahitaji ushindi wa mabao 4-0 ili iweze kusonga mbele katika hatua inayofuata.
Share:

WANATOKEA WAPI SASA HAWA NKANA,JULIO AWAPA MBINU HII OKWI NA KAGERE

NI wazi timu ya Nkana kutoka Zambia wameshakufa kwenye mechi ya marudiano ndivyo naweza kusema baada ya Timu ya Simba kumpa jukumu zito mshambuliaji wake hatari kabisa Emmanuel Okwi, raia wa Uganda la kuwamaliza Wazambia hao. Mfumania Nyavu huyo amepewa kazi maalumu ya kuivusha Simba kwenye hatua ya makundi kwa kushirikiana na wachezaji wenzake ili kuwafunga mabao zaidi ya 2 Nkana FC ya Zambia. Simba wanawakilisha Taifa kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika ili waweze kufika hatua ya makundi wanapaswa wawafunge Nkana bao 1-0 katika mchezo wa marudio utakaochezwa…

Source

Share:

TETESI ZA SOKA ULAYA JUMATANO DEC 19,2018



Kocha wa Tottenham Mauricio Pochettino anataka kurithi mikoba ya Jose Mourinho ambaye amefutwa kazi na Manchester United, ila itawalazimu United kuilipa Spurs dau la pauni milioni 34 kama watataka kumpeleka mkufunzi huyo raia wa Argentina katika uga wa Old Trafford . (Times)

Kocha wa Real Madrid Santiago Solari amesema hana wasiwasi wowote juu ya tetesi kuwa Mourinho anatarajiwa kuchukua kazi yake. (Sky Sports)

Mourinho amekaa siku 895 katika hoteli ya The Lowry wakati akiifundisha United, na gharama za kuishi hapo zimefikia pauni 537,000. (Guardian)

Zaidi ya asilimia 90 ya wachezaji wa Manchester United walikuwa hawamtaki Mourinho - na hata wale wachache ambao walikuwa wakimpenda walihisi muda wake wa kuondoka klabuni hapo umetimia. (Independent)

Msaidizi wa muda mrefu wa kocha wa zamani na gwiji Sir Alex Ferguson, bw Mike Phelan anatarajiwa kurudi Old Trafford akisaidiana na kocha wa muda Ole Gunnar Solskjaer mpaka mwisho wa msimu. (Telegraph)


Mshambuliaji wa Chelsea na Uhispania Alvaro Morata, 26, anatarajiwa "kurudi Italia hivi karibuni", huku taarifa zikionesha kuwa anaweza kujiunga na miamba AC Milan. (The Sun)

Harakati za Arsenal kumsaini mchezaji wa Real Madrid Isco, 26, zinaoneka kugonga mwamba baada ya kudaiwa kuwa Manchester City tayari wameshaanza mazungumzo na nyota huyo wa timu ya taifa ya Uhispania. (The Sun)

Klabu ya Crystal Palace ipo mbioni kumsajili kwa mkopo mchezaji wa Liverpool Dominic Solanke, 21, kwenye dirisha la usajili la mwezi ujao, Januari. (Evening Standard)

Atletico Madrid hawatazamiwi kuongeza mkataba wa beki wao wa kushoto Filipe Luis, 33. (Marca)Adrien Rabiot
Paris St-Germain hawatamuachia Adrien Rabiot anayewindwa na Liverpool kuondoka kama mchezaji huru mwishoni mwa msimu baada ya kukataa kuongeza mkataba wake. Klabu hiyo inapanga kumpiga bei kiungo huyo mwenye miaka 23 pale dirisha la usajili litakapofunguliwa mwezi ujao. (L'Equipe)
Share:

Video Mpya : MAMA USHAURI - SAFARI

Ninayo hapa Ngoma mpya ya msanii wa Nyimbo za asili Mama Ushauri 'Full Melody Classic' inaitwa Safari...ni ngoma kali sana ya kufungia mwaka 2018...Itazame hapa chini
Share:

Ngoma Mpya : MAMA USHAURI - MIGOGORO......DUDE KALI LA KUFUNGIA MWAKA 2018

Msanii wa nyimbo za asili Mama Ushauri maarufu Full Melody Classic kutoka mkoani Shinyanga anakualika kutazama video yake mpya inaitwa Migogoro..Itazame hapa ...Bonge moja la ngoma la kufungia mwaka 2018.
Share:

SAKATA LA MEMBE KUUTAKA URAIS, NI MPASUKO NDANI YA CCM??....WENGINE WADAI MASALIA YA CCM Vs CCM WAKUJA


Sakata la tuhuma dhidi ya kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bernard Membe, kuonyesha mapema nia ya kutaka urais katika uchaguzi ujao, limeelezwa kuwa ni mpasuko ndani ya chama hicho.

