
Tunapenda kufanya marekebisho madogo katika majina yaliyopo kwenye
orodha ya wakurugenzi wa Halmashauri za Majiji, Manispaa, Miji na Wilaya
ambapo Dkt. Leonard Moses Massale ametangazwa kuwa Mkurugenzi wa
Manispaa ya Dodoma.
Jina hilo limeingizwa katika Orodha ya Wakurugenzi wa halmashauri kwa
makosa, na kwa sababu hiyo Dkt. Leonard Moses Massale anaendelea kuwa
Mkuu wa wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza.
Kufuatia marekebisho hayo, uteuzi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma utatangazwa baadaye.
AIDHA, tunapenda kutoa ufafanuzi kuwa makatibu tawala wa wilaya wote
ambao majina yao yamejitokeza katika orodha ya wakurugenzi wa
halmashauri za Majiji, Manispaa, Miji na wilaya, Mhe. Rais Magufuli
ameamua kuwabadilishia majukumu na sasa watatumikia vyeo vyao vya
ukurugenzi badala ya vyeo vya Ukatibu Tawala wa Wilaya.
Kufuatia mabadiliko hayo, nafasi za Makatibu Tawala wa Wilaya ambao
wameteuliwa kuwa Wakurugenzi wa Halmshauri zitajazwa baadaye.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
07 Julai, 2016
0 comments:
Post a Comment