Tuesday, 19 July 2016

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU WANACHUO WALIOKUWA WANASOMA STASHAHADA MAALUM YA UALIMU KATIKA CHUO KIKUU CHA DODOMA

TAARIFA KWA UMMA
 

KUHUSU WANACHUO WALIOKUWA WANASOMA STASHAHADA MAALUM YA UALIMU KATIKA CHUO KIKUU CHA DODOMA
1.0 UTANGULIZI
Itakumbukwa kwamba tarehe 28 Mei, 2016 Serikali iliwarejesha nyumbani wanafunzi 7,805 waliokuwa wanasoma Stashahada Maalum ya Ualimu wa Sayansi na Hisabati Chuo Kikuu Dodoma. Hatua hiyo ilichukuliwa kutokana na mgomo wa walimu uliokuwa umedumu kwa takribani wiki 3. Wanafunzi waliosimamishwa masomo walikuwa wamegawanyika katika makundi makuu mawili. Kundi la kwanza lilikuwa ni  wanafunzi 6,595 waliodahiliwa katika Stashahada Maalumu ya Ualimu wa Elimu ya Sekondari na kundi la  pili lilikuwa  na wanafunzi 1,210 waliodahiliwa katika mafunzo ya Stashahada ya Ualimu wa Elimu ya Msingi.
2.0 SIFA ZA KUJIUNGA NA PROGRAMU MAALUM YA STASHAHADA

Baada ya hatua ya kuwaondoa wanafunzi chuoni kuchukuliwa, Serikali ilifanyaUchambuzi wa wanafunzi hao kwa lengo la kujiridhisha na sifa zao.  Sifa zilizotakiwa ni ufaulu wa Daraja la I hadi la III na credit mbili au zaidi katika  masomo ya Sayansi na Hisabati.Mchanganuo wa ufaulu wa Kidato cha Nne kwa wanafunzi hao ni kama ifuatavyo:

Jedwali Na. 1: Mchanganuo wa wanafunzi kwa ufaulu
KUNDI

 
DARAJA
JUMLA

 
I
II
III
IV
STASHAHADA YA UALIMU WA SEKONDARI
37
354
6183
21
6595
STASHAHADA YA UALIMU WA MSINGI
1
8
1170
31
1210
JUMLA
38
362
7353
52
7805
Chanzo: Baraza la Mitihani Tanzania

Jedwali Na. 1 linaonesha kuwa kulikuwa na wanafunzi 52 waliopata Daraja la IV kinyume na matakwa ya Programu ambapo mwanafunzi alitakiwa awe na ufaulu wa Daraja la I – III.  Aidha, uchambuzi zaidi ulifanyika kwa wanafunzi wenye ufaulu wa Daraja la I-III ili kujiridhisha kama wamekidhi kigezo cha kuwa na ufaulu katika masomo mawili kwa kiwango cha C-A.

3.0   UCHAMBUZI WA SIFA ZA WANAFUNZI

Uchambuzi wa sifa kwa kuzingatia vigezo vya kujiunga vilivyowekwa umebainisha yafuatayo:

1.    Wanafunzi 6,595 walidahiliwa kusoma programu ya Stashahada Maalum  ya Ualimu wa Elimu ya Sekondari kwa Masomo ya Hisabati na Sayansi.Kati yao,6305 walikuwa na sifa stahiki ambazo ni ufaulu kwa Daraja la I – III na ufaulu kwa kiwango cha gredi C-A katika masomo mawili ya Sayansi.



Wanafunzi 4,720 walikuwa mwaka wa kwanza na wanafunzi 1,585 walikuwa mwaka wa pili.  Mchanganuo wa ufaulu wao umeainishwa katika Jedwali Na. 2.

Jedwali 2: Ufaulu wa Wanafunziwa Stashahada ya Ualimu Sekondari Waliokidhi Vigezo vya Udahili
NA
MWAKA WA MASOMO
MADARAJA
JUMLA
I
II
III
1
Mwaka I
8
126
4586 
4720
2
Mwaka II
29
219
1337
1585
JUMLA
37
345
5923
6305


2.    Wanafunzi 290 hawakuwa na sifa za kudahiliwa kwenye Programu maalum ya ualimu wa Shule za Sekondari. Matokeo ya Kidato cha Nne ni kama ifuatavyo:
DARAJA
JUMLA
I
II
III
IV
0
9
260
21
290


Jedwali linaonesha kuwa:

a)      Wanafunzi 21 walikuwa na ufaulu wa Daraja la IV wakati walipaswa kuwa na Daraja la I - III;

b)      Wanafunzi 269 walikuwa na ufaulu wa kati ya Daraja la I-III (II – 9; III - 260) lakini hawakuwa na Ufaulu wa kiwango cha C-A kwa masomo mawili ya Sayansi.

3.1  Programu ya Stashahada ya Ualimu wa Elimu ya Msingi

Uchambuzi wa sifa ulifanyika pia kwa wanafunzi 1,210 waliokuwa wamedahiliwa katika Stashahada ya Ualimu wa Elimu ya Msingi na kubaini yafuatayo:

(i)      Wanafunzi 29 wa mwaka wa II walikuwa ni walimu wa shule za msingi ambao walikuwa wamehitimu Kidato cha Nne na kuhudhuria mafunzo ya Ualimu wa Cheti (Daraja la IIIA) ambao walikuwa na uzoefu kazini wa miaka miwili au zaidi. Mchanganuo wa matokeo yao ya Kidato cha Nne umeainishwa katika jedwali lifuatalo:
Na
KUNDI
DARAJA
JUMLA
I
II
III
IV
1
MWAKA 1
0
0
1
4
5
2
MWAKA 2
1
2
7
14
24
JUMLA
1
2
8
18
29


(ii)    Wanafunzi 1,181 walikuwa ni wahitimu wa Kidato cha Nne ambao mchanganuo wa matokeo yao ya Kidato cha Nne umeainishwa katika Jedwali lifuatalo:

S/N

KUNDI
DARAJA
JUMLA
I
II
III
IV
1
MWAKA 1
0
4
1011
0
1015
2
MWAKA 2
0
2
151
13
166
JUMLA
0
6
1162
13
1181
  4.0  MAAMUZI YA SERIKALI

Kufuatia uchambuzi uliofanyika, Serikali imefanya maamuzi yafuatayo:

4.1  Kundi la Stashahada Maalumu ya Ualimu wa Elimu ya Sekondari

(i) Kwa kuwa uchambuzi umebainisha kuwa Wanafunzi wenye ufaulu wa Daraja la I na la II ambao pia wamefaulu masomo mawili ya Sayansi kwa kiwango cha C-A ni 382 (mwaka wa I -134 na mwaka wa II - 248), wanafunzi hao ndiyo pekee watakaorudishwa katika Chuo Kikuu cha Dodoma ili wakamalizie mafunzo yao katika Chuo hicho.

(ii) Wanafunzi 4,586 wa mwaka wa I wa Programu Maalum ya Stashahada ya Ualimu wa Elimu ya Sekondari waliokidhi vigezo vya ufaulu watahamishiwa katika Vyuo vya Ualimu vya Morogoro, Butimba, Mpwapwa, Songea na Tukuyu kuendelea na masomo yao.

(iii) Wanafunzi 1,337 wa Mwaka II watahamishiwa kwenye Vyuo vya Ualimu vya Korogwe na Kasulu kumalizia masomo yao.

(iv) Wanafunzi 290 waliokuwa wamedahiliwa kusoma Programu Maalum ya Stashahada ya Ualimu wa Elimu ya Sekondari Masomo ya Sayansi na Hisabati ambao hawana sifa stahiki wanashauriwa kuomba mafunzo yanayolingana na sifa walizo nazo kwenye chuo chochote wanachotaka wao.