Mchambuzi wa masuala ya siasa nchini, Profesa Mwesiga Baregu, anasema kwa sasa ndani ya CCM, kuna makundi mawili yanayopingana na yameanza kujionyesha wazi.

Anayataja makundi hayo kuwa ni lile la wanaCCM ambao wamedumu katika chama kwa miaka yote wakati wa shida na raha na pia wapo wanaCCM wa kuja na kwamba makundi hayo yanapingana.

Mwanazuoni huyo anasema wanaCCM, ambao wamedumu ndani ya chama bila kuhama wanaitwa ‘CCM masalio’ na kwamba wale wanaorejea wanaitwa ‘CCM wakuja.’

Anasema haitatokea siku moja makundi hayo yakakubaliana, hivyo ana uhakika makundi na hata mpasuko ndani ya CCM vitaendelea kuwepo, iwapo hakutakuwa na juhudi za ziada za kumaliza tatizo hilo.

“Hata wito wa Katibu Mkuu wa CCM Dk. Bashiru Ally kwenda kwa Membe unaonyesha kuna mpasuko, kwa sababu Dk. Ally ni CCM wa kuja wakati Membe ni CCM masalio,” anasema Prof. Baregu.

Anabainisha kuna haja kwa CCM kujitathmini haraka na kuchukua hatua, kwa vile kitendo cha kumuita Membe ni dalili kuwa hali si shwari na ndiyo maana ya kutuhumiana wenyewe kwa wenyewe.

“Sakata hili linatoa fursa chanya kwa kambi ya upinzani endapo halitatafutiwa ufumbuzi mapema, kwani inaonyesha dhahiri kuwa ndani ya CCM bado kuna makundi...huu ni mwanzo na mwisho wa CCM, mambo yanaweza kuwa magumu kwa CCM, kwa sababu wanaweza kupata mgombea, ila asiungwe mkono,” anasema.

Anabainisha kuwa ki-fursa inaonyesha ni uwanja wa kucheza wa upinzani kwa madai kwamba huo mwendo ndani ya CCM si mzuri, unaweza kusababisha hali kuwa mbaya zaidi kufikia mwaka 2020.

Hivi karibuni kumezuka mvutano wa maneno baina ya Katibu Mkuu wa CCM Dk. Ally kutokana na namna alivyotumia mikutano ya hadhara kumuita Membe ofisini kwake, jambo ambalo Membe alilihoji kupitia akaunti yake ya twitter. 

Membe alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa katika Serikali ya Awamu ya Nne na pia ni miongoni mwa wanachama waliokuwa wakitafuta kuwania urais kupitia CCM mwaka 2015, ingawaje kura zake hazikutosha katika ngazi ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC).

Dk. Ally alimtaka afike ofisini kwake kujibu tuhuma zinazomkabili ikiwamo ya kupanga njama za kumkwamisha Mwenyekiti wa CCM Taifa, ambaye pia ni Rais wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli.

Tangu kumalizika kwa mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, mwanasiasa huyo amekuwa kimya hadi hivi karibuni alivyotuhumiwa kuanza mipango ya kutaka urais mwaka 2020.

Membe ni miongoni mwa makada wakongwe na viongozi wa CCM waliotuhumiwa kuwa wanahujumu chama hicho, akitajwa kufanya vikao vya chinichini kwa ajili ya uchaguzi wa mwaka 2020.

“Hao wanaopingana wamewahi kuwa viongozi wakubwa ndani ya CCM, inashangaza kuona wakitofautiana katika kujadili kile kilichofanywa na katibu mkuu wa chama chao,” anasema.

“Unasikia kuna kauli kwamba CCM imevamiwa na wasaka tonge, hii inatolewa na wanaCCM masalio, ambao sidhani kama itakuja kutokea wakakubaliana na hao wenzao wanaoitwa wa kuja,” anasema.

“Wakati makundi hayo yakipingana, ni nafasi kwa vyama vya upinzani kujipanga vizuri ili kuhakikisha unajiweka katika mazingira mazuri ya kujiongezea wanachama zaidi, hasa wenye nia ya kweli ya kuleta mabadiliko,” anasema.

