Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe
07 Julai, 2016 amemteua Bw. Deogratius John Ndejembi kuwa Mkuu wa Wilaya
ya Kongwa Mkoani Dodoma.
Katibu
Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi amesema Bw. Deogratius John Ndejembi
anachukua nafasi iliyoachwa na aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya
Kongwa Bw. John Ernest Palingo ambaye amehamishiwa Wilaya ya Mbozi
katika Mkoa wa Songwe.
Uhamisho
wa Bw. John Ernest Palingo kwenda Wilaya ya Mbozi, umefanywa baada ya
Mhe. Rais Magufuli kuridhia maombi ya Bw. Ally Masoud Maswanya
aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, kuomba uteuzi wake utenguliwe
kutokana na sababu binafsi.
Bw.
Deogratius John Ndejembi atakula kiapo cha ahadi ya uadilifu kwa
viongozi wa umma siku ya Jumanne tarehe 12 Julai, 2016 Ikulu Jijini Dar
es salaam.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
07 Julai, 2016
0 comments:
Post a Comment