Click Here for more
Sunday, 13 November 2016
Saturday, 12 November 2016
Friday, 11 November 2016
AGIZO LA SERIKALI KWA WAHITIMU WA KIDATO CHA SITA 2016 KWENDA JKT
Serikali
amewaagiza wote waliohitimu kidato cha sita Mei mwaka huu na ambao
hawajajiunga na vyuo vya elimu ya juu, wakaripoti katika kambi za Jeshi
la Kujenga Taifa (JKT) Desemba Mosi, mwaka huu.
Waziri
wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Hussein Mwinyi ametoa agizo
hilo mjini Dodoma alipozungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa
Habari wa Bunge.
Dk
Mwinyi alisema Mei na Juni mwaka huu, JKT iliwafanyia usaili vijana wa
kujiunga na JKT kwa kujitolea. Alisema usaili huo ulifanyika kwa
kushirikiana na kamati za ulinzi za wilaya na mikoa.
“Wizara
ya Ulinzi na JKT inapenda kuwatangazia vijana wote waliosailiwa Juni
mwaka huu, kujiunga na JKT kwa kujitolea, waripoti kwenye kambi
walizopangiwa ifikapo Desemba Mosi mwaka huu kwa nauli zao,” amesema Dk Mwinyi.
Dk Mwinyi amesema mafunzo hayo ni ya miezi mitatu kwa mafunzo yenye utaratibu wa kawaida na miaka miwili kwa wa kujitolea.
Ili
kufanikisha hilo, Wizara ilimuagiza Mkuu wa JKT kufufua kambi ya
Makuyuni JKT iwe miongoni mwa kambi kuanzia Desemba mwaka huu.
Aliagiza kambi za Luwa na Milundikwa za mkoani Rukwa, zirejeshwe kwa shughuli za JKT za kilimo na ufugaji.
Dk
Mwinyi alimuagiza Mkuu huyo wa JKT pia kambi ya Mpwapwa irejeshwe kwa
ajili ya kuendesha mafunzo ya kilimo na ufugaji ndani ya JKT.
LIVE: Fuatilia Hapa Zoezi la Kuuaga Mwili wa Samwel Sitta ambalo Linaongozwa na Rais Magufuli
Leo
kuna shughuli ya kuaga mwili wa aliyekuwa Spika wa Bunge la Tisa la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pia Spika wa Bunge Maalum la
Katiba(BMK), Marehemu Samwel Sitta.
Rais Magufuli ataongoza waombolezaji kuuaga mwili wa Marehemu Sitta katika Viwanja vya Karimjee.
==Fuatilia zoezi hili hapo chini
Thursday, 10 November 2016
HAYA HAPA MAJINA YA WANAFUNZI WALIRUHUSIWA KUHAMIA UDOM 2016/2017
APPROVED CANDIDATES FOR INTER UNIVERSITY TRANSFERS TO UDOM
This is to inform all under mentioned names that their
request for inter university transfer to UDOM have been approved.
Therefore they are required to report to their respective Colleges for
registration and other formalities.For the online admission letters and other documents required for registration please follow this link: alis.udom.ac.tz
Document: TRANSFER
ISSUED BY THE OFFICE OF THE DVC – ARC
10th November, 2016
Wanafunzi hewa 65,198 wabainika shule za msingi, sekondari nchini
Jumla
ya wanafunzi hewa 65,198 wamegundulika kuwepo katika shule za msingi na
sekondari nchini, ambako idadi ya wanafunzi hao isingebainika kiasi cha
Sh milioni 931.3 zingepelekwa shuleni kuhudumia wanafunzi hewa kwa
mwaka wa fedha 2016/2017.
Katika
mkutano na waandishi wa habari jana mjini Dodoma, Waziri wa Nchi, Ofisi
ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George
Simbachawene alisema kati ya wanafunzi hao wa shule za msingi ni 52,783
na sekondari ni 12,415.
Simbachawene
alisema kazi ya uhakiki wa wanafunzi katika shule za msingi na
sekondari ilifanyika mikoa yote nchini kutokana na agizo la Ofisi ya
Rais, Tamisemi kwa makatibu tawala wa mikoa yote ya Tanzania Bara.
Alisema
waliagizwa kuhakiki idadi ya wanafunzi katika shule zote za msingi na
sekondari kwa kulinganisha taarifa ilivyokuwa Machi mwaka huu wakati wa
ujazaji wa madodoso ya takwimu za shule za awali, takwimu za shule za
msingi, sekondari na nyaraka za mahudhurio ya wanafunzi.
Alieleza
kuwa taarifa za idadi ya wanafunzi kabla ya kuhakiki Machi 2016,
zilionesha kulikuwa na wanafunzi 9,746,534 wa shule za msingi na
wanafunzi 1,483,872 wa shule za sekondari.
“Baada
ya uhakiki tuliofanya Septemba mwaka huu, inaonesha kuwepo wanafunzi
9,690,038 wa shule za msingi na wanafunzi 1,429,314 wa shule za
sekondari,” alieleza na kuongeza kuwa uchambuzi umeonesha kuwa
wanafunzi 52,783 wa shule za msingi na wanafunzi 12,415 wa sekondari
hawakutolewa maelezo ya uwepo wao shuleni.
Alisema
kwa tafsiri rahisi hao ni wanafunzi hewa kwa shule za msingi na
sekondari nchini, ambao idadi hiyo ya wanafunzi hewa kama isingebainika
kwenye uhakiki huo na kupelekwa fedha, Sh milioni 931.3 zingepelekwa
shuleni kuhudumia wanafunzi hewa katika mwaka wa fedha 2016/2017.
Alisema kati ya fedha hizo Sh milioni 527.8 ni kwa shule za msingi na Sh milioni 403.4 ni kwa shule za sekondari.
Aliitaja
mikoa inayoongoza kuwa na wanafunzi hewa ni Tabora (12,112), Ruvuma
(7,743), Mwanza (7,349), Dar es Salaam (4,096), Kagera (4,763), Rukwa
(4,054), Singida (3,239), Kilimanjaro (2,594), Kigoma (2,323), Njombe
(2,307), Simiyu (2,081) na Arusha (1,923).
Mikoa
mingine ni Mara (1,855), Tanga (1,378), Geita (1,281), Morogoro
(1,172), Mtwara (882), Mbeya (786), Shinyanga (695), Songwe (512),
Manyara (330), Dodoma (284), Lindi (281), Pwani (187), Iringa (161) na
Katavi (0).
Waziri huyo alisema wanafunzi hewa walianza wakati serikali ilipoanza kupeleka fedha shuleni kama ruzuku.
Alisema
Sh bilioni 27 zimekuwa zikipelekwa kila mwezi kama ruzuku ya uendeshaji
shule za msingi na sekondari na posho ya madaraka kwa ajili ya wakuu wa
shule na walimu wakuu, lakini baadhi ya walimu waliamua kuongeza idadi
ya wanafunzi ili wapate fedha zaidi.
“Huu
ujinga unaweza kufanywa hata katika ngazi ya wizara ni jambo la
uchunguzi, zile fedha hazipiti Tamisemi zinakwenda moja kwa moja
shuleni,” alieleza na kuongeza kuwa hatua za kinidhamu zinaendelea
kuchukuliwa kwa wale wote waliosababisha uwepo wa wanafunzi hewa na
Tamisemi inaendelea kuhakiki takwimu zilizowasilishwa.
“Serikali
haitegemei tena kuwepo suala la wanafunzi hewa. Naagiza makatibu tawala
wa mikoa, wakurugenzi wa mamlaka za serikali za mitaa na wakuu wa shule
kuhakikisha suala la wanafunzi hewa halijitokezi tena katika shule zote
za msingi na sekondari,” alibainisha Simbachawene.