4.2 Kundi la Programu ya Ualimu wa Elimu ya Msingi

Wanafunzi katika kundi hili hawakuwa sehemu ya program maalum ya kupunguza uhaba wa walimu wa Sekondari wa Sayansi na Hisabati. Walikuwa wanaandaliwa kufundisha shule za msingi wakati lengo la Programu Maalum ilikuwa ni kukabiliana na tatizo za uhaba wa walimu wa Sekondari.  Maudhui ya program waliyokuwa wanasoma hayakuwa sawasawa na yale ya Programu ya Ualimu wa Sekondari wa Sayansi na Hisabati.

(v)  Wanafunzi 29 wa mwaka wa II wenye Cheti cha Daraja IIIA waliodahiliwa kusoma Stashahada ya Ualimu wa Shule za Msingi watahamishiwa katika Chuo cha Ualimu Kasulu wamalizie masomo yao kwa gharama zao wenyewe.

(vi)  Wanafunzi 1,181 waliodahiliwa kusoma Stashahada ya Kawaida ya Ualimu wa Elimu ya Msingi waombe  mafunzo yanayolingana na sifa walizonazo mahali popote watakapotaka wao.

5.0  GHARAMA ZA MASOMO

Serikali itaendelea kuwapatia mikopo wanafunzi watakaorejeshwa UDOM. Aidha, wanafunzi watakaohamishiwa kwenye Vyuo vya Ualimu vya Serikali watapewa mkopo wa kiasi cha Sh. 600,000/= kwa mwaka ambayo ni ada ya Mafunzo ya Ualimu itakayolipwa moja kwa moja Chuoni.
6.0 HITIMISHO

(i)  Wanafunzi wote wanaorejeshwa Chuo Kikuu cha Dodoma wataanza masomo mwezi Oktoba 2016.

(ii) Wanafunzi watakaohamia katika Vyuo vya Ualimu wataendelea na mafunzo yao mwezi Septemba mwaka 2016. 

(iii) Wanafunzi wote watatakiwa kuripoti wakiwa na vyeti vyao halisi vya Kidato cha Nne ambavyo vitahakikiwa kabla hawajapokelewa rasmi kwenye vyuo walivyopangiwa. 

(iv) Majina ya wanafunzi wenye sifa na vyuo walivyopangiwa pamoja na wale wasio na sifa yanapatikana katika tovuti ya Chuo Kikuu cha Dodoma ambayo ni www.udom.ac.tz.


IMETOLEWA NA

 
Prof. Joyce Lazaro Ndalichako (Mb)

WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA

19 Julai, 2016
 
Share:

Breaking news:Orodha ya majina ya wanachuo wanaorudi kusoma stashahada maalum ya ualimu (UDOM)

Orodha ya majina ya wanachuo wanaorudi kusoma stashahada maalum ya ualimu (UDOM)
Image result for SERIKALI  YA TANZANIA 


Majina ya wanachuo waliokuwa wanasoma stashahada maalum ya ualimu chuo kikuu cha Dodoma waliopangiwa kurudi kwenye chuo hicho, wanaokwenda kwenye vyuo vya ualimu na ambao hawana vigezo vya kujiunga na vyuo hivyo.


>>> LIST OF SELECTED STUDENT - UDOM (53.28 kB)<<<

  LIST OF SELECTED STUDENTS - TEACHER COLLEGE
  (669.91 kB)

 
 LIST OF NONELIGIBLE STUDENTS (47.38 kB)
 
Share:

Breaking news:Wanafunzi 7800 waliofukuzwa UDOM, ni 382 tu ndio wenye sifa

Elimu nchini Tanzania Pof.Joyce Lazaro Ndalichako atoa msimamo wa Serikali juu ya wanafunzi waliofukuzwa chuo kikuu cha Dodoma, leo jijini Dar es Salaam, ambapo amesema kuwa kati ya wanafunzi zaidi ya elfu saba waliokuwa wamedahiliwa na kuanza chuo kikuu dodoma ni wanafunzi 382 tu ndio wenye sifa ya kurudi chuoni.
Chanzo: Radio One



[​IMG]

Serikali imetangaza orodha ya wanafunzi ambao watarejea kuendelea na masomo katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) baada ya uchambuzi kumalizika na kupatikana idadi ya wanafunzi ambao wana sifa za kuendelea na masomo.

