Sunday, 31 July 2016

Picha- Rais Magufuli Afanya Mikutano Tinde,Isaka na Kahama Mkoani Shinyanga

Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia mamia wa wakazi wa Kahama mkoani Shinyanga mara baada ya kuwasili akitokea Nzega mkoa Tabora Julai 31,2016



Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Mbunge wa zamani wa Kahama James Lembeli mara baada ya kuwasalimia wananchi waliofika kwa ajili ya kumsikiliza Rais katika viwanja hivyo vya Kahama.

Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia mamia wa wakazi wa Isaka mkoani Shinyanga.


Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akiwa ameambatana na Mbunge wa zamani wa Kahama James Lembeli ambaye ni mwanachama wa Chadema mara baada ya kumaliza kuhutubia mkutano mjini Kahama mkoani Shinyanga.

Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akicheza pamoja na Wanakwaya wa Haleluya Kuu kutoka Kanisa la KKKT-Usharika wa Yeru Ndala Shinyanga mara baada ya kumaliza kuhutubia mkutano Kahama mjini mkoani Shinyanga.

Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia mara baada ya kuoneshwa picha yake na kijana mmoja aliyeishika picha hiyo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia mamia ya wakazi wa Tinde mkoani Sinyanga-Picha zote na IKULU
Share:

Pichaz: Waziri Nape, Lowassa, Mbowe walivyoshiriki kuuaga mwili wa marehemu Senga


July 31 2016 mwili wa marehemu Mwanahabari Joseph Senga umeagwa Dar es salaam leo kuelekea Mwanza kwa ajili ya maziko, baadhi ya viongozi wa serikali na siasa wameshiriki wakiwemo Waziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo Nape Nnauye, Waziri mkuu wa zamani Edward Lowassa na wengine.
Marehemu Joseph Senga ndiye mpiga picha aliyenasa tukio la mauaji ya Mwandishi wa habari wa kituo cha talevisheni CHANEL 10 Daud Mwangosi kilichotokea  September 2 2012 katika kijiji cha Nyololo, Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa ambaye alifariki July 28 2016 akiwa India kwa matibabu ya ugonjwa wa moyo.
Ninazo picha kadhaa kutokea Sinza Dar es salaam ambapo ndipo kazi yote ilifanyika
33
Waziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo Nape Nnauye
2X6A0690 copy
Kutoka kushoto Edward lowassa, Nape Nnauye na Freeman Mbowe
5
Mke wa marehemu Joseph Senga (aliyevaa ushungi)
22
WhatsApp Image 2016-07-31 at 13.50.06
WhatsApp Image 2016-07-31 at 13.50.10
Wapigapicha na wanachama wa Press Photographer wakishiriki kubeba jeneza la marehemu
Hii hapa chini ni moja ya picha yake enzi za uhai
uhai
Share:

HAYA HAPA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA CHUO CHA AFYA KOLANDOTO SHINYANGA 2016/2017

Share:

DOWNLOAD JOINING INSTRUCTION CHUO CHA AFYA KOLANDOTO 2016/2017

Share:

LIST OF SELECTED STUDENTS BY NACTE FIRST BATCH 2016/2017 ACADEMIC YEAR

Share:

DOWNLOAD HAPA JOINING INSTRUCTIONS CHUO CHA AFYA BUMBULI 2016/17

Share:

Picha 9: Rais Magufuli alivyoendelea na ziara yake Igunga na Nzega Tabora

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli jana July 30 2016 ameendelea na ziara yake katika Mkoa wa Tabora akitokea Mkoa wa Singida.

Mkoani Tabora, Rais Magufuli alizungumza na wananchi waliosimamisha msafara wake katika vijiji vya Nanga na Ziba na alifanya mikutano ya hadhara Igunga na Nzega ambako amewahakikishia wananchi kuwa serikali yake itahakikisha inatekeleza ahadi zilizopo katika Ilani ya Uchaguzi Mkuu ya Mwaka 2015.

Katika mkutano wa hadhara uliofanyika Igunga, Rais Magufuli amepokea malalamiko ya wananchi kuhusu kutoanza kutumika kwa kituo cha mabasi na soko na amewaagiza viongozi wa Mkoa wa Tabora kuhakikisha kituo cha mabasi cha Igunga na soko la Igunga vinaanza kutumika kuanzia Jumatatu ijayo ya tarehe 01 Agosti, 2016.

Kuhusu kero ya maji, Dkt. Magufuli alisema Tanzania imepata mkopo wa dola za kimarekani Milioni 268.35 kutoka nchini India ambazo zitatumika kutekeleza mradi wa kusambaza maji ya ziwa Viktoria katika Miji ya Tabora, Igunga, Nzega, Sikonge
Rais Magufuli  na Mwenyekiti wa Kijiji cha Nanga Wilaya ya Igunga Masesa Kishiwa Makala kutoka Chadema wakati akiwa safarini kuelekea Nzega Mkoani Tabora.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli na wabunge wa Singida
Rais Magufuli katika Kijiji cha Nanga Wilayani Igunga mkoani Tabora.




Share:

Mtuhumiwa wa Mauaji Jijini Mwanza Auawa akijaribu Kutoroka


MTUHUMIWA wa ujambazi Msafiri Suleiman maarufu kama Juma Msukuma ameuawa wakati akijaribu kuwatoroka Polisi.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea Julai 28 mwaka huu majira ya saa 10.30 jioni katika eneo la Igoma kata ya Igoma jijini Mwanza.

Kamanda Msangi alisema mtuhumiwa siku hiyo alikuwa amekamatwa na Polisi akituhumiwa kufanya matukio ya unyang’anyi wa kutumia silaha akishirikiana na wenzake watatu.

Aliwataja watu hao aliokuwa akishirikiana nao ambao kwa sasa wamekamatwa na polisi kuwa ni Jackson Magesa ( Nyakibimbi), Samwel Mwita na Boniphace Nyamhanga.

Kamanda alisema baada ya mahojiano na polisi mtuhumiwa alikiri kuhusika na uhalifu na akakubali kwenda kuwaonesha askari sehemu aliyoficha silaha maeneo ya Buhongwa mlimani.

Alisema walipofika eneo husika aliwaonesha mkasi mkubwa wa kukatia vyuma na kipande cha nondo, huku akiwathibitishia kuwa silaha alikuwa ameichimbia ardhini katika eneo hilo.

“Wakati askari wakiwa kwenye harakati za kufukua ili waichukue silaha hiyo, mtuhumiwa alitumia mwanya huo kuanza kukimbia huku akiwa na pingu mkononi, askari walifyatua hewani risasi tatu, lakini mtuhumiwa hakutii amri hiyo ndipo alipopigwa risasi mguuni na kufanikiwa kukamatwa”, alifafanua.

Alisema alifariki dunia akiwa njiani kupelekwa hospitali.

“ Watuhumiwa aliokuwa akishirikiana nao tumewakamata na tumewakuta wakiwa na bunduki aina ya Rifle Mark 4 ikiwa na risasi nne, ikiwa na kitako cha bunduki waliyopora, nyundo moja na vipande vitatu vya nondo”, alisema.

“ Watuhumiwa hao tunawashikilia kwa matukio ya unyang’anyi Nyashishi, Buhongwa, Bulale, Nyambichi na Mwananchi ambapo walipora silaha toka kwa mlinzi wa Kampuni ya Paroma Patrol Security Service”, aliongeza
Share:

Wizara ya Elimu kuhamia Dodoma Agosti

Ndalichako 
WIZARA ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imesema imejipanga kuhakikisha inahamia Dodoma kabla au ifikapo Agosti 15 mwaka huu.
Kumekuwa na hekaheka kwa taasisi na wizara mbalimbali za umma kuhamia Dodoma ili kuunga mkono tamko la Rais John Magufuli ambaye Jumamosi ya wiki iliyopita aliuahidi  Mkutano Mkuu Maalumu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa Serikali yake itatekeleza ndoto ya siku nyingi ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere ya kuhamia katika mji mkuu huo.
Jana Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imekuwa ya tatu kutangaza kuhamia Dodoma baada ya ile ya Kilimo, Uvuvi na Mifugo na Wizara ya Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu.
Wizara hizo zinaitikia wito wa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ambaye alitangaza kuhamia Dodoma ifikapo Septemba mwaka huu huku akiwataka mawaziri kumfuata.
Tangazo lililotolewa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa watumishi wake limeeleza kuwa Wizara hiyo itahama kwa awamu mbili.
Awamu ya kwanza ambayo itatakiwa iwe imehamia Dodoma ifikapo Agosti 15 mwaka huu, itahusisha idara na vitengo vipatavyo tisa.
Kwa mujibu wa tangazo hilo vitengo au idara zitakazohusika ni pamoja na Idara ya Utawala na Rasilimali watu, Idara ya sera na mipango.
Nyingine ni Idara ya Elimu ya Juu, Idara ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi. Kwa upande wa vitengo vitakavyohusika ni pamoja na Kitengo cha Ununuzi na Ugavi, Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani, Kitengo cha Sheria, Kitengo cha Habari na Kitengo cha Tehama (ICT).
Tangazo hilo pia limebainisha kuwa awamu ya pili ya kuhamia Dodoma itakuwa ni ifikapo Septemba 15, mwaka huu na itahusisha idara na vitengo vitatu.
“Ofisi ya kamishna wa elimu, Kitengo cha fedha na uhasibu, Kitengo cha uratibu wa elimu kikanda na
Share:

Magazeti ya Leo Jumapili ya Julai 31, 2016

Share:

Saturday, 30 July 2016

Rais Magufuli ndani ya Igunga, mwenyekiti wa CHADEMA aomba amsalimie.

Katika mwendelezo wa ziara yake ya siku nne katika Mikoa ya Singida, Tabora, Shinyanga na Geita, Rais Magufuli amefanya mkutano Igunga.

Katika kuonyesha jinsi ambavyo wananchi wengi wanakubaliana na mtazamo na mwelekeo wake katika hatma ya Taifa, Mwenyekiti wa CHADEMA amewaomba sana walinzi wa Rais ili asalimie Rais kwa sababu anachokifanya Rais kinamgusa katika hali chanya kimaisha na kitaifa.

Rais baada ya kuona tukio hilo aliwaomba walinzi wake kama kuna uwezekano wamruhusu.

Rais Magufuli amezungumza na wananchi waliosimamisha msafara wake katika vijiji vya Nanga na Ziba na amefanya mikutano ya hadhara Igunga na Nzega ambako amewahakikishia wananchi kuwa serikali yake itahakikisha inatekeleza ahadi zilizopo katika Ilani ya Uchaguzi Mkuu ya Mwaka 2015.

Katika mkutano wa hadhara uliofanyika Igunga, Rais Magufuli amepokea malalamiko ya wananchi kuhusu kutoanza kutumika kwa kituo cha mabasi na soko na amewaagiza viongozi wa Mkoa wa Tabora kuhakikisha kituo cha mabasi cha Igunga na soko la Igunga vinaanza kutumika kuanzia Jumatatu ijayo ya tarehe 01 Agosti, 2016.

Kuhusu kero ya maji, Dkt. Magufuli amesema Tanzania imepata mkopo wa dola za kimarekani Milioni 268.35 kutoka nchini India ambazo zitatumika kutekeleza mradi wa kusambaza maji ya ziwa Viktoria katika Miji ya Tabora, Igunga, Nzega, Sikonge


VIDEO:
 

[​IMG]
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwenyekiti wa Kijiji cha Nanga Wilaya ya Igunga Ndugu Masesa Kishiwa Makala kutoka Chadema wakati akiwa safarini kuelekea Nzega Mkoani Tabora.
[​IMG]
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wakazi wa Ziba Wilayani Igunga mkoani Tabora.
[​IMG]
[​IMG]
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na mamia ya wakazi wa Igunga mkoani Tabora katika ziara yake ya kikazi katika Mkoa huo wa Tabora
[​IMG]
Mke wa Rais, Mama Janeth Magufuli akiwasalimia wananchi.
[​IMG]
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wakazi wa Igunga mkoani Tabora mara baada ya kuwahutubia Wilayani hapo.
Share:

Taarifa Ya Bunge Kwa Umma Kuhusu Kamati Za Bunge

Share:

Rais Magufuli atengua uteuzi wa Mkurugenzi siku 23 tangu amteue

Share:

Official VIDEO | Profesor Jay Ft. Sholo Mwamba - Kazi Kazi | Watch/Download


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger