Wednesday, 16 March 2016

Waziri Jaffo: Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali Inanuka Ufisadi

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY


Naibu Waziri wa Tamisemi, Utumishi na Utawala Bora, Selemani Jafo amesema Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya inanuka ufisadi unaofanywa na baadhi ya wakuu wa idara.

Kauli hiyo ya waziri inatokana na tuhuma za upotevu wa zaidi ya Sh800 milioni mwaka 2010/2011 zilizolenga kuboresha elimu ya sekondari wilayani Mbarali.

Fedha hizo ambazo zinaweza kutengeneza madawati 1,600 yanayotosheleza mahitaji ya wanafunzi 4,800, ikiwa dawati moja kwa bei ya soko kwa sasa ni Sh50,000 zilifujwa na watumishi ambao miongoni mwao bado wapo.

Jafo alitoa kauli hiyo juzi alipozungumza na wakuu wa idara, watumishi na madiwani wa halmashauri hiyo kwenye ziara yake iliyolenga kutoa maelekezo ya kiutendaji.

Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Yeremiah Mahinya alimhakikishia Jaffo kwamba watatekeleza maagizo waliyopewa kwa ufanisi na kwa muda, ikiwamo kuondokana na matumizi mabaya ya fedha za umma.

Mkuu wa wilaya hiyo, Gullamhusein Kiffu alisema mtumishi atakayeshindwa kutimiza majukumu vizuri atamchukulia hatua.
Share:

Serikali Yatangaza Rasmi Kugundulika kwa Futi za Ujazo wa Gesi Tirioni 2.17 katika Bonde la Ruvu

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Serikali imetangaza rasmi kugundulika kwa futi za ujazo wa Gesi Tirioni 2.17 katika Bonde la Ruvu mkoani Pwani,  katika eneo lijulikanalo kama Mamba Kofi One ikiwa ni moja ugunduzi ulifanywa na Kampuni ya Dodsal ikishirikiana na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC).

Akitoa tamko hilo mbele ya vyombo vya habari ofisini kwake Dar es Salaam jana asubuhi, Waziri wa  Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo alisema kuwa hadi kufikia Machi mwaka huu jumla ya gesi yote iliyogunduliwa nchini ni trioni 57.23.

"TPDC imerekebisha muundo wake tunataka iwe inajishughulisha  na utafutaji wa gesi ya mafuta hivyo kufuatana na sheria ya petroli ya mwaka jana kazi zote zitasimamiwa na TPDC na haitaendelea kusimamia makampuni mengine badala yake tuameazisha wakala wakusimamia kazi ," alisema Muhongo.

Akitolea ufafanuzi kuhusiana  na kugundulika kwa gesi hiyo asilia iliyopo nchi kavu imefikia futi za ujazo tirioni 10.17, na baharini katika kina kirefu cha futi za ujazo ni 47.08.

Waziri Muhongo alisema ufumbuzi huo umefanywa na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kwa kushirikiana na Kampuni ya Haydrocarbons and Power Limited (DODSAL) hivyo wakiendelea na utafiti wataweza kuvuka hata futi 10 kama walivyo dai.

Alisema kuwa takribani futi za ujazo  elfu moja zina uwezo wakuzalisha jumla ya megawati za umeme zipatazo 5000 wakati huo bado wanaendelea na  utafiti wa gesi katika maeneo ya kusini mwa Tanzania ambapo kumegundulika kuwa na gesi nyingi .

"Nilazima taifa letu liwe na umeme mwingi, na umeme wa kutosha kwani tukifanya hivyo tunaweza kufikia kwenye bigawati kama nchi za kusini walivyoweza kupata umeme mwingi," alisema Muhongo.

Akijibu maswali kuhusiana  na kunufaika kwa wananchi na gesi hiyo alisema tayari wameaza kunufaika kwani kabla ya awamu ya tano ya Rais Dk. Jonh Magufuli,  jumla ya megawati 700 hadi 800 ndizo zilikuwa zikitumika katika matumizi ya umeme ambapo katika kipindi cha  awamu ya tano jumla megawati 1000 zinaendelea kutumika.

"Ifahamike kuwa faida ya gesi kwa wananchi ni ya siku nyingi kwani viwanda takribani 37 vimekuwa vikitumika kwa matumizi ya gesi kikiwemo kiwanda cha Saruji " alisema.

Awali kabla ya uzinduzi huo Meneja Utafiti wa Shirika la Maendeleo ya Mafuta na Gesi (TPDC), Venosa Ngowi alisema wanatarajia kumpatia ripoti ya mapendekezo ya juu ya gharama za uuzaji wa gesi nchini ifikapo Aprili,20 mwaka huu.

Ngowi alisema zoezi linalofanyika ni mazungumzo ya wawekezaji na watalamu wa nchi husika kuweza kufanya uhakiki wa gharama wa bei za gesi nchini.

Alisema moja ya changamoto wanazokutanazo ni kuwepo kwa gharama nyingi  zinazo muhusu mwekezaji
Share:

New AUDIO | Bonta Maarifa Ft. Nikki Wa Pili Belle 9 - Usirudi Jela | Download

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
http://www.kikistarmusic.com/uploads/tracks/112377611_1467494849_1787217896.mp3
Share:

VIDEO:PAUL MAKONDA AKILA KIAPO CHA UKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Image result for paul makonda akila kiapo 
Share:

TAKUKURU na POLISI Nusura Watwangane Makonde wakati Wakimgombea Shahidi.

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Maafisa wa Takukuru na askari wa Jeshi la Polisi waliokuwa wakilinda eneo la Mahakama ya Wilaya ya Bukombe mkoani Geita, juzi nusura watwangane makonde wakati wakimgombea shahidi.

Tukio hilo lilianza kama masihara baada ya shahidi huyo kufika mahakamani akiongozana na maofisa wa Takukuru na ghafla mmoja wa polisi aliyemtambua, alimuweka chini ya ulinzi na kumfunga pingu.

Kamanda wa Takukuru wa wilaya hiyo, Chuzela Shija alilazimika kuingilia kati na kuwaomba polisi kumuachia mtu huyo, Paulo Sitephano ili atoe kwanza ushahidi ndipo hatua nyingine zifuate, ombi lililokubaliwa na polisi kwa kumfungua pingu huku wakimlinda asitoroke.

Sokomoko lilianza mara tu shahidi huyo alipomaliza kutoa ushahidi dhidi ya Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi ya Umoja anayetuhumiwa kuomba na kupokea rushwa ya Sh100, 000.

Polisi hao walimuwahi na kumfunga tena ili wampeleke kituoni. Kitendo hicho kiliwakera maofisa wa Takukuru ambao walitaka kuondoka na mashahidi wao wote watano walioenda nao mahakamani hapo kwa kutumia gari lao.

Maofisa hao wa Takukuru waliwasihi polisi kumuacha shahidi huyo na kuwataka wamkamate baada ya kukamilisha taratibu zao za kiofisi, ombi hilo lilikataliwa na askari hao.

“Hatuwezi kumuachia mtuhumiwa kwa sababu anatafutwa muda mrefu kwa tuhuma zilizofikishwa polisi,” alijibu mmoja wa polisi aliyekuwa na cheo cha sajenti ambaye alikataa kutaja jina lake.

Kitendo hicho kiliwakera maofisa wa Takukuru na kuamua kutumia nguvu kuwazuia polisi kuondoka na shahidi wao, hali iliyozua mtafaruku baina yao na kufikia hatua ya kukunjana mashati kabla ya kuamuliwa kuacha vitendo hivyo.

Baada ya vuta nikuvute na kurushiana maneno makali na vitisho, polisi walioongeza nguvu kwa kuita gari la doria, walifanikiwa kumchukua shahidi huyo na kumpandisha kwenye gari kabla ya kuondoka naye, huku maofisa wa Takukuru wakibaki kulalamikia ubabe wa askari hao.

Katika tukio hilo lililovuta watu wengi, baadhi ya maofisa wa Takukuru walionekana wana nguo zilizochanika, hali iliyosababishwa na mtafaruku huo.

Akizungumzia tukio hilo, mkuu wa waendesha mashtaka wa polisi mahakamani hapo, Elias Mgobela aliwatupia lawama maofisa wa Takukuru kwa kushindwa kuonyesha ushirikiano kwa askari hao wakati wa kumtia mbaroni mtuhumiwa.

“Kisheria, polisi wana haki ya kumkamata mtuhumiwa eneo lolote. Huyo shahidi wa Takukuru alikuwa akitafutwa kwa muda mrefu na polisi. Ilikuwa ni jukumu la maofisa wa Takukuru kushirikiana na polisi kufanikisha kumkamata badala ya kuzuia,” alisema.

Alisema kitendo hicho kilisababisha mmoja wa watuhumiwa aliyemtaja kwa jina moja la Lubango aliyekuwa chini ya ulinzi wa polisi kutoroka baada ya askari wengi kuelekeza nguvu kumgombea shahidi huyo.

Kwa upande wake, kamanda wa Takukuru wa wilaya, Chuzela Shija aliitupia lawama polisi akidai ilitumia ubabe, nguvu na dharau dhidi ya maofisa wake ambao hawakukataa shahidi wao kutiwa mbaroni, bali waliomba wapewe fursa ya kukamilisha taratibu za kiofisi kabla ya kumkabidhi mikononi mwao kwa tuhuma zinazomkabili.

“Isingewagharimu polisi kufuatana na maofisa wa Takukuru hadi ofisini, wakakamilisha taratibu za kiofisi na shahidi huyo, halafu wakamtia mbaroni. Ilihitajika busara ndogo sana kulimaliza suala hili, lakini bahati mbaya wenzetu walichagua kutumia ubabe na kutunishiana misuli,” alilalamika.

Katika kesi dhidi ya mwalimu huyo, Mkuu wa Wilaya ya Bukombe, Amani Mwenegoha aliieleza mahakama jinsi alivyoshiriki kuweka mtego wa kumnasa.

Mkuu huyo wa wilaya alidai kuwa aliandaa mtego huo na kufanikiwa kumtia mbaroni mtuhumiwa huyo, Daniel Nying’ati baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa mmoja wa wananchi aliyedai kuombwa fedha ili mtoto wake apate nafasi ya kurudia darasa la saba shuleni hapo.

Akiongozwa na mwendesha mashtaka wa Takukuru, Kelvin Murusuri, shahidi huyo alidai kuwa alichukua jukumu hilo kutekeleza moja ya majukumu yake ya kupokea, kusikiliza na kutatua kero za wananchi.

Alidai Februari 8, alipokea simu kutoka kwa mwananchi aliyemtaja kwa jina la Marko Elias akimtaarifu kuombwa rushwa na mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Umoja alipoenda kuomba nafasi ya mtoto wake kurudia darasa la saba shuleni hapo.

 “Katika maelezo yake, mwananchi yule aliniambia aliombwa rushwa ya Sh150, 000, ndipo nilipomuambia aende Takukuru na kufanikisha mtuhumiwa kutiwa mbaroni,” alidai Mwenegoha.

Kwa upande wake, shahidi wa pili ambaye ni ofisa wa Takukuru, Redemta Miremi alidai Februari 8, alimpokea mwananchi aliyemtaja kwa jina la Marko Elias akidai kuelekezwa na mkuu wa wilaya kufika ofisi hizo kutoa taarifa ya kuombwa rushwa.
Share:

MAGAZETI YA LEO JUMATANO MARCH 16 2016

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Share:

Tuesday, 15 March 2016

MAOMBI YA NAFASI ZA KUJIUNGA NA KOZI ZA KILIMO NA MIFUGO 2016/2017

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Nacte inatangaza nafasi za kujiunga na mafunzo ya kozi tajwa hapo juu,tafadhali BONYEZA HAPA kudownload na kusoma sifa za kujiunga na jinsi ya kutuma maombi.
Share:

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) apandishwa mahakamani

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

DAVID Mattaka, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL)


DAVID Mattaka, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL), amepandishwa kizimbani kwa kosa la kuliingizia serikali hasara ya Dola za Marekani 772,402.08.

Akisoma mashtaka Vitalis Thimos, wakili wa serikali mbele ya Respicius Mwijage, Hakimu Mkazi katika Mahakama ya Kisutu amesema kuwa, mshtakiwa huyo anakabiliwa na kosa hilo kutokana na matumizi mabaya ya madaraka katika ofisi ya umma.

Tuhuma hizo ni pamoja na kutia saini mkataba wa kukodisha ndege aina ya Air bus A320-214 kwa Kampuni ya Wallis TradingInc bila kufuata sheria na taratibu za zabuni.

Mattaka anadaiwa kuungizia hasara serikali kutokana na hatua yake ya kuidhinisha pesa za matengenezo ya ndege hiyo katika Kampuni ya AEROMANTENIMIENTO.

Hasara nyengine ni matumizi mabaya kwa kununua vifaa vya ndani ya ndege hiyo yaliyoigharimu Dola za Marekani 35,984.82.

Watuhumiwa wengine kwenye kesi hiyo ni Ramadhani Mlinga, Mkurugenzi wa Manunuzi ATCL na Bertha Soka ambaye ni mwanasheria wa shirika. Watendaji hao wanadaiwa kushindwa kuzuia ubadhilfu huo. Kesi hiyo itatajwa tena tarehe 19 Machi.
 
Chanzo: MwanaHalisi
Share:

Kesi ya IPTL Dhidi ya Zitto Kabwe kusuluhishwa Machi 23 Kwa Siri

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Mahakama Kuu inatarajia kusuluhisha kesi iliyofunguliwa na Kampuni ya Kufua Umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) dhidi ya Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe na wenzake Machi 23, mwaka huu.

Kesi hiyo namba 175 ya mwaka 2014 ilipangiwa kuanza kufanyiwa usuluhishi jana mbele ya Jaji Salvatory Bongole, lakini ilishindikana kutokana na upande wa walalamikaji ambao ni IPTL kushindwa kufika mahakamani.

Hata hivyo, Kaimu Msajili wa Mahakama hiyo Kitengo cha Usuluhishi, Beda Nyaki alisema kesi hiyo itasikilizwa kwa siri baina ya pande hizo.

“Kesi hii haiwezi kuripotiwa kwenye vyombo vya habari kwa sababu ipo katika hatua za kwanza za usuluhishi, hivyo kitu kitakachoongolewa baina ya walalamikaji na walalamikiwa kitakuwa ni siri yao,” alieleza Nyaki.

Alisema kusikilizwa kwa faragha kwa kesi hiyo ni hatua ya kupunguza gharama na muda.

Katika kesi hiyo, Kampuni za IPTL, Pan Africa Power Solutions (T) Limited na Mwenyekiti Mtendaji wa kampuni hizo, Harbinder Sing Seth walifungua madai ya Sh500 bilioni dhidi ya Zitto, Mhariri wa gazeti la Raia Mwema, Kampuni ya Raia Mwema na Kampuni ya Flint Graphics ikiwa fidia kwa kuwakashfu kuhusiana na sakata la uchotwaji wa zaidi ya Sh300 bilioni katika Akaunti ya Tegeta Escrow.

Mawakili wanaomtetea Zitto ni Wakili Ntemi Masanja na Ivone Sianga ambao walidai kuwa walalamikaji walishindwa kufika mahakamani hapo na kusababisha kuahirishwa kwa kesi.

Ilidaiwa kuwa walalamikaji hao walichukua hatua ya kufungua kesi hiyo kufuatia makala aliyoyaandika Zitto katika gazeti la Raia Mwema la Agosti 13, 2014 katika ukurasa wa saba na wa 14, ikiwa na kichwa cha habari “Fedha za IPTL ni mali ya umma.’’

