Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, inapenda kuwashukuru wadau na wananchi wote waliotuandikia maoni pamoja na kuuliza maswali mbalimbali kwa kipindi cha mwezi Juni, 2016.
Tunapenda kuwajulisha wale wote waliotuandikia maoni na maswali na hawajafungua baruapepe zao (Emails) na kurasa zao za Facebook wazifungue kwani tumejibu kila swali na kuwatumia katika anwani husika na baadae kuyaunganisha maswali na maoni yanayofanana na kuyatolea majibu ya jumla kwa faida ya wasomaji wetu wengine ili kuendelea kuelimishana kuhusu masuala yanayohusu Uendeshaji wa Mchakato wa Ajira Serikalini.
1. Swali
Mimi ni mtanzania mwenye elimu ya NTA, na nina swali kwa Watendaji wa Utumishi wa Umma wanaosimamia Ajira, Je! walio na ''NTA level/basic certificate''. ''Certificate'' ya mwaka mmoja wanaweza kuajiriwa Serikalini? Na kama hapana, kwa sababu gani?
Jibu
Tunashukuru kwa swali lako. Napenda kukufahamisha kuwa matangazo ya ajira kwa nafasi mbalimbali hutolewa na kuainisha sifa zinazohitajika kwa kila nafasi inayotangazwa na majukumu ya kazi atakayokwenda kutekeleza mwombaji pindi atakapopata nafasi hiyo. Hivyo ni vyema ukawa unapitia kila nafasi za kazi zinapotangazwa na kuangalia kama kazi iliyotangazwa inaendana na sifa za taaluma uliyonayo na pale utakapoona nafasi inayoonesha sifa ulizonazo basi unaweza kuwasilisha maombi yako.
2. Swali.
Habari yako ndugu Katibu, samahani, mimi kama mdau, ningependa kufahamishwa juu ya habari niliyoipata kutoka katika vyanzo visivyo rasmi yenye kudai kuwa ajira za Serikali 2016-2017 zimefutwa zikiwemo ajira za ualimu. nitafurahi nikifahamishwa juu ya hili na ofisi yako. asante ndugu Katibu. Wako katika kujenga taifa, asante na kazi njema.
Jibu.
Tunashukuru kwa swali lako. Awali ya yote napenda kukupongeza kwa kuwa mdadisi mwenye kupenda kufahamu ukweli kwa kupitia mamlaka husika kuliko kuamini taarifa za vyanzo visivyo rasmi. ni kweli ajira za Serikali zimesitishwa kwa muda (si kufutwa) ili kupisha uhakiki wa Watumishi hewa na kukamilisha Muundo wa Utumishi wa Umma na mara baada ya zoezi hilo kukamilika taarifa rasmi ya nini kinafuata itatolewa na mamlaka husika. Hivyo, ni vyema kuwa na subira katika kipindi hiki cha mpito na kuendelea kuwa wabunifu ili kuweza kutambua fursa nyingine halali tunazoweza kuzitumia kujiletea maendeleo kwa ajili ya ujenzi wa Taifa letu.
3. Swali
Mimi ni kijana wa Kitanzania mwenye elimu ngazi ya diploma katika masuala ya Cartography (urasimu ramani ) kutoka Chuo cha Ardhi Tabora naomba kuuliza swali: Mnamo tarehe 14.09.2015 nilifanya interview nikiwa na washiriki wengine tulioitwa pamoja katika interview hiyo tukiwa katika idadi ya washiliki 56 katika fani ya fundi sanifu daraja la pili, nina maswali mawili pamoja na maoni kama ifuatavyo;
A. Kwanza, tangu kipindi hicho mpaka leo hii natuma ujumbe huu au swali hili kwenu sijawahi kujua kinachoendelea mbali na kuona wengine wakiitwa kazini nami sijui tatizo langu lilikua wapi?
B. Pili sijajua fundi sanifu daraja la pili na daraja la kwanza vina tofauti gani sababu tangazo la kazi lilihusisha wenye daraja la pili lakini nimekuja kuwaona wengine waliochaguliwa wakiwa wa daraja la kwanza.
Maoni, Pamoja na Mhe.Rais kusitisha ajira kwa muda nasi tukiwa na muda mrefu mpaka sasa sijui ofisi inatufikiriaje sababu nako huku tunakojitolea katika kazi kama hizi wakituchoka sijui tutakimbilia wapi. Ni huruma yenu ndio inayohitajika katika kutunusuru, natanguliza samahani kama kuna neno nitakua nimeikwaza ofisi yako, pili natoa shukrani zangu kwenu kwa kuiweka barua pepe hii katika mtandao.
Nawatakieni kazi njema.
Jibu
Tunashukuru kwa maswali pamoja na maoni yako. Tunapenda kukujibu kama ifuatavyo kulingana na vipengele ulivyoainisha.
A. Ni kweli Sekretarieti ya Ajira imekuwa ikiendesha saili katika fani mbalimbali na kama ulivyobainisha ulikuwa miongoni mwa waliofanya usaili mwezi Septemba mwaka 2015 na hujapata majibu yoyote baada ya usaili husika. Tunapenda kukujulisha kuwa matokeo ya usaili husika yalishatolewa na wale waliofanya vizuri walishapangiwa vituo vya kazi kulingana na fursa za Ajira zilizokuwepo na wale ambao hawakufanya vizuri walielezwa katika tangazo la kuwataarifu waliofaulu usaili husika kuwa endapo hukuona jina lako katika hao waliopangiwa vituo vya kazi utambue kuwa hukufanya vizuri katika usaili husika hivyo usisite kuomba nafasi ya kazi pindi itakapotangazwa tena.
B. Umesema unapenda kujua tofauti ya Fundi Sanifu daraja la I na II ni ipi? Jibu ni kwamba wote wanaajiriwa wenye stashahada (Diploma) ila wanatofautiana kwenye uzoefu wa kazi. Hivyo huenda wewe uliomba nafasi ya kazi iliyotangazwa kwenye Wizara na mwingine uliyesoma nae akafanya kwa muda kwenye kampuni binafsi akapata uzoefu akawa ameomba nafasi iliyotangazwa kwenye Wizara na Taasisi nyingine na mkafanya usaili pamoja, Hivyo kwa kuwa yeye aliomba nafasi mbili tofauti na akafanya zote kwa siku moja ama nyakati tofauti endapo atafaulu usaili basi atapangiwa kituo cha kazi na mara nyingi unapoona daraja la kwanza tambua ni nafasi zilizotangazwa katika Taasisi na mhusika lazima awe na uzoefu wa kazi kwa muda fulani.
Mwisho kuhusiana na maoni yako ni kwamba ni kweli Serikali imesitisha Ajira kwa muda kama ulivyomsikia Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli alivyotangaza na hilo ni agizo lazima tulifuate. Aidha, kuhusu ofisi kukusaidia hatuna njia nyingine yoyote kwa kuwa ajira za Serikali zinaendeshwa kwa mujibu wa Sera, Sheria, Kanuni na Taratibu ni vyema kuendelea kufanya kazi huko ulipo kwa bidii na kuvuta subira mpaka hapo mamlaka husika itakapotoa maelekezo mengine kuhusu mchakato wa ajira za Serikali.
4. Question
Dear Sir/Madam,
I am grateful for the opportunity to write this email to your esteemed Government Agency. I have read with keen interest the names of the District Executive Directors appointed by our Honorable President yesterday. I have noted that the position of Municipal Director for Dodoma is vacant and would therefore like to submit my CV for your consideration. I am a proud supporter of our President and would like to offer my services to the government having worked in the private sector all along. I feel the time has come to serve my country in Government and would like to help our Honourable President in whatever capacity he intends to give me. I will give my all for the benefit of my beloved country. My major strengths are organization and strategizing and hence the reason why I feel I can make an exceptional Municipal Director for Dodoma Municipal Council if given the opportunity.
Kindly find my attached CV for your perusal. I will be available either on mobile or email should I be contacted in the near future hopefully. Thanking you very much for the opportunity. I am proud of our President and would like very much to serve in government. Yours Sincerely.
Answer.
Thanks for your concern, we would like to inform you that, Public Service Recruitment Secretariat (PSRS) is not Responsible Authority for District Executive Directors appointment, The Authority is under the Ministry responsible for Regional Administration and Local Government. As you have seen the recent appointments was done by President himself.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma. 14 Julai, 2016.