Chanzo - Nipashe
Share:

Utafiti : KUMPAPASA PAPASA 'KUMSHIKA SHIKA' KUNAPUNGUZA MAUMIVU

Kumpapasa papasa mtoto au kumkanda taratibu kunapunguza pakubwa shughuli katika ubongo wake hasa zinazohusiana na maumivu, utafiti umebaini hilo.

Utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu cha Oxford kwa ushirikiano na Chuo Kikuu cha John Moores cha Liverpool, ulifuatilia shughuli za ubongo wa zaidi ya watoto 32, wakati walipokuwa wakitolewa na kupimwa damu.

Nusu yao walipapaswa papaswa na brashi nyororo iliyowekwa mkononi na walionyesha asilimia 40% ya kutokuwa na maumivu kwenye bongo zao.

Mwaandishi vitabu Rebeccah Slater anasema kwamba: "Kumkanda, kumshika au kumpapasa taratibu kuna nguvu na uwezo wa ajabu, na hauna madhara ya pembeni kabisa."

Utafiti huo aidha umebaini pia kuwa, kasi ya kupunguza machungu ni kama sentimita 3 kwa sekunde moja.

"Mara nyingi wazazi huwapapasapapasa watoto wao katika kasi ya kawaida tu," anasema Prof Slater.

"Ikiwa tutaelewa kinachofanyika ndani ya viungo vya mwanadamu hasa mawasiliano ya ubongo pamoja na mbinu za kupasha ujumbe wa kimya ndani ya watoto, tunaweza kuboresha zaidi mashauri ambayo tunawapa wazazi ili kuliwaza watoto wao."

Shughuli za mwendo kasi za kumliwaza mtoto kwa kumpapasa papasa, huzindua aina fulani ya niuroni iliyo na hisia katika ngozi aitwaye C-tactile afferents, ambayo inaonekana kupunguza maumivu kwa watu wazima.

Lakini haikuwa wazi, iwapo watoto wana mwitikio sawa au hukuwa kadri muda unavyokwenda.

"Kuna ushahidi unaoonyesha kuwa, hisia iitwayo C-tactile afferents, inaweza kuzinduliwa ndani ya watoto, na mguso huo wa upole na taratibu, unaweza kuleta mabadiliko makubwa mno kwenye ubongo wa watoto," anasema Prof Slater.
Prof Slater anasema utafiti huo, uliochapishwa katika jarida la Current Biology, na kuelezea ushahidi wa kina na wa nguvu wa mguso ambao umo chini ya mfuko wa kumbebea mtoto maarufu kangaroo care, mahali ambapo watoto ambao wamezaliwa kabla ya muda wao kufika. Sasa wazazi wanashauriwa kuwapa mguso, kupapasa au kuwakanda wana wao katika harakatai za kupunguza machungu ambayo wanaweza kuyapitia baadaye maishani.

"Kazi za awali zimeonyesha bayana kuwa, mguso unaweza kuongeza uhusiano wa karibu mno kati ya mtoto na mzazi, kupunguza shinikizo la moyo kwa mzazi na mtoto, na kupunguza muda mrefu wa kusalia Hospitali," anaongeza Prof Slater.

Waandishi wa uchunguzi huo sasa wana mpango wa kurudia zoezi hilo kwa watoto waliozaliwa kabla ya muda wao wa kuzaliwa kufika, na ambao bado baadhi ya sehemu ya viungo vyao hasa sehemu zao za mwili zinazohusiana na kuhisi zinaendea kukuwa.

Mkurugenzi mkuu wa shirika la Bliss lisilokuwa la kiserikali, na ambalo linalowashughulikia watoto wagonjwa nchini Uingereza, Caroline Lee-Dave , amesifia sana utafiti huo.

Chanzo- BBC

Share:

Video Mpya : MO MUSIC - NAIONA KESHO

Video Mpya: Mo Music – Naiona Kesho

Share:

MKANDARASI ATAKAYE SUASUA KATIKA SUALA LA UMEME KUNYANGANYWA KAZI

  Na Mwandishi wetu Ruvuma. Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Subira Mgalu ameendelea na ziara ya ukaguzi wa miradi ya umeme mkoani Ruvuma ambapo leo amewasha umeme Kijiji cha Palangu na Mang’ua pamoja mtaa wa Luhila Seko katika Wilaya ya Songea ambavyo vimepata umeme kupitia mradi wa usambazaji umeme vijijini wa Awamu ya Tatu (REA III) mzunguko wa kwanza na mradi wa Makambako – Songea. Huo ni muendelezo wa kazi ya ukaguzi na uzinduzi wa miradi ya umeme vijijini mkoani Ruvuma aliyoianza tarehe17 Disemba, 2018 kwa kuwasha umeme katika Vijiji…

Source

Share:

AUMUUA KIKATILI HAWALA YAKE KISHA NA YEYE KUJIUA

Na Allawi Kaboyo Bukoba. Watu wawili wanaodaiwa walikuwa katika mahusiano ya kimapenzi wamefariki baada mmoja kunyongwa na mwingine kujinyonga, katika mtaa wa Mafumbo katika manispaa ya Bukoba mkoani Kagera. Kamanda wa polisi mkoani Kagera Revocatus Malimi alisema kuwa mauaji hayo yamegundulika Desemba 17 mwaka huu saa 11 jioni katika mtaa huo. Malimi alimtaja anayedaiwa kunyongwa na mpenzi wake kuwa ni Regina Temu (29) mkazi wa Kahororo pia katika manispaa hiyo, na mfanyakazi wa kiwanda cha kusindika kahawa cha Tanica, aliyekutwa amenyongwa kwa tai. Alisema kuwa baada ya huyo mpenzi wake…

Source

Share:

Tuesday, 18 December 2018

VYAMA VYA UPINZANI TANZANIA VYATOA TAMKO ZITO KUHUSU DEMOKRASIA... WASEMA 2019 MWAKA WA KAZI

Vyama sita vya upinzani vilivyokaa kikao chao Zanzibar vimesema mwaka wa 2019 ni mwaka ambao watapambana kwa hali zote katika kudai haki zao wanazonyimwa kinyume na sheria za Serikali ya Jamuhuri ya Muungano ya Tanzania.

Kauli hiyo ilitolewa na Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF Maalim Seif Shariff Hamad wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumaliza kikao hicho cha siku tatu kilichofanyika Zanzibar kwa niaba ya vyama hivyo.

"Kama vyama vya siasa vyenye uhalali na uratibu wa uliowekwa rasmin kikatiba, tunatangaza rasimi namna ya kufanya mikutano yetu ya hadhara katika kila kona ya nchi yetu’’ alieleza Maalim Seif.

Alieleza hawatoruhusu katazo haramu ambalo alisema linakwenda kinyume na sheria za nchi na kudai haliwezi kuzuia kazi zao.

Aliwataka wanachi pamoja wanachama wote wa vyama sita, wakati ni sasa wa kuondoa hofu na kuunga mkono vyama vyao ili kulinda Demokrasia.

"Hatupaswi kuwa waoga hata kidogo na hatupaswi kujisalimisha katika kudai haki zetu kama mtu mmoja au kikundi, lazima tupeleke ujumbe huu wa uhuru na Demokrasia kwa viongozi wenzetu wote’’ alieleza.

Sambamba na hilo waliwatangaza viongozi wa vyama vya siasa Freeman Mbowe na Esther Matiko ambao hadi sasa wako mahubusu kuwa ni Wafungwa wa kisiasa na kueleza kuwa tangazo hilo halitofutwa mpaka pale watakapoachiwa.

"Tutapambana kwa nguvu zote kuhakikisha wafungwa wote wa Kisiasa, nchi nzima wanapewa nafasi ya kupata haki katika mfumo ulio huru mbele ya mahakama na macho ya watu’’ alieleza Maalim Seif.

Mwenyekiti wa Chama cha UMMA Hashim Rungwe alisema hawawezi kumruhusu mkandamizaji wa siasa aendelee kuwakandamiza wananchi na demokrasi na kueleza sasa basi.

"Lazima tuwaeleze wananchi wakatae utawala huu wa kibabe kwani ndio uliopomorosha maisha yao’’ alifafanua Rungwe.

Alieleza kuwa Demokrasia ina gharama na wakati ukifika watawaeleza nini watafanya katika kupiga viota uvunjwaji wa Demokrasia.

Akizungumza katika mkutano huo ambao ulitoka na tamko la Azimio la Zanzibar mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia alisema hali iliyopo sasa ni kutokana na ubinafsi ya utawala uliopo.

Alieleza kuwa ubinafsi huu ndio uliopelekea maisha ya watu kubadilika na kuwaona wengine ndio walio na haki hapa nchini.

Kwa upande Wa Zanzibar vyama hivyo vilieleza kuwa hawaitambui Serikali ya Mapinduzi inayo Ongozwa Dr. Ali Muhammed Shein na kuita ni serikali haramu kutokana kile walichodai kupora ushindi wa CUF mwaka 2015.

Akizungumzia baadhi ya wabunge na Madiwani waliohama vyama na kujiunga CCM Waziri Mkuu wa zamani Fredric Sumaye alieleza kuwa viongozi hao hawakuhama bure na wameenda kufanya biashara ya kisiasa.

"Unapoona wabunge na viongozi wa upinzani wanahamia chama tawala ujue chama tawala kimefika mwisho kutawala katika nchi, na hapa ni dhahiri CCM wamefikia mwisho kutawala Tanzania’’ alieleza Sumaye
Share:

DIAMOND PLATNUMZ, RAYVANYY WAFUNGIWA KUFANYA MUZIKI.....TAMASHA LA WASAFI FESTIVAL LAFUTWA

Baraza la Sanaa nchini (Basata) limewafungia wanamuziki Diamond Platnumz na Rayvanny kutojihusisha shughuli za sanaa kwa muda usiojulikana.

Taarifa ya Baraza hilo iliyotolewa leo Desemba 18, imesema limefikia uamuzi huo baada ya wasanii hao kuonyesha dharau kwa mamlaka zinazosimamia shughuli za sanaa nchini, kwa kufanya vitendo vinavyokiuka maadili.

Mbali na kuwafungia wanamuziki hao, Baraza limetangaza kukifuta kibali cha Tamasha la Wasafi Festival linaloendelea nchini.

Wimbo wa Mwanza ambao uliowaingiza matatani ulifungiwa Novemba 12.

Juzi, Basata iliahidi kutoa taarifa rasmi baada ya wasanii hao kuonekana jukwaani katika Tamasha la Wasafi jijini Mwanza wakitumbuiza wimbo huo.

Share:

RAIS MAGUFULI ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA MAKAMU MKUU WA UDOM PROF. EGID BEATUS MUBOFU

Rais John Magufuli ametuma salamu za rambirambi kwa mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom), Benjamin Mkapa kufuatia kifo cha Makamu Mkuu wa chuo hicho, Profesa Egid Mubofu.

Profesa Mubofu amefariki dunia leo Jumanne Desemba 18, 2018 Pretoria, Afrika Kusini alikopelekwa kwa ajili ya matibabu zaidi akitokea taasisi ya tiba ya mifupa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (Moi) alikokuwa akipatiwa matibabu ya kiharusi.

Taarifa iliyotolewa leo na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa inasema Rais Magufuli amemuomba Mkapa kufikisha salamu zake za pole kwa familia ya marehemu, wahadhiri, wanafunzi na wafanyakazi wa Udom na kwenye jumuiya na taasisi zote ambazo marehemu alifanya kazi.

“Nimesikitishwa sana na kifo cha Profesa Mubofu, nitamkumbuka kwa uchapakazi wake, ubinifu, uadilifu na uaminifu mkubwa aliouonesha katika utumishi wake kwa Taifa ikiwemo kazi nzuri aliyoifanya katika Shirika la Viwango la Taifa (TBS) akiwa mkurugenzi mkuu kabla ya kuteuliwa kuwa makamu mkuu wa Udom,” amesema Rais Magufuli.
Share:

WANAUME GEITA WALALAMIKIWA KUINGILIA WAKE ZAO KWA NGUVU


Picha haihusiani na tukio.

Wanaume mkoani Geita wamedaiwa kuwa chanzo cha migogoro ndani ya familia zao kutokana na tabia ya kuwaingilia kwa nguvu wenza wao wakati wanapohitaji tendo la ndoa pasipo kujali kufanya hivyo ni kutenda jinai.

Hayo yameelezwa na baadhi ya washiriki wa mkutano wa Wilaya uliokuwa ukitathimini mikakati ya kupambana na ukatili wa kijinsia ulioandaliwa na shirika la IRS uliomalizika, ambapo wamedai jambo hilo husababisha ongezeko la migogoro mingi kwenye ndoa inayopelekea watu kuuana na hata kupeana vilema vya kudumu.

Washiriki hao wamesema kumekuwa na tabia kwa baadhi ya wanaume kuwaingilia kinguvu wake zao wakati wakihitaji tendo la ndoa pasipo hata kuwaandaa, jambo ambalo ni kinyume cha sheria ya makosa ya kujamiiana lakini pia linahatarisha ustawi wa ndoa husika.

Naye, Wakili wa Serikali Janeth Kisibo, amedai matatizo hayo yanasababishwa kutokaa na ukosefu wa elimu ya kujua namna gani wanandoa wanapaswa kuishi. Jambo ambalo linasababisha ukatili wa kijinsia kuwa mkubwa na makosa mengine yanayopelekea vifo na ubakaji.

Chanzo- EATV
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger