Saturday, 9 July 2016

PICHA MBALIMBALI MAHAFALI CHUO CHA MIFUGO BUHULI -TANGA

Leo tarehe 9 kumefanyika mahafali ya wanafunzi wanaosoma katika vyuo vya mifugo mkoani Tanga ambapo mahafali hayo yamefanyikia katika chuo cha BUHULI lilichopo jijini Tanga.

Jumla ya wahitimu 116 wakiwamo wavulana 80 na wasichana 36 wamefanikiwa kuhitimu mafunzo hayo.
Mgeni rasmi alikuwa ni Mkuu wa vyuo vya mifugo Tanzania.
(Picha zote kwa hisani ya Mdau wa MASWAYETU BLOG)
















Share:

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI JULY TAREHE 9.7.2016

Share:

Friday, 8 July 2016

HIZI HAPA FORM ZA KUAPPLY KOZI ZA UVUVI 2016/2017 DEADLINE NI TAREHE 30/7/2016

 Fisheries Education and Training Agency
Mimi nimekuwa miongoni mwa watu wanaotaka maendeleo yako au ya nduguyo siku zote,Vyuo vya uvuvi Tanzania vilitangaza nafasi za kujiunga na mafunzo kwa ngazi ya cheti na diploma kwa wanafunzi wa form 4 na 6.Lakini wengi hawakuwa na hadi sasa hawana taarifa kamili kuhusina na hili suala.

jinsi ya kutuma maombo ni kwa njia mbili NACTE AU DOWNLOAD FORM NA UTUME CHUONI MOJA KWA MOJA.
Kwa sasa Nina kushauri uombe kwa njia ya form ,idownload weka pasport ijaze vizuri kalipie bank 20000 then tuma kwenye chuo chochote cha uvuvi unachotaka kusoma.

Kama si wewe mjulishe rafiki yajo,mtoto wako,ndugu yako au mtu yeyote unaehisi anaweza kusomea kozi hizi za afisa uvuvi,sifa ni nyepesi uwe na D nne kwa cheti.

Application Form 2016/2017

 


Admission 2016/2017

 
 
 

Share:

Share:

Rais Magufuli amefanya uteuzi mwingine leo July 08 2016



Taarifa niliyoipokea kutoka ikulu jijini Dar es salaam ni kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Leonard Lutegama Maboko kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS).
Taarifa hiyo ya Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi huu umeanza July 07 2016. Kabla ya uteuzi huu Dkt. Leonard Lutegama Maboko alikuwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya binadamu Mbeya (NIMR Mbeya).
 Dkt. Leonard Lutegama Maboko anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Fatma Mrisho ambaye mkataba wake umemalizika tangu June 30 2016.
Share:

Kufanyika kwa uhakiki wa watumishi wote - SUA

Share:

New AUDIO | Dully Sykes - Anaimba | Download

Share:

Rais Magufuli Amteua Deogratius Ndejembi Kuwa Mkuu Wa Wilaya Ya Kongwa Mkoani Dodoma

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 07 Julai, 2016 amemteua Bw. Deogratius John Ndejembi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma.

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi amesema Bw. Deogratius John Ndejembi anachukua nafasi iliyoachwa na aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Bw. John Ernest Palingo ambaye amehamishiwa Wilaya ya Mbozi katika Mkoa wa Songwe.

Uhamisho wa Bw. John Ernest Palingo kwenda Wilaya ya Mbozi, umefanywa baada ya Mhe. Rais Magufuli kuridhia maombi ya Bw. Ally Masoud Maswanya aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, kuomba uteuzi wake utenguliwe kutokana na sababu binafsi.

Bw. Deogratius John Ndejembi atakula kiapo cha ahadi ya uadilifu kwa viongozi wa umma siku ya Jumanne tarehe 12 Julai, 2016 Ikulu Jijini Dar es salaam.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
07 Julai, 2016

Share:

Taarifa ya marekebisho katika majina ya Wakurugenzi yaliyotolewa leo Julai 7, 2016


Tunapenda kufanya marekebisho madogo katika majina yaliyopo kwenye orodha ya wakurugenzi wa Halmashauri za Majiji, Manispaa, Miji na Wilaya ambapo Dkt. Leonard Moses Massale ametangazwa kuwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma.

Jina hilo limeingizwa katika Orodha ya Wakurugenzi wa halmashauri kwa makosa, na kwa sababu hiyo Dkt. Leonard Moses Massale anaendelea kuwa Mkuu wa wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza.

Kufuatia marekebisho hayo, uteuzi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma utatangazwa baadaye.

AIDHA, tunapenda kutoa ufafanuzi kuwa makatibu tawala wa wilaya wote ambao majina yao yamejitokeza katika orodha ya wakurugenzi wa halmashauri za Majiji, Manispaa, Miji na wilaya, Mhe. Rais Magufuli ameamua kuwabadilishia majukumu na sasa watatumikia vyeo vyao vya ukurugenzi badala ya vyeo vya Ukatibu Tawala wa Wilaya.

Kufuatia mabadiliko hayo, nafasi za Makatibu Tawala wa Wilaya ambao wameteuliwa kuwa Wakurugenzi wa Halmshauri zitajazwa baadaye.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam

07 Julai, 2016
Share:

MAGAZETI YA LEO IJUMAA JULY TAREHE 8.7.2016

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger