Taarifa
niliyoipokea kutoka ikulu jijini Dar es salaam ni kwamba Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Leonard
Lutegama Maboko kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya kudhibiti UKIMWI
Tanzania (TACAIDS).
Taarifa
hiyo ya Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi huu
umeanza July 07 2016. Kabla ya uteuzi huu Dkt. Leonard Lutegama Maboko
alikuwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya
binadamu Mbeya (NIMR Mbeya).
Dkt.
Leonard Lutegama Maboko anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Fatma
Mrisho ambaye mkataba wake umemalizika tangu June 30 2016.
0 comments:
Post a Comment