Akizungumza na waandishi wa habari, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako alisema kuwa kwa kipindi chote walikuwa wakifanya uchambuzi ili kuona ni wanafunzi gani walikuwa na sifa za kusoma kozi hiyo maalum ambayo ilianzishwa kutokana na tatizo la walimu wa Sayansi.

Alisema kuwa programu hiyo ilikuwa inahitaji walimu ambao watakwenda kufundisha shule za sekondari lakini kulikuwa na wanafunzi 1,210 ambao walikuwa wanachukua stashahada ya ualimu wa shule za msingi ambao ni kinyume na malengo na 6,595 wakichukua stashahada ya kufundisha shule za sekondari.

“Baada ya hatua ya kuwaondoa wanafunzi chuoni kuchukuliwa, serikali ilifanya uchambuzi wa wanafunzi hao kwa lengo la kujiridhisha na sifa zao. Sifa zilizotakiwa ni ufaulu wa daraja la 1 hadi daraja la 3 na krediti mbili au zaidi katika masomo ya Sayansi na Hisabati,

“Lakini baada ya uchambuzi kufanyika kati ya wanafunzi wanaosomea ualimu wa sekondari 6,595 ni wanafunzi 382 pekee ndiyo wana sifa za kuendelea na masomo yao, 134 ni mwaka wa kwanza na 248 ni mwaka wa pili,” alisema Prof. Ndalichako.

Aidha alisema kuwa wengine 4,586 wa mwaka wa kwanza wa programu maalum wa stashahada ya ualimu wa sekondari waliokidhi vigezo vya ufaulu watahamishiwa katika vyuo vya ualimu vya serikali ambavyo ni Morogoro, Butimba, Mpwapwa, Songea na Tukuyu kuendelea na masomo na wanafunzi 1,337 wa mwaka wa pili watahamishiwa vyuo vya Korogwe na Kasulu ili kumalizia masomo yao.

Pia alisema kuwa serikali itaendelea kuwapatia mikopo wanafunzi watakaoendelea kusoma UDOM na watarejea chuoni mwezi Oktoba mwaka huu, huku wale wa vyuo vya ualimu watakuwa wakilipiwa ada ya 600,000 kwa mwaka ambayo ndiyo ada ya vyuo hivyo na wataripoti chuoni mwezi Septemba.

Kwa upande wa wanafunzi wa kufundisha elimu ya shule ya msingi, Prof. Ndalichako alisema wanafunzi 29 wa mwaka wa pili ambao wana cheti cha daraja A la ualimu watahamishiwa Chuo cha Ualimu Kasulu ili wamalize masomo yao ila tu kwa gharama zao huku wengine 1,181 akiwataka waombe nafasi katika vyuo vingine katika masomo ambayo wana sifa zinazolingana nao.

Aidha katika hatua nyingine, Prof. Ndalichako alisema kuwa migomo iliyokuwa ikitokea chuoni UDOM kwa walimu kugoma kuwafundisha wanafunzi hao yawezekana ilikuwa ikichangiwa na wanafunzi hao kwani uwezo wa chuo cha UDOM ilikuwa ni kupokea wanafunzi 1,180 lakini wakapokea wanafunzi 7,805.

“Walimu kwao mzigo ulikuwa ni mzito wewe utafanya nini?, kwahiyo tukubali kuwa wingi wa wanafunzi ulichangia kutokea mgomo sababu walimu wameajiriwa kufundisha na wengine wa digrii sasa kupokea wanafunzi 7,805 na ilitakiwa 1,180 walikuwa wengi,” alisema Prof. Ndalichako.
Share:

TCU kuanza kudahili wanafunzi wa kujiunga vyuo vikuu kesho


Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), itaanza kudahili wanafunzi waliomaliza kidato cha sita wanaoomba kujiunga na vyuo vikuu kuanzia kesho. 
Akizungumza jana, Kaimu Mkurugenzi wa Udahili na Nyaraka wa TCU, Dk Kokubelwa Mollel alisema udahili kwa wenye diploma utaanza Julai 31. 
Dk Mollel alisema kazi hiyo itaendelea kwa mwezi mzima ili kuruhusu wananchi wengi zaidi kupata fursa ya kuomba kudahiliwa na udahili huo utafanyika kwa njia ya mtandao.
Alisema ili wanafunzi waweze kuelewa programu zinazotolewa na vyuo vikuu, tume hiyo imeandaa maonyesho ya 11 yatakayofanyika kuanzia Julai 20 hadi 22, mwaka huu. 
Alisema maonyesho hayo yatafanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam na kufunguliwa na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako.
Share:

BREAKING NEWS:MWANAFUNZI WA UDSM MWAKA WA TATU AKAMATWA AKIIBA LAPTOP-VIDEO

Mwanafunzi wa chuo kikuu UDSM amekamatwa akitaka kuiba laptop.swala la wizi hasa wakati huu vyuo vinaelekea kufungwa limekuwa ni common sana.

Share:

Monday, 18 July 2016

Rais Magufuli amteua Prof. Sylvester Mpanduji Wa Chuo kikuu SUA kuwa Mkurugenzi SIDO

Uteuzi.jpg
Share:

Audio: Chid Benz na Rayvany wametuletea huu mdundo ‘Chuma’


Baada ya kimya kirefu mkali wa midundo ya Hiphop nchini Chid Benz leo July 18 2016 anatualika kwenye ngoma yake mpya ya ‘Chuma’ aliyomshirikisha Rayvany kutoka WCB, ngoma iliyotayarishwa na proudcer Laizer pamoja na Mr T Touch, usisahahu pia kuniachia comment yako hapa kuhusiana na huu mdundo na wakali hawa wataziona hapa

Share:

Rais Magufuli aibua ufisadi mwingine wa mabilioni ya shilingi ndani ya Jeshi la Polisi

Rais Magufuli amelitaka Jeshi la Polisi kujiepusha na vitendo vya rushwa ambavyo vilinafanya jeshi hilo kukosa heshima katika jamii huku akisema kuwa ana taarifa za jeshi hilo kuingia katika makubaliano ya kifisadi ya mabilioni ya shilingi kwa ajili ya kununua sare za jeshi hilo.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo alipokuwa akiwaapisha makamishna wa Jeshi la Polisi waliopandishwa vyeo na kuongeza kuwa ni jambo la kusikitisha kwamba mabilioni hayo yalitolewa kwa siku moja lakini hadi leo hakuna hata sare moja ya iliyonuuliwa.

Ameshangazwa na jeshi hilo kutoa kiasi cha fedha kinachokadiriwa kuwa kati ya shilingi bilioni 40 hadi 60 kwa ajili ya sare za polisi ambazo hadi leo hakuna hata moja iliyonunuliwa na wakati huohuo jeshi hilo likikosa shilingi bilioni 4 tu za kukomboa magari yao zaidi ya 70 yanayoshikiliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) huko bandarini.

Aidha, Rais Magufuli ameagiza uchunguzi ufanyike na wahusika wafikishwe mbele ya haki ila angalau hata nusu ya fedha hizo ziweze kurudishwa zikalipie magari ya polisi yaweze kutoka bandarini maramoja.

Amelitaka pia Jeshi la Polisi kuachana na utaratibu wa kuwa na watumishi ambao ni raia wa kawaida na badala yake polisi wenyewe ndio washike nafasi hizo kulingana na taaluma husika na kushangazwa na taarifa kuwa  Mhasibu Mkuu wa Polisi aliyetumbuliwa hivi karibuni kwa tuhuma za ubadhirifu alikuwa raia wa kawaida na sio polisi.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger