Thursday, 10 November 2016
Wednesday, 9 November 2016
Rais Barack Obama ampongeza Rais Mteule, Donald Trump na kumualika Ikulu kujadiliana juu makabidhiano ya ofisi.
Rais
Barack Obama wa Marekani amempongeza Rais Mteule wa taifa hilo, Donald
Trump na kumualika Ikulu kujadiliana juu makabidhiano ya ofisi.
Treni Yanusurika Kuchomwa Moto na Wananchi....Vioo 30 vya Mabehewa Vyapasuliwa, 17 Watiwa Mbaroni
TRENI
ya abiria inayofanya safari zake kati ya Kituo Kikuu cha Reli na
maeneo ya Pugu Dar es Salaam maarufu kama ‘Treni ya Mwakyembe’ nusura
ichomwe moto juzi, baada ya wananchi kudai kuchoshwa na usumbufu wa
shirika hilo.
Wananchi
hao walitaka warudishiwe nauli zao kwa kile walichodai Shirika la
Reli Tanzania (TRL) limeshindwa kuwa na ratiba inayoeleweka.
Tukio
hilo lilitokea juzi saa 3:00 usiku eneo la Majumbasita, baada ya treni
hiyo kukaa kituoni hapo kwa muda mrefu bila kuambiwa kuambiwa chochote.
Hali
hiyo iliwafanya abiria kuvamia kituo kidogo cha mawasiliano kilichopo
eneo hilo wakitaka warejeshewe nauli zao vinginevyo wangekichoma moto
pamoja na mabehewa ya treni hiyo.
Mwandishi
aliwashuhudia abiria wakitaka kuingia ndani ya kituo hicho huku
wakiwalazimisha wafanyakazi waliokuwapo wawarudishie fedha zao za nauli.
Purukushani hiyo iliyodumu kwa takribani saa mbili ilimalizika kwa abiria hao kuvunja vioo vya mabahewa ya treni vipatavyo 30.
Wafanyakazi
kuona hivyo walijifungia ndani ya kituo hicho huku polisi waliokuwa
wakisindikiza treni hiyo wakitimua mbio kunusuru maisha yao.
Baadhi
ya abiria walisema tangu Ijumaa iliyopita wamekuwa wakipata
usumbufu kwa kukatishiwa tiketi huku treni ikichelewa na wakati
mwingine kutoonekana kabisa.
Walisema
jambo hilo limekuwa likiwasababishia hasara na kuwalazimu kutafuta
usafiri mwingine na kuchelewa kufika kwenye majukumu yao.
Kufuatia
kukithiri vitendo vya uharibifu wa miundombinu ya reli na treni
vinavyofanywa na baadhi ya wananchi, Kampuni ya Reli Tanzania (TRL)
kupitia kwa Mkurugenzi Mtendaji , Masanja Kadogosa imetoa onyo kwa wananchi kutofanya vitendo hivyo.
“Tukio hili si mara ya kwanza kujitokeza, lilijitokeza tarehe 24, 26 na 28 mwezi wa 10 na Novemba 7 Katika matukio hayo kulitokea uharibifu wa miundombonu na kujeruhi baadhi ya wafanyakazi wa TRL akiwemo Mustapha Omary ambaye ameshonwa nyuzi 8 katika hospitali ya mnazi mmoja,” amesema.
Amesema kutokana na uharibifu huo, watuhumiwa 17 wanashikiliwa na jeshi la polisi na kwamba upepelezi ukikamilika watachukuliwa hatua za kisheria.
Kadogosa amedai kuwa, wahusika wa fujo na uharibifu huo ni makondakta wa dalala kwa lengo la kutisha wananchi kutoutumia usafiri wa treni.
“Kuna watu wa daladala wanafikiri wataendelea kufanya fujo ili wananchi waone kuwa usafiri wa treni si salama wapande magari yao, sisi hatulazimishi wananchi kuutumia usafiri wetu ila kutokana na ubora wa huduma zetu wanakuja wenyewe. Pia hatusitishi kutoa huduma kwa sababu ya fujo zao sababu tutawatesa abiria wetu zaidi ya 21,000,”
Naibu Kamishna wa Polisi na Kamanda wa Reli, Simon Chillery amesema jeshi la polisi linaendelea kufanya uchunguzi ili kubaini wengine waliohusika.
“Tukio hili si mara ya kwanza kujitokeza, lilijitokeza tarehe 24, 26 na 28 mwezi wa 10 na Novemba 7 Katika matukio hayo kulitokea uharibifu wa miundombonu na kujeruhi baadhi ya wafanyakazi wa TRL akiwemo Mustapha Omary ambaye ameshonwa nyuzi 8 katika hospitali ya mnazi mmoja,” amesema.
Amesema kutokana na uharibifu huo, watuhumiwa 17 wanashikiliwa na jeshi la polisi na kwamba upepelezi ukikamilika watachukuliwa hatua za kisheria.
Kadogosa amedai kuwa, wahusika wa fujo na uharibifu huo ni makondakta wa dalala kwa lengo la kutisha wananchi kutoutumia usafiri wa treni.
“Kuna watu wa daladala wanafikiri wataendelea kufanya fujo ili wananchi waone kuwa usafiri wa treni si salama wapande magari yao, sisi hatulazimishi wananchi kuutumia usafiri wetu ila kutokana na ubora wa huduma zetu wanakuja wenyewe. Pia hatusitishi kutoa huduma kwa sababu ya fujo zao sababu tutawatesa abiria wetu zaidi ya 21,000,”
Naibu Kamishna wa Polisi na Kamanda wa Reli, Simon Chillery amesema jeshi la polisi linaendelea kufanya uchunguzi ili kubaini wengine waliohusika.
Msajili wa vyama vya siasa Tanzania, avifutia usajili Vyama Vitatu
Msajili
wa Vyama vya Siasa nchini Tanzania Jaji Francis Mutungi ametangaza
kuvifutia usajili vyama vitatu baada ya kubainika kukiuka sheria ya
usajili wa vyama.
Vyama
hivyo ni pamoja na CHAUSTA kilichopata usajili wa kudumu tarehe 5
Novemba 2001, The African Progressive Party of Tanzania (
APPT-Maendeleo) kilichopata usajili wa kudumu terehe 4 Machi 2003 na
Chama cha Jahazi Asilia kilichopata usajili wa kudumu tarehe 17 Novemba
2004.
Jaji
Mutungi amesema kuwa mchakato wa kufuta usajili wa vyama hivyo
umetokana na zoezi la uhakiki wa utekelezaji wa masharti ya usajili na
matakwa mengine ya sheria ya vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu
lililofanyika kuanzia tarehe 26 Juni hadi 26 Julai 2016.
Amesema
katika zoezi hilo uhakiki ulibaini kuwa vyama hivyo vimepoteza sifa za
usajili wa kudumu kwa kukiuka masharti ya sheria ya vyama vya siasa, na
kwamba kila chama kilipewa ya nia ya msajili kufuta usajili wake, lakini
vikashindwa kutoa utetezi wa kuridhisha ili visifutiwe usajili.
BREAKING NEWS:DONARD TRUMP ASHINDA URAIS MAREKANI
Matokeo Marekani 2016: Trump amshinda Clinton uchaguzi wa urais
Donald Trump amemshinda Hillary Clinton katika matokeo ya uchaguzi wa urais uliokuwa na ushindani mkali.
Bi Clinton amempigia simu Bw Trump kumpongeza kwa ushindi wake.Tuesday, 8 November 2016
TANGAZO:VIWANJA VINAUZWA BAGAMOYO-KINGANI,BEI SAWA NA BURE KABISA
Viwanja vinauzwa maeneo ya Bagamoyo-Kingani,vipo vingi na vinapatikana kwa bei nafuu kabisa.
kama wahitaji mcheki huyu mtu kwa;
Bei ni tshs.10000 kwa square meter 1.
simu namba 0754913664
Tanzia: Mwenyekiti wa Klabu ya Azam, Said Mohammed afariki dunia
Uongozi
wa Klabu ya Azam FC kwa masikitiko makubwa, unatangaza kifo cha
mwenyekiti wake, Mzee Said Mohamed Abeid, kilichotokea alasir ya
Novemba 7, 2016, katika Hospitali ya Aga Khan jijini Dar es Salaam.
Mzee
Said Mohamed, atakumbukwa kama mmoja wa nguzo muhimu kwenye mafanikio
ya klabu ya Azam FC tangu kuanzishwa kwake miaka takribani nane
iliyopita.
Chini
ya uongozi wake kama mwenyekiti wa Azam FC, aliiongoza klabu hii
kunyakuwa mataji mbalimbali makubwa na kwa mafanikio, ikiwemo taji la
Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Ligi Kuu Tanzania Bara na Kombe
la Mapinduzi mara mbili pamoja na Ngao ya Jamii.
Si
hivyo tu, mchango wake Mzee Said Mohamed hauku-ishia nyumbani kwake
Azam FC tu, bali hata kwenye familia ya soka la Tanzania kwa ujumla wake
ambapo hadi umauti unamkuta alikuwa ni makamu mwenyekiti wa bodi ya
ligi kuu Tanzania bara na mjumbe wa kamati mbalimbali za shirikisho la
soka Tanzania, TFF.
Sisi Azam FC, tutamkumbuka Mzee Said Mohamed kwa ucheshi wake, ukarimu na uchapakazi wake kwa ujumla.
Marehemu alizaliwa tarehe 20 Machi 1940 visiwani Zanzibar na anatarajiwa kuzikwa Jumanne leo
tarehe 8 Novemba, 2016 kwenye makaburi ya Kisutu baada ya swala ya
Alasir, mwili wake utaswaliwa kwenye msikiti wa Maamour Upanga.
Mwenyezi Mungu ailaze roho yake Said Mohamed Abeid mahali pema peponi, Amiin,
Innalilah Wa-inna-ilaih Rajioun.
Nassor Idrissa,
Makamu Mwenyekiti,
Azam Football Club.
BUNGE LASIMAMISHWA KWA MBINDE KISA KIFO CHA SITA
Mwenyekiti wa Bunge, Mussa Zungu amekumbana na kibano cha wabune baada ya wawakilishi hao wa wananchi kuzua zogo wakilazimisha shughuli za kikao cha sita ziahirishwe kuenzi kifo cha Spika mstaafu, Samuel Sitta.
Sitta aliyewahi kuwa Spika wa Bunge la Tisa na pia Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba, alifariki dunia nchini Ujerumani.
Tafrani hiyo imeanza baada ya kuwatambulisha wageni waliofika bungeni ambapo Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Munde Tambwe alisimama na kuomba mwongozo kwa Spika.
Amesema kutokana na taarifa za msiba wa Sitta, Taifa na hususani wakazi wa Tabora wamepoteza kiongozi mahiri.
“Sitta alikuwa mbunge wa muda mrefu alikuwa Spika wa Bungekwa muda mrefu na pia alikuwa Mwenyekiti wa Bunge la Katiba la Kihistoria,” amesema akimwaga machozi huku akikatiza mazungumzo.
“Kwa niaba ya wabunge wenzangu, naomba Bunge liahirishwe ili kupata muda wa kuomboleza na kutafakari,” amesema.
Ombo hilo liliungwa mkono na Mbunge wa Manyoni Magharibi (CCM), Elibariki Kingu kwa kumfuata Munde kwenye kiti chake na kumbembeleza.
Hata hivyo, Mwenyekiti wa Bunge, Mussa Zungu, amesema licha ya kwamba anakubaliana na mbunge huyo kuwa msiba ni mkubwa na umeligusa Taifa na kwamba ofisi ya Bunge ilimhudumia kwa matibabu, Bunge linaendeshwa kwa kanuni.
“Kanuni zinasema anapofariki mbunge. Mheshimiwa Spika alishastaafu kuwa mbunge, naomba tuendelee hadi hapo kutakapokuwa na maelekezo mengine,” amesema Zungu.
Kauli ya Zungu ilimnyanyua Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe kwa kutumia Kanuni ya Bunge ya 152 ambayo aliinukuu, “Endapo mbunge atafariki wakati bunge likiwa katika shughuli zake, Spika ataahirisha shughuli za Bunge kwa siku hiyo kwa ajili ya kuomboleza.
“Toka nchi yetu ipate uhuru tulikuwa na maspika kadhaa, maspika wote waliopoteza maisha baada ya kustaafu, Bunge halikuwa kwenye vikao vyake.
“Walipofariki dunia Adam Sapi na Elasto Mang’enya Bunge halikuwa kwenye session (vikao), hivyo leo imetokea tupo kwenye vikao, tunaweza kutumia nafasi hii kwa heshima ya Samuel Sitta,” amesema.
Pia, Zitto amesema Bunge haliendeshwi kwa kanuni peke yake, bali linaendeshwa kwa desturi na kwa maamuzi ya maspika na hivyo anaweza kufanya maamuzi yatakayosaidia baadaye endapo ikitokea hali kama hiyo.
“Naomba kutoa hoja Bunge liahirishe shughuli zake leo (jana) kwa ajili ya kumuenzi Spika Mstaafu Samuel Sitta ambaye ameitumikia nchi kwa muda mrefu sana,” amesema Zitto.
Hata hivyo, Zungu akasisitiza maamuzi yake yanabaki kama aliyoyatoa awali, msimamo ulioibua kelele kutoka kwa wabunge wote ndani ya Bunge na hivyo kupoteza hali ya utulivu.
Baada ya kushindwa kurejesha utulivu, Zungu akasema kwa mujibu wa uzito wa suala lenyewe Kamati ya Uongozi wa Bunge ikutane kwa dakika 15 huku Bunge likiendelea na shughuli zake.
Akasema baada ya kikao hicho cha muda mfupi watatoa majibu ya kile kilichoamuliwa lakini kelele za wabunge ziliendelea.
Baada ya hali hiyo, Zungu akalazimika kusitisha kwa muda wa dakika 15 ili kusubiri majibu ya kikao cha Kamati ya Uongozi.
Baada ya kikao hicho, Zungu akasema kamati hiyo imeridhia Bunge liahirishwe hadi leo saa tatu asubuhi.
Bodi Ya Pamba Kuhamia Mwanza.
Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO, Dodoma
Wizara
ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi imejipanga kuhamishia Bodi ya Pamba katika
Mkoa wa Mwanza kabla ya Novemba 10 mwaka huu ili kuhakikisha wakulima wa
pamba waliopo katika mkoa huo wanapata huduma zilizo bora kwa ukaribu
na haraka.
Hayo
yamesemwa jana mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhe.
William Ole Nasha alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Bukombe Mhe. Doto
Biteko lililohoji juu ya hatua ya Serikali kwa wakulima walioathirika
na pembejeo zilizotolewa ambazo hazikuwa na ubora pamoja na kuhamishia
Bodi ya Pamba katika mkoa huo.
”ili
kuwafikia kirahisi wakulima wa pamba waliopo mkoani Mwanza, Wizara
imeamua kuhamishia Bodi hiyo katika mkoa huo na kwa taarifa zilizopo
Bodi hiyo inatakiwa kuhama haraka iwezekanavyo kabla ya Novemba 10 mwaka
huu”, alisema Mhe.Ole Nasha.
Kwa
upande wa matatizo ya pembejeo, Mhe. Ole Nasha alisema kuwa Serikali
tayari ina taarifa kuhusu tatizo lililowapata wakulima wa pamba katika
maeneo mbalimbali kwa kusambaziwa viuatilifu pamoja na mbegu ambazo
hazikuwa na ubora unaotakiwa hivyo kuathiri wakulima nchini.
“Serikali
iliiagiza Tropical Pesticides Research Institute (TPRI) kufanya
uchunguzi wa malalamiko ya wakulima ambao ulibaini kuwa viuatilifu hivyo
vilikuwa na utendaji hafifu hivyo Serikali itaanza kuzalisha mbegu bora
za pamba za UK08 ili kuhakikisha tatizo hili halijirudii tena”, alisema Mhe. Ole Nasha.
Naibu
Waziri huyo amefafanua kuwa kufuatia changamoto hizo za uotaji wa
mbegu, Serikali iliamua kufanya majaribio ya utoaji wa mbegu ambazo
zilikuwa zikisambazwa hapo awali bila kujua ufanisi katika uotaji wake.
Alithibitisha
kuwa, matokeo ya jaribio hilo yamewezesha kutoa maelekezo kuhusu aina
za mbegu za pamba zenye sifa za msingi ambazo zitasambazwa kwa wakulima
katika msimu wa kilimo wa mwaka 2016/2017.
ASKARI 152 WAFUKUZWA KAZI
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Hamadi Massauni akijibu
hoja mbalimbali za wabunge katika mkutano watano wa Bunge la 11
linaloebdelea Mjini Dodoma Novemba 7, 2016.Jumla
ya askari 152 wamefukuzwa kazi mwaka huu na Jeshi la Polisi kwa sababu
ya kukiuka Sheria, Taratibu na Kanuni ya Jeshi hilo kama zilivyoainishwa
katika Kanuni za Kudumu za Polisi (PGO) namba 103.
Idadi ya askari hao
waliofukuzwa kazi imetolewa leo mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni alipokuwa akijibu swali la Mbunge
wa Viti Maalum Mhe. Maryam Msabaha aliyehitaji kufahamu juu ya idadi ya
askari waliochukuliwa hatua kwa sababu ya utovu wa nidhamu.
Mhandisi Masauni amesema
kuwa kazi ya Vikosi vya Ulinzi na Usalama ni kulinda raia, mali zao
pamoja na mipaka ya nchi lakini kuna baadhi ya askari hao wanakwenda
kinyume na Sheria kwa kuwapiga wananchi na kuwasababishia ulemavu pamoja
na vifo hivyo Jeshi hilo limewachukulia hatua za kinidhamu.
“Jeshi la Polisi hufanya
kazi kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Taratibu zilizopo lakini kuna
baadhi ya askari wamekuwa wakikiuka maadili na mwenendo mwema wa Jeshi
letu hivyo kuanzia Januari 2015 hadi Juni 2016 tuliwachukulia hatua za
kinidhamu askari 200”, alisema Mhandisi Masauni.
Naibu Waziri huyo
amefafanua kuwa baada ya askari hao kuchukuliwa hatua za kinidhamu,
walifanyiwa uchunguzi wa kina na jumla ya askari 152 kati ya 200
walikutwa na hatia hivyo hatua iliyofata ni kuwafukuza kazi.
Akizungumzia kuhusu
mpango wa Serikali juu ya kujenga nyumba za askari Polisi, Mhandisi
Masauni amesema kuwa wanatambua tatizo la makazi ya Askari Polisi katika
maeneo mbalimbali nchini hususani kwenye mikoa mipya hivyo Serikali ina
nia ya kutatua tatizo hilo kwa kuanza ujenzi wa nyumba kwa ajili ya
askari hao.
“Serikali imedhamiria kupunguza tatizo la upu
ngufu wa makazi ya
askari polisi kwa kujenga nyumba kwa awamu kupitia mpango wa ujenzi wa
nyumba 4,136 nchi nzima ambao utaanza kutekelezwa baada ya taratibu za
mkopo wa kuwezesha ujenzi huu kukamilika”, aliongeza Mhandisi Masauni.
Monday, 7 November 2016
HAYA HAPA MAJINA YA WATU WALIOITWA KWENYE INTERVIEW MUHAS KWA AJILI YA AJIRA
Shortlisted Candidates for Interviews
The following candidates have been
shortlisted to several positions Medical Specialists II, Medical Officer
II, Nursing Officer II, Assistant Nursing Officer II, Health Laboratory
Scientist II, Health Laboratory Technologist II, Pharmacist II,
Pharmaceutical Technician II, Radiographer II, Senior Mechanical
Engineer II and Driver II . They are required to attend the interview
as per schedule shown on the advert.
Interview dates: 9th, 10th and 11st November, 2016
Venues: 24 hours Study Hall located at Library Building and MPL Board Room located at 1st Floor, MPL Building (Block C)
Kindly note that:
- The time and venue for the interview for each cadre has been shown.
historia ya samweli sitta
Historia yake;
Samuel John Sitta alizaliwa Desemba 18, 1942 huko wilayani
Urambo Mkoa wa Tabora. Sitta alisoma Shule ya Msingi Urambo kati ya
mwaka 1950 – 1953, kisha alikwenda Wilaya ya Sikonge mwaka 1954 - 1957
na kuendelea na masomo ya “Middle School” katika shule ya “Sikonge
Middle School”. Baadaye mwaka 1958 – 1963 alianza masomo ya sekondari
Shule ya Wavulana Tabora yaani “Tabora Boys” kidato cha I – IV na cha V –
VI.
Mara tu baada ya kuhitimu masomo ya sekondari, Sitta
alijiunga Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kusomea Shahada ya Sheria
(L LB) mwaka 1964 na kuhitimu mwaka 1971.
Sitta amesoma shahada yake kwa miaka 7 kwa sababu mwaka
1966, wakati yuko mwaka wa pili na akiwa kiongozi wa wanafunzi UDSM,
wanafunzi waligoma na kuandamana kupinga kujiunga na Jeshi la Kujenga
Taifa (JKT) na kukatwa mishahara yao baada ya JKT. Hoja ya wanafunzi
ilikuwa na mantiki kubwa, kwamba mbona vigogo wa serikali na wanasiasa
wanalipwa mishahara minono na marupurupu makubwa?
Baada ya shinikizo hilo la wanafunzi Mwalimu Julius Nyerere
alikubali kupunguza mshahara wake wa Sh4,000 bila kodi akaagiza pia
mishahara ya mawaziri ipunguzwe kwa asilimia mbili. Miezi miwili baadaye
akatangaza Azimio la Arusha (Februari 5, 1967) kuyapa uzito malalamiko
ya wanafunzi hao.
Watukutu wawili – Sitta na Wilfred Mwabulambo (sasa
marehemu) na wengine kadhaa – waliojitia wazimu na kutetea kile
walichokiita haki zao, (haki za wakulima na wafanyakazi), walimshutumu
Mwalimu Nyerere kwa maneno makali wakidai “…ni heri wakati wa ukoloni
kuliko utawala wa Mwalimu”.
Mwalimu Nyerere alikasirika na kuwafukuza chuo wanafunzi
wote 400 kwa kile alichokiita “kwenda kufunzwa adabu majumbani mwao”.
Miezi kumi baadaye, baada ya Nyerere kushawishiwa na hasira kutulia
akaamua kuwarudisha chuoni wanafunzi 392. Viongozi wa mgomo; Sitta na
wenzake 7 walitiliwa ngumu, hawakurejeshwa chuoni.
Busara za viongozi wa chuo zilifanya Mwalimu aliliwe zaidi
na kuandikiwa barua mbili maalumu na chuo zenye Kumb. Na. C3/Sa.13 ya
2/3/1967 na C3/Ss.13 ya 9/07/1967. Mwalimu alikubali kilio hicho na
kuwaruhusu vijana hao wanane warudi kwa sharti kwamba wale watukutu
wawili (Sitta na Mwabulambo) watandikwe viboko na “Mwalimu Nyerere”
mwenyewe. Hii ndiyo ilikuwa pona ya Sitta ambaye alirejea UDSM na
kuendelea na masomo kwa miaka kadhaa hadi alipohitimu mwaka 1971.
Wakati Sitta anarudi chuoni tayari alikuwa mwajiriwa wa
Kampuni ya Mafuta ya “CALTEX OIL” kama Meneja wa Tawi (1967 – 1969) na
mwaka 1969 – 1975 aliajiriwa na Shirika la Maendeleo la Taifa kama
Katibu na Mkurugenzi wa Utawala.
Baadaye mwaka 1976 Sitta aliamua kujiendeleza kielimu
katika masuala ya Usimamizi nchini Uswisi kwenye Chuo Kikuu cha IMEDE
ambako alihitimu Stashahada ya Juu ya Usimamizi mwaka huohuo 1976.
Chini ya mfumo wa chama kimoja, Sitta amekuwa kiongozi wa juu wa CCM na serikali akiwa mbunge, mkuu wa mkoa na waziri katika nyakati tofauti na ameendelea kuwa mbunge na waziri katika mfumo wa vyama vingi.
Chini ya mfumo wa chama kimoja, Sitta amekuwa kiongozi wa juu wa CCM na serikali akiwa mbunge, mkuu wa mkoa na waziri katika nyakati tofauti na ameendelea kuwa mbunge na waziri katika mfumo wa vyama vingi.
Sitta amemuoa Margareth Simwanza Sitta na wana familia imara.
Mbio za ubunge
Enzi za chama kimoja 1975 - 1995 Sitta amekuwa mbunge wa Jimbo la Urambo (kabla halijagawanywa na kuwa Urambo Magharibi na Mashariki) na pia alifanikiwa kuwa waziri kwa nyakati tofauti. Kwa mfano wakati wa kipindi cha mwisho cha Mzee Mwinyi, Sitta alikuwa Waziri za Katiba na Sheria.
Mbio za ubunge
Enzi za chama kimoja 1975 - 1995 Sitta amekuwa mbunge wa Jimbo la Urambo (kabla halijagawanywa na kuwa Urambo Magharibi na Mashariki) na pia alifanikiwa kuwa waziri kwa nyakati tofauti. Kwa mfano wakati wa kipindi cha mwisho cha Mzee Mwinyi, Sitta alikuwa Waziri za Katiba na Sheria.
Mwaka 1995 Sitta aliingia kwenye mapambano mapya ya siasa
za vyama vingi na kwa bahati mbaya akawa mmoja wa vigogo walioangushwa
na wabunge wa NCCR. Mshindani wake mkuu alikuwa Msina Jacob Abraham.
Msina alishinda kwa kura 10,788 dhidi ya 9,497 za Sitta.
Sitta alirudi tena kwenye jukwaa la siasa mwaka 2005 kwenye
uchaguzi mkuu na aliwashinda wapinzani wake wakuu Lumatiliza Yotamu
Lubungila wa NCCR na Wilson George Ntakamulenga wa CUF. Sitta alipata
kura 28,660 (72.3%) na kurejesha heshima yake jimboni Urambo Mashariki.
Kurudi kwa nguvu kulimpa nafasi ya kuwania na kuteuliwa na CCM kugombea
uspika wa Bunge la Tanzania na akaliongoza Bunge la Tisa kwa mafanikio
na changamoto nyingi.
Mwaka 2010 Sitta alishiriki tena uchaguzi Urambo Mashariki
akawashinda wapinzani wake wakuu Msafiri Abdulrahmani Mtemelwa (Chadema)
na Zombwe Lotto Edward (CUF) kwa kupata kura 19,947 (70.47%). Baada ya
ushindi huo, Sitta alijaribu tena kuwania uspika bila mafanikio;
utendaji wake wa kuiuma serikali na wakati mwingine kuipuliza kwenye
Bunge la Tisa ulimfanya achukiwe na serikali.
Ilipoonekana ana nguvu akatengenezewa “chui wa karatasi”
(mshindani), Andrew Chenge. Chenge naye akachukua fomu ya uspika ghafla,
likatengenezwa ‘zengwe’ kuwa wagombea wote wana nguvu, hapo CCM ikapata
mwanya wa kutamka kuwa haiwataki wote ili kuondoa mvutano. Sitta
akapoteza ndoto za uspika na ukahamia kwa mwanamama Anne Makinda.
Rais Jakaya Kikwete alipotangaza Baraza la Mawaziri mwaka
2010 alimpa Sitta Wizara ya Afrika Mashariki kama Waziri, wadhifa
aliodumu nao hadi mwaka huu mwanzoni alipobadilishwa na kupelekwa Wizara
ya Mawasiliano na Uchukuzi.
Mbio za urais
Samuel John Sitta alianza mbio za urais “kimyakimya” tangu alipokuwa Spika wa Bunge la Tisa (2005 – 2010). Kuna nyakati alikuwa akitoa kauli zinazoashiria kuwa nchi inayumba na haina uongozi thabiti huku akionyesha kuwa nchi ina viongozi thabiti na hawajapewa uongozi mkuu wa nchi, akiwemo yeye.
Hata alipoliongoza Bunge la Katiba mwaka 2014, mara nyingi Sitta alionekana kama mtu mwenye shauku kubwa na urais na alipohojiwa, mara kwa mara, juu ya urais alionyesha ana ndoto hizo. Mara kadhaa, alilalamika kuwa wala rushwa wakubwa wanampiga vita kwa sababu ni msafi.
Samuel John Sitta alianza mbio za urais “kimyakimya” tangu alipokuwa Spika wa Bunge la Tisa (2005 – 2010). Kuna nyakati alikuwa akitoa kauli zinazoashiria kuwa nchi inayumba na haina uongozi thabiti huku akionyesha kuwa nchi ina viongozi thabiti na hawajapewa uongozi mkuu wa nchi, akiwemo yeye.
Hata alipoliongoza Bunge la Katiba mwaka 2014, mara nyingi Sitta alionekana kama mtu mwenye shauku kubwa na urais na alipohojiwa, mara kwa mara, juu ya urais alionyesha ana ndoto hizo. Mara kadhaa, alilalamika kuwa wala rushwa wakubwa wanampiga vita kwa sababu ni msafi.