Walalamikaji hao walidai kuwa makala hiyo ni ya upotoshaji na ilikuwa na lengo la kuwachafua mbele ya jamii.
Share:

Walimu Wanaotuhumiwa Kufanya Mapenzi na Wanafunzi Jijini Mwanza Waundiwa Kamati Maalum

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Mkoa wa Mwanza kimeunda kamati kuchunguza tuhuma dhidi ya baadhi ya walimu wa Shule ya Sekondari Mihama wilayani Ilemala kujamiiana na wanafunzi wao.

Mwenyekiti wa CWT mkoani hapa, Sibora Kisheri alisema wameunda kamati hiyo baada walimu wanane, akiwamo mkuu, Joseph Marifedha kusimamishwa kazi kwa amri ya aliyekuwa Mkuu wa mkoa huo, Magessa Mulongo kwa tuhuma hizo.

“Haiingii akili kuona walimu wote wakawa na sifa ya makosa yanayofanana, hivi hakuwapo hata mmoja aliyeshtukia mchezo huo na kuwashauri wezake,” alisema Kisheri.

Alisema uchunguzi huo unalenga kubaini kiini cha tuhuma hizo na kuishauri Serikali na vyombo husika hatua stahiki za kuchukua kuhakikisha kila upande unatendewa haki.

Aliwaasa walimu kufuata sheria, kanuni na misingi ya kazi kwa kutimiza wajibu na kuepuka mambo yanayokinzana na taaluma hiyo.

Hivi karibuni Mulongo aliwasimamisha walimu hao baada ya kupata taarifa kuwa walikuwa wakijihusisha na vitendo hivyo.
Share:

Vigogo wa Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli Tanzania (Rahco) Wafikishwa Mahakamani

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Mkurugenzi Mkuu wa zamani wa Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli Tanzania (Rahco), Benhadard Tito na wenzake wawili wamepadishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakikabiliwa na mashtaka manne.

Vigogo wawili wa Rahco na mfanyabiashara wanakabiliwa na mashtaka ya uhujumu uchumi, matumizi mabaya ya madaraka, kula njama na kusababisha hasara ya dola za Marekani 527,540.

Mbali na Tito, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Mwanasheria wa Rahco, Emmanuel Massawe na mfanyabiashara ambaye pia ni mwakilishi wa kampuni ya Rothschild (South Africa) Proprietary Limited, Kanji Mwinyijuma.

Washtakiwa hao watatu walisomewa mashtaka hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, huku upande wa mashtaka ukiwa na Maghela Ndimbo, Janeth Machulya wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kwa kushirikiana na Wakili wa Serikali Mkuu, Timon Vitalis.

Mawakili hao, wakiongozwa na Vitalis walidai kuwa washtakiwa wote watatu katika nyakati tofauti kati ya Septemba Mosi, 2014 na Septemba 30, 2015 katika Mkoa wa Dar es Salaam walikula njama ya kutenda makosa hayo chini ya Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa.

Katika kesi hiyo, ilidaiwa kuwa Februari 27, 2015, Tito katika ofisi za Rahco zilizoko wilayani Ilala, alitumia madaraka yake vibaya kwa kuipitisha kampuni hiyo ya Rothschild kama mshauri wa mradi wa uimarishaji wa Reli ya Kati bila idhini ya Bodi ya zabuni ya Rahco, hivyo kwenda kinyume na Sheria ya Manunuzi ya Umma.

Tito na Massawe wanadaiwa kuwa Machi 12, 2014 katika ofisi hizo za Rahco walitumia madaraka yao vibaya kwa kutia saini barua rasmi ya kuichagua kampuni hiyo, kama mshauri katika mchakato wa uimarishaji wa njia ya Reli ya Kati kwa kiwango cha kisasa (standard gauge).

Kati ya Machi 12 na Mei 20, 2015 katika ofisi za Rahco, Tito na Massawe wanadaiwa kutumia vibaya madaraka yao kwa kushindwa kuwasilisha mkataba wa huduma ya ushauri, baina ya kampuni hizo mbili kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).

Pia wanadaiwa kuwa kati ya Mei 20 na Juni 20, 2015 katika ofisi hizo washtakiwa hao, walishindwa kuwasilisha nakala ya mkataba kati ya kampuni hizo kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Mbali na mashtaka hayo, washtakiwa hao kwa pamoja kwa nyakati tofauti kati ya Machi Mosi na Septemba 30, 2015 walitoa huduma ya ushauri kwa kampuni hiyo, bila kufuata taratibu za ununuzi na malipo na walisababisha hasara ya dola za Marekani 527,540 ambazo zililipwa kama gharama za malipo ya awali.

Agosti 18, 2015, Tito akitekeleza majukumu yake, alitumia vibaya mamlaka kwa kuipatia kampuni ya China Railway Construction Corporation kazi ya ujenzi wa reli kwa kilomita mbili za kiwango cha kisasa kutoka Soga, iliyogharimu dola Marekani 2, 312,229.39 bila ya kuwa na idhini ya bodi ya zabuni ya Rahco.

Washtakiwa hao hawakuruhusiwa kujibu kwa sababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kuisikiliza kesi hiyo hadi Mahakama Kuu. Uamuzi wa dhamana utatolewa Ijumaa.
Share:

Makahaba 287 Pamoja na Wateja Wao Watiwa Mbaroni Jijini Dar es Salaam

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es salaam limefanikiwa kuwakamata jumla ya watu 287 ambao ni dada poa pamoja na kaka poa katika operation maalum iliyofanyika maneo mbalimbali ya Jiji hilo.

Operation hiyo ilitangazwa na kamishna wa kanda maalum mnamo Tarehe 7 mwezi wa 3 na kuazimia kuwakamata madada poa na makaka poa pamoja na wateja wao ambao watakutwa wakiwanunua.

Katika mkoa wa kipolisi wa ilala operation hii imefanikiwa kuwakamata jumla ya madada poa 51 kutoka katika maeneo mbalimbali yakiwemo msimbazi,Buguruni,na stakishari,pia imewakamata jumla ya makaka poa 12 ambapo 11 wanatokea Buguruni na mmoja kutoka msimbazi.

Mkoa wa kipolisi wa temeke umefanikiwa kuwakamata jumla ya madada poa 22,ambapo changombe walipatikana 12,na mbagala walipatikana madada poa 10.
 
Aidha katika mkoa wa kipolisi wa kinondoni operation hiyo imefanikiwa kuwakamata madada poa 76 kutoka maeneo ya osyterbay madada poa 49,magomeni 23,na kawe madada poa 4,pamoja na makaka poa 4.

Akizungumza na wanahabari jana makao makuu ya polisi kanda maalum ya Dar es salaam ,Kamishna wa kanda hiyo CP Simon Sirro aliwataka watu wenye tabia kama hizo kuacha mara moja kwani ni kinyume na mila na desturi za mtanzania ambapo amewataka kutafuta biashara nyingine halali za kufanya.
Share:

Pingamizi La Stephen Wassira dhidi ya ubunge wa ester bulaya Latupiliwa Mbali

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Mahakamaa Kuu Kanda ya Mwanza, imetupilia mbali maombi ya baadhi ya wapigakura wa Jimbo la Bunda Mjini ya kuruhusiwa kukata rufaa kupinga uamuzi wa Makahama Kuu wa kufuta shauri lao la kupinga matokeo ya uchaguzi.

Maombi hayo yaliwasilishwa na Magambo Masato na wenzake wanne wanaompigania Stephen Wassira, wakiiomba mahakama hiyo kuwaruhusu kukata rufaa Mahakama ya Rufani baada ya kutoridhiswa na uamuzi ya kupinga matokeo ya uchaguzi uliofanyika Oktoba 25, mwaka jana yaliyompa ushindi Ester Bulaya (Chadema), dhidi ya Stephen Wasira (CCM).

Jaji anayesikiliza shauri hilo namba 25 la mwaka 2016, Rose Ebrahim alisema jana kuwa anakubaliana na pingamizi lililowekwa na wajibu maombi kuwa hayana mashiko kisheria.

Pingamizi hilo lilowasilishwa na Wakili Mfawidhi wa Serikali, Paschael Marungu alidai aliyesaini hati ya maombi siyo aliyethibitisha kwani hilo ni kosa la kisheria.

Wakili Marungu alidai hati hiyo ilisaniwa na Wakili Denis Kahangwa na kuthibitishwa na Wakili Constantine Mutalemwa kwamba hilo ni kosa kisheria, hivyo kuiomba mahakama kutupilia mbali.

Akitoa uamuzi juu ya pingamizi hilo, Jaji Ebrahim alisema anakubaliana na pingamizi hilo kwani, makosa yaliyofanywa hayarekebishiki.

“Haya maombi nayatupilia mbali hayana miguu ya kusimamia, ni kosa kubwa hati kusainiwa na mtu mwingine halafu ikathibitishwa na mwingine, hakuna namna ya kurekebisha, lazima sheria ifuatwe na taratibu zake,” alisema.

Awali, Magambo na wenzake walifungua kesi Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza kupinga ushindi wa Bulaya, lakini ilitupiliwa mbali kutokana na kushindwa kutimiza masharti ya sheria.
Katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25 mwaka jana, Bulaya alipata kura 29,973 na Wasira wa CCM aliambulia 19,123 ikiwapo tofauti ya kura 10,000.

Hata hivyo, Wasira alilalamikia matokeo hayo akidai uchaguzi ulitawaliwa na udanganyifu.
Share:

SHULE YA IYUNGA SEC YA MBEYA YAFUNGWA

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Uongozi mkoani Mbeya umeifunga Shule ya Sekondari Iyunga baada ya mabweni matatu kuungua moto na wanafunzi kulala nje kutokana na kuyaogopa mabweni yaliyobaki.

Kwa kawaida likizo fupi ilitakiwa kuwa kipindi cha pasaka, lakini shule hiyo ilifungwa Machi 11 hadi 25 na kwamba itaendelea kufungwa hadi Aprili Mosi.

Mkuu wa shule hiyo, Edward Mwantimwa alitoa maelezo hayo kwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Tamisemi), Seleman Jaffo aliyefika shuleni hapo juzi kujionea uharibifu uliotokana na moto uliounguza mabweni matatu kwa nyakati mbili tofauti.

Mwantimwa alisema mara ya kwanza mabweni ya Nyerere na Mkwawa yaliungua Februari 29 na Machi 7 la Shaban Robert, jambo ambalo lilisababisha hofu kwa walimu na wanafunzi na kuanza kuyasusa mabweni mengine.

Awali, Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Nyirembe Munasa akizungumza kwa niaba ya mkuu wa mkoa alimueleza naibu waziri hatua zilizochukuliwa ikiwamo wadau kutoa misaada na kwamba, pia walikuwa wanaandaa harambee ambayo wangependa ifanyike Dar es Saalaam.

Jaffo alilitaja tukio hilo kuwa ni janga na kuahidi kuwashirikisha wabunge wote kuchangia kurudisha hadhi ya shule hiyo.

Kuungua kwa shule hii kumeonyesha mengi yakiwamo ya uchakavu wa miundombinu,” alisema.

Alimtaka Nyirembe kusimamia ukarabati wa shule hiyo na uwe umekamilika ifikapo  Aprili Mosi.
Share:

MAGAZETI YA LEO JUMANNE MARCH 15 2016

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY












Share:

Monday, 14 March 2016

MKUU WA CHUO KOLANDOTO ANATANGAZA NAFASI ZA MASOMO ZINAZOTARAJIWA KUANZA MWEZI MACHI 2016. WAHI NAFASI NI CHACHE.

Share:

WADAIWA MIKOPO ELIMU YA JUU WAPEWA SIKU 60

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
 HESLB LOGO
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) inatoa siku 60 kuanzia tarehe 14 Machi, 2016 kwa wanufaika wote wa mikopo wanaodaiwa na HESLB kujitokeza na kuanza kulipa madeni yao kabla ya kuchukuliwa hatua za kisheria.
Aidha, katika muda huu wa siku 60 waajiri pia wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanatekeleza wajibu wao wa kisheria wa kuwasilisha taarifa za waajiriwa wao waliohitimu katika vyuo vya elimu ya juu ndani na nje ya nchi. Taarifa zinazopaswa kuwasilishwa zijumuishe majina kamili ya waajiriwa, vyuo na mwaka waliohitimu.
Itakumbukwa kuwa Sheria iliyoanzisha HESLB (Sura 178) (kama ilivyorekebishwa) inatoa wajibu kwa mnufaika wa mikopo ya elimu ya juu na pia wajibu kwa mwajiri.
Wajibu wa Mwajiri
Hivyo basi, taarifa hii inalenga kuwakumbusha waajiri ambao bado hawatimizi wajibu wao kisheria (kifungu cha 20) wa kuwasilisha majina ya waajiriwa wao wote ambao ni wahitimu wa vyuo vikuu kwa HESLB ndani ya siku 28 tangu waajiriwe. Adhabu ya kutotekeleza wajibu huu kwa mwajiri ni faini ya shilingi milioni saba (Tshs milioni 7) au kifungo au vyote kwa pamoja.
Kwa mujibu wa sheria hiyo, baada ya HESLB kupokea orodha kutoka kwa mwajiri, itafanya uchambuzi ili kubaini wanufaika wa mikopo ya elimu ya juu na kumwelekeza mwajiri kuingiza makato ya marejesho kwenye mshahara wa mnufaika na kuwasilisha makato hayo kwa HESLB. Adhabu ya kutowasilisha makato kwa HESLB ni faini ya asilimia 10 ya makato yote ambayo hayajawasilishwa na faini hii inapaswa kulipwa na mwajiri.
Wajibu wa mnufaika wa mkopo na wazazi, walezi, wadhamini
Aidha, pamoja na wajibu wa mwajiri kama ulivyofafanuliwa hapo juu, wanufaika wote wa mikopo ya elimu ya juu tangu mwaka 1994, wana wajibu wa kisheria (Kifungu cha 19 cha sheria ya HESLB), pamoja na mambo mengine, kuitaarifu HESLB kwa maandishi mahali alipo na kuandaa utaratibu wa kulipa deni lake la mkopo wa elimu ya juu.
Iwapo mnufaika wa mkopo atashindwa kutoa taarifa hizo, adhabu yake ni kushitakiwa mahakamani.
Aidha, HESLB inapenda kuwakumbusha wazazi, walezi na wadhamini wa wanafunzi walionufaika na mikopo kuwa wana wajibu wa kisheria (chini ya kifungu cha 22 cha sheria ya HESLB) wa kuhakikisha kuwa taarifa muhimu za mnufaika waliyemdhamini zinaifikia HESLB.
Kwa mujibu wa kifungu hicho, taarifa hizo ni pamoja na mahali alipo mnufaika, majina aliyotumia wakati akipata mkopo, mwajiri wake na kuhakikisha mnufaika aliyemdhamini anarejesha mkopo wake kwa HESLB.

Iwapo mwajiri, mnufaika au mdau yeyote ana swali, awasiliane na HESLB kwa simu zifuatazo: 0754 373481; 0763 459 165 au 022 2772432/33.
Lengo la HESLB ni kuhahakisha madeni yote yanakusanywa ili kuongeza uwezo wa kukopesha watanzania wengi zaidi. Ili kutekeleza hili, wanufaika, waajiri na wadau wengine wote wanapaswa kutimiza wajibu wao wa kisheria ili HESLB itekeleze majukumu yake kama ilivyokusudiwa wakati ilipoanzishwa mwaka 2004.
HESLB ilianzishwa kwa sheria ya Bunge na 9 ya mwaka 2004 na kuanza kazi rasmi mwezi Julai, 2005 ili, pamoja na majukumu mengine kutoa mikopo kwa wanafunzi wahitaji waliodahiliwa katika taasisi za elimu ya juu. Aidha, jukumu jingine la Bodi ni kudai na kukusanya mikopo yote iliyotolewa kwa wahitimu wa taasisi za elimu ya juu kuanzia mwaka 1994 wakati Serikali ilipoanza kukopesha wanafunzi.
Mwisho
Imetolewa na:
Bw. Jerry Sabi,
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji – HESLB         
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger